الإبداع في كمال الشرع
وخطر الابتداع
Ubunifu katika Ukamilifu wa Sheria na kutahadhari na Uzushi
la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu
Kila sifa njema zinamstahiki Allah, tunamsifu na kumuomba msaada, na msamaha na kutubia kwake, na tunajikinga kwake kutokana na shari za nafsi zetu na matendo yetu mabaya, yeyote mwenye kuongozwa na Allah hakuna wa kumpoteza na anaepotezwa na Allah hakuna wa kumuongoa.
Na nina shuhudia kua hapana mungu mwingine apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah peke yake hana mshirika na nina shuhudia kua Muhammad nimja wake na ni mtume wake, Allah amemtuma na uongofu na dini iliyo ya Haki, akafikisha ujumbe na akatekeleza amana, na akanasihi ummah na akapigana kwa ajili ya Allah ukweli wa kupigana mpaka ulipo mfikia umauti.
Na ameuacha ummah wake katika njia nyeupe usiku wake ni mithili ya mchana wake haiachi njia hiyo ila mwenye kuangamia, alibainisha ndani yake kila kinacho hitajiwa na Ummah katika mambo yake yote mpaka akasema Abuu Dhari radhi za Allah ziwe juu yake: Hakuacha mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ndege anae ruka angani ila alitupa elimu yake.Alisema bwana mmoja katika washirikina kumwambia Salaiman Alfarisy radhi za Alah ziwe juu yake: aliwafundisha Mtume wenu mpaka na adabu za kukidhi haja, akasema:Ndio, ametukataza tusielekee kibla wakati wa kukidhi haja kubwa au ndogo au kustanji kwa mawe yasiyopungua mawe matatu au kustanji kwa mkono wa kulia,au kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mifupana wewe unaona Qur'an hii tukufu Allah amebainisha ndani yake misingi ya dini na matawi yake, akabainisha Tawhidi na aina zake zote, akabainisha mpaka adabu za vikao, na kuomba idhini, amesema Allah mtukufu:
Enyi mlio amini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi
(Al-Mujadalah 11)Na amesema Allah Mtukufu:
Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu mpate kukumbuka Na msipomkuta mtu humo basi msiingie mpaka mruhusiwe, Na mkiambiwa: Rudini! Basi rudini, hivi ni usafi zaidi kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayo yatenda
(Nur 27-28)Mpaka adabu za kufaa nguo Allah Mtukufu alisema:Na wanawake wazee wasio taraji kuolewa, si vibaya kwao kupunguza nguo zao, bila ya kujishaua kwa mapambo. Na wakijiheshimu ni bora kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua.(Nur 60)
Ewe Nabii! Waambie wake zako, binti zako na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
(Al-Ahzab 59) Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyoficha (Nur 31) Wala sio wema kuzingia nyumba kwa nyuma. Bali mwema ni mwenye kumcha mungu, na ingieni majumbani kupitia milangoni.(Albaqara 189)Na aya zingine nyingi ambazo zinazo bainisha kua dini hii imekusanya pande zote na imekamilika haihitaji ziada kama isivyo hitaji kupunguza na kwa sababu hii amesema Allah mtukufu katika kuisifia Qura'an:Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu(An Nahli 89)Hakuna kitu ambacho watu wanakihitaji katika akhera yao na dunia yao ila Allah amebainisha katika kitabu chake ima kwa kukitaja au kwa ishara na ima kwa kutamka au kwa kuelewa.Enyi ndugu: hakika baadhi ya watu wanatafsiri kauli ya Allah Mtukufu:Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili ila ni ummah kama nyinyi. Hatukupuuza Katika kitu chochote(An-A'am 38)Anatafsiri kwa kusema:Hatukupuuza Katika kitu chochoteKwamba kitabu hapa eti ni Qur'an, na sahihi nikwamba makusudio ya kitabu hapo ni Lauhul Mahfuudh (Ubao uliopo mbinguni unao andikwa ndani yake matendo yote ya mwanadamu) Ama Qur'an hakika Allah ameisifu kwa sifa za kina zaidi kwa kusema:Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kituHizi ni sifa za kina na za wazi kuliko kusema:Hatukuacha katika kitabu chochote kisha kwa mola wao watarejea.
Na huwenda mtu anaweza kusema tutapata wapi idadi ya swala tano katika Qur'an?
Na idadi ya kila swala katika Qur'an?
Na vipi itakuwa sawa kwamba sisi hatuoni katika Qur'an ubainifu wa idadi ya rakaa za kila swala na Allah anasema:Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kituNa majibu juu ya hilo nikwamba Allah Mtukufu ametubainishia katika kitabu chake kwamba ni wajibu juu yetu kuyafanyia kazi aliyo sema mtume rehma na amani ziwe juu yake na alio tuonyeshaMwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao(An-Nisaai 80)Na anacho kupeni Mtume chukueni na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu(Al-Hashr 7)Yale ambayo Sunnah imeyabainisha hakika Qur'an imeyaelezea, kwasababu Sunnah nimoja ya kigawanyo katika vigawanyo vya Ufunuo ambao Allah ameuteremsha kwa Mtume wake na akamfundisha, kama alivyo sema Allah Mtukufu:Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hikima na amekufundisha uliyo kuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa(An-Nisaai 113)Kwa sababu hiyo yote yaliyo kuja katika Sunnah basi yamekuja katika kitabu cha Allah Mtukufu.
Enyi Ndugu zangu: kama hayo yamefahamika Je, Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikufa na kuna jambo katika dini linalo mkaribisha mja kwa Allah Mtukufu hajakifundisha?
Kamwe hamna jambo hilo Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake alibainisha kila jitu katika dini ima kwa kusema, au kwa vitendo, ima kwa kukiri ima kwa kulianzisha au kwa kujibu swali alilo ulizwa,Na wakati mwingine Allah anamtuma Bedui kutoka vijijini ili aje kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ili amuulize chochote katika mambo ya dini ambayo hayaulizwi na maswahaba ambao wamekaa kimya na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwasababu hiyo maswahaba walikuwa wanafurahi pindi anapo kuja bedui kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ili kuuliza maswali.Na dalili nyingine inayo kujulisha kuwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake hakuacha chochote katika mambo ambayo watu wanahitaji katika ibada zao miamala na maisha yao ila alibainisha ni kauli ya Allah Mtukufu:Leo nimekukamiliishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislam uwe ndiyo Dini(Al Maida 3)Ikiwa umefahamu hayo ewe muislam basi fahamu yakuwa kila mwenye kuzua sheria yeyote katika dini ya Allah hatakama ana lengo zuri hakika Uzushi wake huo mbali na kuwa ni upotevu lakini inahesabika nikutia dosari katika Dini ya Allah Mtukufu na pia inazingatiwa ni kumkadhibisha Allah mtukufu katika kauli yake:Leo nimekukamilishieni Dini yenu
Kwasababu huyu aliye zua katika dini ya Allah Mtukufu mambo yasiokuwepo katika dini ya Allah kana kwamba anasema kwamba dini ya Allah haija kamilika na imebaki sheria hii ambayo nimewaletea ambayo ninajikurubisha kwayo kwa Allah Mtukufu.
Na jambo la kushangaza ni mwanadamu kuzua uzushi unao fungamana na dhati ya Allah Mtukufu na majina yake na sifa zake kisha anasema kwamba yeye katika uzushi huo anamtukuza Mola wake, na anamtakasa na anatekeleza kauli ya Allah inayo sema:Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mnajua(Al Baqara 22)Hakika utamshangaa huyo anae leta Bida'a katika dini ya Allah inayo ambatana na dhati ya Allah ambayo watu wema walio tangulia hawakuwa nayo wala viongozi wao, kisha anadai kwamba anamtakasa Allah na kumtukuza na kwamba yeye anaifanya kazi kauli ya Allah:Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirikaNa kwamba mwenye kukhalifu hayo atakuwa anafananishwa na kadha wa kadha katika majina mabaya.
Kama unavyo shangaa kutokana na watu wanao leta Bida'a katika dini ya Allah yasio kuwemo katika dini katika mambo ambayo yanahusiana na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na kwamba wanamtukuza Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na kwamba asie taka kuwafuata katika Bida'aa zao atachukiwa na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na mengineyo katika majina mabaya wanayo muita asie waunga mkono katika mambo yao ya Bida'a katika mambo yanayo muhusu Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake.
Na katika maajabu nikwamba mfano wa watu hao wanasema: sisi tunamtukuza Allah na Mtume wake na wao wanapo zua katika dini ya Allah na katika sheria yake ambayo alio kuja nayo Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake mambo ambayo hayamo katika dini, hakika wao bila shaka wanamtangulia Allah na mtume wake katika kutoa hukumu na amesema Allah Mtukufu:Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikiana mwenye kujua.(Al Hujrati 1)
Ndugu zangu: Mimi nakuulizeni kwa ajili ya Allah mtukufu nataka liwe jawabu lenu litoke katika dhamira zenu wala sio katika kuoneana huruma, litokane na dini yenu na sio katika mambo ambayo mnayo yafuata, Mnasemaje kwa watu ambao wanaleta Bida'a katika dini ya Allah mambo ambayo hayamo katika dini sawasawa katika yale ambayo yanahusiana na dhati ya Allah na sifa za Allah na majina yake, au katika mambo ambayo yanaambatana na mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kisha wanasema kwamba sisi ndio tunae mtukuza Allah na mtume wake, je, hao wana stahiki kuwa ni wenye kumtukuza Allah na mtume wake?
au ni watu ambao hawaiachi sheria ya Allah hata kidogo cha ncha ya kidole, wanasema kuhusu yalio kuja katika sheria ya Allah: Tumeamini na tumesadikisha yote tuliyo elezwa, na tumesikia na kutii yale tuliyo amrishwa au kukatazwa, na wanasema katika yale ambayo hayajaletwa na sheria tumekoma na kuyaacha, na haifai kuyatanguliza mbele ya Allah na Mtume wake na hatufai kusema katika dini ya Allah yasio kuwemo, n iyupi mwenye kustahiki kuwa na mapenzi na Allah na Mtume wake na ni mwenye kumtukuza Allah na Mtume wake?
Hakuna shaka kwamba hao walio sema: Tumeamini na kusadikisha yale tulio ambiwa na tumesikia na kutii katika tulio amrishwa, na wakasema tumeacha na kukoma kuyafanya yale ambayo hatukuamrishwa na wakasema sisi hatuna uwezo wowote wala cheo chochote cha kuongeza katika sheria ya Allah mambo ambayo hayamo, au kuzua mambo ambayo hayamo katika dini, bila shaka hao ndio walio jua thamani ya nafsi zao na thamani ya Allah alie waumba, hao ndio walio mtukuza Allah Mtukufu na mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na ndio ambao walio dhihirisha ukweli wa mapenzi yao kwa Allah Mtukufu na Mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake.
Na sio hao wanao leta Bida'a katika dini ya Allah mambo ambayo hayamo katika itikadi ya uislam wala kauli na matendo na wewe utawashangaa watu wanajua kauli ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake:Tahadhalini na mambo ya uzushi, hakika kila uzushi ni Bida'a, na kila Bida'a ni upotevu na kila upotevu ni motoni.Na wanajua kauli ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeKila Bida'aNeno Kila katika hadithi lina kusanya kila aina ya uzushi katika dini na ni herufi yenye nguvu inayo kusanya kila kituKilaNa alie tamka maneno hayo ya jumla ni Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, anajua maana ya tamko hilo, nae nimfaswaha wa viumbe na ndie aliyekuja kuwanasihi viumbe, hatamki chochote ila ni kwa jambo analo jua maana yake, ikiwa ni hivyo hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake pindi alipo sema:Kila Bida'a ni uzushiAlikuwa anajua anacho kisema na alikuwa anajuwa maana yake, na ametamka maneno hayo kwa kuonyesha ukamilifu wa nasaha zake kwa umma wake.Ikiwa yametimia hayo mambo matatu. Ukamilifu wa nasaha, na irada, kisha ubainifu ulio kamilika na ufasaha, na ukamilifu wa elimu na Maarifa, yote hayo yanaonyesha kwamba maneno yanajulisha juu ya maana, je, baada ya maneno hayo inaswihi kugawanya Bida'a vigawanyo vitatu, au vigawanyo vitano?
Hii haiswihi, na walio dai baadhi ya wanachuoni kwamba Bida'a nzuri, hii ina hali mbili:
Isiwe Bida'a lakini adhanie kuwa ni Bida'a
Iwe Bida'a ni mbaya lakini hajui kuwa ni mbaya.
Kila ilivyo daiwa kwamba ni Bida'a nzuri anajibiwa kwa jawabu hii. na kwa sababu hii hakuna njia kwa watu wa Bida'a kuzifanya bidaa zao ni nzuri na katika mikonoo yetu kuna upanga mkali kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeKila Bida'a ni uzushiHakika upanga huu mkali ulitengenezwa katika kiwanda cha utume, haukutengenezwa katika iwanda ambacho hakina uhakika, bali upanga huo umetengenezwa na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake haya maneno ya kina haiwezekani kwa mwenye upanga mkali akakabiliana na yeyote na Bida'a akisema kuwa ni bida'a nzuri na Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anasema:Kila Bida'a ni uzushiKana kwamba nina hisi kuwepo katika nafsi zenu mdudu anaesema yale mnayo sema katia Amiril Mu'uminina Omar Bin Khatwab Radhi za Allah ziwe juu yake, maneno ya kweli wakati alipo muamrisha Ubaya Bin Ka'ab, na Tamima Ad-Daary wawaswalishe watu katika mwezi wa Ramadhani, wakatoka na wakawswalisha watu kisha akasema:Uzuri ulioje wa Bida'a hii na wanao ifanya ibada hii mwisho wa usiku ni bora kuliko mwanzo wa Usiku.Majibu kuhusu hilo yako namna mbili:Namna ya kwanza: ni kwamba haijuzu kwa yeyote kupinga maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwa maneno yeyote sio kwa maneno ya Abubakari ambae ndie mtu bora katika umma huu baada ya Mtume wake, wala kwa maneno ya Omar, ambae ni mtu bora baada ya Mtume wake, wala maneno ya Othmani ambae ni mtu wa tatu bora katika ummah huu baada ya Mtume, wala maneno ya Ally ambae ni mtu wa nne bora katika Ummah huu baada ya Mtume, wala maneno ya yeyote kwa sababu Allah anasema:Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.(An Nur 63)Amesema Imamu Ahmad Allah amrehemuJe, Unajuwa nini maana ya Fitna?Fitna maana yake ni Shirki huwenda akipinga baadhi ya maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ikaingia katika moyo wake shaka ikawa ni sababu ya kuangamia.Mwisho.Na Amesema Ibn Abasi Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake:Inahofiwa kushukiwa na mawe kutoka mbinguni nina wambia Alisema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na nyie mnasema alisema Abubakar na Omar.Namna ya pili: Hakika sisi tunajuwa kwa yaqini kwamba kiongozi wa waislam Omar Bin Khatwab Radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa ni katika watu wenye kutukuza maneno ya Allah na Mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na alikuwa anajulikana kwa kusimama imara katika mipaka ya Allah Mtukufu mpaka alikuwa anasifika kwa kusimama kwenye maneno ya Allah Mtukufu. Ama kisa cha mwanamke ambae alie mpinga Omar katika maswala ya kuweka kikomo cha mahari -Ikiwa kisa hicho ni cha kweli- hakika alimpinga kwa maneno ya Allah mtukufu:Na mtachukuaje na ili hali mmekwisha ingiliana ninyi kwa ninyi na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?(An-Nisaai 21)Akaishia Omar pale alipo pataka katika kuwekea kikomo MahariLakini jambo hili katika usahihi wake kuna shaka, lakini makusudio nikubainisha kwamba Omar radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa amesimama katika mipaka ya Allah Mtukufu alikuwa haivuki, haipaswi kwa Omar radhi za Allah ziwe juu yake,kukhalifu maneno ya bwana wa viumbe Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, kwamba aseme kuhusu Bida'aNeema iliyoje ya hii Bida'aKisha ikawa Bida'a hiyo ndio aliyo ikusudia Mtumu Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwa kauli yake:Kila Bida'a ni upotevuBali hakuna budi iwekwe Bida'a ambayo aliyo isema Omar kuwa sio katika makusudio ya Mtume Rehma na amani ziwe juu yake katika kauli yake:Kila Bida'a ni uzushiOmar Radhi za Allah ziwe juu yake ana ashiria katika maneno yake Neema iliyoje ya hii Bida'a, kuwakusanya watu waswali nyuma ya imamu mmoja, walipo kuwa wanaswali kila mmoja peke yake.Na ilikuwa asili ya kusimama usiku kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika mwezi wa Ramadhani, imethibiti katika sahihi mbili ya Bukhari na Muslim kutokana na hadithi ya Mama Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake, kwamba Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, aliwaswalisha watu kwa muda wa siku tatu na akachelewa kuja siku ya nne, na akasema:Mimi nimechelea isifaradhishwe kwenu mkashindwa kuitekeleza.
Amesema Imamu Ahmad Allah amrehemu
Je, Unajuwa nini maana ya Fitna?
Fitna maana yake ni Shirki huwenda akipinga baadhi ya maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ikaingia katika moyo wake shaka ikawa ni sababu ya kuangamia.
Mwisho.
Na Amesema Ibn Abasi Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake:
Inahofiwa kushukiwa na mawe kutoka mbinguni nina wambia Alisema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na nyie mnasema alisema Abubakar na Omar.
Namna ya pili: Hakika sisi tunajuwa kwa yaqini kwamba kiongozi wa waislam Omar Bin Khatwab Radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa ni katika watu wenye kutukuza maneno ya Allah na Mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na alikuwa anajulikana kwa kusimama imara katika mipaka ya Allah Mtukufu mpaka alikuwa anasifika kwa kusimama kwenye maneno ya Allah Mtukufu. Ama kisa cha mwanamke ambae alie mpinga Omar katika maswala ya kuweka kikomo cha mahari -Ikiwa kisa hicho ni cha kweli- hakika alimpinga kwa maneno ya Allah mtukufu:
Na mtachukuaje na ili hali mmekwisha ingiliana ninyi kwa ninyi na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?
(An-Nisaai 21)
Akaishia Omar pale alipo pataka katika kuwekea kikomo Mahari
Lakini jambo hili katika usahihi wake kuna shaka, lakini makusudio nikubainisha kwamba Omar radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa amesimama katika mipaka ya Allah Mtukufu alikuwa haivuki, haipaswi kwa Omar radhi za Allah ziwe juu yake,kukhalifu maneno ya bwana wa viumbe Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, kwamba aseme kuhusu Bida'a
Neema iliyoje ya hii Bida'a
Kisha ikawa Bida'a hiyo ndio aliyo ikusudia Mtumu Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwa kauli yake:
Kila Bida'a ni upotevu
Bali hakuna budi iwekwe Bida'a ambayo aliyo isema Omar kuwa sio katika makusudio ya Mtume Rehma na amani ziwe juu yake katika kauli yake:
Kila Bida'a ni uzushi
Omar Radhi za Allah ziwe juu yake ana ashiria katika maneno yake Neema iliyoje ya hii Bida'a, kuwakusanya watu waswali nyuma ya imamu mmoja, walipo kuwa wanaswali kila mmoja peke yake.
Na ilikuwa asili ya kusimama usiku kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake katika mwezi wa Ramadhani, imethibiti katika sahihi mbili ya Bukhari na Muslim kutokana na hadithi ya Mama Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake, kwamba Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, aliwaswalisha watu kwa muda wa siku tatu na akachelewa kuja siku ya nne, na akasema:
Mimi nimechelea isifaradhishwe kwenu mkashindwa kuitekeleza.
Kuswali usiku kwa jamaa katika mwezi wa Ramadhani ni Sunnah ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na akaiita Omar Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa ni Bida'a akizingatia kuwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alipo acha kuwaswalisha watu kila mtu alikuwa anaswali peke yake, au mtu ana swali na mwenzake au watu wawili au kikundi kidogo katika msikiti, Kiongozi wa waumini Omar Radhi za Allah ziwe juu yake akaona kwa muono sahihi awakusanye watu nyuma ya imamu mmoja, likawa jambo hilo ni Bida'a kwa kuwarudisha watu kuwa pamoja, na sio kuanzisha ibada mpya aliyo anzisha Omar Radhi za Allah ziwe juu yake, kwa sababu hiyo ni sunnah na ilikuwepo katika zama za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, jambo hilo ni sunnah lakini iliachwa tangu zama za Mtume, mpaka akairejesha Omar Radhi za Allah ziwe juu yake, kwa sababu hii watu wa Bida'a hawawezi kusema kuwa kauli ya Omar ndio sababu ya kusema kuwa Bida'a ni nzuri.
Anaweza kusema msemaji: kuna mambo yaliyo zuliwa na waislam wakayakubali na kuyafanyia kazi na hayakuwa yanajulikana katika zama za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, kama vile kuanzisha shule na kukusanya na kupangilia vitabu, na mfano wa hayo, na hiyo Bida'a waislam waliifanya ni nzuri na wakaifanyia kazi na wakaona kwamba ni katika kazi bora, vipi utakusanya baina ya huo mtazamo ambao unakaribia kuungwa mkono na waislam wote na baina ya kauli ya kiongozi wa waislam na Mtume wao na Mtume wa mola wa ulimwengu Rehma na amani za Allah ziwe juu yake:Kila Bida'a ni uzushiJawabu la hilo: tunasema kwamba kiuhalisia hilo sio Bida'a bali ni njia ya kufanya jambo lililo amrishwa kisheria, na hizo njia zinatofautiana kwa kutofautiana na sehemu na wakati, na kuna kanuni ya kisheria inayo sema: "hakika njia zina hukumu ya kile kinacho kusudiwa kufanywa kupitia njia hiyo" njia ya kukufikisha katika jambo la kisheria hiyo njia nayo inakuwa ya kisheria, na ile inayo kufikisha katika Haram pia inakuwa njia hiyo ni haramu, bali kila njia inyenzo zinazo kufikisha katika haramu hakika nyenzo hizo ni haramu. na Kheri yoyote itakapo kuwa ni njia ya kwenda kwenye shari hiyo kheri inakuwa shari pia na inapaswa kuzuiliwa na msikilize Allah Mwenye nguvu na ametukuka anasema:Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua(An-A'am 108)
Kila Bida'a ni uzushi
Jawabu la hilo: tunasema kwamba kiuhalisia hilo sio Bida'a bali ni njia ya kufanya jambo lililo amrishwa kisheria, na hizo njia zinatofautiana kwa kutofautiana na sehemu na wakati, na kuna kanuni ya kisheria inayo sema: "hakika njia zina hukumu ya kile kinacho kusudiwa kufanywa kupitia njia hiyo" njia ya kukufikisha katika jambo la kisheria hiyo njia nayo inakuwa ya kisheria, na ile inayo kufikisha katika Haram pia inakuwa njia hiyo ni haramu, bali kila njia inyenzo zinazo kufikisha katika haramu hakika nyenzo hizo ni haramu. na Kheri yoyote itakapo kuwa ni njia ya kwenda kwenye shari hiyo kheri inakuwa shari pia na inapaswa kuzuiliwa na msikilize Allah Mwenye nguvu na ametukuka anasema:
Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua
(An-A'am 108)
Na kuwatukana Miungu ya washirikina sio uadui bali ni haki na nimahala pake lakini kumtukana Mola wa viumbe vyote ni uadui na sio haki wala sio mahala pake na ni uadui na dhulma, kwa ajili hiyo ilipokuwa kuwatukana miungu ya washirikina inayo sifiwa ni sababu ya kutukanwa Mwenyezi Mungu ikawa ni haramu na imekatazwa, dalili hii ndio imepelekea kujulikana kuwa nyenzo na njia zina hukumu ya makusudio ya jambo, Shule na kukusanywa na kupangiliwa vitabu pamoja na kwamba havikuepo wakati wa Mtume kwa namna hiyo sio makusudio bali ni njia na ni nyenzo kwa hali hiyo ina chukua hukumu ya malengo yanayo kusudiwa.
Kwa sababu hiyo lau mtu akijenga Madrasa kwa lengo la kufundisha elimu ya Haram, basi kule kujenga kunakuwa haram na akijenga Madrasa kwa lengo la kujifunza sheria basi ile madrasa inakuwa ni halali.
Akisema mtu: Utajibu vp kauli ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake:Mwenye kuanzisha katika uislam jambo zuri atapata malipo na malipo ya atakae ifanyia kazi mpaka siku ya Qiyama.na neno Sunnah lina maana ya kuweka sheriaJawabu: ni kwamba aliye sema:Mwenye kuanzisha katika uislam jambo nzuriNa ndie alie sema:Kila Bida'a ni uzushihaiwezekani itoke kwa Mtume msema kweli na mwenye kusadikishwa kauli inayo kadhibisha kauli nyengine, wala haiwezekani kupingana maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na kamwe haiwezekani maneno yake kuwa na maana zinazo pingana, na yeyote atakae dhani kuwa maneno ya Allah Mtukufu au maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, yanapingana arejee mtizamo wake, hakika dhana hii imetokana na upungufu wa akili yake, au kwa uzembe wake, na haiwezekani yapingane maneno ya Allah Mtukufu au Mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake.Na kama ni hivyo ni kwamba ubainifu wa kuto kupingana katika maneno ya Mtume ni hadithi hiiKila Bida'a ni uzushiKwa hadithiMwenye kuanzisha katika uislam jambo zuriHakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anasema:Mwenye kuanzisha katika UislamNa Bida'a sio katika uislam, kisha anasema nzuriNa Bida'a sio jambo jema, na tofauti baina ya Sunnah na Bida'a
Mwenye kuanzisha katika uislam jambo zuri atapata malipo na malipo ya atakae ifanyia kazi mpaka siku ya Qiyama.
na neno Sunnah lina maana ya kuweka sheria
Jawabu: ni kwamba aliye sema:
Mwenye kuanzisha katika uislam jambo nzuri
Na ndie alie sema:
Kila Bida'a ni uzushi
haiwezekani itoke kwa Mtume msema kweli na mwenye kusadikishwa kauli inayo kadhibisha kauli nyengine, wala haiwezekani kupingana maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na kamwe haiwezekani maneno yake kuwa na maana zinazo pingana, na yeyote atakae dhani kuwa maneno ya Allah Mtukufu au maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, yanapingana arejee mtizamo wake, hakika dhana hii imetokana na upungufu wa akili yake, au kwa uzembe wake, na haiwezekani yapingane maneno ya Allah Mtukufu au Mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake.
Na kama ni hivyo ni kwamba ubainifu wa kuto kupingana katika maneno ya Mtume ni hadithi hii
Kila Bida'a ni uzushi
Kwa hadithi
Mwenye kuanzisha katika uislam jambo zuri
Hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake anasema:
Mwenye kuanzisha katika Uislam
Na Bida'a sio katika uislam, kisha anasema nzuri
Na Bida'a sio jambo jema, na tofauti baina ya Sunnah na Bida'a
Na kuna jawabu lingine: kwamba maana ya hadithi ya mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake nikwamba: Mwenye kuhuyisha sunnah ambayo ilikuwepo ikawa haifanyiwi kazi, kisha akaihuyisha.
Na kuna jawabu la pili ambalo ndio sababu ya mtume kusema maneno hayo: nalo ni kisa cha kundi la watu walio kwenda kwa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na walikuwa na dhiki kubwa na umasikini, Mtume akawahamisha waislam wajitolee kutoa michango kwa ajili yao, akaleta bwana mnoja katika Answar (watu wa madina) mkoba wenye fedha ambao ulikuwa una muelemea kwa uzito akaweka mbele ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, ukawa uso wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake una toa nuru kwa furaha na shangwe na akasema:Mwenye kuanzisha katika uislam jambo nzuri atapata malipo na malipo ya atakae ifanyia kazi mpaka siku ya Qiyama.Na hapa inakuwa maana ya hadithi ni kutekeleza na sio kuanzisha sheria, ikawa maana ya ibaraMwenye kuanzisha katika uislam jambo nzuriMwenye kuifanyia kazi kwa kutekeleza na sio kuweka sheria kwasababu imekatazwa kuweka au kutunga sheria katika Uislam.Kila Bida'a ni uzushi
Mwenye kuanzisha katika uislam jambo nzuri atapata malipo na malipo ya atakae ifanyia kazi mpaka siku ya Qiyama.
Na hapa inakuwa maana ya hadithi ni kutekeleza na sio kuanzisha sheria, ikawa maana ya ibara
Mwenye kuanzisha katika uislam jambo nzuri
Mwenye kuifanyia kazi kwa kutekeleza na sio kuweka sheria kwasababu imekatazwa kuweka au kutunga sheria katika Uislam.
Kila Bida'a ni uzushi
Na juweni ndugu zangu kwamba kumfuata Mtume hakuwi ila kwa mambo yanayo kubalika kisheria katika mambo sita:
1- Sababu, pindi mwanadamu anapo muabudu Allah ibada ilio ambatana na sababu ambayo sio ya kisheria basi ibada hiyo ni Bida'a ambayo inarudishwa kwa alie ifanya, mfano wa hilo: nikwamba baadhi ya watu wana adhimisha usiku wa tarehe ishirini na saba katika mwezi wa Rajab kwa madai kwamba ni usiku wa miraji -usiku alio pandishwa Mtume mbinguni- ibada ya Tahajudi ni ibada ya kisheria lakini ilipo ambatanishwa na sababu hiyo ya kuhuyisha usiku wa miiraji ikawa ni Bida'a, kwasababu imejengewa ibada hiyo kwa sababu ambayo haijathibiti kisheria, na sifa hiyo ya ibada kuafikiana na sababu ya kisheria ni jambo muhimu, na ndio inayo pambanua mambo ya Bida'a kwa watu wengi wanao dhani kuwa ni Sunnah ilihali sio katika Sunnah.
2- Namna ya Ibada, nilazima ibada iwe ni yenye kuafikiana na sheria katiaNamna yake, lau Mtu atamuabudu Allah kwa ibada ambayo namna yake haijafundishwa kisheria basi ibada hiyo haikubaliwi kisheria, Mfano wa hilo: ikiwa mtu atachinja Farasi katika Udhuhiya, kuchinja huko hakuswihi, kwasababu ni kinyume na sheria katika jinsia yake, Udhuhiya haiwi ila katika wanyama wafuatao: Ngamia, Ng'ombe na Kondoo - Mbuzi
3- Kiwango, akitaka mtu kuzidisha swala kwa sababu ni Faradhi, tunasema: Hiyo ni Bida'a na haikubaliki kwasababu inapingana na sheria katika kiwango kilicho wekwa na sheria, nikama vile mtu akiswali Adhuhuri rakaa tano hakika swala yake haiswihi kwa itifaki ya wanachuoni.
4- Namna yake, lau Mtu akitawadha akaanza kuosha miguu yake, kisha akapaka kichwa chake, kisha akaosha mikono yake, kisha uso wake, tunasema: Udhu wake ni batili kwasababu uko kinyume na sheria katika namna yake
5- Muda, lau mtu atachinja Udhuhiya katia siku ya kwanza ya Dhulhija, udhuhiya yake kwa kuwa kinyume na sheria katika muda wake. na nimesikia baadhi ya watu katika mwezi wa ramadhani wanachinja kondoo kwa kujikurubisha kwa Allah, na kuchinja huko ni Bida'a kwa namna hiyo kwa sababu hakuna kujikurubisha kwa Allah katika kuchinja ila kwa Udhuhiya, Hadyu na Akika, ama uchinja katika mwezi wa Ramadhani kwa kuitakidi kupata malipo kwa kuchinja kama vile kuchinja katika Eid ya kuchinja, kufanya hivyo ni Bida'a, ama kuchinja kwa lengo la kula nyama hilo linajuzu.
6- Sehemu, lau Mtu atakaa itikafu katika maeneo ambayo sio msikitini, hakika itikafu yake sio sahihi, kwasababu itikafu haiwi ila msikitini, na mwanamke akisema nataka nikae itikafu sehemu ninayo swalia nyumbani kwangu hiyo itikafu ni batili kwa kukhalifu sheria katika sehemu, pia katika mifano: lau Mtu anataka kufanya kuizunguka Alkaaba (Twawafu) akakuta hakuna nafasi katika sehemu ya kutufu, akaamuwa kutufu nyuma ya msikiti, basi twawafu yake haiswihi, kwa sababu sehemu ya twawafu ni msikitini, amesema Allah Mtukufu kumwambia Ibrahim Kipenzi chake:na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu,(Al Hajj 26)
na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu,
(Al Hajj 26)
Ibada haiwi ni ibada njema ila ikikamilisha masharti mawili:
1. Ni Ikhlaswi. 2. Kufuata alivyo fundisha Allah na Mtume wake, na hili jambo la kufuata halikamiliki ila kwa kukamilika mambo sita yalio tangulia kutajwa.
Na mimi nasema kuwambia hao walio tihaniwa kwa mambo ya Bida'a ambao huwenda malengo yao yakawa mazuri na wanataka kheri, Mkitaka kheri namuapa Allah mmoja hatujuwi njia ya ya kheri kuliko njia ya watu wema walio tangulia radhi za Allah ziwe juu yao.
Enyi ndugu zangu zishikeni Sunnah za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwa magego na piteni njia ya watu wema walio tangulia, fuateni yale walio kuwa nayo na tizameni je mtadhurika na chochote?
Na mimi nasema. ninajilinda kwa Allah kusema mambo ambayo sina ujuzi nayo. ninasema kwamba utakuta wengi katika hao wenye bidii katika kuzuwa mambo katika dini yasio kuwepo wanakuwa wavivu katika kutekeleza yale ambayo yamethibiti katika sheria na yamefanywa na mtume, wanapo maliza kufanya mambio yao ya Bida'aa wanaelekea kufanya ibada zilizo thibiti kwa Mtume kwa Uvivu, hayo yote nimatokeo mabaya ya Uzushi katika nyoyo, Bida'a madhara yake nimakubwa kwenye moyo, na uhatari wake kwenye dini nimkubwa mno, hawakuzuwa watu katika dini ya Allah chochote ila wanapoteza katika yale yalio thibiti katika sunnah mfano wake au zaidi yake, kama walivyo taja hayo baadhi ya watu wema walio tangulia.
Lakini mwanadamu anapo hisi kuwa yeye ni mwenye kufuata na sio mwenye kuweka sheria, basi anapata uchamungu na kunyenyekea na udhalili na anakuwa nimwenye umadhubuti katika kumuabudu Allah mola wa viumbe vyote, na atakuwa ni mkamilifu wa kumfuata kiongozi wa wachamungu na Bwana wa Mitume wote, mjumbe wa mola wa viumbe wote Muhammad Rehma na amani za Allah ziwe juu yake.
Mimi nina elekeza nasaha kwa ndugu zangu wote waislam ambao wamefanya uzushi kuwa jambo zuri sawa sawa katika mambo ambayo yana ambatana na dhati ya Allah, katika majina yake na sifa zake au yale yanayo ambatana na Mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na kumtukuza, wamuogope Allah na waache mambo hayo na wayafanye mambo yao yote ya dini katika msingi wa kufuata na sio kuzuwa, wayafanye kwa Ikhlas na sio kwa kumshirikisha Allah, yawe yamefanywa na Mtume na sio katika Bida'a, awe anayapenda Allah na sio kwa mapenzi ya Shetani na watazame nyoyo zao zitapata nini kutokana na usalama wa maisha na utulivu na raha ya akili na nuru kubwa.
Na ninamuomba Allah Mtukufu atujalie na waongofu wenye kuongoa watu na niviongozi wenye kuwaelekeza watu katika mema, na azitie nuru nyoyo zetu kwa imani na elimu, na asijalie yale tulio jifunza ni mzigo wa kutuangamiza na atuelekeze kupita katika njia ya waja wake waumini na atujalie katika mawalii wake wachamungu na kundi lake walio faulu na swala na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na ali zake na maswahaba zake wote.