الإسلام
نبذة موجزة عن الإسلام كما جاء في القرآن الكريم والسنة النبوية
Uislamu
Dondoo fupi kuhusu uislamu kama ilivyokuja katika Qur'an tukufu na mafundisho ya Mtume rehema na Amani zimfikie.
Ni kitabu muhimu kinachokusanya maana fupi ya uislamu kina bainisha misingi yake mafundisho yake, na mazuri yake kutoka katika vyanzo vyake asili navyo ni Qur'an tukufu na mafundisho ya Mtume, na kitabu kina wahusu watu wazima waislamu na wasiokuwa waislamu kwa lugha zao na katika kila zama na maeneo kwa tofauti ya mazingira na hali.
(Kopi iliyokusanya ushahidi kutoka katika Qur'an tukufu na mafundisho matukufu ya Mtume)
1- Uislamu ndio ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote, na ndio ujumbe wa Uungu wa milele uliohitimisha jumbe zote za Mwenyezi Mungu:
Uislamu ndio ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukukutuma(Hatukukuleta), ewe Mtume, isipokuwa ni kwa watu wote, uwe mtoaji wa habari nzuri na muonyaji.Lakini watu wengi hawaijui. [Suratu Sabai: 28]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote} (259). [Al A'araf: 158]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki kutoka kwa Mola wenu. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikakanusha basi hakika vilivyomo mbinguni na Ardhini ni vya Mwenyezi Mungu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima}. [An Nisaa: 170].
Uislamu ndiyo ujumbe wa Uungu wa milele, nao umehitimisha jumbe zote za Mwenyezi Mungu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakuwa Muhammad ni baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Manabii, Na Mwenyezi Mungu kwa kila jambo miongoni mwa matendo yenu ni mjuzi, hakuna chenye kufichikana Kwake. [Al Ahzaab: 40].
2- Na uislamu siyo dini ya jinsia au watu maalumu, bali yenyewe ni dini ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote.
Na uislamu siyo dini maalumu kwa jinsia au watu fulani, bali ni dini ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote, na amri ya kwanza katika Qu'ran tukufu ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka}. [Al Baqara: 21]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi watu! mcheni Mola wenu aliyekuumbeni nyinyi kutoka katika nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao}. [An Nisaa: 1]. Na kutoka kwa Ibn Omar radhi za Mwenyezi Mungu ziwafikie ya kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alihutubia siku ya Fat-hi Makka (ufunguzi wa mji wa Makka) akasema: "Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba, basi watu wako aina mbili: mwema mchamungu mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na muovu mbaya dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na watu wote ni wana wa Adam, na amemuumba Mwenyezi Mungu Adam kutokana na udongo. Amesema Mwenyezi Mungu: "Enyi watu hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila tofauti tofauti, ili mfahamiane, hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana khabari (za mambo yote)" [Al Hujuraat: 13]. Kaipokea Tirmidhiy (3270). Na hautokuta katika amri za Qur'an tukufu au amri za Mtume mtukufu rehema na Amani zimfikie sheria inayowahusu watu maalumu au kundi kwa kuzingatia miji yao au utaifa wao au jinsia yao.
3- Uislamu ndiyo ujumbe wa Mungu uliokuja kukamilisha jumbe za Manabii na Mitume waliotangulia -sala na Amani ziwafikie- kwa ummati zao.
Uislamu ndiyo ujumbe wa Mungu uliokuja kukamilisha jumbe za Manabii na Mitume waliotangulia -sala na Amani ziwafikie- kwa ummati zao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika sisi tumekuletea wahyi, ewe Mtume, ili ufikishe ujumbe kama tulivyomletea wahyi Nūḥ na Manabii wengine baada yake. Na tumewapelekea wahyi Ibrāhīm, Ismā’īl, Is-ḥāq, Ya‘qūb na Kizazi chake, nao ni Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya wana wa Isrāīl wanaotokana na kizazi cha Ya’qūb, na pia ‘Īsā, Ayyūb, Yūnus, Hārūn na Sulaimān na tukampa Dāwūd Zaburi, nacho ni kitabu na kurasa zilizoandikwa}. [An Nisaa: 163]. Na hii dini ambayo ameifunua Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie ndiyo dini ambayo Mwenyezi Mungu aliifanya kuwa sheria kwa Manabii waliotangulia na akawaamrisha kuifuata. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Amekupeni sheria ya Dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye}. [Al shuuraa: 13]. Na hiki alichokifunua Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad rehema na Amani zimfikie ni kusadikisha yale yaliyotangulia katika vitabu vya Mungu, kama Taurati na Injili kabla havijapindishwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Qur’ani tuliyokuteremshia wewe, ewe Mtume, ndiyo haki inayosadikisha Vitabu Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume Wake kabla yako. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa mambo ya waja Wake, ni Mwenye kuwajua vyema na mwenye kuwaona}. [Faatwir: 31].
4- Manabii Amani iwe juu yao dini yao ni moja na sheria zao zinatofautiana:
Dini ya Manabii Amani iwe juu yao ni moja na sheria zao zinatofautiana. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na tumekuteremshia wewe Kitabu kwa ajili ya kubainisha haki kinachosadikisha vitabu vilivyokuwa kabla yake na kuvihukumia( kuwa haya ndiyo yaliyosalimika) Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana. [Al Maaidah: 48]. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mimi ndiye mtu wa karibu zaidi kwa Issa bin Mariam katika dunia na Akhera, na Manabii wote ni ndugu wa baba mmoja mama zao tofauti na dini yao ni moja". Ameipokea Bukhari (3443).
5- Uislamu unalingania -kama walivyolingania Manabii wote: Nuhu na Ibrahimu na Mussa na Suleimani na Daudi na Issa Amani iwe juu yao- katika imani ya kuwa Mola ni Mwenyezi Mungu muumbaji mgawaji wa riziki muhuishaji na mfishaji, Mfalme wa wafalme, na ndiye anayepangilia mambo naye ni Mpole mno Mwingi wa huruma.
Uislamu unalingania -kama walivyolingania Manabii wote: Nuhu na Ibrahimu na Mussa na Suleimani na Daudi na Issa Amani iwe juu yao- katika imani yakuwa Mola ni Mwenyezi Mungu muumbaji mgawa riziki muhuishaji na mfishaji, Mfalme wa wafalme, na ndiye anayepangilia mambo naye ni Mpole mno Mwingi wa huruma. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi watu! Kumbukeni, neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu.je kuna muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Anayewaruzuku nyinyi mbinguni, na ardhini?. Hapana Mola aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye, Peke Yake, Basi vipi nyinyi mtaepushwa na kumpwekesha? [Faatwir: 3]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anaye miliki kusikia na kuona? Na nani atoaye kilicho hai kutoka kwa kilichokufa, na akamtoa maiti kutoka aliye hai? Na nani anayetengeneza mambo yote? Watasema:Allah, Mwenyezi Mungu. Basi sema: Je! Hamumuogopi? [Yunus: 31]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli. [An Namli: 64].
Na Manabii wote na Mitume amani iwafikie walitumwa kuja kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu, waje katika ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha}. [An Nahli: 36]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukupata kutuma kabla yako, ewe Mtume, mjumbe yeyote ispokuwa tunampatia wahyi kwamba hapana mwenye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu. Basi mtakasieni ibada Yeye Peke Yake. [Al Anbiyaa:25]. Akaeleza Mwenyezi Mungu kuhusu Nuhu Amani zimfikie yakwamba yeye alisema: Na akasema, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na mumnyenyekee kwa kumtii, nyinyi hamna Mola anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Yeye, hakika mimi nawaogopea msishukiwe na adhabu ya Siku ambayo shida yenu itakuwa kubwa, nayo ni Siku ya Kiyama.» [Al A'raf: 59]. Na amesema kipenzi cha Allah Ibrahimu Amani iwe juu yake- kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu kuhusu yeye- amesema: Mkumbuke ewe Mtume na umtaje, Ibrāhīm, amani imshukie, alipowalingania watu wake kwamba: mtakasieni Ibada Mwenyezi Mungu Peke Yake, na muogope hasira Zake kwa kutekeleza faradhi Zake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi. Hilo ni bora kwenu ikiwa mnakijua kilicho chema kwenu kutokana na kilicho kibaya kwenu. [Al A'nkabut: 16]. Na alisema Swaleh Amani iwe juu yake- kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu kuhusu yeye: , «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hamna mola anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Yeye, nimewajia na hoja juu ya ukweli wa yale ninayowaitia kwayo. Nayo ni kuwa nilimuomba Mwenyezi Mungu mbele yenu, Akawatolea kutoka kwenye jiwe hili ngamia mkubwa kama mlivyoomba, basi muacheni ale kwenye malisho yaliyoko kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, na msimfanyie lolote la kumdhuru, mkifanya hivyo, mtapatwa na adhabu iumizayo. » [Al A'raf: 73]. Na alisema Shuaybu Amani iwe juu yake- kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu kuhusu yeye: Hakika tulimtuma, kwa watu wa kabila linalokaa Madyan, ndugu yao Shu'aib, amani imshukie, akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Hamna mola anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Mtakasieni ibada.Hakika imewajia nyinyi hoja, kutoka kwa Mola wenu, juu ya ukweli wa yale ninayowaitia. Watekelezeeni watu haki zao kwa kutimiza vipimo na mizani. Na msiwapunguzie haki zao mkawadhulumu. Wala msifanye uharibifu katika ardhi, kwa ukafiri na kudhulumu, baada ya kuwa imetengenezwa kwa sheria za Mitume waliopita, amani iwashukie. Hayo niliyowaitia nyinyi ni bora kwenu katika ulimwengu wenu na Akhera yenu, iwapo nyinyi ni wenye kuniamini katika yale ninayowaitia, ni wenye kuzifuata sheria za Mwenyezi Mungu kivitendo. » [Al A'raf: 85].
Na maneno ya kwanza kabisa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwambia Mussa alisema: Na mimi nimekuteua , ewe Mūsā, kwa ujumbe wangu, basi sikiliza yale unayoletewa ya wahyi kutoka kwangu. Mimi Ndiye Mwenyezi Mungu, hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki ispokuwa mimi, sina mshirika, basi niabudu mimi na usimamishe Swala ili unikumbuke ndani yake. [Twaha: 13-14]. Na amesema Mwenyezi Mungu akimuelezea Mussa Amani iwe juu yake, yakwamba yeye alitaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu akasema: Na Mūsā akasema kumwambia Fir'awn na viongozi wa mamlaka yake, «Mimi nimeomba hifadhi kwa Mola wangu na Mola wenu, enyi watu, Anihifadhi na kila mwenye kiburi cha kukataa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, asiyeiamini Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atawahesabu viumbe Wake.» [Ghafir: 27]. Na akaeleza Mwenyezi Mungu kuhusu Masihi Amani zimfikie yakwamba yeye alisema: «Hakika Mwenyezi Mungu Ambaye ninawalingania nyinyi Kwake Ndiye Peke Yake Mola wangu na Mola wenu, basi muabuduni Yeye. Mimi na nyinyi tuko sawa katika uja wetu na unyenyekevu wetu Kwake. Na hii ndio njia iliyonyooka sawa.» [Al-Imran: 51]. Na vilevile Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza kuhusu Masihi Amani zimfikie - yakwamba yeye alisema: {Enyi wana wa israeli muabuduni Mwenyezi Mungu Mola wangu na Mola wenu, hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu amemharamishia pepo na makazi yake ni motoni, na madhalimu hawatokuwa na wa kuwanusuru}. [Al Maaidah: 72].
Bali hata Taurati na Injili ndani yake kuna mkazo juu ya ibada ya Mwenyezi Mungu peke yeke, imekuja katika kumbukumbu la torati kauli ya Mussa amani iwe juu yake: (sikia ee Israeli! Bwana Mungu wetu ni Mungu mmoja). Na umekuja mkazo juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Injili ya Marko pale aliposema Masihi Amani iwe juu yake: (Hakika usia wa kwanza ni: sikia ee Israeli! Bwana Mungu wetu ni Mungu mmoja).
Na akabainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa Manabii wote walitumwa kwa jukumu hili kubwa nalo ni kuwaita watu wampwekeshe Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa hakika tulipeleka kwa kila umma uliopita mjumbe wa kuwaamrisha wao kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii Peke Yake, na kuacha kumuabudu asiyekuwa Yeye miongoni mwa Mashetani, mizimu, wafu na vinginevyo kati ya vile vinavyotegemewa badala ya Mwenyezi Mungu. Basi wakawa miongoni mwao wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaongoa wakafuata njia ya Mitume, na kati yao wakapatikana wakaidi waliofuata njia za upotofu, hapo ikapasa kwao upotevu na Mwenyezi Mungu hakuwapa taufiki. Basi tembeeni katika ardhi na mjionee kwa macho yenu vipi yalivyokuwa marejeo ya hawa wakanushaji na maangamivu yaliyowashukia, mpate kuzingatia? [An Nahli: 36]. Na amesema Allah Mtukufu: Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa makafiri, “Je, mnawaona waungu na masanamu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Hebu nionyesheni, ni sehemu gani waliyoiumba katika ardhi? Au kwani wao wana fungu katika uumbaji mbingu? Nileteeni kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu kabla ya hii Qur’ani au athari iliyosalia ya elimu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.» [Al Ahqaaf: 4]. Amesema Sheikh Ssa'diy Mwenyezi Mungu amrehemu: (Fahamu ya kwamba mijadala ya washirikina katika ushirikina wao haijaegemezwa kwenye hoja wala ushahidi, bali wametegemea dhana za uongo, na rai zilizo haribika, na akili mbovu, kinachokujulisha juu ya ubovu wake ni kusoma hali zao na kufuatilia elimu zao na matendo yao, na kutazama hali za wale walioumaliza umri wao kwa ibada, je vimewasaidia (Yaani hivi vinavyoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu) vimewasaidia chochote katika Dunia na Akhera?) Tafsiirul Kariimul Mannaan: 779.
6- Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye muumbaji na ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa peke yake, na asiabudiwa pamoja naye yeyote asiyekuwa yeye.
Mwenyezi Mungu ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, na asiabudiwe pamoja naye yeyote asiyekuwa yeye, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wito utokao kwa Mwenyezi Mungu kwa binadamu wote: Muabuduni Mwenyezi Mungu Ambaye Amekuumbeni nyinyi, na akawaumba waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mwenyezi mungu. Mola wenu ambaye amewafanyia ardhi iwe ni tandiko, ili maisha yenu yawe mepesi juu yake, na mbingu ziwe zimejengeka madhubuti, na Akateremsha mvua kutoka kwenye mawingu, Akatoa kwa mvua hiyo matunda na mimea aina mbalimbali ili iwe ni riziki kwenu. Basi, msimuwekee Mwenyezi Mungu washirika katika ibada, hali nyinyi mnajua kuwa Mwenyezi Mungu Amepwekeka katika kuumba, kuruzuku na kustahiki kuabudiwa. [Al Baqara: 21-22]. Basi yule aliyetuumba sisi na akaumba vizazi vilivyokuwa kabla yetu na akaifanya ardhi kuwa ni tandiko na akateremsha juu yetu kutoka mawinguni maji, akatutolea kupitia maji hayo matunda kuwa ni riziki kwetu; huyo ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake. Na amesema Mtukufu: Enyi watu! Kumbukeni, kwa nyoyo zenu, ndimi zenu na viungo vyenu, neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Hakuna muumba wenu isipokuwa Mwenyezi Mungu, Anayewaruzuku nyinyi kwa mvua kutoka mbinguni, na kwa maji, madini na vinginevyo kutoka ardhini. Hapana Mola isipokuwa Yeye, Peke Yake, Asiye na mshirika. Basi vipi nyinyi mtaepushwa na kumpwekesha? [Faatwir: 3]. Yule anayeumba na kutoa riziki ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Huyo, enyi washirikina, Ndiye Mola wenu, hapana Mwenye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Yeye; Mwenye kuumba kila kitu. Basi mfuateni na mumnyenyekee kwa kumtii na kumuabudu. Na Yeye ni Mlinzi wa kila kitu. [Al An'am: 102].
Na kila kinachoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu hicho hakistahiki kuabudiwa, kwasababu hakimiliki hata uzito wa punje ndogo mbinguni wala ardhini wala hakina ushirika na Mwenyezi Mungu katika chochote, wala si kisaidizi chake wala hakimsaidii Mwenyezi Mungu, ni vipi anaombwa pamoja na Mwenyezi Mungu au anawekwa mshirika wake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, ewe Mtume, uwaambie washirikina, «Waiteni wale ambao mlidai kuwa wao ni washirika wa Mwenyezi Mungu mkawaabudu badala Yake , miongoni mwa masanamu , Malaika na binadamu, na wakusudieni katika haja zenu. Kwani wao hawatawaitika. Wao hawamiliki chochote, mbinguni wala ardhini, hata kadiri ya uzito wa chungu mdogo, na wala hawana ushirika katika hizo mbili. Na hakuna yeyote miongoni mwa hawa washirikina mwenye kumsaidia kuumba chochote. Bali Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, ndiye Aliyepwekeka kwa uumbaji. Yeye Ndiye Anayeabudiwa Peke Yake, na hakuna mwingine yeyote asiyekuwa Yeye anayestahiki kuabudiwa. [Sabai: 22].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyeumba hivi viumbe na akavifanya viwepo kutoka katika hali ya kutokuwepo, hili linaonyesha uwepo wake na ulezi wake na uungu wake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu zinazoonyesha ukubwa wake na ukamilifu wa uweza Wake, ni kuwa Alimuumba baba yenu Ādam kutokana na mchanga, kisha nyinyi binadamu mnaenea kwenye ardhi kwa kuzaliana mnatafuta fadhila za Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa alama zenye kuonyesha ukubwa Wake na ukamilifu wa uweza wake ni kuwa Amewaumba wake kwa ajili yenu kutokana na jinsi yenu, enyi wanaume, ili nafsi zenu zijitulize kwao na ziburudike, na Akatia mapenzi na huruma baina ya mwanamke na mumewe. Hakika katika uumbaji huo wa Mwenyezi Mungu pana alama zenye kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu na kupwekeka Kwake kwa watu wenye kufikiria na kuzingatia. Na miongoni mwa dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu ni uumbaji mbingu na kuwa juu kwake bila ya nguzo, na uumbaji ardhi ikiwa imekunjuka na kupanuka, na kutofautiana lugha zenu na kuwa mbalimbali rangi zenu. Hakika katika hayo kuna mazingatio kwa kila mwenye elimu na busara. Na miongoni mwa dalili za uweza huu ni kuwa Mwenyezi Mungu Amewawekea usingizi uwe ni mapumziko kwenu ya usiku au mchana, kwani katika kulala yanapatikana mapumziko na kuondokewa na uchovu, na Amewawekea mchana ambapo ndani yake mnaenda huku na kule kutafuta riziki. Hakika katika hayo kuna dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu na upitishaji matakwa Yake kwa watu wanaosikia mawaidha usikiaji wa kutia akilini, kufikiria na kuzingatia. Na miongoni mwa dalili za uweza Wake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake ni kuwaonyesha umeme, mkaogopa vimondo na mkawa na matumaini ya mvua, na Anateremsha mvua kutoka mawinguni ikahuisha ardhi baada ya kuwa katika hali ya ukame na ukavu. Hakika katika hayo kuna dalili ya ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu na ukubwa wa hekima Yake na wema Wake kwa kila Mwenye akili ya kujiongoza. Na miongoni mwa alama Zake zenye kuonyesha uweza Wake ni kuwa mbingu na ardhi zinasimama, zinatulia na zinajikita kwa Amri Yake, zisitikisike na mbingu isianguke juu ya ardhi, kisha Mwenyezi Mungu Atakapowaita nyinyi kwenye kufufuliwa Siku ya Kiyama, muda si muda mtajikuta mnatoka makaburini kwa haraka. Ni wa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, wote waliyoko mbinguni na ardhini, miongoni mwa Malaika, binadamu, majini, wanyama, mimea na visivyo na uhai, wote hao wanafuata amri Yake wanaunyenyekea ukamilifu Wake. {Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyingine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake} (49). [Ar rum: 20-27].
Na alikanusha Namrudi juu ya uwepo wa Mola wake, Ibrahim -Amani iwe juu yake- akasema kumwambia, kama alivyoelezea Mwenyezi Mungu: {Akasema Ibrahim, 'Hakika Mwenyezi Mungu analileta jua kutoka mashariki basi lilete kutoka magharibi, akaduwaa yule aliyekufuru, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu}. [Al Baqara: 258]. Na hivyohivyo Ibrahim alitoa ushahidi kwa watu wake ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyemuongoza na ndiye aliyemlisha na kumnywesha na anapougua ndiye anayemponya, na ndiye anayemfisha na kumhuisha, akasema, kama Mwenyezi Mungu alivyoeleza: Yeye Ndiye Aliyeniumba kwa sura nzuri zaidi. Yeye ananiongoza kwenye maslahi ya dunia na Akhera. Na Yeye Ndiye Anayenineemesha kwa chakula na kinywaji. Na nikipatwa na ugonjwa, Yeye Ndiye Anayeniponyesha. Na Yeye Ndiye Atakayenifisha duniani kwa kuichukua roho yangu, kisha Atanihuisha Siku ya Kiyama, hakuna awezaye hilo ispokuwa Yeye. [As shu'araa: 78-81]. Na amesema Mwenyezi Mungu akimuelezea Nabii Mussa Amani iwe juu yake ya kwamba yeye alitoa hoja kumpa Firauni akasema kumwambia: Hakika Mola wake ndiye: {Aliyekipa kila kitu umbile lake kisha akakiongoza}. [Twaaha: 50].
Na Mwenyezi Mungu amemdhalilishia mwanadamu vyote vilivyoko mbinguni na ardhini na akamzungushia neema; ili amuabudu Yeye na wala asimkufuru, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwani hamuoni, enyi watu, kuwa Mwenyezi Mungu amewadhalilishia vilivyoko mbinguni miongoni mwa jua, mwezi, mawingu na vinginevyo, na vilivyoko ardhini miongoni mwa wanyama, miti, maji na vinginevyo visivyodhibitika, na Akaeneza kwenu neema Zake za nje juu ya miili na viungo, na za ndani, kwenye akili na nyoyo, na zile Alizowawekea katika zile msizozijua? Na miongoni mwa watu kuna anayefanya ushindani juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada bila ya hoja wala ubainifu wala kitabu chenye kubainisha kinachofafanua uhakika wa madai yake. [Luqman: 20]. Na kama Mwenyezi Mungu alivyomdhalilishia mwanadamu vyote vilivyoko mbinguni na ardhini pia amemuumba na akamuandaa kwa kila anayoyahitajia kama maskio macho na moyo, ili ajifunze elimu inayoweza kumnufaisha na imuelekeze kwa Mola wake na Muumba wake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenyezi Mungu , Aliyetakata na kutukuka, Amewatoa nyinyi kutoka kwenye matumbo ya mama zenu baada ya kipindi cha mimba, hali hamtambui chochote kilichoko pembezoni mwenu, na akawapatia sababu za kutambua miongoni mwa masikio ya kusikia na macho ya kuonea na nyoyo, huenda nyinyi mkamshukuru. [An Nahli: 78].
Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaumba walimwengu wote hawa, na akamuumba mwanadamu na akamuandalia kila analolihitajia katika viungo na nguvu, kisha akamkunjulia kila yanayoweza kumsaidia kusimamia ibada za Mwenyezi Mungu, kisha akamdhalilishia vyote vilivyoko mbinguni na ardhini.
Na akatoa hoja Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake kupitia hivi viumbe vyake vikubwa juu ya uumbaji na umiliki na ulezi wake unaopelekea katika uungu wake, akasema aliyetakasika na kutukuka: Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa, «Ni nani anayewaruzuku kutoka juu kwa mvua anayoiteremsha, na kutoka ardhini kwa mimea na miti aina mbalimbali anayoiotesha kutoka humo, ambayo miongoni mwayo mnakula nyinyi na wanyama wenu? Na ni nani anayemiliki hisia za kusikia na za kuona mnazostarehea, nyinyi na wengineo? Na ni nani anayemiliki uhai na kifo, katika ulimwengu wote, akawatoa wenye uhai na wafu, baadhi yao kutoka kwa wengine, katika viumbe mnavyovijua na msivyovijua? Na ni nani anayeyaendesha mambo ya mbinguni na ardhini na yaliyomo ndani yake, (anayeyaendesha) mambo yenu nyinyi na mambo ya viumbe vyote?» Watakujibu kwamba anayefanya yote hayo ni Mwenyezi Mungu. Waambie, «Basi si muogope mateso ya Mwenyezi Mungu mnapomuabudu mwingine pamoja naye?» [Yunus: 31]. Na amesema kweli Mola aliyetakasika: Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa makafiri, “Je, mnawaona waungu na masanamu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Hebu nionyesheni, ni sehemu gani waliyoiumba katika ardhi? Au kwani wao wana fungu katika uumbaji mbingu? Nileteeni kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu kabla ya hii Qur’ani au athari iliyosalia ya elimu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.» [Al Ahqaaf: 4]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ameziumba mbingu bila nguzo (mihimili) mzionazo, na ameiweka milima katika ardhi ili (ardhi) isikuyumbisheni; naye ametawanya humo wanyama wa kila aina, na tumeyateremsha maji kutoka mawinguni, na humo tumeotesha (mimea) mizuri ya kila aina. Vyote hivi ameviumba Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheni ni nini walichoumba wale asiyokuwa yeye}. Lakini madhalimu wa nafsi zao wamo katika upotofu uliodhahiri}. [Luqman: 10-11]. Na amesema kweli Mola aliyetakasika: Je, wameumbwa hawa washirikina bila kuwako mwenye kuwaumba na kuwapatisha au wao wamejiumba wenyewe? Na yote mambo mawili haya yametenguka na hayawezekani. Na kwa hivyo, inalazimika kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewaumba, na Yeye Peke Yake Ndiye Ambaye hakuna anayepasa kuabudiwa, wala kufaa kuabudiwa, ispokuwa Yeye. Au wao wameumba mbingu na ardhi kwa utengenezaji huu wa kipekee? Bali wao hawaamini adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa wao ni washirikina. Au wanazo wao hazina za Mola wako wanazitumia? Au wao ni majabari wanaowagandamiza viumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kuwatenza nguvu na kuwanyanyasa? Mambo si hivyo, bali wao ndio waelemevu walio madhaifu. [Attur: 35-37]. Amesema Sheikh Sa'diy: (Na huu ni ushahidi kwao kwa jambo ambalo hawana namna ila ni kuukubali ukweli au kujitoa (kutokubaliana) na aliyeweka akili na dini. Tafsiri Ibn Sa'diy: 816.
Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa vyote vilivyoko ulimwenguni, katika vile tunavyoviona na vile tusivyoviona, na kila kisichokuwa yeye hicho ni kiumbe katika viumbe vyake, na Mwenyezi Mungu mbingu ameziumba na ardhi kwa muda wa siku sita.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye muumba wa vyote vilivyoko ulimwenguni, katika vile tunavyoviona na vile tusivyoviona, na kila kisichokuwa yeye hicho ni kiumbe katika viumbe vyake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Waambie washirikina, ewe Mtume, «Ni nani muumba mbingu na ardhi na mwenye kuziendesha?» Sema, «Mwenyezi Mungu Ndiye Muumba Mwenye kuziendesha. Na nyinyi mnalikubali hilo.» Kisha waambie ukiwalazimisha hoja, «Je, mnawafanya wasiokuwa Yeye ni waabudiwa wenu, na hali ya kuwa wao hawawezi kuzinufaisha nafsi zao au kuzidhuru, wacha kule kuwanufaisha nyinyi au kuwadhuru, na mkaacha kumuabudu mwenye kuwamiliki wao?» Waambie, «Kwani analingana kwenu nyinyi kafiri, ambaye ni kama kipofu, na Muumini, ambaye ni kama anayeona? Au kwani unalingana kwenu nyinyi ukafiri, ambao ni kama giza, na Imani, ambayo ni kama mwangaza? Au ni kwamba wale wasimamizi wao wanaowafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu wanaumba kama Anavyoumba, vikawatatiza viumbe vya washirika na viumbe vya Mwenyezi Mungu, ndipo wakaitakidi kwamba wao wanastahiki kuabudiwa?» Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ni Muumba kila kilichoko ambacho hakikuwako; Yeye Ndiye Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake na Yeye Ndiye Aliye mmoja Mwenye kutenza nguvu Anayestahiki uungu na ibada, na sio masanamu na mizimu isiyodhuru wala kunufaisha.» [Arra'di: 8]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na anaumba msivyovijua}. [An Nahli: 8].
Na Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi katika siku sita. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi kisha Akawa juu ya 'Arsh Yake iliyo juu ya viumbe Vyake vyote kuwa Juu kunakonasibiana na utukufu Wake. Anavijua vinavyoingia ardhini, miongoni mwa mbegu, mvua na visivyokuwa hivyo, na vinavyotoka humo miongoni mwa mimea, nafaka na matunda, na vinavyoshuka kutoka mbinguni, miongoni mwa mvua na vinginevyo, na vinvyopanda huko, miongoni mwa Malaika na matendo (ya waja), na Yeye , kutakasika ni Kwake, Yuko pamoja na nyinyi kwa ujuzi Wake popote mnapokuwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona matendo yenu mnayoyafanya na Atawalipa kwayo. [Al Hadiid: 4]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika tuliumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili miongoni mwa viumbe kwa muda wa Siku sita, na hatukupata tabu yoyote wala shida. Katika uweza huu mkubwa kuna dalili ya nguvu zaidi ya kuwa Yeye, Aliyetakasika, Ana uweza wa kuhuisha wafu. [Qaaf: 38].
8- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mshirika katika Ufalme wake au katika uumabji wake na upangiliaji wake au ibada zake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mfalme wa wafalme hana mshirika katika kuumba kwake na Ufalme wake au kupangilia kwake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa makafiri, “Je, mnawaona waungu na masanamu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Hebu nionyesheni, ni sehemu gani waliyoiumba katika ardhi? Au kwani wao wana fungu katika uumbaji mbingu? Nileteeni kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu kabla ya hii Qur’ani au athari iliyosalia ya elimu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.» [Al Ahqaaf: 4]. Amesema Sheikh Ssa'diy Mwenyezi Mungu amrehemu: (Yaani: {sema} kuwaambia hawa waliomshirikisha Mwenyezi Mungu na masanamu na mizimu ambayo haimiliki manufaa wala madhara wala mauti wala uhai wala kufufua, sema kuwaambia- Ukibainisha kushindwa kwa masanamu yao, nakuwa hayo hayastahiki chochote katika ibada: {Hebu nionyesheni, ni sehemu gani waliyoiumba katika ardhi? Au kwani wao wana fungu katika uumbaji mbingu?} Je, wameumba chochote katika nyota za mbingu na ardhi? Je wameumba hata mlima? Je wamepasua hata mito? je wametawanya hata wanyama? Je wameotesha hata miti? Je walitoa msaada wowote katika kuviumba hivyo? hakuna chochote katika hayo, kwa kukiri kwao wao wenyewe, achilia mbali watu wengine, basi huu ni ushahidi wa kutumia akili tu, wenye kukata moja kwa moja yakwamba vyote visivyokuwa Mwenyezi Mungu ibada zake ni batili.
Kisha akaeleza kukosekana kwa ushahidi wa kimaandishi akasema: {Nileteeni kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu kabla ya hii Qur’ani} kitabu kinacholingania katika ushirikina {au athari iliyosalia ya elimu} Iliyorithiwa kutoka kwa Mitume wakiamrisha hivyo. Kinachojulikana nikuwa wao walishindwa kuleta kutoka hata kwa mmoja katika Mitume ushahidi unaothibitisha hivyo, bali tunatoa maamuzi na tunajipa uhakika kuwa Mitume wote waliwaita watu katika kumpwekesha Mola wao, na walikataza ushirikina nalo ni jambo kubwa linaloathiri kwao katika elimu). Tafsiri Ibn sa'diy: 779.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mfalme wa wafalme hana mshirika katika ufalme wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema ,ewe Nabii, ukielekea kwa Mola wako kwa dua, «Ewe Ambaye Una ufalme wote, Wewe Ndiye Ambaye Unamtunuku ufalme, mali na umakinifu katika ardhi Umtakaye miongoni mwa waja Wako, na Unauondoa ufalme kutoka kwa Umtakaye. Na Unampa enzi ya ulimwengu na ya Akhera Unayemtaka, na Unamfanya awe na unyonge Unayemtaka. Kheri ipo mikononi mwako. Wewe, Peke Yako, juu ya kila kitu , ni Muweza.» Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya Mkono kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayonasibiana na Yeye, utakatifu ni Wake. [Al-Imran: 26]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha kuwa ufalme kamili ni wake siku ya Kiyama: Siku ya Kiyama watajitokeza viumbe mbele ya Mola wao, hakuna chochote kuhusu wao au kuhusu matendo yao waliyoyafanya ulimwenguni kitakachofichikana kwa Mwenyezi Mungu. Hapo Atasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Ni wa nani ufalme na mamlaka Siku ya Leo?» Na Ajijibu Mwenyewe, «Ni vya Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake, Mwenye kutenza nguvu Aliyevilazimisha viumbe vyote kwa uwezo Wake na enzi Yake.» [Ghaafir: 16}.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mshirika katika Ufalme wake au katika uumabji wake na upangiliaji wake au ibada zake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na useme, «Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, ukamilifu na sifa njema ni Zake, Aliyeepukana na mwana na mshirika katika uungu Wake. Na Mwenyezi Mungu Hana msaidizi yeyote kati ya viumbe vyake, Yeye Ndiye Mkwasi na Ndiye Mwenye nguvu., na wao ndio mafukara wanaomuhitajia.» Na umtukuze matukuzo yaliyotimu, kwa kumsifu, kumuabudu Peke Yake bila ya mshirika, na kumtakasia Dini yote.» [Al Israai: 111]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ambaye Ana ufalme wa mbingu na ardhi, Hakujifanyia mtoto na hakuwa na mshirika katika ufalme Wake. Na Yeye Ndiye Aliyeumba kila kitu, Akakisawazisha kulingana na umbo linalonasibiana nacho na inavyotakikana kulingana na hekima Yake, pasi na kupungua wala kwenda kombo. [Al Furqaan: 2]. Yeye ndiye Mfalme na visivyokuwa yeye hivyo ni mamluki (vyenye kumilikiwa) na Yeye Mtukufu, na Yeye ndiye muumbaji na visivyokuwa yeye ni viumbe (vyenye kuumbwa) na Yeye ndiye anayepangilia mambo, na mwenye kuwa na hali hizi huyo ni lazima kuabudiwa, na ibada za asiyekuwa yeye ni upungufu wa akili na ni ushirikina wenye kuiharibu Dunia na Akhera. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mayahudi walisema kuwaambia umma wa Mtume Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie yeye, “Ingieni kwenye dini ya Kiyahudi mtapata uongofu. Na Wanaswara waliwaambia kama hayo. Waambie, ewe Mtume, “Uongofu ni kuwa sote tufuate Mila ya Ibrāhīm ambaye alijiepusha na kila dini ya ubatilifu na kufuata Dini ya haki, na hakuwa ni miongoni mwa waliomshirikisha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.” [Al Baqara: 135]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakuna yeyote aliye mwema wa dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake, kwa moyo wake na viungo vyake vyote, hali ya kuwa ni mwema wa maneno na vitendo, mwenye kufuata amri ya Mola wake, akawa amefuata mila ya Ibrāhīm na Sheria aliyoileta na amejiepusha na itikadi mbaya na sheria zilizo batili. Na Mwenyezi Mungu Alimteua Ibrāhīm, rehema na amani zimshukie, na Akamfanya ni msafiwa Wake miongoni mwa viumbe Wake. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya al-khullah (ubui-Mapenzi ya ndani) kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, nayo ni daraja ya juu kabisa ya mapenzi na uteuzi. [An Nisaai: 125]. Na Mola wa Haki Mtukufu akabainisha kuwa mweye kufuata mila isiyokuwa ya Ibrahim Amani imshukie atakua kaitia ujinga nafsi yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakuna yeyote anayeipa mgongo Dini ya Ibrahim, nayo ni Uislamu, ispokuwa anaeitia nafsi yake katika upumbavu aliye mjinga. Na hakika tulimchagua Ibrahim duniani kuwa Nabii na Mtume, na kesho Akhera kuwa ni miongoni mwa watu wema ambao wana daraja za juu kabisa. [Al Baqara: 130].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuzaa wala hakuzaliwa na hana anayeendana naye wala hana mfano:
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuzaa wala hakuzaliwa na hana anayeendana naye wala hana mfano. Amesema Mola wa Haki Mtukufu: Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo. Mwenyezi Mungu ndiye mwenyekukusudiwa kwakila haja (2) Hakuzaa wala hakuzaliwa (3) «Wala hakuna yeyote katika viumbe Vyake mwenye kufanana wala kushabihiyananaye katika Majina Yake, Sifa Zake wala vitendo Vyake.» [Al Ikhlaswi: 1-4]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake, Ndiye Mmiliki, Muumba na Mwendeshaji wa hivyo vyote, basi muabudu Yeye Peke Yake, ewe Nabii, na uvumilie katika kumtii, wewe na waliokufuata, Hana mfano Wake kwa kitu chochote katika dhati Yake, sifa Zake na vitendo Vyake.» [Mariam: 65]. Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zake zimetukuka: Muumba mbingu na ardhi na Muanzilishi wa kuzitengeneza kwa uweza Wake na matakwa Yake na hekima Yake. Amewapatia nyinyi wake wanaotokana na nyinyi ili mjitulize kwao, na Amewapatia nyinyi wanyama-hawa wa kila aina, wa kiume na wa kike. Anawafanya nyinyi muwe wengi kwa kuzaana kwa njia hii ya kuingiliana. Hakuna kinachofanana naye, nae ni mwenyekusikia na ni mwenye kuona. [Ash-shura: 11].
10- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu haingii katika kitu chochote, wala hawi kiwiliwili katika kiumbe chake chochote:
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu haingii katika kitu chochote, wala hawi kiwiliwili katika kiumbe chake chochote, na wala haungani na chochote; hayo ni kwasababu Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji na asiyekuwa yeye huyo ameumbwa, na yeye ndiye mwenye kubakia, na asiyekuwa yeye mwisho wake ni kumalizika, na kila kitu ni milki yake na yeye ndiye mmiliki wake, Mwenyezi Mungu hawezi kuingia katika chochote katika viumbe vyake katika dhati yake yeye aliyetakasika, na Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka ni Mkubwa kuliko kila kitu, na ni Mtukufu kuliko kila kitu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akikanusha juu ya madai ya kwamba Mwenyezi Mungu aliingia kwa Kristo (Alifanyika mwili). Kwa hakika wamekufuru Wanaswara wanaosema kwamba Mwenyezi Mungu ni Al-Masīh mwana wa Maryam. Sema, ewe Mtume, kuwaambia Wanaswara hawa wajinga, «Lau Al-Masīh angelikuwa Mungu, kama wanavyodai, angeliweza kuuzuia uamuzi wa Mwenyezi Mungu ukimjia wa kumwangamiza yeye na mama yake na watu wote wa ardhini. Na mama yake ‘Īsā alikufa, hakuweza kumkinga na kifo. Vilevile hawezi kujitetea nafsi yake. Kwani wote wawili ni waja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, hawawezi kujiepusha na maangamivu. Hii ni dalili kuwa yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Na vitu vyote vilivyoko mbinguni na ardhini ni milki ya Mwenyezi Mungu, Anaumba na kupatisha anachotaka na yeye ni muweza wa kila kitu. Hakika ya tawhīd (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) inawajibisha kupwekeka kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa sifa za umola na uungu; hakuna yeyote anayeshirikiana naye, katika viumbe Wake, kwa hilo. Na mara nyingi sana watu huingia kwenye ushirikina na upotevu kwa kuwatukuza Mitume na watu wema kupita kiasi, kama walivyopita kiasi Wanaswara katika kumtukuza Al-Masīh. Ulimwengu wote ni wa Mwenyezi Mungu, na viumbe viko kwenye mkono Wake Peke Yake. Na miujiza na alama kubwa zinazodhihiri, marejeo yake ni Mwenyezi Mungu. Anaumba, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, na Anafanya Anachotaka. [Al Maaidah: 17]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni za mwenyezi mungu pande zote mbili mashariki na magharibi ,ba si popota mgeukiapo alikokuamrisheni mwenyezi mungu mtazikuta huko radhi zake,bila shaka mwenyezi ni mwenye wasaa na mwenyekujua. Na walisema Mayahudi na Wanaswara, “Mwenyezi Mungu Amejifanyia mtoto.” Ameepukana Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, na neno hilo la batili! Kwani wote walioko mbinguni na ardhini ni milki Yake na ni watumwa Wake. Wote wanamnyenyekea Yeye na wanapelekwa wakiwa chini ya uendeshaji Wake. Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Muumba mbingu na ardhi, bila ya kuwa na mfano uliotangulia. Na Anapolikadiria jambo na Akataka liwe, huliambia, “Kuwa,” likawa. [Al Baqara: 115-117]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na walisema, 'Mwingi wa rehema amejifanyia mwana'} (88) Kwa hakika mmeleta, jambo kubwa lililo baya (89). Zinakaribia mbingu kupasuka kwa ubaya mkubwa wa neno hilo, ardhi kuvunjika vipande-vipande na majabali kuanguka kwa nguvu kwa kukasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (90). Kwa kudai kwao kuwa Mwingi wa rehema na mtoto (91). Na Haifai kwa Mwenyezi Mungu na hainasibiani na Yeye Awe na mtoto, kwani kuwa na mtoto ni dalili ya upungufu na mahitajio, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mkwasi Mwenye kuhimidiwa Aliyeepushwa na sifa zote za upungufu (92). Hakuna aliye mbinguni, miongoni mwa Malaika, wala aliye ardhini, miongoni mwa binadamu na majini, isipokuwa atamjia Mola wake Siku ya Kiyama akiwa ni mja mdhalilifu mnyenyekevu mwenye kukubali uja wake Kwake (93). Amewadhibiti viumbe Wake wote na anaijua idadi yao, hakuna yeyote miongoni mwao mwenye kufichikana kwake (94). Na kila mtu, miongoni mwa viumbe, atamjia Mola wake, Siku ya Kiyama, hali ya kuwa hana mali wala watoto pamoja na yeye (95). [Mariam: 88-95]. Na amesema Allah Mtukufu: Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye hakuna yeyote anayestahiki uungu na kuabudiwa ispokua Yeye. Ndiye Aliye hai Ambaye Amekusanya maana yote ya uhai mkamilifu unaolingana na utukufu Wake. Ndiye Msimamizi wa kila kitu. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Kila kilichoko kwenye mbingu na kilichoko kwenye ardhi ni milki Yake. Na hatopata ujasiri mtu yeyote wa kuombea mbele Yake ispokuwa kwa ruhusa Yake. Ujuzi Wake umevizunguka vitu vyote vilivyopita, vilivyoko na vitakavyo kuja. Anajua yaliyo mbele ya viumbe katika mambo ambayo yatakuja na yaliyo nyuma yao katika mambo yaliyopita. Na hakuna yeyote, katika viumbe, mwenye kuchungulia chochote katika elimu Yake ispokuwa kadiri ile ambayo Mwenyezi Mungu Amemjulisha na kumuonyesha. Kursiy Yake imeenea kwenye mbingu na ardhi. Kursiy ni mahali pa nyayo za Mola, uliyo mkubwa utukufu Wake, na hakuna ajuwae namna ilivyo ispokuwa ni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Wala hakumuelemei Mwenyezi Mungu Aliyetakata kuzitunza. (hizo mbingu na ardhi).Yeye Ndiye Aliye juu ya viumbe Vyake vyote, kwa dhati Yake na sifa Zake, Aliyekusanya sifa za utukufu na kiburi. Aya hii ni aya tukufu zaidi katika Qur’ani, na inaitwa Āyah al- Kursīy. [Al Baqara: 255]. Hii ndio habari yake na habari ya viumbe vyake, itawezekana vipi aingie kwa mmoja miongoni mwao? au amfanye kuwa Mungu pamoja naye?.
11- Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mpole Mwingi wa huruma kwa waja wake ndio maana katuma Mitume na akashusha vitabu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mpole Mwingi wa huruma kwa waja wake, na katika huruma yake kwa waja wake ni kuwatumia Mitume na kuwateremshia vitabu; ili awatoea katika giza la ukafiri na ushirikina na kuwaleta katika Nuru ya Tauhidi na uongofu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Yeye Ndiye Anayemteremshia mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, aya za Qur’ani zilizopambanuliwa zilizo wazi, ili Awatoe nyinyi kwa hizo kwenye giza la ukafiri na kuwatia kwenye mwangaza wa Imani. Na hakika Mwenyezi Mungu, kwa kule kuwatoa nyinyi kwenye giza na kuwatia kwenye mwangaza, Anawarehemu rehema kunjufu katika maisha yenu ya sasa ya ulimwenguni na maisha yenu ya baadaye, na awalipe malipo mazuri kabisa. [Al Hadiid: 9].
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukukutuma ,ewe Mtume, ispokuwa ni rehema kwa watu wote. [Al Anbiyaai: 107]. Na Mwenyezi Mungu alimuamrisha Nabii wake kuwa awaambie waja kuwa bila shaka yeye ni Mwingi wa msamaha Mwenye huruma, Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wapashe habari, ewe Mtume, waja wangu kwamba mimi ni mwenye kuwasamehe Waumini wenye kutubia, ni mwenye huruma kwao}. [A Hijri: 49]. Na katika upole wake na huruma yake nikuwa yeye anaondoa madhara na anateremsha kheri kwa waja wake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenyezi Mungu Akikupatia, ewe Mtume, shida au mitihani, basi hakuna wa kuyaondoa hayo ispokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, na akikutakia furaha na neema, basi hakuna yeyote mwenye kuyazuia hayo. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Anampatia furaha na shida Anayemtaka kati ya waja Wake. Na Yeye ni Mwingi wa msamaha wa dhambi za wenye kutubia, ni Mwingi wa rehema kwa wanaomuamini na kumtii. [Yunus: 107].
12- Mwenyezi Mungu Mola Mwingi wa huruma ndiye pekee atakayewahesabu viumbe siku ya Kiyama pale atakapowafufua wote kutoka katika makaburi yao, amlipe kila mtu kwa yale aliyoyatenda katika kheri au shari, atakayefanya mema naye akawa ni muumini basi atapata neema za kudumu, na atakayekufuru na akatenda maovu basi atapata adhabu kubwa siku ya mwisho.
Mwenyezi Mungu Mola Mwingi wa huruma ndiye pekee atakayewahesabu viumbe siku ya Kiyama pale atakapowafufua wote kutoka katika makaburi yao, amlipe kila mtu kwa yale aliyoyatenda katika kheri au shari, atakayefanya mema naye akawa ni muumini basi atapata neema za kudumu, na atakayekufuru na akatenda maovu basi atapata adhabu kubwa siku ya kiyama, na katika ukamilifu wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na hekima zake na huruma zake kwa waja wake ni kuifanya hii Dunia kuwa ni nyumba ya matendo, na akaifanya Nyumba ya pili (Akhera) kuwe na malipo na hesabu na thawabu; ili apate aliyetenda wema malipo ya wema wake, na apate mkosefu na dhalimu na muovu adhabu ya uovu wake na dhulma yake, na ni kwasababu swala hili wanaweza kuliona kuwa liko mbali baadhi ya watu, hakika, Mwenyezi Mungu ameweka ushahidi mwingi unaoonyesha kuwa kufufuliwa kupo kweli na hakuna shaka ndani yake, Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na miongoni mwa alama za upweke wa Mwenyezi Mungu na uweza Wake ni kuwa wewe unaiona ardhi ikiwa kavu haina mimea, na tunapoiteremshia mvua, uhai unatambaa ndani yake inashikana kwa mimea, na ikafura na kunyanyuka. Hakika Yule Anayeihuisha ardhi hii baada ya ukavu wake ni Muweza wa kuwahuisha viumbe baada ya kufa kwao. Hakika Yeye juu ya kila jambo ni Muweza. Na kama usivyoelemewa uweza Wake wa kuhuisha ardhi baada ya kufa kwake, hivyo hivyo uweza Wake hauelemewi kuwahuisha waliokufa. [Fusswilat: 39]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi watu, mkiwa mna shaka ya kuwa Mwenyzi Mungu atawafufua wafu, basi sisi tumemuumba baba yenu Adam kutokana na mchanga kisha kizazi chake kikazaana kutokana na nutfah, nayo ni manii ambayo mwanamume anayarusha kwenye uzao wa mwanamke, yakageuka kwa uweza wa Mwenyezi Mungu yakawa 'alaqah, nalo ni pande la damu nyekundu iliyo nzito, kisha yakawa mudh'ghah, nacho ni kinofu kidogo cha nyama cha kuweza kutafunika, mara nyingine kikawa kitaumbwa, yaani kiumbike kikamilifu mpaka kifikie hadi ya kutoka kwa mtoto akiwa hai, na mara nyingine kisiumbike kikamilifu kikatoka kabla ya kutimia, ili tuwafafanulie ukamilifu wa uweza wetu wa kuendesha miongo ya uumbaji. Na tunakibakisha kwenye zao tunachokitaka, nacho ni kile kinachoendelezwa kuumbwa kwake mpaka wakati wa kuzaliwa kwake na itimie ile miongo ya kuzaliwa wana wa matumboni wakiwa wadogo, wakuwe mpaka wafikie umri wa kuwa na nguvu, nao ni wakati wa ubarobaro na nguvu na kukamilika akili. Na baadhi ya watoto huenda wakafa kabla ya hapo, na baadhi yao wanakuwa mpaka wanafikisha miaka ya ukongwe na udhaifu wa akili, akawa huyu aliyezeeka hajui kitu alichokuwa akikijua kabla ya hapo. Na utaiona ardhi ni kavu, imekufa haina mimea yoyote, tuyateremshapo maji juu yake, inatikisika kwa mimea ikawa inafunguka, inachepua, inanyanyuka na kuongezeka kwa kutosheka na maji na ikaotesha kila aina ya mimea mizuri yenye kuwafurahisha wenye kuangalia. [Al Haji: 5]. Ametaja (Mwenyezi Mungu) wa kweli katika Aya hizi hoja tatu za kiakili zinazoonyesha juu ya kufufuliwa, nazo ni:
1- Nikuwa Mwenyezi Mungu kamuumba mwanadamu mara ya kwanza kutokana na udongo, na aliyemuumba kwa udongo anauwezo kumrejesha katika maisha pale anapokuwa udongo.
2- Nikuwa aliyemuumba kwa tone la manii akawa mtu, anauwezo wa kumrudisha mtu katika uhai baada ya kufa kwake.
3- Nikuwa aliyeihuisha ardhi kwa mvua baada ya kufa kwake anauwezo wa kuwahuisha watu baada kufa kwao, na katika Aya hii kuna ushahidi mkubwa juu ya changamoto ya Qur'an ni namna gani imekusanya Aya hii- pamoja na kuwa si ndefu- hoja tatu za kiakili za kutisha juu ya jambo kubwa.
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Siku ambayo tutaikunja mbingu kama vile ukurasa unaokunjiwa maandishi yaliyomo ndani na tutawafufua viumbe kama vile walivyokuwa mwanzo walipozaliwa na mama zao. Hiyo ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu isiyokwenda kinyume. Tumeliahidi hilo ahadi ya kweli tuliyojilazimisha nayo. Hakika sisi daima ni wenye kufanya tunaloahidi. [Al Anbiyaai: 104]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na mkanushaji Kufufuliwa alitupigia mfano usiofaa kupigwa, nao ni kulinganisha uweza wa Muumba na ule wa muumbwa, na akasahau kulianzaje kule kuumbwa kwake. Akasema, «Ni nani mwenye kuhuisha mifupa iliyochakaa na kumumunyuka? Mwambie, «Atakayeihuisha ni Yule Aliyeiumba mara ya kwanza, na Yeye kwa viumbe vyake vyote ni Mjuzi, hakifichikani Kwake yeye kitu chochote. [Yaasin: 78]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Je, kufufuliwa kwenu, enyi watu, baada ya kufa ni kugumu zaidi, katika vipimo vyenu, au ni kuumbwa kwa mbingu? Amezipanga juu yenu kama jengo. Na Ameinua sakafu yake angani, haina tofauti wala nyufa. Na Ameutia giza usiku wake kwa kutwa kwa jua lake. Na Ameweka wazi mchana wake kwa kuchomoza kwake. Na ardhi baada ya hayo akaitandaza. Na Ametoa humo chemchemu za maji. Na Ameotesha humo mimea inayolishwa. Na Milima akaisimamisha. [An Naazi'ati: 27-32]. Akabainisha (Allah) wa kweli kwamba kuumbwa kwa mwanadamu si jambo kubwa kuliko kuumbwa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, muweza wa kuumba mbingu na ardhi hawezi kushindwa kumrudisha mwanadamu mara ya pili.
13- Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kutokana na udongo, na akafanya kizazi chake kiongezeke baada yake, watu wote asili yao ni moja sawasawa, na wala hakuna ubora wa jinsi kwa jinsi nyingine, wala watu fulani kwa watu wengine ispokuwa kwa ucha Mungu.
13- Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kutokana na udongo, na akafanya kizazi chake kiongezeke baada yake, watu wote asili yao ni moja sawasawa, na wala hakuna ubora wa jinsi kwa jinsi nyingine, wala watu fulani kwa watu wengine ispokuwa kwa ucha Mungu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi watu! Sisi tumewaumba nyinyi kutokana na baba mmoja, naye ni Ādam, na mama mmoja, naye ni Ḥawwā’, hivyo basi hakuna kufadhilishana baina yenu kinasaba, na tumewafanya nyinyi kwa kuzaana kuwa mataifa na makabila mbalimbali ili mjuane nyinyi kwa nyinyi, hakika mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemcha Yeye zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu Anawajua sana wachamungu na Anawatambua. [Al Hujrati: 13]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenyezi Mungu Alimuumba baba yenu Ādam kwa mchanga kisha Akajaalia kizazi chake kitokamane na maji matwevu (dhalili), kisha Akawafanya nyinyi ni wanaume na wanawake. Na hakuna mwanamke yeyote anayeshika mimba wala anayezaa ispokuwa Analijua hilo. Na hakuna mtu anayepewa maisha marefu au umri wake ukapunguzwa ispokuwa hayo yamo ndani ya Kitabu kilichoko Kwake, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa, kabla mama yake hajashika mimba yake na kabla hajamzaa. Hayo yote Mwenyezi Mungu Ameyadhibiti anayajua kabla hajamuumba, hayataongezwa yale aliyoandikiwa wala hayatopunguzwa. Hakika kule kuwaumba nyinyi, kuzijua hali zenu na kuziandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa ni jambo rahisi na sahali kwa Mwenyezi Mungu. [Faatwir: 11]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Yeye Ndiye Aliyemuumba baba yenu Ādam kwa mchanga, kisha Akawafanya mpatikane kutokana na manii kwa uweza Wake, na baada yake mnahamia kwenye mwongo wa damu nzito iliyo nyekundu, kisha mnapitiwa na miongo kadha ndani ya vizazi, mpaka mnapozaliwa mkiwa watoto wadogo, kisha umbile lenu linapata nguvu (na mnaendelea hivyo) mpaka mnapokuwa wazee, na miongoni mwenu kuna wanaokufa kabla ya hapo. Na ili mfikie kwa miongo hii kipindi kilichotajwa ambacho hapo umri wenu ukome. Huenda nyinyi mkazitia akilini hoja za Mwenyezi Mungu katika hilo na mkazizingatia aya zake mkajua kuwa hakuna Mola ispokuwa Yeye Anayefanya hilo, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye haitakiwi kuabudiwa ispokuwa Yeye. [Ghaafir: 67]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha ya kwamba Yeye alimuumba Masihi kwa amri ya 'kuwa' kama alivyomuumba Adam kwa udongo kwa amri ya 'kuwa', Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika mfano wa Mwenyezi Mungu kumuumba lsa, bila ya baba, ni kama mfano wa Mwenyezi Mungu kumuumba Adam, bila ya baba wala mama. Mwenyezi Mungu Alimuumba kutokana na mchanga wa ardhi kisha Akamwabia, «kuwa kiumbe», akawa. Basi madai ya uungu wa 'Īsā kwa kuwa aliumbwa bila ya baba, ni madai ya uongo. Ādam, amani imshukie, aliumbwa bila ya baba wala mama, na wote wamekubaliana kwamba yeye ni mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu. [Al-Imran: 59]. Na nimetangulia kusema katika kipengele namba (2) kuwa Mtume rehema na Amani zimfikie amebainisha kuwa watu wote wako sawasawa, na hakuna ubora wa mmoja kwa mwingine ispokuwa kwa ucha Mungu.
Na kila mwenye kuzaliwa huzaliwa katika maumbile (yakuwa muislamu).
Na kila mwenye kuzaliwa huzaliwa katika maumbile (yakuwa muislamu). Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi simamisha uso wako, ewe Mtume, wewe na waliokufuata na uendelee kwenye msimamo wa dini ambayo Mwenyezi Mungu Amekuwekea, nayo ni Uislamu ambao Mwenyezi Mungu Ameufanya ulingane na maumbile ya watu. Basi kuendelea kwenu kubaki kwenye Uislamu, na kushikamana kwenu nao ni kushikamana na umbile la Mwenyezi Mungu la kumuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake. Hapana ugeuzaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu na Dini Yake, kwani hiyo ndiyo njia iliyonyooka yenye kupelekea kwenye radhi za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na Pepo Yake. Lakini wengi wa watu hawajui kuwa yale niliyokuamrisha nayo, ewe Mtume, ndiyo Dini ya haki na si nyigine. [Ar rum: 30]. Na utakasifu ndio mila ya Ibrahim kipenzi Amani imfikie, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kisha tukakuletea wahyi, ewe Mtume, kwamba uifuate dini ya Uislamu kama alivyoifuata Ibrāhīm na kwamba ulingane juu yake na usiiyepuke, kwani Ibrāhīm hakuwa ni miongoni mwa wale wanaowashirikisha wengine pamoja na Mwenyezi Mungu. [An Nahli: 123]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakuna anayezaliwa ispokuwa anazaliwa katika maumbile, basi wazazi wake ndio wanaomfanya kuwa Myahudi au Mkristo, au Mmajusi, kama anavyozalishwa mnyama mnyama mwenye ulemavu, je hua mnahisi kuwa ndani yake kunaweza kuwa na aliyekatika pua" Kisha anasema Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Basi kuendelea kwenu kubaki kwenye Uislamu, na kushikamana kwenu nao ni kushikamana na umbile la Mwenyezi Mungu la kumuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake. Hapana ugeuzaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu na Dini Yake, kwani hiyo ndiyo njia iliyonyooka yenye kupelekea kwenye radhi za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na Pepo Yake. Lakini wengi wa watu hawajui kuwa yale niliyokuamrisha nayo, ewe Mtume, ndiyo Dini ya haki na si nyigine. [Ar rum: 30]. Sahihi Bukhariy 4775, Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Jueni hakika Mola wangu Mlezi ameniamrisha niwafundishe yale msiyo yajua miongoni mwa yale aliyo nifundisha leo hii: Kila mali niliyompa mja ni halali, na Mimi nimewaumba waja wakiwa ni wenye dini sahihi, ghafla mashetani wakawajia wakawatoa katika dini yao wakaharamisha yale niliyo yahalalisha, na wakawaamrisha wanishirikishe kwa yale ambayo sijayateremshia kwayo dalili) (22). Imepokelewa na Muslim 2865.
15- Na hakuna binadamu anazaliwa akiwa mkosefu, au karithi makosa ya mtu mwingine:
Hakuna binadamu yeyote anayezaliwa akiwa mkosefu, au karithi makosa ya mtu mwingine, na akatueleza Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa Adam Amani iwe juu yake, alipokwenda kinyume na amri ya Mungu na akala yeye na Mkewe Hawa katika mti, alijuta na akatubia na akamuomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mwenyezi Mungu akamfunulia aseme maneno mazuri, na akayasema na Mwenyezi Mungu akawasamehe, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Akasema, “Ewe Ādam! Kaa wewe na mkeo Ḥawwā’ kwenye pepo na stareheni kwa matunda yake kwa furaha na ukunjufu popote pale mnapotaka humo, na tahadharini na mti huu, msije mkaingia katika maasia mkawa ni wenye kukiuka amri ya Mwenyezi Mungu.” Shetani akawaingiza makosani, kwa kuwashawishi mpaka wakala katika ule mti, ikasababisha kutolewa kwao kwenye Pepo na starehe zake. Na Mwenyezi Mungu Aliwaambia, “Shukeni ardhini, mkiteta nyinyi kwa nyinyi- yaani: Ādam, Ḥawwā’ na Shetani-, na nyinyi katika hiyo ardhi mna utulivu na makao na kunufaika kwa vilivyomo mpaka muda wa maisha yenu ukome.” Ādam alipokea matamko ya kuomba ili akubaliwe, aliyoletewa na Mwenyezi Mungu, kwa njia ya ilham (ufunuo), yaliyokusanya toba na kutaka msamaha, nayo ni neno Lake Aliyetukuka, “Ewe Mola wetu! Tumejidhulumu nafsi zetu. Na Usipotusamehe na Kuturehemu, hakika tutakuwa ni miongoni mwa waliyopata hasara.” (7:23). Mwenyezi Mungu Alikubali toba yake na Akamsamehe. Kwani Yeye, Aliyetukuka, ni Mwingi wa kukubali toba ya Mwenye kutubia miongoni mwa waja Wake na ni Mwenye Kuwarehemu. Tulisema, “Shukeni kutoka Peponi nyote! Na utawajia, nyinyi na vizazi vyenu vinavyofuatia, ujumbe wenye mambo ya kuwaongoza kwenye haki. Wenye kuufuata huo kwa vitendo, hawatakuwa na hofu kuhusu mustakbali wao wa Akhera, wala hawatakuwa na huzuni juu ya vitu walivyovikosa vya ulimwenguni. [Al Baqara: 35-38]. Na Mwenyezi Mungu alipomsamehe Adam Amani iwe juu yake, hakuendelea kulibeba kosa lake, na baada ya hapo bila shaka kizazi chake hakiwezi kurithi kosa, kwani tayari limeshaondoka kwa kuomba msamaha, na kimsingi nikuwa mtu habebi mzigo wa dhambi la mwenzie, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala nafsi yoyote haichumi (ubaya) ila ni juu yake; (hatalipwa kiumbe mwingine kwa ubaya wake). wala mbebaji (Mizigo yake ya dhambi) hatabeba mizigo ya mwingine (kumsaidia). kisha marejeo yenu (nyote) ni kwa Mola wenu. Naye atakuambieni mliyokuwa mkihitilafiana}. [Al An'am: 164].
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenye kuongoka anaongoka kwa maslahi ya nafsi yake ,na anaepotea basi anapotea wa khasara ya nafsi yakemwenyewe,wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwengine,na sisi siyo wenye kuwaadhibu viumbe mpaka tuwatumie mjumbe. [Al Israai: 15]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kiumbe yeyote Aliyefanya dhambi hatabeba dhambi za mtu mwingine. Na mtu yeyote aliyeelemewa na dhambi, akiomba mwenye kumbebea dhambi zake, hatopata mwenye kumbebea chochote, hata kama yule aliyemuomba ana ujamaa wa karibu na yeye, kama baba au ndugu na mfano wao. Hakika ni kwamba wewe, ewe Mtume, unawaonya wale wanaoogopa adhabu ya Mola wao pamoja na kuwa wao hawaioni na wakatekeleza Swala inavyotakikana itekelezwe. Na mwenye kujisafisha na ushirikina na maasia mengine, basi yeye anajisafisha nafsi yake. Na kwa Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ndio marejeo ya viumbe wote na mwisho wao, hapo Amlipe kila mmoja kile anachostahiki. [Faatwir: 18].
16- Na lengo la kuumbwa watu ni: Kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake:
Na lengo la kuumbwa watu ni: Kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na sikuumba majini na binadamu ispokuwa kwa lengo tukufu, nalo niabudiwe mimi Peke Yangu, na siyo asiyekuwa mimi. [Adh Dhariyati: 56].
17- Uislamu umemtukuza Mwanadamu- wanaume na wanawake- na ukamuhudumia haki kamilifu, na ukamfanya yeye kuwa ndiyo mbebaji wa jukumu la yale anayoyachagua na matendo yake, na mihangaiko yake, na unambebesha majukumu ya jambo lolote litakalomdhuru yeye au likamdhuru mtu mwingine.
Uislamu umemtukuza Mwanadamu- wanaume na wanawake- na Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuumba mwanadamu ili awe mtawala katika ardhi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na pindi aliposema Mola wako kuwaambia Malaika, 'hakika mimi nitaweka katika ardhi mtawala'}. [Al Baqara: 30].
Na kutukuzwa huku kunawajumuisha wanadamu wote, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa hakika tumewatukuza watu wa kizazi cha Ādam kwa akili na kuwapelekea Mitume, na tukawadhalilishia vilivyoko ulimwenguni vyote: tukawadhalilishia wanyama barani wa kuwapanda na vyombo baharini vya kuwabeba, tukawaruzuku vilaji na vinywaji vizuri na tukawapa daraja kubwa juu ya viumbe wengi. [Al Israai: 70]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika Tumemuumba binadamu katika sura nzuri. [Attin: 4].
Na Mwenyezi Mungu akamkataza mwanadamu asijifanyie yeye mwenyewe cha kukifuata kidhalilifu, chenye kuabudiwa au kufuatwa au kutiiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Pamoja na hizi hoja za kukata, kinatoka kikundi cha watu wakichukua, badala ya Mwenyezi Mungu, masanamu na wategemewa wakiwafanya ni kama Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuwapa mapenzi, heshima na utiifu, Na Waumini, mapenzi yao kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa zaidi kuliko mapenzi ya hawa makafiri kwa Mwenyezi Mungu na kwa waungu wao. Na hao makafiri wamemshirikisha Mwenyezi Mungu katika mapenzi. Na lau wangelijua wale waliojidhulumu nafsi zao kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika maisha ya kidunia, pindi watakapoiona adhabu ya Akhera, kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Peke Yake Mwenye nguvu zote na kwamba Mwenyezi Mungu ni mkali wa adhabu, wasingeliwafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni waungu wakawa wanawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, na kujikurubisha nao Kwake. [Al Baqara: 165-166]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha hali za wafuasi na wenye kufuatwa kwa batili siku ya kiyama: Viongozi watasema kuwaambia wale waliofanywa wanyonge, «Kwani ni sisi tuliowazuia uongofu baada ya kuwajia? Bali ni nyinyi wenyewe mlikuwa wahalifu kwa kuwa mliingia kwenye ukafiri kwa matakwa yenu na hiyari yenu.» Watasema waliofanywa wanyonge kuwaambia wakubwa wao katika upotevu, «Bali ni kule kutupangia kwenu ubaya usiku na mchana ndiko kulikotutia sisi katika majanga. Kwa kuwa mlikuwa mkitutaka tumkanushe Mwenyezi Mungu na tumfanye kuwa ana washirika katika kuabudiwa.» Na watu wa kila mojawapo ya makundi mawili wataficha majuto watakapoiona adhabu walioandaliwa. Na tutaweka minyororo kwenye shingo za wale waliokanusha. Na wao hawatateswa kwa adhabu hii ispokuwa ni kwa sababu ya kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu na kufanya kwao matendo mabaya duniani. Katika hii aya kuna onyo kali dhidi ya kuwafuata walinganizi wa upotevu na viongozi wa ukiukaji Sheria. [Sabai: 32-33].
Na katika ukamilifu wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama ni kuwabebesha walinganizi na viongozi wapotofu mizigo yao na mizigo ya wale ambao wanaowapoteza pasinakuwa na elimu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwisho wao utakuwa ni kuzibeba dhambi zao kamili Siku ya Kiyama, hawatasamehewa chochote, na watazibeba dhambi za wale waliowadanganya ili kuwaepusha na Uislamu, bila ya kupunguziwa dhambi zao. Jueni mtanabahi, ni ubaya ulioje wa dhambi watakazozibeba! [An Nahli:25].
Na uislamu umemdhamini mwanadamu haki zote kikamilifu Duniani na Akhera, na haki kubwa uliomdhamini na ukaibainisha kwa watu: Ni haki ya Mwenyezi Mungu kwa watu na haki ya watu kwa Mwenyezi Mungu. Na kutoka kwa Mu'adhi Bin Jabali radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie amesema: Nilikuwa nyuma ya Mtume rehema na amani zimfikie (katika kipando) akasema: "Ewe Mua'dh!" nikasema: naam, nimekuitika na umetukuka, kisha akasema mfano wa neno hilo mara tatu: "Hivi unajua haki za Mwenyezi Mungu kwa waja?" nikasema: Hapana, akasema: "Haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni wamuabudu na asishirikishwe na chochote" kisha akatembea mwendo wa lisaa limoja, na akasema: "Ewe Mu'adh" nikasema: naam, nimekuitika na umetukuka, akasema: "Je unajua haki za waja kwa Mwenyezi Mungu watakapolifanya hilo?: ni kutokuwaadhibu". Sahihi Bukhariy 6840,
Na uislamu umemdhamini mwanadamu dini yake ya kweli, na kizazi chake na mali yake na heshima yake. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Basi hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha kwenu nyinyi damu zenu na mali zenu na heshima zenu, kama uharamu wa siku yenu hii katika mwezi wenu huu katika mji wenu huu" Sahihi Bukhariy 6501, Na alitangaza Mtume rehema na Amani zimfikie makubaliano mazito katika hija ya kuaga ambayo ilihudhuriwa na zaidi ya maswahaba laki moja (100,000), na akarudiarudia maana hii na akatilia mkazo juu yake katika siku ya kuchinja katika hija ya kuaga.
Na uislamu umemfanya mwanadamu kuwa ndiye mbebaji wa majukumu aliyo na maamuzi nayo na matendo yake na mihangaiko yake, Amesema Mwemyezi Mungu Mtukufu: {Na kila mwanadamu tumemfungia (malipo ya) vitendo vyake shingoni mwake; na tutamtolea siku ya kiyama daftari (lililoandikwa ndani yake kila alilolifanya) atakalolikuta limekunjuliwa}. [Al Israa: 13]. Yaani: aliyoyafanya katika kheri au shari Mwenyezi Mungu atayafanya aambatananaye nayo (mwenyewe) hayamvuki yakaenda kwa mtu mwingine, hatohesabiwa kwa matendo ya mwingine, na hatohesabiwa mtu mwingine kwa matendo yake yeye, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ewe binadamu, wewe unaenda kwa Mwenyezi Mungu na unafanya amali nzuri na mbaya, kisha utakutananaye Siku ya Kiyama. Na huna budi kupata kutoka Kwake malipo mazuri zaidi ya amali yako njema au yanayolingana na amali yako mbaya. [Al Inshiqaaq: 6]. Na amesema Allah Mtukufu: Mwenye kufanya mema, akamtii mwenyezi Mungu na Mtume Wake, atajipatia mwenyewe thawabu za matendo yake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, atajionea mwenyewe dhambi za matendo yake. Na Mola wako si Mwenye kuwadhulumu waja kwa kuwapunguzia japo thawabu ya jema moja au kuwaongezea japo dhambi la ovu moja. [Fusswilat: 46].
Na uislamu umembebesha mwanadamu jukumu la jambo lolote litalomdhuru yeye mwenyewe au kumdhuru mtu mwingine, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenye kufanya dhambi kwa kusudi, hakika huwa akijidhuru nafsi yake peke yake. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mjuzi wa uhakika wa mambo ya waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika hukumu Zake Azitowazo kwa waja Wake. [An Nisaai: 111]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {kwasababu hiyo tuliwafaradhishia wana Israeli, yakwamba yeyote atakayeuwa nafsi bila ya hatia au akafanya ufisadi katika ardhi, atakuwa ni kama amewauwa watu wote, na atakayeihuisha basi atakuwa ni kama amewahuisha watu wote}. [Al Maaidah: 32]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Haitouliwa nafsi yoyote kwa dhulma ispokuwa kutakuwa kwa mwana wa Adam wa mwanzo na fungu (la dhambi) kutoka katika damu hiyo, kwasababu yeye ndiye alikuwa muanzilishi wa kwanza kuua" kaipokea Muslim (5150).
18- Uislamu umemfanya mwanaume na mwanamke kuwa sawasawa kulingana na matendo na majukumu na malipo na thawabu.
Uislamu umewafanya wanaume na wanawake kuwa sawasawa kulingana na matendo na majukumu na malipo na thawabu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na mwenye kufanya matendo mema, awe ni mwanamume au mwanamke, hali ya kuwa anamuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na haki Aliyoiteremsha, basi hao Mwenyezi Mungu Atawaingiza Peponi, nyumba ya starehe ya daima, na hawatopunguziwa chochote katika thawabu za matendo yao, hata kama ni kadiri ya kitone kilichoko kwenye kokwa la tende. [An Nisaai: 124]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenye kufanya tendo zuri, akiwa ni mwanamume au ni mwanamke, na huku ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake , basi tutampa maisha mema yenye utulivu duniani hata kama ni mchache wa mali, na tutawalipa huko Akhera thawabu zao kwa uzuri zaidi ya walivyofanya duniani. [An Nahli: 97]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: «Mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu katika uhai wake na akapotoka kwenye njia ya uongofu, hatalipwa huko Akhera ispokuwa mateso yanayolingana na maasia yake. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akafanya matendo mema, kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, awe mwanamume au mwanamke, na hali yeye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha, basi hao wataingia Peponi na humo Mwenyezi Mungu Atawaruzuku kutokana na matunda yake na starehe zake pasi na hesabu. [Ghaafir: 40]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika wale wanaume na wanawake wenye kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na wanaume na wanawake wenye kuamini, na wanaume na wanawake wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na wakweli wa kiume na wa kike, na wanaume na wanawake wenye kusubiri katika kujiepusha na matamanio na juu ya kufanya matendo ya utiifu na juu ya shida, na wanaume na wanawake wenye kumcha Mwenyezi Mungu, na wanaume na wanawake wenye kutoa sadaka za lazima na za ziada, na wanaume na wanawake wenye kufunga saumu za lazima na za ziada, na wanaume na wanawake wenye kuzihifadhi tupu zao na uzinifu na vitangulizi vyake na kujihifadhi ufunuaji uchi, na wanaume na wanawake wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa nyoyo zao na ndimi zao, Hao Mwenyezi Mungu Amewaandalia msamaha wa dhambi zao na malipo mema makubwa, nayo ni Pepo. [Al Ahzaab: 35].
19- Uislamu umemtukuza mwanamke, na ukawachukulia wanawake kuwa ni ndugu wa damu wa wanaume, na ukamlazimisha mwanaume kumpa matumizi anapokuwa na uwezo, na inamlazimu binti kumpa matumizi baba yake, na mama kwa watoto wake wanapofikia umri wa utuuzima na wakawa na uwezo, na mke kwa mumewe.
Na uislamu umewazingatia wanawake kuwa ni ndugu wa damu wa wanaume. Amesema Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika wanawake ni ndugu wa damu wa wanaume" Kaipokea Tirmidhiy (113).
Na uislamu katika kumtukuza mwanamke ni kwamba umemuwajibishia matumizi mama kwa mtoto wake anapokuwa na uwezo. Amesema Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mkono unatoa kumpa wa juu mama yako na baba yako, na dada yako na kaka yako, kisha wa chini yako kisha wa chini yako". Ameipokea Imamu Ahmad Na utakuja ufafanuzi juu ya nafasi ya wazazi wawili kwa idhini ya Mwenyezi Mungu katika kipengele namba (29).
Na uislamu katika kumtukuza mwanamke ni pale ulipomuwajibishia mume kutoa matumizi kwa mkewe anapokuwa na uwezo, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na atoe matumizi mume kulingana na kile alichokunjuliwa nacho na Mwenyezi Mungu kumpa mkewe aliyeachana naye na amlipie mwanawe, iwapo mume ana ukunjufu wa mapato. Na yule ambaye amebanika kimatumizi naye ni fukara, basi na atoe kulingana na kile alichopewa na Mwenyezi Mungu katika matumizi. Masikini halazimishwi kutoa kama kile anacholazimishwa tajiri. Mwenyezi Mungu Ataleta, baada ya dhiki na shida, ukunjufu wa maisha na kutosheka. [Attwalaaq: 7]. Na mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na Amani zimfikie: 'Ni ipi haki ya mke kwa mume? akasema: "Umlishe unapokula, na umvishe unapovaa, na usipige uso, na wala usitukane (matusi ya kumtia aibu)" Ameipokea Imamu Ahmad Na amesema Mtume rehema na Amani zimfikie akibainisha baadhi ya haki za wanawake kwa waume: "Na wana haki juu yenu ya kuwalisha na kuwavisha kwa wema (yaani: bila kuwapunguzia katika mahitaji yao, wala kuzidisha zaidi ya mahitaji yao)" Swahiih Muslim Amesema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Inatosha kwa mtu kupata dhambi, anapowatelekeza wale anaowahudumia". Ameipokea Imamu Ahmad Na amesema Al khattwaabiy: (Kauli yake: "Anaowahudumia" anakusudia ni wale inaomlazimu kuwahahudumia, na maana yake ni kanakwamba amesema kumwambia mwenye kutoa sadaka: Usitoe sadaka katika yale yasiyokuwa na faida ndani yake ukaacha familia yako ukitafuta kupata malipo; ikageuka sadaka hiyo kuwa dhambi utakapowatelekeza).
Na uislamu katika kumtukuza mwanamke ni pale ulipoweka matumizi ya mtoto wa kike kuwa juu ya baba yake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wazazi wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa atakayetaka kutimiza kunyonyesha, na kwa mzazi wa kiume anawajibika kuwalisha, na kuwavisha kwa wema}. [Al Baqara: 233]. Akabainisha Mwenyezi Mungu kuwa ni juu ya baba mwenye mtoto kumlisha mtoto wake, na kumvisha kwa wema. Na kauli yake Mtukufu: "Ikiwa watakunyonyesheeni basi wapeni ujira wao". [Attwalaaq: 6]. Akawajibisha Mwenyezi Mungu malipo ya (gharama za) kunyonya mtoto juu ya baba, ikaonyesha kuwa swala la matumizi ya mtoto liko juu ya mzazi, na neno mtoto linakusanya wa kiume na wa kike, na katika hadithi ifuatayo kuna ushahidi ya kwamba ulazima wa matumizi ya mke na watoto ni juu ya baba. Na kutoka kwa Aisha radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie: ya kwamba Hindu alisema kumwambia Mtume rehema na Amani zimfikie: 'Hakika Abuu Sufiyani ni mwanaume bakhili, ninalazimika kuchukua katika mali yake? Mtume akasema: "Chukua kinachokutosha wewe na mwanao kwa wema (Yaani bila kuzidisha katika hitajio)". Imepokelewa na Al-Bukhaariy Na akabainisha Nabii Mtukufu fadhila za kuwapa matumizi watoto wa kike na madada, akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani zimfikie: "Atakaye walea mabinti wawili au watatu, au dada wawili au watatu mpaka wakawa watu wazima au wakamfia (mikononi mwake) mimi nitakuwa na yeye kama hivi viwili. Na akaashiria katika vidole vyake viwili cha shahada na cha kati" Silsilatus swahiiha: 296.
20- Na kifo siyo sababu ya mtu kumalizika milele, bali ni kuhama kutoka nyumba ya matendo kwenda katika nyumba ya malipo, na mauti hayo ni ya mwili na roho, na kufa kwa roho ni kutengana na kiwiliwili, kisha itarudi kwake baada ya kufufuliwa siku ya Kiyama, na roho baada ya kifo haihamii katika kiwiliwili kingine, na wala haijipachiki katika mwili mwingine.
Kifo siyo kumalizika milele, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Atakayewafisha nyinyi ni Malaika wa kifo aliyewakilishwa kwenu, atakayezichukua roho zenu utakapokoma muda wenu wa kuishi, na hamtachelewa hata nukta moja, kisha mtarudishwa kwa Mola wenu, Awalipe kwa matendo yenu, yakiwa ni mema Awalipe wema na yakiwa maovu Awalipe uovu. [As sajda: 11]. Na kifo kinaupata mwili na roho, na kufa kwa roho ni kutengana na kiwiliwili, kisha itarudi kwake baada ya kufufuliwa siku ya Kiyama. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Ndiye Anayezifisha nafsi wakati unapofika muda wa kufa kwake.Na zile nafsi ambazo hazikufa katika hali ya kulala kwake,basi huziiua zile alizozihukumia kifo,na huzirudisha zile zingine mpaka zifikie muda wake uliowekwa,bila shaka katika hayo yapo mazingatio kwa watu wanaotafakari. [Az zumar: 42]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika roho inapochukuliwa macho huifuatia" Imepokelewa na Muslim 920. Na baada ya kifo anahama mwanadamu kutoka nyumba ya matendo na kwenda katika nyumba ya malipo, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa Mola wenu ndio marejeo yenu nyote Siku ya Kiyama. Yeye Ndiye Ambaye Anaanza kuumba viumbe kisha Atawarudisha baada ya kufa, Awafanye wawe hai kama walivyokuwa mwanzo, ili Awalipe waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mazuri malipo mazuri zaidi kwa uadilifu. Na wale waliokanusha upweke wa Mwenyezi Mungu na ujumbe wa Mtume Wake watakuwa na vinywaji vya maji moto sana na watakuwa na adhabu inayoumiza kwa sababu ya ukafiri wao na upotevu wao. [Yunus: 4].
Na roho baada ya kifo haihamii katika kiwiliwili kingine wala haijipachiki, madai hayo akili hailikubaliani nayo wala hisia, wala haliwezi kupatikana andiko lolote linalotolea ushahidi itikadi hii kutoka kwa Manabii Amani iwe juu yao.
21- Uislamu unalingania katika imani kupitia misingi mikubwa ya imani, nayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake, na kuamini vitabu vya Mungu kama Taurati Injili na Zaburi - Kabla havijageuzwa na kubadilishwa - Na Qur'an, na kuamini Manabii na Mitume wote Amani iwe juu yao, na kumuamini wa mwisho wao Muhammadi Mtume wa Mwenyezi Mungu wa mwisho katika Manabii na Mitume, na kuamini siku ya mwisho, na tufahamu kuwa maisha ya Dunia yangelikuwa ndiyo mwisho; basi yangekuwa maisha na uwepo wetu ni mchezo mchezo, na (la mwisho) ni kuamini mipango na makadirio.
Uislamu unalingania katika imani kupitia misingi mikubwa ya imani na kwa misingi hiyo wamelingania pia Manabii na Mitume wote Amani iwe juu yao, nayo ni:-
Msingi wa kwanza: Ni kumuamini Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola na muumba na mgawaji wa riziki, na mpangiliaji wa huu ulimwengu, nakuwa yeye peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, na kwamba ibada zote za asiyekuwa yeye ni batili, na kila mwenye kuabudiwa kinyume na yeye huyo ni batili, hazistahili ibada ila kwake yeye, na haziswihi ibada ila kwake yeye. Na tumeshatangulia kulielezea jambo hili, katika kipengele namba: (8).
Na ametaja Mwenyezi Mungu Mtukufu Misingi hii mikubwa katika Aya nyingi tofauti tofauti katika Qur'an tukufu, miongoni mwa hizo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ameamini na kuyakinisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yale aliyoletewa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wake. Na ni haki kwake aiyakinishe.Na Waumini pia wameamini Kila mmoja katika wao amemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola na Muabudiwa, Aliyesifika kwa sifa za utukufu na ukamilifu, na kuwa Mwenyezi Mungu Anao Malaika watukufu, na kuwa Yeye Ameteremsha Vitabu na Ametuma Mitume kwa waja Wake. Hatuwaamini, sisi Waumini, baadhi yao na kuwakanusha baadhi yao. Bali tunawaamini wao wote. Na wanasema, Mtume na Waumini, «Tumeusikia, ewe Mola wetu, wahyi uliouleta na tumetii katika yote hayo. Tunatarajia uyasamehe, kwa wema Wako, madhambi yetu. Wewe Ndiye Ambaye Uliyetulea kwa neema Zako Ulizotuneemesha nazo. Kwako, Peke Yako, ndio marejeo yetu na mwisho wetu.» [Al Baqara: 285]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hapana kheri, mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kuelekea kwenye Swala upande wa mashariki na magharibi, iwapo hilo halitokamani na amri ya Mwenyezi Mungu na sheria Yake. Hakika kheri yote iko katika imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na akamkubali kuwa Ndiye muabudiwa, Peke Yake, Hana mshirika Wake, na akaiamini Siku ya kufufuliwa na Malipo, na akawaamini Malaika wote na vitabu vyote vilivyoteremshwa, na Mitume wote bila kubagua, na akatoa mali yake kwa hiyari yake, pamoja na kuwa anaipenda sana, kuwapa jamaa zake na mayatima wenye uhitaji waliofiliwa na wazazi wao hali wao wako chini ya umri wa kubaleghe, na akawapa masikini ambao ufukara umewaelemea, na wasafiri wanaohitaji walio mbali na watu wao na mali yao, na waombaji ambao imekuwa ni dharura kwao kuomba kwa uhitaji wao mkubwa, na akatoa mali yake katika kuwakomboa watumwa na mateka, na akasimamisha Swala na akatoa zaka za faradhi, na wale wenye kutekeleza ahadi, na mwenye kusubiri katika hali ya ufukara wake na ugonjwa wake na katika vita vikali. Hao wenye kusifika kwa sifa hizo, ndio waliokuwa wakweli katika imani zao, na wao ndio waliojikinga na mateso ya Mwenyezi Mungu wakajiepusha na vitendo vya kumuasi. [Al Baqara: 177]. Na Mwenyezi Mungu ameita waja katika imani kupitia misingi hii na akabainisha kuwa atakayeikufuru basi atakuwa amepotea upotovu wa mbali, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, endeleeni kwenye msimamo mlionao wa kumuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Imani thabiti, kumuamini Mtume Wake Muhammad , rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kuwatii wao wawili, kuiamini Qur’ani Aliyoiteremsha kwake na kuviamini vitabu vyote Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume. Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Malaika Wake waliotukuzwa, vitabu Vyake Alivyoviteremsha ili kuwaongoza viumbe Wake, Mitume Wake Aliowachagua kufikisha ujumbe Wake na Siku ya Mwisho ambayo watu katika siku hiyo watafufuka baada ya kufa ili waorodheshwe na wahesabiwe, atakuwa ametoka kwenye Dini na atakuwa yuko mbali sana na njia ya haki. [An Nisaai: 136]. Na katika hadithi kutoka kwa Omar bin khattwab radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie amesema: Tukiwa sisi tumekaa kwa Mtume rehema na Amani zimfikie siku moja, mara ghafla alitokea kwetu sisi mwanaume mmoja akiwa amevaa nguo nyeupe sana, mwenye nywele nyeusi sana, haionekani kwake athari yoyote ya safari, na hakuna anayemjua yeyote katika sisi, mpaka akakaa kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, akaegemeza (akakunja) magoti yake katika magoti yake, na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake na akasema: 'Ewe Muhammadi! hebu nieleze kuhusu uislamu; Akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimfikie: "Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu, na kuwa Muhammadi rehema na Amani zimfikie ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala na kutoa zaka na kufunga Ramadhani na kuhiji katika nyumba (tukufu Makka) ikiwa utaweza kuiendea" Akasema: swadakta (umesema kweli) tukamshangaa, anamuuliza na anasadikisha! akasema: Hebu nieleze kuhusu imani; Akasema: "Ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho, na kuamini makadirio, kheri zake na shari zake" Akasema: swadakta (umesema kweli); akasema: Hebu nieleze kuhusu ihsan (wema), akasema: "Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kanakwamba unamuona, na ikiwa wewe humuoni, basi yeye anakuona". kaipokea Muslim (8). Katika hadithi hii alikuja Jibril Amani iwe juu yake kwa Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie na akamuuliza kuhusu daraja za dini nazo ni: Uislamu, Imani na Ihsan, Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie akamjibu, kisha Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie akawaeleza maswahaba zake radhi za Mwenyezi Mungu ziwafikie kuwa huyu ni Jibril alikuja kuwafundisha dini yao. Na huu ndio uislamu ujumbe wa Mungu kaunukuu Jibril Amani iwe juu yake, na akaufikisha kwa watu Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie, na wakauhifadhi maswahaba zake radhi za Mwenyezi Mungu ziwafikie, na wakaufikisha kwa watu waliokuja baada yao.
Msingi wa pili: Kuamini Malaika: Nao ni walimwengu wasiyoonekana, aliwaumba Mwenyezi Mungu na akawafanya kuwa katika muonekano maalumu, na akawabebesha kazi kubwa, na katika kazi zao tukufu zaidi ni kuufikisha ujumbe wa Mungu kwa Mitume na Manabii Amani iwe juu yao, Na mtukufu zaidi katika Malaika ni Jibril Amani iwe juu yake, na kinachojulisha kuteremka Jibril na wahyi kwa Mitume sala na salam ziwafikie ni kauli yake Mtukufu: Mwenyezi Mungu Anawateremsha Malaika kuleta wahyi kwa amri Yake kwa anayemtaka miongoni mwa waja Wake waliotumilizwa kwamba watisheni watu na ushirikina na waambieni kwamba hapana wa kuabudiwa kwa haki ispokuwa mimi. Hivyo basi, nicheni kwa kutekeleza faradhi zangu na kunipwekesha kwa kuniabudu na kunitakasa. [An Nahli: 2]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika, hii Qur’ani ambayo ndani yake zimetajwa habari hizi za kweli imeteremshwa na Muumba viumbe na Mmiliki wa mambo yote. ameshuka nayoJibrili muaminifu. akakusomea mpaka ukaikusanya moyoni mwako, kwa kuihifadhi na kuielewa, upate kuwa ni mmoja wa wajumbe wa Mwenyezi Mungu wenye kuwafanya watu wao waogope mateso ya Mwenyezi Mungu, upate kuwaonya, kwa Teremsho hili, binadamu na majini wote. Ameshuka nayo Jibrili kwako kwa lugha ya Kiarabu yenye maana iliyo wazi, yenye ushahidi unaoonekena, ikikusanya kile wanachokihitajia cha kutengeneza mambo ya Dini yao na dunia yao. Na kwa hakika, utajo wa hii Qur’ani umethibitishwa katika Vitabu vya Manabii waliotangulia, vimeibashiri na kukubali kuwa ni ya kweli. [Ash shu'araai: 192-196].
Msingi wa tatu: Ni kuamini Vitabu vya Mungu kama Taurati na Injili na Zaburi- kabla havijabadilishwa na kugeuzwa- na kuamini Qur'an, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, endeleeni kwenye msimamo mlionao wa kumuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Imani thabiti, kumuamini Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kuwatii wao wawili, kuiamini Qur’ani Aliyoiteremsha kwake na kuviamini vitabu vyote Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume. Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Malaika Wake waliotukuzwa, vitabu Vyake Alivyoviteremsha ili kuwaongoza viumbe Wake, Mitume Wake Aliowachagua kufikisha ujumbe Wake na Siku ya Mwisho ambayo watu katika siku hiyo watafufuka baada ya kufa ili waorodheshwe na wahesabiwe, atakuwa ametoka kwenye Dini na atakuwa yuko mbali sana na njia ya haki. [An Nisaai: 136]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Amekuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani kwa haki ambayo haina shaka, inayoshuhudia ukweli wa Vitabu na Mitume kabla yake. Na Aliiteremsha Taurati kwa Musa, amani imshukie, na Injili kwa Īsā, amani imshukie, kabla ya kuteremka Qur’ani, ili kuwaongoza Wacha-Mungu kwenye Imani na kutengeneza dini yao na dunia yao. Na Aliteremsha yenye kupambanua baina ya haki na batili. Na wale ambao wamekanusha aya za Mwenyezi Mungu zilizoteremshwa, wana adhabu kubwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi Asiyeshindwa, ni Mwenye kumtesa anayezikanusha hoja na dalili Zake na kupwekeka Kwake kwa uungu. [Al Imran: 3-4]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ameamini na kuyakinisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yale aliyoletewa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wake. Na ni haki kwake aiyakinishe. Na Waumini pia wameamini na kufanya amali zinazoambatana na Qur’ani Tukufu. Kila mmoja katika wao amemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola na Muabudiwa, Aliyesifika kwa sifa za utukufu na ukamilifu, na kuwa Mwenyezi Mungu Anao Malaika watukufu, na kuwa Yeye Ameteremsha Vitabu na Ametuma Mitume kwa waja Wake. Hatuwaamini, sisi Waumini, baadhi yao na kuwakanusha baadhi yao. Bali tunawaamini wao wote. Na wanasema, Mtume na Waumini, «Tumeusikia, ewe Mola wetu, wahyi uliouleta na tumetii katika yote hayo. Tunatarajia uyasamehe, kwa wema Wako, madhambi yetu. Wewe Ndiye Ambaye Uliyetulea kwa neema Zako Ulizotuneemesha nazo. Kwako, Peke Yako, ndio marejeo yetu na mwisho wetu.» [Al Baqara: 285]. Na amesema Allah Mtukufu: Waambie, ewe Mtume, «Tumemuamini Mwenyezi mungu na tumetii. Hatuna Mola ispokuwa Yeye, na hatuna muabudiwa ispokuwa Yeye. Tumeuamini wahyi Aliouteremsha kwetu na ule Aliouteremsha kwa Ibrāhīm aliye rafiki halisi wa Mwenyezi Mungu, na wanawe wawili, Ismā'il na Is’ḥāq, na mwana wa mwanawe,Ya'qūb mwana wa Is’ḥāq, na Asbāṭ: nao ni Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili wanaotokana na watoto wa Ya'qūb, na wahyi aliopewa Mūsā na ‘Īsā wa Taurati na Injili, na wahyi Aliouteremsha Mwenyezi Mungu kwa Manabii Wake. Tunayaamini hayo yote. Wala hatumbagui yeyote katika wao. Na sisi tunamfuata Mwenyezi Mungu Peke Yake kwa kumtii na kumuabudu, tunakiri Kwake kuwa Yeye Ndiye Mola, Ndiye Mungu na Ndiye wa kuabudiwa. [Al-Imran: 84].
Msingi wa nne: Ni kuwaamini Manabii na Mitume wote Amani iwe juu yao, inalazimu kuwaamini Manabii na Mitume wote Amani iwe juu yao, na kuitakidi kuwa wote ni Mitume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wanazifikishia umma zao ujumbe wa Mwenyezi Mungu na dini yake na sheria zake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Semeni, enyi Waumini, kuwaambia Mayahudi na Wanaswara, “Tumemuamini Mwenyezi Mungu, Aliye Mmoja, Anayeabudiwa kwa haki; na tumeiamini Qur’ani tuliyoteremshiwa ambayo Mwenyezi Mungu alimletea Wahyi Nabii wake na Mtume Wake Muhammad, rehema na amani zimshukie; na tumeziamini Kurasa alizoteremshiwa Ibrāhīm na watoto wake wawili: Ismāīl na Is’ḥāq, na alizoteremshiwa Ya’qūb na Asbāṭ - Manabii wanaotokana na watoto wa Ya’qūb waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya Wana wa Isrāīl-; na tumeiamini Taurati aliyopewa Mūsā na Injil aliyopewa Īsā na Wahyi ulioteremshwa kwa Mitume wote. Hatumbagui yeyote miongoni mwao katika kuamini. Na sisi ni wenye kumdhalilikia Mwenyezi Mungu kwa kumtii na kumuabudu.” [Al Baqara: 136]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ameamini na kuyakinisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yale aliyoletewa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wake. Na ni haki kwake aiyakinishe. Na Waumini pia wameamini na kufanya amali zinazoambatana na Qur’ani Tukufu. Kila mmoja katika wao amemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola na Muabudiwa, Aliyesifika kwa sifa za utukufu na ukamilifu, na kuwa Mwenyezi Mungu Anao Malaika watukufu, na kuwa Yeye Ameteremsha Vitabu na Ametuma Mitume kwa waja Wake. Hatuwaamini, sisi Waumini, baadhi yao na kuwakanusha baadhi yao. Bali tunawaamini wao wote. Na wanasema, Mtume na Waumini, «Tumeusikia, ewe Mola wetu, wahyi uliouleta na tumetii katika yote hayo. Tunatarajia uyasamehe, kwa wema Wako, madhambi yetu. Wewe Ndiye Ambaye Uliyetulea kwa neema Zako Ulizotuneemesha nazo. Kwako, Peke Yako, ndio marejeo yetu na mwisho wetu.» [Al Baqara: 285]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Waambie, ewe Mtume, «Tumemuamini Mwenyezi Mungu na tumetii. Hatuna Mola ispokuwa Yeye, na hatuna muabudiwa ispokuwa Yeye. Tumeuamini wahyi Aliouteremsha kwetu na ule Aliouteremsha kwa Ibrāhīm aliye rafiki halisi wa Mwenyezi Mungu, na wanawe wawili, Ismā'il na Is’ḥāq, na mwana wa mwanawe,Ya'qūb mwana wa Is’ḥāq, nawatoto wake: nao ni Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili wanaotokana na watoto wa Ya'qūb, na wahyi aliopewa Mūsā na ‘Īsā wa Taurati na Injili, na wahyi Aliouteremsha Mwenyezi Mungu kwa Manabii Wake. Tunayaamini hayo yote. Wala hatumbagui yeyote katika wao. Na sisi tunamfuata Mwenyezi Mungu Peke Yake kwa kumtii na kumuabudu, tunakiri Kwake kuwa Yeye Ndiye Mola, Ndiye Mungu na Ndiye wa kuabudiwa. [Al-Imran: 84].
Na kumuamini wa mwisho wao naye ni Muhammad Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wa mwisho katika Manabii na Mitume sala na salamu ziwe juu yao, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: kumbuka, ewe Mtume, pindi Alipochukua Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ahadi ya mkazo kwa Manabii wote kwamba, «Nikishakupeni Kitabu na hekima kisha akaja kwenu mjumbe kutoka kwangu, mwenye kusadikisha vitabu mlivyonavyo, mtamuamini na kumnusuru? Je, mmekiri na kukubali hilo na mmechukua juu yake ahadi yangu ya mkazo?» Wakasema, «Tumekubali hilo.» Akasema, «Kueni mashahidi, baadhi yenu juu ya wengine, na kueni mashahidi kwa hilo juu ya umma wenu, na mimi ni Mwenye kushuhudia pamoja na nyinyi juu yenu na juu yao. Katika haya pana ahadi nzito Aliyoichukua Mwenyezi Mungu kutoka kwa kila Nabii amuamini Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kuchukua ahadi nzito kutoka kwa umma wa Manabii wote juu ya hilo. [Al-Imran: 81].
Uislamu unawajibisha kuwaamini Manabii na Mitume wote kwa ujumla, na una wajibisha kumuamini wa mwisho wao, naye ni Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema, Enyi watu wa kitabu, nyinyi hamko juu ya chohchote mpaka msimamishe Taurati na Injili na yale yaliyoteremshwa kwenu nyinyi kutoka kwa Mola wenu" [Al Maaida: 68]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, ewe Mtume, kuwaambia Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, «Njooni kwenye neno la uadilifu na haki tushikamane nalo sote. Nalo ni sisi kuielekeza ibada yetu kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na tusimfanye yeyote kuwa ni mshirika pamojanaye, liwe ni sanamu au msalaba au Shetani au kinginecho. Na wala wasiwadhalilikie baadhi yetu watu wengine kwa kuwatii badala ya Mwenyezi Mungu.» Basi wakiukataa wito huu mzuri, waambieni wao, enyi Waumini, «Kuweni ni mashahidi kwetu kuwa sisi tumejisalimisha kwa Mola wetu na tumenyoosha shingo zetu Kwake kwa kukubali kuwa ni waja Wake na kwa kumtakasa.» Na wito huu kwenye neno la sawa, kama unavyoelekezwa kwa Mayahudi na Wanaswara, unaelekezwa pia kwa wenye mwenendo kama wao. [Al-Imran: 64].
Na atakayemkanusha Nabii mmoja katika Manabii atakuwa amewakanusha Manabii na Mitume wote Amani iwe juu yao, na ndiyo maana alisema Mwenyezi Mungu akielezea juu ya hukumu yake kwa watu wa Nuhu Amani iwe juu yake: Waliukanusha watu wa Nūḥ ujumbe wa Nabii wao. Wakawa, kwa kufanya hivyo, ni wakanushaji wa Mitume wote, kwa kuwa kila Mtume anaamrisha kuwaamini Mitume wote. [Ash shu'araa: 105]. Na inafahamika kuwa Nabii Nuhu Amani iwe juu yake hakutanguliwa na Mtume, lakini pamoja na hivyo watu wake walipomkanusha kukawa huku kumkanusha kwao ni sawa na kuwakanusha Manabii na Mitume wote; kwasababu ujumbe wao ni mmoja na lengo lao ni moja.
Msingi wa tano: Kuamini siku ya mwisho, nayo ni siku ya Kiyama, na mwisho wa maisha haya ya Dunia Mwenyezi Mungu atamuamrisha Malaika Israafil amani iwe juu yake atapuliza mpulizo mmoja wa kuzimia, atazimia na atakufa kila atakayemtaka Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kutapulizwa kwenye baragumu na hapo atakufa kila aliye mbinguni na ardhini, ispokuwa anayemtaka Mwenyezi Mungu asife. Kisha Malaika Atapuliza mara ya pili kwenye baragumu akitangaza kufufuliwa viumbe wapate kuhesabiwa mbele ya Mola wao, na wakitahamaki wao wamesimama kutoka makaburini mwao wanangojea yale Atakayowafanyia Mwenyezi Mungu. [Azzumar: 68]. Na atakapokufa kila aliyeko mbinguni na ardhini ispokuwa yule atakayemtaka Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ataikunja mbingu na ardhi, kama ilivyokuja katika kauli yake Mtukufu: Siku ambayo tutaikunja mbingu kama vile ukurasa unaokunjiwa maandishi yaliyomo ndani na tutawafufua viumbe kama vile walivyokuwa mwanzo walipozaliwa na mama zao. Hiyo ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu isiyokwenda kinyume. Tumeliahidi hilo ahadi ya kweli tuliyojilazimisha nayo. Hakika sisi daima ni wenye kufanya tunaloahidi. [Al Anbiyaai: 104]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hawa washirikina hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu vile Anavyostahiki kuadhimishwa, kwa kuwa wamemuabudu asiyekuwa Yeye pamoja na Yeye miongoni mwa wale wasionufaisha wala kudhuru, wakamfanya muumbwa, pamoja na uelemevu wake, kuwa ni sawa na Muumba Mtukufu, Ambaye kotokana na uweza Wake mkubwa ni kwamba ardhi yote itakuwa iko mkononi Mwake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa kwa mkono Wake wa kulia. Ametakasika Mwenyezi Mungu na kutukuka kwa kuepukana na kile wanachomshirikisha nacho hao washirikina. Katika aya hii pana dalili ya kuthibitisha kushika kwa mkono, mkono wa kulia na kukunja kwa Mwenyezi Mungu kama vile inavyolingana na haiba Yake na utukufu Wake bila kueleza Yuko vipi wala kufananisha. [Azzumar: 67]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenyezi Mungu Mtukufu atazikunja Mbingu siku ya Kiyama, kisha azichukue kwa mkono wake wa kulia kisha aseme: Mimi ndiye Mfalme wako wapi majabari (wenye jeuri)? wako wapi wenye kiburi?. kisha atazikunja ardhi kushotoni kwake, kisha aseme: Mimi ndiye Mfalme wako wapi majabari (wenye jeuri)? wako wapi wenye kiburi?" Imepokelewa na Imamu Muslim
Kisha Mwenyezi Mungu atamuamrisha Malaika, atapuliza kwa mara nyingine, tahamaki watajikuta wamesimama wakingonjea (kuhukumiwa). {Kisha litapulizwa mara nyingine, tahamaki watajikuta wamesimama wakingonjea (kuhukumiwa). [Azzumar: 68]. Mwenyezi Mungu atakapowafufua viumbe atawakusanya kwaajili ya hesabu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Siku ambayo ardhi itapasukapasuka itoe wafu waliozikwa humo, watoke mbio kuelekea upande wa yule anayeita. Kuwakusanya watu hivyo kwenye Kisimamo cha Hesabu ni jambo sahali kwetu na rahisi. [Qaf: 44]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Siku ya Kiyama watajitokeza viumbe mbele ya Mola wao, hakuna chochote kuhusu wao au kuhusu matendo yao waliyoyafanya ulimwenguni kitakachofichikana kwa Mwenyezi Mungu. Hapo Atasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Ni wa nani ufalme na mamlaka Siku ya Leo?» Na Ajijibu Mwenyewe, «Ni vya Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake, Mwenye kutenza nguvu Aliyevilazimisha viumbe vyote kwa uwezo Wake na enzi Yake.» [Ghaafir: 16}. Na katika siku hii Mwenyezi Mungu atawahesabu watu wote, na amlipize kila aliyedhulumu kwa aliyemdhulumu, na amlipe kila mwanadamu kwa yale aliyoyafanya. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Leo italipwa kila nafsi kwa kile ilichokitenda duniani, chema au kiovu; hakuna uonevu leo wa kufanyiwa yeyote, wa kuongezewa dhambi zake au kupunguziwa thawabu zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu, basi msiione Siku hiyo ni yenye kuchelewa kufika, kwani iko karibu. [Ghaafir: 17]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Hampunguzii yeyote malipo ya matendo yake hata kama ni kadiri ya mdudu chungu. Na iwapo huo uzito wa mdudu chungu ni jambo jema, basi Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa pungufu, Atamuongezea na kumkuzia mwenye kulifanya, na Atamkirimu kwa nyongeza, kwa kumpa kutoka Kwake thawabu kubwa ambazo ni Pepo. [An Nisaai: 40]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi yeyote atakayefanya jambo dogo uzito wa punje la kheri ataliona}. (7) Na yeyote mwenye kufanya baya uzito wa punje ndogo atayaona malipo yake Akhera. [Azzalzalat: 7-8]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenyezi Mungu Ataiweka Mizani ya uadilifu kwa ajili ya Hesabu katika siku ya Kiyama. Hawatadhulumiwa hawa wala wengine kitu chochote, hata kama ni kitendo, kizuri au kibaya, cha kadiri ya mdudu chungu mdogo, kitazingatiwa katika hesabu ya mwenyewe. Na inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyadhibiti matendo ya waja Wake na ni Mwenye kuwalipa kwayo. [Al Anbiyaai: 47].
Na baada ya kufufuliwa na kuhesabiwa ndiyo yanafuata malipo, aliyefanya kheri atapata neema za kudumu ambazo hazimaliziki, na aliyefanya shari na ukafiri atapa adhabu. amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ufalme na mamlaka katika Siku hii ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ataamua baina ya Waumini na makafiri. Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema, ni zao wao starehe za daima kwenye mabustani ya Pepo. Na wale walioukataa upwekwe wa Mwenyezi Mungu, wakawakanusha Mitume Wake na wakazipinga aya za Qur’ani, basi hao watapata adhabu yenye kuwafanya wanyonge na kuwatweza (kuwadhalilisha) ndani ya moto wa Jahanamu. [Al Haji: 56-57]. Na tujue kuwa maisha ya Dunia lau yangekuwa ndiyo mwisho; ingekuwa maisha na uwepo ni mchezomchezo kabisa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Je, mlidhania, enyi viumbe, ya kwamba sisi tuliwaumba Bure: hakuna maamrisho wala makatazo wala malipo mema wala mateso, na kwamba nyinyi hamtorudishwa kwetu Akhera kwa Hesabu na Malipo? [Al Mu'uminun: 115].
Msingi wa sita: kuamini Hukumu na makadirio (ya Mwenyezi Mungu) nayo ni kwamba ni wajibu kuamini kuwa Mwenyezi Mungu alishajua yote yanayotokea na yale yatakayotokea katika ulimwengu huu, na kwamba Mwenyezi Mungu ameyaandika yote hayo kabla ya kuumba mbingu na ardhi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na zipo kwake Mwenyezi Mungu ,Funguo za siri, hakuna azijuwazo ila Yeye. Miongoni mwazo ni ujuzi wa Kiyama, kuteremka mvua, viliyomo ndani ya zao, matendo ya siku zinazokuja na mahala mtu atakapokufa. Na Anajua kila kilichoko barani na baharini. Na hakuna jani, linaloanguka kutoka kwenye mmea wowote, ispokuwa analijua. Na kila chembe iliyofichika ardhini na kila kibichi na kikavu, kimethibitishwa kwenye kitabu kilicho wazi kisicho na utatizi nacho ni Al-Lawh(Al-Maḥfūẓ ( Ubao Uliohifadhiwa). [Al An'am: 59]. Na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kwa ujuzi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Aliyeziumba mbingu saba na Akaumba ardhi saba, na Akateremsha amri kupitia wahyi Aliyowateremshia Mitume Wake na kwa yale Anayowapangia viumbe wake kwayo kati ya mbingu na ardhi, ili mpate kujua , enyi watu, kwamba Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna kinachomshinda na kwamba Mwenyezi Mungu Amekizunguka kila kitu kiujuzi, basi hakuna kitu chochote kilichoko nje ya ujuzi Wake na uweza Wake. [Attwalaaq: 12]. Na kuwa halitokei katika ulimwengu huu jambo lolote ispokuwa amelikusudia na amelitaka Mwenyezi Mungu, na aliliumba na akarahisisha sababu zake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ambaye Ana ufalme wa mbingu na ardhi, Hakujifanyia mtoto na hakuwa na mshirika katika ufalme Wake. Na Yeye Ndiye Aliyeumba kila kitu, Akakisawazisha kulingana na umbo linalonasibiana nacho na inavyotakikana kulingana na hekima Yake, pasi na kupungua wala kwenda kombo. [Al Furqaan: 2]. Na katika hilo, ana hekima ya hali ya juu, ambayo watu hawawezi kuizunguka kwa maarifa na kuijua kikamilifu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hii Qur’ani iliowajia ni hekima kubwa iliyofikia upeo. Basi yatawafalia nini maonyo wale watu waliyoipa mgongo na kuikanusha? [Al Qamar: 5]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na ni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anayeanzisha uumbaji viumbe kutoka kwenye hali ya kutokuwako, kisha Atawarudisha wakiwa hai baada ya kufa. Na kuwarudishia viumbe uhai baada ya kufa ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kuanzisha kuwaumba, na yote mawili ni rahisi Kwake. Na ni ya Mwenyezi Mungu sifa ya hali ya juu katika kila anachosifiwa, Hakuna chochote mfano Wake, na Yeye Ndiye Mwenye kusikia, Ndiye Mwenye kuona, Na Yeye Ndiye Mshindi Asiyeshindwa, Ndiye Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake na uendeshaji mambo ya viumbe Vyake. [Ar Rum: 27]. Na Mwenyezi Mungu ameisifu nafsi yake kwa hekima, na akaiita nafsi yake kuwa ni mwingi wa hekima. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Ameshuhudia kuwa Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa uungu. Na Ameambatanisha ushahidi wake na ule wa Malaika na watu wa elimu juu ya kitu kitukufu zaidi chenye kushuhudiwa, nacho ni Tawhīd umoja Wake Aliyetukuka na kusimamia Kwake haki na uadilifu. Hapana Mola ispokuwa Yeye, Aliye Mshindi Ambaye hakuna kitu Atakacho kiwe kikakataa kuwa, Mwenye hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. [Al-Imran: 18]. Na amesema Mwenyezi Mungu akieleza kuhusu Issa Amani iwe juu yake, yakuwa yeye atamsemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa kusema: Hakika yako wewe , ewe Mwenyezi Mungu, ikiwa utawaadhibu, basi wao ni waja wako, na wewe ndiye Mjuzi wa hali zao, unawafanya unavyotaka kwa uadilifu wako. Na ikiwa utawasamehe, kwa rehema yako, wale waliofuata njia za kuwafanya wasamehewe, basi wewe ndiye Mshindi Asiyeshindwa, Mwenye hekima katika uendeshaji Wake wa mambo na amri Zake. Aya hii inamsifu Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa hekima Yake, uadilifu Wake na ukamilifu wa ujuzi Wake. [Al Maaidah: 118]. Na alisema Mwenyezi Mungu kumwambia Mussa alipomuita naye akiwa pembezoni mwa mlima Tur: «Ewe Mūsā! Hakika yangu mimi ni Mwenyezi Mungu ninayestahiki kuabudiwa peke yangu, ni Mshindi Mwenye nguvu wa kuwaadhibu maadui zangu, niliye na hekima katika uendeshaji wa viumbe vyangu. [An Namli: 9].
Na akaisifu Qur'ani tukufu kuwa ni hekima, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Alif, Lām, Rā’. Maneno yashatangulia, kuhusu herufi zinazokatwa, katika mwanzo wa Sura ya Al-Baqarah. Hiki ni Kitabu ambacho Mwenyezi Mungu Amemteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na ambacho aya zake zimepangwa vizuri zisizo na kasoro wala ubatilifu, kisha zimefafanuliwa kwa maamrisho na makatazo na maelezo ya halali na haramu yatokayo kwa Mwenyezi Mungu Aliye na hekima katika uendeshaji mambo Aliye Mtambuzi wa vile yanavyoishia. [Hud: 1]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hayo tuliyoyaeleza na kuyafafanua kati ya hizi hukumu tukufu za kuamrisha matendo mema na kukataza tabia mbaya, ni miongoni mwa yale tuliyokutumia wahyi nayo. Na usimfanye, ewe binadamu, pamoja na Mwenyezi Mungu yeyote kuwa ni mshirika Wake katika kumuabudu, ukaja kutiwa ndani ya moto wa Jahanamu, hali ukilaumiwa na nafsi yako na watu, na ukawa ni mwenye kufukuzwa na kuepushwa na kila kheri. [Al Israai: 39].
22- Na Manabii wote Amani iwashukie wamekingwa kutokana na kukosea katika yale wanayoyafikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na wamekingwa na yote yanayokwenda kinyume na akili, au umbile salama linayakataa, na Manabii ndio waliopewa jukumu la kufikisha amri za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na Manabii hawana chochote katika mambo maalumu ya kiuungu au kuabudiwa; bali wao ni watu kama watu wengine ila tu Mwenyezi Mungu Mtukufu anawateremshia wahyi wa ujumbe wake.
Na Manabii Amani iwashukie wamekingwa, katika yale wanayoyafikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu Mwenyezi Mungu anachagua wabora katika viumbe wake ili wafikishe ujumbe wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anateua, miongoni mwa Malaika, wajumbe wa kuwatuma kwa Manabii Wake, na Anateua kutokana na watu, wajumbe wakufikisha jumbe Zake kwa viumbe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maneno ya waja Wake, Mwenye kuviona vitu vyote na yule anayemteua kwa utume miongoni mwa viumbe Wake. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, [Al Haji: 75]. Na amesema Allah Mtukufu: Hakika Mwenyezi Mungu Amemchagua Ādam, Nūḥ, jamii ya Ibrāhīm na jamii ya 'Imrān Akawafanya kuwa ni bora wa watu wa zama zao. [Al Imran: 33]. Na amesema Allah Mtukufu: Mwenyezi Mungu Akasema, «Ewe Mūsā, Mimi nimekuchagua kati ya watu kwa ujumbe wangu kwa viumbe wangu niliokutuma kwao na kwa kusema kwangu na wewe pasi na mtu wa kati. Basi chukua niliyokupa kati ya maamrisho yangu na makatazo yangu, ushikamane nayo na uyatumie na uwe ni miongoni mwa wenye kumshukuru Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa utume aliokupa na Akakupendelea kwa maneno Yake. [Al a'raf: 144]. Na Mitume sala na salamu ziwafikie wanajua kuwa yanayoteremka kwao ni wahyi wa Mungu, na wanawashuhudia Malaika wakiteremka na wahyi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni mjuzi wa kisichoonekana na macho. Hatakitoa wazi hicho kisichoonekana kwa yeyote miongoni mwa viumbe Wake. Ispokuwa kwa yule Aliyemchagua Mwenyezi Mungu na kumpendelea kwa kumpa utume, kwani Yeye huwajuza baadhi ya yale yaliyofichika yasionekane. Na Anatuma, mbele ya huyo Mtume na nyuma yake, Malaika wenye kumhifadhi na majini, ili wasisikilize kwa kuiba jambo hilo la ghaibu, kisha wakaambiana kwa siri kisha wakawadokeza makuhani. Ili Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ajue kwamba Mitume kabla yake walikuwa kwenye hali kama yake ya ufikishaji haki na ukweli, na kwamba yeye atalindwa kutokana na majini kama walivyolindwa wao, na kwamba Mwenyezi Mungu, ujuzi Wake umeyazunguka mambo yao waliyonayo ya nje na ya ndani, miongoni mwa sheria na hukumu na mengineyo, hakuna chochote kinachompita katika hayo, na kwamba Yeye Amekidhibiti kila kitu kwa hesabu, hakuna chochote kinachofichikana Kwake. [Al Jinni: 26-28]. Na Mwenyezi Mungu akawaamrisha kufikisha ujumbe wake. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ewe Mtume, fikisha wahyi wa Mwenyezi Mungu uliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako. Na iwapo utapunguza bidii katika kuufikisha, ukaficha chochote katika wahyi huo, basi utakuwa hukuufikisha ujumbe wa Mola wako. Na kwa hakika, Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alifikisha ujumbe wa Mola wake kikamilifu. Basi yeyote atakayedai kuwa yeye alificha chochote, katika yale aliyoteremshiwa, atakuwa amemzulia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake uongo mkubwa. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mwenye kukulinda na kukuokoa na maadui zako. Si juu yako lolote ispokuwa ni kufikisha. Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamuelekezi kwenye uongofu aliyepotea njia ya haki na akayapinga uliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. [Al Maaida: 67]. Na amesema Allah Mtukufu: Nimewatuma wajumbe kwa viumbe wangu wakatoe habari njema ya malipo yangu mema na waonye juu ya adhabu yangu, ili wanadamu wasiwe na hoja watakayoifanya ni kisingizio cha udhuru baada ya kutumiliza Mitume. Na daima Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika mamlaka Yake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake. [An Nisaai: 165].
Na Mitume sala na salamu ziwe juu yao, wanamuogopa Mwenyezi Mungu kumuogopa kwa hali ya juu, na wanamkhofu, hawazidishi katika ujumbe wake wala hawapunguzi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na lau Muhammad angelitusingizia maneno tusiyoyanena tungelimtesa na tungelimkamata kwa nguvu na uweza, kwani nguvu ya kila kitu iko kwenye upande wake wa kulia, kisha tungelimkata mshipa wa moyo wake., hataweza yeyote kuyazuia mateso yetu yasimpate. [Al Haqa: 44-47]. Amesema Imamu Ibni Kathiir Mwenyezi Mungu amrehemu: (Anasema Allah Mtukufu: {Na lau angelitusingizia} Yaani: Muhammadi rehema na Amani zimfikie ingelikuwa kama wanavyodai wanaotuzulia uongo, akazidisha katika ujumbe au akapunguza, au akasema chochote cha kwake halafu akakinasbisha kwetu- na hali si hivyo- Tungelimuadhibu haraka mno, na kwasababu hii akasema: {Tungelimkamata kwa mkono wa kulia} yasemekana kuwa: Maana yake tungemlipizia kwa mkono wa kulia; kwasababu yeye ni mkali katika kukamata, na yasemekana: Tungeliukamata mkono wake wa kulia. Na amesema Allah Mtukufu: {Na aliposema Mwenyezi Mungu, Ewe Isa bin Mariam, hivi wewe uliwaambia watu kuwa nifanyeni mimi na mama yangu miungu wawili kinyume na Mwenyezi Mungu? Atasema, 'Umetakasika, haiwi kwangu kusema lile lisilolahaki kwangu, ikiwa nililisema hilo basi hakika ulilijua, unayajua yaliyomo nafsini mwangu na wala siyajui yaliyo nafsini mwako, Hakika wewe ni mjuzi zaidi wa ghaibu. Sikuwaambia ila yale uliyoniamrisha kwayo, yakwamba muabuduni Mwenyezi Mungu Mola wangu na Mola wenu, na nilikuwa shahidi juu yao katika muda nilipokuwa nao, na pindi uliponifisha, ulikuwa wewe ndiye muangalizi juu yao, na wewe juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia}. [Al Maaidah: 116-117].
Na katika fadhila za Mwenyezi Mungu kwa Manabii wake na Mitume wake sala na salamu ziwe juu yao, anawapa nguvu katika kuufikisha kwao ujumbe wake. Amesema Mungu Mtukufu: {Akasema; mimi namshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, yakwamba mimi niko mbali na hao mnaowashirikisha (na Mwenyezi Mungu)} (54) Mkamuacha yeye (siwaogopi siwajali) Basi nyote nifanyieni hila za kunidhuru na kuniua, kisha msinipe muhula wowote}. (55) «Mimi nimetegemea kwa Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu, Mmiliki wa kila kitu na Mwenye kukiendesha. Hakuna kitu chenye kunipata ispokuwa kwa amri Yake. Na Yeye Ndiye Muweza wa kila kitu, Hakuna kitu chochote kinachotambaa kwenye ardhi hii ispokuwa Mwenyezi Mungu Amekimiliki na kiko chini ya mamlaka Yake na uendeshaji Wake. Hakika Mola wangu Yuko kwenye njia iliyolingana sawa, kwa maana kwamba ni muadilifu katika hukumu Zake, sheria Zake na amri Zake, Anamlipa mwema kwa wema Wake na muovu kwa uovu wake. [Hud: 54-56]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika washirikina walikaribia kukuepusha, ewe Mtume, na Qur’ani Aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu ili utuzulie isiyokuwa hiyo tuliyokuletea wahyi nayo. Na lau ungelifanya walivyotaka, wangelikufanya ni kipenzi msafiwa. Na lau siyo sisi kukuimarisha kwenye haki na kukuhifadhi usikubaliane nao, ungelikaribia kuelemea kwao kidogo katika yale waliyokushauri kwa nguvu za udanganyifu wao na wingi wa hila zao na kuwa na hamu kwako waongoke. Na lau ungelielemea, ewe Mtume, upande wa hawa washirikina maelemeo madogo katika yale waliyotaka kwako, basi tungelikuonjesha mara mbili zaidi ya adhabu ya duniani na mara mbili zaidi ya adhabu ya baada ya kufa kesho Akhera, hivyo ni kwa ajili ya kutimia neema ya Mwenyezi Mungu kwako na ukamilifu wa kumjua Mola wako, kisha hutampata yeyote mwenye kukuepushia adhabu yetu. [Al Israai: 73-75]. Na Aya hizi na zile zilizotangulia kabla yake zinashuhudia na ni dalili kuwa Qur'an ni uteremsho wa Mola mlezi wa walimwengu; kwasababu lau kama ingelikuwa inatoka kwa Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie, isingefungamana na maneno mfano wa haya yanayomuelekea yeye.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakinga Mitume wake kutokana na watu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ewe Mtume, fikisha wahyi wa Mwenyezi Mungu uliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako. Na iwapo utapunguza bidii katika kuufikisha, ukaficha chochote katika wahyi huo, basi utakuwa hukuufikisha ujumbe wa Mola wako. Na kwa hakika, Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alifikisha ujumbe wa Mola wake kikamilifu. Basi yeyote atakayedai kuwa yeye alificha chochote, katika yale aliyoteremshiwa, atakuwa amemzulia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake uongo mkubwa. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mwenye kukulinda na kukuokoa na maadui zako. Si juu yako lolote ispokuwa ni kufikisha. Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamuelekezi kwenye uongofu aliyepotea njia ya haki na akayapinga uliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. [Al Maaida: 67]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wasimulie, ewe Mtume, makafiri wa Maka habari ya Nūḥ, amani imshukie, pamoja na watu wake alipowaambia, «Ikiwa imekuwa ni uzito kwenu kukaa kwangu na nyinyi kuwakumbusha hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake, basi ni kwa Mwenyezi Mungu ndio mategemeo yangu, na matumaini yangu yako Kwake Yeye. Basi tayarisheni mambo yenu na waiteni washirika wenu, kisha msiyafanye mambo yenu yafichike bali yawe waziwazi yenye kuonekana, kisha amueni juu yangu mateso na mabaya mnayoyaweza wala msinipe muhula wa saa moja ya mchana. [Yunus: 71]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akielezea kuhusu kauli ya Mussa Amani imshukie: {Wakasema (Musa na Harun) Ewe Mola wetu! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mpaka juu yetu, au akapandwa kiburi juu yetu. (Mungu) Akasema; 'Msiogope, bila shaka mimi niko pamoja nayi nasikia na ninaona}. [Twaha: 45-46]. Akabainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kwamba Yeye amewahifadhi Mitume wake Amani iwe juu yao, kutokana na maadui zao, hawawezi kuwafikia kwa ubaya, na akaeleza Allah wa Kweli aliyetakasika kwamba Yeye anauhifadhi wahyi (ufunuo) wake hauongezwi wala haupunguzwi ndani yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Nabii Muhammad, rehema na amani zimshukie, na hakika sisi tunachukua ahadi kuitunza isiongezwe, isipunguzwe wala sehemu yoyote katika hiyo isipotee. [Al Hijri: 9].
Na Manabii Amani iwashukie wamekingwa na yote yanayokwenda kinyume na Akili au Tabia njema; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimsifia Nabii wake Muhammadi: Na hakika wewe, ewe Mtume, uko juu ya tabia kubwa, nazo ni zile tabia njema zilizomo kwenye Qur’ani. Kwani kule kuifuata Qur’ani kulikuwa ni sifa yake, akitekeleza amri zake na kukomeka na yale yanayokatazwa nayo. [Al Qalam: 4]. Na akasema kuhusu yeye pia: Hakuwa Muhammad mnayemjua ni mwendawazimu. [Attakwir: 22]. Na hivyo mpaka wasimame kuutekeleza ujumbe, kusimama kwa ubora zaidi, Na Manabii Amani iwashukie ndio waliobebeshwa jukumu la kufikisha amri za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, hawana chochote katika mambo maalumu ya kiuungu au kuabudiwa, bali wao ni watu kama watu wengine waliosalia, Mwenyezi Mungu anawateremshia ujumbe wake tu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mitume waliposikia yale yaliyosemwa na watu wao waliwaambia, «Ni kweli kwamba sisi hatukuwa ispokuwa ni binadamu kama nyinyi, kama mlivyosema. Lakini Mwenyezi Mungu Anawafanyia wema Anaowataka miongoni mwa waja wake kwa kuwapa neema Zake na kuwateua kwa kuwapa utume Wake. Na hizo dalili waziwazi mlizozitaka, haiwezekani sisi kuwaletea ispokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na taufiki Yake. Na kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake wanategemea Waumini katika mambo yao yote. [Ibrahim: 11]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimuamrisha Mtume wake rehema na Amani zimfikie aseme kuwaambia watu wake: Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Kwa kweli, mimi ni binadamu kama nyinyi, ninaletewa wahyi kutoka kwa Mola wangu kwamba mola wenu ni Mola Mmoja. Basi yeyote anayependa kukutana na Mola wake na ana matumaini kupata malipo yake mazuri basi na atende matendo mema kwa ajili ya Mola wake na asimshirikishe yeyote pamojanaye katika ibada.» [Al Kahf: 110].
23- Na uislamu unalingania katika kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, kupitia misingi mikubwa ya ibada nayo ni: Swala ambayo ni kusimama na kurukuu na kusujudu, na kumtaja Mwenyezi Mungu na kumsifia yeye na kumuomba, mtu anatakiwa kuswali kila siku mara tano, na zinaondoka ndani yake tofauti, tajiri na maskini Raisi na raia wote wanasimama katika safu moja katika swala. Na (kutoa) Zaka: Nayo ni kiwango kidogo cha mali- kulingana na sharti na viwango alivyoviweka Mwenyezi Mungu- ni wajibu katika mali za wenye uwezo, zinagawanywa kwa mafukara na wengineo, mara moja kwa mwaka. Na swaumu: Nayo ni: Kujizuia na vyenye kufunguza (kula na kunywa) katika mchana wa mwezi wa Ramadhani, hii inalea nafsi kuwa na maamuzi na uvumilivu. Na Hija nayo ni: Kwenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu katika mji Mtukufu wa Makka mara moja katika umri kwa mwenye uwezo (wa mali) na uwezo (wa Afya), Na katika Hija hii wanalingana watu wote katika kumuelekea Muumba wao Mtukufu, na zinaondoka kati yao tofauti na kujinasibisha na vyeo au chochote.
Uislamu unalingania katika kumuabudu Mwenyezi Mungu kupitia ibada kubwa, na ibada nyinginezo, Na hizi ibada tukufu ameziwajibisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Manabii na Mitume wote sala na salamu ziwe juu yao, na ibada kubwa kuliko zote ni:
Ya kwanza ni Swala: Ameifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa kila muislamu kama alivyoifaradhisha kwa Manabii na Mitume wote sala na salamu ziwe juu yao, na Mwenyezi Mungu akamuamrisha Nabii wake kipenzi Ibrahim Amani iwe juu yake aisafishe nyumba yake (Al ka'aba) kwaajili ya wanaotufu (kuizunguka) na wenye kuswali wenye kurukuu na kusujudu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Kumbuka, ewe Nabii, wakati tulipoifanya Alka'ba ni marejeo ya watu; wanakuja kuikusudia, kisha wanarudi makwao kwa watu wao, kisha wanairudia tena, ni makusanyiko yao katika Hija, Umra, kutufu na kuswali, na pia ni amani kwao: hakuna adui anayewashambulia wakiwa hapo na tukasema, “Pafanyeni hapo Maqām Ibrāhīm ni mahali pa kuswali. Maqām Ibrāhīn ni jiwe ambalo Ibrāhīm alisimama juu yake alipokuwa akijenga Alka'ba. Na tulimletea Wahyi Ibrahīm na mtoto wake Ismāīl kwa kuwaambia, «Isafisheni Nyumba Yangu na kila najisi na uchafu kwa ajili ya wenye kuabudu kwa kutufu pembezoni mwa Alka'ba au kuketi Itikafu (I’tikāf) Msikitini na kuswali hapo.” [Al Baqarah: 125] Na Mwenyezi Mungu akaiwajibisha kwa Mussa katika wito wake wa kwanza kwa Mussa Amani imshukie. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mimi ni Mola wako, vua viatu vyako, wewe sasa uko kwenye bonde la Tuwā. Na mimi nimekuteua , ewe Mūsā, kwa ujumbe wangu, basi sikiliza yale unayoletewa ya wahyi kutoka kwangu. Mimi Ndiye Mwenyezi Mungu, hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki ispokuwa mimi, sina mshirika, basi niabudu mimi na usimamishe Swala ili unikumbuke ndani yake. [Twaha: 12-14]. Na alieleza Masihi Issa Amani imshukie kwamba Mwenyezi Mungu alimuamrisha kuswali na kutoa zaka, akasema kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu Mtukufu: «Na Amenifanya niwe na wingi wa baraka na manufaa popote niwapo, na ameniusia kutunza Swala na kutoa Zaka muda wa mimi kuwa hai. [Mariam: 31]. Na swala katika uislamu, ni kusimama na kurukuu na kusujudu na kumtaja Mwenyezi Mungu na kumsifia yeye na kumuomba, anaswali mtu kila siku mara tano, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Zihifadhini, enyi Waislamu, Swala tano zilizofaradhiwa kwa kudumu nazo katika kuzitekeleza kwa nyakati zake, sharti zake, nguzo zake zinazopasa juu yake. Na muhufadhi swala iliyo katikati ya swala hizo, nayo ni Swala ya Alasir Na simameni katika Swala zenu hali ya kumtii Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea na kumdhalilikia. [Al Baqara: 238]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Simamisha Swala itimie kuanzia kipindi cha kupinduka jua wakati wa mchana mpaka kipindi cha usiku. Inaingia hapa Swala ya Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na Isha. Na simamisha Swala ya Alfajiri na urefushe kisomo chake, kwani Swala ya Alfajiri inahudhuriwa na Malaika wa usiku na Malaika wa mchana. [Al Israai: 78]. Amesema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Ama rukuu Mtukuzeni hapo Mola aliyetakasika na Kutukuka, na Ama sijida jitahidini kuomba dua ndani yake, ni matarajio makubwa ya kujibiwa (mkiwa hapo)" Swahiih Muslim
Ya pili ni Zaka: Ameifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa waislamu kama alivyoifaradhisha kwa Manabii na Mitume waliotangulia sala na salamu ziwe juu yao, nacho ni kiwango kidogo kutoka katika mali -kulingana na sharti za viwango alizoziweka Mwenyezi Mungu- ni wajibu kutoa katika mali za wenye uwezo, hupewa mafukara na wengineo mara moja kwa mwaka. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Chukua, ewe Mtume, kwenye mali zao, sadaka na uwasafishe wao na uchafu na uwatakase madhambi yao,na watakie wao msamaha wa madhambi yao na uwaombee stara ya hayo, kwani maombi yako na utakaji msamaha wako utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Msikivu wa kila maombi na kila neno, ni Mjuzi wa hali za waja Wake na nia zao. [Attauba: 103]. Na pindi Mtume rehema na Amani zimfikie alipomuagiza Mu'adh radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie kwenda Yemen, alisema kumwambia: "Hakika wewe unawaendea watu wa kitabu (Mayahudi na Manaswara), waite katika kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah, nakuwa mimi ni Mjumbe wa Allah, na ikiwa wao watakutii katika hilo, wafahamishe kuwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka amewafaradhishia swala tano usiku na mchana, basi ikiwa kama watakutii katika hilo, wafahamishe kuwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka amewafaradhishia sadaka katika mali zao, zinachukuliwa kutoka kwa wale wenye uwezo katika wao na zinarejeshwa kwa mafukara wao, na ikiwa watakutii katika hilo, Tahadhari sana na mali zao za thamani, na ogopa sana maombi ya mtu aliyedhulumiwa, kwasababu hayo hayana kizuizi kati yake na Mwenyezi Mtukufu". Kaipokea Tirmidhiy (625).
Ya tatu ni Swaumu: Ameifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa waislamu kama alivyoifaradhisha kwa Manabii na Mitume waliotangulia sala na salamu ziwe juu yao, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi ambao mmemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkaifuata Sheria Yake kivitendo, Mwenyezi Mungu Amewafaradhishia kufunga, kama Alivyowafaradhishia umma waliokuweko kabla yenu, ili mpate kumcha Mola wenu na kuweka kinga kati yenu na maasia, kwa kumtii na kumuabudu Peke Yake. [Al Baqara: 183]. Nayo ni: Kujizuia na vyote vyenye kufunguza (vyakula na vinywaji) katika mchana wa ramadhani, inalea na kukuza maamuzi na uvumilivu katika nafsi. Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Swaumu ni ya kwangu mimi, na mimi ndiye ninayeilipa, (Mja wangu) anaacha matamanio yake na vyakula vyake na vinywaji vyake kwaajili yangu, na swaumu ni kinga, na kwa mfungaji ana furaha mbili: furaha wakati anafuturu, na furaha wakati anakutana na Mola wake". Sahihi Bukhariy 7492,
Ya nne ni Hija: Ameifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa waislamu kama alivyoifaradhisha kwa Manabii na Mitume waliotangulia sala na salamu ziwe juu yao, na Mwenyezi Mungu akamuamrisha Nabii wake kipenzi Ibrahim, atoe tangazo la Hija. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: na uwajulishe watu, ewe Ibrāhīm, uwajibu wa Hija juu yao, watakujia kwa kila namna zao, wakiwa wanatembea kwa miguu na wakiwa wamepanda, miongoni mwa ngamia, kila aliyeambata matumbo kwa kutembea na kufanya kazi na sio kwa udhaifu. Watakuja kutoka njia ya mbali, [Al Haji: 27]. Na Mwenyezi Mungu akamuamrisha aisafishe nyumba kongwe kwaajili ya Mahujaji, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Taja, ewe Nabii, pindi tulipomuelezea Ibrāhīm, amani imshukie, mahali pa Nyumba, tukamtayarishia yeye mahali hapo, na palikua hapajulikani. Na tulimuamrisha aijenge juu ya misingi ya kumcha Mwenyezi Mungu na kumpwekesha na aisafishe na ukafiri na mambo ya uzushi na uchafu, ili iwe ni mahali pakunjufu kwa wenye kuizunguka kwa kutufu na wenye kuswali hapo. (Al Hajj 26)
Na Hijja: Ni kuikusudia (kwa kwenda) nyumba ya Mwenyezi Mungu katika mji mtukufu wa Makka, kwaajili ya kazi maalumu mara moja katika umri kwa Mwenye uwezo na akaweza, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko, na atakayekanusha (Na asiende na haliyakuwa anauwezo) Basi Mwenyezi Mungu si muhitaji wa kuwahitajia walimwengu}. [Al-Imran: 97]. Na katika Hija wanakusanyika waislamu sehemu moja wakimtakasia ibada muumbaji aliyetakasika, na mahujaji wote wanatekeleza sheria za Hija kwa mfumo mmoja wenye kufanana, zinaondoka ndani yake tofauti za kimazingira na tamaduni, na daraja za kimaisha.
24- Na katika mambo makubwa yanayozifanya Ibada za uislamu kuwa za kipekee, nikuwa namna ya utekelezaji wake na sharti zake alizoziweka Mwenyezi Mungu Mtukufu kama sheria, na akazifikisha Mtume rehema na Amani zimfikie, na hawakuziingilia binadamu kwa kuongeza wala kupunguza mpaka leo hii, na ibada zote hizi kubwa walilingania juu ya hizo Manabii Amani ziwafikie.
Na katika mambo makubwa yanayozifanya Ibada za uislamu kuwa za kipekee, nikuwa namna ya utekelezaji wake na sharti zake alizoziweka Mwenyezi Mungu Mtukufu kama sheria, na akazifikisha Mtume rehema na Amani zimfikie, na hawakuziingilia binadamu kwa kuongeza wala kupunguza mpaka leo hii, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimezitimiza kwenu nyinyi neema zangu, na nimeridhia kwenu uislamu kuwa ndiyo Dini (yenu). (Al Maida 3) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi shikamana, ewe Mtume, na kile alichokuamrisha Mwenyezi Mungu katika hii Qur’ani ambayo Mwenyezi Mungu amekuletea, kwa njia ya wahyi. Hakika wewe uko kwenye njia iliyonyooka, nayo ni Dini ya Mwenyezi Mungu aliyoamrisha ifuatwe ambayo ni Uislamu. Hapa pana kumpa moyo Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kumsifu. [Azzukhruf: 43]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu swala: Mtakapomaliza Swala, endeleeni kumtaja Mwenyezi Mungu katika hali zenu zote. Na hali ya hofu iondokapo, itekelezeni Swala kikamilifu, wala msiifanyie dharau, kwani Swala ni faradhi katika nyakati zijulikanazo katika Sheria. [An Nisaai: 103]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu mgawanyo ya Zaka: Zaka za lazima zinapewa wahitaji wasiomiliki kitu, masikini wasiomiliki kiwango kinachowatosha kwa mahitaji yao, wenye kuzishughulikia kwa kuzikusanya,wale ambao wanazoeshwa nyoyo zao, miongoni mwa wale mnaotarajia wasilimu au ipate nguvu Imani yao au wawe na manufaa kwa Waislamu au mzuie kwazo madhara ya mtu yeyote yasiwafikie Waislamu. Pia zinatolewa katika kuacha huru watumwa na wale wenye mikataba ya uhuru. Na zinatolewa kupewa wenye kuingia kwenye madeni kwa sababu ya kuleta maelewano baina ya watu na wenye kuelemewa na madeni waliyokopa kwa lengo lisiliokuwa la uharibifu au utumiaji wa kupita kiasi kisha wakashindwa kulipa. Na zinapewa wapiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na zinapewa msafiri aliyeishiwa na matumizi. Ugawaji huu ni lazima Aliyoifaradhisha Mwenyezi Mungu na Akaikadiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mno wa mambo yanayowafaa waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo na sheria Zake. [Attauba:60]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika swaumu: Mwezi wa Ramadhani ambao Ameanza Mwenyezi Mungu kuteremsha Qur’ani, ili iwe ni muongozo wa watu. Ndani yake Amezifungua wazi dalili za uongofu wa Mwenyezi Mungu na upambanuzi baina ya haki na batili. Kwa hivyo, mtu atakayeufikia mwezi huo, akawa ni mzima na mkazi wa mjini, basi na aufunge mchana wake.na atakayekuwa Mgonjwa au nimsafiri wanaruhusiwa kufungua, kisha walipe idadi ya siku walizofungua. Mwenyezi Mungu Anawatakia wepesi katika Sheria Zake, wala Hawatakii uzito na tabu, na ili mpate kukamilisha idadi ya kufunga mwezi mzima na mmalize kufunga kwa kumtukuza Mwenyezi Mungu katika Idi ya Mfungo na mpate kumshukuru. [Al Baqara: 185]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Hija: Wakati wa Hija ni miezi ijulikanayo, nayo ni Mfungomosi, Mfungopili na siku kumi za Mfungotatu. Basi mwenye kujilazimisha nafsi yake kuhiji ndani ya miezi hiyo, kwa kutia nia ya kuhirimia Hija, ni haramu kwake kufanya tendo la ndoa na vitangulizi vyake vya kimaneno na kivitendo. Pia ni haramu kwake kutoka kwenye twaa ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa kutenda maasi, kubishana, katika Hija, Na wema wowote mnaoufanya, Mwenyezi Mungu Anaujua, na Atamlipa kila mtu kwa amali yake. Na jichukulieni matumizi, na akiba ya amali njema kwa nyumba ya Akhera. Hakika akiba iliyo bora zaidi ni kumuogopa Mwenyezi Mungu. Basi niogopeni, enyi wenye akili timamu. [Al Baqara: 197]. Na ibada zote hizo tukufu walilingania kwazo Manabii wote Amani iwashukie.
25- Mtume wa uislamu ni Muhammadi bin Abdillaah kutoka katika kizazi cha Ismail bin Ibrahim Amani iwe juu yao, alizaliwa Makka Mwaka 571 A.D, na akapewa Utume akiwa huko (Makka), na akahama kwenda Madina, na hakushirikiana na watu wake katika mambo ya masanamu, lakini alikuwa akishirikiana nao katika kazi nzuri, na alikuwa katika tabia njema na tukufu kabla hata ya kupewa kwake Utume, na watu wake walikuwa wakimuita 'Muaminifu', Na Mwenyezi Mungu alimpa Utume alipofikisha umri wa Miaka Arobaini, na Mwenyezi Mungu akampa nguvu kwa Alama (Miujiza) Mikubwa, na mkubwa kuliko yote ni Qur'an tukufu, nao ndio muujiza mkubwa kwa Manabii, na ndio muujiza uliobakia katika miujiza ya Manabii mpaka leo hii, na pindi Mwenyezi Mungu alipoikamilisha Dini kupitia yeye, na akaifikisha Mtume rehema na Amani zimfikie kwa kiwango cha kutosha, akafariki na umri wake ukiwa ni Miaka sitini na tatu (63) na akazikwa katika mji mtukufu wa Madina rehema na Amani zimfikie, Na Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie ndiyo mwisho wa Manabii na Mitume, Mwenyezi Mungu alimtuma kwa uongofu na Dini ya haki, ili aje kuwatoa watu katika giza la masanamu na ukafiri na ujinga awalete katika mwangaza wa Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) na Imani, Na Mwenyezi Mungu amemshuhudilia kuwa yeye alimtuma kuwa mlinganizi kwa hilo.
Mtume wa uislamu ni Muhammadi bin Abdillaah kutoka katika kizazi cha Ismail bin Ibrahim Amani iwe juu yao, alizaliwa Makka Mwaka 571 A.D, na akapewa Utume akiwa huko (Makka), na akahama kwenda Madina, na watu wake walikuwa wakimuita 'Muaminifu', na hakushirikiana na watu wake katika mambo ya masanamu, lakini alikuwa akishirikiana nao katika kazi nzuri, alikuwa katika tabia njema na tukufu kabla hata ya kupewa kwake Utume, Na Mola wake amemsifia kwa tabia tukufu akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu yeye: Na hakika wewe, ewe Mtume ni mwenye tabia njema zaidi, nazo ni zile tabia njema zilizomo kwenye Qur’ani. Kwani kule kuifuata Qur’ani kulikuwa ni sifa yake, akitekeleza amri zake na kukomeka na yale yanayokatazwa nayo. [Al Qalam: 4]. Na Mwenyezi Mungu alimpa Utume alipofikisha Miaka Arobaini, na akampa nguvu kwa Alama (Miujiza), Na muujiza Mkubwa kuliko yote ni Qur'an Tukufu: Amesema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakuna yeyote katika Manabii ispokuwa alipewa mfano wa yale waliyoyaamini watu, na hakika niliyopewa mimi ni (wahyi), ufunuo wa Mwenyezi Mungu alionifunulia, basi nataraji kuwa na wafuasi wengi kuliko wao siku ya Kiyama". Swahiih Al Bukhaariy Na Qur'ani tukufu ni wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake rehema na Amani zimfikie. Amesema Mwenyezi Mungu kuhusu yeye: Hicho ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake ,na ni muungozo kwa wanaomcha mwenyezi mungu. [Al Baqara: 2]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hivi kwa nini hawaizingatii Qur'an,na lau kwamba ingekuwa inatoka kwa asiyekuwa mwenyezi mungu basi mnge;iona tofauti nyingi. [An Nisaai: 82]. Na Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto majini na wanadamu juu ya kuleta mfano wake, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, «Lau wataafikiana majini na binadamu kujaribu kuleta mfano wa hii Qur’ani yenye kuelemea, hawataweza kuileta, hata kama watashirikiana na kusaidiana kufanya hivyo.» [Al Israai: 88]. Na akawapa changamoto walete sura kumi mfano wake, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Au wanasema ameizua hii Qur’ani? Waambie basi, «Iwapo mambo ni kama mnavyodai, leteni sura kumi mfano wake za kuzuliwa, na muwaite mnaowaweza miongoni mwa viumbe wote wa Mwenyezi Mungu, ili wawasaidie kuzileta hizi sura kumi, iwapo nyinyi ni wa kweli katika madai yenu. [Hud: 13]. Bali aliwapa changamoto walete sura moja kama mfano wake, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na mkiwa, enyi makafiri, mna shaka juu ya Qurani tuliyomteremshia mja wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukie, na mkadai kuwa haitoki kwa Mwenyezi Mungu, basi leteni sura moja inayofanana na sura ya Qurani, na takeni msaada kutoka kwa yeyote mnayemuweza ili awasaidie, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu. [Al Baqara: 23].
Na Qur'ani tukufu ni Alama (Muujiza) wa kipekee uliobakia katika alama za Manabii mpaka leo, na pindi Mwenyezi Mungu alipoikamilisha dini kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, na akaifikisha kwa kiwango cha kufikisha, Mtume rehema na Amani zimfikie alifariki, na umri wake ukiwa ni Miaka sitini na tatu (63) na akazikwa katika mji mtukfu wa Madina rehema na Amani zimfikie:
Na Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie ndio mwisho wa Mitume na Manabii, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakuwa Muhammad ni baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Manabii, hakuna unabii baada yake mpaka Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu kwa kila jambo miongoni mwa matendo yenu ni mjuzi, hakuna chenye kufichikana Kwake. [Al Ahzaab: 40]. Na katika Sahihi Al-Bukhari pia kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alisema: (Hakika mfano wangu mimi na mfano wa Manabii waliokuwa kabla yangu ni kama mtu aliyejenga nyumba nzuri na akaipendezesha lakini akaacha sehemu ya tofari moja katika kona, ikawa watu wanaizunguka nyumba hiyo na kuishangaa huku wakisema: Kwanini usingeliweka tofari hilo? Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: Mimi ndiyo tofari hilo na mimi ni mwisho wa Mitume) ((188)). Swahiih Al Bukhaariy Na katika Injili alisema Nabii Issa Amani ya Mwenyezi Mungu Imfikie, akimtabiri Mtume Muhammdi rehema na Amani zimfikie: (Jiwe walilolikataa mafundi ndio limekuwa kichwa cha kona, kwani hamkuwahi kusoma katika kitabu: Yesu alisema kuwaambia, limekuwa hili kutoka kwa Mungu nalo ni ajabu machoni mwetu). Na katika kumbukumbu la Torati Agano jipya, imekuja ndani yake kauli ya Mussa amani imfikie: (Ninawaachia Nabii kutoka katikati ya ndugu zao mfano wako, na nitayafanya maneno yangu kuwa kinywani mwake, atawazungumzisha kwa yote niliyokuusia kwayo).
Na Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie Mwenyezi Mungu kamtuma kwa uongofu na Dini ya haki, na akamshuhudilia Mwenyezi Mungu kuwa yeye ni wa haki, nakuwa yeye kamtuma kuwa mlinganiaji katika hilo kwa idhini yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Iwapo Mayahudi na wengineo watakukanusha, ewe Mtume, hakika Mwenyezi Mungu Anashuhudia kuwa wewe ni Mtume Wake Aliyemteremshia Qur’ani tukufu; Ameiteremsha kwa ujuzi Wake. Na vilevile Malaika wanashuhudia ukweli wa wahyi uliyoletewa. Na ushahidi wa Mwenyezi Mungu Peke Yake unatosha. [An Nisaai: 166]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Yeye Ndiye Aliyemtumiliza Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa ubainifu ulio wazi na Dini ya Uislamu, ili aifanye kuwa juu ya mila zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi kwamba Yeye ni Mwenye kukupa ushindi na kuidhihirisha Dini yako juu ya kila dini. [Al Fat-hi: 28]. Mwenyezi Mungu alimtuma kwa uongofu, ili awatoe watu katika giza la masanamu na ukafiri na ujinga, kuwaleta katika mwangaza wa Imani na Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa kitabu hiki chenye ufafanuzi, Mwenyezi Mungu Anawaongoza wenye kufuata yenye kumridhi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, njia za amani na usalama, Anawatoa kutoka kwenye giza la ukafiri kuwapeleka kwenye mwangaza wa Imani na Anawaafikia (anawawezesha) wao kufuata dini Yake iliyolingana sawa. [Al Maaida: 16]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Alif, Lām, Rā. Hii Qur’ani ni kitabu tulichokuletea wahyi ili uwatoe binadamu kutoka kwenye upotevu na upotovu kuwapeleka kwenye uongofu na mwangaza, kwa idhini ya Mola wao na taufiki Yake kwao, kwenye Uislamu ambao ndio njia ya Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda Anayehimidiwa kwa kila hali. [Ibrahim: 1].
26- Na sheria za Uislamu alizokujanazo Mtume Muhammadi rehema na amani zimfikie, ndiyo za mwisho katika jumbe za Mwenyezi Mungu, na sheria za Mola, nazo ni sheria zilizo kamilika, na ndani yake kuna kutengemaa kwa Dini na Dunia ya watu na damu zao na mali zao na akili zao na vizazi vyao, nayo inafuta sheria zote zilizotangulia, kama zilivyofuta sheria zilizotangulia baadhi yake kwa baadhi.
Sheria za Uislamu alizokujanazo Mtume Muhammadi rehema na amani zimfikie, ndiyo za mwisho katika jumbe za Mwenyezi Mungu, na sheria za Mola, na ameikamilisha Mwenyezi Mungu Dini kupitia ujumbe huu, na akazitimiza neema kwa watu kwa kumtuma Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie. Amesema Mwenyezi Mungu: Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini (Al Maida 3)
Na sheria ya Uislamu ndiyo sheria iliyokamilika, na ndani yake kuna kutengemaa kwa Dunia yao, kwasababu sheria hii imekusanya yote yaliyoko katika sheria zilizotangulia, na ikayakamilisha na ikayatimiza. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwa mja wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, inawaongoza watu kwenye njia nzuri kabisa nayo ni mila ya Kiislamu, na inawapa bishara njema Waumini, wanaofanya yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaamrisha kwayo na wanaokomeka na yale ambayo Amewakataza nayo, kwamba watakuwa na malipo makubwa, [Al Israai: 9]. Na sheria ya Uislamu imeweka kwa watu ahadi nzito iliyokuwa katika umma zilizotangulia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ambao wanaomfuata Mtume aliye Nabii, ambaye hasomi wala haandiki, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukie, ambaye wanazipata sifa zake na mambo yake yameandikwa huko kwao katika Taurati na Injili; anawaamrisha kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii na kila lijulikanalo kuwa ni jema, na anawakataza ushirikina na maasia na kila lijulikanalo kuwa ni baya, na anawahalalishia vizuri vya vyakula na vinywaji na kuoana, na anawaharamishia vichafu vya hivyo kama nyama ya nguruwe na vile ambavyo walikuwa wakijihalalishia miongoni mwa vyakula na vinywaji ambavyo aliviharamisha Mwenyezi Mungu, na anawaondolea wao mambo magumu waliokalifishwa nayo kama kukata mahali pa najisi nguoni, kuzichoma moto ngawira, ulazimu wa kisasi juu ya aliyeua kwa kukusudia au kwa kukosea. Basi wale ambao walimuamini Nabii asiyejua kuandika wala kusoma kilichoandikwa, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukie, na wakaukubali unabii wake, wakamuheshimu, wakamtukuza na wakamuhami na wakaifuata Qur’ani aliyoteremshiwa, wakaufuata mwenendo wake kivitendo, hao ni wenye kufaulu kwa kupata yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaahidi waja wake Waumini. [Al A'raf:157].
Na sheria ya Uislamu imefuta sheria zote zilizotangulia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani. Na yote yaliyomo ndani yake ni haki, yanatoa ushahidi juu ya ukweli wa Vitabu kabla yake na kwamba -vitabu hivyo- vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, hali ya kuuthibitisha usahihi uliomo, kuufafanua upotovu uliomo na kuzifuta baadhi ya sheria zake. Kwa hivyo, wahukumu kati ya wale Mayahudi wanaoshitakiana kwako kwa sheria zile ulizoteremshiwa katika hii Qur’ani, wala usiiepuke haki, ambayo Mwenyezi Mungu Amekuamrisha uitumie, ukafuata matakwa yao na yale waliyoyazoea. Kwani kila kundi la watu tumewawekea sheria na njia iliyo wazi ya wao kuifuata. Na lau Mwenyezi Mungu Angelitaka, Angelizifanya sheria zenu kuwa ni moja, lakini Yeye, Aliyetukuka, Alizifanya zitofautiane ili awape mtihani, ili mtiifu na mwenye kuasi wajulikane waziwazi. Basi yakimbilieni yale yaliyo bora kwenu katika Makao Mawili yenu (duniani na Akhera), kwa kuyafuata yaliyomo kwenye Qur’ani kivitendo. Kwani mwisho wenu ni kurudi kwa Mwenyezi Mungu; huko Atawapa habari ya yale mliyokuwa mkitofautiana juu yake, na hapo Atamlipa kila mmoja kwa amali yake. [Al Maaidah: 48]. Hivyo Qur'ani tukufu ambayo imekusanya sheria imekuja kusadikisha yale yaliyotangulia katika vitabu vya Mungu na imekuja kuvitawala na kuvifuta.
27- Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakubali Dini nyingine isiyokuwa Uislamu aliyokujanayo Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie, na atakayeiamini Dini isiyokuwa Uislamu haitokubaliwa kwake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu hakubali baada ya kutumwa Muhammadi rehema na Amani zimfikie Dini nyingine isiyokuwa Uislamu aliokujanao Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie, na atakayetaka Dini isiyokuwa Uislamu haitokubaliwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenye kutafuta dini isiyokuwa dini ya Kiislamu, ambayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha na kumfuata kwa kumtii na kumdhalilikia, na kwa Mtume wake aliye Nabii wa mwisho Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kumuamini na kumfuata na kumpenda kwa dhahiri na kwa siri, basi hiyo haitakubaliwa kwake, na yeye Akhera atakuwa ni miongoni mwa wenye kupata hasara ambao walizifanyia ubahili nafsi zao kwa kuzinyima mambo yenye kuzinufaisha. [Al-Imran: 85]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Bila shaka dini ya haki mbele ya mwenyezi mungu ni uislamu,na hawakutofautiana wale waliopewa kitabu-mayahudi na manaswara- isp[okuwa ni baada ya kupewa elimu kwa sababu ya uhasidi waliokuwa nao,na anayezikataa aya za mwenyezi mungu,mwenyezi mungu atamuadhibu huko akhera na mwenyezi mungu ni mwepesi wa kuhesabu. [Al-Imran: 19]. Na huu Uislamu ndio mila ya Ibrahim kipenzi cha Allah Amani imfikie, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakuna yeyote anayeipa mgongo Dini ya Ibrahim, nayo ni Uislamu, isipokuwa safihi aliye mjinga. Na hakika tulimchagua Ibrahim duniani kuwa Nabii na Mtume, na kesho Akhera kuwa ni miongoni mwa watu wema ambao wana daraja za juu kabisa. [Al Baqara: 130]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakuna yeyote aliye mwema wa dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake, kwa moyo wake na viungo vyake vyote, hali ya kuwa ni mwema wa maneno na vitendo, mwenye kufuata amri ya Mola wake, akawa amefuata mila ya Ibrāhīm na Sheria aliyoileta na amejiepusha na itikadi mbaya na sheria zilizo batili. Na Mwenyezi Mungu Alimteua Ibrāhīm, rehema na amani zimshukie, na Akamfanya ni msafiwa Wake miongoni mwa viumbe Wake. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya al-khullah (mapenzi ya ndani) kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, nayo ni daraja ya juu kabisa ya mapenzi na uteuzi. [An Nisaai: 125]/ Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuamrisha Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie aseme: Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mimi Ameniongoza Mola wangu kwenye njia iliyolingana sawa yenye kufikisha kwenye Pepo Yake, nayo ni Dini ya Uislamu yenye kusimamia mambo ya dunia na ya Akhera; nayo ni Dini ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Dini ya Ibrāhīm, amani imshukie. Na Ibrāhīm, amani imshukie, hakuwa ni miongoni mwa wenye kumshirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu asiyekuwa Yeye.» [Al An'am: 161].
28- Qur'an tukufu ndicho kitabu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimteremshia wahyi Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie, nayo ni maneno a Mola Mlezi wa walimwengu, Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto watu na majini kuwa walete mfano wake au sura moja mfano wake, na bado changamoto hiyo inaendelea kuwepo mpaka siku ya Kiyama, na Qur'an tukufu inajibu maswali mengi muhimu yanayo wachanganya mamilioni ya watu, na Qur'an imehifadhiwa mpaka leo kwa lugha ya kiarabu iliyoteremka kwayo, na haijapungua ndani yake hata herufi moja, nayo imechapishwa na imesambazwa, nacho ni Kitabu kitukufu, kuna umuhimu mkubwa wa kukisoma au kusoma tafsiri ya maana ya maneno yake, kama ambavyo Sunna za Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie na mafundisho yake na mwenendo wake vimehifadhiwa na vimenukuliwa, kwa kuendana na mlolongo wa wapokezi wenye kuaminika, nayo imechapishwa kwa lugha ya kiarabu aliyozungumza Mtume rehema na Amani zimfikie, na imefasiriwa katika lugha nyingi, Na Qur'an tukufu na Mafundisho ya Mtume rehema na Amani zimfikie ndiyo vyanzo pekee vya hukumu za uislamu na sheria zake, uislamu hauchukuliwi kutoka katika harakati za baadhi ya watu wenye kujinasbisha na uislam; Bali unachukuliwa kutoka katika wahyi (ufunuuo) wa Mungu:- yaani- Qur'an tukufu na Mafundisho Matukufu ya Mtume rehema na Amani zimfikie.
Qur'ani tukufu ndicho kitabu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimteremshia wahyi Mtume Muarabu Muhammadi rehema na Amani zimfikie, kwa lugha ya kiarabu, nayo ni maneno ya Mola Mlezi wa walimwengu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika, hii Qur’ani ambayo ndani yake zimetajwa habari hizi za kweli imeteremshwa na Muumba viumbe na Mmiliki wa mambo yote. ameshuka nayoJibrili muaminifu akakusomea mpaka ukaikusanya moyoni mwako, kwa kuihifadhi na kuielewa, upate kuwa ni mmoja wa wajumbe wa Mwenyezi Mungu wenye kuwafanya watu wao waogope mateso ya Mwenyezi Mungu, upate kuwaonya, kwa Teremsho hili, binadamu na majini wote. Ameshuka nayo Jibrili kwako kwa lugha ya Kiarabu yenye maana iliyo wazi, yenye ushahidi unaoonekana, ikikusanya kile wanachokihitajia cha kutengeneza mambo ya Dini yao na dunia yao. [Ash shu'araai: 192-195]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika wewe , ewe Mtume, unapewa Qur’an kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa hekima katika kuumba Kwake na uendeshaji Wake Ambaye Amekizunguka kila kitu kwa kukijua. [An Nahli: 6]. Na hii Qur'an ni uteremsho kutoka kwa Mwenyezi Mungu na inasadikisha yale yaliyotangulia katika vitabu vya Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Haikuwa ni yenye kumkinika kwa yeyote kuja nayo Qur’an hii kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, sababu ni kwamba hakuna yeyote awezae kufanya hilo miongoni mwa viumbe. Lakini Mwenyezi Mungu Aliiteremsha kusadikisha vitabu alivyowateremshia Manabii Wake, kwa kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni moja. Na katika hii Qur’an kuna maelezo na ufafanuzi wa sheria ya Mwenyezi Mungu Aliyowawekea umma wa Muhammad. Hapana shaka kwamba hii Qur’an ni wahyi unaotoka kwa Mola wa viumbe wote. [Yunus: 37]. Na Qur'an tukufu inatatua maswala mengi ambayo walitofautiana ndani yake mayahudi na manaswara katika dini yao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa hakika, hii Qur’an inawapa Wana wa Isrāīl habari ya ukweli katika mambo mengi zaidi ambayo wao wametofautiana juu yake. [An Nahli: 76]. Na Qur'an tukufu imekusanya ushahidi na hoja, inaweza kusimama hoja juu ya watu wote katika kuujua uhalisia unaohusiana na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na dini yake na malipo yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika tumewapigia hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu kila mfano katika mifano ya watu wa karne zilizopita, kwa kuwatisha na kuwaonya, ili wakumbuke na wakomeke na lile ambalo wako nalo la kumkufuru Mwenyezi Mungu. [Azzumar: 27]. Na amesema Allah Mtukufu: {Na tumeteremsha kwako kitabu, kiwe ni upambanuzi wa kila kitu, na muongozo na rehema, na bishara njema kwa waislamu}. (An Nahli 89)
Na Qur'an tukufu inajibu maswali mengi muhimu yaliyowachanganya mamilioni ya watu, Na Qur'an tukufu inabainisha ni namna gani Mwenyezi Mungu aliziumba mbingu na ardhi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwani hawakujua hawa ambao wamekufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikana,, kisha tukazipambanua kwa uweza wetu, tukateremsha mvua kutoka juu na tukatoa mimea kutoka kwenye ardhi na tukajaalia kutokana na maji kila kitu chenye uhai. Basi je hawaamini hawa wakanushaji, wakayasadikisha wanayoyaona na wakamfanya Mwenyezi Mungu kuwa wa pekee katika ibada?. [Al Anbiyaai 30]. Na ni namna gani Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi watu, mkiwa mna shaka ya kuwa Mwenyzi Mungu atawafufua wafu, basi sisi tumemuumba baba yenu Adam kutokana na mchanga kisha kizazi chake kikazaana kutokana na nutfah, nayo ni manii ambayo mwanamume anayarusha kwenye uzao wa mwanamke, yakageuka kwa uweza wa Mwenyezi Mungu yakawa 'alaqah, nalo ni pande la damu nyekundu iliyo nzito, kisha yakawa mudhgha, nacho ni kinofu kidogo cha nyama cha kuweza kutafunika, mara nyingine kikawa kitaumbwa, yaani kiumbike kikamilifu mpaka kifikie muda wa kutoka kwa mtoto akiwa hai, na mara nyingine kisiumbike kikamilifu kikatoka kabla ya kutimia, ili tuwafafanulie ukamilifu wa uweza wetu wa kuendesha miongo ya uumbaji. Na tunakibakisha kwenye zao tunachokitaka, nacho ni kile kinachoendelezwa kuumbwa kwake mpaka wakati wa kuzaliwa kwake na itimie ile miongo ya kuzaliwa wana wa matumboni wakiwa wadogo, wakuwe mpaka wafikie umri wa kuwa na nguvu, nao ni wakati wa ubarobaro na nguvu na kukamilika akili. Na baadhi ya watoto huenda wakafa kabla ya hapo, na baadhi yao wanakuwa mpaka wanafikisha miaka ya ukongwe na udhaifu wa akili, akawa huyu aliyezeeka hajui kitu alichokuwa akikijua kabla ya hapo. Na utaiona ardhi ni kavu, imekufa haina mimea yoyote, tuyateremshapo maji juu yake, inatikisika kwa mimea ikawa inafunguka, inachepua, inanyanyuka na kuongezeka kwa kutosheka na maji na ikaotesha kila aina ya mimea mizuri yenye kuwafurahisha wenye kuangalia. [Al Hajji: 5]. Na ni wapi mafikio yake na ni yapi malipo ya mtu mwema baada ya maisha haya, na umetangulia ushahidi juu ya jambo hili katika kipengele namba (20) na je dunia hii ilikuja yenyewe tu ghafla, au ilipatikana kwa lengo tukufu? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Au kwani hawaangalii, hawa wakanushaji aya za Mwenyezi Mungu, kwenye ufalme wa Mwenyezi Mungu uliyo mkubwa na mamlaka Yake yenye uwezo wa kushinda, mbinguni na ardhini na chochote kile Alichokiumba Mwenyezi Mungu, zimetukuka sifa Zake, kwenye vitu viwili hivyo, wakalitia akilini hilo na wakalizingatia kwa akili zao na wakaangalia muda wa kikomo cha maisha yao ambao huenda ukawa umesogea karibu wakawa watakufa kwenye ukafiri wao na watakuwa kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake makali? Basi ni kitisho gani na onyo gani baada ya onyo la Qur’ani wataliamini na watalifanyia kazi? [Al A'raf: 185]. Na amesema Allah Mtukufu: Je, mlidhania, enyi viumbe, ya kwamba sisi tuliwaumba nyinyi mkiwa mmepuuzwa: hakuna maamrisho wala makatazo wala malipo mema wala mateso, a kwamba nyinyi hamtorudishwa kwetu Akhera kwa Hesabu na Malipo? [Al Mu'uminun: 115].
Na Qur'an tukufu imehifadhiwa mpaka leo hii kwa lugha ya kiarabu iliyoteremka nayo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika sisi tumeiteremsha Qur’an kwa Nabii Muhammad, rehema na amani zimshukie, na hakika sisi tunachukua ahadi kuitunza isiongezwe, isipunguzwe wala sehemu yoyote katika hiyo isipotee. [A Hijri: 9]. Haijapungua ndani yake hata herufi moja, na haiwezekani kupatikana ndani yake kukinzana, au mapungufu au mabadiliko. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwani hawa hawaiangalii Qur’ani na haki iliyokuja nayo, kwa kuitafakari na kuizingatia, namna ilivyokuja kwa utaratibu uliopangika unaomfanya mtu awe na yakini kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake? Na lau ingelikuwa inatoka kwa asiyekuwa Yeye, wangelipata ndani yake tofauti kubwa. [An Nisaai: 82]. Nayo imechapishwa na imesambazwa, nacho ni Kitabu kitukufu, kuna umuhimu mkubwa wa kukisoma au kusoma tafsiri ya maana ya maneno yake, kama ambavyo sunna za Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie na mafundisho yake na mwenendo wake vimehifadhiwa na vimenukuliwa, kwa kuendana na mlolongo wa wapokezi wenye kuaminika, nayo imechapishwa kwa lugha ya kiarabu aliyozungumza Mtume rehema na Amani zimfikie, na imefasiriwa katika lugha nyingi, Na Qur'an tukufu na Mafundisho ya Mtume rehema na Amani zimfikie ndiyo vyanzo pekee vya hukumu za uislamu na sheria zake, uislamu hauchukuliwi kutoka katika harakati za baadhi ya watu wenye kujinasbisha nao; Bali unachukuliwa kutoka katika wahyi wa Mungu uliolindwa: -Yaani- Qur'an tukufu na Mafundisho Matukufu ya Mtume rehema na Amani zimfikie. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika jambo la Qur'an: 'Hakika wale wanaoyakanusha mawaidha yanapowajia (Tutawaadhibu). Bila shaka hicho ni kitabu kiheshimiwacho'. Haitakifikia batili (kitabu hiki) toka mbele yake wala nyuma yake; kimeteremshwa na Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima, ahimidiwe'. [Fusswilat: 41-42]. Na amesema Mtukufu katika jambo la(Sunnah) Mafundisho ya Mtume matukufu, nakuwa hayo ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu: "Na yale aliyokuleteeni Mtume yachukueni, na yale aliyokukatazeni yaacheni, na mcheni Mwenyezi Mungu, Hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu". (Al-Hashr 7)
29- Na Uislamu unaamrisha kutenda wema kwa wazazi wawili, hata kama watakuwa si waislamu, na umetoa usia kwa watoto.
Uislamu unaamrisha kutenda wema kwa wazazi wawili, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mola wako, ewe mwanadamu, Ameamrisha na kulazimisha na kupasisha Apwekeshwe, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kwa kuabudiwa Peke Yake, na Ameamrisha kuwafanyia wema baba na mama, hasa wakiwa katika hali ya ukongwe: usione dhiki wala uzito kwa jambo lolote ulilonalo kwa mmoja wao au kwa wao wawili, wala usiwasikilizishe neno baya, hata kama ni sauti ya kuonyesha kutoridhika ambayo ni neno baya la daraja ya chini kabisa, wala usiwafanyie tendo baya, lakini kuwa mpole kwao na uwaambie wao daima maneno mepesi yenye ulaini. [Al Israai: 23]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na tulimuamuru binadamu kuwatendea wema wazazi wake wawili na kuwafanyia hisani, Mama yake alimbeba tumboni, shida juu ya shida, na mimba yake na kumaliza kunyonya kwake ni ndani ya kipindi cha miaka miwili, na tukamwambia, «Mshukuru Mwenyezi Mungu kisha uwashukuru wazazi wako, kwangu mimi ndio marejeo nipate kumlipa kila mmoja kwa anachostahili. [Luqman: 14]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na tumemuusia binadamu asuhubiane na wazazi wake wawili vizuri, kwa kuwatendea wema wanapokuwa hai na baada ya kufa kwao. Kwa kuwa mama yake alimbeba akiwa mwana wa matumboni kwa shida na tabu, na akamzaa kwa shida na tabu pia. Na muda wa kubeba mimba yake na mpaka kumaliza kumnyonyesha ni miezi thelathini. Katika kutaja shida hizi anazozibeba mama, na siyo baba, pana dalili kuwa haki yake juu ya mtoto wake ni kubwa zaidi kuliko haki ya baba. Mpaka alipofikia binadamu upeo wa nguvu zake za kimwili na kiakili na akafikia miaka arobaini, huwa akimuomba Mola wake kwa kusema, “Mola wangu! Niafikie (niwezeshe) nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu wawili, na nijaalie nifanye matendo mema unayoridhika nayo, na unisuluhishie wanangu. Hakika mimi nimetubia dhambi zangu kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa wanyenyekevu kwako kwa utiifu na ni miongoni mwa wenye kujisalimisha kufuata amri zako na kuepuka makatazo yako, wenye kufuata hukumu yako.” [Al Ahqaaf: 15]. Na kutoka kwa Abuu Hurayra radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani zimfikie akasema: 'Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Ni mtu gani mwenye haki zaidi ya kufanyiwa wema katika watu wangu? Mtume akasema: "Mama yako" Akasema: 'kisha nani? Mtume akasema: "Mama yako" Akasema: 'kisha nani? Mtume akasema: "Mama yako" Akasema kisha nani? Mtume akasema: "Kisha baba yako". Swahiihi Muslim
Na amri hii ya usia kwa wazazi wawili sawasawa wawe waislamu au si waislamu. Na kutoka kwa Asmaa bint Abuubakari Amesema: "Alikuja mama yangu akiwa bado ni mshirikina katika zama za makuraishi na wakati wao, (zama zilizotokea sintofahamu kati ya makuraishi na Mtume) walipoingia makubaliano na Mtume rehema na Amani zimfikie, (Mama) alikuwa pamoja na mwanaye wa kiume, Nikamuuliza Mtume rehema na Amani zimfikie: Nikasema: mama yangu amekuja akiwa na furaha (ya kuniona pamoja na zawadi), je nimuunge (nimpokee kama sehemu ya kuendeleza udugu?) Mtume akasema: "Ndiyo mpokee mama yako". Swahiihi Bukhaariy Bali ikiwa watajaribu na wakafanya juhudi wazazi ya kutaka kumgeuza mtoto kutoka katika uislamu na kwenda katika ukafiri, hapa pia uislamu unamuamrisha, -Na hali hii- Asiwasikilize wala asiwatii, na aendelee kuwa na imani kwa Mwenyezi Mungu, na awafanyie wema na aishi nao kwa wema. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: «Na wakikusukuma kwa bidii wazazi wako wawili, ewe mtoto mwema, ili unishirikishe mimi na mwingine katika kuniabudu katika kitu ambacho huna ujuzi nacho, au wakakuamuru ufanye jambo miongoni mwa mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu basi usiwatii, kwani hakuna kutiiwa kiumbe kwa kuasiwa Muumba. Na suhubiana nao ulimwenguni kwa wema katika mambo mema yasiyo na madhambi. Na ufuate, ewe mwana mwenye Imani, njia ya aliyetubu kutokana na dhambi zake, akarudi kwangu na akamuamini Mtume wangu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Kisha ni kwangu mimi marejeo yenu, niwape habari ya yale mliokuwa mkiyafanya duniani na nimlipe kila mtendaji kwa matendo yake. [Luqman: 15].
Na Uislamu haumzuii mtu kufanya wema kwa ndugu zake wa karibu ambao ni washirikina, wanapokuwa si wenye kumpiga vita. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Hawakatazi nyinyi, enyi Waumini, kuwakirimu kwa wema makafiri ambao hawakuwapiga nyinyi vita kwa ajili ya dini wala hawakuwatoa kutoka majumbani mwenu, na kuwafanyia usawa kwa hisani yenu na wema wenu kwao, kwani Mwenyezi Mungu Anawapenda wale wanaofanya uadilifu katika maneno yao na matendo yao. [Al Mumtahna: 8].
Na uislamu unaamrisha kuwapa usia watoto, na kubwa ulilomuamrisha uislamu mzazi ni awafundishe watoto wake haki za Mola wao juu yao, kama alivyosema Mtume rehema na Amani zimfikie kumwambia mtoto wa baba yake mdogo Abdillahi bin A'bbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwafikie: "Ewe kijana, au ewe kijana mdogo! Je nisikufundishe maneno ambayo Mwenyezi Mungu atakunufaisha kupitia hayo? Nikasema: Ndiyo nifundishe. Akasema: "Muhifadhi Mwenyezi Mungu atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, jipendekeze kwa Mwenyezi Mungu wakati wa raha atakujua (kwa msaada wake) wakati wa shida, na utakapoomba Muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi mtake msaada Mwenyezi Mungu". [Kaipokea Ahmad: 4/287].
Na Mwenyezi Mungu akawaamrisha wazazi wawili kuwafundisha watoto wao yale yenye manufaa kwao katika mambo ya dini yao na dunia yao, Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Zilindeni nafsi zenu kwa kuyatenda yale ambayo Amewaamrisha kwayo Mwenyezi Mungu na kuyaepuka yale ambayo Amewakataza nayo, na walindeni watu wenu kwa kile mnachotumia kujilinda nyinyi wenyewe na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Watasimamia kuadhibiwa watu wa Motoni Malaika wenye nguvu walio thabiti katika usimamizi wao, wasioenda kinyume na Mwenyezi Mungu katika maamrisho Yake na wanaotekeleza yale wanayoamrishwa. [Suratut Tahrim: 6]. Na kutoka kwa Ally radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie (Amesema) katika kauli yake Allah Mtukufu: "Zilindeni nafsi zenu na familia zenu". Anasema: "Waadabisheni na wafunzeni". Na Mtume rehema na Amani zimfikie akamuamrisha mzazi amfudishe mwanaye swala; ili akue na alelewe katika hiyo swala, Akasema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa ni watoto wa miaka saba". Imepokelewa na Abuu Daud, Amesema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Nyinyi wote ni wachunga, na nyinyi wote kila mmoja ataulizwa kuhusu alicho kichunga, kiongozi ni mchunga na ataulizwa kuhusu raia wake, na mwanaume ni mchunga kwa familia yake naye ataulizwa kuhusu familia yake, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mume wake na ataulizwa kuhusu raia wake, na mfanyakazi ni mchunga katika mali ya tajiri yake na ataulizwa kuhusu vile alivyovichunga, na nyinyi wote kila mmoja ni mchunga na ataulizwa juu ya vile alivyovichunga". Sahihi Ibn Hibban: 4490.
Na uislamu ukamuamrisha mzazi kutoa matumizi kwa watoto wake na watu wa nyumbani kwake, na tumetangulia kueleza sehemu katika hilo katika kipengele namba (18) na akabainisha Mtume rehema na Amani zimfikie ubora wa kutoa matumizi kwa watoto akasema: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza. kaipokea Muslim (994).
30- Uislamu unaamrisha uadilifu katika kauli na matendo, hata kama itakuwa ni kwa maadui.
Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka anasifika kwa uadilifu na usawa, katika matendo yake na upangiliaji wake kwa waja wake, naye yuko katika njia iliyonyooka katika yale aliyoyaamrisha na yale aliyoyakataza, na katika yale aliyoyaumba na kuyakadiria. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Ameshuhudia kuwa Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa uungu. Na Ameambatanisha ushahidi wake na ule wa Malaika na watu wa elimu juu ya kitu kitukufu zaidi chenye kushuhudiwa, nacho ni Tawhīd umoja Wake Aliyetukuka na kusimamia Kwake haki na uadilifu. Hapana Mola ispokuwa Yeye, Aliye Mshindi Ambaye hakuna kitu Atakacho kiwe kikakataa kuwa, Mwenye hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. [Al-Imran: 18]. Na Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema, ameamrisha Mola wangu uadilifu" [Al A'raf: 29]. Na Mitume na Manabii wote sala na salamu ziwe juu yao, walikuja na uadilifu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu}. [Al Hadid: 25]. Na Mizani ni uadilifu katika kauli na vitendo.
Na Uislamu unaamrisha uadilifu katika kauli na vitendo hata kama ni pamoja na maadui, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, kuweni ni wasimamizi wa uadilifu, wenye kutekeleza ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hata kama ni kinyume na maslahi ya nafsi zenu au baba zenu au mama zenu au jamaa zenu, namna atakavyokuwa yule mwenye kutolewa ushahidi awe ni tajiri au masikini, kwani Mwenyezi Mungu ni bora kwa wao wawili kuliko nyinyi, na ni Mjuzi zaidi wa mambo ambayo yana maslahi kwao. matamanio na mapendeleo yasiwapelekee nyinyi kuacha uadilifu. Na mkiupotosha ushahidi, kwa ndimi zenu, mkautoa kwa namna isiyokuwa ya kweli, au mkaupuuza kwa kuacha kuutekeleza au kwa kuuficha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa matendo yenu ya ndani na Atawalipa kwayo. [An Nisaai: 135]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala kule kuwachukia watu kwa kuwa walikuzuilieni kufika Msikiti uliotukuzwa (wa Makka) kusikupelekeeni kuwafanyia jeuri (ili kuwalipa jeuri yao; Msifanye) na saidianeni katika wema na Uchamungu, wala msisaidiane katika dhambi na uadui, na mcheni Mwenyezi Mungu; Hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu". [Al Maaida: 2]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,, kuweni wasimamizi wa haki kwa ajili ya kuzitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, muwe mashahidi kwa uadilifu. Wala kusiwapelekee nyinyi kuwachukia watu kuacha kufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu baina ya maadui na vipenzi kwa daraja moja sawasawa. Kufanya uadilifu huko kuko karibu zaidi na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Na jihadharini na kufanya udhalimu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa mnayoyafanya na Atawalipa kwa hayo. [Al Maaida: 8]. Je unaweza kupata katika kanuni za Mataifa ya leo au katika dini za watu mfano wa maamrisho haya, kwa kutoa ushahidi wa kweli na kusema ukweli hata kama itakuwa juu ya nafsi yako na wazazi wawili na ndugu wa karibu, na amri ya kufanya uadilifu hata kwa adui na rafiki?.
Na akaamrisha Mtume rehema na Amani zimfikie kufanya uadilifu kati ya watoto. Na kutoka kwa Aamir Amesema: Nilimsikia Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao naye akiwa katika Mimbari (jukwaa la khutba) akisema: Baba yangu alinipa mimi zawadi, akasema Amrah binti Rawaha: Sitoridhia mpaka umshuhudishe Mtume rehema na Amani ziwe juu yake, akamuendea Mtume rehema na Amani zimfikie, akasema: Mimi nimempa kijana wangu wa Amrah binti Rawaha zawadi, akaniamrisha (Amrah) nikufanye wewe kuwa shahidi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Akasema: "Je umewapa wanao wote mfano wa huyu?" Akasema: 'Hapana' Akasema: "Mcheni Mwenyezi Mungu na mfanye uadilifu baina ya watoto wenu" Akasema: Akarudi na akairudisha ile zawadi yake). Sahihi Bukhariy 2587,
Na hivyo ni kwasababu hayawezi kutengemaa mambo ya watu ispokuwa kwa uadilifu, na hawawezi kupata usalama watu katika dini zao na mali zao na familia zao na heshima zao na damu zao na nchi zao ispokuwa kwa uadilifu, na kwasababu hii tunaona Mtume rehema na Amani zimfikie alipoona makafiri wa Makka wamewabana waislamu wakawanyima uhuru, aliwaamrisha wahame kwenda uhabeshi (Ethiopia); na akatoa sababu ni kuwa huko kuna Mfalme ambaye hakuna anayedhulumiwa kwake.
31- Na Uislamu unaamrisha kuwafanyia wema viumbe wote, na unalingania katika tabia njema, na kazi nzuri.
Uislamu unaamrisha kutenda wema kwa viumbe wote, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kutenda uadilifu na wema, Na kumpa (msaada) ndugu wa karibu". [An Nahli: 90]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wale ambao wanatoa mali yao katika hali ya wepesi na uzito, na wanaozuia hasira zilizo ndani ya nafsi zao kwa kusubiri, na wanaowasamehe waliowadhulumu wanapokuwa na uwezo. Huu ndio wema ambao Mwenyezi Mungu Anawapenda wenye kuwa nao. [Al-Imran: 134]. Na Amesema Mtume Muhammadi Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amefaradhisha (kutenda) wema katika kila kitu, hivyo mtakapoua basi uweni vizuri (kwa wema), na mtakapochinja basi chinjeni vizuri, na anowe mmoja wenu makali yake (makali ya kisu chake), na akistareheshe kichinjwa chake". Kaipokea Muslim (1955).
Na Uislamu unalingania katika tabia njema na kazi nzuri, amesema Mwenyezi Mungu katika sifa za Mtume rehema na Amani zimfikie katika Vitabu vilivyotangulia: Na wanaomfuata Mtume aliye Nabii, ambaye hasomi wala haandiki, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukie, ambaye wanazipata sifa zake na mambo yake yameandikwa huko kwao katika Taurati na Injili; anawaamrisha kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii na kila lijulikanalo kuwa ni jema, na anawakataza ushirikina na maasia na kila lijulikanalo kuwa ni baya, na anawahalalishia vizuri vya vyakula na vinywaji na kuoana, na anawaharamishia vichafu vya hivyo kama nyama ya nguruwe na vile ambavyo walikuwa wakijihalalishia miongoni mwa vyakula na vinywaji ambavyo aliviharamisha Mwenyezi Mungu, na anawaondolea wao mambo magumu waliokalifishwa nayo kama kukata mahali pa najisi nguoni, kuzichoma moto ngawira, ulazimu wa kisasi juu ya aliyeua kwa kukusudia au kwa kukosea. Basi wale ambao walimuamini Nabii asiyejua kuandika wala kusoma kilichoandikwa, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukie, na wakaukubali unabii wake, wakamuheshimu, wakamtukuza na wakamuhami na wakaifuata Qur’ani aliyoteremshiwa, wakaufuata mwenendo wake kivitendo, hao ni wenye kufaulu kwa kupata yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaahidi waja wake Waumini. [Al A'araf: 157]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Ewe Aisha! Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, Na anatoa (na kulipa) katika upole zaidi ya yale anayoyatoa katika ukali, na asiyoyatoa katika mengine yasiyokuwa hilo". kaipokea Muslim (2593). Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha kwenu nyinyi: kuwaasi akina mama, na kuwazika watoto wa kike wakiwa hai, Na akazuia kuombaomba, na akachukia kwenu nyinyi porojo, na kuulizauliza, na kupoteza mali (bila sababu za msingi)". Sahihi Bukhariy 2408, Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu". kaipokea Muslim (54).
32- Na uislamu unaamrisha tabia nzuri, kama ukweli na kutekeleza amana, na kujizuia na machafu, na kuwa na haya (Aibu) na ushujaa, na kutoa misaada na ukarimu, na kumsaidia mwenye uhitaji, na kumuokoa aliyeelemewa na matatizo, na kumlisha mwenye njaa, na kuishi vizuri na majirani, na kuunga udugu, na kuwahurumia wanyama.
Na Uislamu unaamrisha tabia nzuri, Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Hakika bila shaka nimetumwa ili nitimilize tabia njema". sahihil Adabil Mufrad: 207, Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu, na hakika ninaowachukia zaidi kati yenu na watakaokaa mbali zaidi na mimi siku ya kiyama ni watu wenye maneno mengi, na waropokaji, na wenye kujifakharisha, wakasema: Tushajua maana ya watu wenye maneno mengi na waropokaji, nini maana ya wenye kujifakharisha? Akasema: Ni wale wenye kiburi". Silsilatu Sswahiiha: 791. Na kutoka kwa Abdillahi Bin Amru Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: "Mtume rehema na Amani zimfikie hakuwa Muovu, wala mwenye kutaka machafu" Na alikuwa akisema: "Hakika katika wabora wenu ni yule mzuri wenu kitabia" Sahihi Bukhariy 3559, Na zinginezo katika Aya na hadithi zinazoonyesha kuwa Uislamu unahimiza tabia njema, na kazi nzuri, kwa ujumla.
Na miongoni mwa yale ambayo Uislamu unaamrisha: ni ukweli, Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Jilazimisheni kuwa wakweli, kwani ukweli unaongoza katika wema, na hakika ukweli unaongoza na kumpelekea mtu kuingia Peponi, na hatoacha mtu kuendelea kusema ukweli, na akiutafuta ukweli mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli". Kaipokea Muslim (2607).
Na katika mambo ambayo Uislamu unayaamrisha: Ni kutekeleza amana, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni kutekeleza amana kwa wenyenazo". [An Nisaai: 58].
Na miongoni mwa yale ambayo Uislamu unaamrisha: Ni kujizuia na machafu, Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Watu wa aina tatu wana haki kwa Mwenyezi Mungu kuwapa msaada: na akataja miongoni mwao: Ni muoaji anayekusudia kujizuia na machafu". Sunanu Tirmidhiy 1655. Na katika dua zake Mtume rehema na Amani zimfikie alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na ucha Mungu na kujizuia na machafu na kutosheka". Kaipokea Muslim (2721).
Na miongoni mwa yale ambayo Uislamu unaamrisha: Nikuwa na aibu, Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Haya (Aibu) haiji ila kwa kheri" Sahihi Bukhariy 6117, Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Kila dini inatabia zake, na tabia ya Uislamu ni haya (Aibu)". Kaitoa Imamu Baihaqiy katika Shu'abil Imaan 6/2619.
Na katika mambo Uislamu unaamrisha ni ushujaa, kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: "Mtume rehema na Amani zimfikie alikuwa mzuri kuliko watu wote, na ni shujaa kuliko watu wote, na ni mkarimu kuliko watu wote, na watu wa Madina (siku moja) walipatwa na mshituko (wa tukio) Mtume rehema na Amani zimfikie akawa tayari ameshawatangulia (kufika eneo la tukio) naye akiwa kapanda juu ya farasi". Sahihi Bukhariy 2820, Na Mtume rehema na Amani zimfikie alikuwa akiomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uoga, alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na uoga". Sahihi Bukhariy 6374.
Na katika mambo uislamu unayoamrisha, ni utoaji (sadaka) na ukarimu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na mfano wa Waumini wenye kutoa mali yao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa mbegu iliyopandwa kwenye ardhi nzuri, muda si muda ikatoa mche wenye sehemu saba. Kila sehemu ikatoa shuke moja na kila shuke likawa na mbegu mia. Na Mwenyezi Mungu Anamuongezea thawabu anayemtaka, kulingana na kadiri ya Imani aliyonayo yule mtoaji na ikhlasi yake iliyo timamu. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zimeenea, na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mjuzi wa yule anayestahiki kuzipata, ni Mwenye kuchungulia nia za waja Wake. [Al Baqara: 261]. Na ilikuwa tabia ya Mtume rehema na Amani zimfikie ni ukarimu, kutoka kwa Ibni Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, amesema: "Alikuwa Mtume Alayhi salaam ni mbora wa watu katika kufanya kheri, na alikuwa mzuri zaidi pindi anapo kutana na Jibril Alayhi salaam, alikuwa anakutana nae kila siku katika mwezi wa Ramadhani kwa kila mwaka mpaka anaondoka anakuwa amepitia Quraan nzima.Na pindi Jibril alipokuwa akikutana nae alikuwa ni mwingi wa kufanya kheri kuliko upepo unavyo vuma kutokana na wingi wa kheri hizo". Sahihi Bukhariy 1902,
Na katika mambo unayoamrisha Uislamu ni kumsaidia mwenye uhitaji, na kumuokoa mwenye misukosuko, na kumlisha mwenye njaa, na kuishi vizuri na majirani na kuunga udugu, na kuwahurumia wanyama. Kutoka kwa Abdillahi bin Amru radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na Amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua". Sahihi Bukhariy 12, Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Siku moja mtu mmoja alikuwa akitembea barabarani kiu kikamzidia, akapata kisima akashuka ndani yake, akanywa kisha akatoka, mara akamuona mbwa anahema na huku akila udongo kutokana na kiu, yule bwana akasema: 'Huyu mbwa yamemfika kama yaliyonifika mimi ya kupatwa na kiu', kisha akashuka kisimani tena akajaza kiatu chake maji, kisha akakishika kwa mdomo waje akamnywesha yule mbwa, Mwenyezi Mungu akapendezwa na kitendo chake akamsamehe" Maswahaba wakauliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwani na sisi tunamalipo kwa wanyama wetu? Akasema: "Ndiyo, katika kila chenye ini kibichi kuna ujira" (Yaani kila kiumbe hai kukifanyia wema kuna malipo). Sahihi Ibn Hibbaan: 544. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana" Sahihi Bukhariy 5353,
Na Uislamu unatilia mkazo haki za ndugu, na unawajibisha kuwaunga ndugu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni bora kwa Waumini na ni karibu na wao zaidi kuliko nafsi zao katika mambo ya dini na dunia. Na heshima ya wake za Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa umma wake, kama vile heshima ya mama zao, haifai kuwaoa wake za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, baada yake. Na wenye ujamaa wa ukaribu, miongoni mwa Waislamu, baadhi yao wana haki zaidi ya kuwarithi wengine katika hukumu ya Mwenyezi Mungu na sheria Yake kuliko kurithi kwa (misingi ya) Imani na uhamiaji. (Waislamu hapo mwanzo wa Uislamu walikuwa wakirithiana kwa misingi ya hijrah (uhamiaji) na Imani au Dini na si kwa kizazi, kisha hilo likaondolewa kwa aya ya Mirathi), ispokuwa iwapo nyinyi, enyi Waislamu, mtawafanyia wema kwa kuwahami, kuwafanyia wema, kuwaunga na kuwaachia wasia wa kuwafaidisha. Hukumu hii iliyotajwa imekadiriwa, imeandikwa kwenye Ubao uliyohifadhiwa, basi ni lazima kwenu muifuate kivitendo. [Al Ahzaab: 6]. Na ukatahadharisha juu ya kukata ukoo na ukaunganisha swala hili na ufisadi katika ardhi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Huenda nyinyi mkikipa mgongo Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Mwenendo wa Nabii wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, mkaja kumuasi Mwenyezi Mungu katika ardhi, mkamkanusha Yeye, mkamwaga damu na mkakata vizazi vyenu. Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaepusha na rehema Yake Akawafanya wasiyasikie yanayowanufaisha wala wasiyaone na zisiwafunukie hoja za Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa ni nyingi. [Muhammadi: 22-23]. Na amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Haingii Peponi mwenye kukata ukoo (udugu)". Kaipokea Muslim (2556). Na ndugu wa ukoo ambao ni lazima kuwaunga ni: Wazazi wawili na kaka na dada, na baba wadogo na wakubwa, shangazi na wajomba, na mama wadogo na wakubwa.
Na Uislamu unatilia mkazo juu ya haki ya jirani, hata kama atakuwa kafiri, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na muabuduni Mwenyezi Mungu na mtiini Yeye Peke Yake, wala msimfanyie mshirika katika ustahiki wa kuwa Ndiye Mola na Ndiye Mwenye kuabudiwa, na wafanyieni wema wazazi wawili na mtekeleze haki zao na haki za jamaa wa karibu, na mayatima na wahitaji, na jirani wa karibu na wa mbali, na rafiki wa safari na wa mjini, na msafiri mwenye uhitaji, na waliomilikiwa na nyinyi, wanaume na wanawake. Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi, katika waja Wake, wenye kiburi na kujigamba kwa watu. [An Nisaai: 36]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakuacha Jibril kuendelea kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhania kwamba yeye atamrithisha". Sahihi Abuu Daudi 5152.
33- Uislamu umehalalisha vyakula na vinywaji vilivyo vizuri, na ukaamrisha kuutwaharisha moyo na mwili na nyumba, na kwaajili hiyo ukahalalisha ndoa kama walivyoamrisha Manabii Amani iwe juu yao juu ya jambo hilo, wao wanaamrisha kila zuri.
Na Uislamu umehalalisha vitu vizuri katika vyakula na vinywaji, Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" mpaka mwisho wa Aya, akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!". Kaipokea Muslim (1015). Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, ewe Mtume, uwaambie hao wajinga miongoni mwa washirikina, «Ni nani aliyewaharamishia vazi zuri ambalo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amelifanya kuwa ni pambo kwenu? Na ni nani Aliyewaharamishia kujistarehesha kwa chakula kizuri cha halali kilichoruzukiwa na Mwenyezi Mungu?» Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, «Kwa hakika vile alivyoviruhusu Mwenyezi Mungu, miongoni mwa mavazi na vitu vizuri miongoni mwa vyakula na vinywaji, ni haki kwa walioamini pamoja na wengineo katika maisha ya ulimwenguni, na ni haki kwa walioamini peke yao Siku ya Kiyama. Maelezo kama hayo ni mafundisho ambayo Mwenyezi Mungu Anayaelezea kwa watu wenye kuyajua mambo wanayoelezwa na kuyaelewa wanayofafanuliwa. [Al A'raf: 32].
Na Uislamu umeamrisha kuusafisha Moyo na mwili na nyumba, na kwaajili hiyo ukahalalisha ndoa kama walivyoamrisha hilo Manabii na Mitume amani iwe juu yao, basi wao wanaamrisha kila zuri, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Amewaumba wake kutokana na nyinyi ili nafsi zenu ziliwazike na wao, na amewapa kutokana nao watoto, na kutokana na kizazi chao wajukuu, na Amewaruzuku vyakula vizuri miongoni mwa matunda, nafaka, nyama na visivyokuwa hivyo. Je, kwani wanauamini upotofu wa uungu wa washirika wao na wanazikanusha neema za Mwenyezi Mungu zisizohesabika na hawamshukuru kwa kumpwekesha Yeye Peke Yake, Aliyetukuka na kuwa juu, kwa ibada? [An Nahli: 72]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na nguo zako uzisafishe" "Na mabaya yapuuze". [Al Mudathir: 4-5]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "HatoingiaPeponi yeyote ambaye moyoni mwake kuna punje ndogo ya kiburi. Mtu mmoja akasema: 'Hakika kuna mtu anapenda nguo zake kuwa nzuri na viatu vyake kuwa vizuri, akasema: Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri anapenda uzuri, kiburi ni kuukataa ukweli na kuwadharau watu" Kaipokea Muslim (91).
34- Na Uislamu umeharamisha vyanzo vya mambo ya haramu, kama kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na ukafiri na kuabudu masanamu, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, na kuuwa watoto, na kuuwa nafsi iliyojiheshimika, na kufanya uharibifu katika ardhi, na uchawi, na machafu ya wazi na ya siri, na zinaa na ulawiti, na ukaharamisha riba, na kula mizoga na kilichochinjwa kwaajili ya masanamu na mizimu, na ukaharamisha nyama ya nguruwe na najisi zote, na vichafu, na ukaharamisha kula mali ya yatima na kupunja katika kipimo na mzani, na ukaharamisha kukata ukoo. Na Manabii wote kwa ujumla wamekubaliana juu ya haya yaliyo haramishwa.
Uislamu umeharamisha vyanzo vya mambo ya haramu, kama kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na ukafiri na kuabudu masanamu, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, na kuuwa watoto, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Waambie, ewe Mtume, «Njooni niwasomee Yale Aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu: Msishirikishe pamoja na Mwenyezi Mungu kitu chochote, miongoni mwa viumbe Vyake katika kumuabudu Yeye; bali zielekezeni aina zote za ibada Kwake Yeye Peke Yake, kama kucha, kutaraji, kuomba na megineyo. Muwafanyie wema wazazi wawili kwa kuwasaidia, kuwaombea Mungu na mengineyo ya wema kama hayo Msiwaue watoto wenu kwa sababu ya ufukara uliowashukia, kwani Mwenyezi Mungu Anawaruzuku nyinyi na wao. Wala msiyasogelee madhambi makubwa yaliyo wazi na yaliyofichika. Na msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuuawa, ispokuwa kwa njia ya haki, nayo ni kuchukuliwa kisasi kwa aliyeua, au kwa uzinifu baada ya kuoa au kuolewa, au kuacha Uislamu. Hayo yaliyotajwa ni miongoni mwa yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewakataza nayo na Akawapa maagizo muyaepuke na ni miongoni mwa yale Aliyowaamrisha nyinyi kwayo. Amewausia nayo Mola wenu ili mpate kuyatia akilini maamrisho Yake na Makatazo Yake. «Wala msiisogelee, enyi wasimamizi, mali ya yatima ispokuwa kwa namna ya kuitengeneza na kuifanya yenye faida, mpaka atakapofikia miaka ya kubaleghe na awe mwangalifu. Na pindi afikiapo umri huo, mpeni mali yake. Na tekelezeni vipimo na mizani kwa usawa kwa namna ambayo utekelezaji utakuwa umefanyika kwa ukamilifu. Na mtakapojibidiisha uwezo wenu, hapana ubaya kwenu katika yale ambayo huenda yakawa na upungufu upande wenu. Kwani hatumlazimishi mtu ispokuwa uwezo wake. Na msemapo, basi jitahidini katika maneno yenu kuchunga usawa pasi na kupotoka kwenye haki kwenye utoaji habari au ushahidi au hukumu au kwenye uombezi, hata kama yule ambaye neno hilo linamuhusu yeye ana ujamaa na nyinyi, msielemee upande wake bila ya haki. Na tekelezeni yale aliyowaagiza mfanye ya kujilazimisha na sheria Yake. Hukumu hizo mlizosomewa, Mola wenu Amewausia mzifuate kwa matarajio kwamba mkumbuke mwisho wa mambo yenu. [Al An'am: 151-152]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema,ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeyafanya matendo maovu kuwa ni haramu, yale yaliyo waziwazi na yale yaliyofichika, na Ameyakataza maasia yote, na miongoni mwa makubwa zaidi ya maasia ni kuwafanyia watu uadui, kwani hilo liko kando na haki. Na Amewaharamishia kuabudu, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliyetuka, vitu vingine kati ya vile ambavyo Hakuviteremshia ushahidi wala hoja, kwani afanyaye hayo hana kithibitisho chochote. Na Amewaharamishia kumnasibishia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, sheria ambayo Hakuipasisha kwa kumzulia uongo,» kama madai ya kwamba Mwenyezi Mungu Ana mwana na kuharamisha baadhi ya vilivyo halali katika mavazi na chakula. [Al A'raf: 33].
Na Uislamu umeharamisha kuuwa nafsi iliyojiheshimu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wala msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuuawa, ispokuwa kwa haki ya kisheria, kama kisasi au kumpiga mawe mzinifu aliyeingia kwenye hifadhi ya ndoa au kumuua aliyeritadi. Na mwenye kuuawa pasi na haki ya kisheria, basi tumempa msimamizi wa mambo yake , awe ni mrithi au ni hakimu, uwezo wa kutaka muuaji auawe au kutaka dia. Na haifai kwa msimamizi wa mambo ya aliyeuawa kupita mpaka wa Mwenyezi Mungu katika kuchukua kisasi, kama vile kuua watu wawili au wengi kwa mmoja au kumuua muuaji kwa njia ya kumtesa. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumsaidia msimamizi wa aliyeuawa juu ya aliyeua mpaka aweze kumuua kwa njia ya kisasi. [Al Israai: 33]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na ambao wanampwekesha Mwenyezi Mungu na hawamuombi wala kumuabudu mola asiyekuwa Yeye, wala hawaiui nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuuawa ispokuwa kwa kitu kinachopasisha kuuawa, kama vile kukufuru baada ya kuamini au kuzini baada ya ndoa au kumuua mtu kwa uadui, wala hawazini bali wanazihifadhi tupu zao ispokuwa kwa wake zao au wale ambao mikono yao ya kulia imemiliki. Na mwenye kuyafanya madhambi haya makubwa atakuta mateso huko Akhera. [Al Furqaan: 68].
Na Uislamu umeharamisha kufanya uharibifu katika ardhi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na msifanye uharibifu katika ardhi baada ya kutengemaa kwake". [Al A'raf: 56]. Na amesema Mwenyezi Mungu akitoa habari kuhusu Nabii Shu'aibu amani iwe juu yake, aliposema kuwaambia watu wake: Hakika tulimtuma, kwa watu wa kabila linalokaa Madyan, ndugu yao Shu'aib, amani imshukie, akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Hamna mola anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Mtakasieni ibada.Hakika imewajia nyinyi hoja, kutoka kwa Mola wenu, juu ya ukweli wa yale ninayowaitia. Watekelezeeni watu haki zao kwa kutimiza vipimo na mizani. Na msiwapunguzie haki zao mkawadhulumu. Wala msifanye uharibifu katika ardhi, kwa ukafiri na kudhulumu, baada ya kuwa imetengenezwa kwa sheria za Mitume waliopita, amani iwashukie. Hayo niliyowaitia nyinyi ni bora kwenu katika ulimwengu wenu na Akhera yenu, iwapo nyinyi ni wenye kuniamini katika yale ninayowaitia, ni wenye kuzifuata sheria za Mwenyezi Mungu kivitendo. [Al A'raf: 85].
Na Uislamu umeharamisha uchawi, amesema Allah wa Kweli aliyetakasika na kutukuka: «Na irushe fimbo yako iliyoko kwenye mkono wako wa kulia, itazimeza kamba zao na fimbo zao, kwani walichokifanya mbele yako si chochote ispokuwa ni vitimbi vya mchawi na kiinimacho cha uchawi. Na hafaulu mchawi kwa uchawi wake popote anapokuwa.» [Twaha: 69]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na uchawi, na kuuwa nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu ispokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya mapambano (katika uwanja wa vita), na kuwazulia machafu wanawake waumini wenye kujihifadhi wenye kujizuia na machafu". Sahihi Bukhariy 6857,
Na Uislamu umeharamisha machafu ya wazi na ya siri, na zinaa na ulawiti, na imetangulia mwanzoni mwa kipengele hiki kutajwa Aya zinazo onyesha juu ya hilo, na ukaharamisha Uislamu riba, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na mkamfuata Mtume Wake, muogopeni Mwenyezi Mungu na muache kutaka ziada iliyosalia juu ya rasilimali zenu, ambayo mlistahiki kupata kabla riba haijaharamishwa, iwapo imani yenu ni ya dhati kimaneno na kivitendo. Msipokomeka na hilo mlilokatazwa na Mwenyezi Mungu, basi kuweni na yakini ya vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mkirudi kwa Mola wenu na mkaacha kula riba, ni haki yenu mchukue madeni yenu bila ya nyongeza, hamumdhulumu yeyote kwa kuchukua zaidi ya rasilimali zenu wala hamudhulumiwi na yeyote kwa kupunguza kiwango cha pesa mlichokopesha. [Al Baqara: 278-279]. Na Mwenyezi Mungu hakumpa ahadi ya kumpiga vita mtenda maasi, kama alivyompa ahadi mtu wa riba, kwasababu katika riba kuna kuiharibu dini na nchi na mali na nafsi.
Na Uislamu umeharamisha kula mzoga na vilivyochinjwa kwaajili ya masanamu na mizimu, na ukaharamisha kula nyama ya nguruwe, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mmeharamishiwa kwenu nyinyi nyamafu na damu na nyama ya nguruwe, na kitakachochinjwa kwaajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kilichokufa kwa kujinyonga, na kilichokufa kwa kupigwa, na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufa kwa kupigwa pembe (na mwingine) na alichokila mnyama (kikafa) ila mkiwahi kukichinja (kabla hakijafa) na (pia mmeharamishiwa) kilichochinjwa panapofanyikia ibada ya asiyekuwa ya Mwenyezi Mungu (kama mizimu) na (ni haramu kwenu) kutaka kujua siri kwa kuagua kwa mabao (na mfano wake). Hayo yote kwenu nyinyi ni maasi" (Al Maida: 3)
Na Uislamu umeharamisha kunywa pombe na najisi zote na vichafu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu, na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo! Hakika pombe: nayo ni kila kinacholewesha kinachofunika akili,na al-maysir, nayo ni kamari ambayo inakusanya aina za kuwekeana dau na mfano wake, kama zile za kuwekeana badali kutoka pande mbili za wacheza kamari na kuzuia kumtaja Mwenyezi Mungu, na al-ansab: mawe ambayo washirikina walikuwa wakichinja mbele yake kwa njia ya kuyatukuza na yale yanayosimamishwa ili kujisogeza karibu yake kwa ibada na al-azlam: vipande vinavyotumiwa na makafiri kutafuta uamuzi kabla ya kufanya au kuacha kufanya jambo. Hayo yote ni dhambi inayopambiwa na Shetani. Basi jiepusheni na madhambi haya, huenda nyinyi mkafuzu kwa kupata Pepo. Hakika Shetani anataka, kwa kuwapambia madhambi, kuweka baina yenu chenye kuleta uadui na chuki, kwa sababu ya kunywa pombe na kucheza kamari, na kuwaepusha na kumtaja Mwenyezi Mungu na kuswali, kwa kutokuwa na akili katika unywaji pombe na kujishughulisha na pumbao la uchezaji kamari. Basi komekeni na hayo. [Al Maida: 90-91]. Na imetangulia kutajwa katika kipengele namba (30) ameelezea Mwenyezi Mungu ya kwamba miongoni mwa sifa za Mtume rehema na Amani zimfikie katika Taurati kuwa yeye anawaharamishia vichafu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharamishia viovu} ((213)), [Al A'raf: 157].
Na Uislamu umeharamisha kula mali ya yatima, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na wale waliofiliwa na baba zao wakiwa bado hawajabaleghe, na mkawa nyinyi ndio wasimamizi wao, wapeni mali zao wafikapo umri wa kubaleghe, muonapo kutoka kwao kuwa wana uwezo wa kuhifadhi mali zao. Na wala msichukuwe kizuri katika mali zao na mkaweka mahali pake kibaya katika mali zenu. Wala msichanganye mali zao na mali zenu ili mpate kula mali zao kwa hila. Na mwenye kuthubutu kulitenda hilo, hakika huyo amefanya dhambi kubwa. [An Nisaa: 2]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wale wanaozifuja mali za mayatima wakawa wanazichukua pasi na haki, hakika wanakula Moto utakaowaka matumboni mwao Siku ya Kiyama; wataungia Moto ambao watalisikia joto lake. [An Nisaa: 10].
Na Uislamu umeharamisha kupunja kipimo na mzani, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Adhabu kali itawapata wenye kupunguza kipimo". Ambao wakinunua kwa watu cha kupimwa kwa vibaba au kwa mizani hujikamilishia wao wenyewe. Na wakiwauzia watu kinachouzwa kwa vibaba au mizani wanapunguza vipimo. Basi itakuwaje hali ya yule anayeiba na kupunja katika vipimo vyote hivyo, au yule anayeiba katika vipimo hivyo na huku awapunja watu vitu vyao? Hakika huyo anastahiki mateso zaidi kuliko wapunguzaji wa vipimo vya vibaba na mizani. Kwani hawaamini wale wapunjaji ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kuwafufua na kuwahesabu juu ya vitendo vyao. [Al Mutwaffifiin: 1-4].
Na Uislamu umeharamisha kukata udugu (ukoo), na imetangulia katika kipengele namba (31) kutaja Aya na hadithi zinazo onyesha juu ya hilo, na Manabii na Mitume wote wamekubaliana juu ya uharamu wa haya maharamisho.
35- Uislamu unakataza tabia mbaya, kama uongo, na udanganyifu, na usaliti, na hiyana, na utapeli, na husda, na njama ovu, na wizi, na kufanya uovu, na dhulma, na unakataza kila tabia mbovu.
Na Uislamu unakataza tabia mbaya zote kwa ujumla, Amesema Allah Mtukufu: «Na usizungushe uso wako ukauepusha na watu unaposema na wao au wanaposema na wewe, kwa kuwadharau na kuwafanyia kiburi, wala usitembee kwenye ardhi baina ya watu kwa kujigamba na kujivuna. Hakika Mwenyezi Mungu Hampendi kila mwenye kiburi, mwenye kujifaharisha katika nafsi yake, pambo lake na maneno yake. [Luqman: 18]. Amesema Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu, na hakika ninaowachukia zaidi kati yenu na watakaokaa mbali zaidi na mimi siku ya Kiyama ni watu wenye maneno mengi, na waropokaji, na wenye kujifakharisha, wakasema: Tushajua maana ya watu wenye maneno mengi na waropokaji, nini maana ya wenye kujifakharisha? Akasema: Ni wale wenye kiburi". Silsilatu Sswahiiha: 791.
Na Uislamu unakataza uongo, Amesema Allah Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hamuongozi mwenye kuchupa mipaka muongo kupindukia". [Ghaafir: 28]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Na Tahadharini sana na uongo! kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu unampelekea mtu kuingia Motoni, na hatoacha mtu kuendelea kusema uongo, na kuutafuta uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo". Kaipokea Muslim (2607). Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Alama za Mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huenda kinyume, na akiaminiwa hufanya hiyana". Sahihi Bukhariy 6095,
Uislamu unakataza udanganyifu. Na imekuja katika hadithi ya kwamba Mtume rehema na Amani zimfikie alipita katika kapu la chakula akaingiza mkono ndani yake, vidole vyake vikapata unyevunyevu, akasema: "Nini hiki ewe mwenye chakula?" Akasema: kimenyeshewa na mvua ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Akasema: Kwanini usikiweke juu ili watu wakione, yeyote atakayefanya udanganyifu si katika mimi". Kaipokea Muslim (102).
Uislamu unakataza usaliti na hiyana, na utapeli, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na makazifuata sheria Zake kivitendo, msimfanyie hiyana Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa kuyaacha Aliyowalazimisha nayo na kuyafanya Aliyowakataza nayo, na wala msifanye kasoro katika yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaamini nayo, na hali nyinyi mnajua kwamba ni amana inayopasa kutekelezwa. [Al Anfal: 27]. Na amesema Allah Mtukufu: ambao wanatekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu Ambayo Aliwaamrisha kwayo na hawaitengui ahadi ya mkazo ambayo walimuahidi nayo Mwenyezi Mungu. [Ar Ra'di: 20]. Na Mtume rehema na Amani zimfikie alikuwa akisema kuyaambia majeshi yake yanapotoka: "Piganeni vita wala msipore (mali za watu), na wala msifanye usaliti, wala msimtese mtu (kwa kumkata kiungo kimoja kimoja) wala msiuwe mtoto mdogo". Kaipokea Muslim (1731). Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mambo manne yeyote yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na mtu atakayekuwa na jambo moja katika hayo, atakuwa na chembe ya unafiki, mpaka aliache: Anapoaminiwa hufanya hiyana, na anapozungumza husema uongo, na akiingia makubaliano anafanya usaliti, na akigombana anafanya uovu (anachupa mipaka)". Sahihi Bukhariy 34.
Na Uislamu unakataza husda, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Au je, kwani wao wanamuhusudu Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie kwa neema za unabii na utume alizopewa na Mwenyezi Mungu na kuwahusudu Masahaba wake kwa neema ya kuongozwa kwenye Imani, kuukubali utume, kumfuata Mtume na kupewa uwezo katika ardhi, wakawa wanatamani neema hizi ziwaondokee? Hakika sisi tuliwapa watu wa kizazi cha Ibrāhīm, amani imshukie, Vitabu Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwao, wahyi mwingine usiokuwa kitabu chenye kusomwa na tukawapa , pamoja na hayo, utawala wenye kuenea. [An Nisaai: 54]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wengi wa Watu wa Kitabu wanatamani kuwarudisha nyinyi, baada ya kuamini kwenu, muwe makafiri kama mlivyokuwa kabla mkiabudu masanamu. Haya ni kwa sababu ya chuki zilizojaa kwenye nafsi zao, baada ya kuwabainikia ukweli wa Nabii na Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema na amani zimshukie, katika yale aliyokuja nayo. Basi lipuuzeni lolote la ubaya au makosa lililotoka kwao. Na sameheni ujahili wao mpaka Mwenyezi Mungu Alete hukumu Yake ya kupigananao (na hili lilikuwa), na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu; hakuna kitu chochote kimshindacho. [Al Baqara: 109]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Limekuingilieni gonjwa la umma zilizopita kabla yenu: Husda chuki ndilo linalonyoa, sisemi kuwa linanyoa nywele, lakini linanyoa dini, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hamtoingia Peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, hivi nisikufahamisheni jambo linalothibitisha hilo kwenu nyinyi? Toleaneni salamu kati yenu" Sunanu Tirmidhiy: 2510.
Na Uislamu unakataza njama ovu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na mfano huu uliopatikana kwa viongozi wa makafiri huko Makka wa kuzuia dini ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, tumeweka katika kila mji watu waovu wanaongozwa na wakubwa wao, ili wapate kufanya vitimbi humo kwa kuzuia dini ya Mwenyezi Mungu; na wao hawazifanyii vitimbi ispokuwa nafsi zao, na wala hawalihisi hilo. [Al An'am: 123]. Na ameeleza Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa Mayahudi walijaribu kumuuwa Masihi Amani iwe juu yake, na wakapanga njama, lakini Mwenyezi Mungu akawapangia njama, na akabainisha Mwenyezi Mungu kuwa njama ovu hazistahiki ispokuwa kwa watu wake (wapanga njama) Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Alipohisi 'Īsā kutoka kwao ukafiri, aliita kwa watu wake halisi kwa kusema, «Ni nani atakayekuwa na mimi katika kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu.» Wale wasafiwa wa 'Īsā walisema, «Sisi ni wenye kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu na wenye kuilingania, tumemuamini Mwenyezi Mungu na tumekufuata; na ushuhudie, ewe 'Īsā, kuwa sisi tumejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha na kumtii. «Ewe Mola wetu! Tumeiamini Injili uliyoiteremsha na tumemfuata Mtume Wako 'Īsā, amani imshukie, basi tujaalie ni miongoni mwa waliokutolea ushahidi juu ya umoja Wako na kuwatolea ushahidi Manabii juu ya utume wao.» Nao ni umma wa Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ambao wanawatolea ushahidi mitume kuwa wao wamewafikishia umma wao. Wale waliomkanusha 'Īsā, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, walifanya vitimbi kwa kumpangia wenye kumuua. Mwenyezi Mungu akamtoa anayefanana na 'Īsā kwa mtu ambaye aliwaashiria wauaji kwake, wakamshika wakamuua na wakamsulubu wakidhani kuwa ni 'Īsā, amani imshukie. Na Mwenyezi Mungu ni bora wa wenye kufanya vitimbi. Katika haya pana kuthibitisha sifa ya makri (vitimbi) kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu Wake, kwa kuwa ni vitimbi vya haki na ni katika kukabiliana na vitimbi vya wenye vitimbi. Na vitimbi vya Mwenyezi Mungu kwao ni pale Aliposema Mwenyezi Mungu kumwambia 'Īsā, «Mimi nitakutwaa kutoka kwenye ardhi bila ya kupatikana na baya lolote, nitakuinua mpaka kwangu kwa mwili wako na roho yako, nitakuokoa na watu waliokukanusha na nitawafanya wale waliokufuata wewe, yaani, waliyo kwenye dini yako, na kufuata yale uliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya dini na bishara ya Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakamuamini Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, baada ya kutumilizwa kwake, wakashikamana na Sheria aliyokuja nayo, wawe na ushindi juu ya wale walioukanusha utume wako hadi Siku ya Kiyama; kisha mwisho wenu nyote mtarudi kwangu Siku ya Hesabu, ili nitoe uamuzi juu ya tofauti mlizokuwa nazo kuhusu 'Īsā, amani imshukie. [Al Imran: 52-55]. Na akaeleza Mwenyezi Mungu kuwa watu wa Nabii swaleh Amani iwe juu yake, walitaka kumuuwa kwa kufanya vitimbi, wakapanga njama na Mwenyezi Mungu akapanga njama kwao, na akawaangamiza wote, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu tisa hawa wakaambizana wao kwa wao, «Apianeni kwa Mwenyezi Mungu, kila mmoja awaapie wengine:’Tunaapa tutamjia Ṣāleḥ kwa ghafla, kipindi cha usiku, tumuue yeye na tuwaue watu wake kisha tutamwambia atakayesimama kutaka kisasi cha damu yake miongoni mwa jamaa zake: ‘Hatukushuhudia kuuawa kwao.’ Na sisi tutakuwa ni wakweli kwa tuliyoyasema». Basi wakazipanga hila hizi za kumuangamiza Ṣāleḥ na watu wake kwa kuwafanyia vitimbi, tukamuokoa Nabii wetu Ṣāleḥ, amani imshukie, na tukawapatiliza kwa mateso kwa ghafla na hali wao hawatazamii vitimbi vyetu kwao kama malipo ya vitimbi vyao. Basi tazama , ewe Mtume, mtazamo wa mazingatio, mwisho wa njama za ukatili za kundi hili kumfanyia Nabii wao Ṣāleḥ. Sisi tuliwaangamiza wao na watu wao wote. [An Nahli: 49-51].
Na Uislamu unakataza wizi, Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Na hazini mwenye kuzini wakati anazini naye akawa ni muumini, na haibi mwenye kuiba wakati anaiba naye ni muumini, na hanywi pombe wakati anakunywa naye ni muumini, na toba bado iko wazi". Sahihi Bukhariy 6810.
Na Uislamu unakataza uovu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anawaamrisha waja Wake ndani ya Qur’ani hii wawe waadilifu, wafanye usawa katika kutunza haki Yake, kwa kumpwekesha Yeye na kutomshirikisha, na haki ya waja Wake, kwa kumpa haki yake kila mwenye haki. Na Anaamrisha kufanya wema katika kutekeleza haki Yake, kwa kumuabudu na kutekeleza faradhi Zake kwa namna ilivyopasishwa na Sheria, na kuwafanyia wema viumbe Wake katika maneno na vitendo. Na Anaamrisha kuwapa walio na ukaribu wa ujamaa kitu cha kuwaunga na kuwatendea wema. Na Anakataza kila ambalo ni ovu, likiwa ni neno au ni tendo, na ambalo Sheria inalipinga na haikubaliani nalo la ukafiri na maasia, na kuwadhulumu watu na kuwafanyia uonevu. Na Mwenyezi Mungu, kwa maamrisho haya na makatazo haya, Anawawaidhia na kuwakumbusha mwisho mbaya, ili mzikumbuke amri za Mweneyzi Mungu na mnufaike nazo. [An Nahli: 90]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu ameteremsha wahyi kwangu, yakuwa kuweni wanyenyekevu kiasi kwamba asifanye uovu mmoja wenu kwa mwingine, na asichupe mipaka mmoja wenu juu ya mwingine". Sahihi Abuu Daudi 4895.
Na Uislamu unakataza dhulma, Amesema Allah Mtukufu: "Na Mwenyezi Mungu hapendi madhalimu". [Al Imran: 57]. Na amesema Allah Mtukufu: "Hakika hawafaulu madhalimu". [Al An'am: 21]. Na amesema Allah Mtukufu: "Na madhalimu amewaandalia adhabu iumizayo" [Al Insan: 31]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Watu wa aina tatu hayarudishwi maombi yao: Kiongozi muadilifu, na aliyefunga swaumu mpaka atakapofuturu, na maombi ya aliyedhulumiwa, hubebwa juu ya mawingu na yakafunguliwa milango ya mbingu, na anasema Mola aliyetakasika na kutukuka: Naapa kwa Utukufu na uweza wangu, hakika nitakunusuru hata kama baada ya muda". Kaitoa Muslim (2749) kwa ufupi ikiwa na tofauti ndogo, na Tirmidhiy (2526) ikiwa na tofauti ndogo, na Ahmadi (8043) na tamko ni la kwake. Na Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie alipomtuma Mu'adhi kwenda Yemen ilikuwa miongoni mwa yale aliyomwambia: "Na ogopa maombi ya aliyedhulumiwa, kwani hayo hayana kizuizi kati yake na Mwenyezi Mungu". Sahihi Bukhariy 1496. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Tambueni kuwa atakayemdhulumu mtu aliyeingia makubaliano (ya amani) au akamdhalilisha, au akamlazimisha juu ya uwezo wake, au akachukua haki yake bila ridhaa yake, mimi ndiye mtetezi wake siku ya kiyama". Sunanu Abii Daud 3052. Basi Uislamu kama ulivyoona unakataza kila tabia mbaya, au muamala wa kidhalimu, au wakijeuri.
36- Uislamu unakataza miamala ya mali ambayo ndani yake kuna riba au madhara, au ulaghai, au dhulma, au udanganyifu, au unaopelekea katika ugomvi na madhara ya kiujumla kwa jamii na raia na kwa mtu mmoja mmoja.
Uislamu unakataza miamala ya mali ambayo ndani yake kuna riba au madhara, au ulaghai, au dhulma, au udanganyifu, au unaopelekea katika ugomvi na madhara ya kiujumla kwa jamii na raia na kwa mtu mmoja mmoja. Na imetangulia mwanzoni mwa kipengele hiki kutaja Aya na hadithi zinazoharamisha riba au dhulma au udanganyifu au uharibifu katika ardhi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na wale wenye kuwaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike kwa maneno au vitendo bila ya kosa walilolifanya, basi watakuwa wametenda tendo la uongo na uzushi mbaya kabisa, na wamefanya kosa chafu waziwazi, ambalo kwalo watastahili kupewa adhabu huko Akhera. [Al Ahzab: 58]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenye kufanya mema, akamtii mwenyezi Mungu na Mtume Wake, atajipatia mwenyewe thawabu za matendo yake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, atajionea mwenyewe dhambi za matendo yake. Na Mola wako si Mwenye kuwadhulumu waja kwa kuwapunguzia japo thawabu ya jema moja au kuwaongezea japo dhambi la ovu moja. [Fusswilat: 46]. Na imekuja katika mafundisho ya Mtume rehema na Amani zimfikie: "Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie: (Amesema) "Hakuna kudhuru mtu wala kudhuriwa" Sunanu Abii Daud Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi asimuudhi jirani yake, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu mgeni wake, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze. Na katika mapokezi mengine: Basi na amfanyie wema jirani yake." Sahihi Muslim (47). Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Aliadhibiwa mwanamke kwasababu ya paka, alimfunga mpaka akafa, akaingia Motoni kwaajili yake, hakumpa chakula wala maji alipomfunga, wala hakumuachilia ale katika mabaki ya ardhi". Sahihi Bukhariy 3482, Hii ni kwa aliyemuudhi paka, ni vipi kwa anayewafanyia watu maudhi?! Na kutoka kwa Ibn Omari amesema: Alipanda Mtume rehema na Amani zimfikie katika mimbari (jukwaa): Akanadi kwa sauti ya juu, akasema: "Enyi kundi la walioamini kwa ndimi zao na haijapenya imani katika nyoyo zao, msiwaudhi waislamu wala msiwadhalilishe, na wala msifuatilie aibu zao, kwani hakika yeyote atakayefuatilia aibu za ndugu yake muislamu, Mwenyezi Mungu naye atafuatilia aibu zake, na yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atafuatilia aibu zake humfedhehesha hata kama yuko katika tumbo la kipandwa chake, akasema: Na alitazama Ibn Omari katika nyumba yaani katika Al-kaaba, akasema: Ni utukufu ulioje wako wewe (Al-kaaba) na ukubwa wa heshima yako, na Muumini anautukufu mkubwa kwa Mwenyezi Mungu kuliko wewe). Kaitoa Tirmidhiy (2032) na Ibn Hibbaan: (5763). Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi asimuudhi jirani yake, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu mgeni wake, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze." Sahihi Bukhariy 6018. Na kutoka kwa Abuu Huraira, kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie amesema: "Je mnajua ni nani aliyefilisika? wakasema: Aliyefilisika kwetu Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye na Dirham (pesa) wala mali yoyote. Akasema: "Hakika aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakayekuja siku ya kiyama akiwa na (ibada za) swaumu na swala na zaka, na akaja akiwa katukana heshima ya huyu, na kamzulia machafu huyu, na kala mali ya huyu, atakalishwa, kisha atapunguziwa huyu kutoka katika mema yake, na huyu katika mema yake, yakimalizika mema yake kabla hajamaliza kulipa anayodaiwa yatachukuliwa kutoka katika makosa yao yatatupwa kwake kisha atatupwa katika moto". Kaitoa Muslim (2581), na Tirmidhiy (2481) na Ahmadi (8029) na tamko ni la kwake.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu:- "kulikuwa na tawi la mti njiani likiwaudhi watu, mtu mmoja akaliondoa, basi akaingizwa Peponi". kaitoa Bukhariy (652) kwa maana yake, Na Muslim (1914) kwa mfano kama huo, Na Ibn Maajah (3682), Na Ahmadi (10423) na tamko ni lao wawili, Kuondoa udhia njiani kunamuingiza mtu Peponi, unasemaje kwa huyu anayewaudhi watu, na anawaharibia maisha yao.
37- Uislamu umekuja kuihifadhi akili na kuharamisha yote yanayoiharibu, kama kunywa pombe, na ukaipa heshima akili, ukaifanya kuwa ndiyo mahala pakubeba majukumu, na ukaiweka huru na minyororo ya mambo ya hovyo na mizimu. Na hakuna katika uislamu siri zinazolihusu kundi (fulani) kundi jingine halihusiki, na hukumu zake na sheria zake zote zinaafikiana na akili timamu, nazo zinaafikiana na yale yanayopelekea uadilifu na hekima.
Uislamu umekuja kuhifadhi akili na kuipa heshima yake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika maskio na macho, na nyoyo,vyote hivyo kwake vitakuwa ni vyenye kuulizwa". [Al Israai: 36]. Ni lazima kwa mwanadamu ahifadhi akili yake, na kwaajili hiyo uislamu ukaharamisha pombe- Na umetajwa uharamu wa pombe katika kipengele namba: (34) Na Aya nyingi za Qur'ani tukufu zinahitimisha kwa kauli yake Mtukufu: "Huenda mkatia akilini". [Al Baqara: 242]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Maisha ya ulimwengu hayakuwa, katika wingi wa hali zake, ispokuwa ni udanganyifu na ubatilifu. Na matendo mema, kwa kutengeneza nyumba ya Akhera, ndiyo bora kwa wenye kumcha Mwenyezi Mungu, wakajikinga na adhabu Yake kwa kumtii na kujiepusha na mambo ya kumuasi. Kwani hamuelewi, enyi washirikina mliohadaika na pambo la uhai wa kiulimwengu, mkayatanguliza yanayosalia mbele ya yanayomalizika? [A l An'am: 32]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sisi tumekuteremshia Qur’ani kwa lugha ya Waarabu, huenda nyinyi, enyi Waarabu mkaitia akilini maana yake, mkaifahamu na mkatenda kulingana na uongofu wake. [Yusuf: 2]. Na akabainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa uongofu na hekima hawafaidiki navyo ispokuwa wenye akili, nao ni watu wenye uelevu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Anampa taufiki ya usawa katika kunena na kutenda Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yeyote ambaye Mwenyezi Mungu Amemneemesha kwa hilo, Hua Amempa kheri nyingi. Na hatakumbuka hilo na kunufaika nalo ispokuwa wenye akili zenye kung’ara kwa nuru ya Mwenyezi Mungu na uongofu Wake. [Al Baqara: 269].
Na kwaajili hii Uislamu umeifanya akili kuwa mahala pa kubeba majukumu, Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abaleghe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili". Kaitoa Bukhariy akiweka maelezo juu ya mfumo wa tamko la kuthibitisha kabla ya hadithi (5269) kwa mfano wake, na akaitoa ikiwa imeunganishwa Abuu Daudi (4402) na Tirmidhiy (1423) na Nasaai katika (Sunanul Kubraa) (7346) na Ahmadi (956) kwa tofauti ndogo, na Ibn Majah: (2042) kwa muhtasari. Na ukaiacha huru na minyororo ya mambo ya hovyo na mizimu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akielezea kuhusu hali za umma ulivyo shikamana na mambo ya hovyo, kutokana na kuukataa ukweli uliowajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: Hivyo ndivyo ilivyo, hatukutuma kabla yako wewe, ewe Mtume, muonyaji yeyote kwenye kijiji chochote, mwenye kuwaonya na adhabu yetu kwa kutukanusha, na akawaonya na kuwahadharisha juu ya adhabu yetu, ispokuwa wale ambao ziliwatia kiburi neema miongoni mwa viongozi na wakubwa huwa wakisema, ”Sisi tuliwakuta baba zetu kwenye mila na dini, na sisi ni wenye kufuata mwenendo wao na njia yao.” [Azzukhruf: 23]. Na amesema Mwenyezi Mungu akitoa habari kuhusu Nabii Ibrahim kipenzi chake amani iwe juu yake, yakuwa yeye alisema kuwaambia watu wake: "Ni nini masanamu haya mnayakalia wakati wote (kuyaabudu)?. Wakasema, «Tuliwapata baba zetu wakiyaabudu, na sisi tunayaabudu kwa kuwaiga wao.» [Al Anbiyaa: 52-53]. Ukaja uislamu na ukawaamrisha watu kuacha ibada za masanamu, na kujiepusha na mambo ya hovyo yaliyorithiwa kutoka kwa mababa na mababu, na kufuata njia ya Mitume sala na salamu ziwe juu yao.
Na hakuna katika Uislamu siri na hukumu maalumu kwa tabaka fulani bila tabaka jingine. Aliulizwa Ally bin Abii Twalib radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie, naye ni mtoto wa Ammi yake (baba yake mdogo) na Mtume rehema na Amani zimfikie na mume wa binti yake: Je aliwahi kuwapa kitu maalumu Mtume rehema na Amani zimfikie?: Akasema: "Hakuwahi kutupa kitu maalumu Mtume rehema na Amani zimfikie kwa kitu chochote ambacho hakuwajumuisha watu wote, ispokuwa kinachokuwa katika panga langu hili, akasema: Akatoa waraka ulioandikwa ndani yake: Amemlaani Mwenyezi Mungu atakayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na amemlaani Mwenyezi Mungu atakayeiba mipaka ya ardhi, na amemlaani Mwenyezi Mungu atakayemlaani mzazi wake, na amemlaani Mwenyezi Mungu atakayemuhami mzushi". kaipokea Muslim (1978). Na hukumu zote za Uislamu na sheria zake zinaafikiana na akili timamu, nazo zinapelekea uadilifu na hekima.
38- Na dini za batili endapo wasipoweza kufahamu wafuasi wake yale yaliyomo katika migongano, na mambo ambayo yanapingana na akili, wanadhania wakuu wa dini hizo kuwa dini iko juu ya akili, na kuwa akili haina nafasi ya kuielewa dini na kuidhibiti kimaarifa. wakati Uislamu umeichukulia dini kuwa ni nuru inayoiangazia akili njia yake; wakuu wa dini za batili wanamtaka mtu ajiepushe na akili na awafuate wao, Na Uislamu unamtaka mtu aamshe akili yake; ili ajuwe uhalisia wa mambo kama yalivyo.
Na dini za batili endapo wasipoweza kufahamu wafuasi wake yale yaliyomo katika migongano, na mambo ambayo yanapingana na akili, wanadhania wakuu wa dini hizo kuwa dini iko juu ya akili, na kuwa akili haina nafasi ya kuielewa dini na kuidhibiti kimaarifa. wakati Uislamu umeichukulia dini kuwa ni nuru inayoiangazia akili njia yake; wakuu wa dini za batili wanamtaka mtu ajiepushe na akili na awafuate wao, Na Uislamu unamtaka mtu aamshe akili yake; ili azingatie na afikirie na ajuwe uhalisia wa mambo kama yalivyo. Amesema Mwenyezim Mungu Mtukufu: Na kama vile tulivyowapelekea wahyi Manabii kabla yako wewe, ewe Nabii, tulikuletea wewe wahyi wa Qur’ani itokayo kwetu, hukuwa unajua kabla yake ni vitabu vipi vilivyotangulia wala nini Imani wala zipi Sheria zinazotokana na Mwenyezi Mungu, Lakini tumeifanya Qur’ani ni mwangaza kwa watu ambao kwao tunawaongoza waja wetu tunaowataka kwenye njia iliyolingana sawa. Na hakika wewe, ewe Mtume, unaelekeza na kuongoza kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwenye njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu, [Ash shura: 52]. Wahyi wa Mwenyezi Mungu umekusanya ushahidi na hoja zinazoiongoza akili salama katika uhalisia amabo inataka sana kuujua na kuuamini. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi watu, kwa hakika umekuja kwenu ushahidi kutoka kwa Mola wenu, nao ni Mtume wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo miongoni mwa maelezo yaliyo waziwazi na hoja za yakini, kubwa ya hizo ni Qur’ani tukufu, zenye kutolea ushahidi ukweli wa unabii wake na utume wake wa mwisho; na tumewateremshia Qur’ani ikiwa ni uongofu na ni nuru yenye kufafanua mambo waziwazi. [An Nisaai: 174]. Basi Mwenyezi Mungu anamtakia mwanadamu aishi katika nuru ya uongofu na elimu na uhakika, lakini shetani na matwaghuti wanamtakia mwanadamu abakie katika giza la ukafiri na ujinga na upotofu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Anawasimamia Waumini kwa kuwanusuru, kuwaafikia (kuwawezesha) na kuwahifadhi, Anawatoa kutoka kwenye giza la ukafiri kuwapeleka kwenye nuru ya Imani. Na wale waliokufuru, wanusuru wao na wasaidizi wao ni wale wafananishwao na Mwenyezi Mungu na masanamu wanayoyaabudu yasiyokuwa Mwenyezi Mungu. Hao wanawatoa wao kutoka kwenye nuru ya Imani kuwapeleka kwenye giza la ukafiri. Wao ndio watu wa Motoni wenye kukaa humo, wenye kusalia humo milele na si wenye kutoka humo. [Al Baqara: 257].
39- Uislamu unaitukuza elimu sahihi na unahimiza kufanya utafiti wa kielimu ulioepukana na matamanio, na unataka kutazama na kutafakari katika nafsi zetu na katika ulimwengu unaotuzunguka, na matokeo sahihi ya kielimu ya elimu hayapingani na Uislamu.
Na Uislamu unaitukuza elimu sahihi amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Anawanyanyua (daraja) Mwenyezi Mungu wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja za juu zaidi, na Mwenyezi Mungu kwa yale mnayoyafanya ni mjuzi". (Al-Mujadilah: 11). Na Mwenyezi Mungu akaunganisha ushahidi wa wenye elimu na ushahidi wake na ushahidi wa Malaika juu ya kitu kikubwa kilichotolewa ushahidi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu Ameshuhudia kuwa Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa uungu. Na Ameambatanisha ushahidi wake na ule wa Malaika na watu wa elimu juu ya kitu kitukufu zaidi chenye kushuhudiwa, nacho ni Tawhīd umoja Wake Aliyetukuka na kusimamia Kwake haki na uadilifu. Hapana Mola ispokuwa Yeye, Aliye Mshindi Ambaye hakuna kitu Atakacho kiwe kikakataa kuwa, Mwenye hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. [Al-Imran: 18]. Na hili linabainisha ubora wa watu wenye elimu katika uislamu, na Mwenyezi Mungu hakumuamrisha Mtume wake Muhammadi rehema na Amani zimfikie kutaka ziada katika jambo lolote ispokuwa elimu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na sema, Mola wangu nizidishie elimu". [Twaha: 114]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Atakayeshika njia kwenda kutafuta elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi yeye njia ya kwenda Peponi, Na hakika Malaika huweka mbawa zao kwa kuridhishwa na mwenye kutafuta elimu, na hakika mwenye kutafuta elimu huombewa msamaha na vyote vilivyoko mbinguni na ardhini, hata samaki kwenye maji, na hakika ubora wa mtu mjuzi (mwenye elimu) kwa mfanya ibada, ni kama ubora wa mwezi kwa nyota zote, hakika Wanachuoni ni warithi wa Manabii, Hakika Manabii hawakurithisha Dinar wala Dirham (pesa) Hakika walirithisha elimu, atakayeichukua basi kachukua fungu la thamani kubwa". Kaitoa Abuudaud (3641), na Tirmidhiy (2682), na Ibn Majah (223) na tamko ni lake, na Ahmadi (21715).
Na Uislamu unahimiza kufanya utafiti wa kielimu ulioepukana na matamanio, na unaelekeza kutazama na kutafakari katika nafsi zetu na katika ulimwengu unaotuzunguka, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Tutawaonyesha, hawa wakanushaji, aya zetu za kuteka miji na kupata nguvu Uislamu katika majimbo mbalimbali na juu ya dini nyingine na maeneo ya mbingu na ardhi, na katika matukio makubwa Anayoyaleta Mwenyezi Mungu humo na ndani ya nafsi zao, na vile vilivyomo humo miongoni mwa alama za kuvutia za utendajikazi wa Mwenyezi Mungu na maajabu ya utengenezaji Wake, (tutawaonyesha hayo yote) mpaka iwafunukie nyinyi, ufunuzi usiyokubali shaka yoyote, kwamba Qur’ani ndiyo haki iliyoletwa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wa viumbe wote. Je hauwatoshi wao ushahidi wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kuwa ni dalili ya kuwa Qur’ani ni haki na kuwa aliyekuja nayo ni mkweli? Kwani Mwenyezi Mungu Ameishuhudilia kwa kuisadikisha, na Yeye ni shahidi wa kila kitu, na hakuna kitu chochote chenye kutolea ushahidi kuliko ushahidi wa Mwenyezi Mungu, aliyetakasika na kutukuka. [Fusswilat: 53]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Au kwani hawaangalii, hawa wakanushaji aya za Mwenyezi Mungu, kwenye ufalme wa Mwenyezi Mungu uliyo mkubwa na mamlaka Yake yenye uwezo wa kushinda, mbinguni na ardhini na chochote kile Alichokiumba Mwenyezi Mungu,na huenda ukawa umesogea karibu wakawa watakufa kwenye ukafiri wao na watakuwa kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake makali? Basi ni kitisho gani na onyo gani baada ya onyo la Qur’ani wataliamini na watalifanyia kazi? [Al A'raf: 185]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi si waende hawa wanaomkanusha Mwenyezi Mungu, wanaoghafilika na Akhera, mwendo wa kufikiria na kuzingatia, wakapata kuona yalikuwa namna gani malipo ya umma waliowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu, Hakika walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao kimiili na wana uwezo zaidi wa kustarehe na maisha, kwa kuwa waliilima ardhi na kuipanda mimea, na wakajenga majumba ya kifahari na wakayakalia, hivyo basi waliujenga ulimwengu wao kuliko vile watu wa Makkah walivyouamirisha ulimwengu wao, na kusiwafalie kitu kule kuamirisha kwao wala urefu wa maisha yao. Na Mitume wao waliwajia na hoja waziwazi na dalili zenye kung’ara, wakawakanusha na Mwenyezi Mungu Akawaangamiza. Na Hakuwadhulumu kwa huko kuwaangamiza, ispokuwa wao wenyewe walijidhulumu wenyewe kwa kufanya ushirikina na kuasi. [Ar Rum: 9].
Na matokeo ya kielimu yaliyo sahihi hayapingani na Uislamu, na tutataja mfano mmoja ambao Qur'ani imetaja kwa ufafanuzi wa ndani sana kuhusu jambo lake, kabla ya miaka elfu moja na mia nne (140), na elimu ya kisayansi ya sasa imekuja kujua juzi; yakaja majibu ya kitaalamu yakiwa sambamba na yale yaliyoko katika Qur'ani tukufu, nayo ni kuumbwa kwa kichanga katika tumbo la mama yake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika tulimuumba Ādam kutokana na udongo ulio safi Kisha tukamuumba kw tone la manii(mbegu za uzazi) lilowekwa katika mahala palipo hifadhiwa. Kisha tukaliumba hilo tone kwa kuligeuza kulifanya pande la damu iliyo nyekundu, kisha tukaliumba pande la damu kwa kuligeuza kulifanya kinofu cha nyama kadiri ya kutafunika baada ya siku arobaini, na tukakiumba kinofu cha nyama kilicho laini kwa kukigeuza kukifanya mifupa, na tukaivisha nyama ile mifupa, kisha tukamfanya ni kiumbe kingine kwa kupuliza roho ndani yake. Ametukuka Mwenyezi Mungu Mwenye kheri nyingi Ambaye Ametengeneza umbo la kila kitu. [Al Mu'uminun: 12-14].
40- Na hakubali Mwenyezi Mungu jambo lolote, wala hatoi malipo kwalo katika Akhera ispokuwa kwa yule aliyemuamini Mwenyezi Mungu na akamtii yeye, na akawaamini Mitume wake sala na salamu ziwe juu yao, na Mwenyezi Mungu hakubali katika ibada isipokuwa zile alizoziwekea sheria Yeye, inakuwaje mtu anamkufuru Mwenyezi Mungu halafu anataraji amlipe?! Na Mwenyezi Mungu hakubali imani ya yeyote ispokuwa atakapowaamini Manabii Amani iwe juu yao, na akaamini utume wa Muhammadi rehema na Amani ziwe juu yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakubali jambo lolote, wala hatoi malipo kwalo Akhera ispokuwa kwa yule aliyemuamini Mwenyezi Mungu na akamtii Yeye, na akawaamini Mitume wake sala na salamu ziwe juu yao, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Yeyote ambaye matakwa yake ni ulimwengu huu wa sasa na akaushughulikia huo peke yake, asiiamini Akhera na asifanye matendo ya kumfaa huko, Mwenyezi Mungu Atamharakishia, hapa ulimwenguni, Anayoyataka Mwenyezi Mungu na kuyapendelea miongoni mwa yale aliyoyaandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa (Al- Lawḥ Al-Mahfūḍh) kisha Mwenyezi Mungu Atamjaalia huko Akhera moto wa Jahanamu, atauingia akiwa ni mwenye kulaumiwa, ni mwenye kufukuzwa kwenye rehema Yake Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka. Hiyo ni kwa sababu ya kutaka kwake ulimwengu na kujishughulisha nao bila ya Akhera. Na yeyote aliyekusudia kwa matendo yake mema kupata malipo ya Nyumba ya Akhera yenye kusalia na akajishughulisha nayo kwa kumtii Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na hali yeye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kuamini thawabu Zake na malipo Yake makubwa, basi hao matendo yao ni yenye kukubaliwa ni yenye kuhifadhiwa kwa ajili yao mbele ya Mola wao na watapata malipo yake. [Al Israa: 18-19]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi Mwenye kujilazimisha kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake na akafanya awezayo ya matendo mema kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumuabudu. Kwani Mwenyezi Mungu Hayapotezi matendo Yake wala Hayabatilishi, bali Anayaongeza yote hayo mara nyingi, na atayakuta aliyoyatenda kwenye Kitabu chake siku atakayofufuliwa baada ya kufa kwake. [Al Anbiyaa: 94]. Na Mwenyezi Mungu hakubali katika ibada ispokuwa zile alizoziwekea sheria Yeye, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Basi yeyote anayetaraji kukutana na Mola wake, basi na afanye matendo mema, na wala asimshirikishe katika ibada ya Mola wake yeyote". [Al Kahf: 110]. Akabainisha kuwa matendo hayawi mema ispokuwa yatakapokuwa katika yale aliyoyawekea sheria Mwenyezi Mungu, na mtendaji akawa ni mwenye ikh'las katika matendo yake pamoja na kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, naye akawa ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kuwasadikisha Manabii wake na Mitume wake sala na salamu ziwe juu yao, ama yatakayekuwa matendo yake ni kinyume na hivyo, hakika amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hapo tutayaleta yale waliyoyafanya yanayoonekana kuwa ni mazuri na ya kidini, tuyafanye ni yenye kubatilika na kupotea. Hayatawanufaisha na yatakuwa ni kama vumbi linalorushwa, nalo ni lile vumbi lembamba linaloonekana kwenye mwangaza wa jua. Hivyo ni kwamba matendo mema hayawi na manufaa yoyote huko Akhera ispokuwa mwenye kuyafanya awe na imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtakasia na kumfuata Mtume Wake Muhammadi, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. [Al Furqan: 23]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Nyuso za Makafiri, Siku hiyo, zitakuwa ni zenyekudhalilika". "Ni zenye kufanya kazi ngumu kabisa (huko motoni) zichoke (kuchoka kusikokuwa na mfano). "Waingie moto uwakao kweli kweli" [Al Ghashia: 2-4]. Nyuso hizi ni zenye kudhalilika tena zenye kuchoka kutokana na matendo, lakini kwakuwa zilikuwa zikifanya kinyume na muongozo wa Mwenyezi Mungu; ameyafanya Mwenyezi Mungu mafikio yake kuwa ni Motoni; kwasababu zenyewe hazikufanya kupitia yale Mwenyezi Mungu aliyoyawekea sheria, bali ziliabudu ibada za batili, na zikafuata viongozi wapotofu ambao wanawaanzishia wao dini za batili, hivyo amali njema inayokubalika kwa Mwenyezi Mungu ni ile inayoafikiana na yale aliyokuja nayo Mtume rehema na Amani zimfikie, inakuwaje mtu amkufuru Mwenyezi Mungu halafu ataraji amlipe?!.
Na Mwenyezi Mungu hakubali imani ya mtu yeyote ispokuwa atakapowaamini Manabii amani iwe juu yao wote, na akaamini Utume wa Muhammadi rehema na Amani ziwe juu yake- tayari tumetangulia kutaja baadhi ya ushahidi juu ya hilo katika kipengele namba (20) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ameamini na kuyakinisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yale aliyoletewa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wake. Na ni haki kwake ayakinishe. Na Waumini pia wameamini na kufanya amali zinazoambatana na Qur’ani Tukufu. Kila mmoja katika wao amemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola na Muabudiwa, Aliyesifika kwa sifa za utukufu na ukamilifu, na kuwa Mwenyezi Mungu Anao Malaika watukufu, na kuwa Yeye Ameteremsha Vitabu na Ametuma Mitume kwa waja Wake. Hatuwaamini, sisi Waumini, baadhi yao na kuwakanusha baadhi yao. Bali tunawaamini wao wote. Na wanasema, Mtume na Waumini, «Tumeusikia, ewe Mola wetu, wahyi uliouleta na tumetii katika yote hayo. Tunatarajia uyasamehe, kwa wema Wako, madhambi yetu. Wewe Ndiye Ambaye Uliyetulea kwa neema Zako Ulizotuneemesha nazo. Kwako, Peke Yako, ndio marejeo yetu na mwisho wetu.» [Al Baqara: 285]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, endeleeni kwenye msimamo mlionao wa kumuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Imani thabiti, kumuamini Mtume Wake Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kuwatii wao wawili, kuiamini Qur’ani Aliyoiteremsha kwake na kuviamini vitabu vyote Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume. Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Malaika Wake waliotukuzwa, vitabu Vyake Alivyoviteremsha ili kuwaongoza viumbe Wake, Mitume Wake Aliowachagua kufikisha ujumbe Wake na Siku ya Mwisho ambayo watu katika siku hiyo watafufuka baada ya kufa ili waorodheshwe na wahesabiwe, atakuwa ametoka kwenye Dini na atakuwa yuko mbali sana na njia ya haki. [An Nisaa: 136]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: kumbuka, ewe Mtume, pindi Alipochukua Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ahadi ya mkazo kwa Manabii wote kwamba, «Nikiwaletea Kitabu na hekima kisha akaja kwenu mjumbe kutoka kwangu, mwenye kusadikisha vitabu mlivyonavyo, mtamuamini na kumnusuru? Je, mmekiri na kukubali hilo na mmechukua juu yake ahadi yangu ya mkazo?» Wakasema, «Tumekubali hilo.» Akasema, «Kueni mashahidi, baadhi yenu juu ya wengine, na kueni mashahidi kwa hilo juu ya umma wenu, na mimi ni Mwenye kushuhudia pamoja na nyinyi juu yenu na juu yao. Katika haya pana ahadi nzito Aliyoichukua Mwenyezi Mungu kutoka kwa kila Nabii amuamini Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kuchukua ahadi nzito kutoka kwa umma wa Manabii wote juu ya hilo. [Al-Imran: 81].
41- Hakika lengo la jumbe zote za Mungu ni: Dini ya haki impe utukufu mwanadamu, ili awe mja halisi mwenye kumtakasia Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu, na imuweke huru na utumwa wa kuwaabudu watu, au visivyo na uhai au vitu vya hovyo, hivyo Uislamu- kama unavyoona- hauwatukuzi watu na kuwanyanyua juu zaidi ya nafasi zao, na wala haufanyi kuwa waumba na miungu.
Hakika lengo la jumbe zote za Mungu ni: Dini ya haki impe utukufu mwanadamu, ili awe mja halisi mwenye kumtakasia Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu, na imuweke huru na utumwa wa kuwaabudu watu, au visivyo na uhai au vitu vya hovyo, Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani zimfikie: "Amepata hasara mja (mwenye kuabudu) Dinari na Dirhamu na mazao, na mavazi, akipewa anaridhia, na sipopewa huchukia". Sahihi Bukhariy 6435. Hivyo binadamu aliyesawa hanyenyekei ispokuwa kwa Mwenyezi Mungu, mali hazimfanyi kuwa mtumwa wala uheshimiwa wala vyeo, wala kabila, na katika simulizi hii kuna mambo yanayoweka wazi yale waliyokuwa nayo watu kabla ya Utume na ni vipi walikuwa baada yake?.
Pindi walipo hama waislamu wa mwanzo kwenda Ethiopia na akawauliza Mfalme wa Ethiopia -wa zama hizo- Najashi- akawaambia: "Ni dini gani hii ambayo kwasababu ya dini hiyo mmeacha familia zenu na wala hamjaingia katika dini yangu wala katika dini ya yeyote katika umma huu?" Ja'far bin Abii Twalib akamwambia: Ewe Mfalme! sisi tulikuwa ni watu wa zama za ujinga, tunaabudu masanamu na tunakula mizoga, na tunafanya machafu na tunakata udugu, na tunaishi vibaya na majirani, mwenye nguvu katika sisi anamuonea dhaifu, tumeishi hivyo mpaka Mwenyezi Mungu akatuma kwetu sisi Mjumbe miongoni mwetu, tunayeijua nasaba yake (ukoo wake) na ukweli wake na uaminifu wake, na kujizuia kwake na machafu, akatulingania kwa Mwenyezi Mungu ili tumpwekeshe na tumuabudu Yeye, na tuachane na yale tuliyokuwa tukiyaabudu sisi na baba zetu kinyume na Allah katika mawe na mizimu, na akatuamrisha kuwa wakweli katika mazungumzo, na kutekeleza amana, na kuunga udugu, na kuishi vizuri na jirani na kujizuia na maharamisho na kumwaga damu, na akatukataza na machafu na kusema uongo, na kula mali ya yatima, na kuwazulia machafu wanawake waliojihifadhi, na akatuamrisha tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila kumshirikisha na chochote, na ametuamrisha swala na zaka na kufunga" Akasema: Akamuhesabia mambo mengi kuhusu uislamu, tukamsadikisha na tukamuamini na tukamfuata kwa yale aliyokuja nayo, tukamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na hatukumshirikisha na chochote, tukaharamisha aliyotuharamishia na tukahalalisha aliyotuhalalishia". Kaitoa Ahmadi (1740) kwa tofauti ndogo, na Abuu Nua'im katika (Hilyatul Auliyaai) (1/115) kwa mukhtasar. Hivyo Uislamu kama unavyoona hauwatukuzi watu na kuwanyanyua zaidi ya nafasi zao, na wala hauwafanyi kuwa mabwana na miungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, ewe Mtume, kuwaambia Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, «Njooni kwenye neno la uadilifu na haki tushikamane nalo sote. Nalo ni sisi kuielekeza ibada yetu kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na tusimfanye yeyote kuwa ni mshirika pamoja na Yeye, awe ni sanamu au msalaba au Shetani au kinginecho. Na wala wasiwafanye baadhi yetu watu wengine kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu.» Basi wakiukataa wito huu mzuri, waambieni wao, enyi Waumini, «Kuweni ni mashahidi kwetu kuwa sisi tumejisalimisha kwa Mola wetu na tumenyoosha shingo zetu Kwake kwa kukubali kuwa ni waja Wake na kwa kumtakasa.» Na wito huu kwenye neno la sawa, kama unavyoelekezwa kwa Mayahudi na Wanaswara, unaelekezwa pia kwa wenye mwenendo kama wao. [Al-Imran: 64]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na haikuwa kwa yeyote katika wao awaamrishe nyinyi kuwafanya Malaika na Mitume ni miungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu ambao nyinyi mnawaabudu. Je, inaingia akilini, enyi watu, yeye awaamrishe kumkanusha Mwenyezi Mungu baada ya kufuata kwenu amri yake? [Al-Imran: 80]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Msichupe mipaka katika kunisifu kama walivyochupa mipaka manaswara kwa mwana wa Mariam, kwa hakika mimi ni mja wake, basi semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na mjumbe wake". Sahihi Bukhariy 3445.
42- Mwenyezi Mungu ameweka sheria katika Uislamu ya kufanya toba nayo ni: Mwanadamu kurejea kwa Mola wake na kuachana na dhambi, na Uislamu unabomoa yale yaliyofanyika kabla yake katika madhambi, na toba inafuta yaliyokuwa kabla yake katika madhambi, hakuna haja ya kwenda kukiri mbele ya mtu kwa makosa ya mwanadamu.
Mwenyezi Mungu ameweka sheria katika Uislamu ya kufanya toba nayo ni: Mwanadamu kurejea kwa Mola wake na kuachana na dhambi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tubieni kwa Mwenyezi Mungu wote enyi waumini, ili mpate kufaulu} [Nur 31]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwani hawajui, hawa wenye kujikalisha nyuma na kuacha kwenda kwenye jihadi na wengineo, kwamba Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Ambaye Anakubali toba ya waja Wake, Anachukua sadaka na Anatoa malipo yake, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba ya waja Wake warejeapo Kwake, ni Mwenye kuwarehemu warudipo kutaka radhi Zake.? [At Tauba: 104]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenyezi Mungu, aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Anayekubali toba kutoka kwa waja Wake wanaporudi kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, Ndiye Anayesamehe makosa na Ndiye Anayejua mnayoyafanya ya kheri na shari, hakuna chochote kinachofichikana Kwake, na Yeye ni Mwenye kuwalipa kwa hayo. [Ash shura: 25]. Na Amesema Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Mwenyezi Mungu huwa ana furaha kubwa kwa toba ya mja wake muumini, (huwa ana furaha zaidi) kuliko mtu aliye safarini katika ardhi isiyoishi watu yenye kutisha, akiwa na kipando chake na kikiwa kimebeba chakula chake na kinywaji chake, akalala, tahamaki anaamka akakuta kipando chake kimeondoka, akakitafuta mpaka akapatwa na kiu, kisha akasema: Ah! narudi nilipokuwa nalala mpaka nife, akaweka kichwa chake katika muundi (wa mkono) wake ili asubiri kufa, akaamka anakuta kipando chake kiko naye hapo na kiko na chakula chake na kinywaji chake, Hivyo Mwenyezi Mungu huwa na furaha zaidi kwa toba ya mja muumini kuliko huyu na kipando chake na chakula chake". Kaipokea Muslim (2744).
Na Uislamu unabomoa yale yaliyofanyika kabla yake katika madhambi, na toba inafuta yale yaliyofanyika kabla yake katika madhambi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, ewe Mtume, kuwaambia wale waliokanusha upweke wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Washirikina wa watu wako kwamba watakomeka na ukafiri na kumfanyia uadui Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wakarudi kumuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake na kutompiga vita Mtume na Waumini, Mwenyezi Mungu Atawasamehe madhambi yaliyopita, kwani Uislamu unafuta yaliyopita. Na watakaporudia washirikina hawa kukupiga vita baada ya tukio ambalo ulipata ushindi juu yao siku ya Badr, basi mwendo wa watu wa mwanzo umetangulia, nao ni kwamba wao wakikanusha na wakaendelea kwenye ukaidi wao, tutawaletea adhabu na mateso kwa haraka. [Al Anfal: 38]. Na Mwenyezi Mungu amewaita wakristo kuja katika toba, akasema Allah uliyetukuka uwezo wake: Mbona Manaswara hawa hawarudi kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na wakatubia kwa waliyoyasema na wakamuomba msamaha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka? Kwani Mwenyezi Mungu , Aliyetukuka, ni Mwenye kuyasamehe madhambi ya wenye kutubia, ni Mwenye huruma kwao. [Al Maidah: 74]. Na Mwenyezi Mungu akawahamasisha wafanya maasi wote, na wafanya madhambi kufanya toba, akasema Allah Mtukufu: Sema, ewe Mtume, kuwaambia waja wangu waliojidhulumu nafsi zao kwa kuyajia madhambi ambayo nafsi zao zinawaitia, «Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu, kwa wingi wa madhambi yenu, kwani Mwenyezi Mungu Anasamehe dhambi zote kwa mwenye kutubia kutokana nayo na akayaacha namna yatakavyokuwa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya wenye kutubia miongoni mwa waja Wake, ni Mwenye kuwarehemu. [Azzumar: 53]. Na alipoazimia A'mru bunil Aaswi kusilimu, alihofia kutosamehewa makosa yake aliyoyafanya kabla ya uislamu, akasema A'mru akisimulia tukio hilo: (Mwenyezi Mungu alipouingiza Uislamu moyoni mwangu, anasema: Nilimwendea Mtume rehema na Amani zimfikie ili aniunge mkono, akanyoosha mkono wake kwangu, nikasema: Sitokuunga mkono ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mpaka unisamehe yale yaliyotangulia katika makosa yangu, akasema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani zimfikie akaniambia: Ewe A'mru, kwani hujui kuwa kuhama kunafuta yaliyotangulia katika madhambi? Ewe A'mru, kwani hujui kuwa Uislamu unafuta yale yaliyokuwa kabla yake katika madhambi?). Kaitoa Muslim (121) kwa urefu mfano kama hii, na Ahmadi (17827) na tamko ni la kwake.
43- Kupitia Uislamu yanapatikana mahusiano kati ya mtu na Mwenyezi Mungu moja kwa moja, haihitaji kuwa na mtu katikati kama muwakilishi kati yako na Mwenyezi Mungu, Uislamu unakataza kuwakusanya watu kuwa kama miungu au washirika wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji na ulezi na uabudiwa wake.
Katika Uislamu hakuna haja ya kukiri mbele ya mtu makosa ya mwanadamu, Na Kupitia Uislamu yanapatikana mahusiano kati ya mtu na Mwenyezi Mungu moja kwa moja, haihitaji kuwa na mtu katikati kama muwakilishi kati yako na Mwenyezi Mungu, kama ilivyotangulia katika kipengele namba: (36) yakwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaita (aliwalingania) watu wote kuomba toba na kurejea kwake, hivyo hivyo Yeye amewakataza watu wasiwafanye Manabii na Malaika kuwa ni wawakilishi kati yake na waja wake, Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na haikuwa kwa yeyote katika wao awaamrishe nyinyi kuwafanya Malaika na Mitume ni miungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu ambao nyinyi mnawaabudu. Je, inaingia akilini, enyi watu, yeye awaamrishe kumkanusha Mwenyezi Mungu baada ya kufuata kwenu amri yake? [Al-Imran: 80]. Hivyo Uislamu- kama unavyoona- unakataza kuwafanya watu kuwa ni miungu au washirika wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji ulezi na uabudiwa wake, na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Wakristo: Mayahudi na Manaswara wamewafanya wanavyuoni na watu wema kuwa ni miungu wenye kuwawekea hukumu za sheria, wakawa wanajilazimisha kuzifuata na wanaacha sheria za Mwenyezi Mungu. Na pia walimfanya Al- Masīḥ, 'Īsā mwana wa Maryam, kuwa ni mungu, wakamuabudu. Na hakika Mwenyezi Mungu Amewaamrisha wao wamuabudu Yeye Peke Yake, bila ya mwingine. Yeye Ndiye Mungu wa haki. Hakuna mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Yeye. Amejiepusha na Ametakasika na kila kile wanachokizua watu wa ushirikina na upotevu. [At Tauba: 31]. Na Mwenyezi Mungu akawakemea makafiri yakuwa wao wanajiwekea wawakilishi kati yao na Mwenyezi Mungu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Jua utanabahi kwamba ni haki ya Mwenyezi Mungu, Peke Yake, kutiiwa utiifu uliyotimia uliosalimika na ushirikina. Na wale wanaomshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu wakawafanya wasiokuwa Yeye kuwa ni wategemewa, wanasema, «Hatuwaabudu waungu hawa pamoja na Mwenyezi Mungu ispokuwa wapate kutuombea kwa Mwenyezi Mungu na ili watukurubishe daraja Kwake.» Hivyo basi wakakufuru, kwani ibada na uombezi ni wa Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Hakika Mwenyezi Mungu Atawapambanua, Siku ya Kiyama, baina ya Waumini wenye ikhlasi na wale wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, katika yale waliyokuwa wanatofautiana juu yake kuhusu vile walivyoabudu. Hapo amlipe kila mmoja kwa anachostahiki. Hakika Mwenyezi Mungu hawaelekezi kuongoka kwenye njia iliyonyooka wale wenye kumzulia uongo Mwenyezi Mungu, wenye kuzikanusha aya Zake na hoja Zake. [Azzumar: 3]. Na Mwenyezi Mungu akawabainisha waabudu masanamu -watu wa zama za ujinga- walikuwa wakiweka wawakilishi kati yao na Mwenyezi Mungu na wanasema: Wao wanawakurubisha kwa Mwenyezi Mungu:
Na Mwenyezi Mungu anapowakataza watu kutowafanya Manabii au Malaika kuwa ni waombezi kati yake na waja wake; basi wasiokuwa wao ni zaidi! inakuwa vipi haliyakuwa Manabii na Mitume sala na salamu ziwe juu yao hufanya haraka kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akielezea hali ya Manabii na Mitume Amani iwe juu yao: "Hakika wao walikuwa wakienda mbio katika mambo ya kheri, na wakituomba sisi kwa shauku (ya kuyapata yale mazuri waliyoahidiwa) na hofu (ya kuogopa wasipatwe na mabaya ya adhabu walizo tahadharishwa) na walikuwa kwetu sisi ni wanyenyekevu". [Al Anbiyaai: 90]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hao ambao washirikina wanawaomba, miongoni mwa Manabii, watu wema na Malaika, wao wenyewe wanashindana kujiweka karibu na Mola wao kwa matendo mema wanayoyaweza, wanatarajia rehema Yake na wanaogopa adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako ndiyo ambayo inatakikana kwa waja wawe na hadhari nayo na waiogope." [Al Israai: 57]. Yaani: Hakika wale mnaowaomba kinyume na Mwenyezi Mungu- katika Manabii na watu wema- hata wao wanataka ukaribu kwa Mwenyezi Mungu na wanataraji rehema zake na wanaogopa adhabu yake; inakuwaje waombwe kinyume na Mwenyezi Mungu?.
44- Na mwisho wa ujumbe huu tukumbuke kuwa watu wanatofautiana zama na utaifa wao, na miji yao, bali jamii ya kibinadamu yote inatofautiana katika fikra zake na malengo yake yanatofautiana kutokana na mazingira yake na shughuli zake, hivyo ina haja kubwa ya kupata muongozaji wa kuiongoza, na utaratibu unaoweza kuwakusanya, na hakimu anayeweza kuwahami, na walikuwa Mitume Watukufu- sala na salamu ziwe juu yao- wakilisimamia hilo kupitia wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu- wakiwaongoza watu katika njia ya kheri na uongofu, na wakiwakusanya katika sheria ya Mwenyezi Mungu na wakihukumu kati yao kwa haki, mambo yao yakanyooka kulingana na kuwakubalia kwao hao Mitume na ukaribu wa zama zao na jumbe za Mwenyezi Mungu, na akahitimisha Mwenyezi Mungu jumbe zote kwa ujumbe wa Mtume Muhammadi rehema na Amani zimfikie, na akaamrisha ubakie, na akaufanya kuwa ni muongozo kwa watu na huruma na ni muongozo katika njia inayofikisha kwake yeye Allah Mtukufu.
Na mwisho wa ujumbe huu tukumbuke kuwa watu wanatofautiana zama na utaifa wao, na miji yao, bali jamii ya kibinadamu yote inatofautiana katika fikra zake na malengo yake yanatofautiana kutokana na mazingira yake na shughuli zake, hivyo kuna haja kubwa ya kupata muongozaji wa kuiongoza, na utaratibu unaoweza kuwakusanya, na hakimu anayeweza kuwahami, na walikuwa Mitume Watukufu- sala na salamu ziwe juu yao- wakilisimamia hilo kupitia wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu- wakiwaongoza watu katika njia ya kheri na uongofu, na wakiwakusanya katika sheria ya Mwenyezi Mungu na wakihukumu kati yao kwa haki, mambo yao yakanyooka kulingana na kuwakubalia kwao hao Mitume na ukaribu wa zama zao na jumbe za Mwenyezi Mungu, na ulipokithiri upotofu na ujinga ukaenea na masanamu yakaabudiwa; Mwenyezi Mungu akamtuma Nabii wake Muhammad rehema na amani zimfikie kwa uongofu na dini ya haki, ili awatoe watu katika giza la ukafiri, na ujinga na kuabudu masanamu kuja katika imani na uongofu.
45- Hivyo ninakuusia ewe mwanadamu usimame kwaajili ya Mwenyezi Mungu msimamo wa kweli ulioepukana na mazoea na kuiga, na ujue kuwa wewe baada ya kifo chako utarudi kwa Mola wako, na uitazame nafsi yako na anga inayokuzunguka, silimu utapata furaha katika dunia yako na Akhera yako, na ukitaka kuingia katika Uislamu hakuna jambo kubwa linalokulazimu zaidi tu ya wewe kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ujitenge mbali na yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na uamini kuwa Mwenyezi Mungu atawafufua walioko makaburini, na kuwahesabu na malipo nikweli yapo, ukishuhudia kwa ushahidi huu tayari utakuwa Muislamu, unalazimika baada ya hapo umuabudu Mwenyezi Mungu kwa yale aliyoyaweka kama sheria kama swala na zaka na kuhiji, ikiwa utapata uwezo wa kulifanya hilo.
Hivyo ninakuita ewe mwanadamu usimame kwaajili ya Mwenyezi Mungu msimamo wa kweli ulioepukana na kuiga na mazoea, kama alivyokuita Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa wakanushaji washindani, «Mimi ninawapa ushauri mmoja: msimame kumtii Mwenyezi Mungu wawili-wawili na mmoja-mmoja, kisha mfikirie kuhusu hali ya mwenzenu, Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kile alichonasibishwa nacho. Yeye hana wazimu. Hakuwa Yeye ispokuwa ni mwenye kuwatisha na kuwaonya adhabu ya Jahanamu kabla joto lake halijawasumbua.» [Sabai: 46]. Na unajua kuwa wewe baada ya kufa kwako utarudi kwa Mola wako, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kwamba binadamu hapewi malipo ispokuwa kwa kile alichokichuma yeye mwenyewe kwa juhudi zake." "Na kwamba amali yake itaonekana" "Kisha atalipwa malipo yaliyo kamili" "Na kwamba mwisho (wa kila jambo) unarejea kwa Mola wako" [An Najmi: 39-42]. Na utazame katika nafsi yako na katika ulimwengu unaokuzunguka, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Au kwani hawaangalii, hawa wakanushaji aya za Mwenyezi Mungu, kwenye ufalme wa Mwenyezi Mungu uliyo mkubwa na mamlaka Yake yenye uwezo wa kushinda, mbinguni na ardhini na chochote kile Alichokiumba Mwenyezi Mungu, zimetukuka sifa Zake, kwenye vitu viwili hivyo, wakalitia akilini hilo na wakalizingatia kwa akili zao na wakaangalia muda wa kikomo cha maisha yao ambao huenda ukawa umesogea karibu wakawa watakufa kwenye ukafiri wao na watakuwa kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake makali? Basi ni kitisho gani na onyo gani baada ya onyo la Qur’ani wataliamini na watalifanyia kazi? [Al A'raf: 185].
Basi silimu utapata furaha katika dunia yako na Akhera yako, na ukitaka kuingia katika Uislamu, hakuna jambo kuwa juu yako zaidi ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Na Muhammadi rehema na Amani zimfikie alipomtuma Mtume Mu'adhi kwenda Yemen kulingania katika uislamu alisema kumwambia: "Hakika wewe unawaendea watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), waite katika kushuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ikiwa wao watakutii katika hilo, wafahamishe kuwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka amewafaradhishia juu yao swala tano usiku na mchana, basi ikiwa kama watakutii katika hilo, wafahamishe kuwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka amewafaradhishia juu yao sadaka katika mali zao, zinachukuliwa kutoka kwa wale wenye uwezo katika wao na zinarejeshwa kwa mafukara wao, na ikiwa watakutii katika hilo, Tahadhari sana na mali zao za thamani" Kaipokea Muslim (19). Na ujiepushe na yale yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na kujiweka mbali na yale yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu ndio utakasifu ambao ndiyo mila ya Ibrahim Amani iwe juu yake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika imekuwa kwenu nyinyi ni kiigizo chema kwa Ibrahim na wale waliopamoja naye, pale waliposema kuwaambia watu wao; 'Hakika sisi tu tumejitenga mbali na yale mnayoyaabudu kinyume na Mwenyezi Mungu, tumekupingeni na umedhihiri kati yetu sisi na nyinyi uadui na chuki milele mpaka mumuamini Mwenyezi Mungu peke yake" [Al Mumtahna: 4]. Na uamini kuwa Mwenyezi Mungu atawafufua walioko makaburini, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hayo yaliyotangulia kutajwa, miongoni mwa alama za uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, ndani yake pana dalili ya kukata kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kutakasika, Ndiye Mola Mwenye kuabudiwa kwa haki Ambaye hakuna anayefaa kuabudiwa ispokuwa Yeye, na Yeye Ndiye Mwenye kuwahuisha wafu, na Yeye ni Muweza wa kila kitu. Na kwamba wakati wa ufufuzi ni wenye kuja, hilo halina shaka, na kwamba Mwenyezi Mungu Atawafufua wafu kutoka makaburini mwao ili Awahesabu na Awalipe. [Al Haji: 6-7]. Nakwamba hesabu na malipo ni kweli, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Mwenyezi Mungu Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, uadilifu na hekima , na ili kila nafsi ilipwe huko Akhera kwa ilichokitenda cha kheri au cha shari, na wao hawatadhulumiwa malipo ya matendo yao. [Al Jathiya: 22].
Utakaposhuhudia kwa ushahidi huu, tayari utakuwa Muislamu, utalazimika baada ya hapo kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa yale aliyoyaweka kama sheria, kama swala zaka na swaumu na Hija ikiwa utapata uwezo wa kuliendea hilo, na mengineyo.
Hii ni nakala ya tarehe: 19-11-1441
Ameiandika Ustadhi Doctor Muhammadi bin Abdallah Assuhaym
Mwalimu wa somo la itikadi katika kitengo cha masomo ya uislamu (zamani)
kitengo cha malezi katika chuo kikuu cha Mfalme Soud (Malik Soud)
Riyadh Mamlaka Ya Falme Za Kiarabu (Saudi Arabia).