Uwajibu wa kuzifanyia kazi Sunnah za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na ukafiri wa mwenye kuzikanusha (⮫)


  

 Uwajibu wa kuzifanyia kazi Sunnah za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na ukafiri wa mwenye kuzikanusha

وجوب العمل بسنة الرسول صلى الله عليه وسلم

وكفر من أنكرها

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu

   Utangulizi

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyoteNa mwisho mwema ni kwa wenye kumcha AllahSala na amani ziwe juu ya mja wake na mtume wake Mtume wetu Muhammad alietumwa akiwa ni rehma kwa ulimwengu wote na ni dalili za wazi kwa waja wake wote.na ziwe juu ya watu wake na maswahaba zake ambao walio beba kitabu cha mola wao Mtukufu, na Sunnah za Mtume wao Rehma na amani za Allah ziwe juu yake -kwa wale watakao kuja baada yao, kwa uaminifu wa hali ya juu na umakinifu na kwa kuhifadhi kuliko kamilika kwa maana zake na matamshi yake- Allah aliwaridhia na akawafanya watu wawaridhie na Allah atujalie katika wafuasi wao kwa wema.

   Baada ya hayo

Hakika wamekubaliana wanachuoni wa zamani na wazama hizi kwamba misingi inayo zingatiwa katika kuthibitisha hukumu na kubainisha halali na haramu ni kupitia katika kitabu cha Allah mwenye nguvu ambacho hakiingiliwi na batili mbele yake wala nyuma yake,Kisha Sunnah za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake- ambae hatamki kwa matamanio yake bali ni ufunuo anao funuliwa na Allah,Kisha ni kukubaliana kwa wanachuoni wa Ummah na wametofautiana wanachuoni katika misingi mingine ya muhimu, katika hiyo misingi ni Qiyas, Jamuhuri ya wana wa chuoni wamekubaliana kuwa Qiyasi ni Hoja pindi itakapo kamilisha masharti yake yenye kuzingatiwa,Na ushahidi wa misingi hiyo ni mingi mno:

   Misingi inayo zingatiwa katika kuthibitisha Hukumu

Msingi wa kwanza: Kitabu cha Mwenyezi Mungu mwenye nguvu

Ama Msingi wa kwanza: Kitabu cha Mwenyezi Mungu mwenye nguvu,

Maneno ya Mola wetu Mlezi mwenye nguvu katika mahala pengi katika kitabu chake juu ya wajibu wa kufuata Qur'an na kushikamana nacho na kusimama katika mipaka yake.

Anemsema Allah Mtukufu:

Fuateni mlio teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka

Na anemsema Allah Mtukufu:

Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni na mcheni Mungu, ili awarehemu

Na anemsema Allah Mtukufu:

Amekwisha kujieni Mtume wetu anae kufichulieni mengi mlio kuwa mkiyaficha katika Kitabu na anae samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha

Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka

Na anemsema Allah Mtukufu:

Kwa hakika wale walio kufuru ukumbusho ulipo wafikia na bila shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu.

Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hekima na msifiwa.

Na anemsema Allah Mtukufu:

Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kupitia hii nikuonyeni ninyi na kila inayo mfikia

Na anemsema Allah Mtukufu:

Hili ni tangazo liwafikie watu, liwaonye

Na aya katika maana hii ni nyingi na zimekuja hadithi sahihi kutoka kwa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake zenye kuamrisha juu ya wajibu wa kushikamana na Qur'an na kuungana katika kufuata kitabu hicho zikiwa ni zenye kuonyesha kwamba mwenye kushikamana na Quran atakuwa katika uongofu na mwenye kukiacha atakuwa katika upotevu.

Miongoni ni hadithi iliyo toka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, alisema katika hutuba yake katika hijja ya kuaga:

Hakika mimi nimekuachieni kitu ambacho hamta potea kamwe ikiwa mtashikamana nacho ni kitabu cha Allah

Imepokelewa na Imamu Muslim katika Sahihi yake

Na katika Sahihi Muslim pia kutoka kwa Zaidi Bin Arqam -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alisema:

Hakika mimi nimewaachia vizito viwili cha kwanza ni Kitabu cha Allah Mtukufu ndani yake kuna uongofu na nuru kichukueni kitabu cha Allah Mtukufu na shikamaneni nacho

Akahamasisha kukifuata Kitabu cha Allah na akapendekeza kifanyiwe kazi kisha akasema:

   Na watu wa nyumba yangu ninawakumbusheni muwape uangalizi kwa ajili ya Allah, ninawakumbusheni muwape uangalizi kwa ajili ya Allah

Na katika tamko lingine alisema katika Qur'an:

Qur'an ni kamba ya Allah mwenye kushikamana nayo atakuwa kwenye uongofu na mwenye kuiacha atakuwa kwenye upotevu

Na hadithi katika maana hii ni nyingi mnoNa katika ijimai ya wanachuoni miongoni mwa maswahaba na walio kuja baada ya maswahaba wamekubaliana juu ya wajibu wa kushikamana na kitabu cha Allah na kuhukumu kwa kitabu hicho na kuhukumiana kwa kitabu hicho pamoja na sunnah za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake. haya yanatosha haihitaji kurefusha katika kutaja dalili kuhusu jambo hili

Msingi wa pili: Ni yale yalio thibiti kwa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na maswahaba zake na walio kuja baada ya maswahaba wenye Elimu na Imani

Ama msingi wapili: katika msingi wa tatu ambao wanachuoni wamekubaliana nao, ni yale yaliyo swihi kwa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na Maswahaba wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na wale walio kuja baada yao miongoni mwa watu wa elimu na imani, wanaamini msingi huo na wanautolea hoja na kuwafundisha Ummah,Na hakika wametunga katika misingi hiyo vitabu vingiwakaweka wazi jambo hilo katika vitabu vya misingi ya kifiqihi na Istilahi,Na Dalili juu ya hilo hazihesabiki kwa wingi wake,Miongoni mwa dalili hizo ni yaliyo kuja katika kitabu cha Allah mwenye nguvu akiamrisha wanadamu wamfuate na kumtii,na amri hizo walikuwa wakiambiwa watu wa zama za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na watakao kuja baada yake kwa sababu yeye ni Mtume kwa watu wote,Na kwa sababu wameamrishwa kumfuata na kumtii yeye mpaka kitakapo simama Qiyama,Na kwa sababu yeye Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ndie anae tafsiri Qur'an na ndie mwenye kubainisha yale yote yenye yasio julikana utekelezaji wake kwa kauli yake na vitendo vyake na kwa kukiri,Na lau sio Sunnah waislam wasingelijua idadi ya rakaa za swala na namna ya kuswali na mambo ya wajibu katika swala,na wasingelijua upambanuzi wa hukumu za funga, zakah, hijjah, jihadi na kuamrisha mema na kukataza mabayana wasingelijua ufafanuzi wa hukumu za muamalati na yalio haramishwa na mipaka aliyo weka Allah na adhabu

   katika aya zilizo kuja katika hayo

katika aya zilizo kuja katika kueleza hayo ni kauli ya Allah katika surat Al Imran:

Na mtiini Allah na Mtume wake ili mpate kurehemewa

Na kauli ya Allah katika surat An-Nisaai:

Enyi mlio amini! mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndio bora zaidi na ndio yenye mwisho mwema

Na amesema Allah katika surat An-Nisaai pia:

Mwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Mwenyezi Mungu. Na anae kengeuka, basi sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao

Na vipi imewezekana kumtii yeye na kuyarudisha yale walio zozana watu ndani yake kuyarudisha kwa Allah na Sunnah za Mtume wake ikiwa Sunna zake hazichukuliwi kuwa ni hoja au ikiwa hazikuhifadhiwa,Na kwa kauli hii ikiwa ni kweli wanavyo dai atakuwa Allah amewaeleza watu warudi katika jambo ambalo halipoNa kusema hivyo ni batili kubwa na ni kumkufuru Allah ukafiri mkubwa na nikumdhania Allah dhana mbaya

Na amesema Allah mwenye nguvu alie tukuka katika surat An-Hah'l:

Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.

Na amesema pia:

Na hatukukuteremshia Kitabu isipo kuwa uwabainishie yale ambayo wanakhitalifiana, kiwe Uwongofu na Rehema kwa watu wanao amini.

Vipi Allah Mtukufu aegemezee kwa Mtume wake Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kubainisha yale aliyo teremsha kwake ikiwa Sunnah zake hazipo wala sio hoja?

Na mfano wa hayo ni kauli ya Allah Mtukufu katika surat An-Nur:

Sema: mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume. Na mkigeuka, basi yaliyo juu yake ni aliyo bebeshwa, na yaliyo juu yenu ni mliyo bebshwa nyinyi. Na mkimtii yeye mtaongoka. Na hapana juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe wazi wazi.

Na amesema Allah Mtukufu katika sura hiyo hiyo:

Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Mtume, ili mpate kurehemewa.

Na amesema katika suratu Al-A'raaf:

Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye anaye huisha na anaye fisha. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.

Na katika aya hizi kuna dalili za wazi juu ya kwamba uongofu na rehma ni katika kumfuata mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, sasa itakuwaje hivyo bila kufanyia kazi Sunnah zake au pamoja na kusema kuwa haziswihi au hazipo kabisa,

Na amesema Allah mwenye nguvu alie tukuka katika surat An-Nuur:

Basi nawatahadhari wanao halifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.

Na amesema katika suratu Al-Hashir:

Na yale aliyo kuleteeni Mtume basi yachukueni na yale alio kukatazeni yaepukeni

Na aya katika maana hii ninyingi na zote zinaonyesha juu ya uwajibu wa kumtii Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na kufuata yale alio kuja nayo kama zilivyo tangulia dalili zinazo onyesha uwajibu wa kufuata kitabu cha Allah na kushikamana nazo na kutii amri zake na kujiepusha na makatazo yake,Nayo ni misingi miwili inayo lazimiana mwenye kukanusha moja katika misingi hiyo atakuwa amekanusha na wapili na kuukadhibisha, kufanya hivyo atakuwa amekufuru na kufanya upotevu na anatoka katika uislam kwa ijmai ya wanachuoni na Imani.

Na katika hadithi zilizo pokelewa kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake

Na zimekuja hadithi sahihi zenye daraja ya usahihi wa hali ya juu kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake juu ya wajibu wa kumtii Mtume na kufuata yale aliyo kuja nayo na uharamu wa kumuasi na hilo ni kwa yule alie ishi katika zama zake na yule atakae kuja baada ya yeye kuondoka mpaka siku ya Qiyama,Miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi iliyo thibiti katika sahihi mbili ya Imamu Bukhari na Muslim kutokana na hadithi ya Abii Hurayra radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alisema:

Mwenye kunitii atakuwa amemtii Mwenyezi Mungu na atakae niasi atakuwa amemuasi Mwenyezi Mungu

Na katika Sahihi Al-Bukhari pia kutoka kwa Abuu Hurara Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alisema:

Umma wangu wote utaingia peponi ispokua atakae kataa, akaulizwa ewe Mtume ni nani atakae kataa? akajibu mwenye kunitii ataingia peponi na mwenye kuniasi atakuwa amekataa

Na ametoa Imamu Ahmad na Abudawood na Al-Ha'kim kwa upokezi ulio sahihi kutoka kwa Al-Miqdad Bin Ma'ad Krbi kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake hakika alisema:

Fahamuni hakika mimi nimepewa Qur' ani na mfano wake pamoja, haogopi kuingia katika maangamio mmoja wenu baada ya kushiba akaketi kwenye kiti chake kisha akasema: Shikamaneni na Qur'an peke yake yale mliyo yakuta ni ya halali basi yahalalisheni, na yale mliyo yakuta ni ya haramu basi yaharamisheni

Na ametoa Imamu Abudawood na Ibn Majah kwa upokezi sahihi: kutoka kwa Ibn Abii Ra'afy kutoka kwa baba yake kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alisema:

Asiitakidi mmoja wenu akiwa amekaa kwenye kiti chake yanamjia maamrisho yangu na yale niliyo yakataza kisha akasema: sisi hatuyajui,yale tuliyo yakuta katika kitabu cha Allah tutayafanyia kazi

Na kutoka kwa Alhasan Bin Jaabir alisema: nilimsikia Miqdan Bin Maady Karb Radhi za Allah ziwe juu yake akisema:

Aliharamisha Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake siku ya Khaybar vitu vingi kisha akasema: Anakaribia Mmoja wenu kunikadhibisha nae akiwa amekaa kwenye kiti chake, anaelezea hadithi yangu kisha anakataa kuisadikisha kwa kusema baina yetu na baina yenu kuna Kitabu cha Allah yale tuliyo yakuta ndani yake katika mambo ya halali tuta yahalalisha, nayale tuliyo yakuta katika ya haramu tutayaharamisha, juweni kuwa yale aliyo yaharamisha Mtume nikama yale aliyo yaharamisha Mwenyezi Mungu

Ameitoa hadithi hii Imamu Al-Hakim na At-Tirmidhy, na Ibn Majah. kwa upokezi sahihi.

na zimekuja hadithi sahihi zenye daraja ya usahihi wa hali ya juu kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwamba yeye alikuwa anawahusia maswahaba wake katika hutuba yake kwamba alie hudhuria awafikishie ambao hawakuhudhuria, na alikuwa akiwambia: huwenda alie fikishiwa ni mwerevu kuliko alie sikia

Na hadithi hiyo imekuja katika sahihi mbili ya Imamu Al-Bukhary na Muslim hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake pindi alipo hutubiya watu katika hija yake ya kuaga katika siku ya Arafa na katika siku ya kuvhinja aliwambia:

Alie hudhuria amfikishie ambae haja hudhuria, huwenda alie fikishiwa ni mwerevu kuliko alie sikia

Laiti sunah zake zisingekuwa ni hoja kwa yule alie sikia na yule alie fikishiwa, na laiti zisingekuwa zitabaki mpaka siku ya Qiyama asinge waamrisha maswahaba zake kufikisha, ikajulikana hilo kuwa kila mwenye kusikia maneno ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake au yakamfikiya maneno yake kwa upokezi sahihi, basi ni hoja kwake.

Na walihifadhi maswahaba wa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake Sunnah zake za maneno yake na vitendo na wakawafikishia walio kuja baada yao katika mataabi kisha walio wafuata mataabi baada yao,Hivyo hivyo walinukuu wanachuoni wanao aminika kizazi kwa kizazi na karne baada ya karne,Na wakazikusanya katika vitabu vyao na wakaziweka wazi zilizo sahihi na zenye udhaifu,Na wakaweka ili kuzijua misingi ambayo inayojulikana baina yao ambayo itawaongoza kujua sunnah sahihi na dhaifu,Hakika wanachuoni wamevisoma vitabu sahihi na vitabu vingine na wakavihifadhi kuhifadhi kuliko kamilika kama alivyo hifadhi Allah mtukufu kitabu cha Qur'an tukufu kutokana na mchezo wa watu wapuuzi na watu wenye kukanusha kuwepo kwa Allah mmoja, pia akakihifadhi kutokana na wapotoshaji watu wa batili kwa kutimiza maneno ya Allah Mtukufu alipo sema:

   Hakika sisi tuliiteremsha Qur'an na hakika sisi tutaihifadhi

Na hapana shaka kwamba Sunnah za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni ufunuo ulio teremshwa,Allah Mtukufu alihifadhi Sunnah kama alivyo ihifadhi Qur'an na akaiwekea sunnah wanachuoni walio makini kwenye Sunnah, ambao walio kanusha kila upotoshaji wa watu wa batili na kugeuza maandishi ya Sunnah ya watu wajinga na hao wanachuoni wakawa wanaondoa kila uchafu ulio ambatana na sunnah ambao ulio wekwa na wajinga wanao kadhibisha na wakanushaji,Kwasababu Allah Mtukufu aliifanya Sunnah iwe ni tafsiri ya kitabu chake kitukufu na ni ubainifu kwa yale yalio tajwa kwa jumla bila kubainishwa miongoni mwa hukumu zikaja katika sunnah hukumu ambazo hazikutajwa katika Qur'an Tukufu, kama vile kubainisha hukumu za kunyonya kwa mtoto, na baadhi ya hukumu za Mirathi, na uharamu wa mwanaume kukusanya mke na shangazi yake pamoja na mke na mama yake mdogo au mkubwa na mengineyo miongoni mwa hukumu ambazo zilizo kuja katika Sunnah zilizo sahihi ambazo hazikutajwa katika Qur'an tukufu.

Miongoni mwa yalio pokelewa kutoka kwa maswahaba na walio kuja baada ya maswahaba katika wanachuoni

Ametaja baadhi ya yaliyo pokelewa kutoka kwa maswahaba na walio kuja baada ya mswahaba miongoni mwa wanachuoni katika kutukuza Sunnah na uwajibu wa kuifanyia kazi

kutoka katika sahihi mbili kutoka kwa Abuu Hurayra-Radhi za Allah ziwe juu yake- alisema:

Alipo kufa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, wakaritadi walio ritadi katika warabu, alisema Abubakari Swidiq Rdhi za Allah ziwe juu yake:

Nina apa kwa jina la Alah nitampiga vita yeyote mwenye kutofautisha baina ya swala na zaka

Omar radhi ya za Allah ziwe juu yake akamwambia

Vipi utawapiga vita haliyakuwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake amesema:

Nimeamrishwa niwapige vita watu mpaka waseme La ilahaila Allah (Hapana mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allah mmoja) pindi watakapo sema watasalimika na mimi damu zao na mali zao, ila kwa haki yake. yaani pindi watakapo fanya makosa yanayo wawajibisha kuuliwa au kuchukuliwa mali zao vinginevyo watabaki kuwa salama.

Akasema Abubakari Swidiiq:

Je, zaka sio katika haki ya mali?! nina apa kwa Allah wakikataa kulipa ngamia mmoja wa zaka ambao walikuwa wakitoa wakati wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake nitawapiga vita kwa kukataa kutoa zaka.

Omar radhi ya za Allah ziwe juu yake akasema:Kisha punde nikajua kuwa Allah amekifungua kifua cha Abubakari kwa kuwapiga vita walio ritadi ndio nikajua kuwa yuko kwenye haki,Na maswahaba radhi za Alla ziwe juu yake walimuunga mkono juu ya hilo wakawapiga vita walio ritadi mpaka wakawarudisha kwenye uislam, na wakaendelea kupigwa vita walio endelea katika kuritadi,Na katika kisa hiki kuna dalili ya wazi juu ya kuitukuza Sunnah na wajibu wa kuifanyia kazi,Alikuja Bibi kwa Abubakari Swidiq Raadhi za Allah ziwe juu yake akimuuliza kuhusu mirathi yake, akamjibu:Hakuna katika kitabu cha Allah chochote na wala sijuwi kuwa Mtume-Rehma na amani za Allah ziwe juu yake- alihukumu kuhusu bibi chochote, kisha akawauliza maswahaba, wakatoa wengine ushahidi kuwa Mtume-Rehma na amani za Allah ziwe juu yake- alimpa bibi sudus (moja ya sita 1/6) basi akahukumu kwamba bibi apewe sudusi ya mali ya marehemu,Na akujua Omar- radhi za Allah ziwe juu yake- anawahusia wafanyakazi wake wahukumu baina ya watu kwa kitabu cha Allah, na kama hawakupata hukumu yoyote basi wahukumu kwa sunnah za Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeNa wakati ilipo mpa shida hukumu ya mwanamke alie poromosha mimba kwa sababu ya kushambuliwa na mtu aliwauliza maswahaba -radhi za Allah ziwe juu yao- kuhusu hukumu hiyo, akatoa ushahidi swahaba Muhamad Bin Maslama na Mughira Bin Sh'ubah -Radhi za Allah ziwe juu yao- kwamba Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alihukumu katika jambo hilo aliefanya kosa hilo atatoa Mtumwa au Mjakazi mdogo alie salimika na aibu zote. Omar -radhi za Alla ziwe juu yake- akahukumu hivyo.

Na pindi ilipo mtatiza Othmani Bin Afan- Radhi za Alla ziwe juu yake- hukumu ya mwanamke kukaa eda ya kufiwa nyumbani kwa mume baada ya kufiwa na mume wake, Fariah Bint Maliki Bin Sinani dada yake na Abi Sai'id- radhi za Alla ziwe juu yake- alimwambia Othmani kuwa: Hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alimuamrisha akae nyumbani kwa mume wake mpaka amalize eda yake, Othman akahukumu hivyo. radhi za Allah ziwe juu yake

vile vile alihukumu kwa Sunnah katika kusimamisha adhabu ya kunywa pombe kwa Waliid Bin UkbahHabari ilipo mfikia Aly Bin Abii Bi Abii Twalib -radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Othmani anawakataza watu kuhiji kwa Tmatu'u, alihirimia Hija na Umra pamoja (Tmatuu)Na akasema: siachi sunnah Sunnah kwa kufuata kauli ya mtuWatu walipo mtolea hoja Abdilahi Bin Abasi kuhusu kuhiji hija ya Tmatuu wakisema Abubakar na Omar- radhi za Allah ziwe juu yao- wakipendekeza kwamba watu wahiji Ifradi (ambayo ni kuhirimia hija peke yake na kuja kufanya Umra wakati mwingine bila kukusanya hija na Umra katika safari moja) aliwajibu Ibn Abasi kwa kusema:Inahofiwa kushukiwa na mawe kutoka mbinguni nina wambia Alisema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake na nyie mnasema alisema Abubakar na Omar.Ikiwa mwenye kukhalifu Sunnah kwa kufuata maneno ya Abubakari na Omar anahofiwa kuteremkiwa na adhabu, itakuwaje kwa mwenye kukhalifu sunnah kwa kufuata maneno ya watu wengine! au kwasababu ya ijitihada za wanachuoni!,baadhi ya watu walipo zozana na Abdillahi Bin Omar -radhi za Allah ziwe juu yake-katika baadhi ya sunnah Abdillah Bin Omar aliwambia: Je, sisi tumeamrishwa kufuata maneno ya Omar au maneno ya Mtume (Sunnah)?

Na mtu alipo mwambia Imrani Bin Huswayni- radhi za Allah ziwe juu yake- : tuelezee kuhusu kitabu cha Allah na yeye alikuwa akiwaelezea kuhusu Sunnah, alikasirika Imran na akasema: Hakika sunnah ndio tafsiri ya Qur'an, na laiti isingekuwa sunnah tusingejua kuwa Adhuhuri ina rakaa nne, na Magharibi ina rakaa tatu, na Alfajiri ina rakaa mbili, na tusingelijua ufafanizi wa hukumu za zaka na mengineyo katika hukumu ambazo zilizo kuja katika Sunnah katika kuchambua Hukumu,

na Athari kutoka kwa maswahaba-radhi za Allah ziwe juu yao -katika kuitukuza sunnah na wajibu wa kuzifanyia kazi, na kutahadharisha kuzikhalifu sunnah ni nyingi sana,Na katika athari hizo hakika Abdillah Bin Omar -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- alipo zungumzia kauli ya mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yakeMsiwaziwilie vijakazi vya Allah kuingia katika Misikiti ya Allahwalisema baadhi ya watoto wake: nina apa kwa jina la Allah tutawaziwia Abdillah akamkasirikia mtoto wake na akamkemea makemeo makali na akasema: nina wambia alisema Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na wewe unasema tutawaziwia,Na alipo ona Abdillah Bin Mughafal Al-Muzani -radhi za Allah ziwe juu yake- na yeye ni katika maswahaba wa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake baadhi ya watu wake wa karibu wanatupa mawe kuwindwa aliwakataza kufanya hivyoKisha akamwambia: hakika Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yakeAlikataza kurusha mawe akasema: hakika hawindi mmoja wenu kuwindwa wala kumjeruhi adui lakini anamvunja jino na kumtoboa machoKisha baada ya kuwakataza alimuona mmoja wao akirusha mawe akiwa anawinda akamwambia: nina apa kwa Allah sinta kuongelesha kamwe nimekwambia Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake alikataza kuwinda kwa kurusha mawe porini kisha unarudia kufanya hivyo?

   Na ametoa Imamu Albayhaqy kutoka kwa Ayubu As-Sakhtayany Taabiy Mtukufu kwamba alisema:

Pindi atakapo ambiwa mtu kuhusu Sunnah kisha akasema: achana na Sunnah, tueleze kuhusu Qur'an basi tambua kuwa mtu huyo amepotea,

Na amesema Imamu Al-Awzaaiy-Allah amrehemu-: Sunnah inaisherehesha na kuitafsiri Qur'an au kuiwekea mipaka yale ambayo hayajawekewa mipaka au kuweka wazi Hukumu ambazo hazikutajwa katika Qur'an kama alivyo eleza Allah Mtukufu:

Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.

Na imetangulia kauli ya mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake

Fahamuni hakika mimi nimepewa Qur'an na Mfano wake pamoja

Na ametoa Imamu Albayhaqy kutoka kwa Amir Ash-Shaby -Allah amrehemu- kwamba alisema kuwambia baadhi ya watu:Sio sababu nyingine bali mmeangamia wa kuacha kwenu athariYaani kwa sababu ya kuacha hadithi sahihi,Na ametoa Imamu Albayhaqy kutoka kwa Auzaiy -Allah amrehemu- hakika alisema kuwambia baadhi ya jamaa zake: ukifikiwa kutoka kwa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, hadithi yoyote ole wako useme kinyume na hadithi ya mtume kwa sababu mtume wa Allah alikuwa ni mfikishaji kutoka kwa Allah mtukufu.

Na ametoa Imamu Albayhaqy kutoka kwa Auzaiy -Allah amrehemu- hakika alisema kuwambia baadhi ya jamaa zake: ukifikiwa kutoka kwa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, hadithi yoyote ole wako useme kinyume na hadithi ya mtume kwa sababu mtume wa Allah alikuwa ni mfikishaji kutoka kwa Allah mtukufu.

Na ametoa Imamu Albayhaqy kutoka kwa Imamu Mtukufu Sufiyani Bin Sa'ad Athawriy- Allah amrehemu- kwamba alisema: hakika elimu yote ni elimu ya hadithi,

Alisema Maliki -Allah amrehemu-: hakuna yeyote miongoni mwake ila kauli yake inarejeshwa, ila bwana wa kaburi hili akiashiria kaburi la mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake

Alisema Imamu Abuu Hanifah, Allah amrehemu:

Itakapo kuja Hadithi kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, ni juu yetu kufuata kwa kichwa na macho

Na amesema Imamu Shafy, Allah amrehemu:

Wakati wowote nitakapo pokea hadithi sahihi kutoka kwa mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake, kisha sikuifanyia kazi, basi nakuapieni kwa Alla mimi nitakuwa sina akili

Na amesema Imamu Shafy, Allah amrehemu pia:

Nitakapo sema kauli yoyote kisha ikaja hadithi kutoka kwa Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake tofauti na vile nilivyo sema, ipigeni kauli yangu ukutani,

Na alisema Imamu Ahmad Bin Hambal -Allah amrehemu- kuwambia baadhi ya watu wake wa karibu:

Usiniige wala kumuiga Imamu Maliki wala Shafy bali chukuwa kutoka katika vyanzo tulivyo chukua,

Na amesema Imamu Ahmad Allah amrehemu pia:

Nimeshangazwa na watu ambao walio jua upokezi na usahihi wake kutoka kwa Mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake kisha wanaenda kwa Imamu Sufiyani, ili hali Allah mtukufu anasema:

Basi nawatahadharisha wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.

   Je, Unajuwa nini maana ya Fitina?

Fitina maana yake ni Shirki huwenda akipinga baadhi ya maneno ya mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake ikaingia katika moyo wake shaka ikawa ni sababu ya kuangamia.

Na ametoa Imamu Albayhaqy kutoka kwa Mujahid Bin Jabar Tabiy kwamba alisema katika kauli yake Allah Mtukufu:

Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume

Alisema: kurudi kwa Allah ni kurudi katika kitabu chake, na kurudi kwa mtume ni kurudi kwenye Sunnah,

Na ametoa Imamu Albayhaqy kutoka kwa Zuhry-Allah amrehenu- kwamba alisema:

Walikua miongoni mwa walio pita katika wanachuoni wetu wanasema: kushikamana na sunnah ni uokovu,

Na alisema Muwafaqudini Bin Qudamah -Allah amrehemu- katika kitabu chake Raudhwatu Annadhira: katika kubainisha misingi na hukumu mbalimbali,

Na msingi wa pili katika dalili ni sunnah za mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na kauli ya mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni hoja kwa sababu ya kupatikana miujiza ya kweli kutoka kwake, na Allah Mtukufu aliamrisha watu wamtii, na alitahadharisha watu wasimuasi.

   Yamekwisha maneno yalio kusudiwa kusemwa

Na amesema Alhafidh Bin Kathir-Allah amehemu- katika tafsiri ya kauli ya Allah mtukufu:

Basi nawatahadharisha wanao halifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.

Yaani amri ya mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake, nayo ni njia yake na mfumo wake, sunnah zake, sheria yake, maneno na vitendo vinapimwa yale yaliyo afikiana na matendo ya mtume yatakubaliwa, na yale yaliyo pingana basi hayo yatarejeshwa kwa aliye yasema na kutenda vyovyote atakavyo kuwa,

Kama ilivyo thibiti katika sahihi mbili na vitabu vingine kutoka kwa mtume wa Allah rehma na amani za Allah ziwe juu yake alisema:

Yeyote atakae fanya ibada ambayo haipo katika dini yetu basi atarejeshewa

yaani mwanadamu aogope na ajitahadhari mwenye kuhalifu sheria ya mtume ndani ya moyo na nje:

Kupatwa na fitina

Yaani katika nyoyo zao kutokana na Ukafiri Unafiki au Bida'a

Au kupatwa na adhabu kali

Yaani katika dunia kwa adhabu ya kuuliwa au kutekelezewa adhabu ya Allah (Haddi), au kufungwa na mfano wake

Kama alivyo pokea Imamu Ahmad alituhadithia Abdurazaq alituhadithia Miimar kutoka kwa Humam Bin Munabah alisema:

Haya ndio aliyo tuelezea Abuu Hurayrah, akisema:

Alisema Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake:

Mfano wangu na mfano wenu, ni kama mfano wa mtu aliye washa moto na ulipo waka wakawa vipepeo na vidudu wanaangukia katika moto na kuna wadudu wengine wana waziwia wenzio ila wale wanao angakuia katika moto wana washinda nguvu, akasema mtume: huo ndio mfano wangu kwenu, mimi nawaziwia msiingie katika moto lakini mnanishinda nguvu kisha mnaingia motoni

Wameitoa hadithi hii Bukhari na Muslim katika hadithi ya Abdu Razaaq

Na amesema Assuyutwiy-Allah amrehemu- katika risala yake inayo itwa: (Miftahul jannah fil ihtijaji bi Sunnati):

Jueni -Allah awa rehemu- kwamba yeyote mwenye kukanusha kuwa Hadithi ya Mtume Rehma na amani za Allah ziwe juu yake sawa ikiwa ni kauli au kitendo kulingana na sharti zake zinazo julikana katika misingi yake, akakanusha kuwa sio hoja hukumu ya mtu huyu atakuwa amekufuru na kutoka katika Uislamu na atafufuliwa pamoja na Mayahudi na Manaswara au pamoja na wale atakao wataka Allah katika kikafiri

   Yameisha maneno yalio kusudiwa kusemwa

Na athari kutoka kwa maswahaba na Matabii-radhi za Allah ziwe juu yao -katika kuzitukuza sunnah na wajibu wa kuzifanyia kazi, na kutahadharisha kuzihalifu sunnah ni nyingi sana,

Ninatarajia ziwe katika maneno tuliyo yasema katika aya na hadithi na athari ni zenye kutosheleza na kukinaisha kwa kila mwenye kutafuta haki

na tunamuomba Allah Mtukufu na waislam wote atuafikishe kufanya yale anayo yapenda na kuyaridhia na atusalimishe na kufanya yale yanayo mkasirisha,Na atuongoze wote katika njia yake iliyo nyooka hakika yeye ni msikivu na yuko karibu.

Na atuongoze wote katika njia yake iliyo nyooka hakika yeye ni msikivu na yuko karibu.

Na swala na amani za Allah Mtukufu ziwe juu ya mja wake na mtume wake, mtume wetu Muhammad na ziwe juu ya watu wake na maswahaba zake na wafuasi wake kwa wema.

Abdul Aziz Bin Abdillah Bin Baz

Allah amrehemu