KINGA YA MUISLAM ()

Mada hii inazunguzia namna ya kujikinga kutokana na shetani na hatari ya kujikikinga kwa asiyekua Allah.

|

بسم الله الرحمن الرحيم

 KINGA YA MUISLAM

Imeandaliwa na Yunus kanuni ngenda.

Imwpitiwa na Abubakari shabani.

Muislam anatakiwa kujikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa, pamoja na maadui mbalimbali kupitia njia sahihi alizozifundisha Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na hiyo ndiyo hirizi iliyo madhubuti.

ANASEMA MTUME (S.A.W):-

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال:

(من قال: لا إله إلا الله وحده لا شريك له له الملك و له الحمد و هو على كل شيء قدير في اليوم مئة مرة كانت له عدل عشر رقاب و كتبت له مئة حسنة و محيت عنه مئة سيئة و كانت له حرزا من الشيطان يومه ذلك حتى يمسي و لم يأت أحد بأفضل مما جاء به إلا أحد عمل أكثر من ذلك). رواه البخاري و مسلم. Kutoka kwa Abiy Hurayra radhi za Allah zimuendee: ya kwamba Mtume (s.a.w) anasema: (Mwenye kusema:

 LAA ILLAHA ILA LLAHU WAHDAHU LAA SHARIKA LAHU LAHUL MULKU WA LAHUL HAMDU WA HUWA ALAA KULI SHAY-IN QADIIR!

Kwa siku mara mia moja, huandikiwa mtu huyo thawabu za sawa na kuacha huru watumwa kumi, na huandikiwa mema mia moja, na hufutiwa madhambi mia moja, na atakua na (hirizi) kinga kutokana na shetani siku hiyo mpaka jioni, na hatoleta mtu yeyote kilicho bora kuliko alicholeta yeye, (yaani maneno hayo) ila akifanya zaidi ya hapo, (akizidisha).

Ameipokea Bukhar na Muslim.

Ndugu katika imani hii ni bahati iliyoje katika huu ummat Muhammad (s.a.w)?

Allah anatupenda sana hakutuacha ovyo! bali ametuelekeza na kutubainishia kupitia kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w) kila lenye manufaa na sisi na namna ya kuliendea, na kila lenye shari na sisi ametubainishia jinsi ya kuliepuka!. 

Chakushangaza kuna baadhi ya watu wameacha kinga sahihi ya Allah (S.w) na kufuata mambo ya kishirikina wanakwenda kwa waganga wa kienyeji basi huko hupewa karatasi zenye maandishi ya rangi nyekundu kisha huzining'iniza katika milango wakiwa na imani kwamba ndio kinga kwao.

Na wengine hupewa mizigo (vitu vya ajabu) wakaambiwa wavichimbie na kuvifukia katika kona za nyumba zao kwa imani kua ni kinga kwa familia nzima,

 INNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHI RAJIUN!!!!! Huu ni msiba wa hali ya juu na ni haram katika sheria ya kiislam.

TAMBIIH (UZINDUO) Tunawausia wanaofanya shirki (ushirikina) kuyaacha mambo hayo na kufanya Toba haraka, kwani umauti unakuja ghafla, na mtu akifa hali ya kuwa ni mshirikina Allah (S.w) hamsamehe mtu kama huyo. ALLAH ANASEMA:- ((إن الله لا يغفر أن يشرك به و يغفر ما دون ذلك لمن يشاء و من يشرك بالله فقد افترى إثما عظيما)) سورة النساء: ٤٨ Hakika Allah hamsamehe mwenye kumshirikisha na anasamehe mengine yasikua hayo (ya shirki) kwa yule amtakae na anaemshirikisha Allah basi hakika amezua dhambi kubwa. Surat Nisaa aya ya 48. Tunamuomba Allah atuepushe na shirki na atujaalie mwisho mwema. Ameen!!!!