Utunzi wa kielimu

  • PDF

    Haki za muislamu: Hakika muislamu anazo haki juu ya muislamu mwenzake, haki zilizo bainishwa na sheria, na makala hii inakumbusha haki hizo, yafaa kwa kila muislamu azikumbatie.

  • MP3

    Muislamu juu ya muislamu mwenzake, mada ya audio inazungumzia mambo matano kwa njia safi kabisa, kwa muda wa dk 15. 1: Mtapo kutana toleaneni salam. 2: Atakapo kuita muitike. 3: Atakapo kutaka nasaha mnasihi. 4: Atakapo umwa kamuone. 5: Atakapo kufa kamzike.

  • PDF

    Kutoka kwa Abihuraira (r.a), amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita, pakaulizwa nizipi hizo ewe mtume wa Allah? akasema: Utapo kutana nae msalimie, na atapo kuita muitike, na atapo kutaka nasaha mnasihi, na atapo toa chafya akamshukuru Allah muombee dua, na atapo umwa mtembelee, na atapo fariki kamzike. Hizi ndio haki zamsingi zilizo wekwa na uislamu kwa wafuasi wake, ili waja wa Allah wawe ndugu, makala hii imeelezea kwa ufupi haki hizi na namna ya kuzifanyia kazi katika maisha ya kila siku.

Ukurasa : 1 - Kutoka : 1
Maoni yako muhimu kwetu