ADABU ZA KULA ()

Yasini Twaha Hassani

Mada hii inazunguzia adabu na dua ya kula

  |

  بسم الله الرحمن الرحيم

  BISMI LLAHI RRAH MANI RRAHIIM

  Utangulizi

  Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia Rehma na amani Nabii Muhammad (s.a.w) pamoja na familia yake na Maswahaba zake na Waislamu wote watakao fuata mwenendo wake mpaka siku ya mwisho tuna muomba Mwenyezi Mungu atujaalie nasi tuwe miongoni mwahao Aamiin.

  Kutoka kwa AbaHuraira (ﷺ‬.a) amesema: Amesema Mtume Muhammad (s.a.w): (Hakika jambo la kwanza atakalo ulizwa mja siku ya kiyama miongoni mwa neema, ataambiwa: Jee! Sijakupa afya njema na kukunywesha maji ya baridi?). kapokea hadithi hii Imam Tirmidhi.

  MIONGONI MWA ADABU ZA KULA:

  1: Kutaja jina la Mwenyezi Mungu Mwanzo wa kula kwako. Kutoka kwa Bibi Aisha (ﷺ‬.a) kwamba Mtume (s.a.w) amesema: (atapo kula Mmoja wenu ataje jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu, akisahau kutaja jina la Mwenyezi Mungu Mwanzo wa kula, asema: kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake). Kapokea hadithi hii Imam Tirmidhi, na Ahmad, na Daramy.

  2: kusema Bismi llahi, ni kila mtu, sio kwamba akisema Mmoja anawatosheleza wengine anao kula nao, kwa sababu Sunna hii niya kila mtu inatakiwa aiseme, wala usiifananishe na Salamu, Hadithi ya Amru bin Salama (ﷺ‬.a) wakati aliambiwa na Mtume (s.a.w): (Ewe kijana! Sema: Bismillahi, na ule kwa mkono wako wa kulia, na ule mbele yako).

  3: NAMNA YA KUSEMA BISMILLAHI WAKATI WA KULA NA KUNYWA: Aseme: Bismillah, wala asizidishe Arrahmani rrahiim. Laity akisema: Bismillahi Rrahmani Rrahiim, atakuwa kenda kinyume na Sunna.

  Kwa hakika limepokelewa tamko la wazi la (Bismillah) katika hadithi alio ipokea Imam Abii Daud na Tirmidhi, na kaisahihisha Shekh Albani (ﷺ‬.h) kwa hadithi ya Bibi Aisha (ﷺ‬.a) amesema: amesema Mtume (s.a.w): (Atapo kula Mmoja wenu chakula, na aseme: Bismillah). Na katika hadithi nyingine, kutoka kwa Amru (ﷺ‬.a) amesema: nilikuwa kijana mdogo katika malezi ya Mtume (s.a.w) mkono wangu ulikuwa hautulii kwenye sahani ya chakula, akaniambia Mtume (s.a.w): (Ewe kijana! Utakapo anza kula, useme: Bismillah).

  Kapokea hadithi hii Imam Twabarani, na akasema Shekh Albani upokezi wake ni sahihi, kwa sharti za Imam Bukhari na Muslim, zingatia hili kwa sababu ni muhimu sana kwa wale wanao tukuza Sunna, na wala hawakubali kuzidisha zaidi ya Bismillah. Angalia Irwail-Ghaliil, (3/31).

  Kwa haya machache tuna muomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuyafanyie kazi haya na mengine Inshaallah!.

  Ewe Mola wetu zipeleke Rehma na Amani kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) pamoja Familia yake na Maswahaba haze na Waislamu wote hadi siku ya mwisho. Aamiin.