AQIDATUL-WASITWYYAH ()

Ahmed bin Abdul Halim bin Taymiyyah

 

Kitabu hiki kinazunguzia mas’ala ya Aqidah (Tawhid)

|

 al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah

(Rahimahu Allaah)

Mfasiri:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Kimepitiwa Na:

Abu Bilaal ´Uthmaan Nu´umaan

Tafsiri ya kitabu:

al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah

Mwandishi:

Shaykh-ul-Islaaam Ibn Taymiyyah

Chapa ya kwanza:

Nakala 500

Kimefasiriwa na:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Kimepitiwa na:

Abu Bilaal ´Uthmaan Nu´umaan

Wachapishaji wa kitabu:

- Kina mama wa Denmark

- Faatwimah bint Khaliyfah bin Muhammad

Haki Zote Zimehifadhi. Hairuhusiwi Kupiga Chapa Kitabu Hiki Kwa Jinsi Yoyote Ile Bila Idhini Ya Mfasiri

 Utangulizi wa mpitiaji

Himidi ni zake yeye Allaah (وتعالى سبحانه). Mwingi wa Rehmah mwenye kurehemu. Swalah na salaam zimfikishie mbora wa viumbe, Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), ahli zake, Maswahabah wake na kila mwenye kufuata mienendo yao. Amma ba´ad:

Hakika hiki ni kitabu kilichoandikwa kwa ufupi kubainisha I´tiqaad sahihi ya Al-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, kiitwacho “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” alichokiandika Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin ´Abdil-Haliym bin ´Abdis-Salaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) alokufa mwaka 728 H.

Sababu ya kuandika kitabu hichi, alimjilia bwana mmoja alokuwa Qaadhiy katika mji wa Waasitw akamshtakia Shaykh-ul-Islaam uharibifu na upotofu uliopo katika mji wao katika upande wa I´tiqaad ya Majina ya Allaah na Sifa Zake. Akaandika kitabu hichi chenye kuzingatiwa kama tegemeo la msingi wa I´tiqaad sahihi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika mambo ambayo waliyozama nayo watu katika Bid´ah.

Hakika ni kitabu ambacho kilichokusanya mfumo sahihi wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Jambo ambalo Muislamu siku zote hatosheki nalo, bali alihitajia siku zote katika maisha yake, kwa kwamba ´Aqiydah ndio msingi. Kitabu ambacho ni dalili tosha ya kuonesha umuhimu wake katika Ummah wa Kiislamu kwa kule kubahatika kupata Qabuul (kukubaliwa) kwa kushereheshwa na wanazuoni wa Kiislamu wa Ahl-us-Sunnah mbalimbali katika zama tofautitofauti, bali na kusomeshwa katika ulimwengu wa Kiislamu tokea zama hizo mpaka leo na mpaka ulimwengu utakapomalizika.

Na leo nazidi kumshukuru Allaah (وتعالى سبحانه) na kufurahi tena kwa kuwa kijana chetu mpendwa – Allaah Amuhifadhi – al-Akh Abu Bakr Khatwiyb. Amesimama na kukifasiri kitabu hichi kwa lugha ya Kiswahili ili mujtamaa wetu ufaidike na kujua misingi sahihi ya I´tiqaad ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah Ampe kula la kheri hapa duniani na huko Aakhirah na Aijaalie ´amali hii iwe Swadaqat-un-Jaariyah ya mzee wake alokwenda mbele ya haki. Allaah Amrahamu na Amuweke mahali pema. Na yeye ampe afya njema na Ikhlaasw na hima kuendelea kufanya kazi hii ya uandishi na nyinginezo za Da´wah ili mujtamaa wa Kiislamu unufaike na Amuwekee katika mizani ya hasanati zake.

Wa SwallaAllaahu ´alaa Muhammad wa ´alaa alihi wa Aswhaabihi wa Sallam.

Himidi zote ni Zake Allaah Aliyemtuma Mtume Wake kwa uongofu na Dini ya haki ili ipate kushinda dini zote na Allaah Anatosha kuwa Shahidi.

Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allaah Pekee asiyekuwa na mshirika, kwa kukiri hilo na kumpwekesha Yeye Pekee. Na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ahli zake, na Maswahabah zake. Amma ba´ad:

Hii ni I´tiqaad ya al-Firqat-un-Naajiyyah al-Mansuurah[1]mpaka kisimame Qiyaamah, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, nayo ni:

Kumuamini Allaah, Malaika Wake, vitabu Vyake, Mitume Wake, kufufuliwa baada ya mauti na kuamini Qadar; kheri yake na shari yake.

 Kuamini Majina na Sifa za Allaah

Kumuamini Allaah ina maana ni pamoja na kuamini yale Aliyojisifia[2] Nafsi Yake Mwenyewe katika Kitabu Chake na kwa yale aliyomsifia kwayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bila ya Tahriyf,[3] Ta´atwiyl,[4] Takyiyf[5] wala Tamthiyl.[6] Bali, badala yake wanaamini yafuatayo kuhusiana na Allaah (Subhaanahu):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye As-Samiy’ul-Baswiyr (Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima).” (42:11)

Hawakanushi kutoka Kwake yale ambayo Kajisifia Nafsi Yake Mwenyewe, na wala hawabadilishi maana ya maneno kuyatoa mahala pake. Na hawajiweki katika kufuru[7] katika Majina ya Allaah na Uteremsho Wake.[8]Na wala hawaziulizii namna Yake halisi, na wala hawazifananishi wala kuzilinganisha Sifa Zake na sifa za viumbe Vyake.

Kwani, hakika Yeye (Subhaanahu) hana jina lililofanana na Yeye na wala hapana mfano Wake na hana mshirika na wala hakisiwi na viumbe Vyake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwani hakika ni Mjuzi zaidi wa kujijua Mwenyewe na wengine na ni Mkweli zaidi kwa Kauli na Maneno yaliyo bora wazi kuliko Viumbe Vyake.

Halafu Mitume Yake ni wakweli na waaminifu, tofauti na wale wanaosema juu Yake yale wasioyajua. Na kwa ajili ya hili Kasema (Subhaanahu wa Ta´ala):

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَوَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَوَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Subhaana Rabbika Rabbil-‘Izzati ‘Ammaa yaswifuwn (Ametakasika

Mola wako Mola Mtukufu kutokana na yote wanayoelezea) (ya uongo

na upotofu). Wa Salaamun ‘alal-Mursaliyn (na amani iwe juu ya Mitume) (Wetu). Wal-HamduliLLaahi Rabbil-’aalamiyn (na Himidi zote ni za

Mola wa walimwengu.” (37:181-182)

Hivyo Kaelezea Kuitakasa Nafsi Yake Mwenyewe kwa waliyomuelezea wale waendao kinyume na Mitume, Akawasalia Mitume Wake kuonesha dalili ya usalama wa waliyoyasema katika mapungufu na aibu.

Na Yeye (Subhanaahu) kwa yale Aliyojisifu nayo na Kujiita kwa Majina hayo Nafsi Yake, kajumuisha baina ya ukanushaji na uthibitisho. Hakuna upotofu wowote kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa yale waliyokuja nayo Mitume, kwani hakika ni Njia iliyonyooka; Njia ambayo Kawaneemesha Kwayo waifuatayo, miongoni mwa Manabii, wakweli, mashahidi na (waja) wema.

 Kuamini yale Aliyojisifia Allaah Nafsi Yake Mwenyewe katika Kitabu Chake

Kunaingia katika haya yale Aliyojisifia Allaah Nafsi Yake Mwenyewe katika Suurat “al-Ikhlaasw”, ambayo ni sawa na theluthi ya Qur-aan, ambapo Kasema:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌاللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْوَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

”Sema: “Yeye ni Allaahu Ahad (Mmoja Pekee).Allaah ni Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote). Hakuzaa na wala Hakuzaliwa. Na wala

haiwi Awe na yeyote anayefanana (au kulingana) Naye.”(112:1-4)

na Aliyojisifia Nafsi Yake Mwenyewe katika Aayah kubwa katika Kitabu Chake (kujumuisha kati ya kukanusha na kuthibitisha katika kujisifu Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala), ambapo Kasema:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

”Allaah, hapana ilaaha (Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila

Yeye, Al-Hayyul-Qayyuwm (Aliyehai daima, Msimamizi wa

kila kitu). Haumchukuwi usingizi wala kulala. Ni Vyake

pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi.

Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila

ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao (viumbe) na yaliyo nyuma yao. Wala hawadiriki kitu chochote kile katika

Elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy

Yake (Kiti) mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Al-‘Aliyyul-‘Adhwiym (Mwenye

Uluwa – Mwenye Utukufu).”(02:255)

Na kwa ajili hii ndio maana ikawa kwa yule mwenye kuisoma Aayah hii usiku, huwa na Hifadhi ya Allaah na wala hamkurubii Shaytwaan mpaka kupambazuke.

 Dalili ya Uhai wa Allaah

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ

”Na mtegemee Aliye hai Ambaye Hafi.”(25:58)

 Dalili ya Elimu[9] ya Allaah

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

”Yeye Ndiye Al-Awwal (wa Awali hakuna kitu kabla Yake) na Al-Aakhir (wa Mwisho hakuna kitu baada Yake) na Adhw-Dhwaahir (Hakuna kitu juu Yake), na Al-Baatwin (Hakuna kitu karibu kuliko Yeye), Naye kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi daima).”(57:03)

وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ

”Naye Ndiye Al-‘Aliymul-Hakiym (Mjuzi wa yote daima - Mwenye hikmah wa yote daima).”(66:02)

يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا

”Anajua yale (yote) yanayoingia ardhini, na yale (yote) yanayotoka humo, na yale (yote) yanayoteremka kutoka mbinguni, na yale (yote) yanayopanda huko.”(34:02)

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ

”Na Kwake (Allaah) Pekee zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani

na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua. Na wala (haianguki) punje katika viza vya ardhi, na wala (hakianguki) kilichorutubika na wala (hakianguki) kikavu isipokuwa (kimeandikwa) katika Kitabu kinachobainisha (Lawhum-Mahfuwdhw).”(06:59)

وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ

“Na mwanamke yeyote (yule) habebi (mimba) na wala

hazai isipokuwa kwa ujuzi Wake.”(35:11)

لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا

”Ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza daima), na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu

kwa ujuzi (Wake).”(65:12)

 Dalili ya Nguvu za Allaah

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ

”Hakika Allaah Ndiye Ar-Razzaaq (Mwenye kuruzuku vyote daima) Dhul-Quwwatil-Matiyn (Mwenye nguvu kali madhubuti).”(51:58)

 Dalili ya Kuona na Kusikia kwa Allaah

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye As-Samiy’ul-Baswiyr (Mwenye kusikia yote daima, Mwenye

kuona yote daima).” (42:11)

إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا

”Hakika (mawaidha) Anayokuwaidhini nayo Allaah ni mazuri kabisa; hakika Allaah ni Samiy’an-Baswiyraa (Mwenye kusikia yote daima – Mwenye kuona yote daima).”(04:58)

 Dalilia ya Matakwa ya Allaah

وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ

“Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: ‘Maa Shaa Allaah! Laa quwwata illa bilLLaah’ (Ametaka Allaah; hapana nguvu ila za Allaah).” (18:39)

وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ

“Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana wale ambao (walikuja) baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana, basi miongoni mwao (kuna) walioamini na miongoni mwao waliokufuru. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya

Ayatakayo.”(02:253)

أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ الْأَنْعَامِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّي الصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ

”Imehalalishwa kwenu wanyama wenye miguu minne isipokuwa mnaosomewa (kuwa ni haraam). Lakini msihalalishe kuwinda hali mkiwa katika Ihraam. Hakika Allaah Anahukumu Atakayo.(05:01)

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ

”Basi yule ambaye Allaah Anataka kumuongoza, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye (Allaah) Anataka kumpoteza (kwa vile mwenyewe kataka) Humjaalia kifua

 chake kuwa na dhiki chenye kubana kama kwamba

anapanda mbinguni kwa tabu.”(06:125)

 Dalili ya Kupenda kwa Allaah

وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ

”Na fanyeni wema Hakika Allaah Anapenda watendao wema.” (02:195)

وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ

”Na fanyeni haki. Hakika Allaah Anapenda wafanyao haki.”(49:09)

فَمَا اسْتَقَامُوا لَكُمْ فَاسْتَقِيمُوا لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ

”Basi wakikunyokeeni (kwa uzuri), nanyi wanyokoeeni (kwa uzuri). Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa (wanaomcha).(09:07)

فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ

”Basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda.”(05:54)

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ

”Hakika Allaah Anapenda wale wanaopigana katika njia Yake safusafu kama kwamba wao ni jengo lililo imara madhubuti.”(61:04)

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ

”Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, Atakupendeni Allaah.” (03:31)

 Dalili ya Kuridhia kwa Allaah

رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

”Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye.”(98:08)

 Dalili ya Wingi wa Huruma na Kurehemu kwa Allaah

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

”BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym (Kwa Jina la Allaah Mwingi wa Rahmah, Mwenye kurehemu).”(27:30)

رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا

“Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa Rahmah na elimu.”(40:07)

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا

“Na Yeye daima kwa Waumini ni Rahiymaa (Mwenye huruma).”(33:43)

كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ

”Mola wenu Amejiwajibishia juu ya Nafsi Yake Rahmah.”(06:54)

وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ

”Naye ni Al-Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kusamehe - Mwenye kurehemu).”(10:107)

فَاللَّـهُ خَيْرٌ حَافِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُالرَّاحِمِينَ

”Basi Allaah ni Khayrun-Haafidhwaa (Mbora wa kuhifadhi). Naye ni Arhamur-Raahimiyn (Mbora wa kurehemu kuliko wanaorehemu).”(12:64)

 Dalili ya Hasira na Kughadhibika kwa Allaah na kuchukia Kwake ndani ya Qur-aa na kwamba Yeye Allaah Amesifika kwa hilo

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

”Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni (Moto wa) Jahannam, atadumu humo milele na Allaah Atamkasirikia na Atamlaani na Atamuandalia adhabu kuu.”(04:93)

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

”Hivyo kwa kuwa wao wamefuata yale yanayomkasirisha Allaah, na wakachukia radhi Zake, basi Akazibatilisha ‘amali zao.”(47:28)

فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ

”Basi walipotukasirisha; Tuliwapatiliza.”(43:55)

وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ

”Lakini Allaah Amekirihika kutoka kwao, basi Akawazuia.”(09:46)

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ

”Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.”(61:03)

 Dalili ya Kuwasili na Kuja kwa Allaah

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ

Je, wanangojea (nini) isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli

vya mawingu pamoja na Malaika, na itolewe hukumu? Na kwa Allaah hurudishwa mambo.”(02:210)

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ

”Je, wanangojea jingine (lolote) isipokuwa wawafikie

Malaika (kuwatoa roho) au awafikie Mola wako au ziwajie baadhi za Aayah za Mola wako (alama za Qiyaamah kubwa)?”(06:158)

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

”Sivyo hivyo! (Kumbukeni pale) Ardhi itakapovunjwavunjwa. Na Atakapokuja Mola wako, na Malaika wamejipanga safu.”(89:21-22)

وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا

”Na (kumbusha) Siku itakayopasuka mbingu kwa (kutoa) mawingu; na Malaika watateremshwa mteremsho wa wingi.”(25:25)

 Dalili ya Uso wa Allaah

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”Kila aliyekuwa humo (mbinguni na ardhini) ni mwenye kufa. Na utabakia Uso wa Mola wako Dhul-Jalaali wal-Ikraam (Mwenye Utukufu na Ukarimu).”(55:27)

كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa Uso Wake.” (28:88)

 Dalili ya Mikono ya Allaah

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75)

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

”Na Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” (Siyo, bali) mikono yao ndio ilivyofumbwa; na wamelaaniwa

kwa yale waliyoyasema. Bali Mikono Yake (Allaah) imefumbuliwa Hutoa Atakavyo.”(05:64)

 Dalili ya Macho ya Allaah

وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا

”Na subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وسلم) kwa hukumu ya Mola wako. Hapana shaka wewe uko mbele ya Macho Yetu.”(52:48)

وَحَمَلْنَاهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَاحٍ وَدُسُرٍ تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا

”Na Tukambeba kwenye ile (jahazi) iliyo (tengenezwa) kwa mbao na misumari. Inatembea kwa Macho Yetu.” (54:13-14)

وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِّنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي

”Na Nikakutilia mahaba kutoka Kwangu, na ili ulelewe Machoni Mwangu.”(20:39)

 Dalili ya Kusikia na Kuona kwa Allaah

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ

”Allaah Amekwishasikia kauli ya yule (mwanamke) anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Samiy’um-Baswiyr

(Mwenye kusikia yote daima - Mwenye kuona yote daima).”(58:01)

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ

”Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) ambao wamesema: “Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.(03:181)

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ

”Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! (Tunasikia!) Na Wajumbe wetu wako kwao wanaandika.”(43:80)

إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ

”Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”(20:46)

أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ

”Je, hajui kwamba Allaah Anaona?”(96:14)

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ

”Na mtegemee Al-’Aziyzir-Rahiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mwenye kurehemu). Ambaye Anakuona wakati unaposimama.” (26:217-218)

وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ

”Na sema (uwaambie): Fanyeni (mtakavyo). Allaah Ataona ‘amali zenu na Mtume Wake, na Waumini (pia wataona).”(09:105)

 Dalili ya Adhabu na Njama za Allaah

وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ

”Naye ni Shadiydul-Mihaal (Mkali wa kusibu misiba na maangamizi).” (13:13)

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

”Na wakapanga njama, lakini Allaah Akapanga (kuwalipiza) njama. Na Allaah ni Mbora wa kurudisha njama za wenye kupanga njama.”(03:54)

وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

”Wakapanga njama Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha njama (zao kwa kuwaadhibu), nao huku hawatambui.”(27:50)

إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًاوَأَكِيدُ كَيْدًا

”Hakika wao wanapanga njama. Nami napanga mipango (ya kuvunja na kupindua njama zao).” (86:15-16)

 Dalili ya Kusamehe, Kurehemu na Uwezo wa Allaah

إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا

”Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu; basi hakika Allaah ni ‘Afuwwan-Qadiyraa (Mwingi wa kusamehe – Muweza wa yote daima).”(04:149)

وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

”Na wasamehe na waachilie mbali. Je, (nyinyi) hampendi Allaah Akughufurieni? Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).”(24:22)

وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ

”Na hali utukufu ni wa Allaah na wa Mtume Wake na wa Waumini.”(63:08)

فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ

“Naapa kwa Utukufu Wako, bila shaka nitawapotosha wote.”(38:82)

 Dalili ya Majina ya Allaah

تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”Tabaaraka (Limetukuka) Jina la Mola wako Dhil-Jalaali wal-Ikraam (Mwenye Utukufu na Ukarimu).”(55:78)

فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

”Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua (mwengine) mwenye Jina Lake? (Bila shaka hakuna aliyefanana Naye kwa lolote, vyovyote, na wala hana

mshirika!).” (19:65)

 Aayah zinazokanusha ulinganisho na ushirika pamoja na Allaah

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana (au kulingana) Naye.” (112:04)

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye (washirika) na hali ya kuwa nyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana Anayelingana nae).”(02:22)

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ

Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa ni mungu mshirika (anaelingana na Allaah); wanawapenda kama mapenzi (yapasavyo) ya kumpenda

Allaah. Na wale ambao wameamini wana mapenzi

 zaidi kwa Allaah.”(02:165)

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖوَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا

”Na sema: “AlhamduliLLaahi (Sifa njema zote ni za Allaah) Ambaye Hakujifanyia mwana, na wala Hakuwa na mshirika katika ufalme, na wala hakuwa dhaifu hata awe (ahitaji)

 walii (msaidizi); basi mtukuze matukuzo makubwa

kabisa (Sema Allaahu Akbar).”(17:111)

يسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

”Vinamtakasa Allaah (vyote) vilivyomo mbinguni na (vyote) vilivyomo ardhini, ufalme ni Wake na Sifa njema ni Zake. Naye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza daima).”(64:01)

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًاالَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

”Tabaaraak (Ametukuka kwa Baraka) Yule (Ambaye) Ameteremsha Al-Furqaan(Pambanuzi ya haki na batili) kwa

mja Wake ili awe muonyaji kwa walimwengu (wote). Ambaye

 ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, na hakujichukulia mtoto na wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na Ameumba kila kitu; kisha Akakikadiria kipimo sawa sawa.” (25:01-02)

مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ إِذًا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

”Allaah Hakuchukua mtoto yeyote, na wala hakukuwa

pamoja Naye ilaah (miungu yeyote mingine; wangelikuweko kama mnavyodai, basi) hapo bila shaka kila mungu angelichukua vile alivyoviumba, na bila shaka baadhi yao wangeliwashinda wengineo.Subhaana-Allaah (Ametakasika Allaah) kutokana na yale yote wanayoyaelezea (kumshirikisha Allaah kuwa ana mke na watoto). ‘Aalimil-Ghaybi Wash-Shahaadah (Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri) basi Ta’aala(Ametukuka kwa ‘Uluwwa)

kutokana na yale wanayomshirikisha.”(23:91-92)

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

”Basi msipigie mifano Allaah (kwani hakuna kinachofanana Naye kabisa!) Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.”(16:74)

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

”Sema: “Hakika Mola wangu Ameharamisha uchafu (al-kabaair; ueasharati, zinaa, liwati, n.k.) yaliyodhihirika na yaliyo ya

 siri, na dhambi (za kila aina), ukandamizaji bila ya haki, na (Ameharamisha) kumshirikisha Allaah kwa chochote kile ambayo Hakukiteremshia dalili, na kusema juu ya

Allaah yale ambayo hamyajui”.” (07:33)

 Dalili ya kulingana kwa Allaah juu ya ´Arshi

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) juu ya ‘Arshi Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah).”(20:05)

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Kisha Akalingana juu ya ‘Arshi.”(07:54)

Aayah zimekuja kwa sampuli hii mahali saba: al-A´raaf:54, Yuunus:03, ar-Ra´d:02, al-Furqaan:59, as-Sajdah:04 na al-Hadiyd:04.

 Dalili ya kwamba Allaah Yuko juu ya viumbe Vyake

يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.”(03:55)

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ

”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.”(04:158)

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Linapanda neno zuri (dhikru-Allaah), na kitendo chema (cha ikhlaasw) Hukipa hadhi (Hukitakabali).” (35:10)

يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَأَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا

“Ee Haamaan! Nijengee mnara mkubwa ili nifikie njia. Njia za mbinguni ili nimchungulie Ilaah (Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) wa Muwsaa, kwani hakika mimi namdhania ni muongo.” (40:36-37)

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

”Je, mnadhani mko (katika) amani na Aliyeko mbinguni (juu) kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko (katika) amani na Aliyeko mbinguni (juu) kwamba Hatokutumieni kimbunga (cha mawe), basi mtajua

vipi (makali) maonyo Yangu.”(67:16-17)

 Dalili ya Allaah kuwa pamoja na viumbe Vyake kwa Ujuzi Wake

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

”Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana

na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah), Anajua yanayoingia ardhini, na yatokayo humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo, Naye Yu Pamoja nanyi (kwa ujuzi Wake) popote mlipo. Na Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr

(Mwenye kuyaona).” (57:04)

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

”Hauwi mnong’ono wa (watu) watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao (kwa ujuzi Wake), na wala (hauwi mnong’ono wa) watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao (kwa ujuzi Wake), na wala (hauwi mnong’ono wa) chini (kuliko) ya hivyo, na wala (wa) wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao (kwa ujuzi Wake) popote watakapokuwa; kisha Atawajulisha kwa yale (yote) waliyoyatenda Siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah kwa

kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi daima).”(58:07)

لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا

“Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.”(09:40)

إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ

”Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”(20:46)

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

”Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa (wanaomcha), na wale ambao wao ni wema.” (16:128)

وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ

”Na subirini. Hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri.”(08:46)

كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ

“Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi

kwa idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri.”(02:249)

 Dalili ya Maneno na Kuongea kwa Allaah

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا

”Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?”(04:87)

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

”Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?” (04:122)

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ

”Na (Tahadhari) Atakaposema Allaah: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!” (05:116)

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا

”Na limetimia Neno la Mola wako kwa kweli na uadilifu.”(06:115)

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja

kwa moja.”(04:164)

مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ

”Miongoni mwao (yuko) aliyesemeshwa na Allaah.” (02:253)

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ

“Na alipokuja Muwsaa katika miyqaat (pahala pa miadi) yetu,

na Mola wake Akamsemesha.”(07:143)

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.”(19:52)

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

”Na pindi Mola wako Alipomwita Muwsaa (kumwambia): “Nenda kwa watu madhalimu.”(26:10)

وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ

”Na Mola wao Akawaita (wote wawili na kuwaambia): “Je, kwani Mimi Sikukukatazeni (nyote wawili) mti huo.”(07:22)

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ

”Na (kumbusha ee Muhammad صلى الله عليه وسلم,) Siku Atakayowaita; Atasema: “Wako wapi washirika Wangu ambao mlikuwa mnadai (kuwa ni miungu na kuwalinganisha Nami)?”(28:62)

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ

”Na (kumbusha ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم,) Siku (Allaah) Atakapowaita, Atasema: “Mliwajibu nini Mitume?”(28:65)

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

”Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah (Qur-aan).” (09:06)

وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

”Na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia Maneno ya Allaah kisha wakayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?.”(02:75)

يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِۚ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمْ قَالَ اللَّـهُ مِن قَبْلُ

”Wanataka kubadilisha Maneno ya Allaah. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وسلم): “Hamtotufuata! Hivyo

ndivyo Alivyosema Allaah kabla”.”(48:15)

وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ ۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ

”Na soma (ee Muhammad صلى الله عليه وسلم) uliyoletewa Wahy

katika Kitabu cha Mola wako. Hakuna awezaye kubadilisha

Maneno Yake.”(18:27)

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ

”Hakika hii Qur-aan inawasimulia wana wa Israaiyl mengi ambayo wao wanakhitilafiana nayo.”(27:76)

 Dalili ya kwamba Qur-aan inatoka kwa Allaah

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ

”Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa.”(06:155)

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ

”Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya mlima, ungeliuona unayenyekea (na) wenye kupasukapasuka kutokana na

khofu ya Allaah.”(59:21)

وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَقُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَوَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ

”Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine, na Allaah Anajua Anayoyateremsha, (makafiri) husema: “Hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وسلم) ni mzushi.” Bali wengi wao hawajui. Sema: Roho Takatifu (Jibriyl) ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki ili Awathibitishie walo walioamini na ni Hidaayah na bishara kwa Waislamu. Na kwa yakini Tunajua kwamba (makafiri) wanasema: “Hakika bin-Aadam (ndiye) anamfundisha (Muhammad صلى الله عليه وسلم Qur-aan).” (Lakini) Lugha wanayomnasibishia (kuwa anamfunza Mtume) ni

(lugha) ya kigeni, na hii (ya Qur-aan) ni lugha ya

Kiarabu bayana.”(16:101-103)

 Dalili ya kwamba waumini watamuona Allaah siku ya Qiyaamah

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ

(Baadhi ya) Nyuso siku hiyo zitanawiri. Zikimtazama Mola wake.”(75:22-23)

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ

”Kwenye makochi (ya fakhari) wakitazama.”(83:23)

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

”Kwa wale waliofanya wema watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-Husnaa(Pepo) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima

ya kumuona Allaah).”(10:26)

لَهُم مَّا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ

”Watapata humo wayatakayo, na Kwetu kuna yaliyo ziada (ya neema za Pepo na kumuona Allaah عز وجل ).” (50:35)

Mlango huu umekuja katika Kitabu cha Allaah (Ta´ala) sehemu nyingi. Yule mwenye kuizingatia Qur-aan na huku anatafuta uongofu wake, basi itambainikia Njia ya haki.

 Sifa za Allaah zimetajwa katika Sunnah

Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio yenye kuifasiri Qur-aan na kuiweka wazi, kuithibitisha na kuja na maana mpya na hukumu (ambazo hazikuja katika Qur-aan). Hali kadhalika ni wajibu kuamini yale aliyomsifia[10] Mola Wake (´Azza wa Jalla) kutokana na zile Ahaadiyth Swahiyh ambazo wamezikubali watu wa maarifa, kwa mfano wa kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

 Dalili ya kwamba Allaah Huteremka katika mbingu ya chini

“Huteremka Mola Wetu katika mbingu ya dunia kila usiku pale kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na Kusema: “Ni nani

mwenye kuniomba nimjibie? Ni nani mwenye kuniuliza nimpe?

Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?””[11] (Muttafaq)

 Dalili ya Kufurahi kwa Allaah

“Allaah Hufurahi sana kwa Tawbah ya mja Wake muumini anapotubia, kuliko furaha ya mmoja wenu kwa kupata

kipando chake...”[12] (Muttafaq)

 Dalili ya Kucheka kwa Allaah

“Allaah Anawacheka watu wawili ambapo mmoja wao kamuua mwenzake. Halafu wote wawili wanaingia Peponi.”[13]

 Dalili ya Kustaajabu kwa Allaah

“Anastaajabu Mola Wetu kwa kukata tamaa waja Wake licha ya mabadiliko Yake ya hali zao yako karibu.Huwatazama mnapokuwa katika hali ngumu na wenye kukata tamaa. Huanza kucheka kwa kuwa Anajua kuwa faraja yenu iko karibu.”[14] (Hadiyth Hasan)

 Dalili ya Mguu wa Allaah

“Haitoacha Jahannam kutupwa ndani yake (watu na mawe) nayo inasema “Je, kuna zaidi?”, mpaka Mola Aliyetukuka Aweke Mguu Wake kisha pawe sawa. Hapo ndio itasema “Inatosha! Inatosha!”[15]

 Dalili ya Maneno na Sauti ya Allaah

“Allaah (Ta´ala) Atasema: “Ewe Aadam!” Atajibu: “Ninaitikia wito Wako na nakuomba unifanye ni mwenye furaha na Kunisaidia.” Kisha Atanadi kwa Sauti: “Hakika ya Allaah Anakuamrisha

 utoe moja katika kizazi chako Motoni.”[16]

“Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa Atamuongelesha Mola Wake. Kutakuwa hakuna baina Yake Yeye (Allaah) na baina yake yeye mwanaadamu mwenye kutarjumu (kufasiri).”[17]

 Dalili ya kwamba Allaah Yuko juu ya mbingu na Sifa zingine

Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Ruqyah ya mgonjwa:

“Mola Wetu ni Allaah Ambaye Yuko juu ya mbingu, Limetakasika Jina Lako. Amri Yako iko mbinguni na ardhini. Teremsha Rahmah yako katika ardhi kama jinsi Rahmah Yako iko mbinguni. Tusamehe madhambi yetu makubwa na madogo. Wewe ni Mola wa wazuri. Teremsha Rahmah katika Rahmah Yako na dawa

 katika Dawa Yako kwa huyu mwenye maumivu.”[18]

(Hadiyth ni Hasan, kaipokea Abuu Daawuud)

Na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, hamniaminii na mimi nimeaminiwa na Aliye juu ya mbingu?”[19] (Muttafaq)

“... na ´Arshi iko juu ya maji, na Allaah Yuko juu ya ´Arshi, Naye Anajua yale mliomo.”[20] (Imepokelewa na Abuu Daawuud na wengine)

Na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia mjakazi:

“Yuko wapi Allaah?” Akasema: “Mbinguni.” Kisha akamuuliza: “Mimi ni nani?” Akasema: “Wewe ni Mtume wa Allaah.” Akasema: “Muache huru, hakika ni muumini.”[21]

 Dalili ya Allaah Kuwa pamoja na viumbe Vyake kwa Ujuzi wake

“Kiwango bora cha Imani ni wewe ujue kuwa Allaah Yuko pamoja na wewe popote ulipo.”[22] (Hadiyth Hasan)

 Dalili ya Allaah kuwa mbele ya yule mwenye kuswali

“Anaposimama mmoja wenu katika Swalah, asiteme mate mbele yake, wala kuliani kwake, kwani hakika Allaah Yuko mbele Yake. Badala yake (ateme) kushotoni kwake au chini ya mguu

wake.”[23] (Muttafaq)

 Dalili ya kwamba Allaah Yuko juu ya viumbe Vyake na Sifa zingine

“Allaah Ndiye Mola wa mbingu hizi saba na ardhi na Ndiye

Mola wa ´Arshi kubwa. Mola Wetu na Mola wa kila kitu. Mpasuaji wa mbegu na kokwa na Ambaye Umeteremsha Tawrat, Injiyl na Qur-aan. Najikinga Kwako na shari ya nafsi yangu na shari ya kila kiumbe kiovu ambacho wewe una utawala juu yake. Wewe ni wa Kwanza na hakuna kabla Yako kitu. Na Wewe ni wa Mwisho na hakuna baada Yako kitu. Na Wewe ni wa Juu na hakuna juu Yako kitu. Na wewe ni wa Karibu na hakuna kinachojifichika Kwako. Nilipie deni langu na nitajirishe na ufakiri wangu.”[24]

(Kaipokea Muslim)

 Dalili ya kwamba Allaah Yuko Karibu

Na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaambia Maswahabah pindi waliponyanyua masauti yao kwa Dhikr:

“Enyi watu! Zihurumieni nafsi zenu! Kwani hakika hamumuombi ambaye ni kiziwi wala asiyekuwepo. Hakika Yule mnayemwomba ni Mwenye Kusikia Mwenye kuona na Aliye karibu. Hakika yule mnayemwomba Yuko karibu na mmoja wenu kuliko shingo

ya mpando wenu.”[25] (Muttafaq)

 Dalili ya kwamba waumini watamuona Allaah siku ya Qiyaamah

“Hakika nyinyi mtamuona Mola Wenu kama mnavyouona mwezi usiku wa mwezi mng'aro – hamtosongamana katika kumuona. Hivyo ikiwa mnaweza kuswali kabla ya jua

kuchomoza na jua kuzama, basi fanyeni

hivyo.”[26] (Muttafaq)

Tazama Hadiyth hizi na mfano wake ambapo anaelezea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Mola Wake. Hakika al-Firqat-un-Naajiyah, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, wanaamini hayo kama jinsi wanavyoamini Aliyojielezea Allaah katika Kitabu Chake, bila ya Tahriyf, Ta´atwiyl, Takyiyf wala Tamthiyl.

 Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, watu wa kati na kati

Bali wao wako kati na kati baina ya mapote ya Ummah, kama jinsi Ummah ulivyo kati na kati baina ya Ummah zingine.

 Kati ya Jahmiyyah na Mushabbihah

Wako kati na kati katika mlango wa Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) – baina ya Ahl-ut-Ta´twiyl wanaokanusha Jahmiyyah na Ahl-ut-Tamthiyl wanaofananisha Mushabbihah.

 Kati ya Qadariyyah na Jabriyyah

Wako kati na kati katika mlango wa Matendo ya Allaah (Ta´ala) – baina ya Qadariyyah na Jabriyyah na wengineo.

 Kati ya Murji-ah na Wa´iydiyyah

Hali kadhalika katika mlango wa Tishio la Allaah – baina ya Murji-ah na Wa´iydiyyah miongoni mwa Qadariyyah na wengine.

 Kati ya Haruuriyyah[27] na Mu´tazilah na Murji-ah na Jahmiyyah

Hali kadhalika katika mlango wa Imani na majina ya Dini – baina ya Haruuriyyah na Mu´tazilah na Murji-ah na Jahmiyyah.

 Kati ya Rawaafidhw[28] na Khawaarij

Hali kadhalika kuhusiana na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kati ya Rawaafidhw na Khawaarij.

 Kuamini kuwa Allaah Yuko juu ya mbingu na juu ya ´Arshi na kwamba Yuko na viumbe Vyake

Na katika yale tuliyotaja katika kumuamini Allaah, kunaingia kuamini yale Aliyoelezea Allaah katika Kitabu Chake, na yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale waliyokubaliana kwayo Salaf wa Ummah:

Ya kwamba Yeye (Subhaanahu) Yuko juu ya mbingu Zake, juu ya ´Arshi yake na juu ya viumbe Vyake. Na Yeye (Subaanahu) Yuko pamoja nao popote wanapokuwa na Anajua wanayoyafanya, kama Alivyojumuisha baina ya hayo katika Kauli Yake:

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

”Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh(Yuko juu kwa namna inayolingana

na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah), Anajua yanayoingia ardhini, na yatokayo humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo, Naye Yu Pamoja nanyi (kwa ujuzi Wake) popote mlipo. Na Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr

(Mwenye kuyaona).” (57:04)

Na Kauli Yake “Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo” haina maana ya kwamba Kachanganyika na viumbe Vyake. Lugha haidharurishi hilo na linakwenda kinyume na yale waliyokubaliana nayo Salaf wa Ummah na linakwenda kinyume na umbile Aliloliumbia kwalo uumbaji. Mwezi ni Ishara katika Ishara za Allaah na ni katika Kiumbe Chake kidogo. Uko mbinguni daima na unakuwa pamoja na msafiri na asiyekuwa msafiri popote anapokuwa.

Na Yeye (Subhaanahu) Yuko juu ya ´Arshi. Anaona viumbe Vyake, Anawalinda, Ana ujuzi juu yavyo na yasiyokuwa hayo katika maana ya Ubwana[29] Wake. Maneno yote haya ambayo Allaah Kataja – ya kwamba Yuko juu ya ´Arshi na kwamba Yuko pamoja nasi – ni haki[30] kwa uhakika wake na wala hayahitajii Tahriyf, lakini yanatakiwa kulindwa na misingi isiyokuwa na maana ya udanganyifu, kwa mfano kudhania ya kwamba udhahiri wa Kauli Yake “Fiys-Salmaa” maana yake kwamba Yuko mbinguni na mbingu aidha inambeba au iko juu Yake. Hili ni batili kwa Ijmaa´ ya wanachuoni na watu wa Imani. Hakika ya Allaah, imeenea Kursiyy Yake (Kiti) mbingu na ardhi na Yeye Ndiye Anayezuia mbingu na ardhi zisiondoke. Anazuia mbingu na kwa Amri Yake Anafanya zisianguke kwenye ardhi isipokuwa kwa idhini Yake. Na ni katika Ishara Zake kusimama kwa mbingu na ardhi kwa Amri Yake.

 Kuamini kuwa Allaah Yuko karibu na viumbe Vyake

Katika hili kunaingia vile vile kuamini ya kwamba Yuko karibu na viumbe Vyake Mwenye Kuwajibu, kama Alivyojumuisha baina ya hayo katika Kauli Yake:

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ

Na watakapokuuliza (Ee Muhammad صلى الله عليه وسلم) waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Qariyb (Yu karibu daima kwa elimu Yake); Naitikia da’wah (maombi) ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi,

wapate kuongoka.”(02:186)

Na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaambia Maswahabah waliponyanyua masauti yao kwa Dhikr:

“... Hakika yule mnayemwomba Yuko karibu na mmoja wenu kuliko shingo ya kipando chenu.”[31]

Na yaliyotajwa katika Kitabu na Sunnah kuhusu Ukaribu Wake na Kuwa Kwake pamoja, hayapingani na yaliyotajwa kuhusu kuwa Kwake juu[32] ya viumbe, kwa kuwa Yeye (Subhaanahu) hakuna kitu mfano Wake katika Sifa Zake zote. Naye Yuko juu kabisa kwa Ukaribu Wake na Yuko Karibu kwa Ukuu Wake.

 Kuamini kuwa Qur-aan inatoka kwa Allaah na haikuumbwa

Katika kumuamini Allaah na Vitabu Vyake kunaingia kuamini ya kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah, imeteremshwa na haikuumbwa. Uteremsho wake umeanza kutoka Kwake na Kwake itarudi. Allaah Amezungumza kwa hiyo Qur-aan Kauli ya kikweli. Qur-aan hii iliyoteremshwa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Maneno ya Allaah ya kihakika na sio maneno ya mwengine. Na wala haijuzu kusema ya kwamba ni hikaayah[33] au ibara ya Maneno ya Allaah, bali wanapoisoma watu au kuiandika kwenye sahifu, kwa kufanya hivyo haijatoka kuwa ni Maneno ya Allaah ya kihakika. Kwani hakika Maneno yananasibishwa na yule aliyeyatamka mwanzo, na si kwa yule aliyeyawakilisha (kuyafikisha). Hivyo ni Maneno ya Allaah; herufu na maana yake. Maneno ya Allaah sio herufu bila ya maana na wala sio maana bila ya herufu.

 Kuamini kuwa waumini watamuona Allaah siku ya Qiyaamah

Kunaingia vile vile katika yale tuliyoyataja kumuamini Allaah, Vitabu Vyake, Malaika Wake na Mitume Wake, ni pamoja na:

Kuamini ya kwamba waumini watamuona siku ya Qiyaamah kwa macho yao kama wanavyoona jua kwenye anga lililo wazi bila ya mawingu, na hali kadhalika kama wauonavyo mwezi usiku wa mwezi mng'aro – hawatosongamana katika kumuona. Watamuona (Subhanaahu) nao watakuwa katika uwanja wa Qiyaamah na kisha watamuona baada ya kuingia Peponi kwa njia[34] atakayoipenda Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

 Kuamini Aakhirah

Katika kuamini Siku ya Aakhirah kunaingia:

Kuamini yote aliyoelezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa yatakayokuwa baada ya mauti. Wanaamini mitihani ya ndani ya kaburi, adhabu ya kaburi na neema zake. Ama mitihani yake, hakika watu watapewa mitihani kwenye makaburi yao. Kila mtu ataulizwa: “Ni nani Mola wako? Ni ipi dini yako? Na ni nani Mtume wako?

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ

”Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti (ya kuendelea kumwambudu Yeye Pekee bila kumshirikisha)

katika uhai wa dunia na Aakhirah.” (14:27)

Waumini watasema: “Allaah ndio Mola Wangu, Uislamu ndio Dini yangu na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio Mtume wangu.” Ama wenye mashaka watasema: “Aah! Aah! Sijui. Nilisikia watu wanasema kitu na mimi nikakisema.” Hivyo atapigwa chuma cha Moto na atapiga kelele ya juu kabisa ambayo itasikiwa na viumbe vyote isipokuwa binaadamu. Na lau binaadamu aingeliisikia, basi angelizimia.

Baada ya mtihani huu, kuna ima neema au adhabu mpaka kitaposimama Qiyaamah kikubwa. Roho zitarudishwa miilini. Qiyaamah ambacho Allaah (Ta´ala) Kaelezea katika Kitabu Chake na kupitia ulimi wa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakakubaliana juu ya hilo Waislamu, kitasimama. Watu watatoka ndani ya makaburi yao, bila ya viatu, uchi, wasiotahiriwa, wasimame mbele ya Mola wa walimwengu. Jua litajongezwa karibu yao na majasho yao yatafika kwenye vinywa vyao.[35] Mizani itapima na yapimwe matendo ya waja.

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu.”(23:102)

Madaftari yataenezwa ambayo ndani yake kumeandikwa matendo. Kuna ambao watapewa madaftari yao kwa mkono wa kulia, na kuna ambao watapewa madaftari yao kwa mkono wa kushoto au nyuma ya mgongo wao, kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا

”Na kila mtu Tumemuambatanishia twaairahuu (majaaliwa

 ya ‘amali zake) shingoni mwake. Na Tutamtolea Siku ya Qiyaamah kitabu (kilichohifadhi kila alilolifanya hapa duniani) atakachokikuta kimekunjuliwa. (Ataambiwa): “Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosheleze leo kukuhesabia

dhidi yako.” (17:13-14)

Allaah Atawafanyia hesabu viumbe na Atamhifadhi mja Wake muumini halafu atayakubali madhambi yake, kama ilivyokuja katika Kitabu na Sunnah. Ama makafiri, hawatohesabiwa hesabu kwa njia hiyo hiyo ya matendo mema na mabaya kupimwa, kwa kuwa hawana mema yoyote. Badala yake matendo yao yatahesabiwa na watakuja kujua hilo, wayakubali na wawajibike nayo.

 Hodhi (birika), Njia[36] na Shafaa´ah[37]

Katika kiwanja cha Qiyaamah kutakuwa hodhi iliyotajwa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maji yake ni meupe kuliko maziwa na matamu kuliko asali. Vikombe vyake ni wingi wa idadi ya nyota mbinguni na urefu na upana wake ni sawa na mwendo wa mwezi. Anayekunywa humo mara moja, hatopata kiu baada yake kamwe.

Njia imewekwa juu ya Jahannam na ni daraja iliyo baina ya Pepo na Moto. Watu watapita juu yake kadiri ya matendo yao. Kuna ambao watapita kama kufumba na kufumbua, wengine kama umeme, wengine kama upepo, wengine kama mpanda farasi, wengine kama mwenye kusafiri kwa ngamia, wengine kama mkimbiaji, wengine kama watembeaji, wengine kama mtambaaji na wengine watashikwa na kutupwa Motoni. Yule atakayevuka Njia ataingia Peponi. Watapovuka watasimama kwenye daraja baina ya Pepo na Moto na kulipizana kisasi wao kwa wao. Baada ya kusafishwa, watapewa idhini ya kuingia Peponi. Mtu wa kwanza ambaye atafunguliwa mlango wa Pepo ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na watu wa kwanza ambao wataingia Peponi ni Ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Atakuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Qiyaamah na Shafaa´ah tatu. Ama Shafaa´ah ya kwanza atawaombea waliosimamishwa na kusubiri wahukumiwe baada ya Aadam, Nuuh, Ibraahiym, Muusa na ´Iysa bin Maryam kutoa udhuru wa Shafaa´ah, mpaka itaishia kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama Shafaa´ah ya pili atawaombea watu wa Peponi waingie Peponi – na Shafaa´ah hizi mbili ni maalum kwake. Ama Shafaa´ah ya tatu atawaombea wale waliostahiki kuingia Motoni. Na Shafaa´ah hii ni kwake na kwa Mitume wengine, wakweli na wengineo. Atawaombea wale waliostahiki kuingia Motoni wasiingizwe na awaombee wale walioingia watolewe humo. Allaah (Ta´ala) Atawatoa ndani ya Moto watu si kwa sababu ya Shafaa´ah, bali ni kwa sababu ya Fadhila Zake na Rahmah Zake. Kutabaki Peponi nafasi baada ya watu walioingia na Allaah Ataumba watu maalum kwa ajili yake[38] kisha Awaingize Peponi. Hatua hizi mbali mbali zinazokuja kuhusu Nyumba ya ´Aakhirah, hesabu na thawabu, Pepo na Moto.

Ufafanuzi zaidi wa hilo umetajwa katika Vitabu vilivyoteremshwa kutoka mbinguni na Athaar ya elimu iliyopokelewa kutoka kwa Mitume. Na katika elimu iliyorithiwa kutoka kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), katika hayo kuna yanayokinaisha na kutosheleza, yule mwenye kutafuta atapata.

 Kuamini Qadar; kheri na shari yake

al-Firqat-un-Naajiyah, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, wanaamini Qadar kheri na shari yake.

Kuamini Qadar kumegawanyika katika daraja mbili na kila daraja ina mambo mawaili.

Daraja ya kwanza:

Kuamini ya kwamba Allaah (Ta´ala) Alijua kwa Elimu Yake ya milele – ambayo Anasifiwa kwayo milele na daima – ambayo viumbe watafanya, na Akajua hali zao zote kuhusiana na utiifu na maasi, riziki zao na umri wa maisha yao. Kisha Akayaandika Allaah katika Lawh al-Mahfuudh makadirio ya viumbe. Kitu cha kwanza Alichoumba Allaah ni kalamu. Akaiambia: “Andika!” Ikasema: “Niandike nini?” Akasema: “Andika yatayokuwepo mpaka siku ya Qiyaamah.”[39]

Yaliyomfika mtu hayakuwa ni yakumkosa, na yaliyomkosa hayakuwa ni yakumsibu – (wino wa) kalamu umekauka na sahifu zimefungwa. Kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta´ala):

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

”Je, huelewi kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yamo katika Kitabu (Lawhum-Mahfuudhw). Hakika hayo kwa Allaah ni sahali.”(22:70)

Na Akasema:

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

”Hakuna msiba wowote unaokusibuni katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu (Lawhum-Mahfuudhw) kabla Hatujauumba (huo msiba). Hakika hayo kwa Allaah

ni sahali.”(57:22)

Makadirio haya yanafuata[40]Elimu Yake (Subhaanahu), yanakuja katika mahali kwa jumla na kwa ufafanuzi. Kaandika kwenye Lawh al-Mahfuudh Atakayo.

Baada ya Kuumba kijusi cha mtoto,[41] kabla ya kukipulizia roho, Hukitumia Malaika na huamrisha maneno mane. Huambiwa: “Andika riziki yake, umri wa maisha yake, matendo yake na kama atakuwa na maudhiko au mwenye furaha”. Makadirio haya[42] walikuwa wakiyakanusha al-Ghulaat al-Qadariyyah mwanzoni na wanayakanusha (hata) leo japokuwa ni wachache.

Daraja ya pili:

Utashi[43] wa Allaah (Ta´ala) unaoendelea na Uwezo Wake wa kina. Ina maana kuamini ya kwamba Atakayo Allaah, huwa, na Asiyotaka, hayawi. Yenye kufanya harakati na yaliotulia yalioko mbinguni na ardhini hayawi isipokuwa kwa Matakwa ya Allaah (Subhaanahu). Hakukuwi katika Ufalme Wake kile Asichokitaka. Na Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ni Muweza wa kila jambo, sawa yalioko na yasiokuwepo. Hakuna kimechoumbwa katika ardhi wala mbinguni isipokuwa, Allaah (Subhaanahu) ndio Kakiumba. Hakuna Muumba mwengine badala Yake wala Mola asiyekuwa Yeye. Pamoja na hayo, Kawaamrisha waja kumtii Yeye na kuwatii Mitume Wake na Akakataza Kumuasi. Naye (Subhaanahu) Anawapenda wachaji Allaah,[44] wenye kufanya wema[45]na waadilifu.[46]Anakuwa radhi na wale walioamini na kufanya mema. Hawapendi makafiri na wala Hawaridhii wenye kufanya maasi.[47]Na wala Haamrishi machafu. Haridhii kutoka kwa waja Wake kufuru na wala hapendi ufisadi. Na waja ndio wenye kutenda kihakika na Allaah ndio Kaumba matendo yao.

Muumini na kafiri, mchaji Allaah na muasi, mwenye kuswali na mwenye kufunga, wote hawa ni waja. Waja wana uwezo na matakwa katika kufanya kwao matendo yao. Allaah Kawaumba na Kaumba uwezo wao na matakwa yao. Kama Alivyosema (Ta´ala):

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَوَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

”Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika njia

ya haki). Na hamtotaka isipokuwa Atakaye Allaah Mola

wa walimwengu.”(81:28-29)

Aina hii ya Qadar wanaikanusha al-Qadariyyah wote; ambao kawaita Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Waabudu moto wa Ummah huu.”[48]

Na upande mwingine, katika wale wanaothibitisha Qadar, wamechupa mipaka kwa hilo, mpaka wakakanusha uwezo wa mja na utashi wake na wakamtoa katika Matendo ya Allaah na hukumu Yake iliyo juu ya hekima na ustawi Wake.

 Imani, matendo na kauli

Katika misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuwa:

Dini na Imani ni kauli na matendo. Kauli ya moyo na ulimi, na matendo ya moyo na ulimi na viungo. Imani inazidi kwa utiifu na inashuka kwa maasi. Pamoja na hivyo, wao hawawakufurishi[49] Waislamu kwa kutenda maasi na madhambi makubwa, kama wanavofanya Khawaarij, bali udugu wa Imani bado upo pamoja na kuwa kwa maasi. Kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Aayah ya kisasi:

فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ

”Na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema naye alipe kwa ihsani.” (02:178)

Na Akasema (Subhaanahu):

وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ۚ فَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ

”Na mataifa (au makundi) mawili ya Waumini yakipigana, basi suluhisheni baina yao. (Lakini) mojawapo likikandamiza jengine, basi lipigeni (vita) lile linalokandamiza mpaka lielemee kwenye amri ya Allaah. Likishaelemea, basi suluhisheni baina yao kwa uadilifu, na fanyeni haki. Hakika Allaah Anapenda wafanyao haki. Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina

 ya ndugu zenu.”(49:09-10)

Hawapingi Imani ya Muislamu mtenda madhambi moja kwa moja[50] na wala hawasemi kuwa atadumishwa milele Motoni, kama wanavosema Mu´tazilah, bali Muislamu mtenda madhambi anaingia pia katika Imani. Kama ilivyo katika Kauli Yake (Ta´ala):

فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ

”Basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumin.”(04:92)

Na wakati mwingine yawezekana akawa haingii katika Imani kamilifu. Kama ilivyo katika Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا

”Hakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao, zinajaa khofu (na hushtuka), na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia iymaan.”(08:02)

Na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hazini mwenye kuzini pindi anapozini hali ya kuwa ni

muumini, na wala haibi mwenye kuiba pindi anapoiba hali ya kuwa ni muumini, na wala hanywi pombe pindi anapokunywa hali ya kuwa ni muumini, na hapori mwenye kupora pindi anapopora

kitu chenye thamani, jambo ambalo linafanya watu kumwangalia

 kwa ajili ya hilo, hali ya kuwa ni muumini.”[51]

Tunasema: “Ni muumini mwenye Imani pungufu” au “Ni muumini akiwa na Imani yake, mtenda dhambi kwa dhambi yake kubwa.” Kwa hali hiyo hapewi Imani kamilifu na wala haikanushwi moja kwa moja.

 Mfumo sahihi kuhusiana na Maswahabah

Katika misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni:

Wenye nyoyo na ndimi zilizo salama kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama Alivyowasifia Allaah katika Kauli Yake (Ta´ala):

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

”Na wale waliokuja baada yao (wenye) kusema: “Mola wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo (ya chuki, uadui, uhasidi, n.k.) kwa wale walioamini; Mola wetu! Hakika Wewe ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).”(59:10)

Na kumtii vile vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kauli yake:

“Msiwatukane Maswahabah wangu! Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Lau mmoja wenu atatoa dhahabu sawa na (mlima wa) Uhud, haitofikia Mudd[52] iliotolewa nao

wala nusu yake.”[53]

Wanayakubali yaliyokuja katika Kitabu, Sunnah na Ijmaa´ kutokana na fadhila na nafasi zao. Wanawafadhilisha waliojitolea na kupigana vita kabla ya ushindi – nayo ni suluhu ya Hudaybiyah - wao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao waliojitolea baadae na wakapigana. Na wanawatanguliza al-Muhaajiriyn[54] juu ya al-Answaar.[55] Wanaamini ya kwamba Allaah Kawaambia wale waliopigana vita vya Badr – na walikuwa miatatu na kumi na kitu:

“Fanyeni mtakacho. Nimeshawasamehe.”[56]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuwa:

“Hakuna yeyote kati yenu atoae bay´ah chini ya mti

satakayeingia Motoni.”[57]

Bali Yuko radhi nao, nao wako radhi Naye na walikuwa zaidi ya elfu moja na mianne.

Na wanamshuhudia[58] Pepo yule ambaye kamshuhudia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama wale (Maswahabah) kumi, na Thaabit bin Qays bin Shammaas na Maswahabah wengine.

Na wanayathibitisha yale yaliyopokelewa kwa njia nyingi kutoka kwa kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhu) na wengine, ya kwamba mbora wa Ummah huu baada ya Mitume wake ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan na kisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum), kama zilivyotolea dalili hivo Athaar. Hali kadhalika kama walivyokubaliana Maswahabah kumtanguliza ´Uthmaan kwa kumpa bay´ah, pamoja na kuwa baadhi ya Ahl-us-Sunnah wametofautiana kwa ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) – baada ya kukubaliana kwao kumtanguliza Abu Bakr na ´Umar – ni nani aliyebora. Kuna baadhi ambao wamemtanguliza ´Uthmaan kisha baada ya hapo wakanyamaza au wakasema kuwa wanne ni ´Aliy. Na baadhi ya wengine wakamtanguliza ´Aliy na wengine wakasimama.[59]

Lakini, mwishoni walikubaliana Ahl-us-Sunnah kumtanguliza ´Uthmaan kisha ´Aliy, hata kama masuala haya – kuhusu ´Uthmaan na ´Aliy - wengi katika Ahl-us-Sunnah wanaona kuwa sio ya msingi ambayo atahukumiwa upotevu yule atakayeyakhalifu, lakini masuala ambayo mtu atahukumiwa upotevu ni masuala ya Uongozi.[60]Hili ni kwa sababu wanaamini ya kwamba Khaliyfah[61] baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan na kisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Atakayekashifu uongozi wa mmoja katika maimamu hawa, basi ni mpotevu kuliko punda wake.

Wanawapenda na kufanya urafiki na watu wa nyumba ya Mtume[62] wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanafuata wasia wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema siku ya Ghadiyr Khumm:[63]

“Ninawakumbusha kwa Allaah kuhusiana na Ahl-ul-Bayt wangu! Ninawakumbusha kwa Allaah kuhusiana na Ahl-ul-Bayt wangu!”[64]

Kamwambia hali kadhalika ami yake Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye alikuwa amekuja kushtaki ya kwamba baadhi ya Quraysh wanawachukia Banuu Haashim. Akasema:

“Ninaapa kwa Yule ambaye Nafsi yangu iko Mkononi Mwake. Hawatoamini mpaka wawapende kwa ajili ya Allaah na kwa ukaribu[65] wenu kwangu.”[66]

Na akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah Kawachagua Banuu Ismaa´iyl. Na kutoka Banuu Ismaa´iyl Kachagua Kanaanah. Na kutoka Kanaanah Kachagua Quraysh. Na kutoka Quraysh Kachagua Banuu Haashim na Kanichagua

mimi kutoka Banuu Haashim.”[67]

Hali kadhalika wanawapenda na kufanya urafiki na wake za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wao ni wamama wa waumini. Na wanaamini ya kwamba wao ndio wake zake Aakhirah, na hususan Khidiyjah (Radhiya Allaahu ´anha) ambaye ni mama wa watoto wake wengi. Na yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumuamini na kumsaidia kwa kazi yake na alikuwa ni mwenye manzilah ya juu kwake.

Na asw-Swiddiyqah bint asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhumaa),[68] ambaye kasema Mtume kuhusu yeye:

“Ubora wa ´Aaishah kwa kulinganisha na wanawake wengine ni kama ubora wa Thariyd[69] kulinganisha na chakula kingine.”[70]

Na wanajiweka mbali na njia ya Rawaafidhw, ambao wanawachukia na kuwatukana Maswahabah, hali kadhalika Nawaasib, ambao wanawaudhi Ahl-ul-Bayt, aidha kwa kauli au matendo.

Na wanayanyamazia yaliyopitika baina ya Maswahabah na wanasema:

“Kati ya mapokezi haya yaliyokuja kuna ambayo ni ya uongo, na kuna ambayo yamezidishwa juu yake na kupunguzwa, na kuna ambayo yamebadilishwa kwa sura yake ya kihakika na ndani yake kuna ya sahihi ambayo wamepewa udhuru kwayo. Ima walikuwa ni wenye kujitahidi baada ya kuifikia haki wakapatia, au walikuwa ni wenye kujitahidi baada ya kuifikia haki wakakosea.”

Wao pamoja na hivyo hawaitakidi ya kwamba kila mmoja katika Maswahabah kakingwa na madhambi makubwa au madogo. Bali kinyume chake kuna uwezekano wakafanya madhambi kwa ujumla. Wana haki ya kutangulizwa na fadhila ambazo zinafanya wanasamehewa kwa lile wangelolifanya – ikiwa wamefanya kitu. Wanasamehewa hata madhambi ambayo yasingelisamehewa kwa mwengine yeyote baada yao, kwa kuwa wana mema mengi ambayo hana yeyote wa baada yao, na ambayo vile vile yanafuta makosa yao.

Kumethibiti kwa kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba wao ndio karne bora na kwamba akitoa Swadaqah mmoja wao kiasi cha Mudd ina uzito zaidi kuliko inayotolewa na aliye baada yao, hata kama huyu atatoa dhahabu sawa na kiasi cha mlima wa Uhud.

Ikiwa mmoja wao atapitikiwa na dhambi, atakuwa ima katubia kwa dhambi hiyo, au kaleta mema ambayo yameifuta au amesamehewa kwa fadhila za kutangulia kwake, au (kasamehewa) kwa Shafaa´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – na hakuna ambaye ana haki zaidi kwa Shafaa´ah yake isipokuwa wao – au kapewa mtihani kwa majaribio ya duniani ambayo yamefuta dhambi yake.

Ikiwa madhambi haya yaliyofanywa yanafanywa namna hii, vipi kwa mambo ambayo walikuwa ni wenye kujitahidi kuifikia haki? Ikiwa wamepatia wana ujira mara mbili na wakikosea wana ujira mara moja na kosa lao limesamehewa. Isitoshe, matendo mabaya yaliyofanywa na baadhi yao ni machache mno na yasiyokuwa na maana ukilinganisha na fadhila za nafasi yao na mema yao, kama kwa mfano kumuamini Allaah na Mtume Wake, na kupigana Jihaad katika njia ya Allaah, Hijrah, nusra, elimu yenye manufaa na matendo mema n.k. Yule atakayetazana maisha[71] ya Maswahabah kwa elimu na uwazi na fadhila Alizowaneemesha Allaah kwazo, basi atajua kwa yakini ya kwamba wao ndio viumbe bora baada ya Mitume. Kamwe hakukuwahi kuwepo na hakutokuwepo mtu mfano wao. Wao ndio wasomi wa wasomi katika Ummah huu – ambao ndio bora wa wabora na wa karimu kwa Allaah (Ta´ala).

 Kuamini karama za Mawalii[72]

Katika misingi ya Ahl-us-Sunnah ni:

Kusadikisha karama za mawalii na yale matukio yasiyokuwa ya kawaida ambayo Allaah Hufanya yakapitia kwao, aidha katika aina mbali mbali za elimu,[73] maono, uwezo maalum na taathira, na yaliyopokelewa kuhusu watu waliotangulia katika Suurat al-Kahf na kadhalika. Hali kadhalika kuhusu watu waliotangulia katika Ummah huu miongoni mwa Maswahabah, Taabi´iyn na watu wa Ummah zingine zilizobaki, nayo yataendelea kuwepo mpaka siku ya Qiyaamah.

 Kufuata Njia ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake

Katika njia ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni:

Kufuata mapokezi[74] ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa undani na kwa uinje, na kufuata njia ya waliotangulia katika al-Muhaajiriyn na al-Answaar, na kufuata wasia wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi aliposema:

“Shikamaneni na Sunnah zangu na hali kadhalika

mshikamane na Sunnah za Makhalifah wangu waongofu baada yangu. Shikamaneno nazo bara bara na ziumeni kwa majego yenu. Na tahadharini na yakuzua, kwani hakika kila Bid´ah ni upotevu.”

Na wanajua ya kwamba hakika ya maneno ya kweli kabisa, ni Maneno ya Allaah, na uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanaacha Maneno ya Allaah yatangulie mbele kabla ya maoni ya watu wengine na wanatanguliza uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya uongofu wa wengine wote. Na kwa ajili hii ndio wakaitwa “Ahl-ul-Kitaab was-Sunnah”[75]. Wanaitwa vile vile Ahl-ul-Jamaa´ah” kwa kuwa “Jamaa´ah” ni ile iliokusanyika. Na kinyume chake ni “al-Furqa”[76], hata kama lafdhi ya “al-Jamaa´ah” imekuwa ni jina la watu wote waliokuwa kitu kimoja.

Ijmaa´ ndio chanzo[77] cha tatu inayotegemewa katika elimu na Dini. Nao Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanapima[78] kwa misingi hii mitatu mambo yote ya Dini kuhusiana na maneno na matendo ya watu, sawa yaliyojificha na yaliyodhahiri. Ijmaa´ ni yale waliokubaliana Salaf as-Swaalih,[79] kwa kuwa baada yao kulikithiri tofauti na Ummah ukagawanyika ukaenea.

 Sifa tukufu za Ahl-us-Sunnah

Pamoja na misingi hii wanaamrisha mema na wanakataza maovu kwa yale ambayo Shari´ah imeyawajibisha. Wanaonelea kufanya Hajj, kupigana Jihaad, Swalah ya Ijumaa na sikukuu pamoja na viongozi, sawa wakiwa wema au waovu. Wanahifadhi Swalah ya Jamaa´ah na wanaona kuwapa naswaha Ummah ni katika sehemu ya Dini. Na wanaamini maana ya kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”

Halafu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakutanisha baina ya vidole vyake viwili.[80]

Na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mfano wa waumini, katika kupendana kwao, na kuhurumiana kwao na kuhisiana kwao, ni kama mfano wa mwili mmoja. Wakati kiungo cha mwili kinapatwa na maumivu, mwili mzima

unapatwa na homa.”[81]

Na wanaamrisha kuwa na subira wakati wa mitihani, kuwa na shukurani wakati wa raha na kuridhia kwa shida iliyokadiriwa. Wanalingania katika tabia nzuri na matendo mema. Na wanaamini maana ya kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini mwenye Imani kamilifu ni yule mwenye tabia

nzuri zaidi.”[82]

Na wanahimiza uunge uhusiano na yule uliyekata nae, na ummpe yule uliyemnyima, umsamehe yule aliyekudhulumu na kukufanyia ubaya.

Na wanaamrisha kuwatendea wema wazazi wawili na kuunga udugu, kuwatendea wema majirani, kuwafanyia wema mayatima na masikini, na wasafiri na watumwa.

Na wanakataza kujiona na kiburi, ukandamizaji na unyanyasaji kwa viumbe, sawa kwa haki au pasina haki.

Na wanaamrisha kuwa na maadili mema na wanakataza mabaya.

Na katika kila wanayoyasema na kuyafanya – katika haya na mengine – wanafuata Kitabu na Sunnah. Njia yao ni Dini ya Uislamu ambayo Allaah Kamtuma kwayo Muhamammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini alipoelezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba Ummah wake utagawanyika kwa mapote sabini na tatu na yote yataingia Motoni isipokuwa limoja, nayo ni al-Jamaa´ah.”[83]

Na katika Hadiyth nyingine kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Ni wale ambao watakuwemo kwa mfano wa yale niliyomo leo na Maswahabah zangu.”[84]

wamekuwa wale wenye kushikamana bara bara na Uislamu wa wazi na msafi kabisa, ni “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah”. Na miongoni mwao kuna wakweli, mashahidi na watu wema na vile vile kuna wenye kuzuia uongofu na giza la kwenye mwangaza. Wana nafasi kuu na fadhila zingine tulizozitaja. Miongoni mwao kuna ´Abdaal[85] na maimamu[86] wa Dini ambao wamekusanyika Waislamu kwa uongofu wao.

Nao ni at-Twaaifah al-Mansuurah, ambao kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuhusu wao:

“Na hakitoacha kikundi katika Ummah wangu kuwa ni chenye kunusuriwa juu ya haki. Hatowadhuru yule mwenye kuwakhalifu na kuwapinga mpaka itapofika Qiyaamah.”[87]

 Hitimisho

Tunamuomba Allaah Atujaalie katika wao, na wala Asizipotoe nyoyo zetu baada ya Kutuongoza na Aturehemu. Hakika Yeye Ndiye Al-Wahhaab. Na Allaah Anajua zaidi. Swalah na salaam zimwendee Muhammad, ahli zake, Maswahabah wake wote.[1] Pote lililookolewa na kunusuriwa

[2] Kujielezea

[3] Kubadilisha maana

[4] Kukanusha maana

[5] Kuanisha maana au kuulizia namna yake

[6] Kufananisha

[7] Ilhaad. Kasema Shaykh-ul-Islaam Ibn-ul-Qayyim al-Jawziyyah (Rahimahu Allaah): ”Ilhaad katika Majina Yake maana yake ni kuyageuza, tafsiri na maana yake ya kweli kutoka katika uthibitisho wake wa haki.” (Badaa´-ul-Fawaa-´id, uk. 169).

[8] Aayah

[9] Ujuzi wa Allaah

[10] Aliyomuelezea

[11] al-Bukhaariy (1145) na Muslim (758).

[12] al-Bukhaariy (6309) na (2747).

[13] al-Bukhaariy (2826) na Muslim (1890).

[14] Ahmad (4/11) na Ibn Maajah (181). Katika isnadi kuna udhaifu. Katika isnadi amekuja Wakiy´ bin Hadas. Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kasema kuwa ni mdhaifu katika ”Sunan Ibn Maajah”. Hata hivyo Hadiyth iliyopokelewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu): ”Allaah (´Azza wa Jalla) Hustaajabu kwa huyu na huyu... ” ni Swahiyh. (Tazama Swahiyh al-Bukhaariy (4889)).

[15] al-Bukhaariy (7384) na Muslim (2848).

[16] al-Bukhaariy (6529) na Muslim (322).

[17] al-Bukhaariy (6539) na Muslim (1016)

[18] Abuu Daawuud (3892), an-Nasaa´iy (1037), al-Haakim (1/344) na (3/218) na wengine.

[19]al-Bukhaariy (3451) na Muslim (1064).

[20] Abuu Daawuud (3451). Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kasema kuwa ni dhaifu katika kitabu cha Ibn Abiy ´Aasim ”Kitaab-us-Sunnah” (577).

[21] Muslim (537).

[22] Abuu Nu´aym (6/124). Katika isnadi kuna udhaifu. Katika isnadi kumekuja Nu´aym bin Hamaad. Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kasema kuwa ni mdhaifu katika ”Dhwa´iyf al-Jaami´ as-Swaghiyr” (1100).

[23] al-Bukhaariy (406) na Muslim (547).

[24] Muslim (2713).

[25] al-Bukhaariy (4205) na (6384) na Muslim (2704).

[26] al-Bukhaariy (554) na (574) na Muslim (633).

[27] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) anasema: ”Vipi tutamwita yule mwenye kufanya dhambi kubwa? Muumini au kafiri? Ahl-us-Sunnah wako kati ya pande mbili: Haruuriyyah na Mu´tazilah wako katika upande mmoja na Murji-ahJahmiyyah katika upande mwingine. Haruuriyyah na Mu´tazilah wanamtoa katika Imani, lakini Haruuriyyah wanasema: ”Ni kafiri ambaye mali yake ni halali kuichukua.” Kwa ajili hii ndio maana wakawafanyia uasi watawala na kuwachukulia watu kuwa ni makafiri. Ama kuhusiana na Murji-ah Jahmiyyah wamekwenda kinyume na hawa na kusema: ”Ni muumini mwenye Imani kamili! Anaiba, kufanya Zinaa, kunywa pombe, kuua na kupora na wakati huo huo tunamwambia: ”Wewe ni muumini mwenye Imani kamili kama jinsi alivyo mtu mwenye kufanya ´Ibaadah za wajibu na za Sunnah na kujiepusha na ya haramu yote! Wewe na yeye mna Imani sawa sawa.” Hivyo hawa na wale wanatofautiana.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk 71-72, iliyochapishwa na Daar Ibn-ul-JAwziy).

[28] Ni wale wanaojiita Shiy´ah (Mashia) leo.

[29] Rubuubiyyah

[30] Kweli

[31] Tazama footnote ya 25

[32] al-´Uluw

[33] Hadithi

[34] Namna

[35] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Hichi ndio kiwango cha juu kabisa jasho itafikia. Wengine kuna ambaye itamfikia vifundoni na mwengine kwenye magoti n.k. Siku hii watatokwa na jesho kwa sababu ya joto, kwa kuwa watakuwa katika mahali pa msongamano sana ambapo watapitia matatizo makubwa sana na ambapo jua litajongezwa karibu sana. Watu watatokwa na jasho kwa sababu ya yatakayopitika siku hiyo, lakini kila mmoja ni kutokana na matendo yake.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 136-137, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy)

[36] Swiraat/Siraat

[37] Uombezi

[38] Nafasi hiyo

[39] Ahmad (5/317), Abuu Daawuud (4700), at-Tirmidhiy (2155) na (3319). Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kasema kuwa ni Swahiyh katika kitabu cha Ibn Abiy ´Asim “Takhrij-us-Sunnah” (102-105).

[40] Yaani yanatii

[41] al-Janiyn

[42] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Yaani elimu hii na maandiko. al-Ghulaat al-Qadariyyah walikanusha hili mwanzoni na kusema: ”Allaah Anajua matendo ya waja kwanza baada ya kuwa yameshafanywa na hayajaandikwa.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyya, mjaladi. 2, uk. 203, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy).

[43] Matakwa

[44] al-Muttaqiyn

[45] Al-Muhsiniyn

[46] al-Muqsitwiyn

[47] Qawm al-Faasiqiyn

[48] Abuu Daawuud (4691) na al-Haakim (1/85). Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kasema kuwa ni Hasan katika kitabu cha Ibn Abil-´Izz al-Hanafiy ”Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah” (284).

[49] Kumwambia Muislamu ambaye kafanya dhambi chini ya Shirki kuwa ni kafiri.

[50] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawapingi Imani ya Muislamu mtenda madhambi moja kwa moja. Hawasemi: ”Sio Muislamu” bali wanasema: ”Ana Uislamu pungufu” au ”Ana Imani pungufu”.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 241, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy).

[51] al-Bukhaariy (2475) na Muslim (57).

[52] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Mudd ni sawa na kama robo hivo.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 252, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy).

[53] al-Bukhaariy (3673) na Muslim (2541).

[54] Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) waliotoka Makkah wakahamia Madiynah

[55] Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wa Madiynah waliowapokea al-Muhaajiriyn

[56] al-Bukhaariyt (3007) Muslim (2494).

[57] Abuu Daawuud (4649) na (4650), at-Tirmidhiy (3748) na (3757), Ibn Maajah (134) na wengine. Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kasema kuwa ni Swahiyh katika “Swahiyh al-Jaamiy´ as-Swaghiyr” (4010).

[58] Wanamtolea ushahidi wa Pepo

[59] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Walisema: ”Abu Bakr na kisha ´Umar, kisha hawakusema kitu kuhusu ´Uthmaan na ´Aliy na ni nani ambaye ni mbora katika yao.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 270, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy)

[60] Khilaafah

[61] Kiongozi

[62] Ahl-ul-Bayt

[63] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Siku ya Ghadiyr Kumm ni siku ya nane ya Dhul-Hijjah... ” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 275, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy)

[64] Muslim (2408). Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Yaani, ninawakumbusha kwa kumcha Allaah na kisasi Chake ikiwa mtakiuka haki za Ahl-ul-Bayt wangu, na kumbukeni Rahmah na thawabu Zake ikiwa mtawap haki zao.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 275, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy)

[65] Yaani na kwa kuwa nyinyi ni familia yangu

[66] Ahmad katika ”Fadhwaail-us-Swahabah” (1756).

[67] Muslim (2276).

[68] ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha)

[69] Ni mkate uliokuwa ukionekana ni mtamu sana wakati huyo unaowekwa kwenye mchuzi wa nyama

[70] al-Bukhaariy (3770) na Muslim (2446).

[71] Siyrah

[72] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Ni kina nani mawalii? Jibu ni Kauli ya Allaah: ”Tanabahi!  Hakika awliyaa wa Allaah (vipenzi Vyake wanaoamini Tawhiyd ya Allaah na kufuata amri Zake) hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika. Wale walioamini na wakawa wana taqwa (wanafuata amri za Allaah na Mtume Wake Muhammad صلى الله عليه وسلم)”. (10:62-63). Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) kasema: ”Yule ambaye ni muumini na ni mchaji Allaah ni wali. Uwalii sio kitu kinachofikiwa kwa madai na kutamani, isipokuwa ni kwa imani na uchaji Allaah. Ikiwa mtu atamuona mtu na kusema: ”Ni walii” wakati huo huo hamchi Allaah (Ta´ala), yanarudishwa madai yake.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 297, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy)

[73] Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Mfano wa hilo ni yale aliyotaja Abu Bakr; Allaah Alimfanya Akajua ni jinsia gani iliyokuja kwenye tumbo la mke wake, nayo ilikuwa ni binti.” (”Karamaat-ul-Awliyaa´ (63)) (ibid. uk. 304) cha al-Laalikaa´iy. 

[74] Athaar

[75] Watu wa Qur-aan na Sunnah

[76] Mgawanyiko, mpambanuo

[77] Msingi

[78] Hukumu

[79]Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Jibriyn (Rahimahu Allaah):

“Salaf (waliotangulia) ni karne bora katika Maswahabah, kisha waliofuata na kisha waliofuata.”

(at-Ta´liyqaat ´alaa Matn Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 50, Daar-us-Samiy´iy).

[80] al-Bukhaariy (6026) na Muslim (2585).

[81] al-Bukhaariy (6011) na Muslim (2586).

[82] Ahmad (2/472), Abuu Daawuud (4682) na at-Tirmidhiy (1162). Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kasema kuwa ni Swahiyh katika “Swahiyh at-Tirmidhiy” (3/886).

[83] Abu Daawuud (4596), Ahmad (2/333), at-Tirmidhiy (2778). Ibn Maajah (3991) na wengine. Tazama “as-Silsilah as-Swahiyhah” (204) ya Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah).

[84] at-Tirmidhiy (2779) na al-Haakim (1/129).

[85] Umoja. Badala (mbadala). Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kasema: ”Wao ni maalum kutokana na hao wengine kwa elimu na ´Ibaadah. Wamepata jina ´Abdaal” aidha kwa sababu wakati mmoja wao anapofariki, huja badala yake mwengine, au kwa sababu walikuwa wakiyabadili matendo yao mabaya kwa mazuri, au kwa sababu walikuwa kiigizo chema ambao walikuwa wakibadili matendo ya makosa ya watu kwa mazuri.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, mjaladi. 2, uk. 376, iliotolewa na Daar Ibn-ul-Jawziy).

[86] Umoja. Imamu. Wingi. Maimamu. Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) anasema: ”Imaam ni kiigizo chema.” (ibid.).

[87] al-Bukhaariy (3641) na Muslim (1037).