دين الحق

 Dini ya kweli

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu.

 Utangulizi na Muongozo

Shukrani zote njema anastahiki Mola wa viumbe wote,na rehema na amani ziwe juu ya Mitume wote wa Mwenyezi Mungu, na Baada ya kusema hayo:

Huu ni wito wa mafanikio ,nauelekeza kwa kila mtu mwenye akili -sawa awe mwanaume au mwanamke - Hali ya kutarajia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenye uwezo,awape taufiq kwa kupitia wito huu wale wote waliopotea katika njia yake, na anilipe mimi thawabu na kila ambaye atatoa juhudi katika kukisambaza kitabu hiki thawabu nyingi,na ninasema Mwenyezi Mungu ndiye atakiwae msaada:

Tambua ewe mwanadamu mwenye akili- yakuwa hakuna mafanikio wala utukufu katika maisha ya akhera baada ya kufa isipokuwa tu utakapo mjua Mola wako ambaye amekuumba,na ukamuamini na kumfuata,na ukaijua dini ya haki ambayo amekuamrisha Mola kuifuata na kuiamini dini hiyo na ukatenda kwa mujibu wa dini hiyo.

Na hiki kitabu mbele yako kiitwacho (Diinul Haqqi -Yaani: dini ya haki) ndani yake kimebainisha mambo makubwa, ambayo inakupasa kuyajua na kuyafanyia kazi, na nimetaja chini ya ukurasa baadhi ya maneno na mas'ala kwa ajili ya kuweka wazi zaidi,nikitegemea katika mambo haya yote kitabu cha Mwenyezi Mungu na Hadithi za bwana Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kwa sababu maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo marejeo ya Dini ya haki ambayo hamkubalii Mwenyezi Mungu mtu yeyote atakaye fuata dini isiyokuwa ya haki (Uislamu).

Kwa hakika nimewacha ufuataji wa kiupofu ambao umewapoteza watu wengi, bali nimetaja baadhi ya makundi mapotofu ambayo yanadai kuwa yapo kwenye haki,na hali yakuwa yapo mbali na haki, nimeyetaja ili kuwatahadharisha na hali ya makundi hayo wale wasiojua katika wafuasi wa makundi hayo.

Ameyasema na ameyaandika: mwenye kutarajia msamaha wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Abdul Rahman Ibnu Hammad Aali Omar.

Mtaalamu na mwalimu wa masomo ya Dini.

 Sehemu ya kwanza- Ni kumjua Mwenyezi Mungu (1) Muumba Mtukufu

Tambua- ewe mwanadamu mwenye akili- ya kuwa Mola wako ambaye amekuumba kutokana na kutokuwepo na akakulea kwa kukupa neema yeye ndiye Mola wa viumbe wote,na wenye akili wanaomwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu. ([1]) hao waumini hawakumuona kwa macho yao,lakini wameona alama zenye kujulisha uwepo wake,na kuwa yeye ndiye muumba mwenye kuwasimamia viumbe wote wakamjua kwa hilo,na wakamjua kwa hizi alama.

Alama ya kwanza:

Ulimwengu na mwanadamu na maisha: ni vitu vilivyozuka na vina mwanzo na mwisho, na vinahitajia kingine,na chenyekuzuka na kuhitajia kingine,lazima kitakuwa ni kiumbe,na kiumbe lazima awepo aliyekiumba,na huyu muumba Mtukufu ni Mwenyezi Mungu,na Mwenyezi Mungu ndiye ambaye ameuelezea mwenyewe utukufu wake,na kuwa yeye ndiye muumba mwenye kusimamia viumbe wote,na utambulisho huu umekuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika vitabu vyake ambavyo ameviteremsha kwa Mitume wake.

Na kwa hakika Mitume wa Mwenyezi Mungu walifikisha maneno yake kwa watu,na wakawalingania kuyaamini maneno yake,na nakumuabudu yeye peke yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kitabu chake ambacho ni Qur'ani tukufu: Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi kwa siku sita. kisha akawa juu ya Arshi yake. Huufunika usiku kwa mchana,uufuataao upesi upesi Na ameliumba jua na mwezi na nyota na vyote vimetiishwa kwa amri yake Mwenyezi Mungu. Fahamuni kuumba ni kwakwe tu mwenyewe (Mwenyezi Mungu) na amri zote ni zake (Mwenyezi Mungu) ametukuka Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote. Surat- Al- aaraaf Aya ya 54

Maana ya ujumla wa Aya hii

Anawapa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu watu wote, kuwa yeye ni Mola wao,ambaye amewaumba , na akaumba mbingu na ardhi kwa siku sita , na anatoa habari kuwa yeye amelingana sawa juu ya Arshi yake.

Na Arshi ipo juu ya mbingu,na ni kiumbe kilichopo juu na nikipana kuliko viumbe vingine,na Mwenyezi Mungu yupo juu ya hii Arshi naye yupo pamoja na viumbe wote kwa ujuzi wake na usikivu wake na kuona kwake, hakijifichi chochote katika mambo yao,na anatoa habari Mwenyezi Mungu- Liliyetukuka jambo lake- kuwa yeye ameufanya usiku ni wenye kuufunika mchana kwa giza lake,na hulifuata kwa haraka, na hutoa habari kuwa yeye ameumba jua na mwezi na nyota , na akavifanya vyote hivyo ni vyenye kutii, vinakwenda katika njia zake kwa amri yake, na anatoa habari kuwa yeye peke yake ndiye mwenye kuumba na kuamrisha, na yeye Mtukufu aliyekamilika katika dhati yake na sifa zake, ambaye anatoa kheri nyingi zenye kudumu, na yeye ndiye Mola wa viumbe wote, ambaye amewaumba wao na akawalea kwa neema nyingi.

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na miongoni mwa alama za uwepo wa Mwenyezi Mungu, ni usiku na mchana , na mwezi na jua, msilisujudie jua wala mwezi, na sujuduni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ambaye ameviumba vyote hivyo ikiwa nyinyi mnamuabudu yeye. Surat Fuswilat Aya ya (37)

Maana ya ujumla wa Aya hii Tukufu

Anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa miongoni mwa alama zinazomtambulisha: ni usiku na mchana na jua na mwezi, na anakataza kulisujudia jua na mwezi kwa sababu ni viumbe kama viumbe vingine, na kiumbe hafai kuabudiwa, na kusujudu ni miongoni mwa ibada, na anawaamrisha Mwenyezi Mungu watu katika hii aya- kama anavyo waamrisha katika aya zingine- kuwa wamsujudie yeye peke yake, kwa kuwa yeye ndiye muumba muendeshaji anayestahiki kuabudiwa.

Alama ya Pili:

Ni kwamba yeye ameumba jinsia ya kike na kiume: nakuwepo jinsia ya kike na kiume ni alama ya kuwepo muumba.

Alama ya Tatu :

Ni kutofautiana lugha na rangi: na hawapatikani watu wawili wenye kufanana sauti zao zikawa moja au rangi zao kuwa ni moja, bali ni lazima zitofautiane.

Alama ya Nne:

Kutofautiana vipawa: huyu tajiri na huyu masikini, na huyu raisi na raia na hali yakuwa wote hao wana akili, na wanafikra na elimu, na kuwa na pupa kwa yule ambaye bado hajapata utajiri cheo na mke mzuri, lakini hakuna yeyote awezaye kuvipata hivyo isipokuwa yule ambaye

Amemkadiria Mwenyezi Mungu, na kufanya hivyo ni kwa hekima kubwa aliyoikusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu ([2]) Na huko ni kuwapima watu wao kwa wao, na kuwahudumia baadhi yao wengine ili yasipotee maslahi yao yote.

Na yule ambaye hajakadiriwa na Mwenyezi Mungu kupata cheo hapa duniani, ametoa habari Mwenyezi Mungu kuwa anamlimbikizia mtu huyo katika neema zake peponi ikiwa atakufa akiwa anamuamini Mwenyezi Mungu, japokuwa Mwenyezi Mungu kwa kawaida amempa fakiri ziada ambayo anastarehe kwayo ndani ya nafsi na kiafya, ziada ambayo haipo kwa matajiri wengi, na hii ni hekima ya Mwenyezi Mungu na uadilifu wake.

Alama ya Tano:

Kulala usingizi, na ndoto za kweli ambazo Mwenyezi Mungu humuonyesha mwenye kulala vitu vya mbali ikiwa ni bishara au onyo.

Alama ya Sita :

Ni Roho: ambayo hakuna ajuae uhakika wake isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Alama ya Saba :

Ni mwanadamu na yale yaliyoko mwilini mwake kuanzia hisia na mfumo wa neva (mfumo unaoratibu matendo ya hiari) na ubongo, na mfumo wa kumeng'enya chakula, na vinginevyo.

Alama ya Nane:

Huteremsha Mwenyezi Mungu mvua katika ardhi iliyokufa na huota mimea na miti yenye kutofautiana muonekano na rangi, na manufaa yake na pia ladha yake, na hizi ni alama chache tu miongoni mwa alama nyingi ambazo amezitaja Mwenyezi Mungu katika Qur'ani, na ambazo amezitaja kuwa ni alama zinazojulisha juu ya uwepo wake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na zinajulisha kuwa yeye ni muumba mwenye kusimamia viumbe vyote.

Alama ya Tisa:

Umbile ambalo Mwenyezi Mungu amewaumbia nalo wanadamu, huleta hutia imani ya uwepo wa Mwenyezi Mungu mumba wa hilo umbile na msimamizi wake, na mwenye kupinga hilo hakika anaichanganya nafsi yake mwenyewe na kuipotosha, Kwa mfano Mkomonisti ([3]) anaishi katika haya maisha akiwa ni mwenye kukata tamaa, mafikio yake baada ya kufa ni motoni, ikiwa ni malipo ya kupinga uwepo wa Mola wake ambaye amemuumba kutokana na kutokuwepo, na akamlea kwa kumpa neema nyingi, isipokuwa atakapo tubia kwa Mwenyezi Mungu na akamuamini yeye na dini yake na mitume wake.

Alama ya Kumi:

"Al-barakat" ni wingi na kuzidi baadhi ya viumbe kama mbuzi, na kinyume chake ni "Alfashal" ni uchache na kupungua kwa baadhi ya viumbe kama vile mbwa na paka .

Na katika sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuwa yeye.

Ni wa kwanza hakuna kabla yake yeyote, yupo Hai wakati wote, hafi wala hana mwisho, ni Tajiri mwenye kujitosheleza, hahitajii kwa yeyote, na ni mmoja hana mshirika wake Amesema Mwenyezi Mungu: Sema, yeye ndiye Mwenyezi Mungu mmoja tu.(1) Mwenyezi Mungu ndiye mkusudiwa kwa kila haja (2) «Hakuzaa wala hakuzaliwa «Wala hana yeyote mwenye kufanana nae [Surat Al Ikhlaswi: 1-4].

Maana ya hizi Aya .

Makafiri walipomuuliza mwisho wa mitume kuhusu sifa za Mweyezi Mungu; aliwateremshia sura hii na akamuamrisha katika sura hii aseme kuwaambia hao makafiri.

Kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja hana mshirika wake, Mwenyezi Mungu yeye yupo hai na ni mwenye kuendesha mambo, yeye pekee ndiye mwenye ubwana wa kudumu juu ya ulimwengu na watu na kila kitu, na kwake peke yake yapasa watu wote kurudi katika kutekeleza haja (mahitaji) yao.

Hakuzaa wala hakuzaliwa, wala siyo sahihi awe yeye ana mtoto wa kiume au kike au baba au mama, bali amepinga kwa nguvu zote jambo hilo katika nafsi yake kwenye sura hii na zingine, kwa sababu mpangilio wa kuzaa ni sifa za viumbe, na hakika amejibu kauli ya manaswara (wakiristo) waliposema (Masihi (kristo) ni mtoto wa Mwenyezi Mungu) na akawajibu mayahudi kauli yao waliposema uzairu ni mtoto wa Mwenyezi Mungu na akawajibu wengine waliosema: malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akawasema vibaya kwa hii kauli ambayo ni batili.

Na ametoa habari kuwa yeye amemuumba Masihi Issa - juu yake amani -kutokana na mama bila ya baba kwa uwezo wake, kama mfano alivyomuumba Adamu baba wa wanaadamu kwa udongo, na kwa mfano alivyomuumba Hawa mama wa wanadamu kutokana na ubavu wa Adamu akamuona pembeni mwake, kisha akaumba kizazi cha Adamu kutokana na maji ya mwanaume na mwanamke, hakika alikiumba kila kitu mwanzoni kutokana na kutokuwepo,na akawawekea viumbe vyake baada ya kuwaumba utaratibu na nidhamu ambayo hawezi yeyote asiyekuwa yeye kuzibadilisha, na akitaka Mwenyezi Mungu kubadilisha chochote katika hizi nidhamu basi hubadilisha atakavyo.

Kama alivyo jaalia kupatikana Issa -Iwe juu yake Amani- kutokana na mama bila baba na kama alivyo mjaalia aongee akiwa mtoto mchanga, na kama alivyoigeuza fimbo ya Musa -Iwe juu yake Amani- kuwa ni nyoka mwenye kwenda, na alipopiga kwa fimbo hiyo bahari ilipasuka na ikawa ni mapito, akavuka hapo Musa na watu wake, kama alivyompasulia Mwezi Mtume wa mwisho ambaye ni Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, na akaifanya miti inamsalimia anapopita, akawafanya wanyama ni wenye kutoa ushuhuda wa Utume wake kwa sauti wanayoisikia watu, wakisema:Tunashuhudia kuwa wewe ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ulipelekwa kwake kwa kupanda mnyama Buraku kutoka msikiti mtukufu wa Makka mpaka msikiti wa Aqswa, kisha ukapandishwa mpaka mbinguni ukiwa na Malaika Jibrili mpaka ukafika mbinguni, Mwenyezi Mungu akamsemesha -kutakasika na sifa za mapungufu ni kwake- na akamfaradhishia sala na karudi mpaka msikiti wa Makka katika ardhi, na akawaona njiani wote walio katika mbingu, na yote hayo yalikuwa katika usiku mmoja tu kabla ya kuchomoza Alfajiri, na kisa cha Israa na Miraji ni mashuhuri katika Qur'ani na katika Hadithi za Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na pia katika vitabu vya Historia.

Na katika sifa za Mwenyezi Mungu ambazo amejisifia nazo mwenyewe na wakamsifia kwa sifa hizo mitume wake:

1- Nikusikia na kuona, na elimu na uwezo na matashi, anasikia na anaona kila kitu, hakuna kizuizi kinachozuia kusikia kwake na kuona kwake.

Anajua yaliyo ndani ya vizazi, na yaliyofichikana ndani ya vifua, na vitu vilivyokuwapo na vitakavyokuwapo, na yeye ni muweza ambaye akitaka kitu chochote hukiambia: kuwa na kinakuwa.

2- Huongea atakacho wakati atakapo: na hakika alimsemesha Mussa- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kamsemesha mwisho wa Manabii-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, na Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu kwa herufi zake na maana zake aliiteremsha kwa Mtume wake Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, hivyo ni sifa katika sifa zake na Qur'an siyo kiumbe kama wanavyosema kundi potovu la Muutazilah.

Uso na mikono miwili, na kulingana sawa na kushuka ([4]), na kuridhia na kukasirika. Hivyo yeye huwaridhia waja wake wenye kumuamini na huwakasirikia wenye kumkufuru, na pia mwenye kufanya mambo yenye kupelekea kuchukia, na kuridhia kwake na kuchukia kwake ni kama sifa zingine zilizobakia, hazifanani na sifa za viumbe wala hazibadilishwi wala hazitolewi mfano wa namna yake.

Imethibiti katika Qur'ani na Sunnah kwamba waumini watamuona Mwenyezi Mungu Mtukufu wazi wazi kwa macho yao wenyewe viwanja vya siku ya kiyama na katika pepo, na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu zimepambanuliwa katika Qur'ani tukufu na hadithi za Mtume Mtukufu Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Amani-, hivyo rejea vitabu hivyo.

Jambo ambalo kwa sababu yake Mwenyezi Mungu amewaumba wanadamu na majini

Ikiwa utajua -ewe mwenye akili- kwamba Mwenyezi Mungu ni Mola wako aliyekuumba; Basi jua kuwa Mwenyezi Mungu hakukuumba bila faida, na kwa hakika amekuumba ili umuabudu yeye; na ushahidi ni neno la Mwenyezi Mungu. {Sikuumba majini wala watu ila ni kwa lengo la kuniabudu} (56) Sitaki kutoka kwao riziki wala sitaki wanilishe. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mtoaji riziki mwenye nguvu madhubuti [Surat Dhaariat 56-58]

Maana ya Aya kwa ujumla:

Anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aya ya kwanza: kuwa yeye ameuwaumba majini ([5]) na wanadamu ili wamuabudu yeye peke yake. Na anatoa habari katika aya ya pili na ya tatu: kuwa yeye amejitosheleza na hahitajii toka kwa waja wake, hivyo hataki kutoka kwao riziki wala kulishwa; kwa sababu yeye ndiye mtoa riziki na mwenye nguvu, hakuna riziki itolewayo kwa watu na viumbe wengine ila kutoka kwake, na yeye ndiye mwenye kuteremsha mvua, na anatoa riziki kutoka ardhini.

Ama viumbe wengine ambao wapo katika ardhi, kwa hakika ametoa habari Mwenyezi Mungu kuwa ameviumba kwa ajili ya mwanadamu; ili vimsaidie kumtii Mwenyezi Mungu, na avitumie kwa mujibu wa sheria ya Mwenyezi Mungu, na kila kiumbe na kila mtikisiko na utulivu katika ulimwengu hakika Mwenyezi Mungu ameviweka kwa hekima ambayo ameibainisha katika Qur'ani, na wanajua hekima yake wajuzi wote wa sheria za Mwenyezi Mungu kila mmoja kwa kiwango cha elimu yake, na hata kutofautiana umri na riziki na matukio na majanga yote hayo yanakwenda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu; ili awajaribu waja wake wenye akili. Basi yeyote atakayeridhia mipango ya Mwenyezi Mungu na akajisalimisha kwake na akajitahidi kufanya matendo ambayo anayaridhia basi mtu huyo ana radhi za Mwenyezi Mungu, na yule ambaye hatojisalimisha kwake na hatomtii, basi huyo ana hasira toka kwa Mola wake na atapata tabu duniani na Akhera.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupatie radhi zake, na tunajilinda na hasira zake.

Kufufuliwa baada ya kufa, na kuhesabiwa na kulipwa kwa mujibu wa matendo, na pepo na moto.

Utakapojua -ewe mwenye akili kuwa hakika amekuumba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumuabudu yeye, basi jua kuwa Mwenyezi Mungu ametoa habari katika vitabu vyake vyote ambavyo ameviteremsha kwa Mitume wake, kuwa yeye atakufufua ukiwa hai baada ya kufa kwako, na atakulipa kwa matendo yako katika nyumba ya malipo baada ya kufa; na hivyo ni kwasababu mwanadamu anahama kwa kufa kutoka nyumba ya matendo na yenye kuisha -na ndiyo haya maisha- kwenda katika nyumba ya malipo yenye kudumu, nayo ni ile ya baada ya kufa. Na ukishatimia muda ambao ameupanga kwa mwanadamu kuishi, anaamrisha Mwenyezi Mungu Malaika wa mauti na kuitoa roho yake toka mwilini mwake, na kisha hufa baada ya kuonja uchungu wa mauti kabla ya kutoka roho yake toka mwilini mwake.

Ama Roho, hakika Mwenyezi Mungu ataiweka katika nyumba ya neema -peponi- ikiwa ilikuwa ni yenye kumuamini Mwenyezi Mungu na yenye kumtii, ama ikiwa ilikuwa ni yenye kumkufuru Mwenyezi Mungu, na ni yenye kupinga kufufuliwa na kulipwa baada ya kufa, ataiweka Mwenyezi Mungu katika nyumba ya adhabu -motoni- mpaka ifike ahadi ya mwisho wa dunia na kisimame kiyama, na vitakufa viumbe vyote vilivyobakia, na hatobakia isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kisha Mwenyezi Mungu atawafufua viumbe wote -mpaka wanyama- na itarudishwa kila roho katika mwili wake baada ya kurudi mili ikiwa kamili kama ilivyoumbwa mara ya kwanza; na hivyo ni kwasababu ya kuhesabiwa watu na walipwe kutokana na matendo yao, mwanaume na mwanamke, raisi na mfuasi, tajiri na masikini hatodhulumiwa yeyote, na aliyedhulumiwa atalipwa haki yake kutoka kwa aliyemdhulumu, mpaka mnyama atalipwa kutoka kwa mnyama mwenzake aliyemdhulumu na watalipana baadhi yao wao kwa wao. kisha wataambiwa kuweni udongo; kwa sababu wanyama hawaingii peponi wala motoni.

Na atalipwa mwanadamu na jini wote hao wawili kwa matendo yao, na wataingia peponi waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakamtii, hata kama mtu atakuwa ni masikini zaidi, na wataingia motoni makafiri wapingaji hata kama atakuwa ni tajiri mkubwa kuliko wote na mbora zaidi duniani; Amesema Mwenyezi Mungu: Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu kwa Mwenyezi Mungu amchae Mungu zaidi, hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na mwenye habari za mambo yote. [Al Hujrati: 13].

Na pepo ndiyo nyumba ya neema, ndani yake kuna neema aina mbalimbali hawezi yeyote kuzisifia neema hizo, na ina tabaka mia moja, na kila tabaka kuna wakazi, kwa kiwango cha imani yao kwa Mwenyezi Mungu na kumtii kwao, na tabaka la chini zaidi huko peponi watapewa watu wake neema mfano wa neema walizoneemeshwa wafalme wa duniani zaidi yake mara dufu ([6]).

Na Moto- atukinge nao Mwenyezi Mungu- ni nyumba ya adhabu huko akhera baada ya kufa, humo kuna aina nyingi za adhabu, mateso yanayo fadhaisha moyo, na kuyaliza macho.

Na kama mauti yangekuwa yapo akhera wangekufa watu wa motoni kwa kule kuyaona tu mauti. Lakini mauti yanakuja mara moja na humchukua mtu na kumtoa kutoka katika maisha ya dunia kwenda akhera, na imekuja katika Qur'ani tukufu sifa kamili ya kifo na kufufuliwa hesabu na malipo, na pepo na moto, na katika yale tuliyotangulia kuyataja kuna ashiria hilo.

Na dalili juu ya kufufuliwa baada ya kufa na kuhesabiwa ni nyingi sana, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani tukufu. Kutoka kwenye ardhi tumewaumba na humo tutawarudisha tena baada ya kufa. [Surat Twaha: 55], Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake akasema ni nani atakayeihuisha mifupa na imesagika? [Surat Yasin: 79-78].

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Waliokufuru wanadai kuwa hawatofufuliwa, sema 'kwa nini? kwa haki ya Mola wangu hakika nyinyi mtafufuliwa: kisha mtajulishwa mliyokuwa mnayatenda. [Surat Taghaabun: 7]

Maana ya Aya kwa ujumla:

1- Katika aya ya kwanza -anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu -kuwa yeye amemuumba mwanadamu kutokana na ardhi, na huko nipale alipo muumba baba yao Adam -Iwe juu yake amani- kutokana na udongo na anatoa habari kuwa yeye atawarudisha humo ardhini baada ya kufa kwenye makaburi; hiyo ni takrima kwao, na anatoa habari kuwa yeye atawatoa humo kaburini kwa mara nyingine tena, na watatoka kwenye makaburi yao wakiwa hai kuanzia wa mwanzo wao mpaka mwisho.

2- Katika Aya ya pili: anamjibu Mwenyezi Mungu kafiri mwenye kukanusha kufufuliwa ambaye anashangaa kuhuisha mifupa baada ya kusagika.

Na katika Aya ya Tatu: anawajibu Mwenyezi Mungu makafiri wenye kukanusha kufufuliwa baada ya kufa, madai yao ni Batili, na anamuamrisha Mtume wake- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- awaapie kwa jina la Mwenyezi Mungu kiapo chenye nguvu, na Mwenyezi Mungu atawafufua na atawafahamisha waliyoyafanya, na atawalipa malipo yao na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.

Na akatoa habari Mwenyezi Mungu katika aya nyingine kuwa yeye akiwafufua wenye kupinga kufufuliwa na moto, atawaadhibu katika moto wa jahannam na wataambiwa: Hapo wataambiwa, «Hii ndiyo Siku ya Uamuzi wa haki baina ya viumbe, ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani na mkiikataa.» [Surat Sajda: 20].

Udhibiti wa matendo ya mwanadamu na maneno yake

Na hakika ametoa habari -Mwenye nguvu na Mtukufu- kuwa yeye alikwisha jua yote atakayoyasema na kuyatenda kila mwanadamu sawa ni katika mambo ya kheri au mambo ya shari sawa yaliyojificha au yaliyo wazi, na akatoa habari kuwa ameyaandika hayo katika Lauhul mahfuudh (ubao uliohifadhiwa) kwake kabla hajaumba mbingu na ardhi na wanadamu na wengineo, na akatoa habari pamoja na haya yote amemuwakilishia kila mwanadamu Malaika wawili, Malaika mmoja upande wa kulia akiandika mazuri na wa pili upande wa kushoto akiandika mabaya na Malaika hao hawapitwi na jambo lolote, na akatoa habari - kutakasika na machafu ni kwake- kuwa kila mwanadamu atapewa siku ya hesabu kitabu chake ambacho kimeandikwa ndani yake maneno na matendo yake, atayasoma na wala hatopinga chochote, na wenye kupinga chochote Mwenyezi Mungu atayapa uwezo wa kuyaongoa masikio yake macho yake na mikono yake miwili na miguu na ngozi yake kwa kila alichokisema.

Na katika Qur'ani tukufu kumebainishwa hilo kwa uwazi; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hatoi kauli yoyote ispokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayari kuandika anayoyasema. [Surat Qaaf: Aya 18]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hakika juu yenu kuna wenye kuwatunza, watukufu wenye kuandika, wanayajua yote mnayoyatenda. [Surat Infitaar Aya 10-12].

Uchambuzi wa Aya.

Anatoa habari -Mwenyezi Mungu Mtukufu- kuwa yeye amemuwakilishia kila Malaika wawili, mmoja upande wa kulia akiandika mazuri yake na mwingine upande wa kushoto akiandika mabaya yake, na anatoa habari Mwenyezi Mungu katika Aya mbili za mwisho kuwa yeye amewawakilishia watu Malaika watukufu,wanaandika matendo yao yote, na katoa habari kuwa amewapa Malaika uwezo wa kujua matendo yao yote na huyaandika kama walivyoyajua, kama alivyoyajua yeye Mwenyezi Mungu na kuyaandika katika Lauhul mahfuudh kabla hajawaumba.

Ushuhuda.

Nashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa pepo ni kweli ipo, na moto upo, na kuwa kiyama kitakuja na wala hapana shaka, na kuwa Mwenyezi Mungu atamfufua kila aliyoko kaburini kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa, na kila alichokitolea habari Mwenyezi Mungu katika kitabu chake au kupitia ulimi wa Mtume wake -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ni haki na kweli.

Na nina kuita -ewe mwenye akili- kwenye kuamini huu ushuhuda, na kuutangaza na kuufanyia kazi maana yake; na hii ndiyo njia ya mafanikio.

 Sehemu ya pili -Kumjua Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

Utakapo tambua - ewe mwenye akili- kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola ambaye amekuumba, na kuwa atakufufua akulipe kwa matendo yako, basi jua yakuwa Mwenyezi Mungu amekutumia wewe na watu wote Mtume, amekuamrisha umtii na umfuate, na akatoa habari kuwa hakuna njia ya kujua ibada yake iliyo sahihi isipokuwa ni kwa kumfuata huyu Mtume, na kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa sheria zake ambazo amemtuma Mtume kwa ajili ya sheria hizo.

Na huyu Mtume Mtukufu, ambaye yapasa watu wote kumuamini na kumfuata ndiye mwisho wa Manabii, na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyetumwa kwa watu wote, ni Muhammadi Nabii asiyejua kusoma wala kuandika -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- Mtume ambaye Musa na Issa -Ziwe juu yao wawili hao rehema na amani- walimbashiri katika sehemu zaidi ya arobaini katika taurati na injili, vitabu ambavyo wanavisoma mayahudi na manaswara kabla waandishi hawajavichezea vitabu hivi na kuvibadilisha.

Na huyu Mtume Mtukufu, ambaye Mwenyezi Mungu amehitimisha nae ujumbe, na akamtuma kwa watu wote, ni Muhammadi mtoto wa Abdillahi mtoto wa Abdil Muttwalib mtoto toka ukoo wa Haashim katika kabila la kiquraish -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ni Mtukufu na mkweli na anatoka katika kabila tukufu hapa duniani, anafungamana na mgongo (kizazi) cha Mtume wa Mwenyezi Mungu Ismail mwana wa Ibrahim, na hakika alizaliwa huyu nabii wa mwisho wa Manabii wote -Muhammad Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- katika mji wa Makkah mnamo mwaka 570 tangu kuzaliwa Nabii Issa. Na katika usiku aliozaliwa na wakati wa kutoka kwakwe kwenye tumbo la mama yake aliuangazia ulimwengu kwa nuru kubwa, watu walipigwa butwaa, na ikaandikwa katika vitabu vya historia na yakaanguka masanamu ya maquraishi ambayo walikuwa wakiyaabudu mbele ya Al kaaba katika mji wa Makkah na likatikisika jumba la Kisra mfalme wa Fursi, na cheo chake kikaanguka zaidi ya mara kumi, na ukazimika moto waliokuwa wanauabudu wafursi, na ulikuwa kabla ya hapo haukuwahi kuzimika zaidi ya miaka elfu mbili.

Na haya yote ili iwe ni tangazo kwa walimwengu kutoka kwa Mwenyezi Mungu la kuzaliwa wa mwisho katika Manabii ambaye atayaangamiza masanamu ambayo yanaabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na atawaita Wafarisayo na Waroma kuja kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kuingia katika dini yake ya kweli, na kama watakataa atapigana nao jihadi yeye na wafuasi wake, na kisha Mwenyezi Mungu atampa ushindi dhidi ya maadui zake, na ataieneza dini yake ambayo ni nuru katika ardhi, na hiki ndicho kilichotokea kwa hakika baada ya kutumwa Mtume Muhammadi -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-.

Kwa hakika Mwenyezi Mungu alimtofautisha mwisho wa manabii wake Muhammad- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na ndugu zake Mitume waliotumwa kabla yake kwa tofauti nyingi miongoni mwazo:

Tofauti ya kwanza: ni kuwa yeye ni Mtume wa mwisho na hakuna baada yake Mtume wala nabii.

Tofauti ya pili: Ujumbe wake kuenea kwa watu wote, Basi watu wote ni umma wa Mtume, mwenye kumtii na kumfuata ataingia peponi, na mwenye kumuasi ataingia motoni. mpaka mayahudi na Wakristo wanatakiwa kumfuata, na yeyote ambaye hatomfuata na kumuamini basi huyo amemkufuru Mussa na Issa na manabii wote. Na Mussa na Issa na manabii wote wako mbali na kila mtu ambaye hamfuati Mtume Muhammadi -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-; kwa Mwenyezi Mungu amewaamrisha wambashirie na wawalinganie umma wao kumfuata atakapo mtuma Mwenyezi Mungu, kwasababu dini yake ambayo ametumwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili yake ni dini ya Mwenyezi Mungu amewatuma Mitume kwa ajili ya dini hiyo, na akafanya wepesi wa dini hii na ukamilifu wake katika zama za huyu Mtume Mtukufu na mwisho wa manabii, basi haifai kwa yeyote baada ya kutumwa Muhammadi afungamane na dini isiyokuwa ya uislamu ambayo Mwenyezi Mungu amemtuma kwa dini hiyo, kwasababu dini iliyokamilika ambayo Mwenyezi Mungu amefuta dini nyingine zote kwa dini hiyo, na kwasababu ni dini ya haki iliyohifadhiwa.

Ama dini ya kiyahudi na kikristo ni dini zilizobadilishwa na siyo kama zilivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, na kila muislamu anayemfuata Muhammadi anazingatiwa kuwa anamfuata Mussa na Issa na Manabii wote, na mwenye kutoka katika uislamu huzingatiwa kuwa ni mwenye kumkufuru Mussa na Issa na Manabii wote hata kama atadai kuwa yeye ni mfuasi wa Mussa na Issa.

Na kwa hivyo ndiyo maana wakafanya haraka kundi la wanazuoni wa kiyahudi na makasisi wa kikristo wenye akili waadilifu wakamuamini Muhammadi Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kuingia katika uislamu.

Miujiza kumi na mbili ([7]) ya bwana Mtume Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

Na kwa hakika walihesabu wanazuoni wa historia ya Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- miujiza yake ambayo inajulisha juu ya ukweli wa utume wake ikafika zaidi ya miujiza elfu moja, miongoni mwayo:

1- Alama ya utume ambayo Mwenyezi Mungu aliiotesha kati ya mabega yake mawili, nayo ni Muhammad Rasulullahi (Yaani: Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu) kikiwa kwa namna ya (Thaaliil) punje.

2- Kufunikwa na mawingu wakati anapotembea kwenye jua la kiangazi lilokuwa kali.

3-Vijiwe vidogo mikononi mwake vikimsabihi Mwenyezi Mungu, na miti kumsalimia.

4- Kutoa kwake habari kuhusu yaliyofichikana ambayo yatatokea katika zama za mwisho; nayo ndiyo yanayotokea kidogo kidogo kwa mujibu wa alivyo toa habari.

Na haya mambo yaliyofichikana ambayo yanatokea baada ya kufa mwisho wa manabii Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- mpaka mwisho wa dunia, na mambo ambayo ameyatoa Mwenyezi Mungu na akayatolea habari yameandikwa katika vitabu vya hadithi, na vitabu vya alama za kiyama, mfano (an-nihaayat) cha ibnu kathiir na kitabu (Al- akhbaar almushaatu fii ash-raatu saat) yaani Habari zilizoenea katika dalili za kiyama. (Na Ab-waabul fitan walmalaamih) yaani milango ya fitna na alama zake katika vitabu vya hadidhi na hii miujiza inafanana na miujiza ya manabii waliokuwapo kabla yake.

Lakini Mwenyezi Mungu amemchagua kwa kumpa muujiza wa akili ambao umebakia kwenye kurasa za zama mpaka mwisho wa dunia na hakumpa yeyote katika Manabii, na huo muujiza ni Qur'ani -maneno ya Mwenyezi Mungu -ambayo amedhamini kuyahifadhi, basi mkono wa mwenye kubadilisha hauwezi kuifikia, na hata kama yeyote atajaribu kubadilisha herufi moja tu ingejulikana, na hizi hapa milioni nyingi za kopi za Qur'ani zipo kwenye mikono ya waislamu na wala hazitofautiani na kopi nyingine hata herufi moja.

Ama kopi za taurati na injili ni nyingi zinatofautiana baadhi yake na nyingine; kwasababu mayahudi na Wakristo walizichezea na wakazibadilisha pale alipowapa Mwenyezi Mungu dhamana ya kuvihifadhi, ama Qur'ani hakupewa dhamana ya kuihifadhi isipokuwa yeye mwenyewe- kutakasika na machafu ni kwake kwa hifadhi yake kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani na hakika sisi tunachukua ahadi kuihifadhi. [A Hijri: 9].

Alama za kiakili na dalili kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu ya kuwa Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Na katika alama za kimantiki na kiakili zenye kujulisha kuwa Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu: nikuwa Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto makafiri wa kikuraishi pale walipompinga Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kama alivyowapa changamoto wengine katika wale waliowapinga manabii katika nyumati zilizotangulia, na wakasema; hakika Qur'ani siyo maneno ya Mwenyezi Mungu. Aliwapa Mwenyezi Mungu changamoto ya kuleta mfano wa Qur'ani, basi walishindwa japokuwa Qur'ani imeteremshwa kwa lugha yao, na japo kuwa wao ni mafasaha zaidi, na japokuwa kati yao kuna wahubiri wakubwa na mafasaha na vidume vya mashairi, kisha akawapa changamoto kwa kuwataka walete sura kumi mfano wa Qur'ani japo za uongo na pia walishindwa, kisha akawapa changamoto ya kuleta sura moja tu pia wakashindwa, kisha akatangaza kushindwa kwao, na wakashindwa majini na watu kuleta mfano wake, hata kama wangesaidiana wao kwa wao; Basi akasema Mwenyezi Mungu: Sema, «Hata wakijikusanya majini na binadamu wote ili kuleta mfano wa hii Qur’ani yenye kuelemea, hawataweza kuileta, mfano wake hata kama watashirikiana wao kwa wao.» [Al Israai: 88].

Na kama ingekuwa Qur'ani ni maneno ya Muhammadi au mwingine miongoni mwa watu; angeliweza mtu mwingine miongoni mwa watu wa

Lugha yake waliokuwa mafasaha kuleta mfano wake, lakini Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ubora wa maneno ya Mwenyezi Mungu na utukufu wake unazidi maneno ya mwanadamu, kama vile ambavyo ubora wa Mwenyezi Mungu uko juu kushinda ubora wa mwanadamu.

Na kwa mujibu wa hayo Mwenyezi Mungu hana wakufanana naye, na kwa hivyo niwazi kuwa Qur'ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu; kwasababu maneno ya Mwenyezi Mungu hakuna wa kuweza kuja nayo isipokuwa Mtume kutoka kwake, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Muhammadi siyo baba wa yeyote katika wanaume wenu lakini ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Mitume, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu. [Al Ahzaab: 40]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji wa habari nzuri na muonyaji lakini watu wengi hawajui. [Suratu Sabai: 28]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukukutuma, isipokuwa uwe ni rehema kwa watu wote [Al Anbiyaai: 107].

Maana ya Aya kwa ujumla:

1- Anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya ya kwanza yakuwa Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ni Mtume wake kwa watu wote na yeye ndiye mwisho wa Mitume wake na hakuna baada yake mtume, na anatoa habari kuwa amemchagua ili abebe ujumbe wake na ili awe mwisho wa mitume wake; kwasababu yeye anajua kuwa anafaa zaidi kuliko watu wengine.

2- Na anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya ya pili; kuwa yeye amemtuma Mtume wake Muhammadi -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kwa watu wote weupe na weusi, waarabu na wasiokua waarabu, na anatoa habari kuwa watu wengi hawajui ukweli; kwa hivyo wamepotea na wamekufuru baada ya kumfuata Muhammad- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

3- Na anamsemesha Mwenyezi Mungu Mtume wake Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- katika Aya ya tatu na akampa habari kuwa amemtuma ili awe rehema kwa viumbe vyote, basi yeye ni rehema ya Mwenyezi Mungu ambayo amemkirimu kushinda watu wote, na mwenye kumuamini na kumfuata hakika atakuwa amekubali rehema ya Mwenyezi Mungu na atalipwa pepo. Na asiyemuamini Muhammad na akawa hakumfuata kwa hakika amekataa rehema za Mwenyezi Mungu na anastahiki moto na adhabu iliyo kali.

Wito wa kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

Hivyo tunakuita -ewe uliyepewa akili- katika kumuamini Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na kumuamini Mtume wake Muhammad kuwa ni Mtume, na tunakuita kwenye kumfuata na kufanyia kazi sheria zake ambazo amemtuma Mwenyezi Mungu kwa ajili yake, nayo ni dini ya kiislamu ambayo chimbuko lake ni Qur'ani tukufu -maneno ya Allah- na hadithi za mwisho wa mitume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, ambazo zimethibiti toka kwake, kwasababu Mwenyezi Mungu amemuhifadhi basi hawezi kuamrisha isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu na hakatazi isipokuwa yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, basi sema kwa ukunjufu: "Nimeamini kuwa Mwenyezi Mungu ni muumba wangu na Mola wangu wa pekee, na sema nimeamini kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na umfuate; kwasababu hakuna kufaulu isipokuwa kwa kutekeleza hayo".

Mwenyezi Mungu anipe mimi na wewe taufiki ya kupata heshima na mafanikio ewe Mwenyezi Mungu tukubalie dua yetu.

 Sehemu ya tatu: Kuijua dini ya Haki - uislamu.

Ikiwa umeshajua -ewe uliyepewa akili kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wako ambaye amekuumba na akakupa riziki, na kuwa yeye ni Mola mmoja wa haki hana mshirika wake, na kuwa yakupasa kumuabudu peke yake, na umejua kuwa Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwako na kwa watu wote; jua yakuwa haifai imani yako ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- isipokuwa utakapo jua dini ya uislamu na ukaiamini na kuifanyia kazi, kwasababu uislamu ni dini ambayo ameiridhia Mwenyezi Mungu na akaamrisha Mitume wake kuifuata dini hiyo, na akatuma kwenye dini hiyo mwisho wa mitume Muhammad- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kwa watu wote na akawawajibisha kuifanyia kazi.

Utambulisho wa uislamu

Amesema Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- mwisho wa Mitume na ni Mtume wa Mwenyezi Mungu alitumwa kwa watu wote: (Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mmoja tu, na kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Swala na kutoa Zaka, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kwenda kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo) ([8]).

Hivyo basi uislamu ni dini ya ulimwengu mzima, dini ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha watu wote kuifuata, na Mitume wa Mwenyezi Mungu wameiamini, na wakatangaza uislamu wao na Mwenyezi Mungu akatangaza kuwa uislamu ni dini ya haki na kuwa yeye hamkubalii yeyote kufuata dini isiyokuwa uislamu. amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika dini ya haki kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu [Al-Imran: 19]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na atakeyetaka dini isiyokuwa dini ya uislamu, basi haitokubaliwa kwake naye akhera atakuwa ni mwenye hasara kubwa. [Al-Imran: 85].

Maana ya ujumla ya Aya mbili:

1- Anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa dini kwake yeye ni uislamu tu.

2- Na katika Aya pili ametoa habari- kutakasika na machafu ni kwake -kuwa yeye hatomkubalia yeyote dini isiyokuwa ya uislamu, na watakaokuwa na furaha baada ya kufa ni waislamu tu, na wale wanaokufa wakiwa hawapo kwenye uislamu wanahasara katika nyumba ya akhera na wataadhibiwa katika moto.

Na kwa ajili hiyo wametangaza Mitume wote kuwa wamejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, na wametangaza kuwa mbali na wale wasiotaka kusilimu, na yeyote katika mayahudi na manaswara akitaka kufaulu na kuishi kwa furaha basi na aingie kwenye uislamu, na amfuate Mtume wa uislamu Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani- ili awe ni mfuasi wa kweli wa Nabii Mussa na Issa -juu yao wawili hao amani- kwa sababu Mussa na Issa na Muhammad na mitume wote wa Mwenyezi Mungu ni waislamu, wote walilingania uislamu, kuwa ni dini ya Mwenyezi Mungu ambayo wametumwa kwa ajili yake, na haipasi kwa yeyote miongoni mwa waliokuwepo baada ya kutumwa mwisho wa Mitume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani -mpaka mwisho wa dunia, haifai kujiita mwenyewe kuwa amejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (Muislamu) wala Mwenyezi Mungu hamkubalii haya madai isipokuwa atakapo amini kuwa Muhammad ni Mtume toka kwa Mwenyezi Mungu, na akamfuata, na akatenda kwa mujibu wa Qur'an ambayo imeteremshwa kwa ajili hiyo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani tukufu: Sema, ewe Mtume, «Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi Atawapenda Mwenyezi Mungu na Atawasamehe madhambi yenu na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na mwenye huruma. [Al-Imran: 31].

Maana ya Aya kwa ujumla:

Anamuamrisha Mwenyezi Mungu Mtume wake Muhammad amwambie mwenye kudai kumpenda Mwenyezi Mungu: ikiwa mnampenda Mwenyezi Mungu kikweli, basi nifuateni mimi atakupendeni Mwenyezi Mungu, kwa hakika Mwenyezi Mungu hawezi kukupendeni wala kuwasamehe madhambi yenu isipokuwa mkimuamini Mtume wake na mkamfuata.

Na huu uislamu ambao Mwenyezi Mungu amemtuma nao kwa watu wote Mtume wake Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, ndiyo uislamu uliokamilika na ulioenea na wa upole, ambao ameukamilisha Mwenyezi Mungu na akauridhia kuwa ni dini ya waja wake na hawakubalii dini isiyokuwa hiyo, na ndiyo dini ambayo wameibashiria mitume na wakaiamini, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'an tukufu: Leo hii nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema zangu, na nimekuridhieni kuwa Uislamu ndiyo Dini yenu. [Al Maida: 3]

Maana ya Aya kwa ujumla:

Anatuhabarisha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aya hii tukufu ambayo ameiteremsha kwa mwisho wa Mitume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- akiwa amesimama Arafa katika mji wa Makka katika Hijja ya kuaga wakinong'ona na Mola wao na wakimuomba, na ilikuwa tukio hilo ni mwishio wa uhai wake Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- baada ya kunusuriwa na Mwenyezi Mungu , na ukaenea uislamu na ukakamilika uteremkaji wa Qur'an.

Anatoa habari Mwenyezi Mungu kuwa yeye amewakamilishia waislamu dini yao na amewatimizia neema yake kwa kumtuma Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, na kumshushia Qur'an tukufu, na anatoa habari kuwa amewaridhia kuwa uislamu ndiyo dini, na wala hamkubalii yeyote kufuata dini isiyokuwa uislamu kwa hali yoyote.

Anatoa habari- kutakasika na machafu ni kwake- yakuwa uislamu ambao amemtuma nao Mtume wake Muhammad - Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kwa watu wote, ni dini iliyokamilika na kuenea na yenye kufaa katika kila zama na mahala na umma, na dini ya ujuzi na wepesi na uadilifu na kheri, na ni njia ya wazi iliyokamilika na imara kwa nyanja zote za maisha, na yenyewe ni dini na ni serekali ndani yake kuna njia ya haki kwa ajili ya hukumu na maamuzi na pia siasa jamii na uchumi, na kila ambacho anakihitajia mwanadamu katika maisha ya dunia, na ndiyo dini ambaye ndani yake kuna furaha ya maisha katika maisha ya akhera baada ya kufa.

Nguzo za Uislamu

Na uislamu uliokamilika ambao Mwenyezi Mungu kamtuma Mtume Muhammad - Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- wake kwa ajili hiyo, umejengwa kwa nguzo tano, hawezi kuwa mwanadamu muislamu wa kweli mpaka aziamini nguzo hizo na azitekeleze, nazo ni:

1- Ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.

2-Asimamishe swala.

3-kutoa zaka .

4- Kufunga mwezi wa Ramadhani.

5- Kuhuji nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ikiwa ataweza gharama za kwenda huko ([9]).

Nguzo ya kwanza:

Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kuwa Muhammadi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu:

Na tamko la shahada lina maana ambayo inapasa kwa kila muislamu kuifahamu na maana yake, ama mtu ambaye analitamka kwa ulimi wake na wala hajui maana yake na wala halifanyii kazi basi mtu huyo hafaidiki na tamko hilo

Na maana ya Shahada ya "Laa ilaha ila LLah": Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki katika ardhi hii au mbinguni isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, Yeye ndiye Mungu wa kweli na miungu wengine wasiokuwa Yeye ni batili.

Na ambaye anamuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu amemkufuru Mwenyezi Mungu, hata kama atakuwa muabudiwa wake ni nabii au walii, hata kama ni kwa hoja ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na hata kama nikutafuta njia ya kukufikisha kwake, kwa sababu washirikina ambao Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- aliwapiga vita hawakuabudu manabii na mawalii isipokuwa kwa hoja hizi, lakini hoja hizi ni batili na zenye kurudishwa, kwasababu kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kutafuta njia ya kufika kwake haiwi kwa njia ya kubadilisha ibada na kumuabudu asiyekuwa yeye, na hakika si vinginevyo isipokuwa kujikurubisha kuna kuwa kwa majina yake na sifa zake, na kwa matendo mema ambayo ameyaamrisha kama vile swala na sadaka na kuleta dhikri, na kufunga na kupigana jihadi,na kuhiji na kuwafanyia wema wazazi wawili, na mfano wa hayo, na kupitia dua za waumini waliopo hai kumuombea ndugu yake pindi atakapo muomba hilo.

Na ibada zina aina nyingi, miongoni mwazo:

1- Dua :

Na dua ni kutaka haja mbalimbali ambazo hana uwezo wa kuzitatua ispokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mfano kuteremsha mvua, kumponya mgonjwa, kuondoa matatizo ambayo kiumbe hawezi kuyaondoa, kwa mfano kutaka pepo, na kuokolewa na moto na kutaka watoto na riziki, na kuwa na furaha, na mfano wa hayo.

Basi haya yote hayatafutwi isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, na mwenye kuyatafuta kutoka kwa kiumbe hai au kilichokufa au kitu kingine mfano wa hivyo basi hakika amekiabudu, amesema Mwenyezi Mungu akiwaamrisha waja wake kumuomba yeye peke yake na hali yakutoa habari kuwa dua ni ibada, na yeyote atakaye ibadilisha na kumuomba asiyekuwa yeye basi huyo ni katika watu wa motoni. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Anasema Mola wenu, «Enyi waja! Niombeni Peke Yangu na niabuduni mimi tu, nitawakubalia maombi yenu. Hakika ya wale wenye kufanya kiburi kwa kukataa kunipwekesha katika ibada na ustahiki wa kuabudiwa wataingia Moto wa Jahanamu wakiwa watwevu na wanyonge. [Surat ghaafir 60], Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akatoa habari kuwa asiye kuwa yeye katika wanaoombwa hawamiliki manufaa ya yeyote wala madhara, hata kama watakuwa ni manabii au mawalii (vipenzi). Sema, waiteni wale mnaodai kuwa ni waungu mkamuacha yeye hawataweza kukuodosheeni shari wala kubadilisha kuwa heri. [Surat Al-israa 56 na Aya inayofuta], Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na kwa hakika misikiti (yote) ni ya Mwenyezi Mungu, basi msiabudu yeyote pamoja na mwenyezi mungu. [Suratul Jinn: 18]

2- Kuchinja na kuweka nadhiri na kuleta vya kujikurubisha.

Na haifai kwa mtu kujikurubisha kwa kumwaga damu, au kuleta vya kujikurubisha, au kutia nadhiri isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake,- na atakaye chinja si kwa ajili Mwenyezi Mungu- kama mwenye kuchinja kwa ajili ya kaburi au jini- kwa hakika mtu huyo atakuwa amemuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na anahaki ya kulaaniwa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema, «Hakika Swala yangu nakuchinja kwangu wanyama, na uzima wangu na kufa kwangu zote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu muumba wa walimwengu wote [Surat An-aam 162-163]

Na amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-:" Amemlaani Mwenyezi Mungu yeyote atakayechinja kwaajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu"([10]).

Na akisema mtu "Naweka nadhiri kwa Fulani, ikiwa nitapata kitu fulani nitatoa sadaka fulani au nitafanya kitu fulani" hii ni nadhiri ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu; kwa sababu ni nadhiri iliyoegemezwa kwa mwanadamu, na nadhiri ni ibada na ibada haiwi isipokuwa kwaajili ya Mwenyezi Mungu, na nadhiri ya kisheria ni "anatakiwa aseme "Naweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitatoa sadaka fulani au nitafanya kitu fulani katika kumtii Mwenyezi Mungu ikiwa nitafanikiwa kupata kitu fulani.

3- (Al- istiaana) wa (Al-istighaatha) wa (Al- istiaadhatu) ([11]):

Hivyo haombwi uokozi wa msaada wala kinga isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'an tukufu: Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada. [Surat faatiha Aya 5], Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema «Najilinda kwa Mola wa alfalaq (asubuhi) ([12]). kutokana na shari ya alivyoviumba ([13]) [Surat Alfalaq 1-2], Amesema Mtume Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani: "Kwa hakika mimi siombwi msaada hakika anayeombwa msaada ni Mwenyezi Mungu" , Na Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ((Utakapo omba basi muombe Allah, na ukihitaji msaada basi taka msaada kwa Allah))..

Na mwanadamu aliye hai inafaa kumtaka msaada, nahutakwa msaada katika kitu ambacho anakiweza tu, Ama kutaka kinga, haombwi yeyote kinga isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, Na maiti na asiyekuwepo na aliyeko mbali hao hawaombwi kinga kwa lolote, kwasababu hawamiliki chochote, hata kama atakuwa ni Nabii au walii au Mfalme.

Na yaliyo fichikana hakuna ayajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu, Basi yeyote atakayedai kuwa anajua yaliyofichikana basi huyo ni kafiri yapasa kumpinga, hata kama atatabiri jambo lililofichikana na likatokea jambo hilo basi jambo hilo litakuwa limeendana tu, Amesema Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: "Mtu yeyote atakaye mwendea mpiga Ramli, na akamsadikisha kwa anayoyasema, hakika atakuwa amekufuru yaliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad"([14]).

Kutegemea na kutarajia ([15]) Na kunyenyekea : Basi asitegemee mwanadamu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, na asitarajie isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, na wala asinyenyekee isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake.

Na katika sifa ambazo wanasifika nazo wengi miongoni mwa wanaojinasibisha na uislamu ni kuwa wao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu, na wanamuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika viumbe hai vyenye kutukuzwa, na wanaabudu makaburi wanayazunguka makaburi yao na wanawaomba haja zao, na huku ni kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na jua kuwa huyo siyo muislamu, hata kama atadai kuwa ni muislamu, na akasema hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na akasali na akafunga na akahiji nyumba tukufu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa hakika uliletewa wahyi wewe, ewe Mtume, na Mitume waliokuwa kabla yako kwamba lau ulimshirikisha Mwenyezi Mungu na asiyekuwa Yeye amali zako zingalibatilika na ungalikuwa ni miongoni mwa walioangamia waliopata hasara. Surat Zumar (65) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi wana wa Israeli muabuduni Mwenyezi Mungu Mola wangu na Mola wenu, hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu amemharamishia pepo na makazi yake ni motoni, na madhalimu hawatokuwa na wa kuwanusuru}. [Al Maaidah: 72].

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimuamrisha Mtume wake rehema na Amani zimfikie aseme kuwaambia watu wake: Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Kwa kweli, mimi ni binadamu kama nyinyi, ninaletewa wahyi kutoka kwa Mola wangu kwamba Mola wenu ni Mola Mmoja. Basi yeyote anayekuwa ni mwenye kuiogopa adhabu ya Mola wake na ana matumaini ya kupata malipo yake mazuri Siku ya Kiyama, basi na atende matendo mema na asimshirikishe yeyote pamojanaye katika ibada.» [Al Kahf: 110].

Na hawa wajinga wamedanganywa na wasomi waovu na wapotevu, ambao wamejua baadhi ya vipengele na hawakujua Tauhidi ambayo ni msingi wa dini, wakawa wakilingania katika shirki kwa kutokujua kwao maana ya Uombezi na Njia ya kumfikia Allah, na hoja yao ni kutafsiri kimakosa baadhi ya hadithi za zamani za uongo na hadithi za bwana Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na Simulizi na ndoto za usingizini ambazo amewatungia shetani, na yenyekufanana na hayo katika upotevu ambao wameukusanya katika vitabu vyao, ili watilie nguvu kuabudu kwao asiyekuwa Mwenyezi Mungu kupitia simulizi hizo, kwa kumfuata shetani na matamanio na kufuata kiupofu baba zao na babu zao, kama walivyokuwa washirikina wa mwanzo.

Na njia ya kumfikia Allah ambayo ametuamrisha Mwenyezi Mungu tuitafute katika maneno yake (Na muitafute njia ya kumfikia) [Suratu Al-Maida 35], Ni matendo mema katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na swala, na sadaka, na kufunga, na kuhiji, na kupigana jihadi, na kuamrisha mema na kukataza mabaya, na kuunga udugu na mfano wa hayo, Ama kuwaomba Maiti na kuwataka kinga wakati wa shida na matatizo huku ni kuwaabudu wao na kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu.

Na kuwataka uombezi manabii na mawalii na wasio kuwa hao katika waislamu ambao Mwenyezi Mungu amewapa idhini ya uombezi ni haki na tuna amini hivyo, lakini uombezi hautafutwi kwa maiti, kwa sababu hiyo ni haki ya Mwenyezi Mungu na hawezi kuipata haki hiyo isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Basi anautafuta uombezi huo mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa kusema "Ewe Mwenyezi Mungu nijaalie kupata uombezi wa Mtume wako na waja wako walio wema, wala hasemi "Ewe fulani niombee mimi; kwa sababu yeye ni maiti, na maiti haombwi chochote hata kidogo; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Waambie, ewe Mtume, hao washirikina, «Ni wa Mwenyezi Mungu uombezi wote. Ni Yake Yeye mamlaka ya mbinguni na ardhini na vilivyoko baina yake. Amri yote ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na hakuna yeyote atakayeombea mbele Yake isipokuwa kwa idhini Yake. Yeye Ndiye Anayemiliki mbingu na ardhi na anayeendesha mambo yake. Lilo wajibu ni kutakwa uombezi kutoka kwa anayeumiliki na atakasiwe Yeye kwa ibada, na usitakwe kutoka kwa waungu wasiodhuru wala kunufaisha, kisha Kwake Yeye mtarudishwa baada ya kufa kwenu ili mhesabiwe na mlipwe. [Az- zumar: 44].

Na katika uzushi ulio haramishwa wenye kupingana na uislamu, na ambao ameukataza Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- katika hadithi sahihi kutoka katika sahihi Bukhari na Muslim na vitabu vingine vya hadithi, ni kujenga misikiti kwenye makaburi na kuyawekea makaburi taa na kuyajengea hayo makaburi, na kuyaremba kwa kuyapaka chokaa au rangi zingine na kuyaandika, na kuyawekea mapazia na kusali makaburini, yote haya ameyakataza Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, kwa sababu kufanya hivyo kunakuwa ni sababu kubwa inayopelekea kuabudiwa wenye makaburi hayo.

Na kwa hivyo inabainika kuwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu kwa yale wanayoyafanya wajinga kwenye baadhi ya makaburi katika miji mingi, mfano Kaburi la Badawy na Sayyidat Zainabu nchini Misri, na kaburi la Jailani nchini Iraqi, na kaburi linalonasibishwa kuwa ni la watu wanyumba ya Mtume (Ahlu Baiti)- Radhi za Allah ziwe juu yao, katika mji wa Najfu na Karbalaa, na makaburi mengine kwenye miji mingi katika kutufu (kuzunguka) pembezoni mwake, na watu kutaka kukidhiwa haja zao, na kuitakidi madhara na manufaa kutoka kwao.

Na inabainika kuwa hawa waliotajwa kwa vitendo vyao hivyo ni washirikina waliopotea, hata kama watadai kuwa ni waislamu na wakawa wanasali na kufunga na kuhiji, na wakatamka shahada yakuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu mtamkaji wa Laailaha illa llahu Muhammadu rasuululllahi hazingatiwi ni mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu; mpaka ajue maana yake na alifanyie kazi tamko hilo kama ilivyotangulia kubainishwa hilo. Ama yule ambaye si muislamu hakika yeye huingia katika uislamu pale mwanzo tu anapotamka shahada, na huuitwa muislamu mpaka ibainike kwake yenye kupingana na uislamu kwa kubakia kwake katika shirki, kama hawa wajinga, au kupinga kitu chochote katika mambo ya lazima katika uislamu baada ya kubainishiwa, au kuiamini dini ambayo inapingana na dini ya uislamu.

Na manabii na mawalii ([16]) wako mbali na wale wanaowaomba na kuwataka msaada, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewatuma Mitume wake ili wawaite watu katika kumuabudu yeye peke yake, na kuacha kumuabudu asiyekuwa yeye katika manabii au mawalii au wasiokuwa hao.

Na kumpenda Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na mawalii wenye kumfuata Mtume haingii katika kuwaabudu; kwa sababu kuwaabudu wao ni kuwafanyia uadui, na kwa hakika kuwapenda wao ni kuwafuata na kupita katika nyenendo zao, na muislamu wa kweli huwapenda manabii na mawalii, lakini hawaabudu.

Na sisi tunaamini kuwa mapenzi ya kumpenda Mtume ni wajibu na ni lazima kwetu sisi kuliko tunavyozipenda nafsi zetu na wake zetu na watoto wetu bali kuliko tunavyo wapenda watu wote.

Pote lililo okoka

Waislamu kwa idadi ni wengi lakini kwa hakika ni wachache mno, na makundi ambayo yanajinasibisha na uislamu ni mengi mpaka kufikia makundi sabini na tatu ([17]), idadi ya kila kikundi kimoja inafikia milioni elfu moja na zaidi, lakini kundi la kiislamu la kweli ni moja tu, nalo ni kundi ambalo linampwekesha Mwenyezi Mungu na linafuata njia ya Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, na linafuata maswahaba wake katika itikadi na matendo mema kama alivyofahamisha hilo Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kwa maneno yake: "Wamegawanyika mayahudi katika makundi sabini na moja, na wamegawanyika manaswara katika makundi sabini na mbili, na utagawanyika umma huu katika makundi sabini na tatu, makundi yote hayo yataingia motoni isipokuwa kundi moja tu". Akasema swahaba mmoja kumuuliza Mtume: ni kundi gani hilo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Yeyote atakaye kuwa katika mfano wangu mimi leo hii na maswahaba wangu ([18]).

Na aliyokuwa nayo Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na maswahaba zake ni kuamini maana ya" Laailaha illa llahu Muhammad rasuulullah", na kuifanyia kazi maana hiyo kwa kumuomba Mwenyezi Mungu peke yake, na kuchinja na kuweka nadhiri kwa ajili yake peke yake, na kutaka msaada na kimbilio pamoja na kinga kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na kuitakidi kuwa manufaa na madhara ni kutoka kwake, na kutekeleza nguzo za uislamu kwa kumtakasia yeye aliyetakasika na machafu, na kuwasadikisha Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na kufufuliwa na kuhesabiwa na pepo na moto na kuamini Qadar yake kuwa kheri na shari yote inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kuhukumu kwa Qur'ani na Sunna katika nyanja zote, na kuridhia hukumu zake na kuwapenda mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuwapiga vita maadui wake na kulingania kwake na kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kukusanyika kwa ajili ya hilo kwa kumsikiliza na kumtwii mwenye kusimamia mambo ya uislamu atakapo amrisha mema, na kusema neno la haki popote wawapo, na kuwapenda wake za Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kuwatanguliza kwa kiwango cha ubora wao na kuwatakia radhi wote na kujizuia kuingilia ugomvi uliopita kati yao ([19]), na kuacha kusadikisha ubaya wanaotupiwa baadhi yao toka kwa wanafiki, ubaya huo wameukusudia kuwafarakanisha waislamu, na wakadanganyika nao baadhi ya maulamaa wao na wanahistoria wao, na wakauthibitisha ubaya huo katika vitabu vyao kwa nia isiyokuwa njema na hili ni kosa.

Na wale ambao wanadai kuwa wao ni katika (Ahlu baity) watu wa nyumba ya Mtume na wanajiita waheshimiwa, ni wajibu juu yao wahakikishe usahihi wa nasaba zao, kwa sababu Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kujinasibisha kwa mtu asiyekuwa baba yake, na ikiwa itabainika kuwa ni nasaba yao basi ni wajibu juu yao kumfuata Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na vipenzi wake katika kumtakasia itikadi Mwenyezi Mungu, na kuacha maasi na waache kuridhia watu kuwainamia, na kubusu magoti yao na miguu yao na wasijitofautishe na ndugu zao waislamu kwa kuvaa mavazi rasmi, kwa sababu kufanya hivyo ni kwenda kinyume na aliyokuwa nayo Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-naye yuko mbali na hayo na mbora mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu.

Na rehema na amani za Allah ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na ali zake na Maswahaba zake.

Kuhukumu na kuweka sheria ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake na pale panapokuwa na sheria kunakuwa na uadilifu huruma na ubora

Na maana ya kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu ambayo tunapaswa kuiamini na kuifanyia kazi, ni kuwa kuhukumu na kuweka sheria ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake, basi haipasi kwa yeyote katika wanadamu aweke kanuni inayo kwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu katika jambo miongoni mwa mambo, na wala haifai kwa muislamu kuhukumu kwa hukumu ambayo hakuiteremsha Mwenyezi Mungu, na wala haifai kuridhia hukumu ambayo inatofautiana na hukumu ya Mwenyezi Mungu, na wala haifai kwa yeyote kuhalalisha alichokiharamisha Mwenyezi Mungu, na mwenye kufanya hivyo kwa kukusudia kwenda kinyume au akaridhia basi huyo amemkufuru Mwenyezi Mungu; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri". Surat Al- maaidah: [44].

Cheo cha Mtume ambacho ametumwa kwa ajili yake

Ni kuwaita watu katika neno la Tauhiid - laailaha illa llahu- na kufanyia kazi ufahamu wa neno hilo, nako nikumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kuacha kumuabudu kiumbe na kuacha sheria zake, na badala yake kumuabudu muumba na kufuata sheria zake peke yake ambaye hana mshirika wake.

Na mwenye kuisoma Qur'ani tukufu kwa kuizingatia na kujiepusha na uigaji wa kibubusa atatambua yakuwa tuliyoyabainisha ni ukweli, na atatambua kuwa Mwenyezi Mungu ameweka mipaka ya mahusiano kati yake na kiumbe -kutakasika na machafu ni kwake-, na akafanya kuwa mahusiano yake na mja wake muumini ni kumuabudu kwa aina zote za ibada, na wala asiilekeze ibada yoyote kwa asiyekuwa yeye, na akayafanya mahusiano yake na Manabii na waja wa Mwenyezi Mungu walio wema ni kuwapenda wao mapenzi yanayoendana na mapenzi yake,- kutakasika na machafu ni kwake na ni Mtukufu- na kuwafuata hao Manabii, na akafanya mahusiano yake na maadui zake makafiri ni kuwachukia, na pamoja na hayo yote awalinganie kuingia katika uislamu na awabainishie huenda wakaongoka, na awapiganishe na waislamu pindi watakapo ukataa uislamu, na wakakataa kunyenyekea hukumu za Mwenyezi Mungu, ili pasiwepo na fitina na dini yote iwe ni Mwenyezi Mungu, na hizi ndizo maana za neno la Tauhiid (Laailaha illa llahu) inapasa kwa muislamu alitambue neno hilo na alifanyie kazi ili awe muislamu wa kweli.

Maana ya kushuhudia kuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu

Na maana ya kushuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kujua na kuamini kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyetumwa kwa watu wote, na yeye ni mja wala haabudiwi, na Mtume hakadhibishwi, bali hutiiwa na kufuatwa, mwenye kumtii na kumfuata ataingia peponi, na mwenye kumuasi ataingia motoni, na kutambua na kuamini kwa kuzipokea sheria, sawa sawa iwe ni katika alama za ibada alizoziamrisha Mwenyezi Mungu, au ni katika taratibu za hukumu za kuweka sheria katika nyanja zote, au ni katika kuhalalisha na kuharamisha, hayo hayawezi kuwa isipokuwa kwa kupitia njia ya huyu Mtume Mtukufu Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani, kwa sababu yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu mwenye kumfikishia Mwenyezi Mungu sheria zake, basi haifai kwa muislamu akubali sheria zilizokuja pasina kupotea njia ya Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu "Na anacho kupeni Mtume basi kipokeeni na anacho kukatazeni basi jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu" [Al-Hashr: 7], Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anaapa kwa nafsi Yake tukufu, kwamba hawa hawataamini kikweli mpaka wakufanye wewe ni hakimu kwenye ugomvi unaotokea baina yao katika uhai wako na watake uamuzi wa Sunnah yako baada ya kufa kwako, kisha wasiingiwe na dhiki katika nafsi zao kwa matokeo ya hukumu yako, na wakwandame, pamoja na hivyo, kwa kukufuata kikamilifu. Kutoa uamuzi kulingana na aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kutoka kwenye Qur’ani na Sunnah katika kila jambo katika mambo ya kimaisha, pamoja na kuridhika na kusalimu amri, ni miongoni mwa uthabiti wa Imani" [An- nisaa: 65].

Maana ya Aya Mbili:

Ana waamrisha Mwenyezi Mungu waislamu katika Aya ya kwanza kuwa wamtii Mtume wake- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Amani- wamtii katika aliyowaamrisha, na wajizuilie na yote aliyowakataza, kwa sababu yeye hakika anaamrisha kwa amri ya Mwenyezi Mungu na anakataza kwa makatazo ya Mwenyezi Mungu.

Na katika Aya ya pili anaiapia Mwenyezi Mungu nafsi yake iliyotakasika na kutukuka ya kuwa haifai imani ya mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, mpaka amfanye Mtume kuwa ni hakimu katika tofauti iliyotokea kati yake na mtu mwingine ([20]) kisha aridhie hukumu yake na ajisalimishe kwa hali zote. "Yeyote atakaye fanya ibada ambayo haipo katika dini yetu basi atarejeshewa" ([21]).

Wito.

Ukishatambua -ewe uliepewa akili-Maana ya (Laailaha illa llahu ) na ukajua kuwa shahada hii ndiyo ufunguo wa uislamu na msingi wake ambao umejengeka nao, Basi sema kutoka moyoni kwa ikhlas "Ash-hadu an-laailaha illa llahu wa ash-hadu ana Muhammadan rasuulullah" na ufanyie kazi maana ya hii shahada, ili upate furaha duniani na akhera, na ili usalimike na adhabu ya Mwenyezi Mungu baada ya kufa.

Na fahamu ya kuwa inavyotakiwa katika tamko la kushuhudia "kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" Inatakiwa kufanyia kazi nguzo za uislamu zilizobakia; kwa sababu Mwenyezi Mungu amefaradhisha hizi nguzo kwa muislamu ili amuabudu kwa kutekeleza nguzo hizo kwa ukweli na ikhlaas kwa ajili yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mwenye kuacha nguzo moja tu katika hizo pasina kuwa na dharura ya kisheria hakika atakuwa ameiharibu maana ya "Laailaha illa llahu" na wala haitazingatiwa shahada yake kuwa ni sahihi.

Nguzo ya pili miongoni mwa nguzo za uislamu (Sala)

Fahamu -ewe uliyepewa akili- yakuwa nguzo ya pili katika nguzo za uislamu ni :Sala, Nazo ni Sala tano katika wakati wa usiku na mchana amezifaradhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili iwe ni mawasiliano kati yake na muislamu, akimnong'oneza na kumuomba, na ili iwe sala ni yenye kumuepusha muislamu na machafu na maovu, kwa ajili hiyo apate raha kiroho na kimwili ambayo itamfanya awe na raha duniani na akhera.

Na kwa hakika amefaradhisha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya sala, kusafisha mwili na nguo, na sehemu ambayo inasaliwa, na anajisafisha muislamu kwa kutumia maji safi yasiyo na najisi, kwa mfano: haja ndogo na haja kubwa, ili autwaharishe mwili wake na najisi ya kihisia, na autwaharishe moyo wake na najisi ya kimaana.

Na sala ndiyo nguzo ya dini, na ni katika nguzo zake muhimu baada ya shahada mbili; na inapasa kwa muislamu aihifadhi sala kuanzia mwaka wa kubaleghe mpaka kufa kwake, na inampasa amuamrishe mke wake na watoto wake kuanzia mwaka wa saba; ili waizoee, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika sala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa wakati maalumu ." [An Nisaai: 103]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hawakuamrishwa katika sheria zote zilizopita isipokuwa ni wamuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, wakikusudia kwa ibada yao kupata Radhi Zake, hali ya kuepuka upande wa ushirikina na kuelekea kwenye Imani, wasimamishe Swala na watoe Zaka. Kufanya hayo ndio Dini iliyolingana , nayo ni Uislamu". [Al-bayyinah: 5].

Maana ya ujumla wa Aya hizi mbili

1- Anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya ya kwanza ya kuwa sala ni wajibu wa dharura kwa muumini, na wajibu juu yao waitekeleze katika wakati wake uliowekwa maalumu.

Na katika aya ya pili anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu - kutakasika na machafu ni kwake- kuwa jambo ambalo wameamrishwa nalo watu na amewaumba kwa ajili yake ni kuwa wamuabudu yeye peke yake, na wamtakasie yeye ibada zao, na wasimamishe sala na watoe zaka kwa wenye kustahilki kupewa.

Na sala ni wajibu kwa kila muislamu katika hali zake zote hata katika wakati wa hofu na maradhi, kwani atasali kwa kadiri ya uwezo wake akiwa amesimama au amekaa au amelala kwa mgongo, na hata kama hatoweza isipokuwa kwa kuashiria kwa macho yake na moyo wake, basi atasali kwa ishara, na hakika amefahamisha Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kuwa mwenye kuacha sala sio muislamu sawa awe mwanaume au mwanamke; akasema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani: "Ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri" ([22]).

Sala tano ni hizi:

Sala ya Al-fajir, na Sala ya Adhuhuri, na Sala ya Al-asri, na Sala ya Magharibi, na Sala ya Ishaa.

Na wakati wa Sala ya Alfajir unaanza kwa kuonekana mwanga wa asubuhi kutoka upande wa mashariki, na huisha muda wake kwa kuchomoza jua, na wala haifai kuichelewesha mpaka mwisho wa wakati wake, na wakati wa Sala ya Adhuhuri unaanza kuanzia kupinduka jua mpaka kiwe kivuli cha kila kitu sawa na urefu wake baada ya kivuli cha kupinduka jua, na wakati wa Sala ya Alaasiri, unaanza baada ya kuisha wakati wa adhuhuri mpaka kuzama jua, na haifai kuichelewesha mpaka mwisho wa wakati wake bali husaliwa ikiwa litakuwa jua bado leupe safi, na wakati wa Sala ya magharibi unaanza baada ya kuzama jua, na unaisha kwa kuzama mawingu mekundu na wala haicheleweshwi mpaka mwisho wa wakati wake, na wakati wa sala ya Ishaa unaanza baada ya wakati wa Sala ya magharibi mpaka mwisho wa usiku na haicheleweshwi baada ya hapo.

Na lau kama atauchelewesha muislamu wakati wa sala moja tu mpaka ikatoka wakati wake pasina kuwa na kizuizi ambacho kipo nje ya uwezo wake; hakika anakuwa amefanya dhambi kubwa na ni wajibu juu yake atubie kwa Mwenyezi Mungu na wala asirudie, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Adhabu kali itawathibitikia wenye kusali" (4) "ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake". [Al-maaun :5-4].

Hukumu za Sala.

Kwanza : Twahara (Usafi).

Kabla hajaingia muislamu katika sala anapaswa kujitwaharisha, basi ataanza kusafisha matokeo ya najisi, ikiwa ametokwa na haja ndogo au kubwa kisha anatawadha.

Na Udhu: ni kunuia Twahara katika moyo wake na wala asitamke nia, kwa sababu Mwenyezi Mungu anatambua nia yake, na kwa sababu Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- hakuitamka, na atasema (Bismillahir Rahmanir Rahiim) kisha atasukutua na ataingiza maji puani kwake na kuyatoa, na ataosha mikono yake pamoja na kongo mbili akianzia mkono wa kulia, kisha atapaka maji kichwa chake chote, na atapaka masikio yake kisha ataosha miguu yake pamoja na fundo mbili kwa kuanzia mguu wa kulia.

Na baada ya kujitwaharisha mwanadamu kisha kukatoka kwake haja ndogo au kubwa au upepo au kuondokwa na akili au kuzimia, basi atarudia kutawadha kama anataka kusali, na ikiwa muislamu ana janaba na ametokwa na manii kwa matamanio japo alikuwa usingizini awe mwanaume au mwanamke, hakika mtu huyo atajitwaharisha kwa kuoga mwili wake wote, na mwanamke akitwaharika na hedhi na nifasi ni wajibu kwake kuutwaharisha mwili wake kwa kuoga mwili wake wote kwa sababu mwenye Hedhi na Nifasi sala zao hazikubaliki mpaka wajitwaharishe, na hakika amewafanyia wepesi Mwenyezi Mungu akawaondolea kulipa kilichowapita (katika ibada) wakati wapo kwenye hedhi na nifasi, ama udhuru usiokuwa wa hedhi na nifasi ni lazima walipe kilicho wapita kama wanaume wanavyolipa.

Na mwenye kukosa maji au akawa anadhurika kwa kuyatumia maji kama vile mgonjwa, basi huyo atajitwaharisha kwa kutayamamu, na sifa ya kutayamamu: atanuia twahara moyoni mwake, na atataja jina la Mwenyezi Mungu kisha atapiga udongo pigo moja kwa mikono yake miwili na atapaka kwa mikono hiyo uso wake, kisha atapaka mgongo wa mkono wake wa kulia kwa tumbo la mkono wa kushoto, na atapaka mgongo wa mkono wa kushoto kwa tumbo la mgongo wa kulia, na kwa kufanya hivyo anakuwa amekwisha jitwaharisha, na namna hii ya kutayamamu ni kwa kila mwenye hedhi na nifasi watakapotwaharika, na pia mwenye janaba na mwenyekutaka kutawadha ikiwa maji yamekosekana au akahofia kutumia maji.

Ya pili: Sifa ya Sala:

1- Sala ya Alfajir :

Ni Rakaa mbili anaelekea Qibla muislamu wa kike au wa kiume, na ni Al-qaaba iliyopo katika msikiti mtukufu wa Makka, na ananuia moyoni mwake kuwa anasali sala ya Al-fajir (Sub-hi) na wala asiitamke nia kisha ataleta takbira kwa kusema (Allahu Ak-baru) kisha atasoma dua ya ufunguzi wa sala, na miongoni mwa hizo dua ni hii (Sub-hanakallahumma wabihamdika , watabaarakasmuka, wataalajadduka ,walaailaaha ghairuka) audhubillahi minash-shaitwaanir-rajiim, kisha atasoma Suratul Faatiha, nayo ni: Bismillahir Rahmanir Rahiim ([23]) Shukurani zote njema anastahiki Mola wa viumbe vyote  Mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu  Mfalme wa siku ya malipo  Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada  Tuongoze njia iliyonyooka  Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, na siyo ya wale uliowakasirikia wala ya wale waliopotea  [Suratul- Faatiha 1-7]. Na ni lazima aisome Qur-ani kwa lugha ya kiarabu  ikiwa anaweza, kisha atasema "Allahu Akbaru" na anarukuu na kuinamisha kichwa chake na mgongo wake, na anaweka matumbo ya viganja vyake kwenye magoti yake kisha atasema:" Sub-hana Rabbiyal Adhiim" kisha atainuka hali yakusema "Samiallahu liman hamidahu" na akisha inuka na kusimama sawa atasema: "Rabbanaa Walakal Hamdu" kisha atasema: Allahu Ak-bar" na atasujudu ardhini kwa kuweka ncha za vidole vya miguu yake na magoti yake na mikono yake na paji lake na pua yake, kisha atasema katika kusujudu kwake " Sub-hana Rabbiyal Aalaa" kisha atakaa kwa kusema " Allahu Akbaru", na atasema atakapokaa "Rabigh-firlii " kisha atasema "Allahu Akbaru" kisha atasoma Al-faatiha, nayo ni (Al-hamdulillahir Rabbil Aalamiin) mpaka mwisho wa sura kama ilivyotangulia katika rakaa ya kwanza, kisha ataleta takbira na atarukuu, kisha atainuka kisha atasujudu,kisha atasujudu mara ya pili akisema katika sehemu hiyo mfano wa alivyosema mara ya kwanza.

Kisha atakaa na atasema: "Attahiyyaatulillahi, Waswalawaatu wattwayyibaatu, Assalaamu Alaika Ayyuha Nabiyyu Warahmatullahi Wabarakaatuhu, Assalaamu Alaina waalaa ibadillahi swaalihiina, Ash-hadu an-laailaha illa llahu wa anna Muhamadan rasuulullahi" Allahumma swalli alaa Muhammad waalaa ali Muhammad, kamaa swalaita alaa ibrahiim waalaa aali ibrahiim Innaka hamiidun majiid, Allahumma Baariki Alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad, kamaa baarakta alaa ibraahiim wa- alaa aali ibrahiim innaka hamiidun majiid" kisha atageuka upande wake wakulia na akisema "Assalaam alaikum warahmatullahi" kisha atageuka upande wake wakushoto akisema Assalamu alaikum warahmatullahi" na kwa kufanya hivyo anakuwa amekamilisha sala ya Sub-hi.

2- Ama sala ya Adhuhuri na Alasiri na Magharibi na Isha ambayo ni ya mwisho:

Kwa kila moja katika sala hizo ina rakaa Nne, atasali rakaa mbili za kwanza mfano wa rakaa mbili za asubuhi, lakini akikaa baada ya rakaa mbili hizo kwa ajili yaTashahudi na atasema mfano wa alivyosema katika kikao chake kabla ya salamu, hatatoa salamu bali atasimama na ataleta rakaa mbili mfano wa rakaa za mwanzo, na atamswalia Mtume Muhammad, kisha atatoa salamu upande wake wa kulia, kisha upande wake wa kushoto, kama alivyotoa salamu katika sala ya Alfajiri.

3- Ama Sala ya Magharibi:

Nayo husaliwa rakaa tatu, atasali rakaa mbili za mwanzo mfano wa ilivyotangulia, kisha atakaa na atasema alichosema katika kukaa kwake katika sala zingine, lakini hatatoa salamu, bali atasimama na atasali rakaa ya tatu, atasema na atafanya mfano wa alivyosema na kufanya kabla yake, kisha atakaa baada ya kusujudu sijida ya pili, na atasema katika kukaa kwake vile alivyosema katika kukaa kwake kwenye kila sala, kisha atatoa salamu upande wake wa kulia kisha upande wake wa kushoto, na ikiwa atarudia rudia mwenye kusali kutamka yale aliyokuwa anayasema katika kurukuu kwake na kusujudu hilo ni bora zaidi.

Na kwa wanaume ni wajibu kuzisali sala hizi za faradhi msikitini wakitanguliwa na imamu, na anakuwa imamu ni yule mzuri wao katika kusoma Qur'ani, na mjuzi wao wa sala, na mwema wao katika dini, na atadhihirisha imamu kisomo anapokuwa amesimama kabla ya kurukuu katika sala ya alfajiri, na katika rakaa mbili za kwanza za sala ya magharibi na isha, na atamsikiliza imamu mtu aliye nyuma yake.

Na wanawake wanasali majumbani kwa kujisitiri na kujihifadhi, atasitiri mwili wake wote mpaka viganja vya mikono na miguu, kwa sababu vyote hivyo ni uchi isipokuwa uso wake, na anaamrishwa kuufunika uso wake mbele ya wanaume, kwa sababu uso ni fitina akitambuliwa kupitia uso atapata maudhi, na kama atapenda mwanamke kusalia msikitini hazuiliwi, lakini kwa sharti atoke akiwa amejistiri na asipake manukato, na atasali nyuma ya wanaume, ili asiwafitinishe na kuwahuzunisha.

Na ni wajibu kwa muislamu asali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu na kujidhalilisha na kuuhudhurisha moyo, na atatulizana kwenye kusimama kwake na kurukuu na kusujudu kwake na wala asifanye haraka na wala asifanye upuuzi, na wala asiinue macho yake juu, na asiongee chochote kisichokuwa kusoma Qur'ani na adhkaar za sala kila kitu kiwe mahala pale ([24]) kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha sala ili kumtaja yeye.

Na katika siku ya ijumaa watasali waislamu sala ya ijumaa rakaa mbili, imamu atasoma kwa sauti katika rakaa zote mbili, mfano wa sala ya Al-fajir, na ata hutubu kabla ya sala hutuba mbili akiwakumbusha waislamu na kuwafundisha mambo ya dini yao, na ni wajibu kwa wanaume kuhudhuria na imamu, nayo ni kama sala ya Adhuhuri katika siku ya ijumaa.

Nguzo ya Tatu miongoni mwa nguzo za uislamu (Zakka)

Na kwa hakika amemuarisha Mwenyezi Mungu waislamu wenye kumiliki mali yenye kufikia kiwango ([25]) watoe zaka ya mali yao kila mwaka, na awape wenye kustahiki katika mafukara na masikini na wengineo wenye kufaa kutolewa zaka kama ilivyobainishwa kwenye Qur-ani.

Na kiwango cha dhahabu ni uzito wa gramu 85, na kiwango cha fedha ni dir-hamu mia mbili 200 sawa na gramu 595, na bidhaa za biashara nazo ni bidhaa mbalimbali pindi thamani yake itakapofikia kiwango, ni lazima kwa mmiliki wa mali hizo azitolee zaka itakapokuwa imezungukiwa na mwaka, na kiwango cha mazao na matunda ni sawa na pishi mia tatu 300, na kipande cha ardhi kilichoandaliwa kwa ajili ya biashara hutolewa zaka ile thamani yake, na kilichoandaliwa kwa ajili ya kukodisha tu hutolewa zaka yale malipo yatokanayo na kukodisha, na kiwango cha zaka kitolewacho katika dhahabu na fedha na kilichoandaliwa kwa ajili ya biashara hutolewa robo ya kumi 25% kwa kila mwaka, na nafaka pamoja matunda hutolewa 10%, na vilivyo nyweshelezwa pasina tabu yoyote kama vilivyonyweshelezwa na mito na chemchem zenye kutiririka au mvua, na hutolewa nusu ya kumi 5%kwa mimea iliyonyweshelezwa kwa tabu kama mimea iliyonyweshelezwa kwa kuhamisha maji.

Na wakati wa kutoa zaka ya na nafaka na matunda ni wakati wa mavuno, na kama atavuna kwa mwaka mara mbili au mara tatu basi itamlazimu kutoa zaka kila anapovuna, na kuhusu zaka ya ngamia ng'ombe na mbuzi kiwango cha zaka yake kimebainishwa kwenye vitabu vya hukumu za uislamu basi unaweza kurejea katika vitabu hivyo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hawakuamrishwa katika sheria zote zilizopita isipokuwa wamuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, wakikusudia kwa ibada yao kupata Radhi Zake, wajiepushe na ushirikina na kuelekea kwenye Imani, wasimamishe Swala na watoe Zaka.Kufanya hayo ndio Dini iliyolingana , nayo ni Uislamu". [Al-bayyinah: 5]; Na kutoa zaka kunafurahisha nafsi za mafukara na maskini na hukidhi haja zao na huyatia nguvu mapenzi yalipo kati yao na matajiri.

Na dini ya kiislamu haikusimamia kwenye zaka peke yake katika kushikamana na kusaidiana kwa mali, bali amewalazimisha Mwenyezi Mungu matajiri kuwasaidia maskini wakati wa njaa, na akaharamisha kwa waislamu kushiba hali yakuwa jirani yake ana njaa, na akalazimisha kwa waisamu kutoa zakaatul fitri na hutolewa siku ya Eid Al-fitri, na zaka hiyo ni pishi moja la chakula kinacholiwa katika mji, hutolewa kwa kila mtu mpaka mtoto na mtumishi wanalipiwa na walii wao, na amewalazimisha waislamu watoe kafara ya kiapo ([26]) atakapo apa kuwa atafanya kitu fulani kisha asikifanye kitu hicho, na amelazimisha kwa muislamu kuteleza nadhiri ya kisheria, na akahimiza Mwenyezi Mungu kutoa sadaka kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na akawaahidi malipo bora zaidi kwa wenye kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu na kwa wema, na amewaahidi kuwaongezea nyongeza zaida, kwa kuwalipa kila jema moja kwa kumi mfano wake mpaka kufikia maradufu ya mia saba na kuzidi zaidi ya mia saba.

Nguzo ya Nne miongoni mwa nguzo za uislamu (Kufunga)

Kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani, nao ni mwezi wa tisa katika miezi ya Hijiria .

Sifa za ufungaji:

Atanuia muislamu kabla ya kupambazuka kwa asubuhi, kisha atajizuilia kula na kunywa na kumuingilia mwanamke-nako ni kukutana jinsia mbili- mpaka lizame jua kisha atafungua, atafanya hivyo kwa muda wa siku za mwezi wa ramadhani; akikusudia kufanya hivyo kumridhisha Mwenyezi Mungu na kumuabudu yeye.

aNa katika swaumu - funga- kuna manufaa mengi yasiyoweza kuhesabika, na miongoni mwa manufaa yake.

Ni kuwa swaumu ni kumuabudu Mwenyezi Mungu na kutekeleza maamrisho yake, anaacha mja matamanio yake na chakula chake na kinywaji chake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na ni katika sababu kubwa za kupelekea kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na ama manufaa ya funga kiafya na kiuchumi na kijamii ni mengi sana, na hawayapati isipokuwa wafungaji kwa itikadi na imani; na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga saumu kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu". "Ni Siku chache tu kufunga huko na atakaye kuwa mgonjwa katika nyinyi au katika safari akafungua baadhi ya siku basi atimize hesabu katika siku nyingine, na wale wasioweza watoe fidia kwa kumlisha masikini ,na atakaye fanya wema kwa radhi ya nafsi yake basi ni bora kwake na huku kufunga ni bora kwenu ikiwa mnajua . "Mwezi huo wa ramadhani ambao imeteremshwa katika mwezi huo hii Qur'ani ili iwe muongozo kwa watu na hoja zilizo waziwazi na uongozi na upambanuzi, na atakaye kuwa katika mji katika huu mwezi basi na afunge, na mwenyekuwa mgonjwa au yupo safarini basi atimize hesabu katika siku nyingine, Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi na wala hakutakieni yaliyo mazito, na pia anakutakieni mtimize hesabu hiyo na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni ili mpate kushukuru. Surat- Al-baqara (183-185)

Na miongoni mwa hukumu za kufunga ambazo amezibainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani, amezibainisha Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-katika hadithi.

1- Nikuwa mgonjwa na msafiri wanafungua na wanalipa siku ambazo walifungua katika siku zingine baada ya kuisha ramadhani, na vilevile mwenye hedhi na nifasi watafungua kisha watalipa siku walizofungua.

2- Na hivyo hivyo mama mjamzito na mwenye kunyonyesha ikiwa wataziogopea nafsi zao au wakawaogopea watoto wao basi wawili hao watafungua na watalipa siku walizofungua.

3- Na ikiwa mfungaji atakula au kunywa kwa kusahau kisha akakumbuka basi kwa hakika funga yake ni sahihi; kwa sababu kusahau na kukosea kwa bahati mbaya na kulazimishwa jambo kulifanya kwa nguvu, hayo Mwenyezi Mungu ameyasemehe kwa umma wa Mtume Muhammad- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na yampasa akikumbuka akitoe kilichoko mdomoni mwake.

Nguzo ya Tano miongoni mwa nguzo za uislamu (HIJJA)

Nako ni kuhiji nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu mara moja katika umri wote, na Hijja itakayokuwa zaidi ya mara moja basi inakuwa ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na katika Ibada ya hijja kuna manufaa mengi yasiyoweza kuhesabika:

Faida ya kwanza; ni kuwa Hijja ni kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa roho kwa mwili na mali.

Faida ya pili: Ni kuwa katika Hajji wanakutana waislamu kutoka katika kila sehemu, wanakutana sehemu moja na wanavaa vazi moja, na hakuna tofauti kati ya Raisi na raia, wala tajiri na masikini, mweupe na mweusi, wote ni viumbe wa Mwenyezi Mungu na waja wake, basi wanapata waislamu kutambuana na kusaidiana, na wanakumbuka siku ambayo Mwenyezi Mungu atawafufua wote wakiwa katika ngazi moja kwa ajili ya kuhesabiwa; na wanajiandaa kwa kitakachotokea baada ya kufa kwa kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na makusudio ya kutufu (kuzunguka) pembezoni mwa Al-kaaba - muelekeo wa waislamu- ambao amewaamrisha Mwenyezi Mungu kuielekea katika kila sala popote walipo, na makusudio ya kusimama maeneo mengine katika mji wa Makkah katika wakati maalumu uliowekwa, na hizo sehemu ni Arafa na Muzdalifa, na kukaa Minaa; na kusudio la kufanya hivyo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu katika hayo maeneo matakatifu kwa namna ambayo ameamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ama kuhusu Al-kaaba na sehemu za ibada tulizozitaja na viumbe vyote hakika hivyo haviabudiwi, wala havinufaishi wala havidhuru, na kwa hakika ibada ni ya Mwenyezi Mungu peke yake, na mwenye kunufaisha na kudhuru ni Mwenyezi Mungu peke yake, na lau kama asingeamrisha Mwenyezi Mungu kuhiji nyumba tukufu na isingefaa kwa muislamu kuhiji! kwa sababu ibada haiwi kwa rai wala kwa matamanio, na kwa hakika ibada inakuwa kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kitabu chake na sunna za bwana Mtume - Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-; amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko, na atakayekanusha (Na asiende na haliyakuwa anauwezo) Basi Mwenyezi Mungu si muhitaji wa kuwahitajia walimwengu}. [Al Imran: 97]([27]).

Na ibada ya Umra ni wajibu kwa muislamu mara moja katika umri sawa akaifanya pamoja ni hijja au akaifanya wakati wowote, na kuutembelea msikiti wa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- katika mji wa Madina siyo lazima wakati wa hija au wakati mwingine wowote, na kwa hakika ni jambo la kupendeza na hupata thawabu kwa mwenye kuutembelea na wala haadhibiwi atakaye acha kuutembelea. Ama hadithi "yeyote atakaye hijji na hakunitembelea hakika huyo amenitenga "hadithi hii siyo sahihi bali ni hadithi inayomsingizia Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- uongo ([28]).

Na ziara ambazo zinakubalika kisheria ni ziara ya msikiti Mtukufu, na akifika mfanya ziara katika msikiti ni sheria asali sala ya maamkizi ya msikiti, wakati huo ataruhusiwa kulitembelea kaburi la Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na atamsalimia kwa kusema "Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu "kwa heshima na kushusha sauti na wala hatakikani kufanya jambo lolote isipokuwa ni kusalimia tu na kuondoka; kama alivyoamrisha-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- umma wake kufanya hivyo, kama walivyokuwa wakifanya maswahaba- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na amani.

Ama wale ambao wanasimama kwenye kaburi la Mtume kwa unyenyekevu kama wanavyosimama kwenye sala, na wanataka toka kwa Mtume awakidhie haja zao au wanamuomba msaada au wanapitia kwake kutaka kutekelezewa haja zao, watu hawa wanamshirikisha Mwenyezi Mungu, Na Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- yupo mbali nao, Basi na ajihadhari kila muislamu kufanya vitendo hivyo kwa kumshirikisha Mtume au kumshirikisha mtu mwingine, kisha baada ya hapo atatembelea makaburi ya vipenzi wake wawili Abuubakar na Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na amani- kisha atawatembelea watu wa Baq-ii na mashahidi wa uhud, ni ziara ya kisheria ya makaburi ya waislamu, na ziara yenyewe ya kisheria atawasalimia maiti na atawaombea na pia atajikumbusha kifo na kisha ataondoka.

Na hii ni sifa ya hajji na umra:

Anatakiwa mwenye kuhijji kuchagua chumo zuri la halali, na ajiepushe muislamu na chumo la haramu, kwa sababu chumo la haramu ni sababu ya kutokubaliwa Hajji yake, na imekuja katika hadithi ya Mtume - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na amani-: "Kila nyama iliyoota kwa chumo la haramu basi moto ndiyo stahiki yake"([29]), Na Hajji anatakiwa achague rafiki mwema mtu mwenye Tauhiid na imani.

Sehemu za kuhirimia.

Na akifika Hajji miiqaat hapo atahirimia (kunuia), ikiwa atakuwa kwenye gari au mfano wake, na ikiwa atakuwa kwenye ndege atahirimia akikaribia miiqati kabla hajaipita, na sehemu za kuhirimia ambazo amewaamrisha Mtume-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na amani- watu wahirimie sehemu tano.

1- Dhul- huleifa ( Ab-yaar alii) ni kwa ajili ya watu wa Madina.

2- Al- juhfa( Qar-bu raabiy) na hiyo ni ya watu wa shamu na masri na morocco.

3- Qar-nul manaazil ( Al- sailu au Waadi muharram) ni kwa ajili ya watu wa Najdi,Twaaif,na yeyote atokeae upande huo.

4- Dhaatu Ir-qi (ni ya watu wa Iraqi)

5- Yalam lam ni ya watu wa Yemen.

Na yeyote atakaepitia katika sehemu za kuhirimia naye siyo mtu wa sehemu hiyo, basi miiqaati yoyote atakayopitia ndiyo sehemu yake hiyo ya kuhirimia. Na watu wa Makkah na wale ambao wapo nje ya sehemu za kuhirimia (Miiqaat) hao watahirimia majumbani mwao.

Sifa za kuhirimia

Ni sunna na inapendeza ajisafishe na ajitwaharishe na ajipake manukato kabla ya kuhirimia, kisha atavaa mavazi ya kuhirimia akiwa mii-qaat, na mwenye kupanda ndege atajiandaa katika mji wake, kisha atanuia na ataleta talbiya (Tamko la kuitikia)([30]) atakapokaribia mii-qaat au kuwa sawa nayo, na mavazi ya kuhirimia kwa mwanaume ni kikoi na shuka ambazo hazijashonwa atajifunga kwazo mwili wake na asifunge wala kuziba kichwa chake. Ama mwanamke katika kuhirimia kwake hana vazi maalumu, na hakika ni wajibu kwa mwanamke avae mavazi yaliyo mapana yenye kusitiri ambayo hayana ufitinishaji watakapo muona watu, na wala asivae usoni mwake na mikononi nguo zilizoshonwa atakapo hirimia, kama vile Barakoa na Glovsi, na hakika atafunika uso wake kwa ncha ya mtandio wa kichwani mwake atakapowaona wanaume, kama walivyokuwa wakifanya wanawake wa kiislamu na wanawake wa maswahaba wa Mtume- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na amani-

Kisha baada ya kuvaa mwenye kuhiji mavazi ya ihraamu atanuia moyoni mwake kufanya Umra, kisha ataleta tal-biya kwa kusema (Allahumma Labbaika Umratan) kisha atamaliza ibada hiyo ya umra kwa kunyoa na kuvaa mavazi yake ya kawaida na ([31]) atasubiri mpaka wakati wa Hijja. Na Tamattui ni bora zaidi kwa sababu Mtume -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na amani- aliwaamrisha maswahaba wake na akawalazimisha kufanya Tamattui, na akamchukia yeyote aliyesita kutekeleza amri yake, isipokuwa yule ambaye alikuwa anamiliki kichinjwa ([32]) huyo atabakia kuwa Qaarin -mwenye kubakia katika mavazi yake ya ihraam na bila kunyoa- kama alivyofanya bwana Mtume- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na amani-, Na Al- Qaarin: Ni yule ambaye anasema katika kuitikia kwake "Allahumma labaika Umratan wa Hajjan" na wala hatovua vazi lake la Ihraam mpaka achinje kichinjwa chake siku ya Eid ya kuchinja.

Na Al- muf-rid: Ananuia Hijja peke yake na atasema : " Allahumma Labbaika Hajjan"

Mambo yaliyo haramu kwa mwenye kuhirimia (Kunuia kuingia katika ibada)

Na akitia Nia muislamu ya kuingia katika ibada ya hijja au Umra ni haramu kwakwe kufanya yafuatayo:

1- Kufanya tendo la ndoa na vyote vyenye kupelekea kufanya hivyo kama kubusu na kugusa kwa matamanio, na kumchumbia mwanamke, na kufunga ndoa, mwenye kuhirimia haoi wala haolewi.

2- kunyoa nywele au kupunguza chochote katika hizo nywele

3- kupunguza kucha.

4- kufunika kichwa kwa mwanaume kwa kitu chochote chenye kufunika, ama kujikinga kwa kutumia mwamvuli na hema na gari hakukatazwi.

5- Kujipaka marashi na kuyanusa.

6- Kuwinda mnyama pori, basi na asimuwinde wala asimjulishe alipo muwindaji.

7- mwanaume kuvaa mavazi yaliyoshonwa, na mwanamke kavaa kilichoshona kwenye uso wake na mikono yake,na atavaa mwanaume makobazi na ikiwa hatopata basi na avae khofu mbili.

Na ikiwa atafanya hivi vilivyokatazwa kwa kutokujua au kwa kusahau atavua na wala hatowajibika kufanya lolote.

Na atakapofika Al-kaaba yule mwenye kuhirimia atatufu twawafu Al-quduum (ya kufika) ([33]) mizunguko saba, ataanza kuanzia usawa wa jiwe jeusi, na hii ndiyo twawafu ya Umra yake, na katika twawafu hakuna dua maalumu bali atamtaja tu Mwenyezi Mungu na ataomba kwa kadiri ya wepesi wake ([34]) kisha atasali rakaa mbili nyuma ya Maqaam Ibrahiim ([35]) ikiwa itakuwa ni wepesi kwake ikishindikana atasali popote katika Msikiti mtukufu wa Makkah, kisha ataelekea sehemu ya kukimbilia ([36]) Basi na atauanza mlima wa Swafa kwa kupanda juu yake, na ataelekea Qibla na ataleta Takbira naTahliil na ataomba, kisha atakwenda harakaharaka kuelekea mlima wa Marwa na atapanda juu yake na ataelekea Qibla na kuleta Takbira, na atamtaja Mwenyezi Mungu na atamuomba, kisha atarudi kilima cha swafaa mpaka akamilishe mizunguko saba, kwenda kwake huhesabike ni mzunguko mmoja na kurudi kwake kunahesabike ni mzunguko mwingine, kisha atapunguza nywele za kichwa chake, na mwanamke atachukua ncha za nywele zake kwa kiasi cha ncha za vidole, na kwa kufanya hivi anakuwa Mwenye kufanya Tamattui amemaliza Umra yake na atavua mavazi yake ya ihraam, na itakuwa kwake halali kila kitu kilichoharamishwa kwake baada ya kuhirimia.

Na kama ataipata hedhi mwanamke au akajifungua kabla ya kuhirimia au baada yake, basi mwanamke huyo itabadilika ibada yake na itakuwa Qiraan, ataleta tal-biya ya Hijja na Umra baada ya kuhirimia kama mahujaji wengine; kwa sababu Hedhi na Nifasi havimzuilii kuhirimia, wala kusimama katika viwanja vitakatifu, isipokuwa vinamzuia kufanya twawafu katika nyumba tukufu peke yake. Na atafanya yote wanayoyafanya mahujaji isipokuwa twawafu ataichelewesha mpaka atakapotwaharika, na ikiwa atatwaharika kabla ya kuhirimia Hajji au umra na kabla ya kutoka kuelekea Minna, basi ataoga na atatufu na kufanya sa-ayi,na atapunguza nywele zake na hapo atakuwa amemaliza ibada yake ya umra aliyoikusudia kisha atahirimia Hijja pamoja na watu watakapo hirimia siku ya nane, na wakihirimia watu Hijja kabla hajatwaharika basi itabadilika ibada yake na atakuwa ni Qaarin, ataletaTal-biya pamoja akiwa katika vazi lake la ihraam, na atafanya kila alifanyalo Hajji miongoni mwa hayo ni kutoka kuelekea viwanja vya Minna, na kusimama viwanja vya Arafa na Muzdalifa, na kutupa mawe na kuchinja na kupunguza nywele za kichwa chake siku ya Eid ya kuchinja, na akitwaharika na akaoga na akatufu twawafu ya Hijja na akafanya Saa-ayi ya Hijja.

Na hii twawafu na Saa-yi zinamtosheleza kwenye hijja na umra yake, na kama ilivyotokea kwa Aisha mama wa waumini- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- akamfahamisha Aisha kuwa Twawafu yake na Saa-ayi yake zinamtosha kwa ajili ya hajji yake na Umra yake alipotufu pamoja na watu na kusaa-ayi, kwa sababu mwenye kukusanya Hijja na Umra ni kama aliyefanya Hijja peke yake na hahitajiki kufanya isipokuwa Umra moja tu na Saa-ayi moja ([37]), kwa ruhusa ya bwana Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- aliyompa Aisha na pia yeye Mtume kufanya hivyo, na kwa maneno ya bwana Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- katika hadithi nyingine: ''Huingia matendo ya Umra katika matendo ya Hijja mpaka siku ya kiama" na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.

Na ikifika siku ya nane katika mwezi wa Hijja wanahirimia mahujaji Ibada ya Hijja wakiwa majumbani mwao katika mji wa Makkah, kama walivyohirimia Miiqaat, watajisafisha kisha watavaa mavazi ya Ihraam, kisha watanuia kuhijji sawa awe mwanaume au mwanamke, kisha ataleta Tal-biya kwa kusema "Allahumma Labbaika Hajjan" na atajiepusha na yaliyokatazwa kwa mwenye kuhirimia mpaka arudi kutoka muzdalifa kwenda Minna katika siku ya kuchinja, na atatupa mawe katika kiukuta cha Aqabah na mwanaume atanyoa nywele za kichwa chake na mwanamke atapunguza nywele zake.

Na akihirimia Hajji katika siku ya nane anatoka na mahujaji kwenda Minnah, na atalala Mina atasali sala zote kwa wakati wake kwa kupunguza bila kukusanya, na likichomoza jua siku ya Arafa ataelekea Namira na mahujaji na atakaa huko mpaka asali na imamu au sehemu ambayo husaliwa hapo jamaa ya Adhuhuri na Alasiri kwa kukusanya pamoja na kupunguza, kisha ataelekea Arafa baada ya kupinduka jua. ikiwa ataelekea kutoka Minna kwenda Arafa na akakaa kwenye ncha ya sehemu ya Arafa basi yafaa, na Arafa yote ni sehemu ya kusimama.

Na atazidisha Hujaji akiwa Arafa kumtaja sana Mwenyezi Mungu na kuomba dua na kutaka msamaha, na ataelekea Qibla na siyo mlima wa arafa; kwa sababu mlima ni sehemu tu ya Arafa haifai kuupanda mlima huo kwa ajili ya ibada, wala haifai kujipaka kwa kutumia mawe yake; kwa hakika kufanya hivyo ni uzushi ulioharamishwa.

Na wala haondoki Hujjaji kutoka Arafa mpaka lizame jua, kisha baada ya kuzama jua wataondoka mahujaji kuelekea Muz-dalifa, na wakifika Muz-dalifa watasali sala ya Magharibi na Isha kwa ukusanyaji wa kuchelewesha na watapunguza sala ya Isha tu na pia watalala hapo, na likichomoza Al-fajiri watasali Al-fajiri na watamtaja Mwenyezi Mungu, kisha wataelekea Mina kabla ya kuchomoza jua, na wakifika Mina watatupa mawe kwenye Jamratal Aqabah baada ya kuchomoza jua na watatupa vijiwe saba vyenye usawa wa Dengu siyo vikubwa wala vidogo, na wala haifai kuitupia viatu, kwa sababu huu ni mchezo anaowapambia shetani, na kumdhalilisha shetani ni kufuata amri ya Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kufuata muongozo wake, na kuacha aliyoyakataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Kisha baada ya kutupa mawe Hujjaji atamchinja mnyama wake, kisha atanyoa nywele za kichwa chake, na mwanamke atapunguza. Na ikiwa mwanaume atapunguza nywele pia yafaa; lakini kunyoa ni bora zaidi ya mara tatu kuliko kupunguza, kisha atavaa mavazi yake na inakuwa kwake halali kila kitu kilichokuwa haramu baada ya kuhirimia isipokuwa kumuingilia mwanamke, kisha wataelekea Makka na atafanya twawafu ya Hijja na Saa-yi, na kwa hivyo inakuwa kwake halali kila kitu mpaka kumuingilia mke wake, kisha atarudi Mina atakaa huko Mina masiku yaliyobakia kuanzia siku ya Eid na siku mbili na nyusiku zake baada ya Eid atalala Mina kwa lazima, na atatupa mawe kwenye Jamra (Vikuta) vitatu katika siku ya kumi na moja na siku ya kumi na mbili baada ya kupinduka jua, ataanza na kiukuta kidogo ambacho kipo Mina kisha kiukuta cha kati, kisha kiukuta cha Aqabah ambacho alikitupia mawe siku ya Eid, kila kuikuta kimoja atakitupia vijiwe saba, ataleta takbira kwa kila kijiwe, na mawe ya kutupia kwenye vikuta anayachukua kutoka nyumbani kwake ([38]) kwenye viwanja vya Mina. Na yeyote atakaye kosa sehemu ya kufikia katika viwanja vya mina, atafikia pale panapoishia mahema.

Na akitaka kuondoka kutoka Minna baada ya kutupa mawe katika siku ya kumi na mbili ni haki yake kuondoka, na ikiwa atachelewa mpaka siku ya kumi na tatu ni bora zaidi na atatupa vijiwe baada ya kupinduka jua, na kama atataka kusafiri basi atafanya twawafu ya kuiaga nyumba tukufu kisha atasafiri baada ya twawafu wakati huohuo, na mwanamke mwenye Hedhi na Nifasi ikiwa alishatufu twawafu ya Hijja na akafanya Saa-yi atakuwa hana twawafu ya kuiaga nyumba tukufu.

Na kama Hujjaji atachelewesha kumchinja mnyama wake mpaka siku ya kumi na moja au kumi na mbili au kumi na tatu inafaa kwake kufanya hivyo, na kama atachelewesha kufanya twawafu ya Hijja na Saa-yi mpaka atoke kabisa Minna inafaa kwake kufanya hivyo pia, lakini bora zaidi ni vile tulivyotangulia kuweka wazi.

Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi, Na rehma na amani za Allah ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na ali zake na Maswahaba zake.

Imani

Kwa hakika amefanya Mwenyezi Mungu kuwa ni wajibu kwa muislamu kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kuamini nguzo za uislamu, na akawajibisha kuwaamini Malaika wake ([39]), na vitabu vyake ambavyo ameviteremsha kwa Mitume wake, na ambavyo amevihitimisha kwa kuileta Qur'ani na akavifuta vitabu hivyo kwa Qur'ani, na akaifanya Qur'ani ndiyo yenye kivitawala vitabu vyote, na akawajibisha kuwaamini Mitume wa Mwenyezi Mungu kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kwa sababu ujumbe wao ni mmoja na dini yao ni moja nayo ni uislamu, na aliyewatuma ni mmoja naye ni Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote. Na inamlazimu muislamu aamini kuwa Mitume ambao amewataja Mwenyezi Mungu katika Qur'ani kuwa ni Mitume wa Mwenyezi Mungu waliotumwa kwa umma wao uliopita, na aamini kuwa Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ndiyo wa mwisho wao, na ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyetumwa kwa watu wote, na watu wote baada ya kutumwa Muhammad wanakuwa ni umma mmoja wa kwake yeye mpaka mayahudi na manaswara na wengine wasiokuwa hao katika dini nyingine; kwa sababu watu wote waliopo duniani ni umma wa Mtume Muhammad na wanalazimishwa na Mwenyezi Mungu kumfuata.([40])

Na Mussa na Issa na Mitume wote wako mbali na yeyote asiyemfuata Mtume Muhammad- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na wapo mbali na asiyeingia katika uislamu, kwa sababu muislamu ni mwenye kuwaamini Mitume wote na mwenye kuwafuata, na asiye muamini Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kumfuata na kuingia katika uislamu basi huyo amewapinga Mitume wote na amewakadhibisha. hata kama atadai kuwa anamfuata mmoja kati ya hao Mitume, na zimetangulia dalili juu ya hilo katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu sehemu ya pili.

Na Amesema Mtume Muhammadi Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni" ([41]).

Na ni wajibu kwa muislamu aamini kufufuliwa baada ya kufa na kuhesabiwa na kulipwa na aamini pepo na moto, na ni wajibu juu yake kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na maaana ya kuamini Qadar:

Ni Muislamu kuamini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alikwishajua kila kitu, na akajua matendo ya waja kabla ya kuumba mbingu na ardhi, na akaandika ujuzi huo kwenye mbao zilizohifadhiwa kwake na muislamu anajua kuwa alichokitaka Mwenyezi Mungu kiwe basi kitakuwa, na kile ambacho hakutakakiwe hakitakuwa, na kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba waja ili wamtii na akawabainishia na akawapa uwezo na matashi ambayo wanaweza kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu kwa kutumia uwezo na matashi yao; na wakapata kwa ajili hiyo thawabu, na yeyote atakaye muasi atastahiki adhabu.

Na kutaka kwa mja kunafuata kutaka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ama Qadar ndiyo ambayo Mwenyezi Mungu hakuiwekea matashi ya mwanadamu wala hiyari, bali huwapitishia hata kama si kwa kutaka kwao mfano kukosea na kusahau, na yale wayatendayo kwa kulazimishwa, kwa mfano ufakiri na maradhi na misiba na mfano wake, kwa hakika Mwenyezi Mungu hawafuatishii adhabu kwa kutokewa na hayo bali anawalipa malipo makubwa kwa kupatwa na misiba, ufakiri, maradhi ikiwa mtu atasubiri na akaridhia mipango Mwenyezi Mungu.

Yote hayo yaliyotangulia yampasa muislamu kuyaamini.

Na waislamu wenye imani ya juu kwa Mwenyezi Mungu na wenye daraja ya juu peponi (watu wema), ambao wanamuabudu Mwenyezi Mungu na wanamtukuza na wanamnyeyekea kama vile wanamuona, na wala hawamuasi kwa siri wala waziwazi na wanaitakidi kuwa anawaona popote wawapo, na wala hakijifichi kitu katika matendo yao na kauli zao na nia zao, na wanatii amri zake na wanaacha kumuasi, na ikiwa ataangukia mmoja wao katika kosa-kuhalifu amri ya Mwenyezi Mungu; hutubia kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli na haraka na hujuta kwa aliyotenda, na akamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na akawa hakurudia tena; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Kwa hakika Mwenyezi Mungu,Yuko pamoja na waliomcha kwa kuyafuata Aliyoyaamrisha na kuyaepuka Aliyoyakataza; na yuko pamoja na wale wanatenda wema". [An-nahli: 128].

Ukamilifu wa dini ya kiislamu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani tukufu "Leo hii nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema zangu, na nimekuridhieni kuwa Uislamu ndiyo dini yenu". [Al Maida: 3] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwa mja wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, inawaongoza watu kwenye njia nzuri kabisa nayo ni mila ya Kiislamu, na inawapa bishara njema Waumini, wanaofanya yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaamrisha kwayo na wanaokomeka na yale ambayo Amewakataza nayo, kwamba watakuwa na malipo makubwa", [Al Israai: 9]. Na amesema Mwenyezi Mungu- kutakasika na machafu ni kwake na mtukufu- kuhusu Qur'an: "Na tumekuteremshia kitabu hiki kielezacho kila kitu na ambacho ni uongofu na rehema na habari njema kwa waislamu". [An Nahli 89].

Na katika hadithi sahihi amesema Mtume- Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Kwa hakika nimewaacha kwenye njia nyeupe ambayo usiku wake ni kama mchana, hatoachana na njia hiyo yeyote isipokuwa ataangamia"([42]). Na Alisema Mtume -Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Nimewaachieni mambo mawili ikiwa mtashikamana nayo hamtopotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake"([43])

Na katika Aya zilizotangulia:

Anatoa habari Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya ya kwanza kuwa yeye amewakamilishia waislamu dini yao, na hakuna mapungufu ndani yake hata kidogo na haihitajii kuzidishwa hata kidogo, na ni dini yenye kufaa katika kila zama na kila mahala na kila umati, na anatoa habari kuwa ametimiza neema yake kwa waislamu kwa kuwapa dini hii tukufu ya upole na iliyokamilika, na kwa ujumbe wa mwisho wa Mtume Muhammad -Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-na kuudhihirisha uislamu na kunusuru watu wake na wenye kuwafanyia uadui, na anatoa habari kuwa yeye ameuridhia uislamu kuwa ni dini ya watu, na haichukii hata kidogo na wala hamkubalii yeyote kuwa na dini isiyokuwa uislamu.

Na katika Aya ya pili anatoa habari Mwenyezi Mungu kuwa Qur'ani tukufu ni muongozo ulio kamilika, ndani yake kinaweka wazi haki na kutatua mambo ya dini na dunia, na hakuna heri yoyote isipokuwa umeifahamisha wala hakuna shari isipokuwa umeitahadharisha, na kila jambo na kila tatizo la zamani au la sasa au lijalo kwa hakika utatuzi sahihi na wenye uadilifu ni Qur'ani, na utatuzi ambao unakwenda kinyume na Qur'an ni ujinga na dhulma.

Basi na Elimu, na Itikadi na Siasa na utaratibu wa kuhukumu na elimu ya Saikolojia na uchumi pamoja na elimu ya jamii na nidhamu za utoaji adhabu na mambo mengine anayoyahitajia mwanadamu, yote hayo ameyabainisha Mwenyezi Mungu katika Qur'ani na kwa kupitia ulimi wa Mtume wake Muhammad-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ameweka wazi kiukamilifu, kama alivyo habarisha Mwenyezi Mungu Mtukufu jambo hilo katika Aya iliyotajwa, pale alipotoa habari Mwenyezi Mungu kuwa: (Na tumekuteremshia Kitabu chenye kuweka wazi kila kitu ) Surat Nahl (89).

Na katika Sehemu inayofuata kuna ufafanuzi uliochambuliwa kwa ufupi kuhusu ukamilifu wa dini ya uislamu, na njia yake iliyokamilika na iliyokuwa sawa.

 Sehemu ya Nne - Muongozo wa uislamu

Muongozo wa kwanza:

Wajibu wa kwanza aliomuamrisha Mwenyezi Mungu mwanadamu ajifunze elimu; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Basi jua, ewe Nabii, kwamba hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na utake msamaha wa dhambi zako, na uwaombee msamaha Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Mwenyezi Mungu anazijua harakati zenu mnapoangaza mchana na mahali pa kutulia kwenu mnapolala usiku. [Surat muhammad 19], Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Anawanyanyua (daraja) Mwenyezi Mungu wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja za juu zaidi, na Mwenyezi Mungu kwa yale mnayoyafanya ni mjuzi". [Al-Mujadilah: 11]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na sema, Mola wangu nizidishie elimu". [Twaha: 114]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Waulizeni wanao jua ikiwa hamfahamu) [Al-Anbiya:7] Na amesema wa mwisho katika Mitume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani -katika hadithi sahihi: Kutafuta elimu ni lazima kwa kila muislamu" ([44]), Na Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- Ubora wa mwenye elimu ukilinganishwa na mwenye kufanya ibada, mwenye Elimu ni bora kama ulivyo mwezi katika usiku wa kumi na nne unavyoshinda sayari zote kwa kung'aa" ([45])

Na elimu katika uislamu imegawanyika katika vigawanyo vingi kwa upande wa ulazima wake:

Kigawanyo cha kwanza: Ni faradhi ya lazima kwa kila mwanadamu, sawa awe mwanaume au mwanamke, hapewi udhuru yeyote kwa kutoijua, nayo ni kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumjua Mtume wake Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, na kujua mambo ya lazima katika dini ya uislamu ([46]).

Kigawanyo cha pili: Ni faradhi ya kutoshelezana akiifanya yeyote mwenye kutosheleza, huondoka madhambi kwa watu waliobakia, na inabakia kuwa ni jambo lenye kupendeza kwa wengine, na nako ni kujua hukumu za sheria ya uislamu ambayo humuwezesha mjuzi wa elimu hiyo kufundisha na kuhukumu na kutoa fat-wa, na vilevile kujua wanayoyahitajia waislamu kutokana na utengenezaji na kazi za lazima katika maisha yao. basi yampasa mwenye kuyasimamia mambo ya waislamu ikiwa hatopatikana mwenye kutosheleza afanye kazi ya kuwapata wajuzi watakaowatosheleza waislamu kwenye mambo ya lazima katika maisha yao.

Muongozo wa pili: Katika Akida:

Amemuamrisha Mwenyezi Mungu Mtume wake -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- awatangazie waumini wote kuwa wao wote ni waja wa Mwenyezi Mungu peke yake, inawapasa wamuabudu yeye peke yake, na akawaamrisha wafungamane na Mwenyezi Mungu moja kwa moja pasina kupitia kwa yeyote katika ibada zao, kama ilivyotangulia kubainishwa hilo katika maana ya (Laailaha illa llah) na amewaamrisha wategemee kwa Mwenyezi Mungu pekee yake, na wala wasimuogope ila yeye, na wasitarajie ila kwake yeye peke yake ([47]) kwa sababu yeye peke yake ndiye mwenye kuleta manufaa na madhara, na wamsifie sifa za ukamilifu ambazo amejisifia yeye mwenyewe na akamsifia kwa sifa hizo Mtume wake-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kama ilivyobainishwa mwanzo.

Muongozo wa Tatu: Katika mshikamano kati ya watu:

Amemuamrisha Mwenyezi Mungu mwanadamu awe mtu mwema, anayefanya haraka kumuokoa mwanadamu kwa kumtoa katika giza la ukafiri na kumpeleka kwenye nuru ya uislamu; na kwa sababu hiyo nimetunga kitabu hiki na kukisambaza ili kutekeleza baadhi ya wajibu.

Na akaamrisha Mwenyezi Mungu kuwa mshikamano unaomuunganisha muislamu na mtu mwingine ni mafungamano ya kumuamini Mwenyezi Mungu, na awapende waja wa Mwenyezi Mungu walio wema wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata kama atakuwa mtu wa mbali, na awachukie wanaomkufuru Mwenyezi Mungu na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata kama watakuwa ni watu wake wa karibu, na haya mafungamano yanawakusanya waliotengana, na huunganisha waliotofautiana, tofauti na mshikamano wa nasaba na utaifa na maslahi ya kidunia, kwa maslahi hayo huondoka na kuisha kwa haraka sana.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Huwezi kuwapata watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho kuwa wanawapenda wale wenye kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata wakiwa ni baba zao au watoto wao au ndugu zao au jamaa zao". [Al- Mujaadal: 22] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu zaidi". [Al Hujrati: 13].

Anatoa habari Mwenyezi Mungu kutakasika na machafu ni kwake katika Aya ya kwanza: kuwa wenye kumuamini Mwenyezi Mungu hawawapendi maadui wa Mwenyezi Mungu hata kama watakuwa ni watu wao wa karibu.

Anatoa habari Mwenyezi Mungu kutakasika na machafu ni kwake katika Aya ya pili: kuwa mtu bora kwake na mwenye kupendeza kwake ni yule mwenye kumtii awe anatokana na jinsia yoyote au rangi yoyote.

Na kwa hakika ameamrisha Mwenyezi Mungu kufanya uadilifu kwa adui na rafiki, na akajiharamishia dhulma, na akaifanya dhulma kuwa ni haramu kwa waja wake na akaamrisha uaminifu na ukweli, na akaharamisha hiyana, na akaamrisha kuwafanyia wema wazazi wawili, na kuunga udugu, na kuwafanyia wema mafukara, na kushiriki katika mambo ya kheri, na akaamrisha kufanya Ih-saan kwa kila kitu mpaka wanyama, na akaharamisha kumuadhibu mnyama na akaamrisha kumfanyia wema ([48]) Ama wanyama wenye kudhuru kama vile Mbwa mwenye kujeruhi watu ([49]) na Nyoka na Nge na Panya na Ndege Tai na Mjusi kafiri hao huuliwa; ili kuzuia shari zao na sio kuwaadhibu.

Muongozo wa Nne: Katika kujichunga na muumini kuupa mawaidha moyo wake.

Zimekuja Aya katika Qur'ani tukufu zinawabainishia watu kuwa Mwenyezi Mungu anawaona popote walipo, na yeye hujua matendo yao yote, na anazijua Nia zao, na yeye huwahesabia matendo yao na maneno yao, na Malaika ni wenye kuwa nao na kuandika kila walifanyalo kwa siri na wazi, na Mwenyezi Mungu atawahesabu kwa kila wanachokifanya na kukisema, na amewatahadharisha na adhabu zake zenye kuumiza watakapokuwa wamemuasi katika maisha ya hapa duniani, na wakaenda kinyume na maamrisho yake, na adhabu hizi zikawa ni makemeo kwa wenye kumuamini Mwenyezu Mungu, huwazuia kutumbukia kwenye kumuasi; basi kutokana na adhabu hizo wakaacha maovu na kuzivunja sheria kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ama yule ambaye hamuogopi Mwenyezi Mungu na anafanya maovu, akipatikana na maovu hayo, hakika amemuwekea Mwenyezi Mungu Mtukufu mtu huyo adhabu ya kumfanya akome hapa duniani, nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu amewaamrisha waislamu waamrishe mema na wakataze mabaya, basi na Ahisi kila muislamu kuwa yeye anahusika mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kila kosa ambalo analiona mwenzake analifanya, mpaka amkataze kwa ulimi wake kufanya tendo hilo, ikiwa hatoweza kumzuia kwa mikono yake, Basi amemuamrisha Mwenyezi Mungu mwenye kiongozi wa waislamu ([50]) atekeleze adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa wenye kuvunja sheria, nazo ni adhabu kwa kadiri ya makosa yao, ameyaweka wazi Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'an na pia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- katika hadithi zake, na akaamrisha kuzifanyia kazi kwa waovu; na kwa kufanya hivyo utaenea uadilifu na amani na Raha.

Muongozo wa Tano: katika kusaidiana kijamii:

Ameamrisha Mwenyezi Mungu waislamu kusaidiana kati yao kwa hali na mali, kama ilivyo tangulia kuwekwa wazi hilo katika mlango wa zakah na sadaka, na akaharamisha Mwenyezi Mungu watu wasiwaudhi watu kwa maudhi ya aina yoyote, hata chenye kuudhi njiani amekiharamisha Mwenyezi Mungu, na akawaamrisha Mwenyezi Mungu waislamu kukiondosha chenye kuudhi atakapo kiona hata kama atakuwa aliyekiweka ni mtu mwingine, na ameahidi malipo kwa kufanya hilo, kama alivyo ahidi adhabu kwa mwenye kuudhi.

Na amefaradhisha Mwenyezi Mungu juu ya muumini kumpendelea ndugu yake kama anavyojipendelea yeye mwenyewe, na achukie kupatwa ndugu yake kama anavyochukia yeye katika nafsi yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na saidianeni katika wema na uchamungu na wala msisaidiane katika madhambi na kufanya uovu, na muogopeni Mwenyezi Mungu kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu) [Al Maaida: 2]. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Hakika waislamu wote ni ndugu, basi suluhisheni kati ya ndugu zenu) [Al- huj-raat 10] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Hakuna manufaa katika mengi ya maneno ya watu ya siri baina yao, isipokuwa iwapo ni mazungumzo yenye kuita kwenye kufanya mema ya utoaji sadaka au maneno mazuri au kuleta upatanishi baina ya watu. Na mwenye kuyafanya mambo hayo, kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, akitarajia thawabu Zake, tutampa thawabu nyingi zilizo kunjufu). [An-nisaa:114] Na Amesema Mtume Muhammadi Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: "Hawezi kuwa mmoja wenu na imani mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake".([51]) Na amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- katika Hutuba zake tukufu ([52]) ambazo alizitoa mwisho wa maisha yake katika Hijja ya kuaga, akitilia mkazo aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu nyakati zilizopita: na amepokea imamu Ahmad. "Enyi watu eleweni vyema kuwa Mola wenu ni mmoja na baba yenu ni mmoja, na tambueni vyema hakuna ubora kwa mwarabu kwa asiyekuwa mwarabu, wala hakuna ubora kwa asiyekuwa mwarabu kuliko mwarabu, wala mwekundu kwa mweusi wala mweusi kwa mwekundu isipokuwa kwa uchamungu, je nimefikisha?" Wakasema: Amefikisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-([53]) Na alisema Mtume -Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Hakika damu zenu ni haramu (kuzimwaga) na mali zenu kuzila kwa batili na kuzivunja heshima zenu ni haramu kwenu nyinyi, kama ilivyokuwa ni haramu kufanya hayo katika siku yenu hii, katika mji wenu huu, katika mwezi wenu huu, itabakia kuwa haramu mpaka siku mtakayokutana na Mola wenu, Eleweni vyema je nimefikisha? Wakasema: ndiyo. Akainua kidole chake mbinguni, na akasema: "Ewe Mola wangu (wa haki) shuhudia"([54]).

Muongozo wa sita: Katika Uongozi wa ndani:

Amewaamrisha Mwenyezi Mungu waislamu wajitawalishie kiongozi watakayemchagua kuongoza, na akawaamrisha wawe kitu kimoja na wala wasitofautiane na wawe ni umma mmoja, na akawaamrisha Mwenyezi Mungu kumtii imamu wao na viongozi wao isipokuwa hawatowatii ikiwa watawaamrisha kumuasi Mwenyezi Mungu, kwani haifai kumtii kiumbe katika kumuasi Mwenyezi Mungu.

Na amemuamrisha Mwenyezi Mungu muislamu- ikiwa atakuwa katika mji ambao hawezi kuidhihirisha dini ya uislamu, na kuilingania -amemuamrisha auhame mji huo kwenda katika mji wa kiislam, nao ni mji ambao wanahukumu katika mambo yao yote kwa sheria ya Mwenyezi Mungu, na anahukumu kwa sheria hizo kiongozi wa kiislamu kama alivyoteremsha Mwenyezi Mungu.

Uislamu hautambui wala kukubali adhabu zilizowekwa kimikoa na za jinsia fulani au za kitaifa, na kwa hakika jinsia ya muislamu ni uislamu, na waja wote ni waja wa Mwenyezi Mungu, na ardhi ni ardhi ya Mwenyezi Mungu, na anahama muislamu kwenda kwingineko bila kupingwa kwa sharti ashikamane na sheria za Mwenyezi Mungu, na akienda kinyume na sheria yoyote atapitishiwa hukumu ya Mwenyezi Mungu,na katika kufanyia kazi sheria ya Mwenyezi Mungu na kutekeleza adhabu zake ni kutaka amani na watu kusimama sawa, na kuzia umwagaji wa damu zao na usalama wa heshima zao, na mali zao na hayo ni heri tupu, na kuacha kufanya hivyo ni shari tupu.

Amezilinda Mwenyezi Mungu: kwa kuharamisha vyenyekulewesha na madawa ya kulevya na vyenye kulegeza na kuudhoofisha mwili ([55]) na akaweka adhabu kwa mnywa pombe nayo ni viboko kuanzia (40-80) kila anapolewa, kwa ajili ya kumkemea na kulinda akili yake na kuwaepusha watu na shari zake.

Na amezihami Mwenyezi Mungu damu za waislamu: kwa kumlipizia kisasi aliyefanya uadui bila ya haki, basi huuliwa muuwaji, na ni sheria kwenye kujeruhi kufanywa kisasi, kama ilivyowekwa sheria kwa muislamu kujilinda mwenyewe na kulinda cheo chake na mali yake; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hakika katika kuwekwa sheria ya kisasi na utekelezaji wake kwa kutarajia kufikia uchaji Mwenyezi Mungu na kumuogopa kwa kumtii daima, kuna maisha ya amani kwenu, enyi wenye akili timamu" [Al Baqara: 179] Na Amesema Mtume wa Allah rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "yeyote atakaye uliwa kwa kutetea mali yake basi huyo ni shahidi, na atakaye uliwa kwa kutetea dini yake basi huyo ni shahidi, na atakaye uliwa kwa kutetea damu yake basi huyo ni shahidi, na atakayeuliwa kwa kutetea mke wake na watu wake basi huyo ni shahidi" ([56])

Na amezilinda Mwenyezi Mungu heshima za waislamu: kwa kuweka sheria ya kuharamisha kumuongelea muislamu ikiwa hayupo, kwa maneno anayoyachukia isipokuwa kwa haki, na kwa kuweka sheria ya kumuadhibu mwenye kusingizia ambaye humsingizia muislamu kwa kosa la kitabia, kwa mfano: Uzinifu, kufanya mapenzi kinyume na maumbile pasina kuwa na uthibitisho wa kisheria.

Na amezilinda Mwenyezi Mungu nasaba kuchanganywa kinyume na sheria, ([57]) na akazilinda Heshima kuchafuliwa kwa makosa ya kitabia kwa kuharamisha uzinifu uharamu ulio mkubwa kabisa na akaizingatia zinaa ni katika madhambi makubwa: na akaweka adhabu ya kumkomesha mfanyaji wake yatakapo timia masharti ya kupitisha hukumu kwa mzinifu.

Na amezilinda Mwenyezi Mungu Mali: kwa kuharamisha wizi na kughushi na kamari na rushwa na mengine yasiyokuwa hayo katika mapato yaliyoharamishwa, na ameilinda mali kwa kuweka sheria ya kumuadhibu mwizi na jambazi adhabu ya kukomoa, nayo ni kukata kiungo yatakapotimia masharti yake au kumuadhibu kwa adhabu itakayomkomesha, yatakapokuwa masharti haya yametimia pamoja na kuthibitika wizi.

Na aliyeziweka adhabu hizi ni Mwenyezi Mungu mjuzi mwenye hekima, na yeye ndiyo mjuzi zaidi wa mambo yanayowafaa viumbe wake, na yeye ni mwenye kuwahurumia zaidi, na hakika ameweka adhabu hizi ili iwe ni kafara ya makosa ya waislamu waovu, na kinga ya jamii kutokana na shari zao na shari ya wengine, na wale wanaokosoa vibaya kumuua aliyeua na kuukata mkono wa mwizi hao ni katika maadui wa uislamu na ni wenye kuupiga vita, kwa hakika wanakosoa kukata kiungo cha mgonjwa kilichoharibika na kisipokatwa uharibifu wake utaenea katika jamii nzima ([58]) na wakati huohuo wanapenda kuwauwa wasiokuwa na hatia kwa ajili ya malengo yao yenye dhulma.

Muongozo wa sita: Katika Siasa za Nje:

Amewaamrisha Mwenyezi Mungu waislamu na wenye kusimamia mambo ya waislamu, wawalinganie wasiokuwa waislamu waingie katika uislamu, ili wawaokoe kupitia uislamu kutoka katika giza la ukafiri na kuwaleta kwenye nuru ya kumuamini Mwenyezi Mungu, na uovu wa kuzama kwenye anasa za haya maisha ya kidunia na kujinyima furaha ya moyo ambayo ananeemeka nayo muislamu kiukweli. Na amri hii ya Mwenyezi Mungu kwa muislamu, ni kuwa awe mtu mwema anayewafaa wanadamu wote kwa wema wake, na anakwenda mbio ili kuwaokoa wanadamu wote, Ni tofauti na mfumo wa mwanadamu; kwa hakika mfumo huo unamtaka mwanadamu awe mwananchi mwema tu, na hii ni dalili ya ubovu wake na mapungufu yake, na inaonyesha uzuri wa uislamu na ukamilifu wake.

Na amewaamrisha Mwenyezi Mungu waislamu waandae nguvu kiasi cha uwezo wao kwa ajili ya maadui wa Mwenyezi Mungu, ili waulinde uislamu na waislamu, na ili wawatishie maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui wao, kama alivyo ruhusu Mwenyezi Mungu waingie mikataba ya ahadi na wasiokuwa waislamu, ikiwa itahitajika kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria ya kiislamu, na ameharamisha Mwenyezi Mungu kuvunja ahadi waliyokubaliana na maadui zao, isipokuwa wakianza maadui kuvunja ahadi, au wakafanya jambo linalolazimisha kuvunja ahadi, basi watawadhihirishia kuivunja ahadi.

Na kabla ya kuanza vita na wasiokuwa waislamu, ameamrisha Mwenyezi Mungu waislamu wawalinganie maadui zao waingie kwenye uislamu kwanza, ikiwa watakataa watawataka watoe Jiz-ya na wakubali sheria ya Mwenyezi Mungu ([59]), na ikiwa watakataa itapiganwa vita mpaka fitina iondoke ([60]) na iwe dini yote ni ya Mwenyezi Mungu.

Na katika hali ya vita, ameharamisha Mwenyezi Mungu kuwauwa watoto na wanawake na wazee na Watawa ambao wapo kwenye makanisa yao, isipokuwa mwenye kushirikiana na wapiganaji kwa Rai ya kupigana, na akawaamrisha kuwafanyia wema mateka, na kwa haya tunafahamu kuwa vita katika uislamu haikusudiwi kuwa ni kutawala na kuchukua fursa, na kwa hakika hukusudiwa kueneza haki na rehema kwa viumbe, na kuwatoa watu kwenye kumuabudu kiumbe na kuwapeleka katika kumuabudu Mwenyezi Mungu Muumba.

Muongozo wa Nane: Katika Uhuru:

(A): Uhuru wa Itikadi:

Ametoa Mwenyezi Mungu Mtukufu Uhuru wa kiitikadi katika dini ya uislamu kwa yule asiyekuwa muislamu atakapoingia chini ya hukumu ya uislamu. Baada ya kutimia kumfahamisha, na baada ya kulinganiwa, basi ikiwa atachagua uislamu basi ndani ya uislamu atapata furaha na kufaulu kwake, na kama atachagua kubakia katika dini yake basi atakuwa amejichagulia mwenyewe ukafiri na uovu na adhabu ya moto, na kwa namna hii inakuwa ni hoja dhidi yake, na hana udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakati huo waislamu watamuacha katika itikadi yake kwa sharti atoe Jiz-ya (kodi) kwa hiari yao hali yakuwa wametii, na wafuate hukumu za kiislamu, na wala wasijidhihirishe na nembo za ukafiri wao mbele ya waislamu.

Ama muislamu hakubaliwi kutoka katika uislamu (kuritadi) baada ya kuingia, na akitoka hakika malipo yake ni kuuwawa, na hii ni kwa sababu yeye ametoka katika haki baada ya kuijua na hafai kubakia hai, isipokuwa akitubia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na akarudi katika uislamu. ([61])

Na japokuwa kuritadi kwake ni kwa kufanya jambo miongoni mwa mambo yanayo utengua (kuuvunja) uislamu, basi anatakiwa atubie kutokana na hicho kitenguzi kwa kukiacha na kukichukia na kumtaka Mwenyezi Mungu msamaha .

Na vitenguzi vya uislamu ni vingi; vilivyo mashuhuri zaidi ni:

Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, nako ni mja kumfanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu, mungu mwingine, hata kama itakuwa ni kwa kuweka muwakilishi kati yake na Mwenyezi Mungu akikiomba na kujikurubisha kwake, ni sawa akakubali uungu wake kwa jina na maana kwa kujua kwake maana ya uumbaji na ibada, kama washirikina wazama za ujinga ambao waliabudu masanamu yenye alama za watu wema kwa ajili ya kutaka uombezi wao-au hajakubali kuwa yeye ni muumba pamoja na Mwenyezi Mungu na kuwa ibada yake ni kumuabudu yeye kama washirikina wenye kujinasibisha na uislamu ambao hawawakubali wenye kuwaita kwenye Tauhiid, wakidai kuwa shirki ni kusujudia sanamu tu, au mja aseme kisicho Mwenyezi Mungu: huyu ni Mwenyezi Mungu.

Basi wao ni kama mwenye kunywa pombe na akaiita pombe kwa jina lisilo lake, na imeshatangulia kuelezea hali zao, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Basi mwabuduni Mwenyezi Mungu hali ya kumtakasia dini ) (2) Jua utanabahi kwamba wa kuitakidiwa Mola ni Mwenyezi Mungu tu lakini wale wanaofanya wengine kua waungu badala yake (husema) sisi hatuwaabudu hawa ila wapate kutufikisha karibu kabisa na Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atahukumu kati yao katika yale wanayohitilafiana bila shaka Mwenyezi Mungu hamuongoi aliye kafiri). [Al- zumar 2-3] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Huyo ndiye Mola wenu Mwenyezi Mungu mwenye Ufalme, na wale mnao waabudu kinyume chake wao hawamiliki hata ganda la kokwa la tende) (13) "Mnapowaomba, enyi watu, waabudiwa hawa badala ya Mwenyezi Mungu, hawasikii maombi yenu, na lau wangelisikia, kwa kukisia, wasingeliwaitikia nyinyi. Na Siku ya Kiyama, watajiepusha na nyinyi. Na hakuna yeyote wa kukupasha habari, ewe Mtume, mkweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu, Aliye Mjuzi, Aliye Mtambuzi" (14). [Faatir:13-14]

1- Kutowakufurisha washirikina na makafiri wengine kama mayahudi na manaswara na wenye kupinga uwepo wa Mwenyezi Mungu na majusi na matwaaghuuti ambao wanahukumu kinyume na alivyo teremsha sheria Mwenyezi Mungu, na wala hawaridhii hukumu ya Mwenyezi Mungu, na yeyote asiyewakufurisha baada ya kujua kumkufuru kwao Mwenyezi Mungu basi mtu huyo amekufuru.

2- Uchawi ambao unaendana na shirki kubwa, na yeyote atakaye fanya uchawi au akauridhia baada ya kujua kuwa mchawi ni kafiri basi na yeye amekufuru.

3- Kuamini kuwa sheria au nidhamu isiyokuwa ya uislamu ndiyo nzuri zaidi kuliko sheria ya uislamu, au hukumu isiyokuwa ya Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-ndiyo nzuri kuliko hukumu zake, au kufaa kuhukumu pasina kutumia hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Kumchukia Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- au kuchukia kitu ambacho anakijua kuwa ni katika sheria zake.

5- Kukicheza shere (kukejeli) chochote kinachojulikana ni katika dini ya uislamu.

6- Kuchukia ushindi wa Kiislamu au kufurahishwa na kushuka kwa uislamu.

Kuwaweka karibu makafiri kwa kuwapenda na kuwanusuru na hali yeye anajua kuwa mwenye kuwapenda anakuwa ni katika wao.

8- Kuamini kuwa yeye inafaa kwake kutoka nje ya sheria ya Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na hali yakuwa anajua kuwa haifai kwa yeyote kutoka katika sheria kwa jambo lolote.

9- Kuipamgongo dini ya Mwenyezi Mungu, na yeyote atakayeupuuza uislamu baada ya kukumbushwa, hajifunzi wala haifanyii kazi huyo kakufuru.

10- Kukataa hukumu miongoni mwa hukumu za uislamu zilizoafikiwa, na mtu mfano wake hawezi kuacha kuzijua, na dalili za hivi vitenguzi ni nyingi katika Qur'ani na sunna.

B- Uhuru wa kutoa Rai:

Na ametoa Mwenyezi Mungu uhuru wa kutoa Rai katika uislamu kwa sharti rai hiyo isipingane na mafundisho ya uislamu, na akamuamrisha muislamu kusema neno la haki mbele ya yeyote na wala asiogope kwaajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumu, na akalifanya jambo hilo kuwa ni jihadi iliyo bora, na akamuamrisha kutoa nasaha kwa viongozi wa waislamu na kuwakataza kuvunja sheria, na akamuamrisha kumjibu na kumkataza mwenye kulingania katika batili, na hii ndiyo nidhamu tukufu na nzuri katika kuheshimu Rai. Ama Rai yenye kwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu haruhusiwi mwenye rai hiyo kuitoa; kwasababu huko ni kubomoa na kuharibu na kuipiga vita haki.

C- Uhuru binafsi:

Ametoa Mwenyezi Mungu uhuru binafsi ndani ya mipaka ya sheria ya uislamu iliyotwaharika, akamuwekea mwanadamu - mwanaume au mwanamke- uhuru katika harakati zake kati yake na watu wengine, kama kuuza na kununua, na kutoa zawadi na wakfu na kusamehe, na akampa kila mwanaume na mwanamke uhuru wa kuchagua mwenza, na wala halazimishwi mmoja wao pasina ridhaa yake, na katika hali ya mwanamke kumchagua mwanaume asiyeendana naye katika dini, hakika mwanamke huyo hatoruhusiwa katika hilo, kwaajili ya kuhifadhi itikadi yake na ubora wake, na huyo mwanaume amezuiliwa kwa maslahi ya mwanamke na familia yake.

Na walii (msimamizi) wa mwanamke - ni mwanaume wa karibu yake kinasaba au muwakilishi wake -naye ni yule atakayesimamia ndoa yake, kwasababu mwanamke hajiozeshi mwenyewe kwa sababu kitendo hicho kinafananishwa na zinaa, walii atamwambia mume: nimekuozesha fulani na yeye atajibu kwa kusema: Nimekubali hii ndoa, na watahudhuria ufungaji ndoa mashahidi wawili.

Wala hauruhusu uislamu kwa muislamu avuke mipaka ambayo Mwenyezi Mungu amemuwekea, na kuwa yeye na vyote anavyovimiliki ni vya Mwenyezi Mungu, basi inampasa yawe matumizi yake ndani ya mipaka ya Mwenyezi Mungu ambayo amemuwekea hali yakuwa ni kufanya upole kwa waja wake na atakaye shikamana na huu muongozo ataishi kwa furaha, na atakaye kwenda kinyume na huu muongozo atataabika na kuangamia; na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaharamisha uzinifu na kulawiti kwa kutilia mkazo uharamu huo.

Ama kuondoa masharubu na kupunguza kucha na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kunyofoa nywele za kwapani na kutahiriwa, hakika Mwenyezi Mungu ameamrisha hayo.

Na akaharamisha Mwenyezi Mungu kujifananisha muislamu na maadui wa Mwenyezi Mungu kwa mambo ambayo ni maalumu kwao wao, kwasababu kujifananisha nao na kuwapenda katika mambo ya wazi wazi kunapelekea kwenye kujifananisha nao na kuwapenda kutoka moyoni.

Na Mwenyezi Mungu anataka muslamu awe ni chimbuko la fikra ya uislamu sahihi, na asiwe ni mwenye kupokea fikra za watu na rai zao, na Mwenyezi Mungu anamtaka muislamu awe ni mfano mzuri na sio mtu wa kuiga kibubusa.

Ama kuhusu utengenezaji na uzoefu wa fani zilizokuwa sahihi, kwa hakika uislamu umeamrisha kushikamana navyo na kuvichukua, hata kama mtangulizi wa hayo si muislamu; kwasababu Mwenyezi Mungu ndiye aliyemfunza mwanadamu, Amesema Mwenyezi Mungu: "Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua". [Al-alaq: 4].

Na hii ndiyo nasaha ya hali ya juu kabisa, na kumtengeneza mwanadamu katika kufaidi uhuru wake, na kuhifadhi na kuulinda utukufu wake kutokana na shari yake na shari ya mtu mwingine.

D- Uhuru wa makazi:

Amempa Mwenyezi Mungu muislamu uhuru wa makazi, na haifai kwa yeyote kuingia kwenye makazi yake pasina idhini yake, na wala hairuhusiwi kumtazama akiwa kwenye makazi yake bila idhini yake.

E- Uhuru wa Uchumi:

Na amempa Mwenyezi Mungu muislamu uhuru wa kuchuma na kutoa katika mipaka ambayo amewekewa, na akamuamrisha afanye kazi na achume; ili ajitosheleze yeye na familia yake, na ili atoe katika njia za kheri na wema, na wakati huo huo Mwenyezi Mungu amemuharamishia chumo la haramu, mfano: kula riba kucheza kamari kutoa rushwa, kuiba na kupata malipo kwa uganga na uchawi na zinaa na ulawiti, na akaharamisha thamani itokanayo na vitu vya haramu kama thamani ya picha ya vitu vyenye roho ([62]) na pombe na nguruwe na vyombo vya upuuzi vilivyoharamishwa na kukodishwa kwaajili ya kuimba na kucheza, na kama ilivyo chumo litokanalo na vyanzo hivi ni haramu basi vile vile kutoa katika chumo hilo ni haramu, na haifai kwa muislamu kutoa kitu chochote isipokuwa kwa njia iliyowekwa na sheria na hizi ni nasaha za hali ya juu kabisa na muongozo na kumtengeneza mwanadamu kwenye chumo lake na utoaji wake, ili aishi akiwa ni mwenye kujitosheleza kwa chumo la halali na awe mwenye furaha.

Muongozo wa Tisa: Kuhusu Familia:

Amepangilia Mwenyezi Mungu familia katika sheria ya kiislamu mpangilio uliokamilika, na furaha hutimia kwa wenye kufuata nidhamu hiyo, akaweka sheria ya kuwafanyia wema wazazi wawili- Mama na Baba- kwa kuongea nao maneno mazuri na kuwatembelea wakati wote ikiwa atakuwa mbali nao, na kuwahudumia na kuwatekelezea haja zao na kuwapa mahitaji na kuwapatia makazi ikiwa wote wawili ni mafakiri au mmoja kati yao, na ameahidi Mwenyezi Mungu adhabu kali kwa mwenye kuwapuuza wazazi wake, na akaahidi furaha kwa mwenye kuwafanyia wema, na akaweka sheria ya kuoa na akabainisha hekima yake katika kitabu chake, na kwa kupitia ulimi wa Mtume wake -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-.

Hekima ya kuweka sheria ya ndoa:

1- Kwa kuoa kunatimia sababu kubwa miongoni mwa sababu za usafi na kuhifadhi uchi kwa kuepukana na zinaa- na kuyahifadhi macho na kuangalia vilivyo haramu.

2- Kwa kuoa kunapatikana utulivu kwa wanandoa wote wawili; kwasababu Mwenyezi Mungu ameweka kati yao wawili mapenzi na huruma.

3- Kwa kuoa kunazidisha idadi ya waislamu kuzidi kisheria ambako ndani yake kuna usafi na usawa.

4- Kwa kuoa anakuwa kila mmoja kati ya wanandoa wawili ni mwenye kumuhudumia mwenzake ikiwa kila mmoja wao atasimamia majukumu yake ambayo yanaendana na tabia yake kama alivyo jaalia Mwenyezi Mungu kutakasika na machafu ni kwake.

Basi mwanaume hufanya kazi nje ya mazingira ya nyumbani na huchuma mali ili aweze kumuhudumia mke wake na watoto wake, hivyo mke hufanya kazi ndani ya nyumba yake, naye hubeba mimba, hunyonyesha, kulea watoto, na hufanya kazi kumuandalia mume wake chakula, na kuiandaa nyumba na kutandika kitanda, na mume akiingia akiwa amechoka mwenye wasiwasi huondoka uchovu na wasiwasi na huongea na mke wake na watoto, na huishi wote kwa utulivu na furaha. Na wala hakuna kizuizi cha kumsaidia mume wake -ikiwa wataridhiana kwa hilo- kwa kufanya baadhi ya kazi ambazo mwanamke atajichumia mwenyewe ili kumsaidia mume wake kwa chumo lake, lakini hilo limewekewa masharti ya kuwa iwe kazi ambayo anaifanya iko mbali na wanaume pale ambapo hatachanganyikana nao, mfano wa hilo ni kama awe kwenye nyumba yake au shambani kwake au shamba la mume wake au jamaa zake, ama kazi ambayo inamfanya achanganyike na wanaume katika viwanda au ofisini au sehemu ya biashara au mfano wake, hakika hilo halifai kwa mwanamke, na wala haifai kwa mume wake wala wazazi wake wala ndugu zake wa karibu kumruhusu hata kama ataridhia yeye mwenyewe, kwasababu kufanya hivyo kunapelekea kuwa na ufisadi katika jamii. Basi madamu mwanamke ni mwenye kuhifadhiwa na kuchungwa katika nyumba yake na si mwenye kuanikwa mbele za wanaume yuko katika amani haimfikii mikono ya waovu, wala macho ya wenye hiyana hayamfikii, ama akijitokeza mbele za watu yawezekana akapotea na akawa kama mbuzi aliyeko katikati ya mbwa mwitu, na huenda asichukue muda mrefu wakawa wameichanachana hao waovu na wameivunja heshima yake na utukufu wake.

Na ikiwa mwanaume hatosheki na mwanamke mmoja, basi kwa hakika Mwenyezi Mungu amemuhalalishia kuoa zaidi ya mmoja mpaka kufikia idadi ya wake wanne tu, kwa masharti ya kuwafanyia uadilifu kwa mambo anayoyaweza kuanzia makazi chakula na malazi, ama mapenzi ya moyoni hakuna sharti la uadilifu katika hilo, kwasababu ni jambo ambalo mwanadamu halimiliki wala halaumiwi kwa hilo, na uadilifu ambao Mwenyezi Mungu amekanusha kutokuuweza kwake kwa maneno yake kutakasika na machafu ni kwake: (Na wala hamtoweza kufanya uadilifu kati ya wanawake hata kama mtapupia kufanya hivyo) [Al- nisaa: 129], Makusudio ni mapenzi na yenye kuambatana na mapenzi, hivyo kwa uadilifu huu Mwenyezi Mungu hajakataza kwa kutokuuweza uadilifu huo iwe ni kizuizi cha kuoa zaidi ya mke mmoja, kwa sababu yeye hana uwezo, na kwa hakika amewawekea Mwenyezi Mungu sheria ya kuoa zaidi ya mke mmoja Mitume wake na yeyote mwenye kufanya uadilifu wenye kuwezekana; kwasababu yeye Mwenyezi Mungu anajua zaidi chenye kuwafaa na yeye ni mwenye heri kwa wanaume na wanawake, na hii ni kwasababu mwanaume mwenye afya njema ana maandalizi ya kijinsia anaweza kwa maandalizi hayo kuziba hitajio la kujamiiana kwa wanawake wanne na akawatosheleza, ikiwa atabanwa kwa kuwa na mke mmoja tu kama walivyo wakristo ([63]) na wengineo, na kama wanavyopigia kelele hilo maadui wa uislamu, yatapatikana madhara yafuatayo:

Madhara ya kwanza: Ikiwa mume ni muumini mwenye kumtii Mwenyezi Mungu anamuogopa Mwenyezi Mungu kwa hakika huyo huenda akaishi maisha yake huku akihisi kuwa amenyimwa kitu fulani na yamezuiwa matamanio ya nafsi yake yaliyohalali; kwasababu mke mmoja akiwa na mimba katika miezi ya mwisho au nifasi au hedhi au maradhi, humzuia mume wake kustarehe naye, hivyo huishi mume kwa muda kama vile hana mke, na hii kama mke anampenda mume na mume anampenda mke, ama ikiwa hawapendani jambo hilo ni hatari zaidi.

Madhara ya pili: Na ikiwa mume ni muovu na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na mwenye hiyana kwa hakika atazini na atamuacha mke wake. Na wengi wasiokuwa na mtazamo wa kuoa zaidi ya mke mmoja wanafanya kosa la uzinifu na hiyana kwa kuwa na idadi ya wanawake isiyokuwa na mpaka, na jambo baya zaidi kuliko hili mtu huyo huhukumiwa kuwa ni kafiri ikiwa anapiga vita suala la sheria ya mke zaidi ya mmoja, na hulitia dosari suala hilo hali ya kujua kuwa Mwenyezi Mungu amelihalalisha.

Madhara ya tatu: Hakika wanawake wengi wanakosa kuolewa na kukosa watoto ikiwa kutazuiwa kuoa zaidi ya mke mmoja, hivyo mwanamke mwema na msafi huishi hali kama mjane masikini aliyeharamishiwa kuolewa, na huishi mwanamke mwingine akiwa katika hali ya uovu malaya na waovu wanaichezea heshima yake.

Na inavyofahamika ni kuwa wanawake ni wengi sana kuliko wanaume kwasababu wanaume hukutwa na vifo kwa wingi; kutokana na vita na kazi za hatari wazifanyazo, na kama inavyofahamika kuwa mwanamke yuko tayari kuolewa tangu kupevuka kwake, ama wanaume si wote wako tayari kuoa, kwasababu wengi wao hawawezi kuoa kutokana na kushindwa kulipa mahari, na kushindwa gharama za maisha ya ndoa. Na kwa mambo haya hujulikana kuwa uislamu umemtendea haki mwanamke na umemuhurumia, ama wale ambao wanapiga vita sheria ya kuwa na mke zaidi ya mmoja, hakika hao ni maadui wa mwanamke na watu wema na manabii, kuwa na mke zaidi ya mmoja ni sunnah (utaratibu wa) Manabii wa Mwenyezi Mungu -Amani iwe juu yao- hakika wao wanaoa wanawake na wanajumuika nao pamoja katika mipaka aliyowawekea Mwenyezi Mungu.

Na ama wivu na huzuni anayoihisi mke pindi mume wake anapooa mwanamke mwingine, ni jambo la hisia katika maumbile yake, na hisia hizo hazifai kupewa kipaumbele kuliko sheria katika jambo lolote, na yawezekana kwa mwanamke kujiwekea sharti kabla ya kufunga ndoa yakuwa mume wake asimuolee, na ikiwa atakubali basi ni lazima atekeleze sharti, na akilazimisha kumuolea basi mwanamke ana haki na hiyari (kisheria) ya kubakia au kuharibu ndoa, na wala mwanaume hatochukua chochote katika vitu alivyompa mkewe.

Na Mwenyezi Mungu ameweka sheria ya Talaka tena kwa namna maalumu katika hali ya kutofautiana na kutokea uovu baina ya mke na mume, na katika hali ya kutopendana wanandoa wawili; na ili wasiishi katika hali ya uovu na ugomvi, na ili kila mmoja apate mwenza anayeridhika naye na kuwa na furaha naye maisha yake yote na mwisho wa maisha yake ([64]) ni pale watakapo kufa wote wawili katika uislamu.

Muongozo wa kumi: Mambo ya Afya:

Uislamu umekuja na misingi yote ya tiba, na katika Qur'ani tukufu ,na hadithi za Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- umekuja ufafanuzi mwingi wa maradhi ya nafsi na mwili, na kuweka wazi Tiba zake za madawa na za kiroho; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini} ([65]). [Al- Israa: 82] Na Amesema Mtume Muhammadi Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Hakuteremsha Mwenyezi Mungu ugonjwa isipokuwa aliuteremshia na dawa, dawa hiyo aliijua aliyeafikiwa kuijua na hakuijuwa yule ambaye hakuwafikiwa kuijua" .

Na alisema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- (Basi jitibuni na wala msijitibu kwa matibabu yaliyo haramu) ([66]). Na katika kitabu Zaadul maadi fii had-yi khairil- ibaadi) kitabu cha mwanazuoni imamu ibnul Qayyim kuna upambanuzi wa hilo, basi na arejee kitabu hicho kwani ni kitabu cha kiislamu chenye manufaa zaidi na usahihi na kilichojaa ufafanuzi wa uislamu na historia ya mwisho wa Manabii Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

Muongozo wa kumi na moja: Uchumi na Biashara Viwanda na Kilimo: na hitajio la maji na chakula kwa watu, na sehemu za mapumziko ya watu wote na utaratibu ambao unawapa dhamana ya kutengeneza miji na vijiji vyao, na kuzisafisha na kupangilia namna ya kupita humo na kupambana na ghushi na uongo na mengine, yote haya ufafanuzi wake umekuja katika uislamu kwa namna iliyo kamilika.

Muongozo wa kumi na mbili: Katika kuwabaini maadui waliojificha, na njia ya kuepukana nao: amemuwekea wazi Mwenyezi Mungu kutakasika na machafu ni kwake katika Qur'an tukufu amemuwekea wazi muislamu kuwa anao maadui ambao wanamkokota kumpeleka kwenye maangamivu hapa duniani na akhera, ikiwa atawafuata, na amemtahadharisha nao na akambainishia njia ya kuepukana nao hawa maadui:

Wa kwanza wao: Shetani aliye laaniwa: ambaye huwasukuma maadui wote na kuwaelekeza kupambana na mwanadamu, naye ni adui wa baba yetu Adamu na mama yetu Hawaa, ambaye aliwatoa peponi, na ye ni adui wa kudumu wa kizazi cha Adamu mpaka siku ya mwisho wa dunia, anafanya bidii ya kuwatumbukiza katika kumkufuru Mwenyezi Mungu ili awaweke Mwenyezi Mungu pamoja naye motoni- na tunaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na moto huo- na akishindwa kumuingiza kwenye kukufuru hujitahidi kumuingiza katika maasia ambayo yatapelekea Mwenyezi Mungu kuchukia na kumuadhibu.

Na shetani ni roho inatembea kwa mwanadamu kupitia mishipa ya damu, hutia wasi wasi katika moyo wake na humpambia shari mpaka aingie humo kama atamtii. Na njia ya kuepukana naye kama alivyoweka wazi Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni muislamu kusema anapokasirika au akiazimia kufanya maasi "Auudhubillahi minash -shaitwaani rajiim" na hazitofanya kazi hasira zake wala hatofanya maasi, na ajue mwanadamu kuwa kinacho mvutia katika shari ambayo anaihisi kwenye nafsi yake si kingine bali kinatoka kwa shetani; ili amuingize kwenye maangamivu, kisha akae mbali baada ya kumuingiza huko, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Shetani ni adui wa binadamu, basi mchukulieni ni adui na msimtii, hakika ni kwamba yeye anawaita wafuasi wake kwenye upotevu ili wawe ni katika watu wa Moto unaowaka". [Faatwir 6].

Adui wa pili: matamanio ya nafsi: na katika hayo matamanio anaweza akahisi mwanadamu kupenda kukataa haki na kuirudisha ikija toka kwa mtu mwingine, na kupenda kukanusha hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuikataa, kwa sababu ni kinyume na anavyotaka, na miongoni mwa matamanio ni kutanguliza muhemko kwenye haki na uadilifu, na njia ya kuepukana na huyu adui ni kujilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na kufuata matamanio yake, na asikikubali wala kukifuata chenye kumsukuma katika matamanio na pia asikifuate, bali na aseme haki na aikubali japo ni chungu, na ajilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani.

Adui wa tatu: Ni nafsi yenye kuamrisha mabaya: na katika kuamrisha kwake mabaya ni kule kuhisi mwanadamu katika nafsi yake kupenda kufanya vilivyo haramishwa, kama zinaa na kunywa pombe na kufungua mchana wa mwezi wa ramadhani bila kuwa na udhuru wa kisheria, na mfano wa hayo katika mambo aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu. Na njia ya kuepukana na huyu adui ni kujikinga kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na shari yake na shari ya shetani, na afanye subira katika kujiepusha na kufanya haya machafu yaliyoharamishwa, na ajizuie nayo kwa kutarajia radhi za Mwenyezi Mungu, kama anavyoisubirisha nafsi yake katika kuacha kula na kunywa ambako anakutamani, lakini kuna mdhuru kula kwake na kunywa kwake, na hukumbuka kuwa haya machafu yaliyoharamishwa huondoka kwa wepesi sana na kufuatiwa na hasara na majuto daima.

Adui wa Nne: Mashetani wa kibinadamu: nao ni waasi wa kibinadamu ambao amewachezea shetani, na wakawa wanafanya maovu na wakiwapendezeshea wanao kaa nao, na njia ya kuepukana na huyu adui: ni kujihadhari naye na kujiweka mbali naye na kuacha kukaa naye.

Muongozo wa kumi na tatu: Katika lengo kuu na maisha yenye furaha: Na lengo kuu alilomuelekeza Mwenyezi Mungu mja wake muislamu, siyo haya maisha ya dunia na vilivyomo ndani yake vyenye kudanganya na kuisha, kwa hakika lengo kuu ni kujiandaa kwa ajili ya muda ujao wenye uhakika wa kudumu, nayo ni maisha ya Akhera baada ya kufa, Hivyo hufanya muislamu wa kweli matendo mazuri, kwa kuyazingatia kuwa ndiyo sababu ya kuyapata maisha ya Akhera na ni shamba lake na sio lengo lake.

Naye hukumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na sikuumba majini na binadamu isipokuwa kwa lengo tukufu, nalo niabudiwe mimi Peke Yangu, na sio asiyekuwa mimi". [Adh Dhariyati: 56]. Na kauli ya Allah Mtukufu: "Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Muogopeni Mwenyezi Mungu, na kila mtu ayazingatie matendo aliyoyatanguliza kwaajili ya Siku ya Kiyama. Na muogopeni Mwenyezi Mungu kwani kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa mnayoyafanya)" (18) "Na msiwe, enyi Waumini, kama wale walioacha kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Aliyoipasisha juu yao, na kwa sababu hiyo Akawasahaulisha wao kuzifanyia wema nafsi zao, Hao ndio wenye kusifika kwa uasi" (19) "Hawalingani sawa, watu wa Motoni wanaoadhibiwa na watu wa Peponi wanaostareheshwa. Watu wa Peponi ndio wenye kupata kila kinachotakiwa, ndio wenye kuokoka na kila kinachochukiwa". [Al-hashru:18-20], Na Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Yeyote mwenye kufanya jema uzito wa mdudu chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera". (7) "Na yeyote mwenye kufanya baya uzito wa mdudu chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera". [Azzalzalat: 7-8].

Anakumbuka muislamu Aya hizi tukufu na zinazofanana nazo katika maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye anawaelekeza waja wake kwenye lengo ambalo amewaumba kwa ajili hiyo, na wakati ujao ambao unawasubiri na hakuna namna ya kukwepa; basi na ajiandae kwa huo muda ujao wenye uhakika na wenye kudumu, kujiandaa kwa kumtakasia ibada Mwenyezi Mungu peke yake, na kutenda yenye kumridhisha hali ya kutarajia radhi za Mwenyezi Mungu, na kumtukuza yeye katika haya maisha kwa kumtii, na baada ya kufa kumuingiza katika nyumba ya utukufu wake, na humkirimu Mwenyezi Mungu katika haya maisha kwa kumpa maisha mazuri, na kuishi katika utawala wa Mwenyezi Mungu na ulinzi wake huona kwa nuru ya Mwenyezi Mungu, anatekeleza ibada ambazo amemuamrisha Mwenyezi Mungu kuzifanya, na hupata ladha nzuri kwa kumnong'oneza Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtaja Mwenyezi Mungu katika moyo wake na kwa ulimi wake hivyo unatulia moyo wake kwa kufanya hivyo.

Na anawafanyia watu wema kwa kauli zake na matendo yake kisha husikia kutoka kwa watu wema wakiutambua wema wake, na kumuombea yenye kumfurahisha na kumkunjua kifua chake, na huona toka kwa mahasidi wenye kulaumu wakipinga mazuri yake, na wala halimzuii hilo kuwafanyia wema kwa sababu yeye anakusudia malipo na thawabu toka kwa Mwenyezi Mungu, na husikia toka kwa watu wa shari wenye kuchukia dini na watu wake, husikia kejeli na maudhi ambayo humkumbusha Mitume wa Mwenyezi Mungu, na hutambua kuwa jambo hili ni katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi humzidishia mapenzi ya kuupenda uislamu na kudumu katika uislamu. Na hufanya kazi kwa mikono yake ofisini au shambani au masokoni au kiwandani; ili aunufaishe uislamu na waislamu kwa uzalishaji wake; na ili apate malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu siku atakapokutana naye kwa kufanya kwake kwa ikh-las (utakasifu wa nia) na nia njema, na ili apate chumo lililokuwa zuri ambalo atajihudumia mwenyewe na familia yake, na atatoa sadaka katika chumo hilo na ataishi akiwa mwenye moyo uliotosheka mwenye heshima aliye kinai, akitarajia malipo toka kwa Mola wake -kutakasika na machafu ni kwake- kwa sababu Mwenyezi Mungu humpenda muumini mwenye nguvu mwenye kujishughulisha, na anakula na kunywa bila kufanya is-raaf, ili ajiimarishe kwa kufanya hivyo katika kumtii Mwenyezi Mungu. Na huamiliana kimapenzi na mke wake ili amuhifadhi na matamanio na yeye pia ajihifadhi na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, na ili azae watoto wenye kumuabudu Mwenyezi Mungu, na wenye kumuombea dua akiwa hai na baada ya kufa kwake na yawe matendo mema yake ni yenye kuendelea, na ili aongeze idadi ya waislamu na apate kwa kufanya hayo malipo toka kwa Mola wake na amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila neema aipatayo kwa kumsaidia kumtii Mwenyezi Mungu, na kukubali kuwa neema hiyo ni kutoka kwa Mola wake pekee, na kwa hivyo hupata malipo toka kwa Mwenyezi Mungu, na anajua kuwa yanayompata wakati mwingine katika njaa na hofu na maradhi na misiba ni mtihani toka kwa Mola wake ili Mwenyezi Mungu amuone- naye anamjua zaidi- ([67]) ukomo wa subra yake na kuridhia kwake kadari ya Mwenyezi Mungu, basi husubiri na kuridhia na humshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila hali kwa kutaraji thawabu zake ambazo ameziandaa kwa wenye kusubiri, na humuondolea subra misiba na huikubali misiba kama anavyokubali mgonjwa machungu ya dawa kwa kutamani kupona.

Ikiwa ataishi muislamu katika maisha haya kama alivyomuamrisha Mwenyezi Mungu kwa roho ya hali ya juu anafanya kwa ajili ya muda ujao wenye uhakika wa kudumu; ili apate furaha ya kudumu ambayo yasiyochafuliwa na uchafuzi wa maisha haya, wala hayakatishwi na kifo, basi yeye bila shaka ni mwenye furaha katika maisha haya ya dunia na mwenye furaha katika maisha ya akhera baada ya kufa; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hiyo ndiyo Nyumba ya Akhera. Tumewapatia, ile starehe yake, wale ambao hawataki kuifanyia kiburi haki hapa duniani wala kufanya uharibifu humo. Na mwisho wenye kushukuriwa, nayo ni pepo, ni wa yule aliyejikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu". [Al- qaswas 83], Na amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema: "Mwenye kufanya tendo zuri, akiwa ni mwanamume au ni mwanamke, na huku ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake , basi tutampa maisha mema yenye utulivu duniani hata kama ni mchache wa mali, na tutawalipa huko Akhera thawabu zao kwa uzuri zaidi ya walivyofanya duniani". [An Nahli: 97].

Na katika Aya tukufu iliyotangulia na inayofanana nayo, anafahamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu: kuwa yeye humlipa mwanaume mwema na mwanamke mwema ambao wanatenda mema kwa kumtii Mwenyezi Mungu katika maisha haya ya duniani kwa kutarajia radhi zake, kwa malipo ya haraka katika maisha haya nayo ni maisha mazuri yenye furaha ambayo tumekwisha yaelezea,na malipo hapo baadae baada ya kufa ,nayo ni neema ya pepo ya kudumu. Na katika hili anasema Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini: akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake ([68])

Na kwa haya inatubainikia kuwa uislamu peke yake ni fikra salama, na ni kipimo sahihi cha mazuri na mabaya, na ni njia iliyokamilika na ya uadilifu, na kuwa kila rai na mitazamo ya kisaikolojia, na kijamii na malezi na siasa na uchumi, na kila nidhamu na muongozo wa mwanadamu unapasa kusahihishwa kwa kupitia mwanga wa uislamu, na kuutegemea mwanga huo, na ikiwa kinyume na hivyo ni vigumu kufaulu aliyekwenda kinyume, bali uislamu ndiyo chimbuko la ponyo kwa wengine duniani na akhera.

 Sehemu ya Tano- Kuweka wazi baadhi ya Shub-ha(Utata).

Ya kwanza: Na wale wenye kuuchafua uislamu ni watu wa aina mbili:

Aina ya kwanza: Ni watu wanaojinasibisha na uislamu na wanadai kuwa wao ni waislamu, lakini wanakwenda kinyume na uislamu kwa kauli zao na matendo yao, na wanafanya matendo ya kiislamu na uislamu uko mbali na matendo hayo, na wao hawauwakilishi uislamu na wala hawapaswi kujinasibisha matendo yao na uislamu, na hawa ni:

(A) Waliopotea kwenye itikadi zao: kama wenye kufanya twawafu kwenye makaburi, wakiomba haja zao toka kwa waliozikwa humo, na wanaitakidi na kuamini hao waliozikwa wanadhuru na wananufaisha ([69])

(B) Waliokosa maadili katika tabia zao na dini yao:

Na wanaacha aliyoyafaradhisha Mwenyezi Mungu, na wanafanya aliyoyaharamisha, kama vile zinaa kunywa pombe na mengineyo, na wanawapenda maadui wa Mwenyezi Mungu na wanajifananisha nao.

Na miongoni mwa wenye kuuchafua uislamu ni watu miongoni mwa waislamu, lakini imani zao kwa Mwenyezi Mungu ni dhaifu, na utekelezaji wao wa mafundisho ya uislamu unamapungufu, na wao wanamapungufu katika baadhi ya mambo ya wajibu japokuwa hawaachi kabisa kuyatekeleza, wanafanya baadhi ya mambo yaliyoharamishwa ambayo hayafikii kiwango cha shirki kubwa au aina nyingine ya kukufuru, na kwa hakika wamezoea mazoea mabaya yaliyo haramishwa, uislamu uko mbali na hayo, na unayazingatia ni katika madhambi makubwa, kwa mfano: kusema uongo, kughushi,na kutotimiza ahadi na hasadi, na hawa wote wanauchafua uislamu kwa sababu asiyeujua uislamu kwa wasiokuwa waislamu wanadhani kuwa uislamu unaruhusu mambo hayo.

Aina ya pili: Miongoni mwa wenye kuuchafua uislamu ni watu katika maadui wa uislamu, wenye chuki na uislamu, na miongoni mwao ni: Musta-shrikuuna (makafiri wenye kujifanya waislamu ili wausome kwa lengo baya) na mayahudi na wamishionari wa kinaswara na wenye kufanya vitendo sawa na hao miongoni mwa wenye kuuchukia uislamu, ambao umewachukiza ukamilifu wake na upole wake na wepesi wa kusambaa kwake; kwa sababu uislamu ni dini ya kimaumbile, ([70]) ambayo maumbile yanaukubali mara moja pale yanapoupata, na kila asiyekuwa muislamu anaishi kwa wasi wasi, na anahisi kukosa ridhaa na dini yake, au dhehebu lake ambalo ameungana nalo; kwa sababu inatofautiana na maumbile yake ambayo Mwenyezi Mungu amemuumbia isipokuwa muislamu wa kweli, hakika yeye anaishi maisha ya furaha na mwenye kuridhika na dini yake, kwa sababu ni dini ya kweli ambayo ameiweka Mwenyezi Mungu, na sheria ya Mwenyezi Mungu inaafikiana na maumbile ya Mwenyezi Mungu aliyomuumbia mwanadamu, na hivyo tunawaambia manasara wote na mayahudi na kila aliyetoka katika dini ya uislamu: hakika watoto wako wamezaliwa katika umbile la kiislamu lakini wewe na mama yao mmewatoa kwenye uislamu kwa malezi mabaya ya ukafiri, nayo ni malezi ya kidini na kimadhehebu yanayoenda kinyume na uislamu.

Na kwa hakika wamefanya makusudi hao wenye kuuchukia uislamu miongoni mwa hawa mustash-rikiina na wamishionari kuusingizia uislamu, na kumsingizia mwisho wa manabii Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

1- Kwanza kwa kuukadhibisha utume wake wakati mwingine.

2- Kwa kumsingizia mambo ya aibu wakati mwingine, na yeye ni mkamilifu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- aliyeepushwa na Mwenyezi Mungu, licha yakuwa ni mtakasifu zaidi na kila aibu na mapungufu.

3- Kuzichafua baadhi ya hukumu za uislamu zenye uadilifu ambazo ameziweka Mwenyezi Mungu mwenye ujuzi na hekima; ili wawakimbize watu wakae mbali na uislamu.

Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu anabatilisha vitimbi vyao; kwa sababu wao wanaipiga vita haki, na haki hukaa juu na wala haikaliwi juu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hawa madhalimu wanataka kuitengua haki aliyotumilizwa kwayo Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, nayo ni Qur’ani, kwa maneno yao ya uongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuipa nguvu haki kwa kuitimiza Dini Yake japokuwa wale wapingaji wenye kukanusha watachukia". "Yeye Ndiye Aliyemtimiliza Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kwa Qur’ani na dini ya Uislamu, ili Aifanye kuwa juu ya dini zote, ingawa washirikina wanaichukia dini ya haki-Uislamu- na kushinda kwake dini nyingine". [Ali-swaffu:8-9].

Ya pili: Chimbuko la uislamu:

Basi ukitaka -ewe muislamu- mwenye akili kuujua uislamu kwa uhakika, basi soma Qur'ani tukufu, na hadithi za bwana Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- hadithi zilizo sahihi zilizoandikwa katika sahihi Bukhari na Muslimu, na Muwatwau ya imamu maalik, na musnad wa imamu Ahmad ibnu hanmbal, na sunan abii Daaud, na sunan Nasaai na sunan tirmidhiy, na sunan ibnu maajah na sunan Daaramiy. Na soma Historia ya Mtume ya Ibnu Hishaamu, na Tafsiiri ya Qur'an tukufu ya mwanazuoni Ismail ibnu Kathiir, na kitabu Zaadul maad fii had-yikhairul ibaadi cha mwanazuoni Muhammad ibnul Qayyim, na mfano wa vitabu hivyo katika vitabu vya maimamu wa uislamu, watu wa tauhiid na kulingania kwa Mwenyezi Mungu kwa elimu, mfano Sheikhul islamu Ahmad ibnu Taimiyah na Imamu Almujaddidu Muhammad ibnu Abdul wahhab, ambaye Mwenyezi Mungu ameutia nguvu uislamu kupitia kwake na kwa kupitia mkombozi Muhammad ibnu Suud na akaitia nguvu itikadi ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika miji ya kiarabu, na baadhi ya sehemu katika karne ya kumi na mbili tangu kuhama Mtume mpaka sasa, na hilo ni baada ya kuenea Shirki.

Ama vitabu vya Mustash-rikiina na makundi mengine yanayojinasibisha na uislamu na haliyakuwa yanakwenda kinyume kwa kile wanachokilingania miongoni mwa mambo yanayokwenda tofauti na uislamu mengi tumeshatangulia kuyataja, au kuwavunjia heshima maswahaba wa Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- au kuwabughudhi kwa kuwatukana, au kuwasema vibaya maimamu wenye kulingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu mfano: Ibnu Taimia, na Ibnu Qayyim, na Muhammad Ibnu Abdul wahhaab, na kuwazulia uongo na kuvisema vitabu vyao ni venye kupotosha, jihadhari usidanganywe navyo au kuvisoma.

Ya tatu: Madhehebu ya Kiislamu:

Waislamu wote wapo katika dhehebu moja nalo ni uislamu, na marejeo yao ni Qur'an na hadithi za Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ama yenye kuitwa madhehebu ya kiislamu kama madhebu manne kama vile Hanmbali ,Maaliki na Shaafiiy na Hanafiiy hakika madhehebu hayo hukusudiwa ni Madrasa za Fiq-hi (sheria) za kiislamu ambazo wamesoma hawa maulamaa misingi ya kiislamu na marejeo yao wote ni Qur'an, na hadithi za Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na ihitilafu yoyote iliyojitokeza kati yao ni katika maswala ya matawi na sio maswala ya msingi nayo ni machache, kila mwanachuoni amemuamrisha mwanafunzi wake achukue kauli ambayo inatiwa nguvu na Qur'an au hadithi, hata kama itakuwa ni kauli ya mwingine asiyekuwa yeye.

Na muislamu halazimishwi kushika dhehebu moja katika hayo, na kwa hakika hulazimishwa kurudi kwenye Qur-an na hadithi, na ama yanayotokea kwa wengi miongoni mwa wenye kujinasibisha na hayo madhehebu ikiwa pamoja na kwenda kinyume na Itikadi sahihi, kwa wanayoyafanya kwenye makaburi kwa kutufu na kuwaomba msaada walioko humo makaburini, na namna wanavyotumbukia katika kubadilisha sifa za Mwenyezi Mungu, na kuziondoa na kuzitoa katika maana zake zilizokuwa wazi, kwa hakika hawa ni wenye kwenda kinyume na maimamu wa madhehebu zao katika itikadi, kwa sababu itikadi za maimamu ni itikadi ya wema waliotangulia ambao tumekwisha wataja katika kundi lilofaulu.

Ya Nne; Kundi lililotoka nje ya uislamu:

Na hupatikana katika ulimwengu wa kiislamu makundi yaliyotoka kwenye uislamu, nayo yanajinasibisha na uislamu na yanadai kuwa ni makundi ya uislamu, lakini makundi hayo kiuhakika si ya kiislamu; kwa sababu itikadi zake ni kumkufuru Mwenyezi Mungu na Aya zake na upweke wake na miongoni mwa hayo makundi ni:

1- Kundi la Baatwiniyyat:

Kundi ambalo linaitikadi kuwa Mwenyezi Mungu anachanganyikana na viumbe na kuwa kitu kimoja na pia wanaitikadi kuwa roho ya mwanadamu huhama kutoka katika mwili wa aliyekufa kwenda kwenye mwili ulio hai, na kwamba dalili za sheria ya dini ya kiislamu zina maana iliyofichikana inayotofautiana na maana iliyo wazi ambayo ameifafanua Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na waislamu wamekubaliana juu ya hilo, na hii maana iliyofichikana wao ndio wanaoiweka kwa matamanio ya nafsi zao ([71]) Na asili ya kuanza kundi la Baatwiniyyah, ni kuwa kikundi cha mayahudi na majusi na wanafalsafa katika miji ya fursi (Irani) walipoelemewa na ueneaji wa uislamu, walikusanyika na wakashauriana kuweka madhehebu, kusudio lake ni kuwatenganisha waislamu na kuzishawishi fikra kuhusu maana za Qur'an tukufu, ili waweze kuwatenganisha waislamu, basi wakaweka madhehebu hii yenye kuangamiza na wakawaita watu humo, na wakajinasibisha na watu wa nyumba ya bwana Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na wakadai kuwa wao ni katika kundi lao; ili wafikie kilele katika kuwadanganya wasiojua, na wakawakamata watu wengi waliokuwa wajinga na wakawapoteza kwa kuacha haki.

Na miongoni mwa makundi hayo ni (Al-qadiyaaniyat): linanasibishwa kundi hili na Ghulaam Ahmad Al-qadiyaaniy ambaye alipata umashuhuri kwa kudai Utume na akawalingania kabila la Ghaughai katika nchi ya India na pambizoni mwake kumuamini, na wakamtumia waingereza yeye na wafuasi wake wakati walipotawala nchi ya India na wakamshinda yeye na wafuasi wake, mpaka wakamfuata wajinga wengi, na likapatikana kundi la kadiani ambalo linajidhihirisha kuwa ni waislamu na huku linakwenda mbio kuuangamiza uislamu na kumtoa wamuwezae katika mzunguko wake, na alifahamika zaidi kuwa yeye alitunga kitabu kiitwacho "kusadikisha Dalili za Ahmadia" ambacho amedai ndani yake utume, na akabadilisha humo dalili zinazohusu uislamu, na alikuwa katika kubadilisha kwake dalili za uislamu ni kudai kwake.

Kuwa Jihadi katika uislamu ilifutwa, na ni lazima kwa kila muislamu ajisalimishe kwa Waingereza, na akatunga tena wakati huo-Kitabu akakiita(Tir-yaaqul quluub) na alikufa huyu mtunzi baada ya kupoteza watu wengi mnamo mwaka 1908, na akafuata baada yake katika daawa yake na kuongoza kundi lake, mtu aliyepotea anaitwa kwa jina la Al-hakiim Noordin.

3- Na katika kundi la Baatwiniyah ambalo limetoka katika uislamu, ni kundi liitwalo Al-bahaaiyyat, amelianzisha katika karne ya kumi na tisa katika nchi ya Iran mtu ambaye jina lake ni Ally Muhammad na ikasemekana: Muhammad Ally Al-Shiiraziy, na alikuwa ni katika kundi la Shia Ith-naa-asharia, basi akajitenga kwa kuanzisha dhehebu na kudai kuwa yeye ndiye Mahad Al-muntadhwir, kisha akadai baada ya hapo kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amejichanganya kwake, akawa Mungu wa watu-ametakasika kukubwa Mwenyezi Mungu kwa yale wayasemayo makafiri wenye kupinga uwepo wa Mwenyezi Mungu- na akapinga kuwepo kwa kufufuliwa kuhesabiwa na pepo na moto, na akaenda na mwenendo wa kundi la Baraahima na Mabudha waliokufuru na akakusanya baina ya Mayahudi na Manaswara na waislamu, na kuwa hao hawana tofauti, kisha akapinga utume wa mwisho wa manabii Muhammad- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kapinga hukumu nyingi za uislamu, kisha akamrithi baada ya kuangamia kwake waziri wake anajiita (Al-bahaau) na akaeneza daawa yake na wafuasi wake wakawa wengi, basi likanasibishwa hili kundi na jina lake na likaitwa (Al-Bahaaiyyat)

4- Na miongoni mwa makundi yaliyotoka katika uislamu, na hata kama linadai kuwa ni kundi la kiislamu, na linaswali na kufunga na kuhiji, ni kundi ambalo idadi yake ni kubwa linadai kuwa Jibril -Amani iwe Juu yake- alifanya hiyana katika kufikisha ujumbe pale ambapo aliuzuia ujumbe kwa Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na hali yakuwa alitumwa kwa Ally, na baadhi yao wanasema "Ally ni Mungu, na wanapituka mipaka katika kumtukuza na kuwatukuza watoto wake na wajukuu wake na mke wake Fatuma na mama yake Khadija- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote- bali kwa hakika wamewafanya kuwa ni miungu pamoja na Mwenyezi Mungu wanawaomba na wanaitakidi kuwa wao hawakosei na kuwa cheo chao kwa Mwenyezi Mungu ni kikubwa kuliko cheo cha mitume- Amani iwe juu yao.

Na kundi hili linasema: Hakika Qur'an ambayo kwa sasa iko mikononi mwa waislamu imezidishwa na inamapungufu, na wakajitengenezea msaafu wao maalumu, wakaweka humo sura na Aya kutoka kwao wenyewe, na wanamtukana mbora wa waumini baada ya ubora wa Mtume wao, naye ni Abuu bakar- Radhi za Allah ziwe juu yake- na wanamtukana Aisha mama wa waumini wote- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -na wanataka msaada kutoka kwa Ally na watoto wake katika wakati wa shida na raha, na wanawaomba wao kinyume na Mwenyezi Mungu, na Ally na watoto wake wako mbali nao, kwa sababu wao wamewafanya kuwa ni miungu pamoja na Mwenyezi Mungu, na wakamsingizia Mwenyezi Mungu na wakabadilisha maneno yake- ametakasika Mwenyezi Mungu kwa hayo wanayoyasema kutukuka kuliko kukubwa- ([72]).

Na hili kundi la kikafiri ambalo tumelitaja, ni miongoni mwa makundi ya kikafiri ambayo yanadai kuwa ni ya kiislamu nayo yanaubomoa uislamu, Zinduka -ewe mwenye akili na ewe muislamu popote ulipo- kuwa uislamu siyo madai tu, bali uislamu ni kujua Qur'an na hadithi za Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- zilizothibiti toka kwake na kuzifanyia kazi, Basi zingatia Qur'ani tukufu na hadithi za Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- utapata muongozo na Nuru na njia iliyonyooka ambayo inamfikisha mwenye kuifuata katika furaha ya pepo yenye neema kwa Mola wa viumbe wote.

Kulingania katika kufaulu

Ewe mwanadamu mwenye akili, mwanaume au mwanamke miongoni mwa wale ambao hawajaingia katika uislamu... ninauelekeza wito huu kwako kukupeleka katika mafanikio na furaha, Basi ninasema:

Iokoe nafsi yako kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya kifo huko kaburini, kisha katika moto wa jahanamu.

Okoa nafsi yako kwa kumuamini muumba, na Muhammad-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ni Mtume, na kuamini kuwa uislamu ni dini ya kweli. Na sema kwa ukweli "Laailaaha illa llahu Muhammadu rasuulullah," na sali sala tano, na toa zakkah, na funga mwezi mtukufu wa ramadhani, na hijji nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu ikiwa utaweza gharama za safari.

Na utangaze uislamu wako kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; kwani hakuna kufaulu kwako wala furaha isipokuwa kwa kufanya hivyo.

Na mimi nakuapia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye, ni kuwa dini hii ya uislamu ni dini ya haki ambayo hakuna Mola mwingine ila yeye na yakwamba uislamu huu ni dini ya kweli ambayo Mwenyezi Mungu hamkubalii yeyote dini isiyokuwa ya uislamu, na mimi namshuhudilia Mwenyezi Mungu na viumbe vyake vyote kuwa Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kuwa uislamu ni ukweli na mimi ni katika waislamu.

Na ninamuomba Mwenyezi Mungu- kutakata na machafu ni kwake- kwa neema zake na karama zake anifishe nikiwa muislamu wa kweli na kizazi changu na ndugu zangu waislamu-, na atukusanye katika pepo yenye neema pamoja na Mtume wetu Muhammad mkweli na muaminifu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na manabii wote pamoja na wake zake na masahaba wake. Na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amnufaishe kila atakaye kisoma kitabu hiki au akakisikia, Alaa (eleweni vyema) je nimefikisha? Ewe Mola wangu shuhudia.

Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi, na Rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad, na ah-ali zake, na masahaba zake, na shukrani zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu.



([1]) : Neno "Taala"ni neno la kumtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu,na kumsifu yeye kwa utukufu na utakatifu.

([2]) Neno Sub'haanahu: yaani ametakasika Mwenyezi Mungu na ameepukana na mapungufu na aibu.

([3]) Na mfano wake yule asiamini uwepo wa Mwenyezi Mungu

([4]) Na katika hadithi ya Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Amani- (Anateremka Mola wetu Mtukufu kila usiku mpaka kwenye uwingu wa dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, na husema: Ni nani aniombae nimpe, ni nani anaye taka kutoka kwangu nimpatie, na ni nani anayeniomba msamaha nimsamehe). Amesimulia hadithi hii Bukhari hadithi (7494) na Muslim (758) na Tirmidhiy (3498).

([5]) Majini ni viumbe wenye akili amewaumba Mwenyezi Mungu ili wamuabudu yeye kama vile wanadamu, na wataishi na wanadamu ardhini, lakini wanadamu hawawaoni majini.

([6]) kwa hadithi ya Mughira bin shuuba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani kutoka kwa Mtume -Rehema za Mungu ziwe juu yake na amani kwamba Musa alimuuliza Mola wake ni yapi makazi duni ya watu wa peponi? akasema atakuja mtu baada ya watu wa peponi kuingia peponi na ataambiwa: ingia peponi, atasema ewe Mola wangu vipi niingie na hali yakuwa kila mtu amekaa sehemu yake, na wameshachukua stahiki zao, na ataambiwa, je utaridhika kupewa ufalme mfano wa mfalme katika wafalme wa duniani? na atasema nimeridhia ewe Mola wangu, atamwambia basi umeupata huo ufalme na mfano wake. Akasema katika mara ya tano: nimeridhia ewe Mola wangu, kisha atamwambia: huu ufalme ni wako na mara kumi mfano wake, na utapata chenye kutamaniwa na nafsi yako na chenye kuvutia macho yako, atasema: nimeridhia ewe Mola wangu. Atasema: ni watu gani hawa wenye makazi ya juu zaidi? atasema: hao ni wale ambao nimependelea kupanda heshima yao kwenye mikono yangu na nikaipiga muhuri. Jicho halikuwahi kuona wala sikio kusikia na wala moyo haukuwahi kufikiria). Ameipokea hadithi hii Muslim (189).

([7]) Na majina yake katika Qur'ani: Aayaat (Alama) na ndiyo sahihi zaidi na limetajwa Neno muujizaat kwasababu ni neno maalumu ambalo siyo la kawaida.

([8]) Ameitoa hadithi hii imam Muslim(8) na Abuu daud (4695).

([9]) Amesema Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- " Uislamau umejengwa kwa mambo matano: kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa isipokuwa Mwenyezi Mungu , na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala na kutoa zaka na kuhiji nyumba tukufu na kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani" ametoa hadithi hii imamu Bukhari katika kitabu chake sahihi(4515), "na katika Taariikhl kabiir4/213", (319,322/8), na Imamu Muslim (16 ) na dalili kutoka katika Qur'ani zinakuja kutaja nguzo kwa upambanuzi.

([10]) Ameitoa Muslimu (1978), na An'nasaai (4422)

([11]) Al- istiaana) Kutaka Msaada: ni kutaka msaada kiujumla (Al-istighaatha) kutaka kuokolewa katika hali ya dhiki na tabu (Al- istiaadhatu) Ni kutafuta kimbilio na hifadhi kwa mwenye uwezo wa kuzuia ubaya na yenye kuudhi.

([12]) Ameitoa Ahmad (22758/317/5), na Twabraniy (246/10), Na ameisahihisha al-albaniy

([13]) Ameitoa Tirmidhii (2516), na Ahmad (2802),Na Twabaraniy(12989)(2820)= Na Amesema Al-Tirmidhiiy Hadith Hasan na Sahihi.

([14]) Ameitoa Abuu Daud(3904), Na Tirmidhii(135)Na Ibnu Majaah(639), Na akasahihisha Al-albaaniy katika Sahihi Targhiib wa Tarhiib.(3047)

([15]) Na kutegemea ni: Uhakika wa moyo kuegemea kwa mwenye kutegemewa.

([16]) Na mawalii wa Mwenyezi Mungu ni wale wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii yeye, na wenye kumfuata Mtume wake -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, miongoni mwao hujulikana kwa elimu zao na kupigana kwao jihadi, miongoni mwao wapo wasiojulikana, na wanaojulikana hawako radhi kutukuzwa na watu, na mawalii wakweli hawadai kuwa wao ni mawalii bali wanaona kuwa wao wanamapungufu, na hawana vazi maalumu au mfumo maalimu isipokuwa ni kumuiga bwana Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na kwa hivyo, kila muislamu mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume ana uwalii wa Mwenyezi Mungu kwa kiasi cha wema wake na utiifu wake kwa Allah, na kwa hivyo inabainika kuwa wale ambao wanadai kuwa wao ni mawalii wa Mwenyezi Mungu, na wanavaa mavazi maalumu ili watu wawatukuze na kuwatakasa, ni wazi kuwa hao siyo mawalii wa Mwenyezi Mungu bali hao ni waongo.

([17]) Makundi hayo ni kwa mujibu wa sensa iliyotangazwa wakati wa utunzi wa kitabu hiki mnamo mwaka 1395 Hijiria sawa na mwaka 1975G, (miladia)

([18]) Ameitoa Abuu Daudi (3842), wa Ibnu majjah (3226), na ameisahihisha Al baaniy katika swahihi Jaamiiy (1082) na Silsilat Al- swahihat (203)

([19]) Yaani makusudio ni kuacha kuchambua yaliyotokea kati ya maswahaba katika hitilafu kwa kuponda au kujeruhi.

([20]) Inatokea kati yake na mtu mwingine kutofautiana.

([21]) Ameitoa Bukhariy (2697), na Muslim ( 1718) na Tamko ni la Bukhariy.

([22]) Ameitoa at- rimidhiiy (2621), na An-nasaaiy(463), na Ahmad(5/346), na akasahihisha Al-baniiy katika swahihul Jaamiiy

([23]) Kwa sababu akisoma Qur'ani kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu haiwi Qur'ani, na ndio maana maneno na matamshi ya Qur'ani hayafanyiwi tarjama (tafsiri) bali kinachofanyiwa tarjama ni maana yake, kwa sababu zikifanyiwa tarjama herufi zake na maneno yake utaondoka ufasaha wake na muujiza wake, na zitaporomoka baadhi ya herufi zake na haitokuwa tena ni Qur'ani iliyokuwa kwa lugha ya kiarabu.

([24]) isipokuwa akitaka kumzindua yeyote au kumrekebisha basi atasema " Sub-hanallah" atasema maneno hayo maamuma kumwambia imamu akikosea katika kitendo au akazidisha au akapunguza, ili azinduke, na atasema mwenye kusali kumwambia mwenye kukumbushwa kwa mfano, na mwanamke humzindua mtu kwa kupiga makofi na wala haongei kwa sababu sauti yake ni fitina.

([25]) Niswabu -Ni Kiwango ambacho mali ikifikia kiwango hicho ni wajibu kuitolea zaka.

([26]) na kafara ya kiapo hutolewa hiyari baina ya kumwacha huru mtumwa au kuwalisha maskini au kuwavisha, na ikiwa, hatopata basi na afunge siku tatu.

([27]) Ama Hijja ya watu wajinga wenye kuabudu makaburi ya mawalii na kuyashuhudia, hakika huo ni upotevu na ni kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akamuamrisha Mtume wake - Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Haifungwi safari isipokuwa kwa kwenda kutembelea misikiti mitatu msikiti mtukufu wa Makka, na msikiti wangu huu, na msikiti wa Aq-swa "ameipokea hadithi hii Bukhari na Muslimu kutoka katika hadithi ya Abuu huraira.

([28]) Na mfano wake ni hadithi "Tafuteni ukaribu kwa kupitia jaha yangu, kwa hakika cheo changu ni kikubwa kwa Mwenyezi Mungu "na hadithi "yeyote atakaye lidhania jiwe dhana nzuri litamfaa "kwa hakika hadithi hizi zote na za uongo na siyo sahihi na wala hazipatikani katika vitabu vya hadithi vyenyekutegemewa, bali hupatikana vitabu hivyo na vyenye kufanana na hivyo katika vitabu vya wapotoshaji ambao wanalingania kwenye shirki na Bid'aa kwa namna wasiojua.

([29]) Ameitoa hadithi hii Twabraaniy katika kitabu cha Auswat(4480)na Baihaqyyu katika Shuabul iman"(2/173/2), na ameisahihisha Al-baniyy katika silsilat swahihat (212/6)

([30]) Analeta Tal-biyah:"Nimekuitikia kufanya ibada ya Hijja au ibada ya Umra' na inamaanisha kudumu katika kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu.

([31]) Na Al-Tammatui: Ni yule anayetekeleza ibada ya Umra katika msimu wa Hijja, kisha anamaliza kabisa ibada ya umra kwa ukamilifu; kisha atapumzika kwa kufanya yale aliyokatazwa akiwa kwenye ibada ya Umra, kisha atahirimia kufanya ibada ya Hijja katika siku ya nane, na Al-Qaarin: ni yule ambaye anayetekeleza ibada ya Hijja na Umra zote kwa pamoja na anafanya matendo ya mwenye kuhiji tu, lakini atanuia kuingia katika ibada ya umra na kuitekeleza. Na Al- Muf-rid: ni yule ambaye ananuia kufanya ibada ya Hijja peke yake pasina kufanya Umra.

([32]) Al-had-yu: wanyama wa miguu minne miongoni mwao ni Ngamia au Ng'ombe au Mbuzi hupelekwa na hujaaji na kumtoa sadaka na kumla nyama yake.

([33]) Yaani kufika kwenye nyumba tukufu, nayo ni msikiti Mtukufu wa Makkah.

([34]) isipokuwa atakapofika kati ya nguzo mbili atasema maneno yalipo kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema (Ewe Mola wetu tupe duniani yaliyo mazuri na akhera Pia Utupe yaliyo mazuri na utuepushe na adhabu ya moto) [Al- baqara: 201].

([35]) Ni kisimamo cha Nabii Ibrahim- Amani iwe Juu yake.

([36]) Al-mas'aa ni: sehemu ya kukimbilia na ni sehemu ya kutembea na kukimbiakimbia baina ya Swafaa na Marwa, nayo ni milima miwili midogo.

([37]) Twawafu hiyo ataifanya siku ya Eid au baada yake, ama twawafu ya kwanza kabla ya Hajji inayoitwa twawaful Ifaadhwa hiyo ni sunna, na ama Saa-yi ni moja tu kwa mwenye kufanya ifraad na Qiiraan ikiwa ataitanguliza pamoja na twawafu ya kufika kwenye nyumba tukufu twawafu hiyo inamtosha hata kama hatofanya Saa-ayi pamoja na twawaful Ifaadhwa katika siku ya Eid au baada yake.

([38]) Yaani sehemu aliyofikia.

([39]) Malaika: ni Roho amewaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na Nuru, nao ni wengi sana hakuna awezaye kudhibiti idadi yao isipokuwa Mwenyezi Mungu, kuna waliopo mbinguni, na wengine wamewakilishwa kwa wanadamu.

([40]) Yaani muumini anaamini kuwa vitabu ambavyo ameviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake ni haki na kweli, na havikubakia vitabu hivyo isipokuwa Qur'ani, ama taurati na injili ambazo zipo kwenye mikono ya mayahudi na manaswara hizo ni tungo zao, na dalili ya hilo ni kule kutofautiana kwake, na kauli yao ndani ya vitabu hivyo: Miungu watatu, na Issa ni mwana wa Mwenyezi Mungu, na kweli ni kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja naye ni Allah, na Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu kama ilivyokuja katika Qur'ani, na yaliyotajwa humo katika maneno ya Mwenyezi Mungu yalifutwa na Qur'ani, na kwa hakika Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- aliona karatasi ya Taurat kwenye mkono wa Omar akachukia, na akasema: "hivi je unamashaka namimi ewe mwana wa Ibnul khatwab, namuapa Mwenyezi Mungu lau kama ndugu yangu Mussa angekuwa hai asingefanya lolote zaidi ya kunifuata mimi " Omar akaitupa ile karatasi na akasema Niombee msamaha ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu" ameipokea Ahmad (3/387) kutoka kwa Jaabir bin Abdillah, na akaipa daraja ya Hasan hadithi hii Al-baaniy katika kitabu Al- ir-waau (1589).

([41]) Ameitoa hadithi hii Muslim(153), na Ahmad (2/317)

([42]) Ameitoa Abuu daudi (4608) na Tarmidhiy (2676) kwa mfano wake,wa ibnu majah (43) na tamko ni lake, na Ahmad (17142) kwa tofauti kidogo,na ameisahihisha Al-baniy katika sahihi Ibnu Majjah(41).

([43]) ameitoa malik (3338) na ameisahihisha Al-baniy katika sahihi Jaamiy (2937)

([44]) Amitoa ibnu majah (224),na Twabraniy katika Swaghiir (22), na ameisahihisha Al-baaniy katika sahihi Al-jaamiy(3808) na (3809).

([45]) Ameitoa Al- tarmidhii (2322), na ibnu majjah (4112),na ameisahihisha Al-baniy katika swahihi al-jaamiy(1609).

([46]) Na kwa hakika umeshatangulia ufafanuzi wa hilo katika sehemu ya Tatu iliyopita.

([47]) Na makusudio yake ni kuwa Haogopewi wala hatarajiwi katika viumbe kama vile maiti na masanamu ambao hawamiliki uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ama kuogopa kitu akiwezacho kiumbe kama kuogopa simba na mwizi, na vilevile kutarajia kwa mwenye kumiliki kutoa uwezo kama muhusika wa jambo fulani au mkarimu, basi hizo ni khofu na matarajio ya kawaida halaumiwi kwa kutarajia huko na kuogopa huko.

([48]) Hata katika hali ya kumchinja mnyama wa halali, kwa hakika ameamrisha Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kukinoa kisu na kumstarehesha mnyama. Na sehemu ya kumchinjia mnyama ni kukata koromeo na mishipa miwili ya damu mpaka itoke damu, na Ngamia huchinjwa kwa kuchomwa sehemu anayofungiwa kengele chini ya shingo, ama kumuua mnyama kwa kumpiga shoti ya umeme au kumpiga kichwa chake na mfano wa hivi; mnyama huyo anakuwa ni haramu na hafai kuliwa.

([49]) Ni Mbwa mvamizi mwenye kuudhi watu, na inakusanya wanyama wawindao wavamizi na wenye kuudhi watu.

([50]) Mwenye kuhukumu au Raisi (kingozi).

([51]) Ameitoa Bukhari(13) ,na Muslim,na tamko ni la muslim.

([52]) Nayo ni hotuba tukufu yenye kukusanya vilivyo sambaa katika vitabu vya hadithi za Mtume.

([53]) Ameitoa ahmad(22978,na akaisahihisha Al-albaniy katika mlolongo wa hadithi sahihi(199/6)

([54]) Ameitoa bukhariy (105), na muslim( 1718)na Tamko ni la Bukhariy.

([55]) Al- mufataraat ni madawa yenye kusababisha kusinzia kwa muda mrefu na kuuchosha mwili akili pamoja na viungo vya mwili.

([56]) Ameitoa abuu daudi (275/2,) na An-nasaaiyu (316/2), na ahmad(1652),na akaisahihisha Al-abaaniy katika sahihi al-targhiib wa tarhiib: (1411), waswahihul jaamiiy (41720).

([57]) Na amezilinda Mwenyezi Mungu Nasaba na kupotea na kuchanganyikana, kama kujinasibisha mtu kwa asiyekuwa baba yake kwa sababu ya uzinifu.

([58]) Na hili ndiyo bora zaidi kuliko kumkata mgonjwa kiungo kilichoharibika kwa ridhaa ya watu wake tena kwa usalama wa mwili wake!?.

([59]) Katika kivuli cha hukumu ya uislamu waislamu wanatoa Zakah, na wasiokuwa waislamu wanatoa Jiz-ya (kodi) = nayo ni mali ichukuliwayo kwa wanaume waliobaleghe, na sio wanawake wala watoto na wendawazimu wazee na mafukara, na Jiz-ya ni kiasi kidogo cha pesa hakikuzidi katika zama za Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- Diinari moja kwa kila mwaka, nacho ni kiwango cha pesa kidogo sana anachokitoa kila tajiri mara moja kwa mwaka; na kutoa huko ni badala ya kuishi kwao kwa amani chini ya kivuli cha sheria ya uislamu, na wananeemeka kwa maisha yenye amani, na ulinzi wao kamili wa mali zao na heshima zao toka kwa waislamu, zaidi ya hayo hupewa ulinzi wa makanisa yao na dini yao, na ikiwa waislamu watashindwa kuzitekeleza haki zao na kuwalinda na maadui zao basi watawarudishia jiz-ya walioichukua kwa kutotimia sharti; na sharti lenyewe ni ulinzi, na kama watashirikiana kuulinda mji wao, waislamu watawaondolea Jiz-ya, na serekali itawasaidia mafukara wao na kuwatibu wagonjwa wao kama inavyofanya kwa waislamu.

([60]) Na fitina inakuwa ni kuzuia uislamu usiwafikie watu, na kuwanyima uhuru wa kuingia katika uislamu pasina kuwalazimisha.

([61]) Al-riddat ( kuritadi): Ni kuuacha uislamu na kwenda kwenye ukafiri, na kuritadi hakumfanyi atosheke kuuchagua uislamu, na wala hakumbadilishii dini na utamaduni kwa hali yoyote, kwa kuritadi hakumfikishi kwenye kuona ukamilifu wa uislamu na miujiza yake, na katika vichocheo vya kuritadi, ni kuamsha fitina katika jamii ya kiislamu na vinavyomsukuma kuelekeza katika ukafiri na kwenda mbio ni kufukuzia matamanio na maslahi ya mali na ya kijamii, na kutoka katika uislamu kwa namna hii ni kutoka kwenye makubaliano makubwa na muhimu ya muumba, na hilo linafanana na kile wanachokikubali nchi nyingi katika zama zetu hizi miongoni mwa uhalifu mkubwa wa kihaini katika nchi, na kuwekewa adhabu ya kunyongwa kwa ajili hiyo, na mwenye kuritadi anafikia katika hali mbaya kiasi kwamba haimtoshi kumtenga na jamii ya kiisalamu isipokuwa kwa kuuwawa, isipokuwa ripoti kuhusu hali ya murtadi na kupitisha hukumu ya kisheria dhidi yake, hilo lipo mikononi mwa hakimu, kwa mujibu wa hatua za kihukumu za kina, ambazo zinafikia hali ya kumlinda mtuhumiwa asidhulumiwe kwa kuritadi na kuhifadhi dini ya jamii ya kiislamu.

([62]) Picha za viumbe wenye roho zilizo chorwa kwa mkono, au zilizo nakishiwa kwenye ubao au kitu kingine kisichokuwa ubao, au iliyotengenezwa kwa udongo au kitu kingine, navyo vinaingia katika dalili ya makemeo kwa wapiga picha.

([63]) Nabii wa Mwenyezi Mungu Issa -Amani iwe juu yake- hakuharamisha kuwa na mke zaidi ya mmoja kwa hakika wakristo kilichowazuia kulifanya hilo ni kufuata matamanio yao.

([64]) Wanawake wa kiislamu walio wema (ambao hawajaolewa au waliachika) akishawaingiza Mwenyezi Mungu peponi baada ya kufufuliwa na kuhesabiwa atawapa hiyari ya kuchagua wanaume waislamu wa peponi na wataozeshwa yule watakayemridhia, na mwanamke wa kiislamu akifa na akawa ameolewa zaidi ya mara moja atachagua mume aliyekuwa akimpenda zaidi duniani ikiwa atakuwa ni katika watu wa peponi.

([65]) Ameitoa ahmad (453,413,377/1, na ibnu maajah (340/2),na ibnu hibban (1394), na Haakim(196/4),na akisahihisha Al-albaniy katika silsilat swahiihat(451).

([66]) Ameitoa Abuu daudi (3874),na kaisahihisha Al-albaaniy katika swahihiul jaamiy(1762)

([67]) Anawaamrisha Mwenyezi Mungu waja wake na anawakataza na yeye anamjua nani atatii na nani ataasi kabla ya hilo, lakini kafanya hivyo ili aidhihirishe elimu hii na ili amlipe mja kwa matendo yake na asije kusema mkoseaji "Amenidhulumu Mola wangu kwa kuwa ameniadhibu kwa dhambi ambayo sikuifanya"; Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na hakuwa Mola wako ni mwenye kumdhulumu mja.) [Fusswilat: 46]

([68]) ameitoa muslimu(2999)na ahmad(332/4), na Daaramiy(2777),

([69]) Kama makhawaariji ambao wanawauwa watu wasiokuwa na hatia kwa jina la uislamu,na wao kwa ujumla wametokana na vitimbi vya maadui wa uislamu.

([70]) Amesema wa mwisho wa manabii Muhammad- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Hakuna mtoto yeyote isipokuwa huzaliwa katika maumbile ya uislamu, basi wazazi wake wawili ndio wanaomfanya awe yahudi au awe naswara au majuusi" Ameitoa Bukhariy(1292), na muslimu,(2658) na tamko la muslimu, katika hadithi hii anatufahamisha Mtume Muhammad -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kuwa mwanadamu huzaliwa katika umbile la uislamu, huwa muumini kwa umbile hilo, na lau angeachiliwa kuchagua angechagua uislamu pasina kubabaika, na kwa hakika hufikia hatua ya kuuchagua uyahudi na unaswara na umajusi na dini zingine na madhehebu yaliyo batili kwa sababu ya kulelewa kwake katika dini hizo.

([71]) Na Baatwiniyyah wana majina mengi, wanagawanyika makundi mengi katika nchi ya India na Sham, na Irani na Iraqi na miji mingine mingi, na wamelielezea kundi hilo kwa uwazi, wengi katika wanachuoni waliotangulia, kati ya hao ni Al- shaharustaan katika kitabu (Al-milal wa nihal) na kama walivyofafanua wengi waliokuja nyuma, na wakabainisha makundi mapya miongoni mwa hayo makundi: Al-qadiani na Al-bahaaiyah na makundi mengine, na katika waliobainisha makundi hayo ni Muhammad Saidi Al-kailaaniy katika kitabu (Dhailul milal wani-hali), na Sheikh Abdul Qaadir Shaibatul Hamdi, mwalimu katika chuo kikuu cha Madinatul Munawwarah katika kitabu Al-ad-yaan wal-firaqu wal-madhaahibu A-l-muaasirat.

([72]) Na miongoni mwa matendo yao ambayo yanachafua sura ya uislamu kupitia matendo, ni kujipiga makofi nyuso zao na vifua vyao na miili yao kwa minyororo yao na visu.