FUNGA YA RAMADHANI ()

Abubakari Shabani Rukonkwa

Makala hii inazungumzia: Mambo mbalimbali yanayohusu mwezi mtukufu wa Ramadhan, ikiwa ni pamoja na maana ya Swaumu, historia ya funga ya Ramadhan, na ubora wa swaumu na fadhila zake.

  |

  FUNGA YA RAMADHANI.

  Swahili.

  Imeandikwa na :

  Abubakari Shabani Rukonkwa.

  Imrpitiwa na :

  Yunus Kanuni Ngenda.

  صوم رمضان

  السواحيلية

  كتبه:

  أبوبكر شعبان روكونكوا

  راجعه:

  يونس كنون نغندا

  ---------------------

  ﺑﺴﻢ ﺍﻟﻠﻪ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﻟﺮﺣﻴﻢ

  Utangulizi

  Kwajina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma mwenye kurehemu, tunamshukuru sana Allah kwa neema zake nyingi sana juu yetu, na tukijaribu kuzihesabu neema zake kwetu hatuwezi kuzimaliza,

  Mwenyezi Mungu amabae ni Mmoja katika Uungu wake Mfalme wa siku ya qiyama hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hafananishwi na chochote katika viumbe vyake, Rehma na Amani za Allah zimuende Nabii Muhammad (s.a.w), pamoja na familia yake na Maswahaba zake na Waislamu wote watakaofuata mwenendo wake mpaka siku ya qiyama, amma baad.

  MAANA YA SWAUMU

  Kuna maana mbili za neno Swaum.

  1. KILUGHA

  2. KISHERIA

  Katika lugha ya kiarabu neno "Swaumu" lina maana ya:-

  Kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida mtu

  alilozoea kulifanya.

  Qur-ani inatufahamisha kuwa Bi Mariyam baada ya kumzaa Nabii Issa (Alayh Salaam) alijizuilia kusema na Mtu yeyote juu ya Mtoto wake.

  ﻓَﺈِﻣَّﺎ ﺗَﺮَﻳِﻦَّ ﻣِﻦَ ﺍﻟْﺒَﺸَﺮِ ﺃَﺣَﺪًﺍ ﻓَﻘُﻮﻟِﻲ ﺇِﻧِّﻲ ﻧَﺬَﺭْﺕُ ﻟِﻠﺮَّﺣْﻤَﻦِ ﺻَﻮْﻣًﺎ ﻓَﻠَﻦ

  ﺃُﻛَﻠِّﻢَ ﺍﻟْﻴَﻮْﻡَ ﺇِﻧْﺴِﻴًّﺎ

  Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za

  mtoto huyu) Sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa

  mwingi wa rehma ya swaumu(kufunga) kwa hiyo leo sitosema na mtu" (19:26)

  2.KISHERIA

  Katika sheria ya Kiislam neno Swaum lina maana ya:-

  Kujizuia kwa nia ya kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kuacha kula kunywa,kufanya tendo la ndoa,na maaswia mengine kuanzia kuchomoza kwa Alfajri mpaka kuzama kwa jua.

  Swaum kwa Muislam wa kweli ni zaid ya kujizuilia na hayo tuliyoyataja hapo juu.

  Kwa Muislam wa kweli Kufunga/swaum ni pamoja

  kujizuilia kutenda maovu yote yaliyokatazwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ili Swawm ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu- pamoja na fikra na hisia zake na matendo aliyokataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).

  Kwa kufanya hayo ndipo mfungaji ataweza kulifikia lengo la Swaum ambalo ni ili kuweza kupata cheo cha Uchamungu. Kama Allah anavyosema katika Qur'an kuwa:-

  ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁَﻣَﻨُﻮﺍ ﻛُﺘِﺐَ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢُ ﺍﻟﺼِّﻴَﺎﻡُ ﻛَﻤَﺎ ﻛُﺘِﺐَ ﻋَﻠَﻰ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ

  ﻣِﻦْ ﻗَﺒْﻠِﻜُﻢْ ﻟَﻌَﻠَّﻜُﻢْ ﺗَﺘَّﻘُﻮﻥَ

  " Enyi mlio amini mmefaradhishiwa kufunga kama

  walivyo faradhishiwa waliokua kabla yenu ili mpate

  kumcha Allah" (2:183)

  Na kinyume na hapo mtu atajizuia na kula na kunywa na hata kufanya jimai wakati wa Swaum lakini bado hatakuwa na Swaum kisheria na dalili ya hili tunaipata katika Hadith hii. Abu Hurayrah amesimulia kuwa Mtume wa Allaah

  amesema: “Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allaah hana haja na kuona kuwa anaacha chakula chake na kinywaji

  chake (yaani Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hana haja na funga yake.” (Al-Bukhaariy).

  HISTORIA YA FUNGA YA RAMADHANI

  Kwa mujibu wa Qur-ani tukufu tunaona kuwa kufunga si jambo lililoanzishwa na Mtume Muhammad(Swalah Llahu Alahy Wasalaam) bali

  ni ibada iliyotekelezwa na Nyumati za Mitume wa Allah walio pita kabla ya Mtume wetu Muhammad. Allah anasema:-

  ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁَﻣَﻨُﻮﺍ ﻛُﺘِﺐَ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢُ ﺍﻟﺼِّﻴَﺎﻡُ ﻛَﻤَﺎ ﻛُﺘِﺐَ ﻋَﻠَﻰ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ

  ﻣِﻦْ ﻗَﺒْﻠِﻜُﻢْ ﻟَﻌَﻠَّﻜُﻢْ ﺗَﺘَّﻘُﻮﻥَ

  " Enyi mlio amini mmefaradhishiwa kufunga kama

  walivyo faradhishiwa waliokua kabla yenu ili mpate

  kumcha Allah" (2:183(

  Na tukio hili la kufardhishwa funga katika Umma huu lilikuwa katika mwaka wa pili mwezi wa Sha‘abaan siku ya Jumatatu baada ya Hijra. Ila kama tulivyoona hapo mwanzo kuwa Funga/Swaum haikuanza ktk Ummah wa Mtume wetu Muhammad(Swallah Llahu Alayh Wassalam) bali hata kwa Mitume wengine waliopita kabla yake walikuwa wanafunga. Hebu tutizame ni vipi waliokuwa kabla walikuwa wanafunga.

  Watu wa Nabii Ibrahiym(Alayh Salam) Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) aliinuliwa katika jamii ya washirikina. Walikuwa wakiabudu jua, mwezi, nyota na masanamu chungu nzima waliyoyachonga

  wenyewe.

  Pamoja na ushirikina wao huo walikuwa

  wakifunga siku 30 mfululizo katika kila mwaka kwa

  heshima ya mwezi. Mayahudi (Judaism) Dini ya Kiyahudi ni dini waliyoibuni Mayahudi baada ya

  Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) ambapo walimfanya

  Uzairi mwana wa Mungu. Pamoja na hivyo Waumini wa Kiyahudi walikuwa wakifunga Alhamisi na Jumatatu kama kumbukumbu ya kwenda na kurudi

  kwa Nabii Mussa (‘Alayhis Salaam) katika safari yake ya Sinai kwenda kuchukua Taurati. Kutokana na kumbukumbu ya historia, Nabii Musa alikwenda kwenye mlima Sinai siku ya Alhamisi na kurejea

  siku ya Jumatatu baada ya siku arobaini kupita.

  Pia Mayahudi hufunga kwa saa 24 katika kila mwezi 10 Muharamu, kwa kumbukumbu ya siku ambayo Wanaisraili (Mayahudi) walipookolewa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kutokana na udhwalimu wa Firauni. Siku hii ambayo hata Waislamu wamesuniwa kufunga huitwa siku ya ‘Ashuuraa.

  Ukiacha siku ya ‘Ashuuraa ambapo funga huchukua saa 24, funga za Mayahudi huanza alfajiri na huishia pale inapojitokeza nyota ya kwanza usiku.

  Wakristo Hawa wanajnasibisha na Nabii Isaa (Alayhis Salaam. Katika dini hii Nabii ‘Iysaa (‘Alayhis Salaam) amefanywa mwana wa Allaah

  (Subhaanahu wa Ta’ala) na kwamba yeye ndiye

  mkombozi wa Wakristo. Pamoja na hivyo, Wakristo wanakiri kuwa kufunga ni Ibada kubwa miongoni mwa Ibada zao. Wakristo wa mwanzo walikuwa wakifunga siku 40 mfululizo kasoro siku za Jumapili kama kumbukumbu ya siku zile alizofunga Yesu (Nabii ‘Iysaa ‘Alayhis Salaam) kama inavyobainishwa katika kitabu chao(Biblia(

  UBORA WA SWAUMU NA FADHILA ZAKE

  Linalo julisha ubora na fadhila za Funga ni maneno ya Mtume (Swallah Llahu Alayh Wassalam) haya yafuatayo:-

  "ﺍﻟﺼﻮﻡ ﺟﻨﺔ ﻣﻦ ﺍﻟﻨﺎﺭ ﻛﺠﻨﺔ ﺃﺣﺪﻛﻢ ﻣﻦ ﺍﻟﻘﺘﺎﻝ "

  (1). Kufunga ni kinga ya Moto kama vile kinga ya mmoja wenu katika vita".(Ahmad, Nasaiy)

  ﻣﻦ ﺻﺎﻡ ﻳﻮﻣﺎ ﻓﻲ ﺳﺒﻴﻞ ﺍﻟﻠﻪ ﺑﺎﻋﺪ ﺍﻟﻠﻪ ﺑﺬﻟﻚ ﺍﻟﻴﻮﻡ ﺣﺮ ﺟﻬﻨﻢ

  ﻋﻦ ﻭﺟﻬﻪ ﺳﺒﻌﻴﻦ ﺧﺮﻳﻔﺎ

  (2). Atakae funga siku moja katika njia ya Allah, Allah atamwepusha kwa utukufu wa siku hiyo uso wake na joto la moto wa Jahannam umbali wa miaka sabiin" (Ahmad, Nasaiy,Ibn Majah,Tirmidhi(

  ﺃﻥ ﻓﻲ ﺍﻟﺠﻨﺔ ﺑﺎﺏ ﻳﻘﺎﻝ ﻟﻪ ﺍﻟﺮﻳﺎﻥ ﻳﻘﺎﻝ ﻳﻮﻡ ﺍﻟﻘﻴﺎﻣﺔ ﺃﻳﻦ

  ﺍﻟﺼﺎﺋﻤﻮﻥ ﻫﻞ ﻟﻜﻢ ﺇﻟﻰ ﺍﻟﺮﻳﺎﻥ ﻣﻦ ﺩﺧﻠﻪ ﻟﻢ ﻳﻈﻤﺄ ﺃﺑﺪﺍ ﻓﺈﺫﺍ

  ﺩﺧﻠﻮﺍ ﺃﻏﻠﻖ ﻋﻠﻴﻬﻢ ﻓﻠﻢ ﻳﺪﺧﻞ ﻓﻴﻪ ﺃﺣﺪ ﻏﻴﺮﻫﻢ

  3 " Hakika peponi kuna mlango unaitwa Rayyan,

  pata semwa siku ya Qiyama; wako wapi waliokuwa

  wakifunga waingie katika mlango huu? Watakapo ingia hawatohisi kiu tena na utafungwa mlango wake hatoingia humo ila aliyedumu na ibada ya Funga" (Bukhari,Muslimu,Nasaiy) Na hadithi nyinginezo. Na mlango huu umepewa jina hilo kunasibiana na sifa ya Swawm ambayo inampa

  mtu kiu kutokana na athari ya kufunga. Mara

  nyingi mtu anapofunga hatamani chakula kama

  anavyotamani maji.

  FADHILA ZA MWEZI WA RAMADHANI

  Ameeleza Mtume (Swallah Llahu Alayh Wasalam) ubora/fadhila za mwezi wa ramadhani

  katika hadithi zifuatazo:-

  ﺍﻟﺼﻠﻮﺍﺕ ﺍﻟﺨﻤﺲ ﻭﺍﻟﺠﻤﻌﺔ ﺇﻟﻰ ﺍﻟﺠﻤﻌﺔ ، ﻭﺭﻣﻀﺎﻥ ﺇﻟﻰ ﺭﻣﻀﺎﻥ

  ﻣﻜﻔﺮﺍﺕ ﻟﻤﺎ ﺑﻴﻨﻬﻦ ، ﺇﻥ ﺍﺟﺘﻨﺒﺖ ﺍﻟﻜﺒﺎﺋﺮ ) [ ﺭﻭﺍﻩ ﻣﺴﻠﻢ

  1-"swala tano, swala ya Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani (yote hayo) ni yenye kufuta dhambi zilizo baina yake, maadamu madhambi makubwa yataepukwa." (Muslimu)

  ﻣﻦ ﺻﺎﻡ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺇﻳﻤﺎﻧﺎً ﻭﺍﺣﺘﺴﺎﺑﺎً ﻏﻔﺮ ﻟﻪ ﻣﺎ ﺗﻘﺪّﻡ ﻣﻦ ﺫﻧﺒﻪ)) ))

  [ ﻣﺘﻔﻖ ﻋﻠﻴﻪ "

  2- "Atakaefunga Ramadhani hali ya kuamini na kutaraji thawabu atasamehewa dhambi zake zilizo

  tangulia" (Bukhari na Muslimu)

  ﺇﺫﺍ ﻛﺎﻥ ﺃﻭﻝ ﻟﻴﻠﺔ ﻣﻦ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺻﻔﺪﺕ ﺍﻟﺸﻴﺎﻃﻴﻦ ﻭﻣﺮﺩﺓ ﺍﻟﺠﺎﻥ ،

  ﻭﻏﻠﻘﺖ ﺃﺑﻮﺍﺏ ﺍﻟﻨﺎﺭ ﻓﻠﻢ ﻳﻔﺘﺢ ﻣﻨﻬﺎ ﺑﺎﺏ ، ﻭﻓﺘﺤﺖ ﺃﺑﻮﺍﺏ ﺍﻟﺠﻨﺔ

  ﻓﻠﻢ ﻳﻐﻠﻖ ﻣﻨﻬﺎ ﺑﺎﺏ ، ﻭﻧﺎﺩﻯ ﻣﻨﺎﺩٍ : ﻳﺎ ﺑﺎﻏﻲ ﺍﻟﺨﻴﺮ ﺃﻗﺒﻞ ، ﻭﻳﺎ

  ﺑﺎﻏﻲ ﺍﻟﺸﺮّ ﺃﻗﺼﺮ ، ﻭﻟﻠﻪ ﻋﺘﻘﺎﺀ ﻣﻦ ﺍﻟﻨﺎﺭ ،

  ﻭﺫﻟﻚ ﻛﻞ ﻟﻴﻠﺔ )

  3- "Inapokuwa usiku wa kwanza wa Mwezi wa

  ramadhani Masheitwani hufungwa na Majini wakorofi,nao hufungwa pia Milango yote ya moto,na hufunguliwa milango yote ya pepo.Hutangaza mtangazaji (malaika) kwa kusema: Ewe unaetaka kheri elekea katika kheri hiyo,na Ewe mwenye kutaka shari acha shari hiyo, Allah huwa anawaacha huru na moto.Na maneno haya

  husemwa kila usiku" (Tirmidhi.(

  Pia ndani ya mwezi huu ndimo Qur'an iliteremshwa kutoka ktk Lawhum Mahfuudh ilaa samaai dduniya (Kutoka Lawhim-Mahfuudh mpaka mbingu ya

  kwanza. Hivyo kwa ubora wa Qur'an basi inaunyanyua mwezi huu na kuwa bora kama Allah alivyosema katika Qur'an kuwa:-

  "Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi ambao imeteremshwa Qur-aan ili iwe uongozi kwa

  watu na hoja na upambanuzi (Baina ya haki na batil)” (Qur'an Baqarah:185(

  Kitu kingine kinachoupa ubora mwezi huu ni Usiku wa Cheo/Laylahtul qadr kwani ktk usiku huu ndimo Qur'an ilishuka na usiku huu ukafanywa kuwa bora zaidi ya miezi elfu moja. Kama Allah alivyosema:-

  "Huo ni usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu.Huteremka Malaika na roho (za viumbe watakatifu) katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola kwa kila jambo.Ni amani (usiku) huo mpaka

  mapambazuko ya alfajiri" (Qur'an 97:3-5(

  Yaan mtu akifanya Ibada ndani ya usiku huo basi ibada ile huandikwa/hulipwa sawa na mtu aliyefanya ibada hiyo kwa miezi elfu moja.

  Pia ndani ya mwezi huu Dua zetu hupokelewa kwa kila mwenye kuomba na haya tunayapata Katika hadiyth iliyopokewa na Imaam Ahmad: "Kutoka kwa Jaabir (radhiya Allaahu 'anhu) kwa isnadi iliyo nzuri kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Amesema: "Kila Muislam du'a zake ni zenye kukubaliwa atapomuomba Allah katika mwezi wa Ramadhaan". Kuna Fadhila nyingi katika mwezi huu ambazo zimeufanya mwezi huu kuwa na ubora ndani yake na ikawa ni furaha kubwa kwa Muumini kupitikiwa/kufikiwa na mwezi huu na akaudiliki huku akiwa na afya nzuri akawa ni mwenye kutekeleza Ibada zinazopatikana ndani ya mwezi huu.

  UBORA WA AMALI NJEMA NDANI MWEZI WA RAMADHANI.

  Thawabu za amali njema huongezwa kwa sababu

  nyingi miongoni mwazo ni utukufu na ubora wa zama,kama mwezi wa Ramadhani. Zifuatazo ni baadhi tu ya amali njema zinazoongezewa thawabu katika Mwezi wa Ramadhani:

  1.Kusimama usiku kwa Ibada Mtume(Swallah Llahu Alayh Wassalam) kasema:

  ﻣﻦ ﻗﺎﻡ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺇﻳﻤﺎﻧﺎً ﻭﺍﺣﺘﺴﺎﺑﺎً ﻏﻔﺮ ﻟﻪ ﻣﺎ ﺗﻘﺪﻡ ﻣﻦ ﺫﻧﺒﻪ )

  [ ﻣﺘﻔﻖ ﻋﻠﻴﻪ ]

  Atakae simama Ramadhani ilhali ya kuamini na kutaraji thawabu Allah atamsamehe dhambi zake zilizo tangulia" (Bukhari na Muslimu)

  2.Kufanya Umra.Mtume(Swallah Llahu Alayh Wassalam) anasema:

  ( ﻋﻤﺮﺓ ﻓﻲ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺗﻌﺪﻝ ﺣﺠﺔ ﻣﻌﻲ ) [ ﻣﺘﻔﻖ ﻋﻠﻴﻪ ]

  Umrah katika mwezi wa Ramadhani hulingana na Hijja pamoja nami" (Bukhari na Muslimu)

  3.Kusoma Qur-ani tukufu.

  Kwa kuwa Qur'an imeshushwa ndani ya mwezi huu basi kila mwenye kukithilisha kuisoma ktk mwezi huu basi anaujira mkubwa zaidi na baada ya kulitambua hilo Maswahaba walikithirisha sana kuisoma Qur'an ndani ya mwezi huu na mifano yao tunaiona hapa chini.

  'Uthmaan bin 'Afaan (Radhiya

  Allaahu 'anhu) kila siku akisoma Qur-aan yote

  yaani anakhitimisha mara moja kwa siku, kwa

  maana, msahafu mzima anausoma kwa siku moja. Na walikuwa baadhi yao katika wema wakisoma Qur-aan yote kwa siku tatu,wengine kwa wiki moja na wengine kwa siku kumi.Walikuwa wakisoma Qur-aan ndani ya Swalah na nje ya Swalah.