HUSDA NA TIBA YAKE ()

Abubakari Shabani Rukonkwa

MADA HII INAZUNGUMZIA HUSDA NA TIBAYAKE KWA KTK MTIZAMO WA QURAAN NA SUNNAH.

  |


  بسم الله الرحمن الرحيم


  HUSDA NA TIBAYAKE.

  Imeandikwa na Abubakari Shabani Rukonkwa.

  Imepitiwa na Ummu Rahma.


  Kila sifa kamilifu nizake Allah mtukufu ambae katuchagulia uislam kuwa ndio dini ya kweli sala na amani zimuendee mtume Muhammad s.a.w.ambae kaletwa na Allah ili kutufafanulia dini hii na kuwa ndio kiigizo chema,na ziwe juu ya Ali zake na maswahaba zake na woote wenye kumfaata mpaka siku ya Qiyama.

  Baada ya salam

  Leo nakuletea darsa muhimu sana ambalo lina anwani inayoitwa:

  HUSDA NA TIBAYAKE.

  Nitazungumzia ktk darasa hii baadhi ya mambo muhimu kwaufupi mambo yafwatayo:

  1.MAANA YA HUSDA.
  2.DALILI ZA KUTHIBITISHA HUSDA KTK QURAN NA SUNA.
  3.TOFAUTI YA HUSDA NA GHIBTWATU.
  4.SIFA ZA HASIDI.
  5.MADHARA YA HASIDI
  6.NAMNA INAVYO MPATA MTU HUSDA.
  7.NAMNA YA KUITIBU HUSDA.

  Hayo nimachache ambayo nitakuletea ktk darsa hii fupi.
  tunamuomba Allah atuandikie malipo katika dunia na akhera.
  Nakuomba nduguyangu muislam usome darasa hili kwa utulivu ili uifaidishe nafsi yako na ya mwenzako kwani husda nimaradhi makubwa sana ambayo hayachaguwi mwema wala muovu mwanachuoni wala mjinga wote huwapata ao kuwadhuru wengine.

  1.MAANA YA HUSDA.
  Husda maana yake:nikutamani kuondokewa na neema ambayo Allah amemteremshiya mwenzako.
  Pia waweza kusema:nikuchuki kitu chochote chakheri ambacho kiko kwa mwenzako na kutamani kimuondokee kama mtoto ao nyumba gari ao nguo kazi sawasawa imemrudia yule hasidi ao imepotea na Nk.

  kwakuwa husda nisumu kali Allah jallah jalaluhu hakuacha kuizungumzia ktk quraan pia na kipenzichake mtume s.a.w.ktk sunnah.

  2.DALILI KTK QURAN NA SUNNA KUHUSU HUSDA:
  A.Ama ktk Quran.
  Asema m.mungu ktk suratul baqara aya 109{wanatamani wengi ktk mayahudi na manaswara laiti wangeweza kuwarudisha enyi waslam ktk ukafiri baada ya kuamini ikiwa ni HUSDA kutoka kwao baada ya kuwabainikiya kuwa uislam ndio dini ya haki}.
  B.anasema allah ktk suratul annisaa aya ya 54{hivi hao hao makafiri wana wahusudu watu kwayale aliyo wapa allah kutokana na fadhila zake hakika tumewapa watu wa ibrahima kitabu na hekima na tukawapa ufalme mkubwa}.
  C.pia asema allah ktk suratil falaq.aya ya 5.{pia ninajikinga na shari za hasidi pindi anapo husudu watu}.

  Subhana Allah!!!!nduguyangu husda sio kitu kidogo kwani ukiangalia hiyo suratul falaq utakuta myongoni mwavitu alivyo amrishwa mtume s.a.w ajikinge kwa alla ni:
  1.shari zote zilizo umbwa na allah.
  2.shari za usiku pindi unapo ingia.
  3.shari za wachawi wanapo fanya uchawi wao.
  4.nashari za hasidi pindi anapo fanya uhasidi wake.
  Allah atukinge na shari hizo.

  B.DALILI KTK SUNNAH.
  Amepokea Abuu huraira R.a.alisema:alisema mtume s.a.w(hakika utapatwa umma wangu na maradhi.maswahaba wakamuliza nimaradhi gani hayo ewe mtume wa Allah?!akasema:
  1.kupinga haqi.
  2.kuitafuta duniya saaana kuliko akhera.
  3.Nakushindana ktk mambo ya kidunia.
  4.kuchukiyana.
  5.na kuhusudiyana ao kufanyiyana husda mpaka utakuwa uovu mkubwa na maneno mengi kushinda vitendo).imepokelewa na twabraan.

  3.TOFAUTI YA HUSDA NA GHIBTWA NA HIQDI.

  Kuna tofauti kubwa sana baina ya husda na ghibtwa na hiqdi:
  ¤Ama husda:nikutamani kuondokewa na nema kwa nduguyako,ao kumalizika ao kupotea.nahii niharamu.

  ¤Ghibtwa:nikutamani alicho nacho mwenzako pamoja nakumuomba allah akupe mfano wake ao ziyada lakini bila kuondokewa ao kupunguziwa kwa nduguyako.nahii nihalali.

  ¤Hiqdi:nikujenga chuki moyoni ya kumchukiya mwenzako mwislam sawasawa kwasababu ao bila sababu.nahii niharamu kwamwislam kwani niktk sifa za makafiri hiqdi na husda.

  4.SIFA ZA MAHASIDI.
  Sheriya yetu tukufu ilipo yajuwa madhara ya husda ilijaribu kufanya uchunguzi wakina kabisa ktk kumjuwa hasidi ili ujiepushe nae kwani uhasidi niktk mambo hatari sana ktk maisha ya jamii.
  Na mimi nitajitahidi kukupa baadhi ya sifa za mahasidi kama ifwatavyo:
  1.kutizama saana.
  2.kutabasamu kwa uwongo bila ya kuonyesha furaha ya dhati ktk nafsi.
  3.kukunjana kwa uso wakati akitizama .
  4.maneno yake wakati akizungumza.
  TNB:Nialama ambazo unaweza kumjuwa huyo hasidi kwani huwa na mtizamo usio kuwa wa kawaida ktk lile jambo analo lihusudu allah atukinge na husuda.

  5.kuchukia wakati wote na qadari ya allah.
  6.nimwingi wa malalamiko mchache wa kushukuru hata akipewa duniya nzima hatosheki.
  7.yeye hufatiliya makosa sikuzote,na kuya tangaza kwayule ambae anamhusudu ktk vikao.
  8.huficha mazuri yote anayoyafanya yule anae mfanyiya husda nakujifanya hayajuwi mema yake.
  9.wakati mwingine hasidi hukwambia kitu kamavile niutani kumbe moyöni mwake kumejaa chuki na mifundo bila sababu yoyote.
  10.hasidi huyu akipata nafasi ya yakumuombeya ubaya yule anae mhusudu basi haipotezi.

  subhana llah angaliya hizo sifa za hasidi allah atuhifadhi nahawa watu wapo na niwengi mimi nimewahi kuwaona pia nakuwasikia wakiwaombea duwa mbaya wasio kuwa na hatiya yoyote bora vijipesapesa vyake viungue na moto ao makubwa zaidi yahayo.
  Nduguyangu mwislam allah haharamishi jambo ila huwa kuna madhara mengi.

  TMB:Unatakiwa kujuwa sifa hizo kwani husda hutokea hata kwa:
  A.mchamungu.
  B.muovu.
  C.mama.
  D.baba
  É.mkubwa na mdogo.
  F.pia huwenda ikatokea kwako wewe mwenyewe.
  Ndiyo mana uhasidi ukawa nisumu kubwa saaana.sasa ukijuwa sifa hizo itakuwa rahisi sana kuondoa ao kugata matibabu yake.

  5.MADHARA YA UHASIDI.
  Myongoni mwa madhara ya uhasidi :
  1.hukata mafungumano ya kifamiliya.
  2.hukata mafungamano ya kijamii.
  Kwani huleta chuki na maelewano mabaya.

  mwalimu wa umma mtume s.a.w.anatuelekeza sisi waislam njiya safi nzuri ya maisha akisema:(msi husudiane wala msikatiane udugu wala msichukiane kuweni waja wa m.mungu ndugu).

  anasema tena ktk hadidhi nyingine.(ombeni saana msaada kwa allah ktk kufanya mambo yenu kwakuficha ao kufanya siri kwahakika kila mwenye neema anahusudiwa)ameipokea hadidhi hii ibn abi dunyaa.

  6.NAMNA YA KUPATWA NA HUSUDA.
  Adhari ya husda kwa mtu ambae iliye mpata husda Allah atukinge,huwa inampta ktk namna mbili:
  A.uharaka wa kumuuwa papo hapo yule aliye patwa na husuda kwa haraka saana.
  Na namna hii haina dawa,na hii husda huwa kwa mtu ao mifugo,nyumba ao gari,Nk.
  B.nikupatwa na husuda lakini isiyo uwa.
  Na hii inawezekana kutibiwa na tiba yake nikama ifwatavyo:

  7.NAMNA YA KUTIBU MARADHI YANAYO SABABISHWA NA HUSDA.
  Husuda isiyokuwa na adhari ya kuuwa,tibayake imegawanyika maratatu:

  1.TIBA YA KUIREJESHA KABLA HAIJA TOKEA.YANI KAMA KINGA.
  Tiba hii inakuwa kwa kumuombea baraka yule mwenye neema.
  Myongoni mwa hikima ya Allah mtukufu nikwamba mwenye kijicho kibaya pindi anapo muombea baraka yule mwenye neema basi kile kijicho huanguka hapohapo na athari yake huondoka inakuwa M.mungu amerudisha hukumu yake kwa qudura zake.
  Asema mtume s.a.w.{pindi atakapo ona mmoja wenu kwa mwenzake neema yoyote basi amuombee baraka}
  Nakutoka kwa sahli bin haniif R.a.alisema:alisema mtume s.a.w.{atakae ona myongoni mwenu yale yanayo mfurahisha ao kumshangaza ktk mambo mazuri ktk nafsi yake ao malizake basi ajiombee baraka kwasababu kijicho nihaqqi}ameipokea imam
  ahmad.na hakim.

  NINI MAANA YA KUOMBA BARKA!?
  Wana chuoni wanasema kuwa kuomba barka ambako kunaondoa hasad nikusema duwa zifwatazo:
  1.Baaraka allah fiika.
  2.maashaallah tabaaraka allah
  3.allah humma baark.
  Hizo ninamna za kuomba baraka ambazo anatakiwa yule hasidi amwambie mwenye neema.
  TNB:duwa hiyo huziwiya hasad kabla haijatokea
  inatakiwa kwa yule mwenye kitu ambacho anaogopa huwenda ata husudiwa amwambie yule mwenzake ao mama yake ao yoyote aseme:mashaallah tabaarakallah.
  Hii nitiba ya husda kabla ya kutokea.

  2.TIBA BAADA YA KUTOKEA.
  Husuda inapo tokea ikampata mtu tayari.
  Hakika tiba yake iko aina mbili:
  1.pindi atakapo julikana yule hasidi anatakiwa aitwe amrishwe yafwatayo:
  asimame ndani ya beseni ao chombo kikubwa kama sifuriya kubwa kisha afanye yafwatayo:
  1.atawadhe ndani ya chombo kile.kisha aoshe uso na mikono yake na fundo mbili za mikono na magoti aoshe na vidole vya miguu.
  2.zile nguo alizo vaa azioshee ndani ya kile chombo.
  Kisha yachukuliwe yale maji bila kujuwa mgonjwa amwagiwe mgongoni mwake bila kujuwa yule mgonjwa.mtume asema atapona wakati ule ule inshaallah.
  Amepokea muslim ktk kitabu chake:asema mtume s.a.w.{hasadi ni haqqi laiti kama kungekuwa na chochote kinachoweza kushindana na qadar basi hasad ingetanguliya qadar ya allah na atakae ombwa kuoga ili kumtibu aliye patwa na husuda basi aoge}rawahu muslim.

  3.TIBA YA HASAD KWA QURAAN NA SUNNAH.
  Wakati mwingine hutokea hasadi na humjuwi nani kamfanyiya hiyo hasadi,ktk hali kama hiyo hakuna ujanja wa kutibu ispokuwa nikukimbiliya kwa allah kwa kutumiya Quran na sunna sahii,kwani allah hakureta maradhi ispokuwa kateremsha dawa yake.
  Na kutibu hasadi kwaku quraan nikama ifwatavyo:
  1.hatuwa ya kwanza.
  Ikiwa yule mgonjwa anaweza kusoma quraan anatakiwa akusanye viganja vyake viwili,kisha asome:
  A.fatiha.
  B.kursiy.
  C.muawidhati.yaani ikhlas,falaq,na annasi.
  D.myongoni mwa athkari pia zakumsomea bada ya hizo sura:
  :
  1أعوذ بكلمات الله تامات من شر ماخلق.
  2:أعوذ بكلمات الله التامة من كل شيطان وهامة ومن كل عين لامة.
  3:بسم الله أرقيك من كل شيئ يؤذيك ومن شركل نفس أوعين حاسد الله يشفيك بسم الله أرقيك.
  Kisha apulize ktk viganja vyake na mateyake mepesi kisha ajipake.

  2.hatuwa ya pili.
  Nikununuwa mafuta ya zaituni ao haba saudaa kisha asomee mafuta hayo kisha ajipake ktk sehemu zenye maumivu.

  3.hatuwa yatatu.
  Nikuchukuwa maji na kuyasomea hizo sura na adhkari hapo juu.

  kwaufupi hiyo ndiyo tiba ya hasadi ambayo uislamu umetufundisha wakati wowote yakitokea maradhi kama hayo.
  Ninamuomba allah atukinge na maradhi hayo atupe afya njema na atuwezeshe kufanya ibada na kushikamana na sunnah.

  ust.Abubakar Shaaban Rukonkwa
  Al imam islamic University
  Riyadh Saudi Arabia
  .