Misingi Minne Muhimu Katika Uislamu ()

Abubakari Shabani Rukonkwa

Mada hii inazungumzia misingi mine ya Tawhidi ambayo ni muhim sana kwa Muislam kuijua misingi hiyo.

  |

  بسم الله الرحمن الرحيم

  Misingi Minne Muhimu Katika Uislamu

  Imwkusanywa na Abubakari Shabani Rukonkwa.

  Imwpitiwa na Yunus Kanuni Ngenda.


  Namuomba Allaah Mtukufu, Mola wa 'Arshi kubwa Akutawalishe katika Dunia na Akhera na akufanye wewe uwe mwenye baraka popote utakapokuwa na akufanye wewe uwe miongoni mwa wale wanapopewa wanashukuru, na wanapopewa mitihani wanasubiri, na wanapofanya madhambi wanaomba msamaha, hakika haya mambo matatu ni anwani ya kufaulu.

  Jua, Akuongoze Allaah katika kumtii Yeye, hakika kumpwekesha Allaah ni mila ya Nabii Ibraahiym ('Alayhis Salaam) nayo ni kumuabudu Allaah peke Yake hali yakuwa ni mwenye kumtakasia dini kama alivyosema Allah:
  "Na wala Sikuwaumba Majini na Wanaadamu ila kwa lengo la kuniabudu Mimi" Adh-Dhaariyaat: 56.

  Basi pindi takapofahamu kuwa hakika Allaah Amekuumba wewe kwa lengo la 'Ibaadah, itakupasa ujue ya kwamba 'Ibaadah haiitwi 'Ibaadah mpaka ipatikaniwe kumpwekesha Allaah, kama ilivyo Swalah haitwi Swalah mpaka ipatikaniwe twahara basi itakapoingia shirki katika 'Ibaadah inaharibika 'Ibaadah kama hadathi inapoingia katika twahara inaharibu twahara, basi utakapojua hakika ya shirki itakapochanganyika na 'Ibaadah inaiharibu 'Ibaadah na inaporomosha 'amali na atakuwa huyo aliyemshirikisha Allaah katika moto milele, basi utakuwa umejua ya muhimu kwako ni kulijua hilo ili huenda Allaah Akakuokoa na mtego huu nao ni kumshirikisha Allaah, shirki amabayo Allah Alisema kuhusiana nayo:
  "Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa pamoja naye na anasamehe kwa yalio kuwa chini ya shirki kwa amtakaye" An-Nisaa: 116

  Nayo ni kwa kujua misingi minne alioitaja Allaah katika kitabu Chake.

  MSINGI WA KWANZA

  Ni kujua ya kwamba wale makafiri aliopigana nao Mtukufu ndio muumbaji mwenye kupeleka mambo lakini kuamini huko hakukuwaingiza katika Uislamu na ushahidi ni neno lake Allaah:

  "Sema (ewe Muhammad, uwaambie hao washirikina) ni nani anayewaruzu kutoka mbinguni na ardhini, na ni nani anayemilki kusikia kwenu na kuona kwenu, na ni nani anayetoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, na ni nani apangae (apelekae) mambo? Basi watasema ni Allaah sema (kuwaambia) basi hamumuogopi Allaah?"

  Yuunus: 31

  MSINGI WA PILI

  Ni ya kwamba wao washirikina wanasema hatuwaombi na wala hatuelekei kwa hao waungu wao ila kutaka kukurubishwa na kutaka uombezi kwa Allaah na ushahidi ya kwamba wao walikuwa wakiwaabudu kutaka kukurubishwa ni neno Lake Allaah:

  "Na wale ambao waliofanya pasi na Allaah vipenzi wakidai hatuwaabudu ila twataka watukurubishe kwa Allaah hakika Allaah Atahukumu katika yale waliyokuwa wakitofautiana, hakika ya Allaah Hamuongozi yule ambaye ni mkanushaji aliyekufuru" Az-Zumar: 3

  Na dalili ya kutaka uombezi neno Lake Allaah Mtukufu:
  "Na wanaabudu asiyekuwa Allaah yule ambaye hawawadhuru wao wala hawawanufaishi wao na wanasema hawa ndio vipenzi vyetu mbele ya Allaah" Yuunus: 18

  Uombezi Uko Aina Mbili:

  1) Uombeziu liokatazwa

  2) Uombezi uliothibitishwa au kukubaliwa.

  Ama uombezi uliokatazwa ni ule ambao unaombwa asiyekuwa Allaah katika yale ambayo hana uwezo juu yake isipokuwa Allaah tu na ushahidi ni neno Lake Allaah Mtukufu:
  "Enyi mlioamini toeni Alivyokuruzukuni Allaah kabla haijakufikieni Siku ambayo hapatakuwa na kujikomboa ndani yake wala urafiki wala uombezi na waliokufuru ndio madhalimu" Al-Baqarah: 254

  Na uombezi unaokubalika ni ule ambao huombwa Allaah na muombaji amekirimiwa kwa kupewa uombezi na yule mwenye kuombewa ni yule aliyeridhiwa na Allaah kauli yake na vitendo vyake baada ya kupata idhini kama Alivyosema Allaah:
  "Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini Yake Allaah" Al-Baqarah: 255

  MSINGI WA TATU

  Ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitokeza kwa watu wenye 'Ibaadah aina tofauti tofauti wengine wakiabudu Malaika na wengine walikuwa wakiabudu Manabii na watu wema na wengine wakiabudu miti na mawe wengine wakiabudu jua na mwezi na Mtume akapigana nao vita na wala hakuwatofautisha kwa vile wanavyoviabudu, ushahidi wa haya ni neno Lake Allaah Mtukufu:
  "Na pigana nao vita (Makafiri) mpaka kusipatikaniwe fitna (shirki) na dini yote iwe ni ya Allaah peke Yake" Al-Anfaal: 39.

  Na dalili ya jua na mwezi ni neno Lake Allaah:
  "Na katika alama Zake ni usiku na mchana na jua na mwezi, basi msilisujudie jua wala mwezi bali msujudieni Allaah Aliyeviumba hivyo ikiwa nyinyi kweli mnamuabudu Yeye Allaah" Fusswilat: 37
  Na dalili ya Malaika ni neno Lake Allaah Mtukufu:
  "Na wala hatukuwaamrisheni nyinyi kuwafanya Malaika na Manabii kuwa waungu" Aal-'Imraan: 80

  Na dalili ya Manabii ni neno Lake Allaah:
  "Kumbukeni Allaah Atakaposema 'Iysa mtoto wa Maryam je, wewe uliwaambia watu nifanyeni mimi na mamangu waungu badala ya Allaah? Aseme ('Iysa) Wewe umetakasika kuwa na mshirika haiwi kwangu mimi kusema lisilokuwa la haki, ikiwa mimi ningalisema bila shaka ungelijua, unayajua yaliyomo katika nafsi yangu na wala sijui yaliyo katika nafsi Yako, hakika Yako ni mjuzi wa ghayb" Al-Maaidah: 116.

  Na dalili ya watu wema ni neno Lake Allaah:
  "Hao ndio wale wanaowaomba wakitaka kwake kukaribiana na Mola wao walio karibu sana na Mola wao miongoni mwao (na Allaah kama Malaika, wao wanafanya haya haya), wanatumai rehma Zake na wanaogopa adhabu Zake Allaah" Al-Israa: 57

  Na dalili ya miti na mawe ni neno Lake Allaah:
  "Je, mumewaona Laata na 'Uzah na yule Manaata wa tatu wa mwisho?" An-Najm: 19-20

  Na Hadiyth ya Abu Waaqid Al-Laythiy (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema tumetoka na mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda katika vita vya Hanayn na sisi tukiwa tumesilimu karibuni na walikuwa washirikina wana mkunazi wakitundika hapo panga zao kwa ajili ya kupata baraka, mti huo ukiitwa Dhaatu Anwaat, tukapita katika mkunazi tukasema ewe Mtume tufanyie na sisi huo mti wa Dhaatu Anwaat tupate baraka kama vile walivyonao hao Dhaatu Anwaat, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
  “Mungu Mkubwa hakika mmesema maneno makubwa kama vile Banu Israaiyl walivyomwambia Muusa" At-Tirmidhiy.  MSINGI WA NNE

  Hakika washirikina wa sasa wamezidisha kufanya shirki kuliko washirikina wa mwanzo kwa sababu washirikina wa mwanzo walikuwa wakifanya shirki wakati wa raha na wakimtakasia Allaah 'Ibaadah wakati wa matatizo. Na washirikina wa sasa shirki zao ni wakati wote sawa wawe katika raha au katika shida, na dalili ni neno Lake Allaah:
  "Na wanapopanda katika meli (wakiwa katika misukosuko) humuomba Allaah na hali ya kuwa wakimtakasia yeye dini, lakini pindi wakiokolewa wakifika katika nchi kavu wanarudia kaika shirki zao" Al-'Ankabuut 65

  Imetimia hapa hii Misingi Minne na Swala na Salamu ziende kwa Mtume Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa (aalihi wa sallam).