Kimetungwa na Imamu Mujaddid Sheikhul islami Muhammad Ibnu Abdil Wahaab. Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu.
1. Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mimi nimejitosheleza na washirika juu ya kushirikishwa; atakayefanya jambo lolote akamshirikisha pamoja nami mwingine nitamuacha na shirki yake au (na mshirika wake)".
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
2. Kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: “Alisimama kati yetu Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu halali na wala haimstahikii kwake kulala, na hushuka Mizani na kuinyanyua, hunyanyuliwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, kinga yake ni nuru, laiti angeifunua basi mwangaza wa uso wake ungeliunguza kila kitu katika viumbe vyake mpaka mwisho wa linapoishia jicho lake”.
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
3. Na kutoka kwa Abuu Hurayra -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi mar'fuu: “Kuliani mwa Mwenyezi Mungu kumejaa hakupunguzwi na kutoa kokote, humimina usiku na mchana, hebu nielezeni ni kiwango gani alichokitoa tangu ameumba mbingu na Ardhi? kwani hakijapunguza chochote katika yale yaliyoko kuliani kwake, na uadilifu uko katika mkono wake mwingine ananyanyua na kushusha”.
[Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili Al-Bukhari na Muslim]
4- Na Kutoka kwa Abuu Dharri -Radhi za Allah ziwe juu- yake alisema: Aliona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mbuzi wawili wakipigana kwa pembe zao, akasema: "Hivi unajua ni kwa sababu gani wanapigana ewe Abuu Dhari?", Nikasema: Hapana, Akasema: "Lakini Mwenyezi Mungu anajua na atakwenda kuwahukumu kati yao".
[Kaipokea Ahmad]
5- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alisoma Aya hii “Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mtekeleze kufikisha amana kwa watu wake" mpaka katika kauli yake:
}إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَنْ تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَى أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُمْ بَيْنَ النَّاسِ أَنْ تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ إِنَّ اللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُمْ بِهِ إِنَّ اللَّهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا{(النساء-58)
"Hakika Mwenyezi Mungu ni msikivu na mwingi wa kuona" [An Nisaa: 58]
akawa anaweka vidole gumba vyake juu ya masikio yake na kidole kinachofuata dole gumba akakiweka kuliani kwake”.
[Kaipokea Abuudaudi na bin Hibban na bin Abii Haatim]
6- Na imepokelewa kutoka kwa bin omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- amesema: "Funguo za mambo ya ghaibu (yaliyofichikana) ni tano, hakuna azijuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu: Hakuna ajuaye yaliyoko siku ya kesho isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wala hakuna ajuaye yaliyofichwa na fuko za uzazi isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna mtu anajua ni lini mvua itanyesha isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna nafsi inajua itafia ardhi gani isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna ajuaye ni lini kitasimama Kiyama isipokuwa Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka".
[Ameipokea Bukhari na Muslim]
7- Na kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: "Mwenyezi Mungu anapata furaha kubwa kwa toba ya mja wake wakati anapotubia kwake, [furaha kubwa] kuliko furaha ya mmoja wenu aliyekuwa katika kipando chake katika ardhi ya jangwa kikamtoroka huku kikiwa kimebeba chakula chake na maji yake, akakitafuta mpaka akakikatia tamaa, akaenda chini ya mti akajiegemeza katika kivuli chake huku akiwa kakikatia tamaa kipando chake, wakati akiwa katika hali hiyo mara ghafla anakiona kimesimama mbele yake, basi akashika kamba yake na akasema kwa furaha kubwa: Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni mja wangu na mimi ni mola wako, kakosea kutokana na furaha kubwa".
[Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili]
8- Na kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake usiku ili atubie aliyekosea mchana, na ananyoosha mkono wake mchana ili atubie aliyekosea usiku, mpaka jua lichomoze kutokea magharibi yake".
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
9- Na imepokelewa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: "Walikuja kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- mateka wa kabila la Hawazini; ghafla mwanamke mmoja miongoni mwa mateka akaenda mbio pale alipoona kuna mtoto mdogo ndani ya mateka, akamchukua na akampakata tumboni kwake akamnyonyesha, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Je mmeona mwanamke huyu kamtupa mwanaye motoni?!" Tukasema: Hapana Wallah! Akasema: "Basi Mwenyezi Mungu anahuruma kwa waja wake zaidi kuliko mwanamke huyu kwa mtoto wake".
10- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Alipoumba Mwenyezi Mungu viumbe aliandika katika kitabu, kiko kwake juu ya Arshi: Hakika huruma yangu inazidi hasira yangu".
[Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
11- Na kutoka kwao wawili (Bukhari na Muslim) Yakwamba Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Allah ameigawanya rehema katika mafungu mia moja, akachukuwa mafungu ya rehema Tisini na tisa (99), akateremsha ardhini fungu moja la huruma (1), kupitia fungu hilo ndio viumbe wanahurumiana, mpaka mnyama ananyanyua mguu wake akichelea asimkanyage mtoto wake"
12- Na kwa Muslim imekuja maana ya hadithi kama hii, na ni miongoni mwa hadithi za Salman, na ndani ya hadithi hiyo kumeelezwa: "Kila rehema inatabaka lake kati ya Mbingu na Ardhi" na pia "Itakapofika siku ya kiyama ataikamilisha kwa rehema hii".
13- Na kutoka kwa Anas -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Hakika kafiri anapofanya jema hulishwa kupitia jema hilo chakula duniani, ama muumini hakika Mwenyezi Mungu humtunzia mema yake akhera, na humrejeshea riziki katika dunia kwa sababu ya utiifu wake".
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
14- Na amepokea pia hadithi marfu'u: "Hakika Mwenyezi Mungu huridhika kwa mja anapokula chochote, akamshukuru juu ya hicho, au akanywa chochote akamshukuru juu ya hicho".
15- Na kutoka kwa Abuu Dhari -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Imelalamika kwa sauti mbingu na ni haki ipige kelele, kwani hakuna sehemu ya kuweka vidole vinne isipokuwa kuna Malaika akiwa ameweka paji lake la uso chini akimsujudia Mwenyezi Mungu Mtukufu, Wallahi -Namuapa Mwenyezi Mungu lau kama mngejua yale ninayoyajua basi mngecheka kidogo na mngelia sana, na wala msinge starehe na wanawake vitandani, na mngetoka mabarabarani mkinyanyua sauti kwa kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu."
[Kaipokea Tirmidhiy na akasema: Hadithi ni Hasan.]
16- Na kwa Muslim kutoka kwa Jundubi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Mtu mmoja alisema: Wallahi Mwenyezi Mungu hatomsamehe fulani, akasema Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka: Ni nani huyo anayepata ujasiri wa kuapia juu yangu kuwa sitomsamehe fulani? Basi mimi nimemsamehe na nimeporomosha matendo yako."
17- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi mar'fuu: "Laiti angelijua muumini yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa adhabu, hakuna mtu angetamani pepo yake, na laiti kafiri angelijua yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa huruma basi asingekata tamaa yeyote na pepo yake".
[Na amepokea Imamu Bukhari]
18- kutoka kwa bin Mas'udi Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: amesema Mtume Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Pepo iko karibu na mmoja wenu kuliko hata kisigino cha kiatu chake, na moto mfano huo huo".
19- Na kutoka kwa Abuu Hurayra -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi mar'fuu: "Hakika mwanamke malaya siku moja aliona mbwa wakati wa joto kali akizunguka kisimani ulimi wake ukiwa umetoka nje kwa sababu ya kiu, akamvulia kiatu hapo kisimani akamnywesha akasamehewa kwa sababu kitendo hicho".
20- Na akasema: "Aliingia motoni mwanamke mmoja kwa sababu ya paka alimfunga; wala hakumlisha, na wala hakumfungulia ili ale katika masalia ya ardhi".
Amesema Zuhri : “hii ni kuwa asibweteka yeyote na wala asikate tamaa yeyote”.
[ Wameitoa hadithi hii Maimamu wawili]
21- Na kutoka kwake hadithi marfuu: "Anawastaajabu Mola wetu watu ambao wanasukumwa kwenda peponi".
[Ameipokea Ahmad na Al-Bukhari]
22- Na kutoka kwa Abuu Musa Al Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Na wala hakuna yeyote mwenye subira kubwa kwa maudhi anayoyasikia kuliko Mwenyezi Mungu; wanamsingizia kuwa anamtoto kisha anawapa afya na anawaruzuku".
[ Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
23- Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka anapompenda mja hunadi kwa sauti: Ewe Jibrili! Hakika Mwenyezi Mungu anampenda fulani basi mpende, basi Jibrili humpenda, kisha Jibrili ananadi mbinguni: Hakika Mwenyezi Mungu anampenda fulani basi mpendeni, basi wanampenda walioko mbinguni, na anawekewa kukubalika katika ardhi".
24- Na kutoka kwa Jariri bin Abdillahi Al Bajali -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa tumekaa kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- ghafla akatazama katika mwezi usiku wa katikati ya mwezi akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnvyouona mwezi huu, hamtosukumana katika kumuona kwake, ikiwa mtaweza kuwa msishindwe kuswali kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" kisha akasoma:
}فَاصْبِرْ عَلَى مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا وَمِنْ آنَاءِ اللَّيْلِ فَسَبِّحْ وَأَطْرَافَ النَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرْضَى{(طه-130)
"Na utakase sifa za Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake" [Twaha: 130].
[Imepokewa na Al-Bukhari, Muslim, Abu Dawud, An-Nasa’i, At-Tirmidhiy, Ibn Majah, na Ahmad.]
25- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, Na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi, na hakuna budi kwake hilo".
[Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
26- Na kutoka kwae (Bukhari) Yakwamba Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Huteremka Mola wetu aliyetakasika na kutukuka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho anasema: Nani mwenye kuniita, nimjibu, nani mwenye kuniomba nimpe, nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe".
[Wamekubaliana Bukhari na Muslim]
27- Na kutoka kwa Abuu Musa Al Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Pepo mbili zimejengwa kutokana na dhahabu na vyombo vyake ni vya dhahabu, na pepo mbili ni za fedha na vyombo vyake ni vya fedha, kizuizi kilichopo baina ya watu wa peponi na kumuona Allah ni shuka la kiburi lililopo usoni kwake.
[Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
28- kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alinihadithia mimi mtu mmoja katika maswahaba wa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- katika watu wa Madina (Maanswari) yakwamba wao wakiwa wamekaa usika pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- ghafla ikarushwa nyota pakaangaza, akasema: "Mlikuwa mkisema nini kukirushwa mfano wa kitu kama hiki?". Wakasema: Tulikuwa tukisema (zama za kabla ya uislamu): usiku wa leo kazaliwa mtu mtukufu au kafa mtukufu. Akasema: "Hakika haikurushwa kwa kifo cha yeyote wala uhai wake, lakini Mola wetu aliyetakasika na kutukuka anapohukumu jambo humtukuza Malaika wanaobeba Arshi, mpaka wanamsabihi (wanamtukuza) Malaika wa mbingu wanaowafuatia, mpaka zinawafikia tasbihi Malaika wa mbingu ya dunia, husema wale walioko katika mbingu inayofuatana na mbingu ya Malaika wabeba Arshi: Nini amesema Mola wenu? Wanawaeleza nini amesema, basi wanaanza kuelezana Malaika wa mbingu zote baadhi yao kwa baadhi, mpaka zinawafikia habari Malaika wa mbingu ya dunia hapo majini huiba kusikia habari hizo na kuzileta kwa vipenzi vyao, habari watakayo kuja nayo kama ilivyo basi hiyo huwa ya kweli, lakini wao huongopa na huzidisha (uongo)".
[ Imepokelewa na Muslim na Tirmidhiy na Nasaai.]
29- Na kutoka kwa Nawwasi bin Samaan -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Anapotaka Mwenyezi Mungu kutoa wahyi wa jambo huzungumza kwa wahyi, hapo mbingu huanza kutetemeka, au alisema: hupata mtikisiko mkubwa, kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka, wanaposikia hivyo viumbe walioko mbinguni huzimia, au alisema: huporomoka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wakimsujudia, anakuwa wa mwanzo kunyanyua kichwa chake ni Jibrili -Amani iwe juu yake-, hapo Mwenyezi Mungu humsemesha katika wahyi wake kwa kile anachokitaka, kisha anapita Jibrili kwa Malaika, kila anapopita katika mbingu wanamuuliza Malaika wake: Amesema nini Mola wetu ewe Jibrili? Husema: Amesema kweli naye ni mtukufu na mkubwa, hapo wote husema kama alivyosema Jibrili, hapo huenda Jibrili na wahyi mpaka mahala alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu".
[Kaipokea bin Jariri na bin Khuzaima na Twabaraani na bin Abii Haatim na lafudhi ni ya kwake]
30- Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"
[kaipokea Bukhari]
31- Na imepokelewa kutoka kwa bin omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu atazikamata ardhi zote siku ya kiyama na mbingu zote zitakuwa katika mkono wake wa kulia, kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme".
32- Na katika riwaya nyingine kutoka kwake "Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alisoma Aya hii siku moja akiwa juu ya mimbari: "Na hawa washirikina hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu vile anavyostahiki kuadhimishwa, kwa kuwa wamemuabudu asiyekuwa yeye pamoja na yeye miongoni mwa wale wasionufaisha wala kudhuru, wakamfanya muumbwa, pamoja na uelemevu wake, kuwa ni sawa na Muumba Mtukufu, Ambaye kutokana na uweza wake mkubwa ni kwamba ardhi yote itakuwa iko mkononi mwake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa kwa mkono wake wa kulia. Ametakasika Mwenyezi Mungu na kutukuka kwa kuepukana na kile wanachomshirikisha nacho hao washirikina. Katika Aya hii pana dalili ya kuthibitisha kushika kwa mkono, mkono wa kulia na kukunja kwa Mwenyezi Mungu kama vile inavyolingana na haiba yake na utukufu wake bila kueleza yuko vipi wala kufananisha". Na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema hivi kwa vidole vyake, akivitikisa na huku akivigeuza mbele na nyuma: "Anajitukuza Mwenyezi Mungu mwenyewe nafsi yake, mimi ndiye Jabari mwenye kiburi, mimi ndiye mwenye nguvu, mimi ndiye mkarimu" Ikamtikisa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mimba mpaka tukasema hakika itamuangusha".
[Kaipokea Ahmad]
33- Na kaipokea Muslim kutoka kwa Abdillahi bin Muksimu, yakwamba yeye alitazama kwa Abdillahi bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao yeye na baba yake- ni jinsi gani alivyokuwa akielezea kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Atachukua Mwenyezi Mungu mbingu zake na ardhi zake kwa mikono yake kisha atazikamata, atasema: Mimi ndiye Mfalme, na atakunja vidole vyake na atavikunjua na atasema: Mimi ndiye Mfalme" Mpaka nikatazama katika mimbari nikaiona ikitikisika kiasi kidogo kutoka chini, mpaka mimi nikasema: itamdondosha hii Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake?!".
34- Na katika sahihi Bukhari na Muslim, kutoka kwa Imran bin Huswain -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Pokeeni bishara njema enyi kabila la bani Tamim".
Wakasema: Umetueleza habari njema basi tupe.
Akasema: pokeeni bishara njema enyi watu wa Yemen".
Wakasema: Tumekubali basi tueleze mwanzo wa jambo hili.
Akasema: "Alikuwa Mwenyezi Mungu kabla ya kila kitu na Arshi yake ilikuwa juu ya maji, na akaandika katika ubao uliohifadhiwa (Lauhul Mahfudh) kumbukumbu za kila kitu".
Akasema: Akanijia mtu mmoja akasema: Ewe Imran! Ngamia wako amefungua kamba yake.
Akasema: Nikaondoka nikiifuatilia sikujua ni nini kiliendelea baada ya kuondoka".
35- Na kutoka kwa Jubairi bin Muhammad bin Jubairi bin Mutw'im kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: “Alikuja mtu wakijijini kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nafsi zimetaabika, na familia zimetawanyika, na mali zimepungua, na wanyama wamekufa, tuombee mvua sisi kwa Mola wako, kwani sisi tunaomba utetezi kupitia wewe kwa Mwenyezi Mungu na kupitia kwa Mwenyezi Mungu juu yako. Akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- "Koma, unajua unachokisema?, Na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akamsabihi Mwenyezi Mungu (akasema: Sub-haanallaah) akaendelea kumsabihi mpaka likajulikana hilo kwa maswahaba zake, kisha akasema: "Ole wako, hakika haombi utetezi kupitia Mwenyezi Mungu juu ya yeyote katika viumbe vyake, jambo la Mwenyezi Mungu ni kubwa kuliko hilo, koma, hivi unamjua ni nani Mwenyezi Mungu? Hakika Arshi yake juu ya mbingu zake imekaa hivi, akaashiria kwa vidole vyake mfano wa kuba iliyoko juu yake, na hakika huzielemea kwa uzito mfano wa kuelemewa kwa kipando kinapombeba mtu".
[Kaipokea Ahmad na Abuu daud]
36- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Amesema Mwenyezi Mungu: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo, na ama kunipinga kwake ni kauli yake: Mwenyezi Mungu hatonirudisha kuwa hai, kama alivyonianzisha, na si kuanza kuumba ni kwepesi zaidi kwangu kuliko kurudisha, na kunitukana kwake ni kauli yake: kuwa Mwenyezi Mungu kajifanyia mwana, na mimi ndiye mmoja mwenye kukusudiwa, sikuzaa wala sikuzaliwa, na wala hakuna anayefanana nami hata mmoja".
37- Na katika riwaya ya bin Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao yeye na baba yake-: "Na ama kunitukana kwake mimi ni kauli yake: nina mtoto, na nimetakasika na kujifanyia mpenzi au mtoto".
[Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
38- Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- “Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ananiudhi mimi mwanadamu, anatukana nyakati na mimi ndiye nyakati, ninaugeuza usiku na mchana”.
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
}إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُمْ مِنَّا الْحُسْنَى أُولَئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ{(الأنبياء-101)
"Hakika wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo" [Al Anbiyaa: 101].
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}مَا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّهُ لَهُ سُنَّةَ اللَّهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلُ وَكَانَ أَمْرُ اللَّهِ قَدَرًا مَقْدُورًا{(الأحزاب-38)
"Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyokwisha kadiriwa" [Ahzab: 38].
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ{(الصافات-96)
"Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni na hayo mnayoyafanya". [Asswaafat: 96].
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ{(القمر-49)
"Hakika sisi kila kitu tumekiumba kwa kipimo tulichokikadiria na kukipitisha, na ilitangulia elimu yetu ya kukijua kitu hicho na kukiandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa". [Al- qamar: 49]
39- Na katika sahihi Muslim, kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu alikadiria makadirio ya viumbe kabla hajaumba mbingu na ardhi kwa miaka elfu hamsini, akasema: na Arshi yake ikiwa juu ya maji".
40- Na kutoka kwa Ally bin Abi Twalib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: "Hakuna yeyote isipokuwa ameandikiwa makazi yake motoni na makazi yake peponi" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! kwanini tusikae kusubiri tulichopangiwa na tuache kufanya matendo?! Akasema: "Fanyeni matendo kwani kila jepesi hupatikana kwa sababu zake ziliumbwa na kuwekwa ziwe za kheri au za shari, atakayekuwa miongoni mwa watu wema Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi wa kufanya matendo ya watu wema, na atakayekuwa ni katika watu waovu naye Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi wa kufanya matendo ya watu waovu. kisha akasoma:
}فَأَمَّا مَنْ أَعْطَى وَاتَّقَى (5) وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَى (6) فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَى (7) وَأَمَّا مَنْ بَخِلَ وَاسْتَغْنَى (8){(الليل-5_8)
"Basi, ama mwenye kutoa na akamchamungu* "Na akaliafiki lilojema* "Tutamsahilishia yawe mepesi" [Lail: 5-8]
[Wamekubaliana Bukhari na Muslim]
41- Na kutoka kwa Muslim bin Yasari Al Juhaniy Amesema: “Aliulizwa Omari bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuhusu Aya hii:
}وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنْ بَنِي آدَمَ مِنْ ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنْفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ قَالُوا بَلَى شَهِدْنَا أَنْ تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ{(الأعراف-172)
"Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Alipowatoa wana wa Ādam kutoka kwenye migongo ya baba zao." [Al Araf: 172] Akasema Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Nilimsikia Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake aliulizwa kuhusu hilo, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kisha akafuta mgongo wake kwa mkono wake wa kulia, akatoa katika mgongo huo kizazi, akasema: Nimewaumba hawa kwa ajili ya kuingia peponi na matendo ya watu wa peponi ndiyo watakayoyafanya, kisha akafuta mgongo wake akatoa humo kizazi, akasema: Nimewaumba hawa kwa ajili ya moto na kwa matendo ya watu wa motoni ndiyo watakayoyafanya" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu yanini kufanya matendo? Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu akimuumba mja kwa ajili ya pepo humshughulisha kwa matendo ya watu wa peponi mpaka anakufa katika amali miongoni mwa amali za watu wa peponi, akamuingiza peponi kwa matendo hayo, na anapomuumba mja kwa ajili ya moto, humshughulisha na matendo ya watu wa motoni mpaka anakufa katika amali miongoni mwa amali za watu wa motoni anamuingiza motoni".
[Kaipokea Maliki na Hakim na akasema: Iko katika sharti za Muslim]
Na kaipokea Abuudaudi kwa njia nyingine kutoka kwa Muslim bin Yasar kutoka kwa Nuaim bin Rabi'a kutoka kwa Omari.
42- Na amesema Is-haka bin Rahawaihi: Alituhadithia Bakia bin Walidi, Akasema: Alinieleza Zubaidi Muhammadi bin Walidi kutoka kwa Rashidi bin Sa'di kutoka kwa Abdulrahman bin Abii katada kutoka kwa baba yake kutoka kwa Hisham bin Hakim bin Hizami :”Yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi matendo huanza kufanyika kutoka kwa mtu mwenyewe au tayari yalikwisha pangiliwa? Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu alipotoa kizazi cha Adam mgongoni mwake aliwataka washuhudilie nafsi zao, kisha akawajaza katika viganja vyake, akasema: Hawa ni wa peponi na hawa ni wa motoni, watu wa peponi hufanywa kuwa wepesi kufanya matendo ya watu wa peponi, na watu wa motoni hufanywa kuwa wepesi kufanya matendo ya watu wa motoni".
43- Kutoka kwa Abdillah bin Masudi-Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Alituhadithia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-naye ni mkweli mwenye kusadikiwa: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake katika tumbo la mama yake siku arobaini ni tone la Manii, kisha linakuwa pande la damu mfano huo, kisha linakuwa pande nyama mfano huo (siku Arobaini), kisha Mwenyezi Mungu analitumia Malaika akiwa na maneno manne: Anaandika matendo yake, na ajali yake, na riziki yake, na mwema au muovu, kisha analipulizia roho. Namuapa yule ambaye hakuna Mola zaidi yake, hakika mmoja wenu atafanya matendo ya watu wa peponi mpaka ikawa hakuna kati yake na pepo isipokuwa dhiraa (futi) moja, kikamtangulia kitabu, akajikuta anafanya matendo ya watu wa motoni na akauingia; na hakika mmoja wenu anaweza kufanya matendo ya watu motoni mpaka ikawa hakuna kati yake na moto isipokuwa dhiraa (futi) moja, kikamtangulia kitabu akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia".
[ Wamekubaliana Bukhari na Muslim]
44- Na kutoka kwa Hudhaifa bin Usaid -Radhi za Allah ziwe juu yake- imemfikia kuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Huingia Malaika katika tone la Manii baada yakuwa limetulia katika mfuko wa uzazi kwa muda wa siku Arobaini au arobaini na tano, husema: Ewe Mola ni mwema au muovu? Basi huandika, kisha anasema: Ewe Mola ni wa kiume au wa kike? Basi wanaandika, na anaandika matendo yake na nyenendo zake na ajali yake na riziki yake, kisha kurasa zinafungwa hakiongezwi kitu wala hakipunguzwi".
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
45- Na katika sahihi Muslim kutoka kwa Aisha Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Aliitwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika jeneza la mtoto mdogo katika maanswari (watu wa Madina), nikasema hongera kwake, ndege miongoni mwa ndege wa peponi hajafanya dhambi lolote wala halijamfikia dhambi, akasema: "Kuna zaidi ya hilo ewe Aisha! Hakika Mwenyezi Mungu ameiumbia pepo watu wake amewaumba kwa ajili yake nao wakiwa katika migongo ya baba zao, na akauumbia moto watu wake akawaumba kwa ajili yake nao wakiwa katika migongo ya baba zao".
46- Na kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Kila kitu kimekadiriwa hata uvivu na uchangamfu".
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
47- Na kutoka kwa Katada -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- katika kauli yake Mtukufu:
} تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ مِنْ كُلِّ أَمْرٍ{(القدر-4)
"Huteremka Malaika na roho miongoni mwao (Jibril) kwa idhini ya Mola wao mlezi na kila jambo" [Al Kadri: 4]. Akasema: "Hupitishwa ndani yake yote yanayokuwa ndani ya mwaka mpaka mwaka mwingine mfano wake"
[kaipokea Abdulrazzaq na bin Jariri]
Na imepokelewa kwa maana kama hiyo kutoka kwa bin Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Na Hasan na bin Abii Abdulrahman Assulami na saidi bin Jubairi na Muqaatil.
48- Na kutoka kwa bin Abbas- Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu aliumba ubao uliohifadhiwa (Lauhul Mahfudh) kwa madini meupe, kurasa zake zimetokana na madini mekundu ya yakuti, kalamu yake ni nuru, upana wake ni kama ulioko katika mbingu na ardhi, hutazama hapo mara mia tatu na sitini kwa siku, katika mtazamo mmoja kati ya hiyo anaumba na kuruzuku, na anahuisha na kufisha na anapandisha daraja na anadhalilisha na anafanya ayatakayo, na hii ndio kauli yake Mtukufu:
}يَسْأَلُهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ{(الرحمان-29)
"Siku zote yeye yuko katika jambo" [Al Rahman: 29].
[ Kaipokea Abdurrazzaq na bin Mundhiri na Twabaraniy na Hakim]
Na amesema bunul Qayyim -Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu- zilipotajwa hadithi hizi na zenye maana kama hii, akasema: "Haya ni makadirio ya kila siku, na yale yaliyo kabla yake ni makadirio ya mwaka, na yaliyo kabla yake ni makadirio ya umri mzima wakati nafsi inapoambatana nayo, na yale yaliyo kabla yake vile vile ni wakati wa mwanzo wa kuumba kwake na muda ambao kiumbe kinakuwa ni mudhgha (pande la nyama), na yaliyo kabla yake ni makadirio yaliyotangulia kuwepo kwa hayo lakini ni baada ya kuumba mbingu na ardhi, na yaliyo kabla yake ni makadirio yaliyotangulia kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi kwa miaka elfu hamsini, na kila moja katika makadirio haya ni sawa na ufafanuzi wa makadirio yaliyotangulia".
Na katika hilo kuna ushahidi juu ya ukamilifu wa elimu ya Mola na kudra zake na hekima zake, na ziada ya kuwaelimisha kwake Malaika na waja wake waumini kuhusu nafsi yake na majini yake.
Kisha akasema: Zikaafikiana hadithi hizi na mfano wake yakuwa kadari iliyotangulia kuelezwa haizuii kufanya matendo na wala haipelekei kubweteka na kuacha kufanya, bali inawajibisha kufanya bidii na jitihada. Na kwa sababu hii walipolisikia hilo baadhi ya maswahaba wakasema: Sikua najitihada kubwa zaidi awali kuliko hivi sasa.
Na alisema Abuu Othman An nahdi kumwambia Salman: Kwangu mimi sinafuraha sana na jambo hili kuliko la mwisho wake.
Kwa sababu ikiwa imekwisha tangulia kwake kutoka kwa Mwenyezi Mungu tangu zamani, na Allah akamuandaa na akamfanyia wepesi wa kulifikia basi itakuwa furaha yake ni kwa lile lililotangulia ambalo limepitia kwa Mwenyezi Mungu ndio kubwa zaidi kuliko kufurahia kwake sababu ambazo zinakuja baada yake.
49- Na kutoka kwa Walidi bin Ubada amesema: “Niliingia kwa baba yangu naye akiwa mgonjwa nikimdhania kuwa huenda atakufa, nikasema: Ewe baba yangu niusie na ujitahidi kunipa nasaha, Akasema: Nikalisheni; walipomkalisha akasema: Ewe mwanangu hakika wewe hutopata ladha ya imani na wala hutofikia uhalisia wa elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka uamini makadirio, mazuri yake na mabaya yake, nikasema: ewe baba yangu, nitawezaje kujua ni yapi mazuri yake na mabaya yake? Akasema: ujue kuwa yaliyokukosa hayakuwa ni yenye kukupata, na yaliyokupata hayakuwa ni yenye kukukosa, ewe mwanagu hakika mimi nilimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Cha mwanzo alichoumba Mwenyezi Mungu ni kalamu akasema: Andika, yakapita katika saa ile mambo ambayo yatatokea mpaka siku ya kiyama." Ewe mwanangu hakika ukifa na ukawa hauko juu ya hilo (hujashikamana na hilo) utaingia motoni}.
[Kaipokea Ahmad.]
50- Na kutoka kwa Abuu khizama kutoka kwa baba yake -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: {Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hebu tueleze tiba za asili tunazojitibia na dawa tunazotumia na tahadhari tunazochukua je zinazuia chochote katika kadari ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Hizo pia ni katika kadari za Mwenyezi Mungu}
[Ameipokea Ahmad na Tirmidhiy na akaifanya kuwa hadithi Hasan]
51- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningefanya kadha basi ingelikuwa kadha na kadha, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" linafungua matendo ya shetani".
[ Imepokelewa na Imamu Muslim]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
}لَيْسَ الْبِرَّ أَنْ تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَى حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ أُولَئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ{(البقرة-177)
"Hapana kheri, mbele ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka, kuelekea kwenye Swala upande wa Mashariki na Magharibi, iwapo hilo halitokamani na amri ya Mwenyezi Mungu na sheria yake. Hakika kheri yote iko katika imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na akamkubali kuwa ndiye muabudiwa, peke yake, Hana mshirika wake, na akaiamini Siku ya kufufuliwa na Malipo, na akawaamini Malaika wote na vitabu vyote vilivyoteremshwa, na Mitume wote bila kubagua" Mpaka mwisho wa Aya. [Al Baqara: 177].
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنْتُمْ تُوعَدُونَ{(فصلت-30)
"Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa". [Fusswilat: 30]
} لَنْ يَسْتَنْكِفَ الْمَسِيحُ أَنْ يَكُونَ عَبْدًا لِلَّهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ وَمَنْ يَسْتَنْكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا{(النساء-172)
Na kauli ya Allah Mtukufu: "Kamwe, hawezi kufanya kiburi Masihi kuwa mja wa Mwenyezi Mungu na wala Malaika waliokaribu" [An nisaa: 172].
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}وَلَهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَنْ عِنْدَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ (19) يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ (20){(الأنبياء-19_20)
{Na ni vyake vyote vilivyomo Mbinguni na Ardhini, na wale walioko kwake (Malaika) hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu na wala hawachoki. (19) "Wanamtakasa usiku na mchana wala hawanyong'onyei" [Al Anbiyaa: 19,20]
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}الْحَمْدُ لِلَّهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَثْنَى وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ{(فاطر-1)
"Aliyewafanya Malaika kuwa ni wajumbe wenye mabawa mawili na matatu na manne" Mpaka mwisho wa Aya. [Faatwir 1]
Na kauli ya Allah Mtukufu:
} الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ{(غافر-7)
"Wale wanaobeba Arshi, na wanaoizunguka wanamtakasa na kumuhimidi Mola wao na wanamuamini na wanawaombea msamaha walioamini." Mpaka mwisho wa Aya. [Ghafiri: 7]
52- Na kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Wameumbwa Malaika kutokana na Nuru, na wameumbwa majini kutokana na muwako wa moto, na ameumbwa Adam kwa kile mlichoelezwa"
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
53- {Na imethibiti katika baadhi ya hadithi za safari ya miraji yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Ilinyanyuliwa ikaletwa kwake nyumba iliyoimarishwa (Baitul Ma'muru) ambayo iko katika mbingu ya saba, na inasemekana: iko mbingu ya sita usawa wa Al'kaba katika Ardhi, nayo kulinganishwa kwake na Alka'ba utukufu wake mbinguni ni kama utukufu wa Alka'ba Ardhini, ghafla akaona wanaingia ndani yake kila siku Malaika elfu sabini kisha hawarudi mpaka mwisho wao}.
54- Na kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- {Hakuna mahala mbinguni pa kuweka mguu mmoja isipokuwa kuna Malaika ima amesujudu au amesimama, na hiyo ndiyo kauli ya Malaika}:
}وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ (165) وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ (166){(الصافات-165-166)
{Na hakika sisi tumepanga safu (165) "Na hakika sisi tunamtukuza Mwenyezi Mungu(166) } [Al swaaffati: 165-166].
[Kaipokea Muhammadi bin Nasiri bin Abii Haatim na bin Jariiri na Abuu sheikh]
55- Na amepokea Twabarani kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Hakuna katika mbingu saba nafasi ya kuweka mguu wala shibri moja (nusu futi) wala kiganja, isipokuwa kuna Malaika amesimama au Malaika amerukuu, itakapofika siku ya kiyama watasema wote: Umetakasika wewe hatukukuabudu upasavyo kuabudiwa! Isipokuwa sisi hatukukushirikisha wewe na chochote".
56- Na kutoka kwa Jabiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Nilipewa idhini ya kuuelezea kuhusu Malaika miongoni mwa Malaika wa Mwenyezi Mungu katika wale wanaobeba Arshi, umbali ulioko baina ya nyama ya sikio lake mpaka mabega yake ni mwendo wa kutembea miaka mia saba".
[Kaipokea Abuudaudi na Baihaqi katika "Al Asmaau wasswifaat" na Dhiyaa katika "Al Mukhtara"]
Hivyo miongoni mwa watukufu wao ni Jibrili Amani iwe juu yake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu kamsifia kwa uaminifu na tabia nzuri na nguvu,
akasema Mtukufu:
} عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَى (5) ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَى (6){(النجم-5_6)
"Amemfundisha Malaika mwenye nguvu kabisa" "Mwenye kutua akatulia". [Al Najmi: 5,6].
Na miongoni mwa nguvu zake nyingi nikuwa yeye aliinyanyua miji ya watu wa Lutu -Amani iwe juu yake- na ilikuwa ni miji saba- na wote waliomo miongoni mwa umma na walikuwa takribani laki nne (400,000), na vyote walivyo navyo miongoni mwa wanyama na mifugo, vyote pamoja na ardhi ya miji hiyo na majengo yote; kwa ncha ya ubawa wake, mpaka akawafikisha katika kilele cha mbingu, mpaka Malaika wakasikia mibweko ya mbwa wao, kisha miji yote akaigeuza akafanya juu yake kuwa chini yake.
Huyu ndiye mwenye nguvu nyingi. Na kauli yake: Mwenye kutua, yaani: mwenye tabia nzuri haiba nzuri na nguvu nyingi.
Na amesema maana hii Ibn Abasi Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Na akasema mwingine: mwenye kutua, yaani: mwenye nguvu
. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kueleza sifa zake:
}إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ (19) ذِي قُوَّةٍ عِنْدَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ (20) مُطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ (21){(التكوير-19_21)
"Hakika hiyo ni kauli ya mtume mtukufu" (19) Mwenye nguvu katika kuyapitisha yale anayoamrishwa. Mwenye cheo cha juu kwa Mwenyezi Mungu. Anayesikilizwa na Malaika. "Anayeaminiwa juu ya Wahyi anaoteremka nao". [Attakwir: 19-21] Yaani: Ana nguvu na ushupavu, ni mkali na ananafasi na cheo cha juu na heshima kubwa kwa mwenye Arshi "Anayeaminiwa juu ya wahyi anaoteremshiwa" Yaani: mwenye kutiiwa kwa walioko juu mwaminifu uaminifu mkubwa, na ndio maana akawa yeye ndiye balozi baina ya Mwenyezi Mungu na mitume wake.
57- Na alikuwa akija kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kwa sifa tofauti tofauti, na aliwahi kumuona kwa sifa yake ambayo Mwenyezi Mungu kamuumba nayo mara mbili, na ana mbawa mia sita. Ameipokea Imam Bukhari Kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-.
58- Na amepokea Imamu Ahmad kutoka kwa Abdallah amesema: "Alimuona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Jibrili katika sura yake, ana mbawa mia sita, kila ubawa miongoni mwa mbawa hizo umeziba anga, kunadondoka kutoka katika mbawa zake madini yanayomeremeta na lulu na yakuti ambavyo hakuna avijuaye zaidi ya Mwenyezi Mungu".
[ Isnadi yake inanguvu]
59- Na kutoka kwa Abdillahi bin Mas'ud -Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Alimuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake Jibrili akiwa katika pambo la kijani akiwa amejaza nafasi iliyoko kati mbingu na ardhi"
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
60-Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- amesema: "Nilimuona jibrili akiteremka akiwa kajaza pande zote katika anga mbili akiwa kavaa nguo ya hariri ikiwa imewekewa madini ya Lulu na Yakuti".
[Imepokelewa na Abuu Sheikh]
61- Na imepokelewa na bin Jariri kutoka kwa bin Abbasi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake, amesema: Jibrili ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mikaeli ni mja wa Mwenyezi Mungu na kila jina ambalo ndani yake kuna neno {il} basi hilo maana yake ni mja wa Mwenyezi Mungu.
62- Na amepokea pia kutoka kwa Ally bin Hasan mfano wake, na akaongeza: na Israfili ni mja wa Rahman (mwingi wa rehema)
63- Na amepokea Twabaraniyu kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Je nisikuhabarisheni mbora wa Malaika? Ni Jibraeli".
64- Na kutoka kwa Abii Imrani Al jauni yakwamba yeye ilimfikia kuwa Jibrili alikuja kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akiwa analia, Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Nini kinakuliza?". Akasema: "Na nina nini mimi mpaka nisilie, namuapa Mwenyezi Mungu hayajawahi kukauka macho yangu tangu Mwenyezi Mungu alipoumba moto, kwa kuhofia nisije kumuasi akanitupa ndani yake".
[Kaipokea Imamu Ahmadi katika "Azzuhudi"]
65- Na amepokea Bukhari kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Alisema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kumwambia Jibrili: "kwanini hututembelei zaidi ya jinsi unavyotutembelea?" Ikateremka:
}وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَلِكَ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا{(مريم-64)
"Na wala hatuteremki ila kwa amri ya Mola wako mlezi, ni yake yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu" Mpaka mwisho wa Aya. [Mariam: 64].
Na katika watukufu wao ni Mikaeli -Amani iwe juu yake-, naye kapewa jukumu la matone (mvua) na mimea.
66- Na amepokea imamu Ahmadi kutoka kwa Anasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- alisema kumwambia Jibrili: "Kwanini sijawahi kumuona Mikaeli akicheka katu? Akasema: Hajawahi kucheka Mikaeli tangu ulipoumbwa moto"
Na miongoni mwa watukufu wao ni Israfili -Amani iwe juu yake, Naye ni mmoja katika Malaika wabeba Arshi naye ndiye atakayepuliza Baragumu.
67- Amepokea Tirmidhi -na akaifanya kuwa hadithi Hasan- Na Imamu Hakim kutoka kwa Abuu Saidi Al khudriy- Radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Nitastarehe vipi hali yakuwa mwenye Baragumu kaliweka mdomoni na uso wake umeinama na ametega sikio lake anasubiri ni wakati gani ataamrishwa ili apulize?". Wakasema: Tuseme nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Semeni: Anatutosha Mwenyezi Mungu na ndiye msimamizi bora, kwa Mwenyezi Mungu ndiko tuliko tegemea".
68- Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- amesema: "Hakika Malaika mmoja miongoni mwa wanaobeba Arshi aitwaye Israfili, yuko katika kona miongoni mwa kona za Arshi katika nguzo yake, zimetokeza nyayo zake chini katika ardhi ya saba, na kimetokeza kichwa chake juu katika mbingu ya saba"
[Kaipokea Abuu Sheikh na Abuu Nuaim katika "Hilya".]
69- Na amepokea Abuu sheikh kutoka kwa Auzai amesema: Hakuna yeyote katika viumbe wa Mwenyezi Mungu mwenye sauti nzuri kuliko Israfili, akianza kumtakasa Mwenyezi Mungu anawakatisha Malaika walioko mbingu ya saba swala zao na tasbihi zao.
Na miongoni mwa watukufu wao ni Malaika wa kifo -Amani iwe juu yake-: Na wala halikutajwa jina lake wazi ndani ya Qur'ani wala hadithi sahihi, na imekuja katika baadhi ya nukuu jina la Izraeli, Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi amelisema hilo Mwanachuoni bin Kathiri. Na akasema: Hakika wao kwa mujibu wa yale aliyowaandalia wana migawanyiko ya majukumu: Wako miongoni mwao wanaobeba Arshi. Na miongoni mwao ni -karubiyyun-Yaani ni Malaika ambao wako pembezoni mwa Arshi, wao pamoja na wanaobeba Arshi ni Malaika watukufu sana, na hao ndio Malaika waliowekwa karibu na Mwenyezi Mungu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
}لَنْ يَسْتَنْكِفَ الْمَسِيحُ أَنْ يَكُونَ عَبْدًا لِلَّهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ وَمَنْ يَسْتَنْكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا{(النساء-172)
"Kamwe, hawezi kufanya kiburi Masihi kuwa mja wa Mwenyezi Mungu na wala Malaika waliokaribu" [An nisaa: 172]. Na wako miongoni mwao wakazi wa mbingu saba wanaiimarisha kwa ibada daima usiku na mchana asubuhi na jioni, kama alivyosema Mtukufu:
}يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ{(الانبياء-20)
"Wanamtakasa usiku na mchana wala hawanyong'onyei" [Al Anbiyaa: 20]. Na wako miongoni mwao wanaopeana zamu kuingia katika msikiti ulioko juu (Baitul Ma'muur). Nikasema: Kinachoonekana nikuwa wanaopishana kuingia katika nyumba iliyoimarishwa (Baitul Ma'muur) ni wakazi wa mbinguni.
Na wako waliopewa majukumu ya pepo na kuandaa takrima kwa watu wa peponi na kuandaa makazi kwa ajili ya wakazi wake, miongoni mwa mavazi vyakula na vinywaji na mapambo na sehemu za kupumzika na mengineyo katika yale ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio halijawahi kusikia, wala haijawahi kufikirika katika moyo wa mtu yeyote.
Na wako waliopewa majukumu ya moto -Mwenyezi Mungu atuepushe na moto- Na wako -Mazabania- na wa mwanzo wao ni kumi na tisa, na mlinzi wa moto ni Maliki, na yeye ndiye wa mwanzo katika hao walinzi, na hao ndio waliotajwa katika kauli yake Mtukufu:
}وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ{(المؤمنون-49)
"Na watasema wale walioko motoni kuwaambia walinzi wa Jahanam, muombeni Mola wenu atupunguzie siku moja katika adhabu" [Al Mu'minun: 49],
Na amesema Allah Mtukufu:
}وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ قَالَ إِنَّكُمْ مَاكِثُونَ{(الزخرف-77)
"Nao watapiga kelele watasema: Ewe Maliki, tunaomba atufishe Mola wako, atasema: hakika nyinyi mtakaa humo humo". [Azzukhruf: 77]. Na amesema Allah Mtukufu:
}يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ{(التحريم-6)
"Moto, wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa yale anayowaamrisha na wanatekeleza wanayoamrishwa" {Surat Tahriim: 6}
Na amesema Allah Mtukufu:
}عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ (30) وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَذَا مَثَلًا كَذَلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَى لِلْبَشَرِ (31){(المدثر-30_31)
"Juu yake wako Malaika kumi na tisa (30) Na hatukuwafanya walinzi wa moto ila ni Malaika" Mpaka kauli yake: "Na hakuna yeyote ajuaye majeshi ya Mola wako mlezi isipokuwa yeye". [Mudathiri, 30,31]
Na wako miongoni mwao waliopewa jukumu la kumuhifadhi mwanadamu kama alivyosema Mtukufu:
}لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُ وَمَا لَهُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَالٍ{(الرعد-11)
"Kila mtu analo kundi la Malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu" [Al Ra'di: 11].
Amesema bin Abbasi: Ni Malaika wanamlinda mbele yake na nyuma yake, inapokuja amri ya Mwenyezi Mungu (kifo) hujitenga naye.
Na amesema Mujahidi: Hakuna mja yeyote isipokuwa huwa na Malaika anayemlinda usingizini mwake na anapokuwa macho kutokana na majini na watu na viumbe wenye kudhuru, hakuna chochote kinachoweza kumuijia isipokuwa Malaika humwambia geuka nyuma yako, isipokuwa kitu ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu ameidhinisha kwake kimdhuru.
Na wako miongoni mwao waliopewa jukumu la kuhifadhi matendo ya waja; kama alivyosema Mtukufu:
} إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ (17) مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ (18){(ق-17_18)
"Pindi wanapopokea wapokeaji wawili, wanaokaa kuliani na kushotoni (17) "Hatoi kauli yoyote isipokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayari kuandika anayoyasema". [Qaaf: 17,18].
Na amesema Allah Mtukufu:
}وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ (10) كِرَامًا كَاتِبِينَ (11) يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ (12){(الإنفطار-10_12)
"Na hakika bila shaka wapo walinzi juu yenu" "Waandishi wenye heshima" (11) "wanayajua mnayoyatenda" [Al Infitwari: 10-12]
70- Amepokea Al bazzari kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
"Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kukaa uchi, basi waoneeni haya Malaika wa Mwenyezi Mungu wanaokaa pamoja nanyi; waandishi wenye heshima ambao huwakuacheni mahala popote isipokuwa sehemu moja kati ya tatu: wakati wa kukidhi haja, na mnapokuwa na janaba, na wakati wa kuoga, hivyo atakapooga mmoja wenu sehemu ya wazi basi na ajisitiri kwa nguo yake au kipande cha ukuta au kwa kinginecho"
Amesema mwanachuoni bin Kathiri: Na maana ya kuwakirimu ni mtu kuwaonea haya, asiwajazie matendo mabaya katika yale wanayoyaandika, kwani Mwenyezi Mungu amewaumba ni watukufu katika maumbile yao na tabia zao.
kisha akasema katika maana ya maneno yake: Hakika katika utukufu wao nikuwa wao hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa wala picha wala mwenye janaba wala sanamu, na wala hawaambatani na msafara ambao ndani yake kuna mbwa au kengele.
71- Na amepokea Maliki katika sahihi Bukhari na Muslim kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Wanapishana kwenu Malaika wakati wa usiku, na Malaika wakati wa mchana, na wanakusanyika katika swala ya alfajiri na swala ya laasiri, kisha wanapanda kwake wale waliolala kwenu, basi huwauliza haliyakuwa anajua: mmewaachaje waja wangu? Husema: Tumewaacha wakiwa wanaswali, na tuliwakuta wakiwa wanaswali"
72- Na katika riwaya nyingine nikuwa Abuu Huraira alisema: someni mkitaka:
}أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا{(الإسراء-78)
"Na Qur'ani ya alfajiri, hakika Qur'ani ya alfajiri hushuhudiwa" [Al Israai: 78].
73- Na amepokea hadithi imamu Ahmadi na Muslim: "Hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana kati yao isipokuwa huwashukia utulivu, na rehema huwagubika, na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja kwa wale walioko kwake, na mtu ambaye matendo yake yatakwenda taratibu yake basi hautokwenda mbio ukoo wake".
74 Na katika kitabu cha Al Musnadi na sunan kuna hadithi: "Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwanafunzi kwa kuridhishwa na anachokifanya".
Na hadithi zilizokuja kuwataja Malaika Amani iwe juu yao ni nyingi mno.
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
}اتَّبِعُوا مَا أُنْزِلَ إِلَيْكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ{(الأعراف-3)
"Fuateni mlio teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka" [Al A'raf: 3].
75- Kutoka kwa Zaidi bin Arqam -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alihutubia akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamtukuza, kisha akasema: "Ama baada ya hayo; Tambueni enyi watu hakika mimi ni mtu, nachelea wakati wowote huenda akanijia Mjumbe wa Mola wangu nikamuitikia, na mimi ninakuachieni vizito viwili, cha kwanza ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndani yake kuna uongofu na mwangaza, basi chukueni kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamane nacho" Akahimiza juu ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na akahamasisha ndani yake, kisha akasema: "Na watu wa nyumba yangu" Na katika tamko jingine: "Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndiyo kamba madhubuti; atakayekifuata atakuwa katika uongofu na atakayekiacha atakuwa katika upotovu".
[ Imepokelewa na Imamu Muslim]
76- Na amepokea pia katika Aya ndefu ya Jabiri yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amesema: katika hotuba ya siku ya Arafa: "Na hakika nimekuachieni kwenu nyinyi mambo ambayo kamwe hamtopotea ikiwa mtashikamana nayo, kitabu cha Mwenyezi Mungu, na nyinyi mnaniulizia mimi; sasa mnasema nini?" Wakasema: Tunashuhudia kuwa wewe umefikisha na umetekeleza amana na umenasihi- Akasema kwa kuashiria kwa kidole chake cha shahada akikinyanyua juu mbinguni na akikiashiria kwa watu:- Ewe Allah shuhudia" Akalisema hilo mara tatu.
77- Na Kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu- yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakika itakuja kutokea fitina" Nikasema: Ni ipi njia ya kujitoa katika fitina hiyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Amesema: kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake kuna habari za yale yaliyokuwa kabla yenu, na habari za yale yatakayokuwa baada yenu, ndicho kinachokata mzozo, na wala si mzaha, atakayekiacha miongoni mwa watu majeuri Mwenyezi Mungu atamvunja vunja, na atakayetafuta uongofu tofauti na kitabu hiki Mwenyezi Mungu atampoteza, na ndio kamba ya Mwenyezi Mungu madhubuti, na ndio ukumbusho wenye hekima, na ndio njia iliyonyooka, na ndio kitabu ambacho matamanio yoyote hayapotei, na wala ndimi haziwezi kupata shaka, na wala wanachuoni wakishibi, na wala hakiharibiki kwa wingi wa majibu, na wala hayamaliziki maajabu yake, na ndicho kitabu ambacho majini hawakukimaliza pindi walipokisikia, mpaka wakasema:
} قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا (1) يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا (2){(الجن-1_2)
"Hakika sisi tumesikia Qur'ani ya ajabu (1) Inaongoza katika uongofu tukaiamini" [Al Jinni: 1,2] Atakayesema kwa Qur'ani atakuwa kasema kweli, na atakayeifanyia kazi atalipwa, na atakayehukumu kwa Qur'ani atatenda uadilifu, na atakayelingania katika Qur'ani ataongozwa katika njia iliyonyooka".
[Kaipokea Tirmidhiy na akasema: Ni hadithi Gharib]
78- Na kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi marfu'u: "Yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake hayo ndio halali na yale aliyoyaharamisha hayo ndio haramu, na yale aliyoyanyamazia basi hiyo ni huruma, pokeeni kutoka kwa Mwenyezi Mungu huruma yake kwani Mwenyezi Mungu haiwezekani kwake kusahahu kitu chochote
}وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَلِكَ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا{(مريم-64)
" kisha akasoma: "Na hakuwa Mola wako mlezi ni mwenye kusahau" [Mariam: 64].
[Kaipokea Al Bazzar na bin Abii Hatim na Twabaraniy]
79- Na kutoka kwa Ibnu masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Amepiga mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka, na pembezoni mwake kuna ngome mbili, ngome hizo zina milango miwili iliyofunguliwa, na katika milango yake kuna mapazia yaliyoshushwa, na juu ya njia kuna muitaji anasema: Nyookeni katika njia na wala msipinde, na juu yake kuna muitaji anaita kila anapotaka mja yeyote kufungua sehemu ya milango hiyo anasema: Ole wako usiufungue kwani ukiufungua utaingia hapo".
Kisha akaitafsiri akaeleza kuwa njia ni uislamu, nakuwa milango iliyofunguliwa ni maharamisho, na kuwa mapazia yaliyozibwa ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kwamba muitaji aliyeko juu ya njia ni Qur'ani, na kwamba muitaji aliyeko juu ya Qur'ani ni mtahadharishaji wa Mwenyezi Mungu aliyeko ndani ya kila moyo wa muumini"
[Kaipokea Ruziin, na kaipokea Ahmadi na Tirmidhi kutoka kwa Nawwasi bin Sam'ani mfano wake. ]
80- Kutoka kwa Mama Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema: Alisoma Mtume wa Allah Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Yeye ndiye aliyekuteremshia kitabu ndani yake ziko Aya muhkamu (zenye maana ya wazi) hizo ndizo msingi wa kitabu" Akasoma mpaka katika kauli yake:
}هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ{(آل عمران-7)
"Na hawazingatii ila watu wenye akili..." [Al-Imran: 7]. Aisha akasema: Akasema: "Mkiwaona wale wanaofuata yale yenye kutatiza ndani ya Qur'ani, hao ni wale aliowatia sumu Mwenyezi Mungu, jitengeni nao".
[Wamekubaliana Bukhari na Muslim]
81- Na kutoka kwa Abdillahi bin Mas'ud -Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
“Alituchorea msitari Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, akachora kwa mkono wake, kisha akasema: "Hii ndio njia ya Mwenyezi Mungu", kisha akachoro misitari upande wake wa kulia na kushotoni mwake, na akasema: "Hivi ni vinjia njia, katika kila njia kuna shetani anawaita watu kuja hapo", Na akasoma:
}وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ{(آل عمران-153)
«Na miongoni mwa mambo aliyowausia Mwenyezi Mungu ni kwamba huu Uislamu ndio njia ya Mwenyezi Mungu, aliyetukuka, iliyolingana sawa. Basi ifuateni wala msifuate njia za upotevu zikawatawanya na kuwaepusha na njia ya Mwenyezi Mungu iliyolingana sawa. Muelekeo huo upande wa njia nyoofu, ndio aliowausia nao Mwenyezi Mungu ili mjikinge na adhabu yake kwa kuyatekeleza maamrisho yake na kujitenga na makatazo yake.» [Al-anaam: 153]
[Ameipokea Ahmad na Daaramii na Al- nasaai]
82- Na Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu- yake amesema: "Kuna watu katika maswahaba wa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake walikua wakiandika Taurati, wakalieleza hilo kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: "Hakika upumbavu mkubwa na upotovu mkubwa ni watu walioyaacha aliyokuja nayo Nabii wao wakachukua aliyokuja nayo Nabii asiyekuwa Nabii wao, na ya umma usiokuwa umma wao, kisha akateremsha Mwenyezi Mungu:
}أَوَلَمْ يَكْفِهِمْ أَنَّا أَنْزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَى عَلَيْهِمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَى لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ{(العنكبوت-51)
"Hivi haijawatosheleza kuwa sisi tumewateremshia juu yao kitabu kinachosomwa kwao, hakika katika hilo kuna rehema na ukumbusho kwa watu wanaoamini". [Al Ankabuti: 51].
[Kaipokea Al Ismaili katika "Mu'jam”]
83- wake na bin Mardawaihi. Na kutoka kwa Abdillahi bin Thabiti bin Harithi Al Answari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Aliingia Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa na kitabu ndani yake kukiwa na sehemu za Taurati, akasema: Hiki nimekipata kikiwa na mtu mmoja katika watu wa kitabu, nikusomee, ukabadilika uso wa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake sana, sijawahi kuona mfano wake katu, akasema Abdullahi bin Harithi kumwambia Omari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hivi huoni uso wa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- ?! Omari akasema: Tumeridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wetu, na uislamu kuwa ndio dini, na Muhammadi kuwa ndiye Nabii, akafurahishwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake na kauli hiyo na akasema: "Laiti Mussa angeliteremka mkamfuata na mkaniacha mimi basi mgepotea, mimi ndiye thamani yenu kwa Manabii na nyinyi ndio thamani yangu kwa umma zingine"
[Kaipokea Abdurrazzaq na bin Sa'di na Hakim katika "Al-kunaa"]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
}يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنْكُمْ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا{(النساء-59)
"Enyi mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka miongoni mwenu" Mpaka mwisho wa Aya. [Al Nisaa: 59],
Na kauli ya Allah Mtukufu:
} وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ{(النور-56)
"Na simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Mtume, ili mpate kurehemewa". [Al Nur: 56].
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
}مَا أَفَاءَ اللَّهُ عَلَى رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَى فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ{(الحشر-7)
"Na yale aliyo kuleteeni Mtume basi yachukueni na yale aliyo kukatazeni yaepukeni" mpaka mwisho wa Aya. [Al-Hashr 7]
84- Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu."
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
85- Na kutoka kwa Anas -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Mambo matatu yatakayekuwa kwake basi atapata kwa mambo hayo ladha ya imani: Awe Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapendeka zaidi kwake kuliko yeyote asiyekuwa wao, na ampende mtu si kumpenda kwa lolote ila ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Mwenyezi Mungu kumuokoa kama anavyochukia kutupwa motoni"
86- Na kutoka kwao wawili wameipokea kutoka kwake mar'fuu "Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka niwe napendeka kwake zaidi kuliko mtoto wake, na mzazi wake, na watu wote."
87- Na kutoka kwa Mikidadi Ibnu Ma'di yakrib Al kindiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Zinakaribia zama mtu ataegemea katika kiti chake akihadithia hadithi miongoni mwa hadithi zangu, akisema: kati yetu sisi na nyinyi ni kitabu cha Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- tutakalolikuta ndani yake ni halali tunalihalalisha, na tutakalolikuta ndani yake ni haramu tunaliharamisha!! Tambueni kuwa aliyoyaharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake ni sawa na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu"
[Kaipokea Tirmidhi na bin Majah]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
}لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا{(الأحزاب-21)
(Bila shaka mnao mfano mwema kwa mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na kumtaja Mwenyezi Mungu sana) (Surat Ahzaab: 21)
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُمْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ{(الأنعام-159)
"Hakika wale walioigawa dini yao na wakawa makundi makundi, huna uhusiano nao wowote" Mpaka mwisho wa Aya." [Al An'am: 159].
Na kauli ya Allah Mtukufu:
}شَرَعَ لَكُمْ مِنَ الدِّينِ مَا وَصَّى بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ اللَّهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَنْ يُنِيبُ{(الشورى-13)
{Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Issa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo}. Mpaka mwisho wa Aya. [Al shuuraa: 13].
88- Na kutoka kwa Irbadhi bin Sariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: {Alitupa mawaidha Mtume -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Mawaidha yenye kiwango cha hali ya juu, tukasema kana kwamba ni mawaidha ya kuaga basi tuusie ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Akasema: "Ninakuusieni kumcha Mwenyezi Mungu -Mwenye nguvu na utukufu- Na kusikiliza na kutii hata kama atawaamrisha mtumwa, kwa hakika atakayeishi muda mrefu miongoni mwenu basi ataona tofauti nyingi, Basi wakati huo shikamaneni na sunnah zangu na sunnah za Makhalifa waongofu walioijua haki na kuifuata, zikamateni sunnah hizo kwa magego, na jiepusheni na mambo ya uzushi, kwani kwa hakika kila uzushi ni upotevu}.
[ Kaipokea Abuu daudi na Tirmidhi na akaisahihisha bin Majah].
Na katika mapokezi yake pia: "Nimekuacheni katika weupe ambao usiku wake ni kama mchana wake, hakuna atakayepotea juu yake isipokuwa ataangamia, na atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu basi ataona tofauti nyingi". Kisha akaitaja hadithi kwa maana hiyo hiyo.
89- Na katika sahihi Muslim kutoka kwa Jabiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Ama baada ya hayo; Hakika mazungumzo bora ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na uongofu bora ni uongofu wa Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na mambo ya shari zaidi kuliko yote ni yale yenye kuzushwa, na kila chenye kuzushwa ni upotovu".
90- Na kwa Bukhari Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakayekataa". "Pakasemwa: Na ni nani atakayekataa? Akasema: "Atakayenitii mimi ataingia peponi na atakayeniasi mimi atakuwa amekataa".
91- Na imepokelewa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Anasi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: "Yalikuja makundi matatu kwa wake za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- wakiuliza kuhusu ibada za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- walipoelezwa wakawa kana kwamba wamezidogesha, wakasema: Tuko wapi sisi tukijilinganisha na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Hali yakuwa yeye amesamehewa madhambi yake yaliyotangulia na yajayo. Akasema mmoja wao: Ama mimi nitasali usiku milele, na akasema mwingine: Mimi nitafunga mchana na wala sitofungua, na akasema mwingine: Mimi nitajitenga na wanawake na wala sitooa milele, Akawajia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: "Nyinyi ndio ambao mmesema kadhaa wa kadhaa? Tambueni, Wallahi -Namuapa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninamuogopa Mwenyezi Mungu zaidi kuliko nyinyi na ni mchamungu kwake, lakini mimi ninafunga na ninakula, na nina swali na ninalala na ninaoa wanawake, yeyote atakayeichukia sunna yangu basi huyo miongoni mwangu".
92- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: {Ulianza uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza,Basi shangwe ni kwa wale wanao onekana kuwa ni wageni }
[Imepokelewa na Imamu Muslim]
93- Na kutoka kwa Abdalla bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: "Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo" Kaipokea Baghawi katika "Sharhus sunna" [na akaisahihisha Nawawi. ]
94- Na kutoka kwake pia Amesema , Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Watayafanya Umma wangu mambo waliyoyafanya Mayahudi na Manaswara kidogo kidogo hatua kwa hatua, hata kama kulikuwa katika hao Mayahudi na Manaswara aliyemuingilia mama yake hadharani basi kutakuwa na watu katika umma wangu watakaoiga na kufanya hivyo, na kwa hakika wana wa Israail walitofautiana mpaka kufikia makundi sabini na mbili (72) na utatofautiana umma wangu katika makundi sabini na tatu (73) yote hayo yatakwenda motoni isipokuwa kundi moja". Wakasema: Ni lipi kundi hilo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni lile litakalokuwa katika haya niliyonayo mimi leo na maswahaba zangu"
[Kaipokea Imamu Tirmidhiy]
95- Na kwa Muslim kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi mar'fuu: "Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote".
96- Na kutoka kwa Abuu Saidi Al Answar -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: "Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Hakika mimi nimekatikiwa safari nakuomba unibebe katika kipandwa chako, Akasema: Sina uwezo, Mtu mmoja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi naweza kumuelekeza kwa mtu anayeweza kumsaidia kumbeba, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Atakayejulisha juu ya kheri yoyote, atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake."
97- Na kutoka kwa Amri bin Aufi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Atakayehuisha sunna miongoni mwa sunna zangu iliyofishwa (iliyoachwa) baada yangu, basi atapata malipo mfano wa malipo ya yule atakayeifanyia kazi miongoni mwa watu hakitopungua chochote katika malipo ya watu, na atakayezua uzushi wowote asiouridhia Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake basi atapata mfano wa mzigo wa madhambi ya yule atakayeifanyia kazi miongoni mwa watu, hakitopungua chochote katika madhambi ya watu".
[ Kaipokea Tirmidhi na akaifanya kuwa ni Hasan na bin Majah -na lafudhi hii ni ya kwake.]
98- Kutoka kwa Ibnu Masoud- Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: "Mtakuwa vipi nyinyi itakapokuvaeni fitina, mdogo akakuwa nayo na mkubwa akazeeka nayo, na ikafanywa kuwa ndiyo sunna ambayo watu wanakwenda nayo; kikibadilishwa chochote katika fitina hiyo: watasema: Sunna imeachwa. Pakasemwa: Litakuwa lini hilo ewe baba Abdulrahman? Akasema: Watakapozidi wasomi wenu, na wakapungua waelewa wenu, na wakapungua waaminifu wenu, na dunia ikatafutwa kwa matendo ya Akhera, na watu wakatafuta elimu si kwa masilahi ya dini".
[ Imepokelewa na Addaramy]
99- Na kutoka kwa Ziadi bin Hadiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Alisema Omari kuniambia mimi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hivi unajua ni kitu gani kinachobomoa dini? Nikasema: Hapana, Akasema: Inabomolewa na kuteleza kwa mwanachuoni, na mijadala ya wanafiki kuhusu kitabu, na hukumu za viongozi wapotofu".
[Kaipokea Darami pia]
100- Na Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu- yake amesema: "Kila ibada ambayo hawaifanyi ibada hiyo watu wa Mtume rehema na Amani zimfikie basi msifanye ibada hiyo kuwa ni ibada kwa hakika waliotangulia hawakuwaachia waliokuja baada yao makala kuhusu ibada hizo, na muogopeni Mwenyezi Mungu Enyi kungamano la wasomi- wajuzi- na chukueni na kufuata njia ya waliokuwa kabla yenu".
[Imepokelewa na Abuu Daud]
101- Na kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Mwenye kutaka kuchukua kiigizo basi na achukue kwa waliokwisha kufa, kwani aliyehai haaminiki na kutopata fitina, hao ni maswahaba wa Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- walikuwa ni wa bora wa umma huu; wenye nyoyo za wema mno, na wenye elimu ya ndani mno, na walikuwa wachache wa kujilazimisha, aliwachagua Mwenyezi Mungu kusuhubiana na Nabii wake Rehema na Amani ziwe juu yake- na kushikamana na dini yake, basi tambueni ubora wao, na muwafuate katika nyenendo zao, na mshikamane na yale myawezayo katika tabia zao na historia yao, kwani wao walikuwa katika uongofu ulionyooka.
[ Kaipokea Raziin. ]
102- Na kutoka kwa Amri bin Shuabu kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake Amesema: Aliwasikia Mtume rehema na Amani zimfikie watu wakizozana katika Qur'ani, akasema: Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa jambo hili; walikigonganisha kitabu cha Mwenyezi Mungu baadhi yake kwa baadhi, bali kiliteremka kitabu cha Mwenyezi Mungu kikisadikisha baadhi yake kwa baadhi, mtakachokijua miongoni mwake basi kisemeni, mtakachokuwa hamkifahamu basi kiegemezeni kwa mjuzi wake".
[ Kaipokea Ahmadi na bin Maaja]
103- Kuna hadithi (katika sahihi mbili) inayoelezea mitihani ya kaburini (Yakwamba mwenye kuneemeka anasema ulitujia ubainifu na uongofu tukaamini na tukakubali na tukafuata, na kwamba mwenye kuadhibiwa husema: Nilisikia watu wakisema jambo nami nikasema)!.
104- Na katika sahihi mbili pia kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Anayemtakia Mwenyezi Mungu heri humpa ufahamu katika dini".
105- Na pia kutoka kwa Abii Musa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfano wa mvua kubwa iliyonyesha katika ardhi; kukawa na kundi moja zuri lililokubali maji likaotesha malisho na majani mengi, na ilikuwa ni ardhi ni kame iliyomeza maji Mwenyezi Mungu akanufaisha watu kupitia ardhi hiyo wakanywa na wakanywesha na wakalima, na mvua hiyo ikashuka katika sehemu nyingine ya ardhi laini haitulizi maji na wala haioteshi mimea; Huu ndio mfano wa mtu aliyejifunza akaelimika katika dini ya Mwenyezi Mungu na yakamnufaisha aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu akajua na akafundisha, na mfano mwingine ni wa mtu ambaye hakuyatilia maanani na wala hakukubali uongofu wa Mwenyezi Mungu ambao nimetumwa nao".
106- Na wamepokea pia kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mkiwaona wale wanaofuata yale yenye kutatiza ndani ya Qur'ani, hao ni wale aliowatia sumu Mwenyezi Mungu, jitengeni nao".
107- Na kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu katika umma wowote kabla yangu, isipokuwa kunakuwa katika umma wake na watu wake wapendwa na watu wanaoyachukua mafundisho yake na wanafuata amri yake, kisha wanakuja kutofautiana baada yao watu wanaowafuata, wanazungumza yale wasiyoyafanya, na wanafanya ambayo hawakuamrishwa, atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ndio muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake basi naye ni muumini, na atakayepigana nao kwa ulimi wake basi naye ni muumini, na hakuna zaidi ya hapo katika imani punje ndogo ya ulezi" (yaani kwa asiyefanya hivyo hana imani hata punje ndogo).
[ Imepokelewa na Imamu Muslim ]
108- Na kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sisi tunasikia habari kutoka kwa mayahudi zenye kutufurahisha, je unaona ni sawa tuziandike baadhi yake?!, Akasema -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hivi mna shaka nyinyi kama walivyopata shaka mayahudi na manaswara! Hakika nimekuleteeni ikiwa nyeupe safi, na lau kama Musa angekuwa hai asingepata nafasi zaidi ya kunifuata" [Kaipokea Ahmad]
109- Na kutoka kwa Tha'laba Al Khushani -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi mar'fuu: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute"
[Hadithi Hasan kaipokea Addaraqutni na wengineo.]
110- Na katika sahihi Bukhari na Muslim kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao"
111- Na kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Mwenyezi Mungu amng'arishe mja aliyesikia toka kwangu kauli yoyote akaihifadhi na akaizingatia, na akaitekeleza, huenda mbeba maarifa akawa si muelewa, na huenda mpeleka maarifa akayapeleka kwa muelewa zaidi yake, mambo matatu haupati kifundo kwayo moyo wa muislamu: Kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kuwanasihi waislamu, na kubaki katika umoja wao, kwani maombi yao humfunika kila aliye mbele yao" (Yaani: Mwenye kuwa na mambo haya hawezi kuweka chuki moyoni mwake)
[Kaipokea Imamu Shafi na Baihaqi katika "Al Madkhali]
112- Na kaipokea Ahmadi na Abuu daudi na Tirmidhi kutoka kwa zaidi bin Thabit -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
113- Na kutoka kwa Abdalla bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: "Elimu iko katika mambo matatu: Aya za wazi, au sunna yenye kufanyiwa kazi, au faradhi ya uadilifu, na itakayokuwa tofauti na hayo basi ni ziada"
[Kaipokea Darimi na Abuu daud.]
114- Na kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Atakayesema ndani ya Qur'ani kwa rai yake basi aandae makazi yake motoni" Kaipokea Imamu Tirmidhiy
115- Na katika riwaya nyingine: "Atakayesema ndani ya Qur'ani bila elimu basi aandae makazi yake motoni"
[Kaipokea Imamu Tirmidhiy ]
116- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Atakayetoa majibu bila ya elimu madhambi yake yatakuwa juu ya yule aliyemuuliza, na atakayemuelekeza ndugu yake katika jambo ambalo anajua kuwa ukweli uko katika jambo jingine basi atakuwa kamfanyia hiyana".
[Imepokelewa na Abuu Daud ]
117- Na Kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- : Yakuwa, alikataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwajaribu (wanachuoni).
[Imepokelewa na Abudaud pia.]
118- Na kutoka kwa kathiri bin kaisi Amesema: Nilikuwa nimekaa na Abuu Dardaa katika msikiti wa Damaskasi (Siria), akaja mtu mmoja akasema: Ewe Abuu Dardaa Hakika mimi nimekujia kutoka katika Mji wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa sababu ya hadithi iliyonifikia kutoka kwako kuwa wewe unaisimulia kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wala sijaja kwa haja nyingine zaidi ya hiyo, akasema: Hakika mimi nilimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-akisema: "Atakayeshika njia kwenda kutafuta elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi yeye njia ya kwenda Peponi, Na hakika Malaika huweka mbawa zao kwa kuridhishwa na mwenye kutafuta elimu, na hakika mwenye kutafuta elimu huombewa msamaha na vyote vilivyoko mbinguni na ardhini, hata samaki kwenye maji, na hakika ubora wa mtu mjuzi (mwenye elimu) kwa mfanya ibada, ni kama ubora wa mwezi kwa nyota zote, hakika Wanachuoni ni warithi wa Manabii, Hakika Manabii hawakurithisha Dinar wala Dirham (pesa) Hakika walirithisha elimu, atakayeichukua basi kachukua fungu la thamani kubwa".
[ Kaipokea Ahmadi na Darimi na Abuudaudi na Tirmidhi na bin Maajah.]
119- Na kutoka kwa Abuu Hurayra -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi mar'fuu: "Neno la hekima ni kiwindwa cha muumini, mahala popote anapokipata basi yeye ndiye mwenye haki zaidi kuliko yeyote"
[Kaipokea Tirmidhi na akasema ni hadithi : Gharib, na bin Majah.]
120- Na kutoka kwa Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Hakika muelewa ni haki ya muelewa, asiyewakatisha watu tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, na akawa hajawaruhusu katika yale yenye kumuasi Mwenyezi Mungu, na akawa hakuwaaminisha na adhabu za Mwenyezi Mungu, na akawa hakuiacha Qur'ani kwa kuthamini kingine, hakika hakuna ubora katika ibada ambazo hazina elimu ndani yake, na wala elimu isiyokuwa na uelewa, na wala kisomo kisichokuwa na mazingatio ndani yake"
121- Na kutoka kwa Hasan -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Atakayefikwa na mauti hali yakuwa anatafuta elimu kwa ajili ya kuuhuisha uislamu basi kati yake na Manabii ni daraja moja peponi"
[Kazipokea hadithi hizi mbili Darimi]
122- Na Kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu- yake alisema: {Tulikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akanyanyua macho yake mbinguni, kisha akasema: Hizi ni nyakati ambazo elimu inanyakuliwa kutoka kwa watu mpaka wasiweze chochote katika elimu}.
[Kaipokea Imamu Tirmidhiy.]
123- Na kutoka kwa Ziadi bin Labidi -Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Alitaja Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- jambo akasema: Hilo litakuwa katika nyakati za elimu kutoweka, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu inatowekaje elimu hali yakuwa na sisi tunasoma Qur'ani na tunawasomesha watoto wetu na watoto wetu wanawasomesha watoto wao mpaka siku ya kiyama? Akasema: "Umepata hasara zaidi ya kumpoteza mama yako ewe ziadi! Kwani mimi nilikuwa nakuona ni katika watu waelewa katika mji huu, kwani si hawa mayahudi wanasoma Taurati na Injili na hawaelewi chochote katika yale yaliyomo ndani yake?”.
[Kaipokea Ahmadi na bin Maaja.]
124- Kutoka kwa Ibnu Masoud- Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: "Shikamaneni na elimu kabla haijaondolewa, na kuondolewa kwake ni kuondoka kwa wasomi, shikamaneni na elimu kwani mmoja wenu hajui ni lini ataihitajia au ni lini yatahitajika aliyonayo katika elimu, na mtawakuta watu wanadai kuwa wao wanalingania katika kitabu cha Mwenyezi Mwenyezi Mungu haliyakuwa wamekiacha nyuma ya migongo yao, shikamaneni na elimu ni tahadharini na uzushi na misimamo mikali na kujikita katika mambo, na shikamaneni na vya zamani".
[Kaipokea Daarami mfano wake. ]
125- Na katika sahihi mbili kutoka kwa bin Amri Hadithi Marf'uu: "Hakika Mwenyezi Mungu hainyakui elimu kwa kuikwapua kuitoa katika vifua vya waja, lakini anaichukua elimu kwa kuwafisha wanachuoni, mpaka atakapokuwa hajabakia mwanachuoni yeyote, watu watajifanyia viongozi wajinga, wataulizwa; na watatoa majibu bila ya elimu, watapotea na watapoteza"
126- Na kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Zimekaribia kuja zama kwa watu hakuna kitakachobakia katika uislamu isipokuwa jina lake tu, na wala hakuna kitakachobakia katika Qur'ani isipokuwa michoro yake, misikiti yao imeboreshwa hali yakuwa imeharibika kwa kukosa uongofu, wanachuoni wao ni waovu kutoka chini ya mbingu, na kwao ndiko fitina zinakotokea, na kwao ndiko zinakorudi".
[Kaipokea Baihaki katika "Shua'bil Iman"]
127- Na kutoka kwa Ka'bu bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: "Atakayetafuta elimu ili awe karibu na wanachuoni, au akabishane na wapumbavu, au akafanye watu wamkubali, Mwenyezi Mungu atamuingiza motoni".
[Kaipokea Imamu Tirmidhiy.]
128- Na kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi marfu'u: "Hawajawahi kupotea watu katika uongofu walikuwa nao isipokuwa hupewa mijadala
}وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ{ (الزخرف-58)
" Kisha akasoma kauli yake Mtukufu: "Hawakukupigia mfano huo isipokuwa kwa ajili ya ubishi tu, bali wao ni watu wagomvi" [Azzukhruf: 58].
[Kaipokea Ahmadi na Tirmidhi na bin Maaja]
129- Na kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Hakika Watu wanaochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi zaidi"
[Wamekubaliana Bukhari na Muslim.]
130- Na kutoka kwa Abuu wail kutoka kwa Abdillah -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Atakayetafuta elimu kwa ajili ya mambo manne ataingia motoni -Au alisema mfano wa neno hili- Ili awatambie wanachuoni, au abishane na wapumbavu, au anatafuta watu wamkubali, au ili achukue kwa elimu hiyo sehemu nafasi za viongozi".
[Imepokelewa na Addaramy.]
131- Na kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Alisema kuwaambia watu aliwasikia wakibishana katika dini: Hivi hamjui kuwa Mwenyezi Mungu ana waja ambao kumewanyamazisha kumuogopa Mwenyezi Mungu si viziwi wala mabubu, na hakika wao ndio wanachuoni mafasaha na wazungumzaji wazuri na werevu; ni wanachuoni kwa siku zote za Mwenyezi Mungu, isipokuwa wao wanapokumbuka ukubwa wa Mwenyezi Mungu zinaruka akili zao na zinavunjika nyoyo zao, na zinakatika ndimi zao, mpaka wanapozinduka kutoka katika hilo huenda mbio kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo safi, wakizihesabu nafsi zao kuwa ni katika wazembe, na hakika wao ni werevu wenye nguvu, na wako pamoja na wapotevu na wakosefu, pamoja nakuwa wao ni wema walio mbali na maasi, tambueni kuwa wao huomba ziada kwake ya mambo mengi, na wala hawaridhiki kwake kwa machache, na wala hawajionyeshi kwake kuwa na matendo mazuri, kiasi ambacho yale waliyokutana nayo wameyatilia maanani na wana wasi wasi na wogo na hofu kuwa huenda yasikubaliwe".
[ Imepokelewa na Abuu Nuaim]
132- Amesema Al hasan -Alisikia watu wakijadiliana: {Hawa ni watu ambao zimewachosha ibada, na mazungumzo kwao yamekuwa mepesi, na umepungua unyenyekevu wao wakawa wanazungumza}.
133- Na kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- katika hadithi mar'fuu: "Haya na kujiepusha na maneno yenye kumtia mtu kwenye makoasa ni sehemu mbili miongoni mwa sehemu za imani, na uchafu wa maneno na uwazi ni sehemu mbili miongoni mwa sehemu za unafiki"
[Kaipokea Imamu Tirmidhiy]
134- Na kutoka kwa Abuu Tha'laba -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hakika anayependeka zaidi kwangu na atakayekuwa karibu zaidi na mimi miongoni mwenu siku ya kiyama ni yule mwenye tabia nzuri kuliko wote, na hakika anayechukiza zaidi kwangu na atakayekuwa mbali na mimi ni yule mwenye tabia mbaya; wenye maneno mengi, waropokaji wanyekujitia kujua kila kitu". Kaipokea Baihaki katika " Shua'bil Iman".
135- Na Tirmidhi mfano wake kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
136- Na kutoka kwa Sa'di bin Abi Waqqas -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-: "Hakitosimama kiyama mpaka watokee watu wanakula kwa ndimi zao kama ng'ombe wanavyokula kwa ndimi zao"
[Kaipokea Ahmad na Abuu daud Tirmidhi.]
137- Na kutoka kwa Abdillahi bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake Hadithi marfu'u: "Hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu fasaha anayetoa maneno kwa ulimi wake kama ng'ombe anavyotoa mabaki ya chakula kwa ulimi wake"
[Kaipokea Tirmidhi na Abuu daud.]
138- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- "Atakayejifunza kugeuza maneno ili ateke nyoyo za wanaume au za watu basi Mwenyezi Mungu hatokubali toka kwake siku ya kiyama cha kumuokoa wala fidia"
[ Imepokelewa na Abuu Daud ]
139- Na kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Yalikuwa maneno ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake ni yenye uwazi anayaelewa kila mwenye kuyasikia, na akasema: na alikuwa akitusimulia hadithi laiti angeyahesabu maneno yake mtu yeyote basi angeweza kudhibiti idadi yake, na akasema: Na wala hakuwa anaunganisha mazungumzo kama mnavyounganisha nyinyi".
[Kapokea Abuudaudi baadhi yake.]
140- Na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Mkiona mtu anapewa kutoijali dunia, na uchache wa maneno, basi mkaribieni, kwani mtu huyo hutiwa hekima".
[Kaipokea Baihaki katika "Shua'bil Iman".]
141- kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakika katika ufasaha kuna uchawi, na hakika katika elimu kuna ujinga, na hakika katika mashairi kuna hekima, na hakika katika maneno kuna kuchoshana"
142-Na kutoka kwa Amru bin Aaswi-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-alisimama na kuanza kuzungumza, akasimama mtu mmoja akazungumza maneno mengi, akasema Amru: Laiti angelifupisha maneno ingekuwa bora kwake, nilimsikia Mtume rehema na Amani zimfikie akisema: "Hakika niliona-au nimeamrisha kufupisha katika maneno; kwani kufupisha ndio bora"
[Imepokelewa na Abuu Daud.]
Mwisho wa kitabu hiki, Na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa viumbe wote sifa nyingi.
Misingi ya Imani 1
Mlango wa kumfahamu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka na kumuamini 3
Mlango wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ". 11
Mpaka mfadhaiko unapowaondokea kwenye nyoyo zao wanaulizana wao kwa wao, «Amesema nini Mola wenu?» Malaika watasema, «Amesema kweli! Na yeye yuko juu kwa dhati yake, utendaji nguvu wake na utukufu wa cheo chake, aliye Mkubwa juu ya kila kitu.» [Sabai: 23] 11
Mlango wa kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu: 13
{Hawakuwa wakimwogopa Mwenyezi Mungu. Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa kwenye mshiko wake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kulia. Ametakasika na ametukuka juu ya yote wanayo mshirikisha nayo!} [Surat az-Zumar: 67] 13
Mlango wa kuamini kadar: 17
Mlango wa kuwaelezea Malaika Amani iwe juu yao na kuwaamini: 24
Mlango wa usia wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu: 36
Mlango wa haki za Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: 41
Mlango wa kuhamasisha kwake Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, juu ya kushikamana na sunna na kutia moyo juu ya hilo na kuacha uzushi na kufarakana na kutofautiana na tahadhari juu ya hilo. 43
Mlango wa kuhamasisha juu ya kutafuta elimu na namna ya kutafuta. 49
Mlango wa kuchukuliwa elimu. 54
Mlango wa kemeo kali la kutafuta elimu kwa ajili ya ubishi tasa au mijadala. 56
Mlango wa kuacha mazungumzo na kuacha kujilazimisha na misimamo mikali. 58