Uislamu Vyanzo vyake na misingi yake ()

 

Mtunzi wa kitabu hiki ameelezea kuhusu Uislamu kwa ufupi kwa kutaja maana yake nguzo zake na vyanzo vyake vitukufu, pia ameeleza mambo yanayo takiwa kubainishwa katika hali ya kulingania dini ya Uislam.

|

 Utangulizi

Hakika sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu, tuna msifu na tunamuomba msaada na tunamuomba msamaha, na tuna jilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari za nafsi zetu, Mwenye kuongozwa na Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na nina shahidilia kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika, na nina shahidilia kuwa Muhamad ni mja wake na nimtume wake wake rehma na amani za Mwenyezi Mungu zilizo kuwa nyingi ziwe juu yake.

Ama baada ya hayo: Kwa hakika Mwenyezi Mungu ametuma Mitume wake kwa ulimwengu wote, ili wanadamu wasiwe na hoja kwa Mwenyezi Mungu baada ya Mitume, na akateremsha vitabu vikiwa ni uongofu, rehema, nuru na ponyo, walikuwa Mitume katika zama zilizopita wanatumwa kwa watu wao maalum, na wanaombwa wahifadhi vitabu vyao, na kwa ajili hiyo maandishi yao yalisambaa, na ikabadilishwa na kugeuzwa sheria yao, kwasababu viliteremshwa kwa umma maalum, na katika zama maalum.

Kisha Mwenyezi Mungu akamuhusisha Mtume wake Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake kwa kumfanya awe ni Mtume wa mwisho, Amesema Allah Mtukufu: Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii,([1]) Akamkirim kwa kumpa kitabu bora alicho mteremshia nayo ni Qur'an tukufu, na Mwenyezi Mungu akachukua dhamana ya kuihifadhi, na hakuiacha ihifadhiwe na kiummbe wake, akasema Mwenye Mungu: Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda,([2]) Na akaifanya sheria yake ni yenye kubaki mpaka kitakapo simama Qiyama, na Mwenyezi Mungu akabainisha kuwa miongoni mwa vitu vinavyo lazimu sheria yake kubaki ni kuiamini na kuilingania na kufanya subra juu yake, ikawa njia ya Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake na njia ya wafuasi wake baada yake ni kulingania kwa elimu na busara, amesema Mwenyezi Mungu akiweka wazi kuhusu njia hiyo: Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina,([3]) na Mwenyezi Mungu akamuamrisha Mtume wake afanye subra juu ya maudhi katika njia ya Mwenyezi Mungu, akamesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa.([4]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zake zimetukuka: Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa([5]), na wafuasi wa njia hii ya Mwenyezi Mungu mtukufu, nimeandika kitabu hiki nikilingania katika njia ya Mwenyezi Mungu nikikitumia kitabu cha Mwenyezi Mungu na kupata mwongozo wa Sunna za Mtume wake rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na nimebainisha ndani yake kwa ufupi habari za kuumbwa kwa ulimwengu na kuumbwa kwa mwanadamu na kukirimiwa kwake, na kutumiwa Mitume na hali ya dini zilizo tangulia, kisha nimeutambulisha Uislamu kwa maana yake na nguzo zake, yeyote anaetaka uongofu basi huu ndio mwongozo uliopo mbele yake, na mwenye kutaka kuokoka nimemuwekea wazi njia yake, na mwenye kutaka kufuata athari za Mitume na watu wema basi hii ndio njia yao, na mwenye kuwakataa atakuwa ametia nafsi yake katika ujinga na amepita njia ya upotovu, hakika watu wa dini zote wanalingania watu katika dini zao, na wanaitakidi kwamba wao ndio wenye haki kuliko wengine, na kila wenye itikadi wanawalingania watu wafuate itikadi yao na kumuheshimu kiongozi wa njia yao.

Ama Muislamu hawalinganii watu wafuate njia yake kwasababu hana njia yake maalum, hakika dini yake ni dini ya Mwenyezi Mungu aliyo iridhia, Amesema Allah Mtukufu: Hakika dini inayo kubaliwa kwa Mwenyezi Mungu ni Uislam,([6]) na halinganii ili atukuzwe mwanadamu, viumbe wote katika dini ya Mwenyezi Mungu ni sawa hawana toufauti isipokuwa kwa ucha Mungu, bali anawalingania watu wapiti katika njia ya Mola wao na wawaamini Mitume wake na waifuate sheria yake aliyoiteremsha kwa Mtume wa mwisho Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na akamuamrisha awafikishie watu wote.

Na kwa ajili hiyo nimeandika kitabu hiki kwasababu ya kulingania kunako dini ya Mwenyezi Mungu aliyo iridhia na akaiteremsha kwa Mtume wake wa mwisho, na kwa lengo la kutoa mwongozo kwa mwenye kutaka uongofu, na ni dalili kwa mwenye kutaka mafanikio, nina apa kwa Mwenyezi Mungu mmoja kiumbe yeyote hatopata mafanikio ya kweli isipokuwa dini hii, na hatoujua utulivu isipokuwa yule aliye muamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola wake, na Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuwa ni Mtume wake, na Uislamu kuwa ndio dini yakewametoa ushuhuda maelfu ya walio ongoka kunako Uislamu katika enzi za zamani na za sasa kwamba wao hawakuyatambua maisha ya kweli ila baada ya kusilimu kwao, na hawakuonja mafanikio isipokuwa walipokuwa katika kivuli cha Uislamu, na kwakuwa kila mwanadamu anatamani apate mafanikio na anautafuta utulivu na uhakika, nye kazi iwe ni kwa ajili yake na ni yenye kulingania kunako kunako njia yake, na kiwe ni chenye kukubaliwa na akifanye kuwa ni katika matendo mema yatakayo mfaa aliyekiandika katika dunia na akhera.

Nimetoa idhini kwa atakae taka kukichapisha kitabu hiki kwa lugha yoyote au kukitafsiri kwa lugha yoyote, kwa sharti awe ni mwaminifu katika kukibadilisha kwake kwenye lugha nyingine.

Kama ninavyo tarajia kwa kila mwenye angalizo au kusahihisha, sawasaw iwe ni katika kitabu cha asili cha lugha ya kiarabu au tafsiri yoyote ya kitabu hiki anitumie katika anuwani iliyotajwa hapo.

Nina mshukuru Mwenyezi Mungu mwanzo na mwisho, kwa dhahiri na kwa siri, na sifa njema ni zake za wazi na za siri, na ana sifa njema duniani na akhera, ana sifa njema zilizo jaa mbingu na ardhi na vyote anavyo vitaka Mola wetu mlezi, na rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad na Maswahaba wake na atakae pita katika njia yake, na ziwe juu yake amani nyingi mpaka siku ya Qiyama.

Mtunzi

Dr. Muhammad Bin Abdallah Bin Swaleh Al-Ssuhaym

Riyadh 13/10/1420H (SLP 1032 Riyadh 1342)

SLP 6249 Riyadh 11442.

 Njia Iko Wapi?

Mwanadamu anapokua na kupata akili yanamjia maswali mengi katika akili yake, kama vile nimetoka wapi? Na kwanini nimekuja? Na ninaelekea wapi? Na ni nani aliyeniumba na akaumba ulimwengu huu unaonizunguka? Na anaemiliki ulimwengu huu na kuuendesha?  Na maswali mengine kama hayo.

Na mwanadamu hawezi kujitegemea kujua majibu ya maswali haya, wala elimu ya kisasa haiwezi kuleta majibu hayo, kwasababu hayo yanayo zungumzwa katika maswali ni katika mambo ya kidini, na kwa ajili hiyo zimekuja riwaya tofauti na uzushi mwingi na habari za uongo juu ya mas'ala haya miongoni mwa yanayo mzidishia mtu kuendelea kuwa katika mshangao na dhiki. Na mtu hawezi kutoa majibu yenye kutosheleza kuhusu maswali hayo isipokuwa Mwenyezi Mungu atakapo muongoza kuijua dini sahihi inayo muwekea wazi mas'ala hayo na mengineyo, kwasababu mambo haya yanahesabika ni katika mambo ya ghaibu, na dini iliyo sahihi ni ile ya haki na ukweli, kwasababu ndiyo dini pekee inayotoka kwa Mwenyezi Mungu na ameifunua kwa Mitume wake na Manabii wake, na kwa ajili hiyo imekuwa ni lazima kwa mtu aishike dini ya haki na ajifunze na aiamini, ili mshangao umuondokee na mashaka yaondoke na aongoke kunako njia ilinyooka.

Na katika kurasa zijazo ninakuita ili ufuate njia iliyo nyooka, nikuonyeshe mbele ya macho yako dalili na hoja zilizo wazi ili uziangalie kwa makini na utulivu.

 Kuwepo Kwa Mwenyezi Mungu Na Uungu Wake Na Kuabudiwa Kwake Utakasifu Ni Wake*:

Makafiri wanaabudu miungu iliyoumbwa na kutengenezwa kama vile miti na mawe na viumbe, na kwa ajili hiyo Mayahudi na washirikina walimuuliza Mtume rehme na amani za Allah ziwe juu yake kuhusu sifa za Mwenyezi Mungu na anatokana na nini, Mwenyezi Mungu akateremsha: Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja,([7]) akajitambulisha mwenyewe Allah kwa kusema: Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote,([8]) na amesema Mwenyezi Mungu: Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona, ametawala kwenye Ufalme wake, na amefanya jua na mwezi yamt'ii, kila kimoja kinakwenda kwa kiwango maalumu. Anayapanga mambo, na anazipambanua Ishara ili mpate kuwa na yakini kukutana na Molawenu Mlezi. Na ndiye aliye itandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya dume na jike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri. Mpaka kauli yake Allah: Na wale walio kufuru husema: Mbona hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi?  Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa kuwaongoa.([9]) na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi?  Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajifai wenyewe kwa jema wala baya?  Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona huwa sawa?  Au hebu huwa sawa giza na mwangaza?  Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia?  Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja([10]).

Na akawawekea Mwenyezi Mungu dalili na ushahidi na ubainifu kwa kusema:Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu. Na ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki. Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapo iteremshia maji mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka aliye ihuisha ardhi ndiye atakaye huisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu([11]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi. Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake([12]).

Na akaisifu nafsi yake sifa kwa sifa nzuri zenye ukamilifu akasema:(Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake?  Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe([13])

Na alisema: Anaye samehe dhambi na anaye pokea toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye ukarimu, hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake([14] Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka:Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha([15])

Huyu Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye hekima na muweza aliyeitambulisha Nafsi yake kwa waja wake, na akawasimamishia dalili zake na ushahidi na ubainifu, na akaisifu Nafsi yake kwa sifa za ukamilifu, sheria zilizo kuja kwa Mitume na akili zilizo kuwa salama na maumbile ya kuumbwa vyote hivyo vinaonyesha juu ya kuwepo kwake na Uungu wake na kuabudiwa kwake, na nyumati zote zimekubaliana hivo, na nitakubainishia kidogo kuhusu hilo katika yanayo kuja, ama dalili za kuwepo kwake na Uungu wake:

 1. Kaumba Ulimwengu Huu Na Vilivyomo Kwa Umahiri Wa Hali Ya Juu:

Ewe mwanadamu ulimwengu huu mkubwa unakuzunguka kutokana na mbingu na sayari na vitu vinavyo tembea, na ardhi iliyo tandikwa ndani yake kuna vipande vilivyo kurubiana vinatofautiana vinavyo ota ndani yake kwa tofauti zake, na ndani yake kuna kila aina tofauti za matunda na katika kila kiumbe Allah kajaalia viwili viwili, na ulimwengu huu haujajiumba wenyewe kwa hali yoyote kuna muumbaji, kwasababu haiwezekani kujiumba wenyewe, basi nani aliyeuumba kwa nidhamu hii nzuri na akaukamilisha kwa ukamilifu huu mzuri, na akaufanya kuwa ni dalili kwa wenye kuangalia, uumbaji huu hawezi kuufanya yeyote ila ni Mwenyezi Mungu Mmoja mwenye kutenza nguvu ambae hakuna Mola mwingine isipokuwa Yeye wala Mungu asiyekuwa Yeye, amesema Allah Mtukufu: Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?  Au wao wameziumba mbingu na ardhi?  Bali hawana na yakini.([16]) Aya hizi mbili zimekusanya utangulizi wa aina tatu nao:

1-Je! Wanadamu wameumbwa kwasababu hawakuwepo?

2-Je! Walijiumba wenyewe?

3-Je! Wao ndio walioumba mbingu na ardhi?

Ikiwa hawakuumbwa kwasababu hawakuwepo, na hawakujiumba wenyewe, na hawakuumba mbingu na ardhi, hapo imebainika kwamba hakuna budi wakiri ya kuwa kuna Muumbaji aliyewaumba na akaumba mbingu na ardhi naye ni Mwenyezi Mungu Mmoja mwenye kutenza nguvu.

             2. Maumbile:

Viumbe wameumbwa na maumbile ya kukiri kuwepo kwa Muumbaji, na kwamba Yeye ni Mtukufu na ni Mkubwa na ni Mwenye cheo na ni mkamilifu kuliko kila kitu, na jambo hili limewekwa na likatulia katika maumbile kuliko vyanzo vya elimu ya kuhesabu wala haihitajikutoa dalili isipokuwa kwa mtu ambae fikra zake zimebadilikana zikapatwa na hali ambayo inazitoa fikra hizo katika usalama.([17])

Amesema Allah Mtukufu: Ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.([18]) Alisema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: ((Hakuna mtoto anaezaliwa isipokuwa anazaliwa katika maumbile ya Dini ya Uislamu, basi wazazi wake ndio wanamgeuza kuwa Myahudi au Mnaswara au Mmajusi, kama vile mnyama anavyozaa mtoto aliyesalimika je! Mnaona aibu yoyote kwa mtoto yule?  Kisha Abuu Hurayra akasema mkipenda someni: Ni maumbile ya Mwenyezi Mungu aliyowaumbia watu hakuna wa kubadilisha maumbile ya Mwenye).([19]) Alisema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: (Jueni hakika Mola wangu Mlezi ameniamrisha niwafundishe yale msiyo yajua miongoni mwa yale aliyo nifundisha leo hii: Kila mali niliyompa mja ni halali, na Mimi nimewacha waja kuwa wenye dini sahihi, hata kama shetani akiwajia akawatoa katika dini yao wakaharamisha yale niliyo yahalalisha, na akawaamrisha wanishirikishe na yale ambayo([20]).

 3. Kukubaliana Nyumati:

Zimekubaliana nyumati za zamani na za sasa kwamba ulimwengu huu una muumbaji naye ni Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, nae ni muumbaji wa mbingu na ardhihana mshirika katika kuumba kwake kama vile asivyo na mshirika katika Ufalme wake.

Na hakunukuliwa kwa wowote katika nyumati zilizo tangulia ya kwamba zilikuwa zinaitakidi kuwa miungu yao ilishirikiana na Mwenyezi Mungu katika kuumba mbingu na ardhi, bali walikuwa wakiitakidi ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliye waumba wao na miungu yao na kwamba hakuna muumbaji asiye kuwa Yeye wala mtoaji rizki asiye kuwa Yeye, na manufaa na madhara yako mikononi mwake Mwenyezi Mungu.([21]) Amesema Mwenyezi Mungu akielezea kukiri kwa washirikina juu ya Uungu wake: Na ukiwauliza; Nani aliye umba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kuti'ii amri yake?  Bila ya shaka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanako geuzwa?  Mwenyezi Mungu humkunjulia, na humdhikishia, riziki amtakaye katika waja wake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Na ukiwauliza: Ni nani anaye teremsha maji kutoka mbinguni, na akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake?  Bila ya shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi.([22]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi?  Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi.([23])

 4. Dharura Za Kiakili:

Akili haina budi kukiri kwamba ulimwengu huu una Muumbaji Mtukufu, kwasababu akili inaona kwamba huu ulimwengu umeumbwa, na haukujileta wenyewe, na kila kicho kuja lazima kuna aliyekileta.

Na mwanadamu anajua ya kwamba zama zinampitia pamoja misiba, na wakati mwanadamu anaposhindwa kuizuia misiba hiyo huwa anaelekeza moyo wake mbinguni na kuomba msaada kwa Mola wake ili amtatulie hamu zake na matatizo yake, hata kama katika masiku mengine humkanusha Mola wake na ana abudu sanamu lake, hili ni jambo la dharura lisilo ondoka ni lazima kulikubali, bali hakika mnyama anapopatwa na msiba ananyanyua kichwa chake na macho yake mbinguni. Mwenyezi Mungu ameeleza kuhusu mwanadamu anapopatwa na madhara hukimbilia kwa Mola wake akimuomba amuondolee madhara yaliyo mpata, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na taabu inapo mfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyo kuwa akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu njia yake.([24]) Na amesema Mwenyezi Mungu akielezea hali ya washirikina:Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wameshazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru. Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda,([25]) na amesema Mwenyezi Mungu: Na wimbi linapo wafunika kama wingu, wao humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapo waokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa sawa Wala hazikanushi Ishara zetu ila aliye khaini kafiri mkubwa.([26])

Huyu Mwenyezi Mungu aliyeuleta ulimwengu na akaumba wanadamu katika maumbile mazuri na akaweka katika maumbile ya mwanadamu utumwa wa kumuabudu Yeye na kujisalimisha kwake, na akazifanya akili zimnyenyekee katika Uungu wake na katika ibada zake, na umma ukajikusanya katika kukubali Uungu wake…huyu Mungu lazima atakuwa ni mmoja katika Uungu wake na ibada zake, kama vile asivyo na mshirika katika kuumba vile vile hana mshirika katika ibada, na dalili kuhusu jambo hilo ni nyingi miongoni mwa hizo ni*

1-Hakuna katika ulimwengu isipokuwa Mwenyezi Mungu Mmoja, Yeye ndiye Muumbaji na mtoa rizki, hakuna anaeleta manufaa au kuzuia madhara isipokuwa Yeye, na laiti ingekuwa katika ulimwengu huu kuna Mungu mwingine angekuwa na vitendo na kuumba na amriasingependa mmoja wao kushirikiana na mungu mwingine, ([27]) na ni lazima mmoja wao amshinde mwingine na kumtenza nguvu, na huyo aliyeshindwa hawezi kuwa Mungu, na huyu aliyeshinda ndiye Mungu wa kweli hana mshirika katika ibada zake kama alivyokuwa hana mshirika katika Uungu wake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu. ([28])

2-Hakuna anestahiki kuabudiwa isipokuwa ni Mwenyezi Mungu ambae ana Ufalme wa mbungu na ardhi, kwasabaabu mwanadamu anajikurubisha kwa Mungu ambae anampa manufaa na anamkinga na madhara, na anamuondoshea shari na fitina, mambo haya hawezi kuyafanya yeyote isipokuwa Mfalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo, laiti ingekuwa kuna Miungu wengine pamoja nae kama wanavyo dai washirikina waja wangeliwafanya kuwa ni njia ya kuwafikisha katika ibada ya Mwenyezi Mungu Mfalme wa kweli, kwasababu wote wanao abudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu walikuwa wanamuabudu Mwenyezi Mungu na wanajikurubisha kwake, basi ni bora kwa mwenye kutaka kujikurubisha kwa ambae anamiliki manufaa na madhara amuabudu Mola wa kweli ambae ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, ikiwemo hiyo miungu inayo abudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangeli tafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi. ([29]) Na anaetaka haki asome kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipo kuwa kwa aliye mpa idhini. Hata itapo ondolewa khofu kwenye nyoyo zao watasema: Mola wenu Mlezi kasema nini?  Watasema: Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa. Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi?  Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi,([30]) hakika Aya hizi zinakata kufungamana moyo na kisichokuwa Mwenyezi Mungu:

(1) Hao wanao shirikishwa pamoja na Mwenyezi Mungu hawamiliki hata kiasi cha mdudu chungu, na asiyemiliki hata kiasi cha mdudu chungu hawezi kunufaisha wala kudhuru na wala hastahiki kuwa Mungu au kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye anae wamiliki na ndiye anae waendeshea mambo.

(2) Hakika wao hawamiliki chochote katika mbingu na ardhi, na hawana hata kiasi kidogo cha ushirikiano wao na Mwenyezi Mungu.

(3) Mwenyezi Mungu hana msaidizi katika viuumbe wake bali Yeye ndiye anaewasaidia katika yale yanayo wanufaisha, na anawakinga na yale yanayo wadhuru kwa ukamilifu wake na kuto wahitajia, bali wanadamu ndio wanao muhitajia Mola wao.

Hakika hao washirika hawawezi kuwaombea wafuasi wao kwa Mwenyezi Mungu wala hawapewi idhini ya uombezi, na Mwenyezi Mungu hawapi idhini ya uombezi isipokuwa vipenzi vyake, na Mawalii wa Mwenyezi Mungu hawamwombei isipokuwa yule aliyeridhiwa na Mwenyezi Mungu kauli yake, vitendo vyake na itikadi yake. ([31])

4-Kutengamaa mambo ya dunia nzima na mambo yake kufanywa kwa mpangilio ni dalili ya wazi kwamba anaepangilia ni Mwenyezi Mungu Mmoja na Mfalme Mmoja na Mola Mmoja, viumbe hawana Mungu mwingine na hawana Mola asiekuwa Yeye, kama inavyozuilika kupatikana waumbaji wengine katika dunia hii, vile vile haiwezekani kupatikana Miungu wawili, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika,([32]) lau kungesemwa kwamba katika mbingu na ardhi kuna Mungu asiyekuwa Allah basi zingeharibika, na namna ya kuharibika kwake: Ni kwamba kukiwa pamoja na Mwenyezi Mungu Mungu mwingine inalazimika kuwa kila mmoja miongoni mwao ni mwenye uwezo wa kuamua na kuendesha, basi katika hali hiyo utatokea ushindani na utaofauti, na kutatokea uharibifu na uovu.([33]) haiwezekani mwili kuendeshwa na roho mbili zinazo lingana, na ikitokea hivo basi mwili utaharibika na kuangamia, na hili ni jambo lisilo wezekana la kupatikana roho mbili katika mwili mmoja, kwanini watu wanajua kwamba roho mbili haziwezi kukaa katika mwili mmoja na wasijue kwamba haiwezekani kuwa na Miungu wawili.([34])

4. Kukubaliana Mitume juu ya hilo:

Umma unajikusanya kwa Manabii na Mitume wao ndio wakamilifu wa akili na nafsi zao zimetakasika na tabia zao ni bora na ni wenye kuwanasihi raia wao na ni wajuzi zaidi katika kuujua muradi wa Mwenyezi Mungu na ni waongofu zaidi kunako njia ya sawa na iliyonyooka, kwasababu wao wanapokea Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na wanaufikisha kwa watu, wamekubaliana Manabii wote na Mitume kuanzia kwa Nabii Adam alayhi salam mpaka kwa Mtume wa mwisho ambae ni Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake juu ya kuwalingania watu wao katika kumuami ni Mwenyezi Mungu na kuacha ibada ya asiyekuwa Yeye na Yeye ndiye Mola wa kweli, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu,([35]) na amesema Mwenyezi Mungu zimetukuka sifa zake kumwambia Nuhu alayhi salam, hakika alisema kuwaambia watu wake: Ili msimuabudu isipo kuwa Allah, Mwenyezi Mungu. Hakika mimi kwenu ni mwonyaji na mbashiri nitokae kwake,([36]) na amesema Mwenyezi Mungu kumwambia Mtume wa mwisho ambae ni Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake, hakika alisema kuwaambia watu wake: Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?.([37])

Mwenyezi Mungu huyu aliyeleta ulimwengu na akauweka vizuri, na akamuumba mwanadamu katika maumbile mazuri na akamkirimu, na akaweka katika maumbile ya mwanadamu kukiri Uungu wa Mwenyezi Mungu na ibada yake, na kaifanya nafsi ya mwanadamu isitulizane isipokuwa pale itakapo jisalimisha kwa Muumba wake, na ikapita katika njia yake, na roho yake isitulie isipokuwa itakapo tulizana kwa Muumba wake na ikafanya mawasiliano na Muumba wake, na haina mafungamano isipokuwa kupitia njia iliyo nyooka ambayo iliyofikishwa na Mitume watukufu, na akampa akili mambo yake hayanyooki wala hawezi kuifanyia kazi akili kwa ukamilifu zaidi isipokuwa atakapo muami ni Mola wake.

Maumbile yakiwa imara, na roho na nafsi vikatulizana, na akili ikaamini, basi ndipo anapopata mafanikio na amani na utulivu katika dunia na akhera. Na ikiwa mwanadamu atakataa yasiyo kuwa hayo ataishi bila umadhubuti na kuhangaika katika mabonde ya dunia, na anajigawa katika miungu ya duniani hajua nani atakaempa manufaa na nani atakaemkinga na madhara, na ili imani itulie katika nafsi yake na bainike uombezi wa kikafiri, Mwenyezi Mungu amelipigia jambo hilo mfano, kwasababu mfano ni katika vitu vinavyo leta maana katika akili, amelinganisha baina ya mtu ambae mambo yake ameyaweka katika miungu tofauti, na mwingine anamuabudu Mola wake peke yake akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanao gombana, na wa mtu mwengine aliye khusika na bwana mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao?  Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu! Lakini wengi wao hawajui.([38]) Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mja mwenye kumpwekesha na mja mwenye kumshirikisha, kapigia mfano wa mtumwa anaemilikiwa na washirika wengi wanazozana wao kwa wao kuhusu yeye, na yeye amejigawa kwa wote, na kila mmoja katika hao washirika amempa majukumu, na kila mmoja katika wao amempa kazi ya kufanya, na yeye ni mwenye kushangaa hajui amridhishe nani katika kutekeleza hayo majukum hatulii katika njia moja, wala hawezi kuwaridhisha hao washirika wake wanao zozana kutokana na wanayo yataka, kwasababu ya kutofautiana miongozo yao na nguvu zao! Na Mwenyezi Mungu akapiga mfano wa mtumwa mwenye bwana mmoja nae anajua yale anayo yataka bwana kwake na anayomuagiza atekeleze, mtumwa huyo amestrehe na ametulizana katika njia moja iliyo wazi. Basi hawawi sawa, huyu anamnyenyekea bwana mmoja na ananeemeka na raha ya msimamo katika kazi na maarifa na yakini, na yule mwingine ananyenyekea mabwana wanao zozana, basi yeye anateseka na ana dhiki hatulizani katika hali moja, wala hawezi kumridhisha mmoja achilia mbali na kuwaridhisha wote.

Na baada ya kuweka wazi dalili zinazo onyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu na Uungu wake na ibada zake, inapendeza tujue juu uumbaji wake wa ulimwengu na binadamu, na tujue hekima yake katika hilo.

 Kuumbwa Kwa Ulimwengu

Huu ulimwengu na mbingu zake na ardhi zake na nyota zake na sayari zake na bahari zake na miti yake na wanyama wake, Mwenyezi Mungu kaviumba kutokana na kutokuwepo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika?  Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza. Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu. Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua.([39])

Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua?  Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai?  Basi je, hawaamini?  Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka. Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake.([40])

Ulimwengu huu ameuumba Mwenyezi Mungu kwa hekima kubwa zisizo hesabika kila kipande katika dunia kina hekima kubwa na Aya zilizo wazi, lau ukizingatia Aya moja katika dunia utakuta kuna maajabu, angalia maajabu ya utengenezaji ya Mwenyezi Mungu katika mimea ambayo kila jani au mzizi au tunda haukosi kuwa na manufaa ambayo akili za mwanadamu haziyajui na upambanuzi wakena angalia mapito ya maji katika mishipa myembamba midogo na dhaifu ambayo haiwezi kuonekana kwa macho isipokuwa kwa kuangalia kwa makini, vipi inakuwa na uwezo wa kuvuta maji kutoka chini kwenda juu!, kisha maji yanahama katika yale mapito yake kutokana na uwezekano wa kupita na upana wake, kisha hiyo mishipa inasambaa na kuwa mingi kiasi ambacho macho hayawezi kuiona, kisha tazama namna miti inavyo beba mimba na kubadilika kutoka katika hali na kwenda katika hali nyingine, ni kama vile anavyo mtoto anavyo badilika katika tumbo la mama yake kutoka katika hali kwenda katika hali nyingine bila kuonekana. Unaweza ukaona mti kama uko uchi hauna nguo kumbe Mwenyezi Mungu Mola wake na Muumbaji wake kauvisha kutokana na majani nguo iliyo bora, kisha akatoa ndani ya mti huo mimba dhaifu baada ya kuyatoa majani yake kwa ajili ya kuulinda, na nguo za hayo matunda dhaifu ili yafunikwe kutokana na joto na bardi na maafa, kisha Mwenyezi Mungu akapeleka katika yale matunda rizki yake na kuyalisha kupitia mishipa na sehemu nyinginezo za kupitishia chakula kama anavyo kula mtoto maziwa ya mama yake, kisha Mwenyezi Mungu akayalea na kuyakuza mpaka yaka sawa sawa na yakakamilika, basi akayatoa hayo matunda yakiwa matamu na laini kutokana na mti mgumu.

Na ukiitazama ardhi na jinsi ilivyo umbwa utaona ni katika alama kubwa ya aliyeiumba na akaifanya vizuri, Mwenyezi Mungu kaiumba ikiwa imetandikwa na imetengenezwa vizuri na akaifanya ni dhalili kwa waja wake, na akajaalia ndani yake rizki zao na vyakula vyao na maisha yao, na akajaalia ndani yake njia ili wapite wakiwa katika shida zao na shughuli zao, na akaitia umadhubuti kwa kuiwekea milima akifanya kuwa vigingi vinavyo ihifadhi ili isiyumbe, na akaupanua wigo wa ardhi na kuufanya mpana na akaifanya ni yenye kukusanya vilivyo hai juu ya mgongo wake, na yenye kukusanya vilivyo kufa katika tumbo lake, basi mgongo wake ni maskani ya walio hai na tumbo lake ni maskani ya waliokufa, kisha tazama kunako mbingu iliyozungukwa na jua, mwezi, nyota na sayari zake, ni namna gani vinauzunguka ulimwengu kwa mzunguko huu wenye kudumu mpaka mwisho wa dunia kwa utaratibu huu na nidhamu hii, na yaliyomo katika jumla ya hayo miongoni mwa kutofautiana kwa usiku na mchana na nyakazi za joto na baridi na yaliyomo katika hayo miongoni mwa manufaa yaliyopo juu ya ardhi miongoni mwa aina tofauti za wanyama na mimea.

Kisha zingatia katika kuumbwa kwa mbingu, kisha rejesha macho mara kwa mara utaiona ni alama kubwa katika kuwa juu na upana wake na kutulizana kwake, hakuna nguzo chini yake wala kilichoishika kwa juu, bali imeshikwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ambae ndiye anaezishika mbingu na ardhi ili zisiondoke.

Na wewe ukiutizama ulimwengu huu na sehemu zake zilivyowekwa na namna ulivyo pangiliwa kwa mpangilio wake mzuri inaonyesha juu ya ukamilifu wa uwezo wa Muumbaji, na ukamilifu wa kazi yake, hekima yake na upole wake, na utakuta ulimwengu ni kama vile nyumba iliyoandaliwa ndani yake vifaa vyote na maslahi yakena kila kinacho hitajika ndani yake, basi mbingu sakafu yake imenyanyuliwa na ardhi imetandikwa imetulizana kwa wenye kuishi, na jua na mwezi ni taa mbili zinazo ipamba mbingu, na nyota ni taa zinazo ipamba mbingu, na dalili (na mwongozo) kwa mwenye kusafiri katika dunia hii, na madini na vitu vyenye thamani vilivyo wekwa ndani yake ni kama vile vimeandaliwa kwa kazi maalum, kila kitu kina kazi yake maalum, na aina za mimea zimeandaliwa kwa kazi yake, na aina za wanyama wanatumiwa kwa maslahi tofauti miongoni mwao kuna vipandwa, na wengine ni wa maziwa, na wengine ni wa kuliwa, na wengine ni kwa ajili ya mavazi, na wengine nikwa ajili ya ulinzi. Na akamuweka mwanadamu kama vile mfalme katika vitu hivyo anaevitumia katika dunia kwa matakwa yake na amri zake.

Na wewe laita utazingatia katika ulimwengu huu au sehemu katika ulimwengu huu utakuta kwamba kuna maajabu, na laity utaangalia kwa makini na ukawa muadilifu katika nafsi yako na ukaacha kufuata matamanio na kuiga, utayakinisha ukweli wa yakini kwamba ulimwengu huu umeumbwa, ameuumba Mwenye hekima, Muweza na Mwenye ujuzi, na akaukadiria makadirio mazuri na akaupangilia mpangilio ulio mzuri, na hakika aliyeumba ulimwengu haiwezekani kuwa ni wawili, bali ni Mola Mmojahapana apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye,na laiti kungekuwa katika mbingu na ardhi Mungu asiyekuwa Yeye basi mambo ya mbingu na ardhi yange haribika na nidhamu zinge vurugika na maslahi yangeisha.

Ukilikataa hilo na ukanasbisha kuumba kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, unasemaje kuhusu sanduku linalo elea juu mto vifaa vyake na mpangilio wake viko madhubuti, kiasi kwamba mwenye kulitazama haoni aibu yoyote kwenye sanduku lenyewe au muonekano wake, kisha likawekwa kwenye bustani kubwa ndani yake kuna kila aina ya matunda anayo yahitaji, na katika hiyo bustani kuna anaesambaza mambo yake na kuichunga na kuna anaesimamia maslahi yake yotehakuna kitu kinacho vuruga wala kuharibu matunda yake, kisha anagawa thamani yake wakati wa kuvuna kwa watu wengine kulingana na shida zao na dharura zao, kila aina na stahiki yake na siku zote anagawa hivo.

Je inawezekana watu wakakubaliana kuwa haya yanaweza kutokea bila ya mtengenezaji wala mpangiliaji? Bali wamekubaliana kupatikana sanduku na bustani, ya kwamba yote hayo yapatikane bila ya mtengenezaji wala mpangiliaji? Ingekuwaje kama akili yako ingekwambia hivo? Na ni nani atakupa hiyo fat'wa? Na ni nani aliyekuongoza kulijua hilo? ([41]).

 Hekima Ya Kuumbwa Kwa Ulimwengu

Baada ya kupata mazingatio katika kuumbwa kwa ulimwengu inapendeza tukataja baadhi ya hekima ambazo kwa ajili yake Mwenyezi Mungu ameumba viumbe hivi vikubwa na alama zilizokuwa wazi, na miongoni mwa hekima hizo:

1-Ni kumdhalilishia mwanadamu: pindi alipo hukumu Allah kuweka katika Ardhi kiongozi atakae muabudu ndani yake, na kuijenga Ardhi, alimuumbia yote hayo, ili maisha yake yawe imara na maisha yake yatengamae na maskani yake, anasema Allah Mtukufu: Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake.[42] Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni. a akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu. Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.([43])

       2- Iwe Mbingu na Ardhi na vilivyomo Ulimwenguni ni ushahidi wa Uungu wake na ni dalili ya Upweke wake:

kwa sababu mambo makubwa yaliyopo katika dunia hii ni mtu kukiri Uungu wa Allah na kuamini Upweke wake Allah, na kwasababu hilo ni jambo kubwa ndio maana Allah ameliwekea ushahidi mkubwa, na akaliwekea dalili kubwa na hoja zilizo wazi, akaweka Allah Mbingu na Ardhi, na viumbe vingine vilivyopo ili iwe ni ushahidi juu ya kuwepo kwa Allahkwa sababu hiyo ndio maana imekithiri katika Qur'an neno (Na miongoni mwa alama zake) kama ilivyo kuja katika kauli yake Allah Mtukufu: Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchanaNa katika Ishara zake hukuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na tamaaNa katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake.([44])

3- Ili iwe ni ushahidi wa kufufuliwa: wakati ilipokua maisha ni aina mbili, maisha ya Duniani na ya Akhera,na maisha ya akhera ndio yenye uhakika, alisema Allah Mtukufu: Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!([45]) Kwa hakika ni nyumba ya malipo na hesabu, na kwasababu ndani yake kuna kuishi milele ima katika neema mbali mbali kwa wenye kufanya mema, au kuishi katika adhabu kwa wenye kufanya maovu.

Na ilipokua nyumba hii ya Akhera hakuna mwenye kuifikia ila ni baada ya kufa na kufufuliwa baada ya kufa, alikanusha kila asie muamini Allah na zikabadilika fikra zake na kuharibika akili yake, kwa sabau hiyo Allah aliweka hoja na dalili za wazi, ili uamini kuwa kuna kufufuliwa watu, na uyakinishe kwa moyo, kwasababu kumrejesha kiumbe ni rahisi kuliko kumuumba kwa mara ya kwanza, bali kuumba Mbingu na Ardhi ni kukubwa kuliko kurudia kumuumba mwanadamu.Amesema Allah Mtukufu: Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake.([46]) Na amesema Allah Mtukufu: Bila ya shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu.([47]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona, ametawala kwenye Ufalme wake, na amefanya jua na mwezi yamt'ii, kila kimoja kinakwenda kwa kiwango maalumu. Anayapanga mambo, na anazipambanua Ishara ili mpate kuwa na yakini kukutana na Mola wenu Mlezi.([48])

 Baada ya kusema hayo enyi watu:

Itakapo kua ulimwengu huu wote umedhalilishwa kwa ajili yako wewe, na ikiwa dalili zote na ushahidi vimewekwa mbele ya macho yako ili ushahidilie kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah peke yake hana mshirika, na ukijua kuwa maisha yako baada ya kufufuliwa ni wepesi zaidi kwa Allah kuliko kuumbwa Mbingu na Ardhi, na kwamba wewe utakutana na Mola wako na atakuhesabia matendo yako, na ukijua kuwa ulimwengu wote unamuabudu Mola wake kila kiumbe kina muabudu Allah na kina mtukuza Allah, anasema Allah Mtukufu: Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima,([49]) Na vinamsujudia kwa utukufu wake, anasema Allah Mtukufu: Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu,([50]) Bali hivi viumbe vina swali kwa mola wake swala inayo nasibiana na viumbe hivyo, anasema Allah Mtukufu: Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu vinamtakasa vilivyomo katika mbingu na ardhi, na ndege wakikunjua mbawa zao?  Kila mmoja amekwisha jua Sala yake na namna ya kumtakasa kwake.([51])

Ikiwa mwili wako unaenda kwa mpangilio wake kama alivyo upangilia Allah moyo na mapafu mawili na ini na baki ya viungo vingine vinakuwa vimejisalimisha kwa Mola wake, vimejisalimisha viongozwe na aliye viumba.Yanaweza kuwa maamuzi yako ya kujitakia ambayo uliyo yachagua wewe baina ya kumuamini Mola wako, na kumkufuru,maamuzi hayo yaliyo kwenda kinyume na mwenendo alio uweka Mola wako wenye Baraka katika ulimwengu na katika mwili wako, yakawa ndiyo chaguo lako!

Hakika mwanadamu mwenye akili iliyo kamilika anaiweka mbali nafsi yake isiende kinyume na maadili katika ulimwengu huu mkubwa.

 Kuumbwa Kwa Mwanadamu Na Kukirimiwa

Alihukumu Allah mtukufu kuwaumba kiumbe ili kuimarisha ulimwengu huu, na kiumbe huyo ni mwanadamu, na ikapelekea hekima yake Allah mtukufu kuwa vifaa vya kumuumbia mwanadamu ni Ardhi, akaanza kumuumba kutokana na udongo, kisha akamuumba kwa picha hii nzuri ambayo anaonekana nayo mwanadamu, na alipo stawi na kutengamaa katika kukamilika kwa maumbile yake, alimpulizia roho, ghafla akawa mtu alie umbika katika maumbile mazuri, anasikia na anaona na anatembea na kuzungumza, Mola wake mlezi akamuweka peponi, na akamuelimisha yote anayo hitajia kuyafahamu, na akamuhalalishia kila vilivyomo peponi, na akamkataza aikurubie mti mmoja - kwa lengo la kumpa mtihani na majaribio- na Allah akataka kuonyesha cheo chake na daraja lake, akaamrisha malaika wake wamsujudie, wakasujudu malaika wote, ispokuwa Iblisi alikataa kumsujudia kwa kiburi na jeuri, Mola wake akamkasirikia, kwa kukhalifu amri yake, na akamfukuza katika rehma zake, kwasababu alimfanya jeuri Mola wake, akaomba iblisi kwa Mola wake ampe umri mrefu na ambakishe mpaka siu ya Qiyama, Allah akampa umri mrefu mpaka siku ya Qiyama, Shetani akamhusudu Adam, wakati Allah alipo mfadhilisha yeye na kizazi chake, na akamuapia kwa Mola wake kuwa atawapoteza kizazi chake chote, na kwamba atawaendea mbele yao na nyuma yao na kuliani mwao na kushotoni mwao, ila kwa waja wa Allah wenye ikhlasi wakweli na wacha Mungu, hakika Allah mtukufu atawahifadhi na vitimbi vya shetani, Allah mtukufu akamtahadharisha Adam kutokana na vitimbi vya Shetani, Shetani akamshawishi Adam na mke wake Hawa, ili awatoe katika pepo, na ili awavue nguo, na akawaapia kuwa yeye anawapa nasaha, na kwamba Allah hakuwakataza mti ule ila kwa sababu mkila mtakuwa malaika au mtaishi milele.

Wakala kutokana na ule mti ambao alio wakataza Allah Mtukufu, basi ikawa jambo lakwanza lililo wapata katika adhabu ya kuasi amri ya Allah, ziliwadondoka nguo, Allah akawakumbusha kuwa aliwatahadhalisha kutokana na vitimbi vya Shetani, Adam akaomba msamaha kwa Mola wake Allah akamkubalia tawba yake na akamsamehe akamtakasa na akamuongoza, akamuamrisha ashuke kutoka katika pepo aliyo kuwa anaishi aende Ardhini, ambapo ni makazi yenye utulivu, na ndani yake kuna chakula chake kwa mda maalum, na akamueleza kuwa ameumbwa kutokana na Ardhi na ataishi juu ya ardhi na katika Ardhi atakufa na atafufuliwa kutoka katika Ardh.

Akashuka Adam Ardhini yeye na mke wake Hawa, wakazaana, na walikuwa wakimuabudu mwenyezi mungu kulingana na alivyo waamrisha, kwani Adam alikuwa ni Nabii.

Ametueleza Allah habari hii pale aliposema: Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipokuwa Ibilisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha?  Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo. Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe u miongoni mwa walio duni. Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa. Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula. Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani. Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote. Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu. Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele. Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini. Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri. Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika. Akasema: Teremkeni! Mtakuwa nyinyi kwa nyinyi maadui. Na kwenye ardhi itakuwa ndio makao yenu na starehe yenu mpaka ufike muda. Akasema: Humo mtaishi, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa.([52])

Na wakati unapo zingatia ukubwa Allah katika kumtengeneza mwanadamu, pindi alipomuumba kwa umbo zuri, na akamvisha nguo ya utukufu kutokana na: akili, elimu, ubainifu, kutamka, maumbile, sura nzuri, umbo tukufu, mwili wa kati na kati na kupata elimu kwa dalili na kufikiria, na kuchuma tabia nzuri na bora kutokana na wema na utiifu na kutekeleza, ni mara ngapi katika hali yake akiwa tone la manii katika kizazi akiwa amewekwa, na akiwa katika hali yake katika pepo ya milele na Malaika akiingia kwao? Ametukuka Mwenyezi Mungu mbora wa waumbaji. ([53])

Dunia ni kijiji na mwanadamu ndiye anayeishi katika kijiji hicho, kila mtu ameshughulika na dunia anaenda mbio katika maslahi yake, na kila mmoja anaitumikia na dunia na shida zake, na Malaika wamewakilishwa kwake wanamuhifadhi usiku na mchana, na kuna Malaika waliowakilishwa kwa mvua na mimea wanafanya bidii katika rizki ya mwanadamu na wanaitumikia, na sayari zimedhalilishwa zikifuata yale yenye maslahi kwa mwanadamu, na jua na mwezi vimelainishwa vinakwenda kwa hesabu ya muda wake na wakati wake, na kutengeneza mpangilio wa chakula chake, na ulimwengu wa anga umedhalilishwa kwake kwa upepo na hewa yake na mawingu na ndege zake na vile vilivyowekwa katika mawingu, na ulimwengu wa ardhini wote umelainishwa kwake, umeumbwa kwa maslahi yake, ardhi yake na milima yake na bahari zake na mito yake, miti yake na matunda yake, mimea yake na wanyama wake, na vyote vilivyomo katika ardhi, kama alivyosema Allah: Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni. a akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu. Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema.([54]) Na katika ukamilifu wa kumkirimu mwanadamu ni kwamba kamuumbia yote anayoyahitaji katika maisha ya dunia, na yale anayoyahitaji katika mambo ambayo yatamfikisha katika daraja la juu Akhera, akamteremshia vitabu na akamtumia Mitume wakimbainishia sheria ya Allah na wanamlingania aifuate.

Kisha Allah akamuumbia kutokana na nafsi yake (yaani katika nafsi ya Baba yetu Adam) mke ili apate utulivu kwake, akiwa ni mwenye kuitikia haja zake za kimaumbile, na za kinafsi, za kiakili na za kimwili, ili apate kwake raha na utulivu, na ili wapate utulivu, mapenzi na huruma kwa kuwa kwao pamoja, kwasababu mpangilio wao wa kimwili na wa kinafsi ni vyenye kuhitajiana, ili kuanzisha kizazi kipya, na zimewekwa hisia hizo katika nafsi zao na kufanywa ndio utulivu wa nafsi na raha ya kiwiliwili na moyo, na akajaalia umoja ndio utulivu wa uhai na maisha, na ni burudani kwa nyoyo na dhamira, na ndio utulivu wa mwanaume na mwanamke unaolingana.

Na Allah akawahusisha Waumini baina ya wanadamu akawafanya ndio wenye kustahiki uongozi akawatumia katika twaa yake, wanamfanyia kazi kutokana na sheria yake, ili wawe ni wenye kustahiki kuwa karibu na Mola wao katika pepo yake, alichagua miongoni mwao mwawalii, na mashahidi, na Manabii, na Mitume na akawapa katika dunia hii neema kubwa ambayo nafsi zina neemeka kwayo nayo ni kumuabudu Allah na kumtii, na kumnyenyekea,na akawahusisha na neema kubwa ambayo hawaipati neema hiyo isipokuwa waislamu, miongoni mwa neema hiyo ni amani na utulivu na mafanikio, bali kubwa kuliko hilo ni kwamba wao waijua haki waliyokuja nayo Mitume na wanaiamini, na amewahifadhia katika nyumba ya Akhera miongoni mwa neema za milele na kufaulu kuliko kukubwa yale yanayoendana na ukarimu wake Allah Mtukufu, na atawapa malipo kwa kumuamini na kumtakasia ibada.

 Cheo Cha Mwanamke

Amefikia mwanamke katika uislamu cheo cha juu, ambacho hakijafikiwa na dini zote zilizopita, wala umma utakaokuja hautakifikia cheo hicho, kwani uislamu katika kumkirimu mwanadamu kunashirikiana ndani yake mwanaume na mwanamke, wao mbele ya hukumu za Allah katika dunia wako sawa kama walivyo sawa katika kulipwa thawabu na malipo Akhera, amesema Allah Mtukufu: Na hakika tumewatukuza wanaadamu.([55]) Na amesema Mwenyezi Mungu: Wanaume wana sehemu katika wanayo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Na wanawake wanayo sehemu katika waliyo yaacha wazazi na jamaa walio karibia.([56]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Nao wanawake wanayo haki kisheria kama ile haki iliyo juu ya wanaume kwa wema.([57]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki.([58]) Na amesema Allah Mtukufu: Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.([59]) Na alisema Allah Mtukufu: Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke.([60]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.([61]) Na amesema Mwenyezi Mungu: Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende.([62])

Na hii takrima ambayo aliyoipata mwanamke katika uislamu haina mfano katika dini yoyote au mila au kanuni, utamaduni wa Romania umekiri kuwa mwanamke ni mtumwa wa mwanaune, na wala mwanamke hana haki yoyote, na walikusanyika katika mji wa Roma mkutano mkubwa na wakafanya utafiti kuhusu mambo ya mwanamke, wakatoa maamuzi ya kwamba mwanamke ni kiumbe asiyekuwa na nafsi na kwamba mwanamke kwasababu hiyo hataweza kupata maisha ya Akhera, na yeye ni uchafu.

Na alikuwa mwanamke katika mji wa Athens kusini mwa Ugiriki anahesabika kama mzigo usio na thamani, alikuwa anauzwa na kununuliwa, na alikuwa anahesabika ni uchafu na katika kazi za Shetani.

Na sheria za kihindi za zamani zilipitisha: Kwamba msiba na kifo na moto na sumu ya nyoka ni bora kuliko mwanamke, na ilikuwa haki yake ya kuishi inaisha kwa kufariki mume wake ambae ndiye bwana wake, mwanamke anapoona kiwiliwili cha mume wake kinaunguzwa anajitupa katika ule moto, na kama hakufanya hivo basi anakuwa ni mwenye kustahiki laana.

Ama mwanamke katika Uyahudi imekuja hukumu yake katika agano la kale kama ifuatavyo: "Nimezunguka mimi na moyo wangu ili nijue na nitafute hekima na akili, na nijue kuwa shari ni ujinga na upumbavu kuwa ni wendawazimu, nikakuta jambo chungu kuliko kifo: Mwanamke ambae yeye ndio mtego, na moyo wake ndio shirika, na mikono yake ndio kamba" ([63]).

Huyo ndiyo mwanamke katika enzi za zamani, ama hali yake katika zama za kati na zama za sasa ufafanuzi wake ni kama ifuatavyo:

Sherhe ya kitabu cha mtu wa Denmark kiitwacho (Wieth kordsten), mwelekeo wa kanisa Katoliki kuhusu mwanamke alisema: "Katika zama za kati thamani ya mwanamke wa Ulaya ilikuwa ni ndogo sana kwa kufuata mwongozo wa madhehebu ya Katoliki ambayo yalikuwa yakimuhesabu mwanamke kuwa ni kiumbe wa daraja la pili" na katika nchi ya Ufaransa kiliwekwa kikao mwaka wa 586M, kilichokuwa kikizungumzia mambo ya mwanamke na usahihi wake kuwa ni binadamu au sio binadamu? Na baada mjadala wajumbe waliohudhuria walipitisha kwamba mwanamke ni binadamu na ameumbwa ili amuhudumie mwanaume.Na katika katiba ya nchi ya Ufaransa mada ya 217 imetaja yafuatayo: "Mwanamke aliyeolewa hata kama ndoa yake imesimamia msingi wa kila mmoja kuwa na mamlaka ya kumiliki vitu vyake mwenyewe haijuzu kwa mwanamke kutoa chochote au kuhamisha umiliki au kuweka rehani au kumiliki kitu kwa badala au bila ya badala bila ya kumshirikisha mume wake katika makubaliano au mume kukubali kwa maandishi".

Na katika nchi ya Uigereza Mfalme wa nane aitwae (Henry V11) aliharamisha (alikataza) juu ya mwanamke wa Kiingereza kusoma Biblia, wakabaki wanawake bila ya kusoma Biblia mpaka mwaka 1850 hawahesabiki kuwa ni wananchi na wakabaki hivo mpaka mwaka 1882 wakiwa hawana haki za kibinadamu ([64]).

Ama wanawake wa kisasa katika nchi za Ulaya na Amerka na nyenginezo katika nchi za Scandinavia, ni viumbe wasio na thamani wanaotumika kwa malengo ya biashara, kwani yeye ni sehemu katika mabango ya matangazo, bali imefikia hali ya kuvuliwa nguo zake ili kuonyeshewa biashara, na kiwiliwili chake kimehalalishwa na heshima yake pia kufuatia nidhamu zilizopitishwa na wanaume ili awe ni chombo cha starehe katika kila sehemu.

Naye mwanamke ndiye anaesaidia kwa muda ambao anaweza kutoa kwa mkono wake au fikra yake au mwili wake, anapokuwa mkubwa na akakosa cha kutoa jamii na taasisi vinamuacha, na anaishi peke yake katika nyumba yake, au kujitegemea mwenyewe.

Alilinganisha haya -lakini akuna usawa wa hayo- na yaliyokuja katika Qur'an Tukufu kutoakana na kauli yake Allah Mtukufu: Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki.([65]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Nao wanawake wanayo haki kisheria kama ile haki iliyo juu ya wanaume kwa wema.([66]) Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtufu: Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni ([67]).

 Mwenyezi Mungu wakati alipomkirimu mwanamke kwa takrima hii aliweka wazi kwa viumbe wote kwamba Yeye alimuumba mwanamke ili awe Mama na awe mke, na awe binti na dada, kwa ajili hiyo Allah akaweka sheria zinazomuhusu mwanamke kinyume na mwanaume.

  

 Hekima Ya Kuumbwa Kwa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu Mtukufu ana hekima nyingi katika hilo ambazo akili haziwezi kujua wala ndimi kuzielezea sifa zake, na tutaeleza katika yanayokuja baadhi ya hekima hizo:

1.Ni kwamba Allah ana majina mazuri, na miongoni mwa majina Yake: Al Ghafur, Al Rahim, Al A'fuw, Al Halim,…Na ni lazima zionekane athari za majina hayo, ikawa hekima ya Allah ni kumteremsha Adam na kizazi chake katika nyumba ambayo itaonekana juu yao katika nyumba hiyo athari za majina mazuri, ili amsamehe amtakae na amhurumie amtakae na mengineyo yanayoonyesha kuonekana athari za majina ya Allah na sifa zake.

2.Ya kwamba Allah Mtukufu ni Mfalme wa kweli na mwenye kubainisha, na Mfalme ni yule ambae anaamrisha na kutakataza, na anatoa thawabu na anaadhibu na anamdhalilisha mtu na kumkirimu, na anampa mtu nguvu na anadhalilisha, ukapelekea Ufalme wake Allah kumteremsha Adam na kizazi chake katika nyumba ambayo itakuwa inapitia juu yao hukumu za Mfalme, kisha anawahamisha katika nyumba nyingine atakayo walipa ibada zao.

3.Ya kwamba Allah Mtukufu alitaka kuwafanya miongoni mwao Manabii na Mitume na Mawalii na Mashahidi ili awapende na wao wampende, Allah akawaacha baina yao na baina ya maadui zao na akawapa mtihani kwa hao maadui, pindi walipo mfadhilisha na wakatoa nafsi zao na mali zao kwa kutaka radhi zake na mapenzi yake, waliyapata mapenzi ya Allah na radhi zake na ukaribu wake ambayo asingeweza kuyapata yeyote bila ya mitihani hiyo, basi cheo cha Utume na Unabii na Shahada ni katika daraja bora kwa Allah, na mwanadamu hawezi kuyapata hayo isipokuwa kwa namna hiyo aliyoihukumu Allah Mtukufu ya kuteremsha Adam na kizazi chake ardhini.

4.Nikwamba Allah alimuumba Adam na kizazi chake kutoka na mpangilio unaokubali kufanya kheri na shari, na unaolazimu kuwa na matamanio na kuwa na fitna, na wenye kupelekea kuwa na akili na ujuzi, hakika Yeye Allah Mtukufu aliumba katika kiwiliwili cha mwanadamu akili na matamanio na akaviweka ili mwanadamu awe na akili na aweze kutamani ili makusudio ya Allah ya kuviweka yatimie, na awaonyeshe waja wake utukufu wake na nguvu zake na huruma yake, na wema wake na upole wake katika utawala wake na Ufalme wake, ikawa ndiyo hekima yake ya kumteremsha Adam na kizazi chake ardhini, ili mtihani ukamilike na zionekane athari za maandalizi ya mwanadamu kwa madai hayo, na kuyatekeleza na kumkirimu au kumfedhehesha.

             5-Nikwamba Allah Mtukufu aliumba viumbe ili wamuabudu, nayo ndiyo makusudio ya kuwaumba, amesema Allah Mtukufu: Sikuumba majini wala watu ila ni kwa lengo la kuniabudu,([68]) na inajulikana kwamba ukamilifu wa Utumwa unaotakiwa kwa viumbe haupatikani katika nyumba yenye neema isiyoondoka, hakika hayo yanapatikana katika nyumba ya shida na balaa, ama nyumba ya kudumu hiyo ni nyumba neema na ladha na siyo nyumba ya mitihani na majaribio.

6.Kuamini ghaibu ndiyo imani yenye manufaa, ama kuamini kwa kuona hakuna manufaa kwasababu siku ya Qiyama watu wote wataamini:

laiti kama wangeumbwa katika neema wasingepata daraja ya kuamini ghaibu ambayo yenye ladha na utukufu unaopatikana kwasababu ya kuamini ghaibu, kwasababu hiyo Allah alimteremsha Adam na kizazi chake duniani ili wapate kuiamini ghaibu.

7.Yakwamba Allah alimuumba Adam alayhi salam kutokana na mkusanyiko wa udongo wote wa ardhi, na ardhi ndani yake kuna udongo mbaya na mzuri na kuna huzuni na furaha, Allah Mtukufu akajua kwamba katika kizazi cha Adam kuna ambae hafai kuishi nae katika nyumba yake (pepo), akamteremsha duniani na wakazaliwa ndani yake wema na waovu, kisha Allah akawapambanua kwa nyumba mbili: Akawafanya watu wema wawe jirani na Adam na waishi nae, na akawafanya watu waovu wawe katika nyumba ya uovu na uchafu.

8.Yakwamba Allah Mtukufu kwa kuwaumba wanadamu alitaka awajue watu wema aliowaneemesha ili awapende zaidi na awape neema mabali mbali, akawaonyesha aina tofauti za neema ili wawe na furaha kubwa na waonewe wivu, huko ndiko kukamilika kwa neema za Allah juu yao, na Allah akataka awaadhibu walio maadui ikawa hakuna budi lazima wateremke ardhini ili wapewe mtihani na wachaguliwe, na awape taufiq wale anaowataka miongoni mwao kwa huruma yake, na awaache kwa kuwatelekeza anaowataka miongoni mwao kwa hekima yake na uadilifu wake. Naye ni Mjuzi na mwenye hekima.

9.Yakwamba Allah alitaka Adam na kizazi chake warudi peponi wakiwa katika hali nzuri, akawaonjesha kabla ya hapo tabu za duniani na shida zake na masononeko yake yatakayo wafanya waone kuingia peponi kwao ni jambo kubwa.([69])

Baada ya kuwa nimebainisha mwanzo wa mwanadamnu inapendeza pia nibainishe uhitajio wa mwanadamu dini iliyo sahihi.

 Wanadamu Kuihitajia Dini

Watu wanahitajia dini zaidi kuliko mahitaji mengine ya dharura katika maisha, kwasababu mwanadamu ni lazima ajue mambo yanayo mridhisha Allah na mambo yanayo muudhi, na ni lazima apate msukumo unaomletea manufaa na unamzuia na madhara, na sheria ndiyo inayopambanua baina ya vitendo vyenye manufaa na vyenye madhara, na sheria ni uadilifu wa Allah kwa viumbe wake na ni nuru baina ya waja wake, haiwezekani kwa watu kuishi bila sheria inayofanya wapambanue yanayopaswa kufanywa na yasiyopaswa kufanywa.

Na mwanadamu akiwa anahitaji ni lazima ajue anahiji nini, je! Anachokitaka kina manufaa au kina madhara? Je! Kinamfaa au kinamuharibu? Na hayo wanaweza kuyajua baadhi ya watu kwa maumbile yao na baadhi yao wanajua kwa kutumia dalili za kiakili na wengine wanayajua kwa kufahamishwa na Mitume wanapo wabainishia na kuwapa mwongozo. ([70])

Vyovyote watakavyo tangaza watu wenye mitazamo ya kumkanusha Allah na wakapambia mambo yao, na vyovyote zitakavyo kuwa nyingi fikra na mitazamo hazitawatosha watu na jamii kutokana na kupata dini sahihi, na fikra hizo hazitaweza kukidhi mahitaji ya moyo na kiwiliwili, bali mtu kila anapozama katika fikra hizo anapata yakini ya kwamba hazimpi amani wala hazimkati kiu na kwamba hakuna makimbilio isipokuwa katika dini sahihi, nasema Ernest Renan: (Hakiaka inawezekana kudhoofika kila kitu mtazamo wake, na kubatilika uhuru wa kutumia akili na elimu na ubunifu, lakini haiwezekani kufutika dini, na itabaki ni yenye kutamka juu ya ubatilifu wa mitazamo ya wasiomuamini Allah na Dini ambayo inataka kumzingira mtu aonekane anaishi katika dhiki ya kidini kwa sababu ya maisha ya duniani) .([71])

Anasema Muhammad Farid Wajdiy: (Haiwezekani kuondoka fikra ya dini kwasababu ndio kitu kinachofuatwa na nafsi zaidi na kupendwa, ukiachilia mbali na mtu kujivunia dini, Bali maumbile ya dini yatakutana na mtu kwa muda ambao ana akili na anajua kitu kizuri na kibaya, na yatazidi maumbile haya kwa kiwango cha juu kila yanapozidi maarifa yake. ([72])

Mwanadamu anapojiweka mbali na Mola wake kutokana na ufahamu wake na kupanuka Nyanja za elimu yake ndipo anapojua ukubwa wa yeye kutomjua Mola wake na anayopaswa kumfanyia Mola wake, na kutoijua nafsi yake na yale yanayoifaa nafsi au kuharibu, na kuifanyaiwe njema na iwe mbaya, na kutokujua kwake mambo ya kisayansi kama vile elimu ya sayari na njia zake, na elimu ya hesabu na mengineyo… Na wakati huo anajirudi mwanachuoni kutoka katika daraja la kujikweza na kuwa na kiburi na kuwa ni mnyenyekevu na mwenye kujisalimisha, na kuamini kuwa kila elimu ina mjuzi mwenye hekima, na nyuma ya kila kichopo duniani kuna Muumbaji na mwenye kukipangilia, na ukweli huu unamlazimu mwenye kufanya utafiti wa mambo haya aamini mambo ya ghaibu na kufuata dini ya kweli na awe ni mwenye kuitikia wito wa maumbile ya asili katika nafsi yake…Na mwanadamu anapoachana na hayo maumbile yake yanageuka na kuwa kama mnyama.

Na tunahitimisha hayo kwa kusema kwamba hakika dini ya kweli ambayo imeegemea juu ya mwanadamu kumpwekesha Allah na kumuabudu Yeye kulingana na sheria yake ni jambo la msingi na la lazima katika maisha ili mtu atomize kupitia ibada hiyo utumwa wake kwa Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote,ili naweze kupata mafanikio na amani kutokana na maangamizi na tabu na uovu Duniani na Akhera, nalo ni jambo la muhimu ili kukamilisha nguvu za mtazamo kwa mwanadamu, kwasababu ya dini peke yake ndio akili inashiba na ikikosekana dini akili haipati matarajio yake.

Na Dini ni jambo la muhimu kwa ajili ya kuitakasa roho na kupangilia nguvu za mwili, kwani fikra njema zinapata nafasi yenye athari katika Dini.

Dini ni jambo la muhimu kwa ajili ya kukamilisha nguvu za matashi na kuepukana na sababu zinazovunja nguvu na kukatisha tama.

Kwasababu hiyo ikiwa kuna anaesema kuwa mwanadamu asili yake ni kuishi na watu, basi tunatakiwa tuseme kwamba mwanadamu anahitaji dini kwa maumbile yake.([73]) Kwasababu mwanadamu ananguvu mbili, ananguvu ya elimu ya mtazamo na ananguvu ya elimu ya utashi, na mafanikio yake yaliyokamilika yamesimamishwa juu ya kukamilika nguvu ya maarif na utashi, na uhakika wa nguvu zake za kielimu haukamiliki isipokuwa kwa kufahamu mambo yafuatayo:

1.Kumjua Mola Muumbaji mwenye kutoka rizki ambae amemleta mwanadamu kutokana na kutokuwepo na akampa neema mbalimbali.

2.Kujua majina ya Allah na Sifa zake, na yale anayopaswa afanyiwe na athari ya majina yake kwa waja wake.

3.Kuijua njia inayokufikisha kwa Allah.

4.Kujua vikwazo na maafa vinavyozuia baina ya mwanadamu na njia hiyo, na baina ya kujua njia inayomfikisha katika neema kubwa.

5.Kuijua nafsi yako ukweli wa kuijua, na kujua nafsi inacho kihitaji, na kinachoifaa nafsi na kinachoiharibu na yanayo ambatana nayo miongoni mwa mambo mazuri au mambo ya aibu.

Na maarifa haya matano ndio mwanadamu anakamilisha nguvu zake za kielimu, na ukamilifu wa nguvu za kielimu na kimatakwa haupatikani isipokuwa kwa kuchunga haki za Allah juu mja, na kuzifanya kwa ikhlas na ukweli na kutoa nasaha na kutekeleza, na kwakutoa ushuhuda juu ya neema zake kwa mwanadamu, na hakuna njia ya kukamilisha nguvu hizo mbili isipokuwa kwa kupata msaada wake, mwanadamu anahitaji aongozwe na Allah katika njia iliyo nyooka aliyo waongoza kwayo watu wema.([74])

Baada ya kuwa tumejua ya kwamba dini sahihi ni msaada kwa Allah kwa nguvu za nafsi tofauti hakika dini pia ni kinga kwa jamii, kwasababu maisha ya wanadamu hayawi isipokuwa kwa kusaidiana baina ya watu, na huko kusaidiana hakukamiliki isipokuwa kwa nidhamu inayopangilia mahusiano na kupangilia mambo ya wajibu juuyao na kuzitunza haki zao, na nidham hiyo ina kiongozi ambae anazirejesha nafsi pindi zinapokiuka na anazihimiza kuihifadhi hiyo nidham na inalea heshima yake katika nafsi za watu, na inakataza kuvunja heshima yake. Ni yupi huyo kiongozi? Nasema hakuna juu ya mgongo nguvu zinzolingana na nguvu ya dini au inayokurubia katika kulea na kuheshimu nidham na kuifanya jamii ni yenye mshikamano na kutulia kwake na kuleta sababu za raha na utulivu ndani yake.

Na siri katika hayo ni kwamba mwanadamu anasifika juu ya vimbe wengine wote walio hai, kwasababu harakati zake na mambo yake ni ya kujitakia kinacho yaongoza ni kitu ambacho hakisikii wala hakionibali ni itikadi ya kiimani inayoupangia moyo na kuvipamba viungo, siku zote mwanadamu anaongozwa kwa itikadi sahihi au mbovu, itikadi yake inapokuwa sawa basi na mambo yake yote yanakuwa sawa, inapoharibika kinaharibika kila kitu.

akida na imani ndio viangalizi vya dhati ya mtu navyo viko aina mbili:

1.Imani ya kuijua thamani ya fadhila na kujua utukufu wa kibinadamu na mengineyo miongoni mwa mambo ambayo nafsi inaona aibu kuyapinga katika mambo mazuri.

2.Imani ya kumuamini Allah Mtukufu, na kwamba Yeye Allah anajua mambo ya siri na yaliyo fichikana, sheria na usimamizi wake vinatokana na amri yake na makatazo yake, na hisia zinazidi kwa kumuonea haya Allah au kwa kumpenda au kwa kumuogopa au vyote…Na hakuna shaka kwamba aina hii ya imani ndio yenye nguvu katika nafsi ya mwanadamu, nayo ndio yenye nguvu kwa kukabiliana na matamanio na mabadiliko ya nafsi na ni nyepesi kutekelezwa katika nyoyo za watu wote au baadhi.

Kwaajili hiyo dini imekuwa ndio dhamana bora ya kuamiliana na watu juu ya misingi ya uadilifu, na ndio sababu ya dini kuwa ni jambo la muhimu katika jamii, hakuna ajabu ikiwa nafasi ya dini katika umma nafasi ya moyo katika kiwiliwili.([75])

Na ikiwa dini ina daraja hii, basi yanayoshuhudiwa leo kutokana na dini kuwa nyingi na mila tofauti katika ulimwengu huu na kukuta watu kila mmoja anafurahia dini yake na ameshikamana nayo, ni ipi dini sahihi ambayo inaitimizia nafsi ya mwanadamu matarajio yake?  Na vipi vigezo vya dini ya haki?

 Vigezo Vya Dini Sahihi

Kila mwenye anaamini kwamba dini yake ndio ya kweli na kila wafuasi wa dini wanaamini kuwa dini yao ndio ya kipekee na misingi yenye nguvu, na kila unapouliza wafuasi wa dini zilizowekwa na watu juu ya ushahidi wa itikadi zao wanatoa hoja kwamba wao waliwakuta baba zao wakiwa katika njia hiyo, na wao wanafuata dini ya baba zao, kisha wanataja historia na habari ambazo hazina ukweli na hazisalimiki kutokana na mapungufu, na wanategemea vitabu vilivyorithiwa haijulikani ni nani aliyesema na ninani aliyeandika, na viliandikwa kwa lugha gani kwa mara ya kwanza, na vilipatikana katika nchi gani, si vinginevyo bali ni vitabu vilivyo kusanywa vikatukuzwa vikarithiwa na vizazi bila ya kuwa na uhakiki wa kielimu unaochambua upokezi wake na kupangilia matini yake.

Na vitabu hivyo visivyojulikiana na ambavyo ni hikaya na kumfuata kipofu havifai kuwa ni hoja katika dini na katika itikadi, je! Dini zote hizi zilizobadilishwa na mila za kibinadamu ni sahihi au ni batili?

Haiwezekani zote kuwa ni za haki kwasababu haki ni moja na haigawanyiki, na pia haiwezekani dini zote hizi zilizopotoshwa, na mila za kibinadamu kuwa zimetoka kwa Allah na zote ni za kweli,na pindi zinapokuwa nyingi wakati haki ni moja dini iko wapi?  Ikiwa ni hivo lazima kuwe na vigezo ambavyo tutaijua dini ya kweli au ya batili kupitia vigezo hivyo, tutakapokuta vigezo hivyo vinaafikiana na dini ndio tutajua kwamba ni haki, na vitakapo kosekana vigezo hivyo au kimoja katika hivyo tutajua kwamba ni batili.

 Vigezo Vinavyo Pambanua Dini Ya Haki Na Dini Ya Batili:

1. Iwe dini imetoka kwa Allah ameiteremsha kwa njia ya Malaika kwa Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake awafikishie waja wake, kwasababu dini ya haki ni dini ya Allah, na Allah Mtukufu Yeye ndiye anayeweka dini na Yeye ndiye atakayewahesabia waja wake siku ya Qiyama kutokana na dini aliyowateremshia amesema Allah Mtukufu: Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi.([76]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.([77]) Kwasababu hiyo hakika dini yoyote anayoleta mtu na akainasibisha na nafsi yake na siyo kwa Allah basi bila shaka dini hiyo ni batili.

2. Alinganie juu ya kumpwekesha Allah katika ibada na kuharamisha ushirikina na kuharamisha njia inayopelekea katika ushirikina, kwasababu kulingania juu ya kumpwekesha Allah ndio msingi wa ulinganizi wa Manabii, na kila Nabii alisema kuwaambia watu wake: Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye).([78]) Kwasababu hiyo kila dini iliyoambatana na shirki na ikamshirikisha pamoja na Allah mtu mwingine miongoni mwa Manabii au Malaika au Walii basi ni dini batili hata kama wakijinasibisha wenye hiyo kwa Nabii miongoni mwa Manabii.

3. Iwe inaafikiana na misingi miongoni mwa misingi walioilingania Mitume ikiwemo kumuabudu Allah peke yake, na kulingania katika njia yake, na kuharamisha ushirikina na kuharamisha kuwaasi wazazi wawili na kuharamisha kuuwa nafsi bila ya haki na kuharamisha mambo machafu yaliyodhihiri na yaliyojificha, amesema Allah Mtukufu: Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.([79]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini.([80]) Na amesema Allah Mtukufu: Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah'mani?([81])

4. Zisiwe ni dini zinazo pingana au kutofautiana, dini isiamrishe jambo kisha dini nyingine ikaja kulipinga, na isiharamishe jambo kisha nyingine ikaja ikahalalisha bila ya sababu, na isiharamishe jambo kwa baadhi ya watu na kujuzisha kwa watu wengine, amesema Allah Mtukufu: {Hebu hawaizingatii hii Qur'ani?  Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi}.([82])

5. Dini iambatane na mambo yatakayo wahifadhia watu dini yao na heshima zao na mali zao na nafsi zao na kizazi chao kwa yale yaliyowekewa sheria miongoni mwa maamrisho na makatazo na makemeo na tabia njema zitakazo hifadhi mambo haya matano.

6. Dini iwe ni rehma kwa viumbe kutokana na watu kuzidhulumu nafsi zao au kudhulumiana wao kwa wao, sawasawa dhulma hii iwe ni kwa kukiuka haki, au kufanya jeuri au wakubwa kuwapoteza wadogo, amesema Allah Mtukufu akiwa anatoa habari kuhusu rehma iliyoelezwa na Torati iliyoteremshwa kwa Nabii Mussa alayhi salam: {Na Musa ilipo mtulia ghadhabu aliziokota zile mbao. Na katika maandiko yake mna uwongofu na rehema kwa wanao mwogopa Mola wao Mlezi}.([83]) Na amesema Allah Mtukufu akitoa habari kuhusu kutumwa kwa Yesu alayhi salam: {Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu}.([84]) Na amesema Allah Mtukufu akimzungumzia Nabii Swaleh alahi salam: {Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake}.([85]) Na amesema Allah Mtukufu kuhusu Qur'ani tukufu:{Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini}.([86])

7. Iwe inakusanya uongofu wa sheria ya Allah na mwongozo wa mwanadamu juu kujua ni kipi anakitaka Allah kwa mwanadamu, na kumweleza mwanadamu ametokea wapi na mwisho wake ni wapi? Amesema Allah Mtukufu akiielezea Taurati: {Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru}.. ([87]) amesema Allah Mtukufu kuhusu Injili: {Na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru}.([88]) Na amesema Allah Mtukufu kuhusu Qur'ani tukufu:{Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki).([89]) Na dini ya kweli ni dini inayoambatana na uongofu na sheria ya Allah, na inaleta amani na utulivu wa nafsi, kwani inaondosha wasiwasi na inajibu maswali yote na inabainisha matatizo yote.

8. Ilinganie tabia njema na matendo mazuri kama vile ukweli na uaminifu na haya na kuacha machafu na ukarimu, na inakataza mambo mabaya kama vile kuwaasi wazazi wawili na kuuwa nafsi na kuharamisha machafu na uongo na dhulma na uovu.

9. Ilete mafanikio kwa yeyote mwenye kuiamini, amesema Allah Mtukufu: {Twaha! Hatukukuteremshia Qur'ani ili upate mashaka}.([90]) Na iendane na maumbile ya sawa, amesema Allah Mtukufu:([91])na iafikiane na akili iliyo sahihi, kwasababu dini ya kweli ndiyo sheria ya Allah na akili iliyo sahihi ni kiumbe cha Allah, na haiwezekani sheria ya Allah ipingane na kiumbe chake.

10. Ionyeshe haki na itahadharishe batili, iwaongoze kunako uongofu na iwaondoshe katika upotovu, iwalinganie watu katika njia iliyonyooka na sio katika njia iliyopinda, amesema Allah Mtukufu akiwaelezea Majini ya kwamba walipoisika Qur'an waliambizana wao kwa wao:{Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilicho teremshwa baada ya Musa, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake, na kinacho ongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyo Nyooka}.([92]) Isiwalinganie watu katika mambo ya uovu, amesema Allah Mtukufu: {Twaha! Hatukukuteremshia Qur'ani ili upate mashaka}.([93]) Wala isiwaamrishe katika mambo yenye kuwaangamiza, amesema Allah Mtukufu: {Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni}.([94]) Na isiwabague wafuasi wake kwa tofauti ya rangi au jinsia, amesema Allah Mtukufu: {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari}.([95]) Vipimo vinavyo zingatiwa vya mtu kuwa bora katika dini ya haki ni ucha Mungu.

Baada ya kuelezea vigezo vinavyo tofautisha baina ya dini haki na dini ya batili, na nikatoa ushahidi kwa yale yaliyokuja ndani ya Qur'an tukufu kwa yale yanayo onyesha kwamba vigezo hivi vinakusanya Mitume wote walio wakweli waliotumwa kutoka kwa Allah, basi ni wakati munasaba kuzungumzia vigawanyo vya dni.

 Vigawanyo Vya Dini

Watu wamegawanyika sehemu mbili kutokana na dini zao:

kuna watu wana kitabu kilicho teremshwa kutoka kwa Allah kama vile Mayahudu, Manaswara na Waislamu, ama Mayahudi na Manaswara kwasababu ya kutokuyajua yaliyokuja katika vitabu vyao, na kwasababu ya kuwafanya wanadamu ni waungu kinyume na Allah, na kwasababu ya kupita muda mrefu wa Utume, vilitoweka vitabu vyao vilivyo teremshwa na Allah juu Mitume wao; Watawa wao wakawaandikia vitabu wakadai kwamba vimetoka kwa Allah ilihali havijatoka kwa Allah kumbe ni maneno ya watu wa batili na ni upotoshashaji wa aliochupa mipaka.

Ama kitabu cha Waislamu (Qur'an tukufu) ni kitabu cha Allah cha mwisho, na ni cha kweli na uhakika Allah amechukua dhamana ya kukihifadhi; Na hakuwakilisha kazi hiyo kwa mwanadamu, amesema Allah Mtukufu: {Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda}.([96]) Nacho kimehifadhiwa katika vifua na katika vitabu, kwasababu ni kitabu cha mwisho ambacho Allah amedhamini uongofu kwa wanadamu kupitia kitabu hicho, na akakijaalia kuwa ni hoja mpaka siku ya Qiyama, na akahukumu kibakie na akakiandalia katika kila zama watakaosimamia hukumu zake na kisomo chake na wataifanyia kazi sheria zake na kukiamini, na utakuja upambanuzi wa ziada wa kitabu hicho kitukufu katika vipengele vijavyo.([97])

Na ninaapa kwamba hawana kitabu kilichoshushwa kutoka kwa Allah walichokirithi kinachonasibishwa na muanzilishi wa dini yao kama vile Hindus na Majusi na Mabudhi na Makonfoshisina Warabu kabla ya kutumwa Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake.

Na hakuna umma wowote ila una ujuzi na matendo kulingana na maslahi ya dunia yao, na huu mwongozo wa jumla ambao Allah aliuweka kwa kila mwanadamu, bali kwa kila mnyama, kama anavyoongozwa mnyama kufanya yale yanayo mnufaisha miongoni mwa kula na kunywa, na kuzuia yanayomdhuru, na hakika Allah ameumba kwa mwanadamu kupenda jambo na kuchukia jambo, amesema Allah Mtukufu: {Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa. Aliye umba, na akaweka sawa. Na ambaye amekadiria na akaongoa}.([98]) Na alisema Mussa kumwambia Firauni: {Akasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliye kipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa}.([99]) Na alisema Al Khalili (Ibrahim) alayhi salam:{Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa}.([100]) Na inavyojulikana kwa kila mwenye akili mwenye mtazamo wa chini ya kwamba watu wenye dini wana ukamilifu zaidi katika elimu zenye manufaa na matendo mema, kuliko wale wasio na dini, kheri yoyote inayopatikana kwa wasiokuwa waislamu isipokuwa utaikuta kwa waislamu ni yenye ukamilifu zaidi, na kwa watu wenye dini kuna mambo yasiyopatikana kwa watu wengine, kwasababu elimu na matendo yako aina mbili:

1.Yanapatikana kwa kutumia akili kama elimu ya hesabu na ufundi, mambo haya wanayo wenye dini na pia wanayo wasiokuwa na dini, bali wenye dini katika elimu hizi ni wakamilifu zaidi, ama yale ambayo hayajulikani kwa kutumia akili pekee kama vile elimu za kumjua Allah, na elimu zinazo zungumzia dini tofauti hizi ni maalum kwa wale wenye kuzijua elimu za dini, katika haya kuna yanayotakiwa kujengewa hoja za kiakili, na Mitume waliotoa mwongozo watu ili wazijue elimu za dini na kumjua Allah, akili zenye mafunzo kama hayo ni akili za kisheria.

2.Yale yasiyojulikana isipokuwa kwa kuelezewa na Mitume, elimu hii haiwezekani kuipata kwa njia ya akili kama vile kupata habari kuhusu Allah na Majina yake na Sifa zake na yaliyomo katika nyumba ya Akhera miongoni mwa neema kwa mwenye kumtii Allah na adhabu kwa mwenye kumuasi na ubainifu wa sheria zake na habari za Mitume waliotangulia pamoja na nyumati zao na mengineyo. ([101])

 Hali Ya Dini Zilizo Kuwepo Zamani

Zimekuwa dini kubwa, na vitabu vyake vitakatifu, na sheria zake za zamani ni zenye kuwindwa na wachafuzi na wenye kufanya mchezo (wapuuzi), na ni mchezo wa waposhoshaji na wanafiki, mpaka ikakosa roho yake na umbile lake, laiti kama wakifufuliwa watu wa dini wa mwanzo na Mitume wangekataa wakasema hawaijui.

Dini ya Uyahudi* imekuwa ni mkusanyiko wa ibada na kuiga, hamna roho ndani yake wala uhai, mbali na hayo dini hiyo ni dini ya vizazi vya watu na jinsia maalum, haina ujumbe wowote katika ulimwengu, wala kwa umma unaohitaji kuelimishwa, wala huruma ya kiubinadamu.

Na ilipatwa dini hii katika itikadi yake ya asili ambayo ilikuwa na nembo (maarufu) baina ya dini zilizo tangulia, na ilikuwa siri ya utukufu wake ni itikadi ya kumpwekesha Allah ambayo aliusia Nabii Ibrahimu watoto wake na Nabii Yaqub, na Mayahudi walichukua itikadi nyingi za watu waovu walio tangulia walioishi nao karibu au waliowatawala, na mengi miongoni mwa ada zao na desturi zao zakijinga na zakishirikina, na wameyakubali hayo watunzi wa Kiyahudi waadilifu, imekuja katika kitabu (Daairatu Al Maarifi Al Yahudiyah) maneno yenye maana hii:

"Hakika chuki za Manabii na hasira zao juu ya kuyaabudu masanamu inaonyesha kwamba kuabudu masanamu na miungu mingine ilikuwa imeenea katika nafsi za wana wa Israeli, na ni kwasababu walikuwa wamezikubali itikadi za kishirikina na za kizushi, hakika Talmudi inatoa ushahidi pia kwamba ibada za masanamu zilikuwa na mvuto wa kipekee katika Uyahudi.([102])

Na inaonyesha Talmud.([103]) Kitabu ambacho kinatukuzwa sana na mayahudi, na wanakifadhilisha wakati mwingine na Torati, na kilikuwa kina patikana kwa wingi katika mikono ya mayahudi katika karne yasita ya kikristo. Na yalio jaa miongoni mwa mifano ya ajabu ambayo yanaonyesha wepesi wa akili na kauli chafu, na kumzulia Allah, na kufanyia mchezo mambo ya hakika, na kuichezea dini na akili, kwa ilipo fikia jamii ya kiyahudi katika karne hii miongoni mwa mporomoko wa kiakili na kuharibika kwa dhauku ya kidini. ([104])

Ama Unaswara: * Ulitihaniwa kwa kupotoshwa na watu walio chupa mipaka, na kugeuzwa na watu wajinga, na wasiokuwa na dini na warumi wanao jiita manaswara, tangu enzi zake za mwanzo,Ukawa unaswara ni kifusi, ambacho kilicho zikwa chini yake mafunzo makubwa ya Nabii Issa (Yesu) na ikafichikana nuru ya kumpwekesha Allah na kumtakasia utii Allah nyuma ya mawingu mengi.

Anazungumza mwandashi wa kinaswara kuhusu kuenea itikadi za utatu katika jamii za kinaswara, tangu mwisho wa karne ya nne toka kuzaliwa kwa Issa (Yesu), anasema: Ili enea itikadi ya kwamba Mungu mmoja ameambatana na vitu vitatu katika maisha ya ulimwengu wa kikristo na fikra zake, tangu robo ya karne ya nnena ikadumu itikadi hiyo rasmi ikiwa ni yenye kutegemewa duniani kote, na haikuondoshwa pazia ya kuendelea itikadi za Utatu na siri zake ila ni katika nusu ya karne ya kumi na tisa toka kuzaliwa kwa Issa (Yesu).([105])

Na mtunzi wa Kinaswara wa zama hizi anazungumza katika kitabu chake (Taarekh Al Masihiyah Fi Dhwaui Elmi Al Muaaswir) "Historia ya Ukristo katika elimu ya kisasa" kuhusu kudhihiri ibada ya masanamu katika jamii ya kinaswara katika mionekano na maeneo tofauti, na Manaswara wakajipa uhodari wa kuchukua alama na desturi na sikukuu za waabuduo masanamu kutoka katika nyumati na dini tofauti katika kufanya ushirikina, wamechukua mambo hayo kwasababu ya kuiga au kustaajabishwa au kwa ujinga.Anaendelea kusema mtunzi wa kitabu:(Hakika imekwisha ibada ya kuabudu masanamu, lakini ibada hiyo haikuangamizwa kiukamilifu, bali ilizidi kuwepo katika nafsi za watu na kuendelea, kila walichokifanya katika ibada hizo walikiita kuwa ni Ukristo na kukistiri, wale ambao walijitenga na miungu yao na mambo yao ya batili na wakaachana nao waliwaua na wale waliokufa (Mashahidi) walitwa kwa sifa za miungu kisha wakatengenezewa masanamu, na hivohivo iliendelea kuhama hiyo shirki mpaka kwa mashahidi wengine, na karne hiyo haikuisha mpaka ikawa imeenea ibada ya kuabudu Mashahidi na Mawalii, ikatengenezeka itikadi mpya kwamba Mawalii wa Allah wana sifa za Uungu, wakawa hao Mawalii na watu wema ni viumbe wa katikati baina ya Allah na wanadamu (yaani ili mwanadamu afanikiwe kwa Allah lazima apitie kwa hao Mawalii), na yakabadilishwa majina ya sikukuu za waabuduo masanamu kwa kupewa majina mapya, mpaka mwaka 400 m. sikukuu ya zamani ya kuabudu jua iligeuzwa na kuitwa krismasi yaani sikukuu ya kuzaliwa Issa (Yesu).([106])

Ama dini ya Majusi walijulikana tangu zamani kwa kuabudu vitu vya asili kama vile moto, na hivi karibuni wamekuwa wakikusanyika kwa ajili ya ibada hiyo, na wamekuwa wakijenga kwa ajili ya ibada hizo Mahekalu na maholi ya ibada, na zikaenea nyumba za kuabudu moto katika nchi nyingi, na dini zote zikaondoka ikabakia dini ya kuabudu moto na kulitukuza jua, na zikawa dini kwao ni kuabudu na kuiga na wanazitekeleza ibada hizo katika sehemu maalum.([107])

Anasifu mtunzi wa kitabu hicho cheo cha viongozi wa dini na wadhifa wao kwa kusema:

(Ilikuwa ni lazima kwa hao wafanya kazi waabudu jua mara nne kwa siku, na iongezwe juu ya ibada hiyo kuabudu mwezi na moto na maji, na walikuwa wameamrishwa kwamba wasiuache moto uzimike na wasiguse moto wala maji na wasiache vitu vyenye madini vikapata kutu kwasababu, vitu vyenye madini kwao ni vitakatifu).([108])

Na dini yao ilikuwa ni ya kuamini miungu wawili katika kila zama, na ikawa ndio alama yao wakaamini miungu wawili: Mmoja: Ni mungu nuru, au mungu wa kheri (na wanamwita Ahuwar mazda, au Yazdani). Na wa pili: Ni mungu giza, au mungu wa shari,(na wanamwita Ahraman). Na hao miungu wawili wanazozana kupigana vita kila siku.([109])

Ama Mabudha: Ni dini iliyoenea katika nchi ya India na katikati ya Asia, nayo ni dini ya kuabudu masanamu, unabeba sanamu popote utakapokuwa, na yanajengwa mahekalu kwa ajili ya ibada zao, na yanawekwa masanamu popote inapokuwa dini hiyo.([110])

Ama Al Barhamiyah: Ni dini ya Kihindi, imejulikana kwa kuwa na miungu wengi, katika karne ya sita baada ya kuzaliwa kwa Nabii Issa,miungu yao ilifikia idadi ya milioni 330.([111]) Na kila kitu kizuri au chenye kutisha au chenye manufaa kwao kilikuwa ni mungu, fani ya kutengeneza masanamu ikawa na thamani katika zama hizo, wakayapamba wenye kupamba kwa mandhari nzuri.

Anasema "Say Way Wayd" Al Hindukiy, katika kitabu chake (Tarekh Al Hindi Al Wustwa) alikuwa akiongelea zama Mfalme Harshi (606-648 M), nazo ni zama ambazo Uislamu ulidhihiri katika visiwa vya kiarabu: Ilikuwa dini ya Kihindukia na dini ya Kibudhi ni dini za kuabudu masanamu sawa kwa sawa, bali dini ya Kubudhi iliizidi dini ya Kihindukia kwa kuabudu masanamu, ilikuwa mwanzo wa dini hii ya Kibudhi ni kukanusha kuwepo kwa Allah, lakini ilikuwa kwa hatua walimuweka huyo Budha kuwa ndio mungu mkubwa, na wakaongeza miungu wengine kama vile (Bodhistavas), na imefikia dini hiyo ya kuabudia masanamu kuwa na ni aina tofauti katika nchi ya India mpaka likafikia neno "Buddha" lina maana ya mizimu au masanamu katika baadhi ya lugha ya mashariki ya India.

Bila shaka jambo la kuabudu masanamu limeenea katika ulimwengu wote wa sasa, dunia yote kuanzia bahari ya Atlantic mpaka bahari ya Pacific umezama katika kuabudia masanamu, kana kwamba Unaswara na dini za Mabudha zinashindana katika kuyaadhimisha masanamu na kuyatukuza, na zilikuwa kama vile farasi zinapiata katika msafara mmoja wa mashindano.([112])

Anasema Hindukiyah katika kitabu chake (Al Hindukiyah Al Saaidah): (Hakika kazi ya kutengeneza miungu haikuishia hapo, iliendelea kuongezeka miungu midogo midogo kila siku zinavyokwenda mpaka ikawa haiwezi kuhesabika).([113])

Haya ndio mambo yanayohusu dini, ama miji ambayo ilikuwa na serikali kubwa, na zikaenea ndani yake elimu nyiingi, ikawa ndio chanzo cha maendeleo na ufundi na sanaa, ilikuwa ni miji ambayo haina dini, dini zilifutwa na zikakosa nguvu, wakakosekana wasuluhishaji na walimu wakapotea na ikatangazwa itikadi ya kuwa hakuna Mungu, uovu ukazidi na mwanadamu akaipuuzia nafsiyake, kwa ajili hiyo kujiua kukawa kwingi na familia zikatengena na mahusiano ya kijamii yakasambaratika, na zikazidi clinic za wagonjwa wenye maradhi ya nafsi, yakawekwa masoko ya matapeli na mazingara, mwanadamu akazijaribu starehe zote, na akafuata kila kilicho zushwa kwa kutaka kuiridhisha roho yake na kuifurahisha nafsi yake, na kutulizana moyo wake, hazikufaniikiwa starehe hizo na mitazamo hiyo katika kukipata wanacho kihitaji, na mwanadamu ataendelea kuwa katika uovu wa nafsi yake na adhabu ya kiroho mpaka atakapo shikamana na Mola wake na amuabudu Yeye kwa kufuata njia yake aliyoiridhia na akawaamrisha Mitume wake waifuate njia hiyo, amesema Allah Mtukufu akiweka wazi hali zawatu walio mkengeuka Mola wao na wakataka uongofu kwa mwingine asiekuwa Yeye: {Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu}.([114]) Na amesema Allah Mtukufu akielezea amani ya waliomuamini Allah katika maisha haya: {Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka}.([115]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: {Na ama wale walio fanikiwa, wao watakuwamo Peponi wakidumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisio na ukomo}.([116])

Dini hizi zisizokuwa Uislamu laity zikipimwa na dini zilizo tangulia tutazikuta zimekosa vifungu vingi kama ilivyokuwa wazi katika mazungumzo hayo tuliyo yazungumza kwa ufupi,

na kitu kikubwa kilichokosekana katika dini hizo ni kumpwekesha Allah Mmoja, na wafuasi wa dini hizo wakamshirikisha pamoja na Allah mungu mwingine, kama zilivyokuwa dini hizi zilizo geuzwa haziwapi watu sheria inayo wafaa katika kila zama na sehemu na kuwahifadhia watu dini yao na heshima yao na heshima ya vizazi vyao na mali zao na damu zao, na wala haziwaonyeshi na kuwaongoza kunako sheria ya Allah aliyo iamrisha, wala haziwapi wafuasi wake utulivu na mafanikio kwa yale yaliyokusanywa kutokana na mapungufu na kupingana.

Katika vifungu vinavyokuja, utakujia ubainifu unaohusu Uislamu kwamba ni dini ya Allah na ni ya kweli na ni yenye kubaki ambayo Allah kairidhia kwa nafsi yake na kwaridhia viumbe wake.

Na hitimisho ya kifungu hiki, inanasibiana sisi kueleza ukweli kuhusu Utume na dalili za Utume, na haja za wanadamu juu ya Utume, na tubainishe misingi ya da'awa ya Mitume, na ukweli kuhusu ujumbe wa mwisho wenye kudumu.

 Ukweli Kuhusu Utume

Hakika jambo kubwa linalopaswa kujua kwa mwanadamu katika maisha haya ni kumjua Mola wake ambae kamleta kutokana na kutokuwepo, na akampa neema mbalimbali, hakika malengo makubwa ya Allah kuwaumba waja wake ni kwasababu ya kumuabudu Yeye peke yake,

lakini ni vipi mwanadamu atamjua Mola wake ukweli wa kumjua? Na yale yanayomlazimu miongoni mwa haki mbalimbali za Allah na mambo ya wajibu na ni vipi atamuabudu Mola wake?  Hakika mwanadamu anapata mwenye kumsaidia katika matatizo ya kidunia, na anamkidhia mahitaji yake ikiwemo ya kimatibabu na dawa, na msaada wa kujenga nyumba na mfano wa hayo...Lakini hatapata kwa watu wengine atakae muelimisha kuhusu Mola wake na kumbainishia ni vipi atamuabudu Mola wakekwasababu akili haziwezi kujitegemea kujua makusudio ya Allah katika uumbaji, kwasababu akili ya mwanadamu ina udhaifu zaidi kiasi kwamba haiwezi ikajua makusudio ya mwenzake kabla hajamwambia, inaweza vipi kujua makusudio ya Allah, na kazi hii ni maalum kwa Mitume na Manabii ambao anawachagua Allah kwa ajili ya kufikisha ujumbe na wale wanaokuja baada ya Mitume miongoni mwa Maimamu waongofu warithi wa Mitume, wanaopita katika njia zao na kufuata athari zao, na wanafikisha ujumbe wa Mitume; kwasababu wanadamu hawawezi kupokea ujumbe kutoka kwa Allah moja kwa moja, amesema Allah Mtukufu: {Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima}.([117]) lazima apatikane mtu wa katikati na balozi anayefikisha kutoka kwa Allah sheria yake kwa waja wake, hao mabalozi na watu wa katikati ndio Mitume na Manabii, Malaika anabeba ujume wa Allah kuupeleka kwa Nabii kisha Nabii anawafikishia watu, na anapeleka Malaika ujumbe kwa watu moja kwa moja, kwasababu ulimwengu wa Malaika unatofautiana na ulimwengu wa watu, amesema Allah Mtukufu: {Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu}.([118])

Na imepelekea hekima ya Allah kwamba Mitume wawe ni katika jinsia ya watu wao, ili wajifunze na kufahamu kutoka kwake na waweze kuzungumza naye, laity kama angetumwa Mtume miongoni mwa Malaika wasingeweza kukabiliana naye wala kujifunza kwake.([119] Na alisema Allah Mtukufu: {Na wao husema: Mbona hakuteremshiwa Malaika?  Na kama tungeli teremsha Malaika, basi bila ya shaka ingesha hukumiwa amri, tena hapo wasingeli pewa muhula. Na kama tungeli mfanya Malaika bila ya shaka tungeli mfanya kama binaadamu, na tungeli watilia matatizo yale wanayo yatatiza wao}.([120]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa wakila chakula, na wakenda masokoni...Mpaka kauli yake Allah: Na walisema wale wasio taraji kukutana nasi: Mbona sisi hatuteremshiwi Malaika au hatumwoni Mola wetu Mlezi?  Kwa yakini hawa wamejiona bora nafsi zao, na wamepanda kichwa vikubwa mno!}.([121])

Amesema Allah Mtukufu: {Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo).([122]) Na alisema Allah Mtukufu: {Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia}.([123]) Na wanasifika hao Mitume na Manabii kwa ukamilifu wa akili na maumbile yaliyo salimika, na ukweli katika kauli na vitendo, na uaminifu katika kufukisha waliyotumwa, na kuhifadhiwa na kila kinacho haribu historia yao, na viwiliwili vilivyo salimika na yale yasiyopendeza katika macho, na hisia zilizo salimika.([124]) Na Allah amezitakasa nafsi zao na tabia zao, wao ni wakamilifu wa tabia nzuri na wenye nafsi zilizo takasika na ni wenye ukarimu, Allah amewakusanyia tabia njema kama alivyo wakusanyia upole na elimu, na kusamehe na ukarimu, na ushujaa na uadilifu, mpaka wakatambulika kwa watu wao kutokana na tabia hizo, watu wa Swaleh walimwambia Mtume wao kama alivyoeleza Allah Mtukufu: {Wakasema: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa kheri kwetu. Je, unatukataza tusiwaabudu waliyo kuwa wakiwaabudu baba zetu?}.([125]) Na watu wa Shuaibu walimwambia Shuaibu:{Wakasema: Ewe Shua'ibu! Ni sala zako ndizo zinazo kuamrisha tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu?  Ama hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu}.([126]) Na Muhammad rehma za Allah ziwe juu yake na amani alijulikana kwa watu wake kwa jina la "Muaminifu" kabla ya kuteremshiwa Utume na Mola wake akamsifu kwa kusema:{Na hakika wewe una tabia tukufu}.([127])

Mitume ni watu bora kwa Allah katika viumbe wake, amewateua na akawachagua kwa ajili ya kubeba Utume na kufikisha amana, amesema Allah Mtukufu{Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake} ([128])Na amesema Allah Mtukufu:na amesema Allah Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote}.([129])

na hayo waliyosifiwa na Allah miongoni mwa sifa nzuri na wakajulikana kwa sifa hizo lakini wao ni viumbe wanapatwa nay ale yanayowapata viumbe wengine, wao wanahisi njaa na wanalala na wanakula na wanaoa na wanakufa, amesema Allah Mtukufu: {Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa}.([130]) Na amesema Allah Mtukufu: {Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya}.([131]) Bali huenda wakateswa na kuuliwa au kutolewa katika majumba yao, amesema Allah Mtukufu: {Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango}.([132]) Lakini pia wana ushindi katika Dunia na Akhera, amesema Allah Mtukufu: {Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu atamnusuru yule anaye inusuru yake}.([133]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda}.([134])

 Alama Za Utume

Pindi ulipokuwa Utume ni njia za kuzijua elimu tukufu, na kusimamia kazi bora, ilikuwa rehma ya Allah kuwawekea hao Mitume alama zinazo watambua, na watu watazitolea dalili juu yao, na watawajua kupitia hizo dalili, ikawa kila anaedai kuwa yeye ni Mtume zinadhihiri kwake dalili zinazoonyesha ukweli wake na uongo wake, na alama hizo ni nyingi, miongoni mwa hizo:

1. Ni Mtume kulingania katika ibada ya Allah Mmoja na kuacha ibada ya visivyokuwa Allah, kwasababu hayo ndiyo malengo ya kuumbwa kwa mwanadamu.

       2. Awalinganie watu kunako kumuamini Allah, na kumsadikisha na kuufanyia kazi ujumbe wake, na Allah alimuamrisha Mtume wake Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake aseme:: {Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote}.([135])

3. Ni kupewa nguvu na Allah kwa miujiza mbalimbali miongoni mwa miujiza ya Utume, na katika miujiza hiyo: Ni miujiza anayoileta Mtume ambayo watu wake hawawezi kuileta au kuleta mfano wake, na katika hiyo ni muujiza wa Nabii Mussa alayhi salam wakati ile fimbo yake ilipogeuka na kuwa nyoka, na muujiza wa Nabii Issa alayhi salam wakati alipokuwa anawaponya viziwi na vipofu na waugua ukoma kwa idhini ya Allah,na muujiza wa Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni Qur'an tukufu pamoja na kuwa yeye hajui kusoma wala kuandika na mengineyo, na miujiza mingine ya Mitume,

na miongoni mwa miujiza hiyo: Ni ukweli ulio wazi wanaousema Mitume ambao wapinzani wao hawawezi kuupinga wala kuukanusha, bali hao wapinzani wajua kuwa waliyokuja nayo Mitume yanatoka kwa Allah.

Na miongoni mwa miujiza hiyo ni ile Allah aliyowahusisha Mitume wake miongoni mwa hali ya ukamilifu na sifa nzuri na ukarimu na tabia njema.

Na miongoni mwa miujiza hiyo ni nusra ya Allah kwa Mtume kutokana na adui zake na kudhihirisha yale anayo yalingania.

4. Ni ulinganizi wake uwafikiane na misingi waliyiilingania Mitume na Manabii waliotangulia.([136])

5. Asilinganie ili watu wamuabudu au wamfanyie ibada yeye, na asilinganie ili watu walitukuze kabila lake au kundi lake, Allah alimuamrisha Mtume wake Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake awaambie watu: {Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu}.([137])

6. Asitafute kwa watu kutokana na ulinganizi wake maslahi ya kidunia, amesema Allah Mtukufu akielezea kuhusu Mitume wake: Nuh, Hud, Swaleh, Lutwi na Shuaibu, kwamba wao walisema kuwaambia watu wao: {Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote}.([138]) Na amesema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuwaambia watu wake: {Sema (Ewe Mtume) : Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu}.([139])

Hao Mitume na Manabii ambao umetajiwa kwa ufupi sifa zao na miujiza ya Utume wao ni wengi sana, amesema Allah Mtukufu: {Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani}.([140]) Hakika jamii ilikuwa na mafanikio ilipokuwa na Mitume, na watu wa historia washerehekea kuandika habari zao, na zikawa za kweli habari za kuandikwa sheria ya Dini yao, na kwamba Dini yao ni ya haki na uadilifu, na zikawa ni sahihi habari za matukio aliyoyafanyia Allah, ikiwemo kuwanusuru Mitume wake na kuwaangamiza maadui zao, kama vile Mafuriko ya watu wa Nuh, na kuzamishwa Firauni, na adhabu ya watu wa Lutwi, na kunusuriwa Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake kutokana na maadui zake, na kuenea Dini yake... Basi mwenye kuyajua hayo atajua kwa yakini kwamba wao walikuja kwa kheri na uongofu, na ni mwongozo wa viumbe kwa yale yanayo wafaa, na ni tahadhari kwa yale yanayo wadhuru, na Mtume wa kwanza ni Nuh alayhi salam, na wa mwisho wao ni Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake.

 Watu Kuhitajia Mitume

Manabii ndiyo wajumbe wa Allah Mtukufu kwa waja wake, wanawafikishi amri zake na wanawapa bishara kwa yale aliyo waandalia Allah kutokana na neeema mbalimbali ikiwa watatii amri zake, na wanawahadharisha kutokana na adhabu ikiwa wataenda kinyume na matakazo yake, na wanawaelezea habari za nyumati zilizo tangulia na yaliyo wapata miongoni mwa adhabu na matatizo katika dunia kutokana na kukhalifu kwao amri ya Mola wao.

Na amri hizi na makatazo ya Allah, akili hazitoshi zenyewe ili kuyajua, na kwa ajili hiyo Allah ameweka sheria na akaweka amri na makatazo kwa kumkirimu mwanadamu na kumtukuza na kuhifadhi maslahi yao, kwasababu watu wanaweza wakapelekwa na matamanio yao wakavunja amri za Allah na wakajikweza kwa watu na kuchukua haki zao, ikawa ni hekima kubwa Allah kuwatumia Mitume kwa nyakati tofauti ili wawakumbushe amri za Allah na wawatahadharishe wasifanye maasi, na wawasomee mawaidha na wawakumbushe habari za watu waliotangulia, kwasababu habari za ajabu na maana zake zinapo sikilizwa zinaamsha akili na kuongeza elimu na kuamsha uelewa, na watu wengi wanaosikiliza sana ndio wanye mawazo mengi na ndio wenye kufikiria sana, na wenye kufikiria sana ndio wenye elimu nyingi, na watu wenye elimu nyingi ndio wenye matendo mengi. Haikupatikana kiwango chochote katika kutumwa Mitume, na hakuna kama wao katika kufuata haki.([141])

Amesema Sheykhul Islam Bun Teymiyah([142])Allah amrehem: Na Utume ni muhimu katika kumfanya mja awe mwema katika maisha yake na Akhera yake, kama ilvyo kwamba hawezi kuwa mwema katika Akhera kwa kufuata Utume, vilevile hawezi kuwa mwema katika maisha yake ila kwa kufuata Utume, mwanadamu analazimika kufuata na sheria kwasababu yuko baina ya mambo mawili, yanayo mletea manufaa na yanayo mkinga na madhara, na sheria ndiyo nuru inayo mbainishia yanayo mfaa na yanayo mdhuru, sheria ni nuru ya Allah katika ardhi yake, na ndiyo uadilifu wake baina ya waja wake, na ndio ngome yake ambayo mwenye kuingia atakuwa na amani.

Makusudio ya sheria siyo kubainisha chenye manufaa na chenye kudhuru kwa akili ya kawaida kwasababu hilo pia linapatikana kwa wanyama, hakika punda na ngamia wanatofautisha baina ngano na mchanga, bali kupambanua kunako kusudiwa ni baina ya vitendo vinavyo mdhuru mwenye kuvifanya au kumnufaisha katika Dunia yake na Akhera yake, na miongoni mwa vitendo vinavyomfaa mwanadamu katika maisha ya dunia yake na Akhera yake kama vile imani, tauhidi, uadilifu, wema, ihsani, uaminifu, kujizuia na maasi, ushujaa, elimu, subira, kuamrisha mema na kukataza mabaya, kuunga udugu, kuwafanyia wema wazazi wawili, kuwafanyia ihsani wanyama, kutekeleza haki, na kumtakasia ibada Allah, kumtegemea Allah na kumuomba msaada, kuridhika na qadari zake, kujisalimisha katika hukumu zake, na kumsadikisha Allah na kuwasadikisha Mitume wake katika yote waliyo yaeleza, na mengineyo miongoni mwa yenye manufaa kwa mwanadamu katika dunia yake na Akhera yake, na kinyume na hayo, ni uovu na madhara yake yanapatikana katika dunia na Akhera.

Na laity kama siyo Utume akili isingeongoka katika kubainisha yenye manufaa na yenye madhara katika maisha, miongoni mwa neema kubwa za Allah kwa waja wake ni Allah kuwatumia Mitume wake na kuwateremshia Vitabu vyake na akawabainishia njia iliyo nyooka, na laiti isingelikuwa hivo wangekuwa kama wanyama bali wangekuwa wabaya zaidi kuliko wanyama, basi mwenye kukubali ujumbe wa Allah na akasimama imara katika ujumbe huo atakuwa ni katika viumbe bora, na mwenye kukataa na akaenda kinyume na ujumbe huo atakuwa ni katika viumbe waovu, na atakuwa na hali mbaya kuliko mbwa na nguruwe, na atakuwa ni dhalili kuliko kiumbe yeyote,na hakuna kubaki kwa yeyote katika ardhi isipokuwa ni athari za Utume zinazobaki baina yao, utakaposoma athari za Utume ardhini na ukafuta alama za uongofu wao (yaani watui watakapo acha mwongozo wa Mitume na wakayaelekea maasi) Mwenyezi Mungu ataiangamiza dunia na atasimamisha Qiyama.

Watu watu ardhini haja yao ya kupa Mtume sio kama haja yao ya kupata jua au mwezi au upepo au mvua, wala siyo kama wanavyohitaji maisha yao, wala si kama jicho linavyohitaji mwangaza au mwili kuhitaji chakula na kinywaji, bali haja yao ni kubwa kuliko hayo na kuliko anavyo fikiria mtu, Mitume rehma na amani ziwe juu yao ni watu wa katikati baina ya Allah na viumbe wake katika amri yake na makatazo yake, wao ni mabalozi baina ya waja wake, na Mtume wa mwisho ndiyo mbora wao kwa Mola wao ambae ni Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake na juu ya Mitume wote, na Allah amemtuma awe ni rehma kwa walimwengu wote, na ni hoja kwa viumbe wote, na Allah amewalazimisha waja wote wamtii, wampende, wamheshimu na kumtukuza, na kusimamia haki zake, na kuchukua ahadi ya kumuamini na kumfuata juu ya Mitume wote na Manabii, na Allah akawaamrisha wazichukue hizo haki kwa walewatakao kuja baada yake miongoni mwa Waumini, Allah amemtuma mbele yake kuna Qiyama akiwa ni mwenye kuwabashiria watu na mwenye kuwaonya, na ni mlinganizi kwa Allah kwa idhini yake na ni taa yenye mwangaza, Allah akamfanya wa mwisho katika Mitume na akawaongoza watu na kuwatoa katika ujinga kupitia Mtume, na kwa Utume wake akafungua macho ya vipofu na masikio ya viziwi na nyoyo zilizo ghafilika, ardhi ikang'aa kwa Utume wake baada kuwa ina giza, na nyoyo zikaungana baada ya kutengena, Allah ikasimamisha Dini kupitia yeye Mtume na akaziweka wazi hoja za kwaeli na nyoyo zikafunguka na kuacha madhambi, na akanyanyua utajo wake na akajaalia unyonge na udhalili ni kwa mwenye kukhalifu amri yake, Allah amemtuma Mtume rehm na amani za Allah ziwe juu yake katika kipindi kidogo cha Utume pindi mambo yalipopotoshwa na kubadilishwa sheria, na kila mmoja akaegemea katika dhulma za fikra zake na wakatoa huhukumu baina Allah na waja wake kwa maneno yao ya uovu na matamanio yao, Allah akawaongoza kupitia Mtume viumbe na akawawekea wazi njia na akatoa watu katika giza na kuwaingiza katika nuru, na akabainisha kupitia kwa Mtume watu wema na waovu, aliyeongoka ni yule aliyefuata uongofu wake, na atakaye kwenda kinyume na njia yake atakuwa amepotea na kuchupa mipaka, rehma na amani za Allah ziwe juu yake na ziwe juu ya Mitume Manabii wengine.([143])

Na tunaweza kufupisha katika kuelezea haja ya mwanadamu juu ya kuhitajia Utume katika haya yafuatayo:

1. Hakika mwanadamu ameumbwa na amelelewa, na nilazima amjue aliyemuumba, na ajue ni kitu gani anachokitaka Allah kutoka kwake na ni kwanini amemuumba, na mwanadamu hawezi kujitegemea katika kuyajua hayo wala hakuna njia ya kuyajua hayo isipokuwa ni kwa kuwajua Mitume na Manabii,na kuyajua waliyokuja nayo miongoni mwa uongofu na nuru.

2. Hakika mwanadamu ameumbwa kutokana na mwili na roho, na chakula cha mwili ni chochote katika chakula na kinywaji, na chakula cha roho kimewekwa na Allah aliyeiumba roho, nayo ni Dini iliyo sahihi na matendo mema, na Mitume pamoja na Manabii walileta Dini sahihi na wakaongoza watu kunako matendo mema.

3. Hakika mwanadamu ni mwenye Dini katika maumbile yake, na hakuna budi awe na Dini anayoifuata na hiyo Dini lazima iwe ni sahihi, na hakuna njia ya kuifikia Dini sahihi isipokuwa kwa kuamini Mitume na Manabii na kuamini yale waliyokuja nayo.

4. Hakika mwanadamu anahitaji kujua njia ya kumfikisha katika radhi za Allah duniani na katika Pepo yake na neema zake katika nyumba ya Akhera, na njia hii hakuna anaeitolea mwongozo isipokuwa ni Mitume na Manabii.

5. Hakika mwanadamu ni mdhaifu katika nafsi yake na anaviziwa na maadui wengi miongoni mwa mashetani wanaotaka kumpoteza na marafiki wabaya wanaompambia mambo machafu, na nafsi inayoamrisha mabaya, kwa ajili hiyo anahitaji kinga ya nafsi yake kutokana na vitimbi vya maadui zake, na Mitume na Manabii walielekeza kuhusu hilo na wakabainisha ukomo wa kubainisha.

6. Hakika mwanadamu ameumbwa kuisha na watu, na kujumuika na watu na kuishi nao lazima ipatikane sheria ambayo itawafanya waishi kwa uadilifu, tofauti na hivyo maisha yao yatakuwa kama maisha ya watu wa porini, na sheria hii ni lazima imuhifadhie kila mwenye haki haki yake, bila kupunguza wala kuzidisha, na hakuna yeyote anaeleta sheria iliyo kamilika isipokuwa ni Mitume na Manabii.

7. Hakika mwanadamu anahitaji kuyajua yale yanayomletea utulivu wa moyo na amani ya nafsi, nay ale yanayo muongoza kujua sababu za mafanikio ya kweli, na hayo ndiyo yanayo ongozwa na Mitume na Manabii.

Na baada ya kubainisha mahitajio ya viumbe kwa Mitume tunalazimika kutaja maadi na kubainisha hoja na dalili juu ya hilo.

  

 Marejeo (Almaadi):

Kila mwanadamu anajua kwa yakini kwamba atakufa lakini atafikia wapi baada ya kufa?  Na je ni mwema au muovu?.

Hakika mataifa mengi na nyumati wanaamini kwamba watafufuliwa baada ya kufa na watahesabiwa kwa matendo yao, yakiwa ya kheri basi watapata kheri, na yakiwa ya shari watapata shari.([144]) Na jambo hili la kufufu na kuhesabiwa akili zilizo salama zinakiri na sheria za Allah zilitilia nguvu, na limejengeka katika misingi mitatu:

1. Ni kukiri ukamilifu wa Allah Mtukufu.

2. Ni kukiri ukamilifu wa uwezo wa Allah Mtukufu.

3  Ni kukiri ukamilifu wa Hekima ya Allah Mtukufu.([145])

Na zimekuja dalili nyingi za kunukuu na za kiakili zikithibitisha jambo hilo, na miongoni mwa dalili hizo ni hizi zifuatazo:

1. Ni kutoa dalili kwamba ikiwa Allah Mtukufu aliumba mbingu na ardhi basi kufufua wafu ni jambo dogo kwake, amesema Allah Mtukufu: {Je! Hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliye ziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu?  Kwani?  Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu}.([146]) Na amesema Allah Mtukufu: {Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao?  Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi}.([147])

2. Ni kutoa dalili ya uwezo wake Allah wa kuumba viumbe bila ya kuwa na mfano uliotangulia, kama anaweza hivo basi ana uwezo wa kumuumba tena kwa mara nyingine, Mwenye uwezo wa kuleta kitu kisicho kuwepo ana uwezo zaidiwa kukirejesha upya, amesema Allah Mtukufu: {Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi}.([148]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: Amesema Allah Mtukufu: {Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika? Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba}.([149])

3. Kuumbwa kwa mwanadamu katika umbile zuri, kwa sura iliyo kamilika na viungo vyake na nguvu zake na sifa zake, na yaliyo katika mwili wa mwanadamu kama vile nyama, mifupa, mishipa, misuri, matundu, na vifaa mbali mbali, na elimu, na kutaka, na ubunifu, ndani yake kuna dalili kubwa juu ya uwezo wa Allah Mtukufu wa kuhuisha waliokufa.

4. Ni kutoa dalili juu ya kuhuisha walio kufa katika maisha ya dunia, kwamba anao uwezo wa kuwahuisha tena katika nyumba ya Akhera, na zimekuja habari kuhusu hilo katika Vitabu vya Allah alivyo vishusha kwa Mitume wake,na miongoni mwa habari hizo ni kuhuisha waliokufa kwa idhini ya Allah kupitia kwa Nabii Ibrahim na Issa rehma na amani ziwe juu yao, na mengineyo mengi.

       5. Ni kutoa dalili juu ya uwezo wake wa kufanya mambo yanayofanana na kufufua, kwamba anauwezo wa kufufua waliokufa, na miongoni mwa mambo hayo:ikiwa vipande hivyo vilivyo sambaa amevikusanya na akaumba ndani yake mtu, na pindi vitakapo sambaa kwa sababu ya kifo vipi itashindikana kwake kuvikusanya kwa mara nyingine?  amesema Allah Mtukufu: {Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?  Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? }.([150])

       (B) Hakika mbegu za mimea pamoja na tofauti zake zinapowekwa katika ardhi yenye rutba zikapata maji na kufunikwa na udongo, mtizamo wa kiakili unadhani kuwa ile mbegu itaoza na kuharibika, kwasababu moja katika ya maji na undongo ni sababu ya kuoza kwa mbegu hizo na vikiwa vyote viwili ndio vinaziozesha kabisa, lakini mbegu hizo haiziharibiki bali zinabaki zikiwa zimehifadhika, kisha ubichi unapozidi mbegu zile hujifungua na kuchomoza mmea, je hilo halionyeshi uwezo uliokamilika na hekima iliyoenea? Huyu Allah mwenye hekima na mwenye uwezo atashindwa vipi kuvikusanya viungo na kuvirejesha mahala pake? Amesema Allah Mtukufu: {Je! Mnaona makulima mnayo yapanda?  Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? }.([151]) Na mfano wa Aya hiyo ni kauli ya Allah Mtukufu inayosema:{Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri}.([152])

6. Ya Mwenyezi Mungu ni muumbaji mwenye uwezo na ni mjuzi mwenye hekima, na ametakasika kutokana na kuumba viumbe kwa upuuzi na kuwaacha bure, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake kwa batili. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata}.([153]) Bali aliumba viumbe wake kwa hekima kubwa ba kwa malengo matukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Sikuumba majini wala watu ila ni kwa lengo la kuniabudu}.([154]) Haiendani kwa Mungu huyu mwenye hekima walingane yule anaye mtii na anaye muasi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi?  Au tuwafanye wachamngu kama waovu?}.([155]) Kwasababu hiyo miongoni mwa ukamilifu wa hekima yake na nguvu za uwezo wake ni kuwafufua viumbe siku ya Qiyama ili amlipe kila mwanadamu kwa matendo yake, aliyefanya mema alipwe kwa mema yake na aliyefanya maovu aadhibiwe, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwake Yeye tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye aliye anzisha uumbaji, na kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walio amini na wakatenda mema. Na walio kufuru, wao watapata vinywaji vinavyo chemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru}.([156])

Na kuamini siku ya kufufuliwa kuna athari nyingi kwa mtu mmoja mmoja na katika jamii na miongoni mwa athari hizo:

1-Ni mtu kufanya bidii ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kutafuta thawabu za siku hiyo, na kujiepusha na maasi kwa kuogopa adhabu za siku hiyo.

2-Kuamini siku ya Mwisho kuna maliwazo kwa Muumini kutokana na yale yanayompita miongoni mwa neema za dunia na starehe zake, akitarajia neema za Akhera na malipo yake.

3-Kuamini siku ya Mwisho kunamjulisha mwanadamu juu mafikio yake baada ya kufa kwake, na anajua kuwa atapata malipo ya matendo yake, kama ni kheri atalipwa kheri, na kama ni shari atalipwa shari, na kwamba atasimamishwa kwa ajili ya kuhesabiwa na atalipizwa kisasi kwa yule aliye mdhulumu, na zitachukuliwa haki zake wapewe waja alio wadhulumu au alio wafanyia uadui.

4-Kuamini siku ya Mwisho kunamzuia mtu kuwadhulumu wenzake na kuvunja haki zao, endapo watu wataamini siku ya mwisho watasalimika wao kwa wao na zitahifadhika haki zao.

5-Kuamini siku ya Mwisho kunamfanya mwanadamu aiangalie dunia kwamba ni hatua miongoni mwa hatua za maisha na kwamba dunia siyo maisha yote.

Na mwisho wa kipengele hiki inapendeza tutoe ushahidi kwa kauli ya Wen bet Muamerka alikuwa Mkristo akifanya kazi katika moja ya Makanisa huko kisha akasilimu, akapata matunda ya kuamini siku ya mwisho pale aliposema: "Hakika mimi sasa hivi ninajua majibu ya maswali manne yaliyo shughulisha maisha yangu sana nayo ni: Mimi ni nani?  Na ninataka nini?  Na kwanini nimekuja duniani?  Na mafikio yangu ni wapi? "([157]).

 Misingi Ya Ulinganizi Wa Mitume

Walikubaliana Mitume na Manabii juu ya kulingania misingi iliyokusanya mambo yote,([158]) kama vile kumuami ni Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na kuamini siku ya Qiyama na Kuamini Qadari kheri zake na shari zake, na kuamrisha watu wamuadu Allah peke yake bila ya kumshirikisha, na kufuata njia yake na kutokufuata njia ya wenye kumukhalifu, na kuharamisha vitu vyenye jinsia nne navyo ni: Mambo machafu yaliyo wazi na yaliyofichikana, na madhambi, na kuwafanyia watu uovu bila ya haki, na kumshirikisha Allah na kuabudu mizimu na masanamu. Na kumtakasa Allah kutokana na kutokuwa na mke na mtotona mshirika na mfano wake, na kusemea Allah yasiyokuwa ya haki, na kuharamisha kuuwa watoto, na kuharamisha kuuwa nafsi bila ya haki, na kukataza riba na kula mali za mayatima, na kuamrisha kutekeleza ahadi na uadilifu katika mizani, na kuwafanyia wema wazazi wawili na kufanya uadilifu baina ya watu, na kuwa mkweli katika maneno na matendo, na kukataza kufanya israfu na kiburi, na kula mali za watu kwa batili.

Amesema Ibn Alqayim Allah amrehem:([159]) Sheria zote pamoja na kuwa mbalimbali lakini katika misingi yake zinakubaliana, uzuri wake unaingia akilini, na laiti ingetoka sheria katika malengo ambayo siyo makusudio basi sheria hiyo ingekuwa mbali na hekima yake na maslahi yake na rehma yake, balini mhali sheria kuja tofauti na malengo yake, {Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani}.([160]) Itakuwa vipi mtu mwenye akili kuiweka sheria ya Hakimu wa mahakimu (Allah) iwe kinyume na malengo yake?([161]).

Na kwa ajili hiyo Dini ya Mitume ilikuwa ni moja kama alivyosema Allah Mtukufu: {Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda. Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi}.([162]) Na amesema Mwenyezi Mungu: {Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Issa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo}.([163])

Bali kinacho kusudiwa katika Dini ni waja kufikia malengo waliyoumbiwa kwayo ikiwemo kumuabudu Mola wao peke yake hana mshirika([164]) anawawekea sheria na haki ambazo wanapaswa kuzisimamia, na anawawekea mabo ya wajibu, na anawapa msaada kwa kuwapa mambo ambayo yanawasaidia kufikia katika malengo hayo ya kumuabudu, ili waweze kupata radhi zake na mafanikio ya nyumba mbili duniani na Akhera, kulingana na mwongozo wa Allah ambao haumpi tabu mjawala haumtii dosari katika utu wake wala kupingana na maumbile yake, roho yake na ulimwengu unao mzunguka.

Mitume wote wanalingania katika Dini ya Allah ambayo inawapa wanadamu msingi wa kiitikadi ili wauamini, na sheria ambayo wanaipitia katika maisha yao, kwasababu hiyo Taurati ilikuwa ni itikadi na ni sheria, na watu wake walilazimishwa kuhukumiana kwa Taurati, amesema Allah Mtukufu: {Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi}.([165]) Kisha akaja Nabii Issa amani iwe juu yake na Injili ndani yake kuna uongofu na nuru, na ni yenye kusadikisha yaliyokuwa kabla yake miongoni mwa Taurati, amesema Allah Mtukufu: {Na tukawafuatishia hao Issa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu na nuru}.([166]) Kisha akaja Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake na sheria ya mwisho na Dini iliyo kamilika yenye kulinda sheria zilizokuwa kabla yake, na yenye kusadikisha vitabu vilivyokuwa nyuma yake, amesema Allah Mtukufu: {Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia}.([167]) Na Allah Mtukufu akabainisha kwamba Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake na wale walioamini pamoja nae waliiamini sheria hiyo kama walivyo iamini waliokuwa kabala yake miongoni mwa Mitume, amesema Allah Mtukufu:{Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako}.([168])

 Ujumbe Wenye Kudumu*

Yaliyo tangulia katika kuzungumzia hali ya dini za Mayahudi na Manaswara na Majusi na za Zoroastrianism na wasiokuwa na dini kwa aina tofauti yanabainisha hali za wanadamu ((176)) katika karne ya sita ya kuzaliwa kwa Issa, na Dini inapo haribika inaribika; Inaribika pia hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi...na huwa ni sababu ya kuenea vita yenye kuangamiza, na kudhihiri udikteta, na wanadamu kuishi katika kiza kinene, na nyoyo zinapata giza kwasababu ya dhulma na ukafiri na ujinga, na tabia zinachafuka na heshima huvunjwa na haki, huvamiwa na unadhihiri uovu nchi kavu na baharini, pindi anapo zingatia mwenye akili atajua kwamba viumbe katika muda huo walikuwa katika muda wa kifo, na utu wakati huo ulikuwa mahtuti na ulikaribia kutoweka, kwa muda ambao Allah alikuwa hajaleta mtu mwenye kuutengeneza mwenye sifa ya Utume na uongofu, ili aungazie njia ya kupita na auongoze katika njia ya sawa.

Na katika zama hizo Allah alitoa idhini ichomoze nuru ya Utume kutoka katika Mji Mtukufu wa Makkah ambao ndani yake kuna nyumba tukufu, na yakuwa mazingira yake yana fanana na mazingira mengine ya kibinadamu kutokana na ushirikina na ujinga na dhulma na jeuri na udikteta, isipokuwa Mji huo ulifahamika kwa sifa nyingi miongoni mwa hizo:

1-Ni Mji wenye mazingira mazuri, haukuathirika na fikra za kifalsafa za Kiyunani au za Kiromania au za Kihindi, na watu wa Mji huo walikuwa wenye ufasaha na akili iliyo safi na vipaji vyenye ubunifu.

2-Ni kwamba upo katika roho ya dunia katika sehemu ya kati na kati baina ya Ulaya, Asia na Afrika, kitu ambacho imekuwa ni sababu kubwa ya kuenea kwa haraka kufika ujumbe katika Miji hiyo kwa muda mchache.

3-Ni Mji wenye amani kiasi kwamba Mwenyezi Mungu aliulinda wakati alipokusudia Abraha kuupiga vita, na hakuna koloni la karibu lililoutawala kati ya Fursi na Roma, bali kulikuwa na amani mpaka na biashara zilizo fanyika kaskazini na kusini,na hayo yote yalikuwa ni maandalizi ya kutumwa Mtume mtukufu, na Mwenyezi Mungu amewakumbusha wa Makka juu ya neeema hiyo akasema: {Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu?  Lakini wengi wao hawajui}.([169])

4-Mji huo mazingira ya jangwa yamehifadhi sifa nyingi zilizo nzuri kama vile ukarimu na kuhifadhi ujirani na kuonea wivu familia na mengineyo katika mambo mazuri ambayo yameupa Mji huo hadhi ya juu kuwa ndiyo sehemu stahiki kwa ajili ya ujumbe wa (Uislamu) wa milele.

Na kutoka katika sehemu hii tukufu na katika kabila la kiqureshi lililojulikana kwa ufasaha na balagha na tabia njema na ambalo lilikuwa na utukufu na hadhi...Mwenyezi Mungu alimchagua Mtume wake Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake awe ni Nabii na Mtume wa mwisho, alizaliwa katika karne ya sita Miladia mwaka wa 570, na alikuwa ni yatima kwasababu Baba yake alikufa Mtume akiwa katika tumbo la Mama yake, kisha Mama yake alikufa na Babu pia wa upande wa Baba, na umri wake wakati huo ulikuwa ni miaka sita, akalelewa na Baba yake mdogo Abuu Twaalib, akakuwa akiwa ni kijana yatima, na zikajionyesha kwake yeye alama za kuwa na kipaji cha akili zikawa desturi zake na tabia zake na mambo yake ni tofauti na watu wake, akawa hasemi uongo katika mazungumzo yake na hamuudhi yeyote, na akajulikana kwa ukweli na kujizuia kutokana na mambo machafu na uaminifu, mpaka ikawa wengi katika watu wake wanamuwekeza mali zao zenye thamani, na akawa anazihifadhi kama anavyoihifadhi nafsi yake na mali yake, ndiyo sababu iliyo wafanya wamuite kuwani muaminifu, na alikuwa ni mwenye aibu sana hakuna mtu aliyeuona mwili wake tangu alipo baleghe na alikuwa mbali na vitendo vichafu na alikuwa mcha Mungu yakawa yanamuumiza yale anayo yaona kwa watu wake miongoni mwa kuabudu masanamu na kunywa pombe na kumwaga damu, na alikuwa akiishi na watu wake kwa kufuata misingi anayoiridhia yeye na anajitenga mbali nao katika hali uovu wao na uchafu wao, na alikuwa akiwanusuru mayatima na wasiokuwa na waume, mpaka alipokaribia miaka arobaini alipata dhiki kwa yale aliyoyaona ya uovu,ikabidi akaanza kujitenga mbali na watu kwa ajili ya kumwabudu Mola wake na anamuomba amuongoze katika njia iliyo ya sawa. Na wakati akiwa katika hali hiyo mara akateremkiwa na Malaika na Wah'yi (Ufunuo) kutoka kwa Mola wake, akamuamrisha aifikishe Dini hii kwa watu, na awalinganie kunako Ibada ya Mola wao na waache kuabudu asiyekuwa Yeye, Wah'yi (Ufunuo) ukaendelea kuteremka kwake siku baada ya siku na mwaka baada ya mwaka ukiwa umebeba sheria na hukumu mbalimbali, mpaka Mwenyezi Mungu alipoikamilisha Dini hii kwa viumbe, na akawatimizia neema kwa ukamilifu wake, na zama yalipo kamilika majukumu yake Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake Mwenyezi Mungu alimfisha na umri wake wakati huo ulikuwa ni miaka 63, miongoni mwa miaka hiyo ni kwamba miaka 40 kabla ya Utume na miaka 23 akiwa ni Nabii na Mtume.

Na mwenye kuzingatia hali za Manabii na akasoma historia zao atafahamu ufahamu wa yakini ya kwamba kila njia iliyothibiti kwa Manabii waliopita basi imethibiti pia kwa Mtume Muhammad rehma na amanin za Allah ziwe juu yake.

Utakapo tazama namna ulivyo nukuliwa Utume wa Mussa na Issa amani ya Allah iwe juu yao, utajua ya kwamba Utume huo ulinukuliwa kwa njia ya upokezi usiokuwa na mashaka (Mutawatir), na upokezi huohuo usiokuwa na shaka ulionukuliwa juu ya Utume wa Muhammad ndio upokezi mkubwa na wenye usahihi zaidi kwasababu zama za Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake ndiyo zama za karibu.

Na vilevile habari zilizo nukuliwa kuhusu miujiza yao na alama za Utume wao, vyote hivyo kwa Mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni vikubwa, kwasababu miujiza yake ni mingi, na muujiza mkubwa kuliko yote ni Qur'ani tukufu ambayo mpaka leo imeendelea kunukuliwa kwa riwaya sahihi zisizokuwa na shaka (Mutawatir) kwa sauti na kwa kuandika.([170])

Na mwenye kulinganisha kati ya aliyokuja nayo Mussa na Issa amani ya Allah iwe juu yao na yale aliyokuja nayo Mtume wetu Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake miongoni mwa aqida iliyo sahihi na sheria madhubuti na elimu zenye manufaa atajua kwamba vyote hivyo vinatoka katika chanzo kimoja nacho ni chanzo cha Utume,

na mwenye kulinganisha baina hali za wafuasi wa Mitume waliotangulia na wafuasi wa Mtume Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake atajua ya kwamba walikuwa wote ni watu bora na watu wa kheribali kila wafuasi wa Mitume waliotangulia walikuwa na athari kubwa kuliko waliokuja baada yao, walieneza Tauhidi na uadilifu na walikuwa ni rehma kwa watu madhaifu na masikini.([171])

Na ukitaka ubainifu zaidi utakaotolea ushahidi juu ya Umtume wa Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake nitakutolea dalili na alama alizopata Ally bin Rabban Twabriy wakati alipokuwa Mkristo akasilimu kwasababu ya dalili na alama hizo, na miongonimwa alama hizo:

1-Ni kwamba Mtume alilingania watu kumuabudu Allah Mmoja na kuacha kuabudu asiyekuwa Allah ambayo ni kazi ya Mitume wote.

2-Alionyesha miujiza ya wazi ambayo hakuna anaeweza kuileta isipokuwa Mtume wa Allah.

3-Alielezea matukio yatukio yatakayo tokea baadae na yakatokea kama alivyo elezea.

4-Alielezea juu ya matukio yote katika matukio ya dunia na mzunguko wake na yakatokea.

5-Kitabu alichokuja nacho Mtume wetu Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake ni Qur'an ambayo ni alama miongoni mwa alama za Utume, kwasababu ni Kitabu chenye ufasaha zaidi, na Mwenyezi Mungu akakiteremsha kwa mtu asiyejua kusoma wala kuandika, na akawapa changamoto wenye ufasaha kwamba walete mfano wake au mfano wa Sura moja tu! Na kwasababu Allah alichukua dhamana ya kukihifadhi na akaihifadhi aqida sahihi kupitia Qur'an na sheria iliyo kamilika akaiweka katika Qur'an na akakisimamisha Kitabu hicho kwa Umma ulio bora.

6-Yeye ni mwisho wa Mitume na laiti kama asingelitumwa ungebatilika Utume wa Manabii waliobashiria Utume wake.

7-Hakika Mtume amani za Allah ziwe juu yao waliutabiri Utume wake kabla hajatokea kwa muda mrefu, na wakasifia Utume wake na Nchi yake na Umma na Wafalme kumnyenyekea na wakataja kuenea Dini yake.

8-Hakika kuwashinda nyumati waliompiga vita ni dalili miongoni mwa za Utume wake, haiwezekani mtu kudai kuwa yeye ni Mtume wa Allah ilihali yeye ni muongo kisha Mwenyezi Mungu anamnusuru na kumpa nguvu na kuwashinda maadui zake na kuenea ulinganio wake nakuwa wengi wafuasi wake, hakika haya hayawezi kuwa isipokuwa kwa Mtume mkweli.

9-Yale aliyokuwa nayo katika ibada zake na kujizuia na maasi na ukweli wake na historia yake nzuri na Sunna zake na sheria zake vyote hivi havikusanyiki isipokuwa kwa Nabii ambae ni mkweli.

Na alisema huyo aliyeongoka baada ya kuzungumza ushuhuda huu: (Haya ni mambo yenye nuru na ushahidi wenye kujitosheleza mwenye kuyapata atakuwa ni Nabii na atakuwa ameshinda kombe lake na haki yake imeshinda na itakuwa ni wajibu kumsadikishana mwenye kukataa na kukanusha Utume huo juhudi zake zitakuwa zimeenda patupu na atakuwa amepata hasara duniani na Akhera).([172])

Na katika hitimisho la kipengele hiki nitakuletea ushahidi wa aina mbili, ushahidi wa Mfalme wa Roma ambaye aliishi katika zama za Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake na ushahidi wa Muhubiri wa Kiingereza wa zama hizi anayejulikana kama John Senet.

 Ushuhuda wa Hiraqli:

Ametaja Imamu Bukhar Allah amrehemu khabari ya Abiy Sufiyani alipoitwa na Mfalme wa Roma akasema: (Alituelezea Abuu Al Yamama Al Hakam bin Naafi'i alitueleza Shuaybu kutoka kwa Zuhri alisema: Alinieleza Ubeydi LLahi bin Abdillahi bin Utbah bin Mas'ud ya kwamba Abdillahi bin Abas alimueleza kuwa Abaa Sufiyani bin Harbi alimueleza ya kwamba Hiraqli alimtumia mjumbe Abuu Sufiyani katika msafara wa Maqureshi na walikuwa ni wafanya biashara katika Mji wa Sham katika muda ambao Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake([173])alikuwa amefanya mapatano ya Sulhul Hudaybiya baina ya Abuu Sufiyani na makafiri wa Kiqureshi - na mkataba huo ulikuwa ni wa miaka kumi na ujumbe huo ulifika katika mwaka wa sita tangu Mtume kuhama kutoka Makka kwenda Madina, rejea Fathul Baar, V.1, Uk. 34 – wakamwendea Hiraqli wakiwa katika Mji wa Iliyaai([174])(ni Mji katika Miji ya Sham), Hiraqli akawaita katika kikao chake (majlisi) akiwa amezungukwa na viongozi wakubwa wa Kiroma na akamwita mtu wa kutafsiri maneno yake akasema: Ni nani mwenye nasabu ya karibu na mtu huyu ambaye anadai kwamba yeye ni Mtume?  Abuu Sufiyani akasema: Nikajibu mimi ndiye mwenye nasabu ya karibu, Hiraqli akasema: Msogezeni karibu yangu na wasogezeni ndugu zake karibu mgongo wangu, kisha akamwambia mfasiri wake: Waambie mimi namuuliza huyu Abuu Sufiyani kuhusu mtu huyo (Mtume) akinidanganya basi mkadhibisheni, Abuu Sufiyani akasema: Namuapia Allah lau ingekuwa siyo aibu wao kunijua mimi ni muongo basi ningesema uongo kuhusu Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake, kisha ikawa swali la kwanza aliloniuliza kuhusu Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake alisema hivi: Vipi nasabu yake kwenu?  Nikasema: Yeye ana nasabu tukufu kwetu, Hiraqli akauliza: Kuna yeyote aliyedai Utume miongoni mwenu kabla yake?  Nikasema: Hapana, Hiraqli akauliza: Katika Baba zake kulikuwa kuna Mfalme?  Nikasema: Hapana, akauliza: Watu watukufu wanamfuata au ni madhaifu tu?  Nikasema: Wanaomfuata ni watu madhaifu, akauliza: Hao wanaomfuata wanazidi kila siku au wanapungua?  Nikasema: Wanazidi kila siku, akauliza: Je! Kuna mtu anaritadi miongoni mwao kwa kuchukizwa na Dini yake baada ya kuwa ameshaingia?  Nikasema: Hapana, akauliza: Je! Mlikuwa mnamtuhumu uongo kabla hajasema hayo aliyo yasema?  Nikasema: Hapana, akauliza: Je! Anafanya khiyana?  Nikasema: Hapana, anasimulia Abuu Sufiyani: katika hali ambayo sisi tupo kwa Mfalme Hiraqli hatukujua ni nini atakacho tufanya baada ya hayo maswali, na sijkuweza kusema chochote zaidi ya neno ndiyo au hapana.

Hiraqli akaendelea kuuliza: Je! Mlimpiga vita?  Nikasema: Ndiyo, akauliza: Vita vyenu kwake vilikuwaje?  Nikasema: Vita baina yetu na yeye ilikuwa ni kushindana mara anatupiga na sisi tunampiga, akauliza: Anawaamrisha nini?  Nikasema: Anasema muabuduni Allah Mmoja na msimshirikishe na chochote, na acheni yanayosemwa na Baba zenu, na anatuamrisha kuswali na kuwa wakweli na kujiepusha na mambo machafu na kuunga udugu.

Hiraqli akamwambia mfasiri wake: Mweleze nimekuuliza kuhusu nasabu yake ukasema kuwa ana nasabu tukufu, vilevile Mitume wanatumwa katika nasabu ya watu wake, na nimekuuliza kuna yeyote miongoni mwenu aliyewahi kusema maneno kama yake, ukasema hapana, lau kama kungelikuwa na yeyote aliyewahi kusema maneno kama yake kabla yake ningelisema mtu huyo anafuata kauli iliyosemwa na mtu kabla yake, na nimekuuliza kwamba katika Baba zake kulikuwa na Mfalme, ukasema hapana, nasema: Katika Baba zake kama kungelikuwa na Mfalme ningesema mtu huyo anatafuta Ufalme wa Baba yake, na nimekuuliza je! Mlikuwa mnamtuhumu uongo kabla hajasema hayo aliyoyasema, ukasema hapana, kama angeliwahi kusema uongo tungejua kwamba hawezi kuacha kudanganya watu na kumsemea uongo Mwenyezi Mungu, na nimekuuliza watu watukufu ndio wanaomfuata au ni watu madhaifu, ukasema kuwa watu madhaifu ndio wanao mfuata, na watu madhaifu ndio wanaofuata Mitume, na nimekuuliza je! Wanazidi au wanapungua, ukasema kwamba wao wanazidi, hivo ndivyo linavyokuwa jambo la imani mpaka litakapo timia, na nimekuuliza hivi anaritadi yeyote kwa kuichukia Dini yake baada ya kuingia, ukasema hapana, vilevile imani pindi furaha yake inapoingia moyoni haiwezi kutoka, na nimekuuliza je! Anafanya khina, ukasema hapana, vilevile Mtume hawafanyi khiyana, nimekuuliza nini anakuamrisheni, ukasema kwamba anakuamrisheni juu ya kumuabu Allah na msimshirikishe na chochote na anakukatazeni kuabudu mizimu na anakuamrisheni kuswali na kutoa sadaka na kujizuia na mambo machafu, ikiwa kama unayoyasema ni kweli mtu huyo atamiliki sehemu nilipoweka miguu yangu miwili, na nilikuwa najua kuwa mtu huyu niwa nje sikuwa najua kama ni miongoni mwenu, lau ningekuwa najua kuwa ndiye ninaye mtakasia niya basi ninge weka uzito wa kuonana naye, na laiti ningekuwa kwake basi ningemuosha miguu yake, kisha akaitisha barua ya Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake ambayo Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake alimpa Dihiyah aipeleke kwa Mfalme wa Buswriy akampa Hiraqli akaisoma ikawa yaliyomo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, kutoka kwa Muhammad ambae ni mja wa Allah na Mtume wake kwenda kwa Hiraqli Mfalme wa Roma, amani iwe juu ya mwenye kufuata uongofu, baada ya hayo, mimi nina kulingania kwa ulinganio wa Kiislamu, silimu utasalimika na Mwenyezi Mungu atakupa malipo mara mbili, na ukikataa utakuwa na madhambi sawa na wanaoabudu moto.([175]) Na enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Miungu badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi eni ya kwamba sisi ni Waislamu.([176])

 Ushuhuda Wa Muhubiri Wa Kiingereza Wa Zama Hizi John Senet:

Anasema: Baada ya kufanya utafiti endelevu juu ya ufafanuzi wa Uislami na vyanzo vyake katika kuhudumia mtu mmoja mmoja na jamii, na uadilifu wake katika kuisimamisha jamii juu ya misingi iliyo sawa ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu,nimejikuta ninauelekea Uislamu kwa akili yangu yote na roho yangu, na nimemuahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu tangu siku hiyo nitakuwa mlinganizi wa Uislamu nikiwa ni mwenye kubashiria watu juu ya uongofu wake katika kila sehemu.

Na amefikia katika yakini hiyo baada ya kusoma kwake Ukristo na kuzama katika Ukristo, akakuta Ukristo haujibu maswali mengi yanayo zunguka katika maisha ya watu, akaanza kuingiwa na mashaka kisha akaanza kusoma Ukomunisti na Ubuddha hakupata anacho kitafuta, kisha akasoma Uislamu na akazama ndani yake akauamini na akaulingania.([177])

 Mwisho Wa Utume

Umefahamu katika yaliyo tangulia ukweli kuhusu Utume na alama zake, na dalili za Utume wa Nabii wetu Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na kabla sijazungumzia mwisho wa Utume lazima ufahamu kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hamtumi Mtume isipokuwa kwa sababu zifuatazo:

1-Ujumbe wa Mtume uwe ni maalumu kwa watu wake, na Mtume huyu hajaamrishwa kufikisha ujumbe wake kwa umma ulio karibu yake, Mwenyezi Mungu hutuma Mtume mwingine kwa ujumbe maalum kwa ule umma mwingine.

2-UJumbe wa Mtume aliyetangulia uwe umesahaulika, Mwenyezi Mungu humtuma Mtume kwa ajili ya kuhuisha Dini yao.

3-Sheria ya Mtume aliyetangulia iwe ni ya watu wa zama zake na isinasibiane na zama zijazo, Mwenyezi Mungu humtuma Mtume akiwa na ujumbe na sheria zinazo nasibiana na zama na mahala walipo, na hekima ya Allah Mtukufu ilipelekea kumtuma Mtume Muhammad amani za Allah ziwe juu yake na ujumbe wa wote wa ardhini, unaonasibiana na wakati na zama, na akauhifadhi ujumbe huo kutokana na mikono ya wenye kubadilisha na kugeuza, ili ujumbe wake ubaki hai na uhuishe maisha ya watu, ukiwa umetakasika kutokana na uchafu wa wapotoshaji na wabadilishaji, na kwasababu hiyo Mwenyezi Mungu kaufanya uwe ni ujumbe wa mwisho wa Mitume.([178])

Miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyafanya ni maalum kwa Mtume amani za Allah ziwe juu yake ni kwamba yeye ni mwisho wa Mitume hakuna Mtume baada yake, kwasababu Mwenyezi Mungu amekamilisha ujumbe wake kwa Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake na akahitimisha sheria yake kwake na kwa ajili hiyo utabiri wa Yesu juu ya Mtume Muhammad amani za Allah ziwe juu yake ukakamilika pale aliposema: (Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.([179]) Na Mchungaji Ibrahimu Khalili "ambae alisilimu baadae" ameichukulia Aya hii kuwa inaafikiana na kauli ya Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake aliyojiongelea mwenyewe akisema: Hakika mfano wangu mimi na mfano wa Manabii waliokuwa kabla yangu ni kama mtu aliyejenga nyumba nzuri na akaipendezesha lakini akaacha sehemu ya tofari moja katika kona, ikawa watu wanaizunguka nyumba hiyo na kuishangaa huku wakisema: Kwanini usingeliweka tofari hilo?  Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake akasema: Mimi ndiyo tofari hilo na mimi ni mwisho wa Mitume.([180])

Na kwasababu hiyo Kitabu alichokuja nacho Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake Mwenyezi Mungu alikifanya kiwe ni chenye kutawala na kufuta Vitabu vilivyopita, kama alivyoifanya sheria ya Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake kuwa ni yenye kufuta sheria zote zilizo tangulia, na Mwenyzi Mungu akachukua dhamana ya kuuhifadhi ujumbe wake, ikapokelewa upokezi usio na shaka, kwani Qur'an tukufu imekuja kwa upokezi usiokuwa na shaka vilele Sunna zake za maneno na vitendo, na umepokelewa utekelezaji wa kivitendo ambao upo katika sheria ya Dini hii na Ibada zake, Sunna zake na hukumu zake kwa upokezi usiokuwa na mashaka ndani yake.

Na mwenye kusoma vitabu vya kihistoria na hadithi za Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake atajua ya kwamba Maswahaba wa Mtume radhi za Allah ziwe juu yao walihifadhi hali zote za Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake na kauli zake na vitendovyake vyote, wakapokea Ibada zake alizokuwa akimfanyia Mola wake na Jihadi zke na namna alivyokuwa akimtaja Mola wake na kumuomba msamaha, pia walihifadhi ukarimu wake, ushujaa wake na maisha yake yote aliyoishi na Maswahaba wake, na namna alivyokuwa akipokea wageni, na kama walivyopokea kuhusu furaha yake na huzuni yake na safari zake na kuishi kwake, na sifa za kula kwake, kunywa kwake, kuvaa kwake, kulala kwake na kuamka kwake nk. Utakapohisi hayo utapata yakini ya kwamba Dini imehifadhiwa kwa hifadhi ya Mwenyezi Mungu, na wakati huo utajua ya kwamba Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake ndiye Mtume wa mwisho; kwasababu Mwenyezi Mungu ametueleza ya kwamba Mtume huyu ndiye Mtume wa mwisho, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii.([181]) Na alisema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake akijizungumzia mwenyewe: (Na nimetumwa kwa watu wote na Mimi ndiyo hitimisho la Mitume. ([182])

Na huu ndio muda wa kuweka wazi maana ya Uislamu na kubainisha uhakika wake na vyanzo vyake, nguzo zake na daraja zake.

 Maana Ya Neno Uislamu

Utakapo rejea vitabu vya lugha utafahamu ya kwamba maana ya neno Uislamu "Ni kuzingatia na kunyenyekea na kutii na kujisalimisha na kutekeleza amri ya mwenye kuamrisha na makatazo yake bila kupinga" na Mwenyezi Mungu ameiita Dini ya haki kuwa ni Uislamu, kwasababu ni Dini inayomfanya mtu amtii Mwenyezi Mungu na atekeleze amri zake bila kupinga na kumtakasia Ibada Mwenyezi Mungu na kumuamini, na limekuwa jina la Uislamu ndilo jina la Dini aliyokuja nayo Muhammad rehma na amani ziwe juu yake.

Maana Ya Uislamu*([183])

Kwanini Dini imeitwa Uislamu?  Hakika dini tofauti zilizopo duniani zimeitwa kwa majina yake, ima kwa kunasbishwana jina la mtu maalum au umma maalum, Ukristo umetokana na jina "Kristo", na Ubuddha umetokana na aliye uanzisha (Budha), na dini ya Zaraadishiyah (Zoroastrianism) ilijulikana kwa jina hilo kwasababu muasisi wake alikuwa ni Zoroaster, na vilevile ulidhihiri Uyahudi kutokana na kabila linalojulikana kama Yahudha ukaitwa "Uyahudi" na kuendelea. Isipokuwa Uislamu, haunasibishwi na mtu maalum wala umma, Uislamu jina lake linaonyesha sifa maalum ambayo ni miongoni mwa maana za neno Uislamu, na miongoni mwa yanayodhihiri kuhusu jina hili ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyekusudia kuileta Dini hii au kuiasisi, na wala siyo Dini maalum kwa umma mmoja tu, bali hakika lengo la Uislamu ni kutaka watu wote duniani wajipambe na sifa ya Uislamu, na anakuwa ni Muislamu yeyote mwenye kujipamba na sifa hii iwe ni kwa wale waliotangulia au hawa wa zama hizi na watakaokuja.

 Ukweli Kuhusu Uislamu

Inajulikana kwamba kila kitu katika dunia hii kinaongozwa na kanuni maalum na njia iliyothibiti, jua na mwezi na nyota na ardhi vimeamrishwa kufuata kanuni maalum, haviwezi kuhama mahala pake wala kuondoka hata kiasi cha unywele, hata mwanadamu mwenyewe ukizingatia mambo yake itakubainikia kwamba yeye ameumbwa kwa ajili ya kutii amri za Mwenyezi Mungu, hapumui wala kuhisi shida yoyote ya kuhitaji maji na vyakula na nuru na joto isipokuwa kwa mipangilio ya Mwenyezi Mungu mwenye kupangilia maisha yake, na viungo vyote vinatekeleza mipangilio hiyo, kazi zinazo fanywa na viungo hivyo haziwezi kufanyika isipokuwa kwa kutekeleza yale aliyoyapanga Mwenyezi Mungu.

Hii ni mipangilio ya vitu vyote, na kila kilichopo ulimwenguni kinalazimika kujisalimisha chini ya mipangilio hiyo kuanzia sayari kubwa kuliko zote mbinguni mpaka na mdudu chungu aliyoko ardhini, nayo ni mipangilio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenye Ufalmena Mpangiliaji wa mambo. Ikiwa vitu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini vinafuata mipangilio hiyo basi ulimwengu ni wenye kumtii huyo Mfalme aliyepangilia na kuviweka vitu vyote, na ni wenye kutekeleza na kufuata amri zake, na inabainika kutokana na muelekeo huo kwamba Uislamu ni Dini ya ulimwengu mzima, kwasababu Uislamu maana yake ni kufuata na kutekeleza amri za mwenye kuamrisha na makatazo yake bila kupinga kama ilivyo elezewa hapo nyuma. Jua na mwezi na ardhi vimejisalimisha, na hewa, maji, nuru, giza na joto vimejisalimisha, miti, mawe na wanyama vimejisalimishabali hakika mwanadamu asiyemjua Mola wake na anakanusha kuwepo kwake na kuzikataa Aya zake au ana abudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na anamshirikisha kitu kingine, mtu huyo pia amejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa maumbile yake aliyombiwa na Mwenyezi Mungu.

Na kama umeyafahamu hayo basi njoo tumtazame mwanadamu, utamkuta mwanadamu anavutwa na mambo mawili:

1-Maumbile aliyoumbiwa na Mwenyezi Mungu, ikiwemo kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na mapenzi ya kumuabudu na kujikurubisha kwake, na kuyapenda yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu miongoni mwa haki na mambo ya kheri na ukweli, na kuyachukia yale yote anayo yachukia Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo ya batili na shari na jeuri na dhulma,na mfano wa hayo katika mambo yanayo pendwa na nafsi, kama vile kupenda mali na mke na watoto, na kupenda kula, kunywa na kuoa, na yote na yanayo fanana katika mambo yanayo fanywa na viungo.

2-Matakwa ya mwanadamu na khiyari yake, Mwenyezi Mungu amemtumia mwanadamu Mitume na akateremsha Vitabu ili apambanue baina ya haki na batili uongofu na upotevu, kheri na shari, na akampa akili na ufahamu ili awe na busara katika kuchagua kwake, akitaka atapita katika njia ya kheri njia ambayo itampeleka katika haki na uongofu, na akitaka atapita katika njia ya shari njia ambayo itampeleka katika balaa na maangamizi.

Ukimtazama mwanadamu kwa kuzingatia lile jambo la kwanza utamkuta kaumbwa kwa maumbile ya kujisalimisha, na kulazimika kufuata sheria,

Na ukimtazama mwanadamu kwa kuzingatia jambo la pili utamkuta ni mwenye khiyari wa kuchagua anacho kitaka, ima awe ni Muislamu au awe ni kafiri, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru}.([184])

Kwasababu hiyo utawakuta wameganyika katika sehemu mbili:

Mwanadamu anaemjua Muumba wake na kuamini kuwa ni Mola wake na Mfalme wake na Mungu wake ambae anamuabudu, na anafuata sheria yake katika maisha yake ya kuchagua dini anayoitaka, kama alivyoumbwa kutokana na maumbile ya kujisalimisha kwa Mola wake, hakunawa kumtoa katika maumbile hayo na ni mwenye kufuata mipangilio ya Mola wake, na huyo ndiye Muislamu aliye kamilika ambae Uislamu wake umekamilika, na elimu yake imekuwa sahihi kwasababu yeye kamjua Mwenyezi Mungu aliye muumba na akamtumia Mitume na akamruzuku maarifa na elimu yenye nguvu, na akili yake ikawa sahihi na rai yake ni yenye kupatia, kwasababu ameyafanyia kazi mawazo yake kisha akahukumu ya kwamba hawezi kumuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mola aliyemkirimu kipaji cha ufahamu na kufikiria katika mambo, na ulimi wake ukawa salama katika kutamka haki, kwasababu yeye hamkubali yeyote isipokuwa Mola Mmoja ambae amemneemesha uwezo wa kutamka na kuzungumza, mtu huyo hawezi kusema chochote katika maisha yake isipokuwa ukweli,kwasababu yeye anafuata sheria ya Mwenyezi Mungu katika yale ambayo anakhiyari nayo, na kuna uhusiano mzuri baina yake yeye na viumbe wengine ulimwengunikwasabu yeye hakiabudu chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mwenye Hekima na Mjuzi ambae viumbe wote wanamuadu Yeye na kutekeleza amri yake, na wanafuata mipangilio yake, na amevidhalilisha viumbe hivyo kwa ajili yako wewe mwanadamu.

 Uhakika Wa Ukafiri

Na kwa upande mwingine ni mtu aliyezaliwa na akaishi maisha yake yote akiwa ni mwenye kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu bila ya kujua kuwa amejisalimisha kwake, na hakumjua Mola wake wala kuamini sheria yake wala kumfuata Mtume wake, na hakuitumia elimu naakili aliyopewa na Mwenyezi Mungu katika kumtambua Mola wake liyemuumba na akampa masikio na macho, akakanusha kupo kwa Mwenyezi Mungu na akafanya kiburi katika kumuabudu, na akakataa kufuata sheria yake katika yale ambayo ana haki ya kuyatumia na anakhiyari nayo katika maisha yake au akamshirikisha Mola wake na kitu kingine, na akakataa kuamini dalilizake zinazo onyesha kuwa Yeye ni Mmoja, na huyo ndiyo kafiri.Kwasababu maana ya ukafiri ni kukisitiri kitu na kukifunika, mtu anitwa kafiri kwasababu ameyaficha maumbile yake na akayafunika kwa kifuniko cha ujinga na upumbavu, na imefahamika kwamba yeye amezaliwa katika maumbile ya Uislamu, na viungo vya mwili wake havijui chochote isipokuwa kufuata maumbile ya Uislamu, na dunia inayomzunguka haiendi isipokuwa kwa ni njia ya kujisalimisha, lakini yeye amejifunika kwa ujinga na upumbavu, na akaondokewa na maarifa ya kujua maumbile ya duni na maumbile yake mwenyewe, utamuona hawezi kutumia elimu yake na fikra zake isipokuwa katika yale yanayo tofautiana na maumbile yake, na haoni chochote isipokuwa kile kinachopingana na maumbile yake, na hafanyi bidii isipokuwa ni katika kufanya yale yanayo batilisha maumbile yake.

Ni juu yako sasa kukadiria mwenyewe juu ya yale ambayo yamewafanya makafiri wazame katika upotevu wa mbali na wawazi.([185])

Na Uislamu huu ambao wewe unatakiwa kuutekeleza sio Dini ngumu bali ni Dini nyepesi kwa yule aliyefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu, Uislamu ni Dini ambayo Ulimwengu mzima unaufuata, Na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda kisipende.([186]) Nayo ni Dini ya Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Hakika dini inayo kubaliwa kwa Mwenyezi Mungu ni Uislam}.([187]) Na Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata}.([188]) Na amebainisha Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwa kusema: (Ni kuusalimisha moyo wako kwa Mwenyezi Mungu, na kuuelekeza uso wako kwa Mwenyezi Mungu, na kutoa Zaka iliyofaradhishwa).([189]) Na bwana mmoja alimuuliza Mtume rehma na amani ziwe juu yake, Uislamu ni nini?  Mtume akasema: (Uislamu ni moyo wako kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na Waislamu wasalimike kutokana na ulimi wako na mikono yako), kisha akasema: ni Uislamu gani ulio bora?  Mtume akasema: (Ni Imani), akasema: Imani ni nini?  Mtume akasema: (Ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake, na Vitabu vyake, Mitume wake, na kufufuliwa baada ya kufa)).([190]) Kama Alivyo sema Mtume wa Allah Rehma na amani za Allah ziwe juu yake: (Uislamu ni kushahidilia ya kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa isipokuwa Allah Mmoja na kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allah, na kusimamisha Swala na kutoa Zaka, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan, na kwenda kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo.([191]) Na kauli yake Mtume: (Muislamu ni amabae wamesalimika Waislamu kutokana na ulimi wake na mkono wake.([192])

Na Dini hii ndiyo Dini ya Uislamu ambayo Mwenyezi Mungu hapokei dini isiyokuwa hiyo, si kwa watu wa zamani wala kwa watu wa sasa, hakika Mitume wote ni Waislamu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimzungumzia Nabii Nuhu: {Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula. Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu}.([193]) Na amesema Allah Mtukufu kuhusu Nabii Ibrahim{Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote}.([194]) Amesema Allah Mtukufu kuhusu Nabii Mussa:{Na Musa alisema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu}.([195]) Na amsema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Nabii Issa: {Na nilipo wafunulia Wanafunzi kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu}.([196])

Na Dini hii ya Uislamu sheria zake na itikadi zake na hukumu zake zinatokana na Ufunuo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunnah za Mtume rehma na amani ziwe juu yake, na nitakutajia kwa ufupi historia ya Uislamu kwa ufupi.

 Misingi Ya Uislamu Na Vyanzo Vyake

Wafuasi wa dini batili wamezoea kukitukuza kitabu kilicho rithiwa katika jamii zao kilichoandikwa katika zama zilizo pita, na anaweza asijulikane aliyekiandika wala aliye kitafsiri, wala zama ambazo viliandikwa vitabu hivyo, na si vinginevyo walioviandika viatabu hivyo ni watu ambao wanapatwa na udhaufu, mapungufu, matamanio na kusahau kama watu wengine.

Ama Uislamu unatofautiana na dini zingine kwasababu unategemea vyanzo vyenye ukeweli (Ufunuo wa Mwenyezi Mungu) ambao ni Qur'an na Sunnah, na yafuatayo ni ufafanuzi wa Qur'an na Sunnah kwa ufupi.

 Qur'an Tukufu:

Umejua katika yaliyo tangulia ya kwamba Uislamu ni Dini ya Mwenyezi Mungu, na kwasababu hiyo Mwenyezi Mungu aliteremsha Qur'an juu ya Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake ikiwa ni uongofu kwa wacha Mungu na ni katiba ya Waislamu na ponyo kwa nyoyo ambazo Mwenyezi Mungu amezipangia kupona na ni taa kwa wale ambao MwenyeziMungu ametaka wafanikiwe, Qur'an imekusanya misingi ambayo ndio sababu ya kutumwa Mitume([197])Na Qur'an haikuwa ya kwanza kushuka katika Vitabu vya Allah kama ilivyokuwa kwamba Mtume rehma na amani ziwe juu yake siyo wa kwanza kutumwa katika Mitume, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alimteremshia Nabii Ibrahim Kurasa na akamkirimu Nabii Mussa kwa Taurati, na Daud akampa Zaburi, na Nabii Issa akaja na Injili, na Vitabu hivyo ni Ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliowafunulia Manabii wake na Mitume wake, lakini Vitabu hivyo vilivyo tangulia vingi vilipotea na vikafutika baadhi yake na vikaingia na upotoshaji na kubadilishwa.

Ama Qur'an tukufu Mwenyezi Mungu amechukua dhamana ya kuihifadhi na akaifanya ndiyo kiongozi wa Vitabu vilivyo tangulia na ndiyo yenye kufuta hukumu ya Vitabu vilivyo tangulia, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda}.([198]) Na Mwenyezi Mungu aliyeiteremsha Qur'an akaisifia kuwa inabainisha kila kitu akasema:{Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu}.([199]) Na Qur'an ni uongofu na rehma amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema}([200])na inaongoza kunako Dini iliyo sahihi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa}.([201]) Na Qur'an inaongoza viumbe kunako njia ya sawa katika kila jambo miongoni mwa mambo ya kimaisha.

Qur'ani hii ni muujiza uliobaki wa Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake miongoni mwa miujiza itakayo baki mpaka siku ya Qiyama, hakika ilikuwa miujiza ya Mitume waliotangulia inaisha kwa kufa kwao,ama hii Qur'an Mwenyezi Mungu ameijalia kuwa ni hoja yenye kubakia.

Nayo ni hoja iliyo wazi na ni muujiza bora ambao Mwenyezi Mungu amewapa changamoto wanadamu walete mfano wake au Sura kumi mfano wake au Sura moja tu katika Sura zake, wakashindwa pamoja na kwamba Sura hizo zinatokana na herufi na maneno, na umma ulioteremshiwa Qur'an hiyo ni umma wenye lugha sanifu na fasaha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Ndiyo wanasema ameizua?  Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli}.([202])

Na miongoni mwa ushahidi ya kwamba Qur'an ni Ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kuwa imekusanya habari nyingi za watu walio tangulia, na ilieelezea matukio yatakayo tokea na yametokea kama ilivyo elezea, na imetaja hoja nyingi za kielimu ambazo Wanachuoni hawakuweza kuzikusanya isipokuwa katika zama hizi. Na miongoni mwa ushahidi unao onyesha kuwa Qur'an ni Ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba Mtume rehma na amani ziwe juu yake haikuzoeleka kwake yeye kutamka maneno ya Qur'an wala haikunukuliwa kwake maneno yanayo fanana na Qur'an kabla ya kushuka Qur'an, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Mwenyezi Mungu angeli taka nisingeli kusomeeni, wala nisingeli kujuvyeni. Kwani nalikwisha kaa nanyi umri mzima kabla yake! Basi, je! Hamzingatii?}.([203]) Bali Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa hajui kusoma wala kuandika wala hajawahi kwenda kwa Shekh kusoma, wala hakukaa kwa mwalimu yeyote lakini anawapa changamoto ya kuleta mfano wa Qur'an tukufu wataalamu wa lugha sanifu na fasaha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Na wewe hukuwa kabla yake unasoma kitabu chochote, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kulia. Ingeli kuwa hivyo wangeli fanya shaka wavunjifu}([204])Na huyu mtu asiyejua kusoma wala kuandika amesifiwa katika Taurati na Injili ya kwamba hajui kusoma wala kuandika lakini Mapadri wa Kiyahudi na Kinaswara waliokuwa na masalia ya Taurati na Injili walikuwa wakimwendea na kumuuliza juu ya yale waliyokuwa wanakhitilafiana ndani yake, na wanamfanya hakimu katika mambo wanayo zozana kwayo,amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akieleza habari ya Mtume katika Taurati na Injili:{Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu}.([205]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha swali la Mayahudi na Manaswara walilo muuliza Mtume rehma na amani ziwe juu yake: {Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni}.([206]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: {Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu}.([207]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake}.([208]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Qur'ani hii inawasimulia Wana wa Israili mengi wanayo khitalifiana nayo}.([209])

Na Askofu Ibrahim Filiphs alijaribu kufanya Research ya PHD kwa anuwani ya "Makosa yaliyomo katika Qur'an" lakini akashindwa kufanya hivo, Qur'an ikamshinda kwa hoja zake na dalili zake, akatangaza kushindwa kwaken na akajisalimisha kwa Mola wake na akasilimu.([210])

Na mmoja katika Waislamu pindi alipomzawadia Dr. Jeffrey Lang kutoka Marekani kitabu cha tafsiri ya maana ya Qur'an tukufu alikuta kwamba Qur'an inamzungumzia yeye na inajibu maswali yake, na inaondoa matatizo yaliyopo baina yake na baina ya nafsi yake,kisha akasema: "Hakika aliyeiteremsha Qur'an hii kana kwamba ananijua kuliko ninavyo ijua nafsi yangu"([211]) Kwanini asiseme maneno hayo wakati aliyeiteremsha Qur'an tukufu ndiye aliye muumba mwanadamu, naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari? }.([212]) Kisha ilikuwa kusoma kwake kile kitabu cha tafsiri ya maana ya Qur'an tukufu alicho zawadiwa ikawa ndiyo sababu ya kusilimu kwake, kisha akatunga kitabu hicho nilicho kunukulia maneno hayo.

Na Qur'an tukufu imekusanya yote anayo yahitaji mwanadamu, imekusanya misingi ya kanuni mbalimbali na itikadi na hukumu na miamala mbalimbali na adabu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote}.([213]) Ndani yake kuna ulinganizi wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutajwa majina yake na sifa zake na matendo yake, na inalingania kunako usahihi wa yale waliyokuja nayo Mitume na Manabii, na inathibitisha siku ya Qiyama na malipo na hesabu, na inatoahoja na dalili za wazi juu ya hilo,na inataja habari za nyumati zilizo pita na adhabu walizopata duniani, na yale yanayo wasubiri miongoni mwa adhabu na mateso siku ya Qiyama.

Na ndani ya Qur'an kuna dalili na hoja nyingi jambo ambalo linawashitua na kuwashangaza Wanachuoni, na Qur'an inakubaliana na kila zama, watafiti na Wanachuoni wanapata ndani ya Qur'an kile wanacho kitafuta na kukikusudia, na nitakutajia mifano mitatu ambayo itakuwekea wazi hayo niliyotaja, na miongoni mwa mifano hiyo:

1-Ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho}.([214]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru}.([215])

Na inajulikana kwamba Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake hakusafiri kwa njia ya maji, na haikuwa katika zama zake njia yoyote ya kifedha inayosaidia kugundua vina vya bahari. Hakuna aliyemweleza Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake kuhusu habari hizi isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Mtukufu.

2-Ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji}.([216]) Na Wanachuoni hawakugundua ufafanuzi huu wa kina kuhusu hatua za kuumbwa mtoto katika tumbo la ama yake isipokuwa katika zama hizi.

3-Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha}.([217]) Wanadamu hawakuzoea kufikiria mawazo haya yaliyokusanya vitu hivyo wala hawavifikirii, bali Wanachuoni wanapo gundua mmea fulani au mdudu na wakaandika yale wanayoyajua kuhusu huyo mdudu au mmea huwa tunastaajabishwa na jambo hilo pamoja na kwamba yale wasiyo yajua kuhusu vitu hivyo ni mengi kuliko waliyo yagundua.

Na Mwanachuoni wa Kifaransa Morris Bockay alilinganisha kati ya Taurati, Injili na Qur'an, na yale yaliyo gundulika kutokana na tafiti za kisasa kuhusu kuumbwa kwa mbingu na ardhi na kuumbwa kwa wanadamu, akakuta kwamba tafiti zote za kisasa zinaafikiana na yaliyokuja katika Qur'an, na akakuta katika Taurati na Injili zilizopo katika zama hizi zimekusanya taarifa nyingi zenye makosa kuhusu kuumbwa kwa mbingu na ardhi na kuumbwa kwa wanadamu na wanyama.([218])

 B- Sunnah Za Mtume:

   Mwenyezi Mungu Mtukufu aliteremsha kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake Qur'an tukufu, na akamfunulia mfano wa Qur'an ambayo ni Sunnah yenye kusherehesha kubainisha Qur'an, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Fahamuni hakika mimi nimepewa Qur'an na Mfano wake pamoja).([219]) Hakika Mwenyezi Mungu alimpa idhini ya kubainisha yaliyomo ndani ya Qur'an miongoni mwa hukumu zilizokuja kwa watu wote au zilizokuja kwa watu maalum au zilizokuja ujumla, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri}.([220])

Na Sunnah ipo katika chanzo cha pili katika vyanzo vya Uislamu, na maana ya Sunnah ni yote yaliyo pokelewa kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake kwa upokezi sahihi ulio shikamana mpaka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake katika kauli au vitendo au sifa au jambo lolote lililofanyika wakati wake na hakulikataza.

Na Sunnah ni Wah'yi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenda kwa Mtume wake Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, kwasababu Mtume rehma na amani ziwe juu yake hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa. Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu}.([221]) Nakika yeye anawafikishia watu yale aliyoamrishwa ayafikishe, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi}.([222])

Na miongoni mwa Sunnah zilizo takasika ni kutekeleza kwa vitendo Uislamu, hukumu zake, itikadi zake, ibada zake, miamala yake na adabu zake, Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa akitekeleza yale aliyo amrishwa na akiwabainishia watu na akiwaamrisha wafanye mfano wa vitendo vyake, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake:(Salini kama mlivyo niona nikisali).([223]) Na Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waumini wamfuate yeye katika vitendo vyake na maneno yake, ili ikamilike imani yao, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana}.([224]) Na Maswahaba watukufu radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao walinukuu kauli za Mtume rehma na amani ziwe juu yake na vitendo vyake kwa wale waliokuja baada yao na wao wakayahamishia kwa waliokuja baada yao, kisha yakaandikwa katika Vitabu vya Hadithi, na wale wenye kuandika hadithi walikuwa wanaweka masharti makali kwa wale wapokezi wa hadithi hizo, na walikuwa wakimtaka yule mwenye hadithi awe aliichukua moja kwa moja kwa yule mpokezi wa asili (kwa maana ya kuishi wote katika zama moja) ili upokezi uungane mpaka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake ((233)), na walikuwa wanaweka sharti kwamba wale wapokezi wa hadithi wawe ni waaminifu, waadilifu, wakweli na wenye kutunza amana.

Na Sunnah kama ilivyokuwa maana yake ni kutekeleza Uislamu kwa vitendo vilevile inabainisha maana ya Qur'an tukufu na kusherehesha Aya zake, na inapambanua hukumu zilizokuja kwa ujumla,kwasababu Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa anabainisha yale yanayo mshukia wakati mwingine kwa kauli na wakati mwingine kwa vitendo au vyote viwili kwa pamoja, na Sunnah inaweza ikajitegemea ikabainisha baadhi ya hukumu na sheria ambazo Qur'an haija zizungumzia.

Ni wajubu kuamini Qur'an na Sunnah ya kwamba ni vyanzo viwili vya msingi katika Dini ya Uislamu, vyanzo ambavyo ni wajibu kuvifuata na kurejea katika vyanzo hivyo na kufuata amri zake na kujiepusha na makatazo yake, na kusadikisha habari zake, na kuaminivyote vilivyomo ndani yake miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake na vitendo vyake, na yale Mwenyezi Mungu aliyo waandalia vipenzi vyake Waumini, na adhabu alizo waahidi makafiri, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa}.([225]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na yale aliyo kuleteeni Mtume basi yachukueni na yale alio kukatazeni yaepukeni}.([226])

Na baada ya kuweka wazi vyanzo vya Dini hii, inapendeza tukitaja daraja za Uislamu nazo ni: Uislamu, Imani na Ihsani, na tutazungumza kwa ufupi nguzo za daraja hizo.

 Daraja La Kwanza*

Uislamu: Na Nguzo Zake Ni Tano, Nazo Ni: Shahada Mbili, Na Swala, Na Zaka, Na Kufunga Mwezi Wa Ramadhan, Na Kuhiji.

Nguzo Ya Kwanza: Ni kushahidilia ya kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake.

Na maana ya Shahada ya "Laa ilaha ila LLah": Hapana anaepasa kuabudiwa kwa haki katika ardhi hii au mbinguni isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, Yeye ndiye Mungu wa kweli na miungu wengine wasiokuwa Yeye ni batili([227]) na neno hilo linampelekea Muislamu kumtakasia Ibada Mwenyezi Mungu peke yake, na kukanusha Ibada kwa asiyekuwa Yeye peke yake, na neno hilo halimnufaishi mwenye kulisema mpaka yakamilike mambo mawili:

1-Ni kusema "Laa ilaha ila LLah" kwa kuitakidi moyoni na kuwa na elimu na yakini na kusadikisha pamoja na mapenzi.

2-Ni kukufuru yote yanayo abudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, mwenye kutamka Shahada hiyo bila ya kukufuru kinacho abudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu neno hilo halitomfaa.([228])

Na maana ya Shahada ya kwamba "Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu": Ni kumtii Mtume katika yale aliyo yaamrisha, na kumsadikisha katika yale aliyo yaeleza, na kujiepusha na yale aliyo yakataza na kuyakemea, na asiabudiwe Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa namna alivyo elekeza,na ifahamike na kuaminiwa ya kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote, na kwamba yeye ni mja tu wala haabudiwi, na ni Mtume asiye kadhibishwa na anatiiwa na kufuatwa, mwenye kumtii ataingia Peponi na mwenye kumuasi ataingia Motoni, ifahamike na kuaminiwa kwamba kupokea sheria sawa ni katika Itikadi au Ibada alizo amrisha Mwenyezi Mungu, au nidhamu za utawala na kuweka sheria au katika mambo ya kimaadili au katika nyanja za kujenga familia au katika mambo ya kuhalalisha na kuharamisha...yote hayo hayawi isipokuwa kwa njia ya Mtume huyu mtukufu Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, kwasababu yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu mwenye kufikisha sheria yak.([229])

Nguzo Ya Pili Ni Swala:* Nayo ni nguzo ya pili katika Uislamu na ni muhimili wa Uisalamu, kwasababu ni kiunganisho kati mja na Mola wake, mja anaswali kila siku mara tano, anaitakasa imani na anaisafisha nafsi yake kutokana na uchafu wa madhambi, na Swala inazuia uchafu na madhambi, mja anapoamka asubuhi anasimama mbele ya Mola wake akiwa twahara na msafi kabla ya kujishughulisha na kazi za kidunia, kisha anamtukuza Mola wake na anakiri utumwa wake na anamuomba Mwenyezi Mungu msaada na uongofu, na anatekeleza ahadi iliyopo kati yake na Mola wake ya utiifu na utumwa pindi anaposujudu na kusimama na kurukuu, anafanya hivo mara tano kwa siku, na ili atekeleze Ibada hiyo ya Swala inalazimika awe ni msafi katika moyo wake, mwili wake, nguo zake na sehemu ya kuswalia, Muislamu aitekeleze kwa jamaa pamoja na ndugu zake Waislamu wakiwa ni wenye kuzielekeza nyuso zao upande wa Al Kaabah tukufu nyumba ya Allah, Swala imewekwa kiukamilifu zaidi na iliyo bora ni ile ambayo mja anaifanya kwa ajili ya Mola wake aliyemuumba, pamoja na kumtukuza Mola wake kwa kushirikiana na viungo vyake, ikiwemo kutamka kwa ulimi na kazi za mikono miwili na miguu miwili na kichwa na mawazo na viungo vingine vilivyobaki, kila kimoja kinachukua nafasi katika Ibada hii tukufu.

Na mawazo na viungo vinachukua nafasi yake, na moyo unachukua nafasi yake, Ibada hiyo imekusanya sifa na shukurani na kutukuza na kutakasa na kuadhimisha, na ushuhuda wa kweli,na kusoma Qur'an na kusimama mbele ya Mola mlezi kisimamo cha mja aliyedhalili na aliye mnyenyekea Mola mwenye kumpangilia mambo yake, kisha ajidhalilishe kwake katika kisimamo hicho na anyenyekee na ajikurubishe kwake, kisha baada ya hapo arukuu, asujudu na akae kwa unyeyekevu moyo wake ukiwa umevunjika vunjika na viuongo vyake vikiwa ni vyenye khofu kwa kujidhalilisha kutokana na Utukufu na Ukubwa wa Mwenyezi Mungu, kisha amalize Swala yake kwa kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, kisha amuombe Mola wake kheri za dunia na Akhera.([230])

 Nguzo Ya Tatu Ni Zaka:*

Nayo ni nguzo ya tatu katika nguzo za Uislamu na ni wajibu kwa Muislamu tajiri atoe Zaka ya mali yake nayo ni sehemu ndogo sana, na anaitoa kwa masikini na fakiri na wengineo katika wale wanaopaswa kupewa.

Muislamu ni wajibu kuitoa Zaka kwa wanao stahiki kwa moyo ulio safi, wala asiwasimbulie na kuwaudhi wale aliowapa, na ni wajibu kuitoa Zaka kwa kutarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu asitake malipo wala shukurani kutoka kwa mwanadamu, bali aitoe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na siyo kwa kujionyesha.

Na kutoa Zaka kunaleta baraka, na kunafanya nafsi za mafukara na masikini na wenye shida kusafika, na kuwatoshelezea kutokana na udhalili wa kuomba, na kuwahurumia kutokana na shida pamoja na kuharibikiwa pindi watakapo achwa na matajiri, na kutoa Zaka ni kusifika na sifa ya ukarimu na kutoa na kuwapendelea watu kheri na huruma, na ni kuepukana na sifa za ubakhili na kujikweza, na ndani yake kuna kushikamana Waislamu na matajiri kuwahurumia masikini, na Zaka hii ikitekelezwa ipasavyo hatopatikana fukara wala mtu mwenye madeni wala msafiri aliye katikiwa na safari katika jamii.

Nguzo Ya Nne Ni Swaumu* : Nayo ni Swaumu ya mwezi wa Ramadhan kutoka kuchomoza kwa alfajiri mpaka kuzama kwa jua, mfungaji anacha chakula na kinywaji na tendo la ndoa kwa ajili ya kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anaizuia nafsi yake kutokana matamanio, Na Mwenyezi Mungu amemfanyia wepesi mgonjwa na msafiri na mwenye mimba na kunyonyesha na mwenye hedhi na nifasi, kila mmoja ana hukumu yake inayo muhusu.

Na katika mwezi huo Muislamu anajizuia nafsi yake kutokana na matamanio, kutokana na ibada ya Swaumu nafsi ya Muislamu inatoka katika kufanana na wanyama na kuelekea kufanana na Malaika, kiasi kwamba aliyefunga anafanana na mtu asiyekuwa na shida yoyote katika dunia hii isipokuwa anatafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Swaumu inahuisha moyo, na inamfanya mtu aipe nyongo dunia, na kuyatarajia yale yaliyopo kwa Mwenyezi Mungu, na inawafanya matajiri wawakumbuke masikini na hali zao na inakuwa ni sababu ya nyoyo zao kuwahurumia na kujua waliyonayo miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu basi huwafanya wazidi kumshukuru Mwenyezi Mungu.

Na Swaumu inatakasa nafsi na kuifanya imche Mwenyezi Mungu, na Swaumu pia inamfanya mtu mmoja mmoja au jamii wahisi kuwa Mwenyezi Mungu anawaona katika raha na dhiki, na katika siri na dhahiri, kiasi kwamba jamii inaishi mwezi mzima ikiwa ni yenye kuhifadhi ibada hii na ikiwa ni yenye kufatiliwa na Mola wake, sababu ya yote hayo ni mja kumuogopa Mola wake na kumuamini Yeye na siku ya Mwisho, na kuwa na yakini ya kwamba Mwenyezi Mungu anajua mambo ya siri na yaliyo fichikanana kwamba ipo siku mja atasimamishwa mbele ya Mola wake na kuulizwa juu ya matendo yake yote madogo na makubwa ([231])

Nguzo Ya Tano Ni Kuhiji* : Nako ni kwenda kuhiji katika Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, katika Mji mtukufu wa Makkah, na ni wajibu kwa Muislamu aliyebaleghe na mwenye akili na mwenye uwezo anaemiliki ghalama za usafiri wa kumfikisha Makkah katika nyumba tukufu ya Allah,Na anamiliki ghalama za matumizi ya kutosha kwenda na kurudi, na matumizi hayo yawe ni baada ya kukamilika matumizi katika familia yake, na iwe kuna amani katika safari ya kwenda Makkah, na familia yake ibaki katika amani kwa muda ambao hatokuwepo, na ni wajibu kuhiji mara moja katika umri wa mtu kwa mwenye kuweza.

Na inampasa mwenye kutaka kuhiji atubie kwa Mwenyezi Mungu ili nafsi yake itoharike kutokana na uchafu wa madhambi, na atakapofika katika Mji wa Makkah na katika sehemu takatifu atatekeleza Ibada ya Hija kwa udhalili na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ajue ya kwamba Al Kaabah na sehemu nyenginezo zilizo tukufu haziabudiwi kinyume na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na laiti kama Mwenyezi Mungu asingeamrisha watu kwenda kuhiji huko isingeswihi kwa Muislamu kwenda kuhiji huko.

Na Ibada ya Hija mwenye kuhiji anavaa kikoi cheupe na shuka jeupe, Waislamu wote wanakusanyika sehemu moja na wanavaa nguo aina moja, na wanamuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, hakuna tofauti kati ya Raisi na Raia wala tajiri na masikini, wala mweusi na mweupe, wote ni viumbe wa Mwenyezi Mungu na waja wake, hakuna ubora kwa Muislamu juu ya Muislamu mwenzie isipokuwa kwa ucha Mungu na matendo mema.

Waislamu wanajuana na kusaidiana, na wanakumbuka siku ambayo Mwenyezi Mungu atawafufua wote, na atawaweka sehemu moja kwa ajili ya kuhesabiwa, wanajiandaa kumtii Mwenyezi Mungu kutokana na yale yakayokuwa baada ya kufa.([232])

 Ibada Katika Uislamu*

Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu katika dhamira na uhalisia, Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji na wewe ni kiumbe, wewe ni mtumwa na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuabudiwa, ikiwa ni hivo basi ni lazima katika maisha haya kila mtu apite katika njia ya Mwenyezi Munguiliyo nyooka akiwa ni mwenye kufuata sheria yake na athari za Mitume wake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka kwa waja wake sheria tukufu kama vile kuwepo kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote (Tauhidi) na Swala, Zaka, Funga na Hija.

Lakini kufanya Ibada hizo haina maana kwamba umemaliza Ibada zote katika Uislamu, kwasababu Ibada katika Uislamu ni mkusanyiko wa vitu vingi, na maana yake: "Ni kila kitu anacho kipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu na akakiridhia, katika matendo na kauli za wazi na za siri". Kila kitendo ulicho kifanya au kauli uliyoiongea katika yale anayopenda Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuyaridhia basi hiyo ni Ibada, bali kila jambo jema la kawaida ulilofanya kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu nayo pia ni Ibada, na kuishi kwako vizuri na Baba yako na familia yako na mke wako na watoto wako na majirani zako ikiwa utakusudia kupata radhi za Mwenyezi Mungu hiyo pia ni Ibada, na muamala wako mzuri nyumbani, sokoni na ofisini ukikusudia kupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu ni Ibada, na ukitekeleza amana na ukawa mkweli na ukazuia maudhi pamoja na kumsaidia dhaifu na kuchuma chumo la halali na kumuhudumia mke na watoto na kumliwazamasikini na kumtembelea mgonjwa na kumlisha mwenye njaa na kumnusuru aliyedhulumiwa, yote hayo ni Ibada utakapo kusudia kupata malipo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi kazi yoyote utakayoifanya kwa ajili ya nafsi yako au familia yako au kwa ajili ya jamii yako au nchi yako, ukikusudia kupata malipo kwa Mwenyezi Mungu hiyo ni Ibada, bali hata kupata starehe ya nafsi katika mipaka ya yale aliyo kuhalalishia Mwenyezi Mungu Mtukufu; itakuwa ni Ibada ikiwa ni kwa nia njema, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Na katika tupu ya mmoja wenu kuna sadaka), wakamuuliza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Kwa kukidhi mmoja wetu matamanio yake anapata thawabu?  Mtume akajibu akasema: (Mnaonaje kama atakidhi matamanio yake katika haramu atapata dhambi?  Vilevile akikidhi matamanio yake katika halali atakuwa na malipo).([233])

Alisema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake: Na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Ni juu ya Muislamu kutoa Sadaka), akaulizwa: Je! Ikiwa hakupata?  Akasema: (Atafanya kazi kwa mkono wake ili ajinufaishe na atoe Sadaka), akauliza tena: Je! Ikiwa hawezi kufanya kazi?  Mtume akasema: (Atamsaidia mwenye shida asiye weza kujisaidia), akaulizwa tena: Je! Ikiwa hakuweza?  Mtume akasema: (Awaamrishe watu kufanya wema), akaulizwa tena: Je! Ikiwa hakuweza?  Mtume akasema: (Ajizuie na shari kwasababu kufanya hivo ni Sadaka).([234])

 Daraja La Pili*

Ni Imani Na Nguzo Zake Sita: Nazo Ni Kumuamini Mwenyezi Mungu Na Malaika Wake Na Vitabu Vyake Na Mitume Wake Na Kuamini Siku Ya Mwisho Na Kuamini Qadari.

Nguzo Ya Kwanza:

Ni kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na vitendo vyake, ya kwamba Yeye ndiye Mola Muumbaji mwenye Ufalme mwenye kupangilia mambo yote, na kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na vitendo wa waja, ya kwamba Yeye ni Mola wa kwelina kila kinacho abudiwa kinyume na Yeye ni batili, na kuamini Majina yake na Sifa zake, ya kwamba Yeye ana Majina mazuri na Sifa za juu zilizo kamilika,

na kuamini upweke wa Mwenyezi Mungu katika hilo, ya kwamba Yeye hana mshirika katika Uungu wake wala katika Ibada zake wala katika Majina yake na Sifa zake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na udumu katika ibada yake. Je, mnamjua mwenye jina kama lake?}.([235])

Na kuamini ya kwamba Yeye hapatwi na usingizi wala kulala, na Yeye ndiye mwenye kujua mambo ya ghaibu na yaliyo wazi, na Yeye ndiye Mfalme wa mbingu na ardhi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha.([236])

Na kuamini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu yuko ya A'rshi yake iliyo juu ya viumbe wake, na Yeye Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa juu lakini yuko pamoja na waja wake, anajua hali zao na anasikia kauli zao, na anawaona mahala walipo na anapangilia mambo yao, na anamruzuku fukara na anamsaidia mwenye shida, humpa Ufalme amtakae na anamvua Ufalme amtakae na Yeye ni muweza wa kila kitu.([237])

Miongoni Mwa Matunda Ya Kumuamini Mwenyezi Mungu Ni Kama Yafuatayo:

1-Inamfanya mja ampende na Mwenyezi Mungu na amtukuze, mambo hayo mawili yanamfanya mtu atekeleze amri ya Mwenyezi Mungu na ajiepushe na makatazo yake, na mja anapofayanya hayo anapata mafanikio yaliyo kamilika duniani na Akhera.

2-Kumuamini Mwenyezi Mungu ni jambo linalo zalisha katika nafsi utukufu, kwasababu mwanadamu atajua ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye Ufalme wa kweli kwa kila kilichopo duniani, na kwamba hakuna mwenye kuleta manufaa wala madhara isipokuwa Yeye, na elimu hii itamtosha kumjua asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na hatamuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi, na hatamtegemea yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu.

3-Kumuamini Mwenyezi Mungu kunaleta unyenyekevu katika nafsi, kwasababu mwanadamu anajua ya kwamba neeme yoyote aliyonayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwahiyo shetani hawezi kumdanganya wala hawezi kuipinga haki wala kuwa na kiburi, wala hawezi kufurahia nguvu yake na mali yake.

4-Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu anafahamu kwa yakini ya kwamba hakuna njia ya kufanikiwa isipokuwa kwa kufanya matendo mema anayo yaridhia Mwenyezi Mungu, wakati ambao wenzake wanaamini itikadi iliyo batili kama kuamini kwamba Yesu ni mtoto wa Mungu na anasamehe madhambi yake, au anaamini kuwa wapo miungu wengine na wanamtimizia anayo yataka, hali ya kuwa miungu hao hawanufaishi wala hawadhuru, au watu wengine wanakuwa hawana dini hawaamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na matumaini yote hayo watajua uhakika wake na kujua kwamba walikua katika upotevu ulio wazi watakapofika kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Qiyama.

5-Kumuamini Mwenyezi Mungu kunampa mwanadamu nguvu kubwa na maamuzi na kusonga mbele na kusubiri na kuthibiti na kutegemea, pindi anapo simamia mambo makubwa katika dunia kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu,na anakuwa na yakini iliyotimia kuwa anamtegemea Mfalme wa mbingu na ardhi, na kwamba Mwenyezi Mungu anampa nguvu na kumuelekeza, basi anakuwa ni mwenye kuthibiti kama inavyo thibiti milima kwa subira yake na kuthibiti na kutegemea kwake.([238])

Nguzo Ya Pili Ni Kuamini Malaika: Ya kwamba Mwenyezi Mungu aliwaumba ili wamtii, na Mwenyezi Mungu aliwasifu ya kuwa{Na wanasema: Arrahman, Mwingi wa Rehema, ana mwana! Subhanahu, Ametakasika na hayo! Bali hao (wanao waita wana) ni watumwa walio tukuzwa. Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake. Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamwombei yeyote ila yule anaye mridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea}.([239]) Na kwamba wao: {Na ni vyake Yeye tu Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Na walioko kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki. Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei}.([240]) Mwenyezi Mungu aliwawekea hijabu hatuwaoni, Mwenyezi Mungu anaweza akawaondolea hijabu wakaonekana na baadhi ya Mitume wake na Manabii.

Na Malaika wana kazi na majukumu waliyopewa, miongoni mwao ni Jibril aliyewakilishwa kwa ajili kufikisha Ufunuo, anateremsha Ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa yule anaemtaka miongoni mwa waja wake katika Mitume,na kuna Malaika aliye wakilishwa kwa ajili ya kuchukua roho, na Malaika walio wakilishwa kwa ajili na ya watoto walio tumboni mwa mama zao, na kuna walio wakilishwa kwa ajili ya kuwahifadhi wanadamu, na walio wakilishwa kwa ajili ya kuandika matendo ya wanadamu, na kila mtu ana Malaika wawili: {Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni. Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari}.([241])

 Miongoni mwa Matunda Ya Kuamini Malaika:

1-Ni kusafika kwa imani ya Muislamu kutokana na uchafu wa shirki, kwasababu Muislamu anapo amini kuwepo kwa Malaika waliopewa majukumu hayo makubwa na Mwenyezi Munguataondokana na itikadi ya kuamini kuwa kuna viumbe wasiojulikana wanaosaidia katika kuendesha ulimwengu huu.

2-Ni Muislamu kujua ya kwamba Malaika hawanufaishi wala hawadhuru, bali wao ni viumbe walio tukuzwa hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa yale aliyo waamrisha na wanatekeleza yale waliyo amrishwa, basi mwanadamu asiwaabudu Malaika wala kuwaelekea wala asiwaelekee kwa maombi.

Nguzo Ya Tatu Ni kuamini Vitabu: Ya kwamba Mwenyezi Mungu aliteremsha Vitabu juu ya Mitume wake Manabii kwa lengo la kubainisha ukweli wake na kulingania katika njia yake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu}.([242]) Na Vitabu hivi ni vingi miongoni mwa Vitabu hivyo: Ni Kurasa za Nabii Ibrahim na Taurati aliyopewa Nabii Mussa na Zaburi aliyopewa Nabii Daud na Injili aliyopewa Nabii Issa amani ziwe juu yao.

Na Vitabu hivi ambavyo Mwenyezi Mungu ametuelezea vilitoweka, Kurasa za Nabii Ibrahim hazipo tena duniani, ama Taurati, Injili na Zaburi pamoja na kwamba majina yake yapo kwa Mayahudi na Manaswara lakini Vitabu hivyo vilipotoshwa na kubadilishwa, na maandiko mengi yakakosekana yakaingizwa yasiyo kuwemobali yalinasibishwa kwa wasiokuwa wenyewe, Agano la kale ndani yake kuna zaidi ya vitabu arobaini, na vinavyo nasibishwa kwa Nabii Mussa ni vitabu vitano tu, na Injili zilizopo kwa sasa hakuna hata moja inayo nasibishwa kwa Nabii Issa.

Basi kuamini Vitabu hivyo vilivyo tangulia ni kuamini ya kwamba Mwenyezi Mungu aliviteremsha juu ya Mitume wake, na vimekusanya sheria ambayo Mwenyezi Mungu alitaka kuifikisha kwa waja wake katika zama hizo.

Ama Kitabu cha mwisho kilicho teremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni Qur'an tukufu ambayo imeteremshwa kwa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, na itaendelea kuhifadhiwa na Mwenyezi Mungu na haijageuzwa wala kubadilishwa katika herufi zake au maneno yake au haraka zake au maana yake.

Na tofauti kati ya Qur'an tukufu na Vitabu vilivyo tangulia ipo sehemu nyingi miongioni mwa hizo:

1-Ni kwamba Vitabu vilivyo tangulia kwanza vilipotea na kisha vikaingiliwa na upotoshwaji na kubadilishwa, na vikanasibishwa kwa wasiokuwa wenyewe, na zikaongezwa ndani yake sherehe, maelezo na tafsiri, vikakusanya mambo yanayo kanusha Ufunuo wa MwenyeziMungu na akili na maumbile.

Ama Qur'an tukufu bado itaendelea kuhifadhiwa na Mwenyezi Mungu kwa herufi zilezile na maneno aliyo yashusha Mwenyezi Mungu kwa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, haijapatwa na upotoshwaji wala kuzidishwa, kwasababu Waislamu walifanya buidii ili Qur'an ibaki ikiwa imetakasika kutokana na kila aina ya uchafu, hawakuichanganya na chochote kutokana na historia ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake au historia ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao au tafsiriya Qur'an tukufu au hukumu za Ibadan a miamala mbalimbali.

2-Ni kwamba Vitabu vilivyo tangulia havina upokezi wa kihistoria katika zama zetu za sasa, bali baadhi ya Vitabu hivyo havijulikani vilishuka kwa nani na viliandikwa kwa lugha gani, na sehemu ya Vitabu hivyo ilinasibishwa kwa watu ambao sio walio shushiwaVitabu.

Ama Qur'an tukufu Waislamu waliipokea kutoka kwa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake upokezi sahihi na usiokuwa na shaka ndani yake kwa mdomo na kwa kuandika, na Waislamu katika kila zama wana maelfu ya watu walio kihifadhi Kitabu hicho na maelfu ya kopi ya Kitabu hicho, na kopi yoyote ya mdomo isiyo kubaliana na kopi iliyo andikwa basi haikubaliki, ni lazima ziende sawa kati ya kopi iliyo hifadhiwa kifuani na kopi iliyo andikwa.

Na juu ya hayo hakika Qur'an tukufu ilipokelewa kwa mdomo hakikupata nafasi hiyo Kitabu chochote duniani, bali haikupatikana picha ya upokezi wa sampuli hiyo isipokuwa katika Umma wa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, na njia ya upokezi huo: Mwanafunzi anahifadhi Qur'an kwa Shekh wake kuhifadhi kwa moyo, na Shekh wake anakuwa ameihifadhi kwa Shekh wake, kisha Shekh anampa anampa mwanafunzi wake Shahada (Ijaaza), Shekh anatoa ushuhuda katika Shahada hiyo ya kwamba amemsomesha mwanafunzi wake yale aliyo yasoma kwa Mashekh zake, anataja ndani yake Shekh baada Shekh, kila mmoja kwa jina lake mpaka upokezi unafika kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, na hivohivo unaendelea upokezi wa mdomo kutoka kwa mwanafunzi mpaka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake.

Na zimekuja dalili nyingi na zenye nguvu na ushahidi wa kihistoria wenye upokezi ulioungana unaothibitisha kujulikana kila Sura na Aya katika Qur'an tukufu mahala zilipo teremkia kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake na muda wake.

3-Ni kwamba lugha zote zilizo teremshiwa Vitabu vilivyo tangulia zimesha toweka zamani sana, hakuna yeyote anayezungumza kwa lugha hizo na ni wachache wanao zifahamu katika zama za sasa. Ama lugha ya Qur'an ni lugha iliyo hai inayo zungumzwa na mamilioni ya watu na isomeshwa na kufundishwa katika kona zote za dunia, na ambaye hakujifunza kiarabu atapata mtu wa kufundisha maana ya Qur'an tukufu.

4-Ni kwamba Vitabu vya zamani vilikuwepo kwa muda maalum na vilielekezwa kwa watu maalum, na kwa ajili hiyo vilikusanya hukumu maalum kwa Umma huo na watu wa zama hizo, na Vitabu sampuli hiyo haviwezi kuwa ni vya watu wote.

Ama Qur'an tukufu ni Kitabu kilicho kusanya zama zote, kinacho nasibiana na kila sehemu, kilicho kusanya hukumu, miamala na tabia zinazofaa kwa kila Umma na kuafikiana na kila zama, maelezo yaliyomo ndani yake yanaelekezwa kwa watu wote.

Na kupitia hayo inabainika kwamba Mwenyezi Mungu hamuhukumu wanadamu kupitia Vitabu ambavyo kopi yake ya asili haipo, wala hapatikani juu ya mgongo wa ardhi mtu anaezungumza lugha ya Vitabu hivyo vilivyo tangulia baada ya kupotoshwa,bali Mwenyezi Mungu anawahukumu waja wake kupitia Kitabu kilicho hifadhiwa na kilicho salimika kutokana na ziada, mapungufu na kugeuzwa, kopi yake imeenea kila sehemu na imeandikwa katika lugha iliyo hai na wanaisoma mamilioni ya watuna kufikisha Ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa wengine, na Kitabu hicho ni "Qur'an tukufu" ambayo Mwenyezi Mungu aliiteremsha juu ya Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, na Qur'ani ndiyo kiongozi wa Vitabu hivyo vilivyo tangulia, na ndiyo yenye kusadikisha na kuvitolea ushahidi,na ni Kitabu ambacho watu wote ni wajibu kukifuata, ili kiwe ni nuru, ponyo, uongofu na rehma, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni na mcheni Mungu, ili awarehemu).([243]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zimetukuka: {Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote}.([244])

 Nguzo Ya Nne Ni Kuamini Mitume Rehma Za Mwenyezi Ziwe Juu Yao:

Hakika Mwenyezi Mungu alituma Mitume kwa waja wake ili wawabashirie watu neema mbalimbali pindi watakapo muamini Mwenyezi Mungu na wakasadikisha Mitume, na ili wawaonye kutokana na adhabu ikiwa watamuasi Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu{Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani}.([245]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zake zimetukuka: {Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume}.([246])

Na Mitume hao ni wengi wa kwanza wao ni Nuhu na wa mwisho wao ni Muhammad rehma na amani ziwe juu yao, miongoni mwao kuna ambao alitueleza Mwenyezi Mungu kama vile Ibrahim, Mussa, Issa, Daud, Yahya, Zakariya na Swaleh…, na miongoni mwao Mwenyezi Mungu hakutaja habari zao, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mitume tulio kwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia}.([247])

Mitume wote hao ni viumbe walioumbwa na Mwenyezi Mungu hawana chochote katika sifa za vitendo vya Mwenyezi Mungu (kama vile kutoa rizki na kuhuisha nk.), wala sifa za kuabudiwa, hafanyiwi chochote katika Ibada,hawadhuru wala kunufaisha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimzungumzia Nabii Nuhu ambae ni Mtume wa mwanzo alisema kuwambia watu wake: {Wala sikwambieni kuwa nina khazina za Mwenyezi Mungu; wala kuwa mimi najua mambo ya ghaibu; wala sisemi: Mimi ni Malaika}.([248]) Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuamrisha Mtume wa mwisho aseme: {Sema: Mimi sikwambieni kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambieni kuwa mimi ni Malaika}.([249])  Na aseme: {Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, ila apendavyo Mwenyezi Mungu}.([250])

Na Mitume ni waja waliokirimiwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewachagua na akawatukuza kwa kuwapa Utume na akawasifu kuwa ni waja, Dini yao ni Uislamu, na Mwenyezi Mungu hakubali dini isiyokuwa Uislamu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika dini inayo kubaliwa kwa Mwenyezi Mungu ni Uislam}([251])Ujumbe wao uliafikiana katika misingi, na sheria zao zikawa tofauti, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake}.([252]) Na mwisho wa sheria hizo ni sheria aliyopewa Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, nayo ni yenye kufuta sheria zote zilizo tangulia, na Ujumbe wake ndio Ujumbe wa mwisho, na yeye ndiye Mtume wa mwisho.

Mwenye kumuamini Mtume ni lazima aamini Mitume wote, na mwenye kumkadhibisha Mtume basi amekadhibisha Mitume wote, kwasababu Mitume wote wanalingania juu ya kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya mwisho, na kwasababu Dini yao ni moja, yeyote mwenye kuwabagua au akaamini baadhi na akakufuru wengine basi atakuwa amewakufuru wote, kwasababu kila mmoja wao anawalingania watu kuwaamini Manabii wote na Mitume wote.([253]). Alisema Allah Mtukufu: {Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako}.([254]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zake zimetukuka: {Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya}.([255])

 Nguzo Ya Tano Ni Kuamini Siku Ya Mwisho:

Kwasababu mwisho wa kila mwanadamu duniani ni kufa, je! Ni yepi mafikio ya mwanadamu baada ya kufa?  Na ni yepi mafiko ya madhalimu waliosalimika duniani kutokana na adhabu?  Je! Watasalimika kutokana na dhulma zao? Na wale waliofanya wema na hawakupata malipo ya mema yao duniani je! Malipo yao yatapotea?

Hakika viumbe wanafatuatana katika kufa kizazi baada ya kizazi, mpaka Mwenyezi Mungu atakapo toa idhini dunia imalizike na viumbe wote wakamalizika juu ya mgongo wa ardhi, baada ya hapo Mwenyezi Mungu atawafufua viumbe wote katika siku yenye kushuhudiwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu atawakusanya siku hiyo wa mwanzo na wa mwisho, kisha atawahesabia waja juu ya matendo yao ya kheri au ya shari waliyo yachuma duniani, Waumini wataingizwa Peponi na makafiri wataingizwa Motoni,

na maana ya Pepo ni neema alizo ziandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa vipenzi vyake Waumini, ndani yake kuna aina mbalimbali za neema ambazo hakuna anaeweza kuzisifia, ndani yake kuna daraja mia moja na kila daraja kuna wanaoishi ndani yake kadri ya imani yao na matendo yao, na daraja la chini kabisa Peponi ni yule atakae pewa neema zinazo fanana na Ufalme wa Wafalme wa duniani, kisha neema hizo zitazidishwa mara kumi,

na Moto ni adhabu ambayo Mwenyezi Mungu kaiandaa kwa mwenye kumkufuru, ndani yake kuna aina tofauti za adhabu ambazo zinaogopesha kuzitaja, na laiti kama Mwenyezi Mungu angetoa idhini ya watu kufa siku ya Qiyama basi watu wa Motoni wangekufa baada ya kuuona Moto,

na Mwenyezi Mungu amejua kutokana na elimu yake iliyo tangulia yale atakayo yasema au kuyafanya kila mwanadamu kutokana na kheri au shari ya siri na ya dhahiri, kisha Mwenyezi Mungu akamuwekea kila mwanadamu Malaika wawili, mmoja anaandika mema na mwingine anaandika maovu, na hakuna kinacho wapiti, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari}.([256]) Na Malaika wanaandika matendo hayo katika Kitabu atakacho pewa mwanadamu siku ya Qiyama, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyo ogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika?  Na watayakuta yote waliyo yatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote}.([257]) Atasoma Kitabu chake na hatakanusha chochote ndani yake, na yeyote mwenye kukanusha chochote katika matendo yake Mwenyezi Mungu atavifanya viungo vyake vitaje matendo yake yote, masikio yake yatatamka na macho yake na mikono yake na miguu yake na ngozi yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukuf{Hata watakapo ufikia Moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa waliyo kuwa wakiyatenda. Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia?  Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliye kuumbeni mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa. Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika mliyo kuwa mkiyatenda}.([258])

Na kuamini siku ya mwisho ni kuamini siku ya Qiyama ambayo ni siku ya kufufuliwa, imani hiyo imefundishwa na Mitume na Manabii wote amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapo iteremshia maji mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka aliye ihuisha ardhi ndiye atakaye huisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu}.([259]) Mwenyezi Mungu utakasifu niwake na ametukuka {Je! Hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliye ziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu?  Kwani?  Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu}.([260]) Na hiyo ndiyo hekima ya Mwenyezi Mungu, kwasababu Mwenyezi Mungu hakuumba viumbe wake kwa mchezo, na hakuwaacha bure, kwasababu mtu mwenye udhaifu wa akili hawezi kufanya kazi yoyote bila kuwa na malengo na makusudio, kwanini mwanadamu halifikirii hilo kwa kiumbe mwenzie anaefanya kazi kwa malengo, kisha anadhani kwamba Mwenyezi Mungu kaumba waja wake kwa mchezo na kawaacha bure, ametakasika Mwenyezi Mungu kutokana na hayo wanayosema, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? }([261])Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zake zimetukuka:{Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake kwa batili. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata}.([262])

Na watu wenye akili wameshuhudia juu ya kumuamini Mwenyezi Mungu, na jambo hilo linakubalika kiakili na maumbile yaliyo salama yanajisalimisha katika jambo hilo, kwasababu mwanadamu anapoamini siku ya Qiyama atajua kwanini mtu anaacha makatazo na anafanyamaamrisho kwa kutarajia yale yaliyopo kwa Mwenyezi Mungu,kisha atajua kwamba mtu mwenye kudhulumu watu atapata fungu lake pia, nalo ni kulipiza kisasi kwa wale alio wadhulumu siku ya Qiyama, na kwamba mwanadamu lazima apate malipo yake ikiwa ni ya kheri atapata kheri, na kama ni ya shari atapata shari, ili kilanafsi ilipwe kutokana na ilicho chuma,na uadilifu wa Mwenyezi Mungu ndipo utakapo kamilika, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!}.([263])

Na hakuna kiumbe yeyote anayejua Qiyama kitakuwa siku gani, siku hiyo haijui Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu wala Malaika aliye karibu na Mwenyezi Mungu, sipokuwa jambo hilo Mwenyezi Mungu kalihusisha na elimu yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini?  Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye}.([264]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Hakika kuijua Saa (ya Kiyama) kuko kwa Mwenyezi Mungu}.([265])

 Nguzo Ya Sita Ni Kuamini Hukumu Ya Mwenyezi Mungu Na Mipangilio Yake (Qadar):

Ni kuamini ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua yale yaliyotokea na yatakayo tokea, na anajua hali za waja wake na matendo yao, na muda wao wa kuishi na rizki zao, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu}.([266]) Na amesema Mwenyezi Mungu sifa zake zimetukuka: {Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha}.([267]) Na yote hayo ameyaandika katika Kitabu kilichopo kwake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha}.([268]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi?  Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi}.([269]) Mwenyezi Mungu Mtukufu anapotaka huliambia kuwa na linakuwa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa}.([270]) Na Mwenyezi Mungu Mtukufu kama alivyo pangilia kila kitu basi Yeye ndiye Muumbaji wa kila kitu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo}.([271]) Na amesema Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu}.([272]) Amewaumba waja kwa ajili ya Ibada, na akawawekea wazi Ibada hiyo na akawaamrisha waitekeleze na akawakataza kufanya maasi na akawabainishia, na akawawekea uwezo na utashi ambavyo vitawawezesha kupata thawabu, na mwenye kufanya maasi atastahiki kupata adhabu.

Mwanadamu pindi anapo amini hukumu ya Mwenyezi Mungu na mipangilio yake (Qadar) anapata yafuatayo:

1-Anakuwa ni mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu wakati wa kufanya jambo lolote, kwasababu anajua ya kwamba sababu na anaesababisha vyote vinakuwa kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na mipangilio yake.

2-Nafsi inapata raha na moyo unatulia, kwasababu pindi anapojua kwamba mambo mazuri hayapatikani isipokuwa kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na mipangilio yake, na kwamba jambo baya lililopangwa na Mwenyezi Mungu litatokea tu hakuna namna, atakapo yajua hayo nafsi yake itatulia na atairidhia hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakuna yeyote mwenye maisha mazuri na mwenye furaha ya nafsi na mwenye utulivu kuliko yule aliyeiamini Qadar.

3-Inaondoa kujikweza pindi mtu anapopata mafanikio, kwasababu kuyapata hayo ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa yale aliyo mpangilia miongoni mwa sababu za kheri na mafanikio, atamshukuru Mwenyezi Mungu juu ya hilo.

4-Inaondoa dhiki na msongo wa mawazo pindi anapokosa mafanikio au akapatwa na jambo baya, kwasababu hayo yaliyo mpata yamempata kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu hukumu ambayo hakuna awezae kuizuia wala kuipinga, basi atasubiri na kutaka thawabu kwa Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. Ili msihuzunike kwa kilicho kupoteeni, wala msijitape kwa alicho kupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye jivuna akajifakhirisha}.([273])

5-Ni kumtegeme Mwenyezi Mungu Mtukufu kikamilifu, kwasababu Muislamu anajua ya kwamba manufaa na madhara vyote viko katika Mikono Mwenyezi Mungu Mtukufu, hawezi mwenye nguvu kwasababu ya nguvu zake, wala hataacha kufanya jambo la kheri kwa kumuogopa kiumbe, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake kumwambia Ibni Abas radhi za Allah ziwe juu yake: (Fahamu ya kwamba Ummah laiti wakijikusanya kwa lengo la kukunufaisha hawawezi kukunufaisha isipokuwa kwa kile alicho kuandikia Mwenyezi Mungu, na laiti wakijikusanya kwa lengo la kukudhuru hawawezi kukudhuru isipokuwa kwa kile alicho kuandika Mwenyezi Mungu.([274])

 Daraja La Tatu Ni Ihsani: Ihsani ina nguzo moja nayo ni:

Kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona na ikiwa humuoni basi Yeye anakuona,basi mwanadamu anamuabudu Mola wake kwa sifa hiyo, nayo ni kuuhudhurisha ukaribu wake na kujiona kuwa yupo mbele ya Mola wake, na kufanya hivo kunaleta unyenyekevu na woga na haiba na kumtukuza Mwenyezi Mungu, na inampelekea mtu kuhamasika katika kutekeleza Ibadan na kufanya juhudi katika kuifanya vizuri na kuitimiza

Mja anamtazama Mola wake katika kutekeleza Ibada na apata hisia za kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kana kwamba anamuona, na ikiwa yeye hamuoni basi aamini ya kwamba Mwenyezi Mungu anamuona na anaviona vitendo vyake vya siri na vya dhahiri, vya ndani na vya nje, na hakuna kinacho fichikana kwake.([275])

Mja aliyefikia cheo hicho humuabudu Mola wake kwa ikhlas, haangalii isipokuwa kwa Mola wake, wala haangalii sifa za watu, na haogopi matusi yao, kwani tegemeo lake ni kumridhisha Mola wake ili Mwenyezi Mungu amsifu.

Ni mwanadamu ambae mambo yake ya siri na ya dhahiri yanalingana, anamuabudu Mola wake kwa uficho na uwazi, anayakini iliyotimia ya kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yaliyofichwa na moyo wake na yale yanayo mtia wasiawasi, moyo wake umeshiba imani, na akahisikuwa Mola wake anamchunga,viungo vyake vikajisalimisha kwa aliyeviumba, havifanyii kazi viungo hivyo isipokuwa kwa yale anayo yapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia.

Katika hali ambayo moyo wake umeambatana na Mola wake mtu huyo haombi msaada kwa kiumbe yeyote kutokana na kutosheka kwake na Mola wake, wala hashitakii mambo yake kwa mwanadamu, kwasababu shida zake zote amezipeleka kwa Mwenyezi Mungu, na Yeye anatosha kuwa msaidizi wake, wala hahisi upweke popote na wala hamuogopi yeyote, kwasababu anajua kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja nae katika hali zote, na Yeye ndiye anaye mtegemea na nineema iliyoje ya mwenye kunusuru, na mtu huyo haachi jambo lolote lililo amrishwa na Mwenyezi Mungu, wala hafanyi maasi, kwasababu anamuonea haya Mwenyezi Mungu, na anachukia kukosekana mahala alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu au kupatikana sehemu aliyo katazwa na Mwenyezi Mungu, hafanyi uadui wala kumdhulumu mja yeyote au kuchukua haki yake, kwasababu anajua ya kuwa MwenyeziMungu anamuona, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atamuhesabu kwa matendo yake, wala hafanyi uharibifu katika ardhi kwasababu anajua kwamba kheri zote zilizomo katika ardhi ni milki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu amezilainisha kwa waja wake, mja anachukua katika kheri hizo kulingana na shida yake, na anamshukuru Mola wake kwa kumfanyia wepesi.

* * *

Hayo niliyo kutajia nikayaweka wazi mbele yako katika kitabu hiki kidogo si jambo jengine isipokuwa ni mambo muhimu, na ni nguzo kubwa katika Uislamu, na nguzo hizo ni zile ambazo mja anapo ziamini na akazifanyia kazi anakuwa Muislamu, na si vinginevyo hakika Uislamu kama nilivyo kueleza unakusanya Dini na dunia na ni Ibada na mfumo sahihi wa maisha, hakika ni mpangilio wa Mwenyezi Mungu uliokusanya vitu vyote na ni wenye kukamilika, umekusanya katika sheria zake kila anacho kihitaji mtu mmoja mmoja na Umma mzima sawa kwa sawa katika pande zote za kimaisha kiitikadi, siasa, uchumi, jamii na amani…na mwanadamu anapata ndani yake kanuni na misingi na hukumu zinazo pangilia maisha katika hali ya usalama na vita na haki za muhimu kwa wanadamu, na hukumu hizo zinahifadhi utukufu wa mwanadamu, ndege, wanyama na mazingira yanayo wazunguka, na hukumu hizozina wabainishia ukweli kuhusu mwanadamu, maisha, kifo na kufufuliwa baada ya kufa, na anapata pia ndani ya hukumu hizo mfumo wa kipekee wa kuamiliana na watu wanao mzunguka, kwa mfano kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na semeni na watu kwa wema}.([276]) Na kauli ya Allah Mtukufu: {Na wasamehevu kwa watu}.([277]) Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu}.([278])

Na inapendeza baada ya kuweka wazi daraja za Dini hii na nguzo zake tutaje kwa ufupi mambo mazuri ya Uislamu.

 Miongoni Mwa Mambo Mazuri Katika Uislamu* :

Miongoni mwa mambo mazuri ya Uislamu kalam haiwei kuandika mazuri yote ya Uislamu na hakuna ibara inayoweza kuelezea ubora wa Dini hii, na yote hayo ni kwa sababu Dini hii ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama ilivyo kwamba macho hayawezi kumuona Mwenyezi Mungu wala mwanadamu hawezi kuwa na elimu ya kujua namna alivyo Mwenyezi Mungu vilevile sheria ya Mwenyezi Mungu haiwezi kusifiwa kwa maandishi. Amesema Ibn Alqayim Allah amrehem: Na amesema Ibnul Qayyim Allah amrehemu: (Na utakapo zingatia hekima kubwa katika Dini hii imara na Dini iliyo takasika, na sheria ya Muhammad ambayo hakuna maneno yanayotosha kuelezea ukamilifu wake, na sifa haziwezi kumaliza uzuri wake, wala akili haziwezi kupendekeza chochote katika sheria hata kama zitajikusanya zikawa katika kichwa cha mtu mmoja, na akili zinakamilika na kupata ubora pindi zinapojua jua uzuri wa sheria na zikashuhudia ubora wake, na kwamba dunia haijawahi kupata sheria tukufu na iliyokamilika kuliko sheria ya Muhammad,na hata kama Mtume asingeleta hoja yoyote ya kuthibiti sheria hiyo ingetosha kuwa ni hoja na alama na ushahidi ya kwamba imetoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na sheria yote inashuhudia ukamilifu wa elimu ya Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa hekima yake na upana wa rehma zake na wema na ihsani, na kujua elimu ya ghaibu ya wazi, na kujua elimu ya mwanzo na ya mwisho, na sheria hiyo ni katika neema za Mwenyezi Mungu kubwa alizo waneemesha waja wake, hakuna neema yoyote kubwa aliyo waneemesha waja wake kama kuwaongoza kunako kuifuata sheria hiyo, na akawajaalia kuwa ni katika watu wa sheria hiyo na ni miongoni mwa walealio wachagua, kwasababu hiyo Mwenyezi Mungu aliwapa neema waja wake na akawaongoza kunako sheria hiyo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini vile alivyo waletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi}.([279]) Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwajulisha waja wake na kuwakumbusha juu ya neema kubwa alizo waneemesha, akiwataka wamshukuru: {Leo nimekukamilishieni Dini yenu}.([280])

Na miongoni mwa kumshukuru Mwenyezi Mungu katika Dini hii ni kutaja baadhi ya mazuri ya Dini hii:

 1-Ni Dini Ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Dini ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameichagua mwenyewe na akawatuma Mitume na akawaruhusu waja wake wamuabudu Yeye kupitia Dini hiyo, kama ilivyo kwamba Mwenyezi Mungu hafananishwi na viumbe wake, vilevile Dini yake ya Uislamu haifananishwi na sheria za wanadamu na dini zao, na kama alivyo sifika Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu vilevile Dini yake imesifika kwa ukamilifu katika kutekeleza sheria zinazofaa katika maisha ya watu,na zilizo kusanya haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu na mambo yanayo walazimu waja kumfanyia Mwenyezi Mungu, na haki za wao kwao na mamba ya wajibu wanayo paswa kufanyiana.

 2-Ni Dini Iliyokusanya Kila Kitu:

Miongoni mwa mambo mazuri ya Dini hii ni kwamba imekusanya kila kitu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote}.([281]) Dini hii imekusanya yote yanayo ambatana na Mwenyezi Mungu miongoni mwa Majina na Sifa na haki mbalimbali, na yote yanayo ambatana na viumbe miongoni mwa sheria, majukumu, tabia na kuamiliana, na Dini hii imekusanya habari za watu wa mwanzo na wa mwisho, na habari za Malaika, Mitume na Manabii, na imeelezea kuhusu mbingu na ardhi na sayari na nyota na milima, miti na ulimwengu, na imetaja sababu za kuumba na malengo yake na mwisho wake, na ikataja Pepo na mafikio ya Waumini, na ikataja Moto na mwisho wa makafiri.

 3-Ni Dini Inayo Muungnisha Mja Na Mola Wake:

Kila Dini batili inaunganisha kati ya mtu na mtu mwingine kwasababu ya kifo au udhaifu au maradhi, na inaweza ikamuunganisha na mtu aliyefariki miaka mingi iliyopita na akawa mifupa na mchanga…Ama Dini hii ya Uislamu inamuunganisha mtu na Muumba wake moja kwa moja, hamna kuhani wala mtakatifu wala sakramenti tukufu (sakramenti ni aina ya ibada inayofanywa na Wakristo ikiwemo kula mkate wa Yesu), bali Dini ya Uislamu ni mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mja na Mola wake, ni mawasiliano yanayo unganisha akili ya mja na Mola wake, mja anapata nuru na uongofu na anakuwa na daraja na anaomba ukamilifu, na anapanda daraja kutokana na kujiepusha kwake na mambo ya kipuuzi pamoja na mambo madogo madogo yasiyo na maana, kila moyo ambao hauja fungamana na Mola wake basi umepotea zaidi kuliko wanyama, nayo ni mawasiliano katika ya mja na Mola wake na kwa kupitia mawasiliano hayo mja anajua yale anayo yataka Allah kwake atamuabudu kwa elimu, na atajua sehemu ya kupata radhi zake na atazitafuta, na atazijua sehemu zinazo muudhi Allah na atajiepusha nazo.

Na Dini hii ya Uislamu ni mawasiliano kati ya mja dhaifu tena masikini na Mwenyezi Mungu Mtukufu, mja anamuomba Mola wake msaada na taufiqi, na anamuomba amuhifadhi kutokana na vitimbi na michezo ya shetani.

 4-Dini Ya Uislamu Inachunga Maslahi Ya Dunia Na Akhera:

Sheria ya Kiislamu imejengwa katika kulinda maslahi ya dunia na Akhera pamoja na kutimiza tabia njema,

ama ubainifu wa maslahi ya Akhera: Sheria hii imebainisha namna ya maslahi hayo, na haikughafilika na chochote bali imeyatafasiri maslahi hayo na kuyaweka wazi ili yajulikane, akaahidi neema zake na akatahadharisha adhabu zake.

Ama ubainifu wa maslahi ya kidunia: Mwenyezi Mungu ameweka sheria katika dunia hii inayo muhifadhi mwanadamu kwa yale yanayo muhifadhia mtu dini yake, nafsi yake, mali yake, heshima yake na akili yake.

Ama ubainifu kuhusu tabia njema: Mwenyezi Mungu ameamrisha tabia njema za ndani na za nje, na amekataza tabia mbaya na mambo ya kipuuzi, miongoni mwa tabia za wazi ni usafi, kujitwaharisha na kujiepusha na uchafu, na kupendelea kujitia manukato na kuwa na muonekano mzuri, na Mwenyezi Mungu ameharamisha mambo machafu kama vile zinaa, kunywa pombe, kula mizoga na damu na nyama ya nguruwe, naameamrisha kula vitu vizuri na kukataza kufanya israafu (kutumia vitu kwa fujo).

Ama usafi wa ndani unarejea kwenye kuacha tabia zilizo katazwa na kujipamba na tabia njema, ama tabia mbaya kama vile kusema uongo, kufanya uovu, kukasirika, kuwa na husda, kuwa na ubakhili, kuto kuiheshimu nafsi, kupenda vyeo, kuipenda dunuia, kuwa na kiburi, kujikweza na kujionyesha. Na miongoni mwa tabia nzuri ni mtu kuwa na tabia njema na kuwa na marafiki wazuri na kuwafanyia wema, na kufanya uadilifu na kunyenyekea na kuwa mkweli na kuwa mkarimu na kutoa sadaka na kutegemea kwa Mwenyezi Mungu na kuwa na ikhlas na kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusubiri na kushukuru.([282])

 5-Uislamu Ni Dini Nyepesi:

Moja ya sifa ambazo Dini hii inasifika nazo ni kwamba katika kila Ibada miongoni mwa Ibada zake kuna wepesi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini}.([283]) Na wepesi wa kwanza: Ni kwamba yeyote anaetaka kuingia katika Dini hii hahitaji mtu wa kumuunganisha, au kukubali (kuungama) madhambi yaliyopita, bali anacho takiwa kufanya ni kujitwaharisha na kujisafisha, na kutoa shahada ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mmoja na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na aitakidi maana yake na kufanyia kazi yanayo mpasa kufanya baada kusilimu.

Kisha katika kila Ibada kuna wepesi ndani yake, kwani mwanadamu anaposafiri au akiugua anaandikiwa malipo ya matendo ambayo alikuwa akiyafanya pindi akiwa mzima au akiwa siyo msafiri, bali kwa hakika maisha ya Muislamu ni mepesi na yenye utulivu tofauti na maisha ya kafiri kwani maisha yake ni ya dhiki na shida, vilevile kifo cha Muumini ni chepesi, roho yake inatoka kama linavyodondoka tone la maji kutoka katika chombo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia:Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda}.([284]) Ama kafiri wakati wa kufa kwake wanamjia Malaika wakali na wenye hasira wanampiga kwa bakora, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake}.([285]) Na alisema Allah Mtukufu: {Na laiti ungeli ona Malaika wanapo wafisha wale walio kufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao, na kuwaambia: Ionjeni adhabu ya Moto}.([286])

 6-Uislamu Ni Dini Ya Uadilifu

Hakika aliyeweka sheria za Kiislamu ni Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, na Yeye ndiye aliyeumba viumbe wote weusi na weupe, wakiume na wa kike, na wote wako sawa mbele ya hukumu yake na uadilifu wake na rehema zake, na ameweka sheria inayo afikiana kwa mwanaume na mwanamke, kwasababu hiyo inashindikana kwa sheria kumpendelea mwanaume kuliko mwanamke, au ikampendelea mwanamke kuliko mwanaume, au kumuhusisha mambo fulani mtu mweupe na kumnyima mtu mweusi, watu wote wapo sawa mbele ya sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu hamna tofauti baina yao isipokuwa kwa ucha Mungu.

 7-Uislamu Unaamrisha Mema Na Kukataza Mabaya:

Sheria hii imekusanya sifa tukufu na iliyotimia, nayo ni kuamrisha mema na kukataza mabaya, ni wajibu kwa kila Muislamu mwanaume na mwanamke aliye baleghe na mwenye akili na mwenye kuweza aamrishe mema na akataze mabaya kadri ya uwezo wake kutokana na hatua zake, nazo ni: Kuamrisha mema na kukataza mabaya kwa mkono wake, ikiwa hakuweza akataze kwa ulimi wake, ikiwa hakuweza achukie moyoni,kwasababu hiyo umma wote unakuwa ni wenye kujichunga wenyewe, kila mtu ni wajibu kwake kuamrisha mema na kukataza mabaya juu ya kila mwenye kupuuzia kufanya mema au mwenye kufanya maovu, sawa awe ni kiongozi au raia afanye hivo kadri ya uwezo wake na kulingana na misingi ya kisheria iliyowekwa kwa jambo hilo.

Jambo hilo kama unavyoona ni wajibu juu ya kila mtu kadri ya uwezo wake, katika wakati ambazo nidhamu nyingi za kisiasa za zama hizi zina jifakharisha ya kwamba zinatoa nafasi kwa vyama vya upinzani vifuatilie mwenendo wa kazi za kiserikali na utekelezajiwa majukumu yaliyo pitishwa na serikali.

Na haya ni baadhi ya mambo mazuri ya Uislamu, lau ningetaka kurefusha basi ingepelekea kufafanua kila kipengele na kila faradhi na kila amri na kila katazo ili kubainisha yaliyomo miongoni mwa hekima kubwa na sheria madhubuti na uzuri wa hali ya juu na ukamilifu, na mwenye kuzingatia sheria za Dini hii atajua kwa yakini ya kwamba sheria hizo zimetoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba ni ukweli usiokuwa na shaka ndani yake na ni uongofu usiokuwa na upotevu ndani yake.

Na ukitaka kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na kuifuata sheria yake na kufuata athari za Mitume wake basi mlango wa toba upo wazi mbele yako, na Mola wako mwingi wa kusamehe na mwenye huruma anakuita ili akusamehe.

 Toba

Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Kila mwanadamu ni mwenye kukosea na mbora wa kukosea ni yule mwenye kutubia) ((303)), na mwanadamu ni mdhaifu katika nafsi yake na ni mdhaifu katika kufanya bidii na katika kuazimia jambo, na hawezi kuvumilia tabu ya dhambi zake na makosa yake, Mwenyezi Mungu akamfanyia wepesi kwa kumuhurumia; akamuwekea sheria ya kutubia, na ukweli wa Toba: Ni kuacha dhambi kwa ubaya wake kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutarajia yale Mwenyezi Mungu aliyo waandalia waja wake, na kujutia mema yaliyompita, na kuazimia kutokurudia dhambi, na kufanya yale yaliyo baki katika matendo mema.([287])

Wala huhitaji kutubia kupitia kwa mtu atakae tangaza mambo yako na kufichua siri zako na atakaetumia udhaifu wako, kwa hakika Toba ni mazungumzo kati yako na Mola wako, unamuomba msamaha na unamuomba akuongoze, basi Mwenyezi Mungu anakubali Toba yako na anakusamehe,

na ndani ya Uislamu hakuna makosa yenye kurithiwa wala hakuna mwenye kusamehe makosa kutoka katika viumbe, bali tunaweza kusema kama alivyosema Muhammad Asad ambae ni Myahudi aliyesilimu kutoka Austria alisema: "Sikuweza kupata sehemu yoyote katika Qur'aniliyotajwa kwamba shida ina mtu maalum wa kuimaliza, katika Uislamu hakuna kosa lolote lililo bora na la kurithiwa analokuwa nalo mtu mpaka mwisho wa maisha yake, kwasababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe}.([288]) Na wala mwanadamu haombwi kutoa sadaka au kuua nafsi yake ili afunguliwe milango ya Toba aweze kuepukana na makosa". ([289]) Bali pia ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine}.([290])

Toba ina athari na matunda makubwa, miongoni mwa hayo:

1-Ni mja kujua upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu na ukarimu wake katika kumsitiri, na kama Mwenyezi Mungu Mtukufu angetaka angemharakisha kufanya madhambi na angeyafanya mbele ya waja wake na asingeishi na waja hao vizuri, bali Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtukuza kwa kumsitiri na akamfunika kwa huruma yake na akampa nguvu na ujanja na rizki na chakula.

2-Ni kujua ukweli wa nafsi yake ya kwamba inaamrisha mabaya, na ama yale yanayoitokea nafsi kutokana na kufanya kosa na dhambi na uzembe ni dalili tosha juu ya udhaifu wa nafsi na kushindwa kwake kusubiri juu ya matamanio na mambo ya haramu, na kwamba nafsi hiyo haiwezi kuacha kumuhitaji Mwenyezi Mungu ili aitakase na kuiongoza hata kwa muda mchache.

3- Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka Toba ili mja ajipatie sababu kubwa ya mafanikio, nayo ni kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu na kumuomba msaada, kama anavyo jipatia aina za dua na unyenyekevu na umasikini na mapenzi na kuogopa na kutarajia kupitia Toba, nafsi inakuwa karibu na Mola wake ukaribu maalum ambao isinge upata kama siyo Toba na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

4-Ni Mwenyezi Mungu kumsamehe madhambi yote yaliyo tangulia, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Waambie wale walio kufuru: Wakikoma watasamehewa yaliyo kwisha pita}.([291])

5-Ni kugezwa makosa ya mwanadamu na kuwa mema, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}.([292])

6-Ni mwanadamu kumsamehe mwenzake pindi anapokosea kama anavyo samehewa na Mwenyezi Mungu pindi anapo mkosea; hakika malipo ni kutokana na jinsi ya kazi, atakapo mfanyia mwenzake jambo zuri anapata mfano wake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwasababu Mwenyezi Mungu anamfanyia wema mja wake kwa kumsamehe kama vile mja alivyokuwa akiwasamehe wenzake pindi wanapo mkosea.

7 -Mwanadamu ajue kwamba nafsi yake ina makosa mengi na aibu, kwasababu hiyo ni wajibu kwake kujizuia na aibu za waja, na ajishughulishe kunako kuitengeneza nafsi yake kuliko kufikiria aibu za watu wengine.([293])

Nina hitimisha kipengele hiki kwa kusimulia habari ya mtu mmoja aliyeenda kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake akamwambia: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu sikuacha dhambi kubwa wala ndogo isipokuwa nimeifanya, Mtume akasema: (Unashahidilia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?) Alimuuliza mara tatu, akajibu: Ndio, Mtume akasema: (yale madhambi uliyofanya unasamehewa kwa kuingia kwako katika Uislamu), na katika riwaya: (Hakika shahada hii inasamehe madhambi yote).([294])

Na katika upokezi mwingine ni kwamba mtu huyo alimjia Mtume rehma na amani ziwe juu yake akamuuliza: Unaonaje kuhusu mtu aliyefanya dhambi zote lakini akawa hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, na yeye katika hali hiyo haachi dhambi dogo wala kubwa je! Mtu huyo ana Toba?  Mtume akajibu: (Je! Umesilimu? ) Akasema ama mimi nina shuhudia ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika na wewe ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mtume akasema: (Ndio unakubaliwa Toba, lakini fanya mema na uache maovu Mwenyezi Mungu Mtukufu atakubadilishia maovu yote na kuwa mema), akauliza: Na makosa yangu na uovu wangu?  Mtume akasema: (Ndio!) Akasema: Mwenyezi Mungu ni mkubwa, hakuacha kutoa takbira mpaka akapotea.([295])

Uislamu unafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, na Toba ya kweli inasamehe madhambi yaliyokuwa kabla yake, kama ilivyo thibiti hadithi kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake.

 Mwisho Wa Mtu Asiye Fuata Uislamu

Kama ilivyo kubainikia katika Kitabu hiki ya kwamba Uislamu ndiyo Dini ya Mwenyezi Mungu na ndiyo Dini ya kweli, ndiyo Dini waliyo kuja nayo Mitume wote na Manabii, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka malipo makubwa duniani na Akhera kwa mwenye kuuamini Uislamu, na akaweka adhabu kwa mwenye kuukufuru Uislamu.

Kwakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Muumbaji ambaye ni Mfalme na mwenye kuuendesha ulimwengu huu, na wewe mwanadamu ni kiumbe katika viumbe vyake, amekuumba na akakulainishia vilivyomo katika dunia, na akakuwekea sheria yake na akakuamrisha kuifuata, ukiamini na kutii yale aliyo kuamrisha na ukajiepusha na makatazo yake utakuwa umefuzu kwa yale aliyo kuahidi katika nyumba ya Akhera kutokana na neemaza kudumu, na utapata mafanikio katika dunia kwa neema mbalimbali alizokupa, na utafanana na watu wenye akili zilizo timia na wenye nafsi zilizo takasika nao ni Manabii na Mitume na watu wema na Malaika walio karibu na Mwenyezi Mungu.

Na kama utakufuru kumuasi Mola wako utapata hasara katika dunia yako na Akhera yako na utajisababishia kupata ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu zake duniani na Akhera, na utafanana na viumbe wachafu na wenye alikili pungufu na wenye nafsi chafu kulikoShetani na madhalimu na mafisadi na matwaghuti, hayo ni maelezo kwa ujumla.

Nitakubainishia mwisho wa ukafiri kwa ufafanuzi zaidi nao:

 1-Ni Kuwa Na Woga Na Kutopata Amani.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaahidi wale walio muamini wakafuata Mitume wake kwamba watakuwa na amani katika maisha yao ya dunia na Akhera, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka}.([296]) Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kutoa amani na ndiye msimamizi wa kila jambo, naye ndiye Mfalme wa vyote vilivyomo ulimwenguni, anapo mpendelea mja wake imani anampa amani na utulivu, na mja anapo kufuru basi Mwenyezi Mungu anamuondolea utulivu na amani, mtu huyo utamuona ni mwenye khofu ya Akhera, na ni mwenye kuikhofia nafsi yake kutokana na maradhi, na anakuwa ni mwenye khofu na mustakibali wake katika dunia, kwasababu hiyo utakutamashirika ya bima ndiyo yanayo simamia nafsi yake na mali zake, kutokana na kukosa kwake amani na kutomtegemea kwake Mwenyezi Mungu.

 2-Ni Kuwa Na Maisha Ya Dhiki:

Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuumba mwanadamu na akamlainishia vitu vyote katika ulimwengu, na akamgawia kila kiumbe fungu lake, rizki yake na umri wake, angalia ndege wa angani anaruka asubuhi kutoka katika kiota chake ili apate rizki yake,anaruka kutoka katika tawi kwenda tawi jingine huku akiimba kwa sauti nzuri, na mwanadamu ni kiumbe miongoni mwa viumbe hivyo ambavyo vimegawiwa rizki zao na muda wao, atakapo muamini Mola wake na akaisimamia sheria yake Mwenyezi Mungu atampa mafanikio nautulivu na atamfanyia wepesi mambo yake hata kama atakuwa na uwezo mdogo wa kimaisha,

na akimkufuru Mola wake na akafanya kiburi katika ibada yake Mwenyezi Mungu atayafanya maisha yake kuwa ni ya dhiki na atamkusanyia matatizo na huzuni hata kama atamiliki nyenzo za kumpa furaha na aina za starehe, kwani huoni wenye kujinyonga ni wengi katika nchi ambazo zime wawekea watu wake mambo ya kuwafurahisha? Kwani huoni israafu kuwa na aina tofauti za vyombo majumbani na safari za kila aina kwa ajili ya kwenda kustarehe? Hakika kinacho pelekea mtu kufanya israafu ni moyo kukosa imani na kuhisi dhiki, na kujaribu kuiondoa dhiki hiyo kwa nyenzo mpya na tofauti, na amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema: {Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu}.([297])

 3-Ni Kuishi Katika Ugomvi Wa Nafsi Yake Na Watu Wanao Mzunguka.

Kwasababu nafsi yake imeumbwa juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu}.([298]) Mwili wake umejisalimisha kwa Mola wake ukafuata nidhamu zake, kafiri akapingana na maumbile yake na anaishi katika maisha ya khiyari yanayo pingana na amri za Mola wake, kwasababu nafsi yake imejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwahiyo khiyari yake inapingana na nafsi yake.

Mtu huyo anagombana na ulimwengu unaomzunguka, kwasababu ulimwengu mzima kuanzia katika sayari kubwa mpaka kwenye mdudu mdogo zaidi vitu vyote vinakwenda kutokana na mpangilio wa aliye viumba na akaviwekea sheria, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu}.([299]) Bali ulimwengu huu unampenda yule mwenye kuafikiana nao katika kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na unamchukia yule mwenye kwenda kinyume nao, na kafiri ndiye mkaidi katika viumbe hivyo kwasababu ameiweka nafsi yake kuwa mpinzani wa Mola wake na anadhihirisha ukaidi wake, kwasababu hiyo mbingu na ardhi na viumbe vingine vimestahiki kumchukia na kuchukia ukafiri wakena ukanushaji wake, amesema Mwenyezi Mungu: {Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana! Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno! Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande. Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana. Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana. Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake}.([300]) Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimzungumzia Firauni na majeshi yake: {Mbingu na ardhi wala hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula}.([301])

 4-Ni Kuishi Katika Hali Ya Ujinga:

Kwani ukafiri ni ujinga, bali ndio ujinga ulio mkubwa kwasababu kafiri hamjui Mola wake, pamoja na kuwa anauona ulimwengu huu aliouumba Mwenyezi Mungu akaufanya vizuri na anaona uumbaji mkubwa uliomo katika nafsi yake, na utukufu wa kuumba kwake, lakini hamjui aliyeumba ulimwengu huu na nani aliyeipangilia nafsi yake, je! Huu siyo ujinga ulio mkubwa? .

 5-Ni Kuishi Akiwa Ni Mwenye Kuidhulumu Nafsi Yake Na Kuwadhulumu Wanao Mzunguka:

Kwasababu ameilainisha nafsi yake kuyafanya ambayo hajaamrishwa ayafanye, na hakumuabudu Mola wake bali ameabudu asiyekuwa Yeye, na dahulma ni kuweka kitu mahala ambapo si pake, na ni dhulma ipi iliyo kubwa kuliko kuielekeza ibada kwa isiye stahiki kuabudiwa?  Na amesema Luqmaani mwenye hakima akibainisha uchafu wa shirki: {Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa}.([302])

Anakuwa amevidhulumu vinavyo mzunguka miongoni mwa watu na viumbe wengine, kwasababu hajui ni nani mwenye haki, itakapo fika siku Qiyama atasimama mbele yake kila aliye mdhulumu miongoni mwa wanadamu au wanyama wakimuomba Mwenyezi Mungu awalipizie kisasi.              

 6-Ni Mwenye Kuisababishia Nafsi Yake Kulaaniwa Na Mwenyezi Mungu Na Kuchukiwa Katika Dunia.

Inakuwa ni sababu ya kuteremkiwa na misiba na yanampata majanga, ikiwa ni adhabu ya haraka, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Wameaminisha wanao fanya vitimbi vya uovu kwamba MwenyeziMungu hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafika adhabu kutoka wasipopajua?  Au hatawashika katika nyendo zao, na wala hawataponyoka?  Au hatawashika kwa kitisho na kuwapunguza kidogo kidogo?  Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu}.([303]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake}.([304]) Na amesema Mwenyezi Mungu: {Au watu wa mijini wameaminisha ya kuwa adhabu yetu haitawafika mchana, nao wanacheza?}.[305] Na hii ndiyo hali ya kila mwenye kupuuzia utajo wa Mwenyezi Mungu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akielezea adhabu za makafiri katika nyumati zilizopita: {Basi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosa yake. Kati yao wapo tulio wapelekea kimbunga cha changarawe; na kati yao wapo walio nyakuliwa na ukelele; na kati yao wapo ambao tulio wadidimiza katika ardhi; na kati yao wapo tulio wazamisha. Wala Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao}.([306]) Na kama unavyoona misiba kwa majirani zako miongoni mwa walioteremshiwa adhabu na Mwenyezi Mungu.

 7-Anaandikiwa Hasara Na Kukosa.

Kwasababu ya dhuluma yake amekosa kitu kikubwa chenye kufurahisha na roho, na kitu hicho ni kumtambua Mwenyezi Mungu Mtukufu na kupata faraja katika kumuomba na kupata utulivu kwake, na amepata hasara katika dunia kwasababu ameishi ndani yake maisha ya dhiki na shida, na amepata hasara ya nafsi yake ambayo alikuwa akikusanyia mali, na hakuilainisha nafsi hiyo ili itekeleze ibada na haikuwa ni yenye mafanikio katika dunia kwasababu iliishi ikiwa ni yenye uovu na ikafa na uovu wake, na itafufuliwa pamoja na waovu siku ya Qiyama, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na watakao kuwa na uzani khafifu, basi hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzipinga Ishara zetu}.([307]) Na wamepata hasara watu wake kwasababu waliishi wakiwa ni makafiri wao wamefanana naye katika uovu na dhiki na mafikio yao ni Motoni, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Hakika walio khasirika ni wale walio jikhasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama}.([308]) Na amesema Allah Mtukufu: {Hakika wapatao khasara ni hao walio khasiri nafsi zao na ahali zao siku ya Kiyama. Ama hakika wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya daima},[309] na siku ya Qiyama watafufuliwa na kuingizwa katika Moto na ni ubaya ulioje wa mafikio hayo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!}.([310])

 8-Anaishi Akiwa Ni Kafiri Na Mwenye Kupinga Neema Za Mwenyezi Mungu.

Hakika Mwenyezi Mungu amemleta mwanadamu duniani baada ya kuwa hakuwepo, na akamkunjulia neema zote lakini mwanadamu huyu anamuabudu na kumpenda na kumshukuru asiyekuwa Mwenyezi Mungu…Ni kukanusha gani kuliko kukubwa kuliko ukanushaji huo? Na ni kukataa gani kubaya zaidi kuliko kukataa huko? .

 9-Anakosa Maisha Ya Kweli:

Hakika mwanadamu anayestahiki kuishi ni yule aliye muamini Mola wake na akajua malengo yake na mafikio yake yakawa wazi na akayakinisha juu ya kufufuliwa kwake na akamjua kila anayestahiki kupata haki yake, hafichi ukweli wala hamuudhi kiumbe yeyote, akaishi maisha ya watu bora na akapata maisha mazuri duniani na Akhera, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda}.([311]) Na kuhusu mafikio yake siku ya Qiyama amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa}.([312])

Ama mwenye kuwa katika dunia hii akaishi maisha yanayo fanana na ya wanyama, akawa hamjui Mola wake wala hajui malengo yake, wala hajui mafikio yake, bali malengo yake ikawa ni kula, kunywa na kulala…kuna tofauti gani kati yake na wanayama?  Bali yeye ni mpotevu zaidi kuliko wanyama, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika}.([313]) Na amesema Mwenyezi Mungu: {Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa?  Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia}.([314])

 10-Ataishi Milele Ndani Ya Adhabu

Kwasababu kafiri anahama kutoka katika adhabu kwenda katika adhabu nyingine, anatoka duniani akiwa amechoshwa na maumivu ya dunia na misiba yake kwenda katika nyumba ya Akhera, na hatua ya mwanzo ya kwenda katika maisha hayo wanamshukia Malaika wa mauti wakitanguliwa na Malaika wa adhabu ili wamuonjeshe adhabu anayostahiki, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na laiti ungeli ona Malaika wanapo wafisha wale walio kufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao, na kuwaambia: Ionjeni adhabu ya Moto}.([315]) Kisha inapotoka roho yake na kupelekwa kaburini anapata adhabu kali zaidi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwaelezea watu wa Firauni: {Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!}.([316]) Kisha itakapo kuwa siku ya Qiyama na viumbe wakafufuliwa na ibada zikaonyeshwa, na kafiri akaona kwamba Mwenyezi Mungu matendo yake yote katika Kitabu kile ambacho Mwenyezi Mungu amekielezea kwa kusema: {Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyo ogopa kwa yale yaliomo humo. Na watasema: Ole wetu! Kitabu hichi kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika}.([317]) Hapo ndipo kafiri atatamani kuwa mchanga, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo}.([318])

Na kulingana na ukali wa adhabu ya siku ya kisimamo, hakika mwanadamu laiti angekuwa anamiliki vilivyomo ardhini vyote angevitoa fidia ili aokoke na adhabu ya siku hiyo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na lau kuwa walio dhulumu wangeli kuwa na vyote viliomo duniani na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikomboa katika adhabu mbaya hiyo Siku ya Kiyama}.([319]) Na amesema Allah Mtukufu: {Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe. Na mkewe, na nduguye. Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu. Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye}.([320])

Na kwasababu Akhera ni nyumba ya malipo na siyo nyumba ya matarajio, ni lazima mwanadamu apate malipo ya ibada zake, ikiwa ni kheri atapata kheri na ikiwa ni shari atapata shari,na shari atakayopata kafiri katika nyumba ya Akhera ni adhabu ya Moto, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewawekea watu wa Motoni aina tofauti za adhabu ili waonje adhabu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha. Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka}.([321]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akielezea vinywaji vyao na mavazi yao: {Basi walio kufuru watakatiwa nguo za moto, na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayo chemka. Kwa maji hayo vitayayushwa viliomo matumboni mwao, na ngozi zao pia. Na kwa ajili yao yatakuwapo marungu ya chuma}.([322])

 Hitimisho

Ewe Mwanadamu

Haukuwepo hapa duniani na haukuwa lolote wala chochote, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?}.([323]) Kisha Mwenyezi Mungu akakuumba kutokana na tone la manii, akakujaalia ukawa unasikia na kuona, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa. Hakika Sisi tumemuumba mwanadamu kutokana na tone la maji ya mwanaume na mwanamke yaliyo changanyika, tumfanyie mtihani, kwahiyo tukamfanya ni mwenye kusikia mwenye kuona}.([324]) Kisha ukakua kwa hatua kutoka katika udhaifu kisha kupata nguvu, na marejeo yako ni kwenye udhaifu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza}.([325]) Kisha mwisho wako usikuwa na shaka ni kifo. Na wewe katika hatua hizo unahama kutoka katika na kwenda kwenye udhaifu, huwezi kujikinga mwenyewe kutokana na madhara, wala huwezi kujiletea manufaa mwenyewe isipokuwa kwa kuomba msaada kupitia neema za Mwenyezi Mungu juu yako ambazo ni hila, nguvu na chakula, na wewe ni masikini mwenye kuhitaji kutokana na maumbile yako, ni vitu vingapi unavyo vihitaji ili vikusaidie kukuweka hai wakati haviko katika uwezo wako?  Mara unavipata na mara vinakuondokea, na ni vitu vingapi vyenye manufaa unapenda uvipate? Unaweza kufanikiwa kuvipata au usifanikiwe, na vitu vingapi vyenye kukudhuru vinakupotezea malengo na juhudi zako na vinakuletea tabu na maafa unataka kuvizuia visikupate mara unafanikiwa na wakati mwingine unashindwaJe! Hukuhisi kuwa wewe ni masikini na ni muhitaji kwa Mwenyezi Mungu?  Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa}.([326])

Unapatwa na virusi dhaifu visivyo onekana kwa macho ya kawaida kisha unapatwa na maradhi huwezi kuyazuia, kisha unaenda kwa mwanadamu dhaifu kwa wewe ili akutibu, mara anafanikiwa kukutibu na wakati mwingine Daktari anashindwa kukutibu, Daktari na mgonjwa wapatwa na mshangao.

Tambua ewe mwanadamu udhaifu wako ni mkubwa, lau nzi akichukua kitu mkononi mwako basi huwezi kukirejesha kutoka kwa nzi huyo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kweli aliposema: {Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawatoumba hata nzi ijapo kuwa watajumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa}.([327]) Ikiwa huwezi kukiokoa kilicho chukuliwa na nzi ni kipi unacho miliki? (Watu wako na nafsi yako viko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na moyo wako upo katikati ya Vidole vya Mwenyezi Mungu anaugeuza atakavyo, maisha yako, kifo chako, mafanikio yako na uovu wako viko Mikononi mwa Mwenyezi Mungu, harakati zako, utulivu na kauli zako vinakuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na utashi wake, havitikisiki isipokuwa kwa idhini yake, na huwezi kufanya jambo isipokuwa kwa utashi wake, akikuwakilisha katika nafsi yako basi atakuwa amekuwakilisha kwenye kushindwa na udhaifu na kuchupa mipaka na kufanya dhambi na kukosea, na akikuwakilisha kwa asiyekuwa Yeye basi atakuwa amekuwakilisha kwa asiyemiliki kwako madhara wala manufaa, kifo wala uhai wala kufufliwa, huwezi kumtegemea hata kwa kupepesa jicho, bali wewe unamuhitaji Mwenyezi Mungu muda wote wa maisha yako kwa siri na dhahiri, anakuteremshia neema, na wewe unamkasirisha kwa kumuasi na kumkufuru pamoja na kumuhitajia zaidi kwa kila kitu, umejifanya kumsahau na marejeo yako ni kwake na utasimamishwa mbele yake) ([328]).

Ewe mwanadamu kulingana na udhaifu wako na kushindwa kwako kujiepusha na adhabu zitakazo tokana na madhambi yako, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu}.([329]) Mwenyezi Mungu alituma Mitume na akateremsha Vitabu na akaweka sheria na akakuwekea mbele yako njia iliyo nyooka, na akaweka ubainifu na hoja zilizo wazi na ushahidi, mpaka akakuwekea katika kila kitu dalili inayo onyesha juu ya upweke wake na Uungu wake katika Uumbaji na katika Ibada, na wewe unaiondoa haki kwa kufanya batili, {Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi}.([330]) Mijadala hiyo imekusahaulisha neema za Mwenyezi Mungu ambazo unaishi nazo mwanzo mpaka mwisho! Kwanza kabisa kumbuka uliumbwa kutokana na tone la manii! Na mwisho wako ni shimoni na utakapo fufuliwa ima utaingia Peponi na Motoni, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii?  Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri! Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?  Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba}.([331]) Amesema Allah Mtukufu: {Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?  Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha. Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga}.([332])

Ewe mwanadamu kwanini unainyima nafsi yako utamu wa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ukimuomba akutajirishe kutokana na umasikini, na akuponye kutokana na maradhi, na akuondoshee matatizo yako, na akusamehe madhambi yako, na akuondolee madhara, na akunusuru ukidhulumiwa, na akuonyeshe njia ukipotea, na akufundishe usiyo yajua, na akupe amani ukipata khofu, na akuhurumie katika hali ya udhaifu, na awakimbize maadui zako, na akuletee rizki zako.([333])

Ewe mwanadamu hakika neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu kamneemesha mwanadamu baada ya neema ya Dini basi ni neema ya akili, ili aweze kupambanua kati ya mambo yenye kumnufaisha na yenye kumdhuru, na ili ajue maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, na ayajue malengo makubwa ambayo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kutomshirikisha na chochote, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakikuguseni madhara mnamyayatikia Yeye. Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi}.([334])

Ewe mwanadamu hakika mwanadamu mwenye akili anapenda mambo ya juu na anachukia mambo yasiyokuwa na faida, na anapenda kumfuata kila mtu aliye mwema na mkarimu miongoni mwa Mitume na watu wema,na nafsi yake inatarajia kukutana nao hata kama hakuwaona, na njia ya kuyafikia hayo ni kutekeleza yale aliyo yatolea mwongozo Mwenyezi Mungu kwa kusema: {Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni}.([335]) Na atakapo tekeleza hayo Mwenyezi Mungu atamkutanisha na Manabii, Mitume, Mashahidi na watu wema, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!}.([336])

Ewe Mwanadamu!Hakika ninakupa mawaidha ukae peke yako na nafsi yako kisha zingatia haki iliyokufikia na dalili zake, na uzingatie hoja zake, ukiona ni kweli basi njoo na uifuate, na usiwe mateka wa mazoea na desturi, na fahamu ya kwamba nafsi yako ni tukufu zaidi kwako kuliko ndugu zako, watu wa rika yako (mnao lingana) na mirathi ya babu zako, na Mwenyezi Mungu amewapa mawaidha makafiri na akawahimiza kuyafuata akasema: {Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali}.([337])

Ewe Mwanadamu! Hakika wewe utakapo silimu hutopata hasara kwa lolote, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ingeli wadhuru nini wao lau wangeli muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakatoa katika aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu?  Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema}.([338]) Amesema Imamu Ibni Kathiir Mwenyezi Mungu amrehemu: (Ni kitu gani kitakacho wadhuru lau wakimuamini Mwenyezi Mungu na wakapita njia ya sawa, na wakamuamini Mwenyezi Mungu wakitarajia ahadi yake siku ya Qiyama kwa mwenye kufanya ibada yake vizuri, na wakatoa katika vile walivyo ruzukiwa na Mwenyezi Mungu katika namna ambazo anazipenda Mwenyezi Mungu na kuziridhia, na Mwenyezi Mungu anajua nia zao njema na mbaya, na anajua anayestahiki kupata taufiq kati yao, anamuafiqisha na kumwelekeza katika uongofu, na anamuhukumia mja kufanya amali njema ambayo atairidhia, na Mwenyezi Mungu anamjua mtu anayestahiki kutelekezwa na kufukuzwa katika rehma zake, na mwenye kufukuzwa katika mlango wake hakika atakuwa amekosa na amepata hasara duniani na Akhera).([339]) Hakika Uislamu wako hautazuia kati yako na chochote unacho taka kukifanya au kukitumia katika yale aliyo kuhalalishia Mwenyezi Mungu, bali Mwenyezi Mungu anakulipa thawabu juu ya kila kazi unayoifanya ikiwa unatafuta thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hata kama yatakuwa ni mambo yanayo itengeneza dunia yako na yanazidisha mali zako au cheo chako au utukufu wako, bali hata kile unacho kula katika vitu vya halali utakapo tosheka nacho na ukaacha haramu kwa kutaka malipo kwa Mwenyezi Mungu utapata thawabu, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Na katika tupu ya mmoja wenu kuna sadaka), wakamuuliza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Kwa kukidhi mmoja wetu matamanio yake anapata thawabu?  Mtume akajibu akasema: (Mnaonaje kama atakidhi matamanio yake katika haramu atapata dhambi?  Vilevile akikidhi matamanio yake katika halali atakuwa na malipo).([340])

Ewe Mwanadamu! Hakika Mitume walikuja na ukweli na wakafikisha makusudio ya Mwenyezi Mungu, na mwanadamu anahitaji kuijua sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili apite katika maisha haya kwa elimu na uangalifu, na ili siku ya Qiyama awe ni miongoni mwa walio faulu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikakanusha basi hakika viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima}.([341]) Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu}.([342])

Ewe Mwanadamu! Ukisilimu hutomnufaisha yeyote isipokuwa nafsi yako, na ukikufuru hutamdhuru yeyote isipokuwa nafsi yako, hakika Mwenyezi Mungu ni tajiri hahitajii kwa waja wake, wala hayamdhuru maasi ya wenye kuasi, na wala hazimnufaishi ibada za wenye kuabudu, Mwenyezi Mungu Mtukufu hafanyiwi maasi isipokuwa atajua, na wala hafanyiwi ibada isipokuwa kwa idhini yake, na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kupitia kwa Mtume wake: (Enyi waja wangu hakika Mimi nimeharamisha dhulma juu ya Nafsi yangu na nikaifanya kuwa ni haramu baina yenu, basi msidhulumiane, enyi waja wangu nyote ni wapotevu isipokuwa yule niliye muongoza, basi niombeni uongofu nami nitakuongozeni, enyi waja wangu nyote ni wenye njaa isipokuwa yule niliye mlisha, basi niombeni chakula nami nitakulisheni, enyi waja wangu nyote mpo uchi isipokuwa yule niliye mvisha, basi niombeni kuvaa nami nitakuvisheni, enyi waja wangu hakika nyinyi mnakosea usiku na mchana na mimi ninasamehe madhambi yote, basi niombeni msamaha nami nitakusameheni, enyi waja wangu hamtafikia kufanya madhara ili mnidhuru wala hamtafanya mambo yenye manufaa ili mninufaishe, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakawa na ucha Mungu wa mtu mmoja hilo lisinge niongezea chochote katika Ufalme wangu, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakafanya uovu wa mtu mmoja hilo lisinge punguza chochote katika Ufalme wangu, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wangejikusanya katika uwanja mmoja wakaniomba nikampa kila mtu alicho kiomba hilo lisinge punguza chochote katika Ufalame wangu isipokuwa ni kama inavyo punguza maji pindi inapo ingizwa baharini, enyi waja wangu si vinginevyo bali hakika matendo yenu yote nina wahifadhieni kisha nitawapa malipo yenu, mwenye kupata kheri amshukuru Mwenyezi Mungu, na mwenye atakaepata kinyume na hayo basi asimlamu yeyote isipokuwa nafsi yake).([343])

Na kila sifa kamilifu zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote na rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wetu Muhamad na watu wake na maswaaba zake wote([1]) Ahzaab: 40) -Hii ni dalili kutoka katika Qur'an Tukufu ambayo Allah aliiteremsha kwa Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake, na katika kitabu changu hiki dalili hizi ni nyingi kutoka katika Qur'an tukufu, nazo zinaanza kwa kusema: Amesema Allah Mtukufu, au amesema ambae zimetukuka sifa zake, na utakuta utambulisho mfupi juu ya Qur'an tukufu katika ukurasa wa 95-100, na 114-117. Katika kitabu hiki.

([2]) Al Haji: 9.

([3]) (Yusuf: 108).

([4]) .(Ahqaaf: 35).

([5]) Al Imran: 1200.

([6]) (Al Imran:19)..

*  Kwa ziada ya hayo rejea kitabu: (Al-Aqiidatu Al Swahiiha wama yudhwaaduha) kimetungwa na Shekh Abdul Aziz Bin Baazi - Allah amrehemu- na (Aqidatu Ahli Sunnati waljamaa) kimetungwa na Shekh Muhammad bin Swaleh Uthaymin.

(Ikhlas: 1-4)

([8](Suratul A'raafu 54)..

([9])  Raad 2،3،7،8.

([10])  Raad16

([11](Fusswilat: 37-39),

([12])  Al Ruum: 22-23

([13])  Al Baqara: 255

([14])  Ghaafir: 3.

([15])  Hashri: 17

([16](Al Tuur: 35-36),

([17]) (Rejea Majmuul Fataawah Ibun Taymiyah, Vol. 1, Uk. 47-73,49),

([18]) (Al Ruum: 30),.

([19]) (Imepokelewa na Imamu Bukhari katika kitabu cha Qadar mlango wa tatu. Na Imamu Muslim katika kitabu cha Qadar hadithi No. 2658).

([20]) (Ameipokea Imamu Ahmad katika Musnadi wake, Vol. 4, Uk. 162, na Imamu Muslimu katika kitabu cha Pepo na sifa zake, hadithi No. 2865).

([21]) (rejea Majmuul Fataawah Ibun Taymiyah, Vol. 14, Uk. 380-383, na Vol. 7, Uk. 75).

([22]) (Al-Ankabuut: 61-63)..

([23]) (Al-Zukhruf: 9).

* Anaetaka ufafanuzi zaidi aangalie Kitaabu Al Tauhiid Utambulisho wa Imaamul Mujaddid Muhammad bin Abdul Wahhaab- Allah amrehemu.

([24]) (Al Zumar: 8).

([25]) (Yunus: 22-23)

([26]) (Luqman: 32).

([27])Tazama Kitabu: Sharhul A'qiidati Al Twahaawiyyah, Uk. 39.

([28]) (Al Muuminun: 91).

([29]) ((Israa: 42).

([30])(Sabaa: 23-24),

(Rejea kitabu: Quratu Ayuuni Al Muwahiidina, cha Shekh Abdul Rahman Hassan, Uk. 100).

([32]) (Al Ambiyaa: 22).

([33]) (Rejea: Fat'hul Qadiir, Vol. 3, Uk. 403).

([34]) (Miftaah Daaru Al Saadah, vol. 1, Uk. 260).

([35]) (Al Ambiyaa:25)..

([36]) (Huud: 2),

([37]) (Al Ambiyaa: 108).

([38]) (Al Zumar: 29).

([39]) (Fusswilat: 9-12).

([40]) (Al Ambiyaa: 30-32).

([41]) Kipande hiki cha maneno kimechukuliwa sehem tofauti katika kitabu "Miftaahu Daru Al Saadah" Vl. 1, Uk. 251. 269.

([42]) (Aljaathiya: 13).

([43]) . {Ibrahim 32-34}.

([44]) (Ruum: 22-25).

([45]) (Al Anqabuut: 64).

([46]) (Al Ruum: 27).

([47]) (Ghaafir: 57).

([48]) (Raad: 2).

([49])(Al Jumaa: 1).

([50]) (Hajji: 18).

([51]) (Al Nnuur 41).

([52]) (Suratul A'araafu 11-25).

([53]) (Al Muuminun: 14).

([54]) (Ibrahim: 32-34). Miftahu Darus Saada, V. 1, Uk. 327-328.

([55]) ((Israa:70)..

([56]) (Al Nisaa: 7).

([57]) (Al Baqara: 228).

([58](Al Tawba: 71).

([59]) (Israa: 23-24).

([60]) (Al Imran: 195)..

([61]) (Al Nahli: 97).

([62]) (Al Nisaa: 124).

([63]) Safarul Jamia, Al Isw'haahu. 7.2, 25/26. Na ijulikane ya kwamba hilo agano la kale walitukuza na kuliamini Mayahudi na Manaswara..

([64]) Rejea Kitabu "Silsilatu Muqaarant Al Adiyaan" Mtunzi: Dr. Ahmad Shalabiy, V. 3, Uk. 210-213.

([65]) (Al Tawba: 71)..

([66]) (Al Baqara: 228)..

([67]) (Israa: 23-24).

([68]) (Dhariyaat: 56).

([69]) Rejea Miftaahu Daru Ssaada, V.1, Uk. 6-11.

([70]) Rejea kitabu: Al Tadmuriyah, cha Shekh Al Islamu Ibni Taymiyah. Uk. 213-214, Miftaahu Daaru Saadah. V. 2, Uk. 383.

([71]) Rejea katika kitabu (Al Deen), kilichotungwa na Muhammad Daraaz, Uk. 87.

([72]) Rejea katika kitabu (Al Deen), kilichotungwa na Muhammad Daraaz, Uk. 88.

([73]) Tazama kitabu (Al Deen), kilichotungwa na Muhammad Daraaz, Uk. 84-98

([74]) Rejea kitabu (Al Fawaaid, Uk. 18-19).

([75]) (Rejea katika kitabu (Al Deen), Uk. 98-102).

([76]) (Al Nisaa: 163).

([77]) (Al Ambiyaa: 25)..

([78]) (Suratul Arafu 73).

([79]) (Al Ambiyaa: 25).

([80]) (Al An'am: 151).

([81]) (Al-Zukhruf: 45)..

([82]) (Al Nisaa: 82).

([83]) (Suratul Arafu 154).

([84]) (Mariyam: 21).

([85]) (Huud: 63).

([86]) (Israa: 82).

([87]) (Maida: 44)..

([88]) (Maida: 46).

([89]) (Al Tawba: 33).

([90]) (Twaha: 1-2).

([91]) (Al Ruum: 30).

([92]) (Al Ruum: 30).

([93]) (Twaha: 1-2)..

([94]) (Al Nisaa: 29)..

([95]) (Al Hujurat: 13)..

([96]) (Al Haji: 9).

([97])Tazama Ukurasa wa 95-100, na 114-117, katika kitabu hiki.

([98]) (Al A'alaa: 1-3).

([99]) (Twaha: 50).

([100]) (Al Shuaraa: 78). Rejea Kitabu "Al Jawaabu Swahiihi Fiy Man Baddala Diinal Masiihi" V.4, Uk.97.

([101]) (Angalia: Majmuu Al Fataawah cha Shekhul Islamu Ibn Taymiyah, V. 4, uk. 210-211).

* Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu Uyahudi rejea Kitabu "Ifhaamul Yahuudi" kilicho tungwa na Prince Al Bin Yahya kutoka Morocco, alikuwa Myahudi kisha akasilimu.

([102]) (Jewish Encyclpaedia Vol.7, Uk. 7/ V.7, Uk. 568-569).

*        Mwenye kutaka ufafanuzi zaidi arejee kitabu: "Al Jwaabu Al Swahiihu Liman Baddala Diinal Masiihi" kilicho tungwa na Sheykhul Islaam bin Taymiyah Allah amrehemu, na kitabu: "Idh'haarul Haqq" kilicho tungwa na Rahmat LLah bin Khaliili Al Hindy, na kitabu: "Tuhfatul Ariibi Fiy Raddi Alaa Ubbaadi Al Swaliib" kilicho tungwa na Abdallah Al Tarjumaan, alikuwa mkristo kisha akasilimu.

([103]) (Neno Talmud maana yake ni kitabu kinacho zungumzia dini ya kiyahudi na adabu zake, nacho ni mkusanyiko wa ufafanuzi wa kitabu cha sheria kwa wanachuoni wa kiyahudi katika zama tofauti).

(Rejea kitabu: (Uyahudi kulingana na kitabu cha Talmud) kimeandikwa na Dr. Rohlang kimetafsiriwa kwa lugha ya kiarabu kutoka katika lugha ya kifaransa. Pia kitabu "Hazina iliyo patikana katika kitabu cha Tarmud" Dr. Yusuf Hanaa Nasru LLah).

([105]) (Rejea: Muhtasari wa yalio kuja katika maarifa ya Ukatoliki mpya. Makala ya Utatu mtakatifu Vl. 14 Uk. 295).

(Rejea kitabu: Jamecs Houstoin Baxter In the History of Christionity in the Light of Modern Knowledge. Glasgow, Uk. 407, kilichoandikwa mwaka: 1929).

([107]) (Rejea kitabu: (Iraan Fi Ahdi Saasaniyiina) cha "Prof. Arthur Christensen" Ni Muhadhiri katika Chuo Kikuu cha Copenhagen, Denmark, amesomea historia ya Iran. Na kitabu: "Taariikhu I'raan" kilicho tungwa na Shahin Makarios Mmajusi.

([108]) (Rejea kitabu: (Iraan Fi Ahdi Saasaniyiina). Uk. 155).

(Rejea kitabu: (Iraan Fi Ahdi Saasaniyiina), Uk. 183-233).

([110]) (Rejea kitabu: (Al Hindu Al Qadima), kilichotungwa na Aishuraa Tuuba, Muhadhiri wa history katika Chuo Kikuu cha Haidary Abadi, India. Na kitabu: (The Discovery of India), Uk. 201-202, kilichotungwa na Jawaahir Lali Nahroo, Waziri Mkuu wa zamani wa India).

([111]) (Rejea kitabu: (Al Hindu Al Qadima), Vl. 3, Uk. 276, kilichotungwa na Ar Dat. Na kitabu (Al Hindukiyah Al Saaidah), Uk. 6-7, kilichotungwa na LS.S. O.Malley).

([112]) (Rejea kitabu: C.V Vidya: History of Mediavel Hindu India Vol. 1 (poone 1921).

([113])(Rejea kitabu (Al Siiratu Anabawiyah), Uk. 19-28, kilichotungwa na Abul Hassan Al Nadawy).

([114]) (Twaha: 124)..

([115]) (Al An'am:82).

([116]) (Huud: 108).

([117]) (Al Shuura: 51).

([118]) (Al Haji:75)..

([119]) (Rejea Tafsiri ya Ibni Kathir kilicho tungwa na Abul Fidaa Ismail bin Kathir Al Qurashy V. 3, Uk. 64).

([120]) (Al An'am: 8-9).

([121]) (Al Furqaan: 20-21).

([122]) (Al Nahli 43).

([123]) (Ibrahim: 4).

([124]) (Rejea: Lawaamiu Al Anuwaar Al Bahiyah, V. 2, Uk. 265-305, na kitabu: "Al Islaamu" kilicho tungwa na Ahmad Shalaby, Uk. 114).

([125]) (Huud: 62).

([126]) (Huud: 87).

([127]) (Al Qalam: 4).

([128]) (Al An'am:124).

([129]) (Al Imran:33)..

([130]) (Al Zumar:30).

([131]) (Raad:38)..

([132]) (Al Anfaal: 30).

([133]) (Al Haji:40).

([134]) (Al Mujadala: 21).

([135]) (Suratul A'raafu: 158).

([136])(Angalia: Majmuu Al Fataawah cha Shekhul Islamu Ibn Taymiyah, V. 4, uk. 212-213).

([137]) (Al An'am:50)..

([138]) (Surat Shuaraa: 127,145,164, 180, 109).

([139]) (Swaad: 86).

([140]) (Al Nahli:36)..

([141]) (Rejea kitabu: (A'alaamu Nubuwah, Uk. 33).

([142])(Ahmadi Bin Abdul Haliim Bin Abdil Salaam maarufu kwa jina la Ibn Taymiyah, alizaliwa mwaka wa 661H, na alikufa mwaka wa 728H, naye ni katika wanachuoni wakubwa wa Kiislamu, ana vitabu vingi alivyotunga).

([143]) (Rejea kitabu: (Qaaidatu Fiy Wujuubi Al I'itiswaamu Bi Al Risaalah), cha Sheykhul Islam Bin Teymiyah, V. 19, Uk. 99-102. Na kitabu: (Lawamiu Anuwaar Al Bahiyah), cha Al Safaariniy, V. 2, Uk. 261-263.).

([144])(Rejea kitabu: (Aljawaabu Al Swahihi), V. 4, Uk. 96.)

([145]) (Rejea Kitabu "Al fawaaidu" cha Ibnil Qayyim, Uk.6-7).

([146]) (Ahqaaf 33).

([147]) (Yasin: 81).

([148]) (Al Ruum:27)..

([149]) (Yasin: 78-79)..

([150](Al Waaqia: 58-59).

([151]) (Al Waaqia: 63-64).

([152]) (Al Haji 5)..

([153]) (Swaad: 27).

([154]) (Dhariyaat: 56)..

([155]) (Swaad: 28).

([156]) (Yunus: 4). Rejea Kitabu "Al Fawaaid" cha Ibnil Qyyim, Uk.6-9, na "Al Tafsiirul Kabiir" cha Imamu Raazy, V.2, Uk.113-116.

([157]) (Rejea "Majallatu Daawah As Suudiyyah" No.1722, lilitoka 19/9/1420h, Uk.37).

([158]) Zimekuja ishara mbalimbali kuhusu msingi huu uliokusanya mambo mengi katika Surat Al Baqara Aya ya 285-286, na katika Surat Al An'am Aya ya 152-153, na katika Surat Al A'araf Aya ya 33, na katika Surat Al Israa Aya ya 23-37.

([159]) Muhammad Bin Abubakar Bin Ayub Al Zari'y, amezaliwa mwaka 691, na amekufa mwaka 751H, na alikuwa ni katika wanachuoni wakubwa wa kiislam, na ametunga vitabu vingi na vikubwa.

([160]) (Al Muuminun:71).

([161]) Rejea kitabu: Miftaahu Daru Saada, Vl. 2, Uk. 383, pia rejea kitabu: Aljawaabu Swahiih Liman Badala Diinal Masiih, VL. 4, Uk. 322, pia rejea kitabu: Lawaamiu Al Anuwaar, Vl. 2, Uk. 263.

([162]) (Al Muuminuun: 51-52),

([163]) (Al Shuura: 13)..

([164]) Rejea kitabu: Majmuu Al Fataawah, Vl. 2, Uk. 6.

([165]) (Maida: 44).

([166]) (Maida: 46)..

([167]) (Maida:48)..

([168]) (Al Baqara: 285).

([169]) (Al Qaswas: 57).

([170]) (Angalia ukurasa wa kitabu hiki namba 95 na 100 na 114 na 117). 117

([171]) (Majmuul Fataawah cha Sheykhul Islaam Ibn Teymiyah V.4, Uk.201-211, Ifhaamul Yahud, kimeandikwa na Samweli wa Morocco ambaye alikuwa Myahudi akasilimu Uk.58-59).

([172]) Rejea kitabu: Al Diini wa Al Daula fiy ithbaat Nubuwwat Nabiyyinaa Muhammad, Kimetungwa na Ally bin Rabban, Uk.47, Au Rejea kitabu: Al I'ilaam kilichotungwa na Qurtubiy, Uk.263)

([173]) Na mkataba huo ulikuwa ni wa miaka kumi na ujumbe huo ulifika katika mwaka wa sita tangu Mtume kuhama kutoka Makka kwenda Madina, rejea Fathul Baar, V.1, Uk. 34

([174])(ni Mji katika Miji ya Sham)..

([175]) (Na imekuja katika "Kitaabul Jihaad" katika Swahii Bukhar katika lafdhi ya (wanaoabudu moto).

([176]) Imepokelewa na Bukhar katika Bad'ul Wah'yi, mlango namba 1

([177]) (Rejea Al Diinul Fitwriy Al Abadiy, kimetungwa na Mubashir Al Twaraaziy Al Huseiniy, V.2, Uk.319).

Rejea Al Aqidatu Twahaawiy, Uk.156, na Jwaamiu Al Anuwaar Al Bahiyyah, V.2, Uk.269-277, na Mabaadiul Islaam, Uk.64

([179]) (Rejea Mthayo 21:42).

([180])Rejea kitabu: Muhammad Fiy Taurat Wal Injiil, Uk. 73, kimetungwa na Ibrahimu Khalili, na Hadithi ameitoa Bukhar katika kitabu: Manaaqib, 18, na Muslim katika mlango wa Fadhwaaili hadithi namba 2286, na imekuja katika Musnadi, V.2, Uk.256-312.

([181]) Al Ahzaab: 40

([182]) mepokelewa na Imamu Ahmad katika Musnadi wake, V.2, Uk.411-412, na ameipokea Muslim katika kitabu: Al Masaajid, hadithi ya 523.

*        Kwa maelezo zaidi rejea kitabu: Mabaadiul Islaamu, kilichotungwa na Shekh Hamoud bin Muhammad Al Laahim, na kitabu: Daliilul Mukhtaswari Lifahmil Islaamu, kilichotungwa na Ibrahim Harbi.-.

([184]) Al Insaan: 3

([185]) Rejea Kitabu: Mabaadiul Islaami, Uk.3-4.-

([186]) Al Imran:83.

([187]) Al Imran:19

([188])Al Imran: 20

([189]) Ameipokea Imamu Ahmad, V.5, Uk.3, na Ibn Hibaan, V.1, Uk.377

([190]) Ameipokea Imamu Ahmadi katika Kitabu chake (Musnad) V.4, Uk.114, na amesema Alhaythamy katika kitabuchake Almujamaa V1, 59, imepokelewa na Ahmad na twabrani katika kitabu chake Alkabir mfano wake, na wapokezi wake ni waaminifu, rejea Risalatu Fadhlul Islam, cha Imam Muhamad bin Abdulwahab -Allah amrehemu. Uk8

([191]) Ameipokea Imamu Muslim katika Kitabu "Al Imaan" hadithi no.8

([192]) Ameipokea Imamu Bukhar katia kitabu cha Imani, mlango unao sema: Muislam ni yule ambae wailam wamesalimika kutokana na ulimi wake na mikono yake, na tamko la hadithi nilake, na Muslim katika sahihi yake katika kitabu cha Imani, hadithi namba 39.

([193]) Yunus: 71-72),.

([194]) (Al Baqara: 131)

([195]) (Yunus: 84),.

([196]) (Al Maaida: 111)-Al Tadmuuriyyah: Uk.109-110

([197]) Rejea Kitabu "Al Sunnah Wa Makaanatuha Fiy Tashrii Al Islaam" kilichio tungwa na Mustafa Al Sibaaiy, Uk.376.-

([198]) Al Maaida: 48)

([199]) (Al Nahli:89)..

([200]) Al An'am: 157.

([201]) (Israa:9).

([202]) Yunus: 38).

([203]) (Yunus: 16).

([204]) (Al Anqabuut: 48).

([205]) (Suratul A'raafu: 157).

([206]) (Al Nisaa:153).

([207])(Israa:85)

([208]) (Al Kahfi: 83).

([209]) (Al Nnamli: 76).

([210]) (Rejea Al Mustashiriquuna Wal Mubashiruuna Fil A'lamil A'rabiy, kimetungwa na Ibrahim Khalili Ahmad).

( Rejea kitabu: Al Swaraau Min Ajilil Imaan, cha Dr. Joffrey Lang, Uk.34, kimetafsiriwa na Dr. Mundhiri Al Issa, kimesambazwa na Darul Fikri).

([212]) Al Mulku: 14)

([213]) (Al An'am:38).

([214]) (Al Furqaan: 53).

([215]) (Al Nnuur: 40)..

([216]) (Al Muuminun:12-14).

([217]) (Al An'am: 59).

([218]) (Rejea Kitabu "Attauraat Wal Injiil Wal Qur'an Fi Dhwaui Maarifil Hadiithi" Uk.133-283, kimetungwa na Morris Bockay, alikuwa ni Daktari wa Kinaswara katika nchi ya Ufaransa kisha akasilimu).

([219]) (Ameipokea Ahmad katika Kitabu chake cha Musnadi, V.4, Uk.131, na Abuu Daud katika Sunani Abii Daud hadithi namba 4604, V.4, Uk.200).

([220]) (Al Nahli: 44)..

([221]) (Al Najmu: 4-5).

([222])(Ahqaaf : 9)..

([223]) (Ameipokea Imuma Bukhar katika mlango wa Adhana, namba 18, V.1, Uk.155)..

([224]) (Al Ahzaab: 21).

([225]) (Al Nisaa:65).

([226]) (Hashri:7).

*        Kwa ufafanuzi zaidi rejea Kitabu "Al Tauhiid" na "Al Uswuuli Al Thalaathah" na Kitabu "A'daabul Mashiy ilaa Sswalaat" vilivyo tungwa na Al Imaamul Mujaddid Muhammad bin Abdul Wahhaab Allah amrehemu, na kitabu "Dinul Haqi" kilicho tungwa na shekh Abdul Rahman Al Umar, na kitabu "Ma'ala buda min maarifatihi anil Islam" kilicho tungwa na Shekh Muhamad bin Ally Al Arfaji, na kitabu "Arkanul Islam" kilicho andikwa na Shekh Abdullah bin Jarillah Al-Ja'arillah, -Allah amrehemu, na kitabu "Sharhu Arkanul Islam walimani" kilicho tungwa na kundi la wanafunzi, na kupitiwa na shekh Abdallah bin Jibriin.

([227]) (Rejea Kitabu "Diinul Haqq" Uk.38).

([228]) Rejea kitabu "Qurratu Uyuunil Muwahidiin" Uk.60).

*        (Kwa ufafanuzi zaidi rejea Kitabu "Kayfiyyatu Al Swalaati Al Nabiy Swalla LLahu alayhi Wasallam" kilicho tungwa na Sheykh Abdul Aziz bin Baaz, Allah amrehem).

*        (Kwa ufafanuzi zaidi rejea Kitabu "Risaalataan fiy Al Zakaat Wa Al Swalaat" kilicho tungwa na Sheykh Abdul Aziz bin Baaz, Allah amrehem).

([230]) (Tazama kitabu "Miftaah Daaru Al Saadah" vol. 2, Uk. 384).

*        Kwa ufafanuzi zaidi rejea kitabu "Daliilul Hajji Wal Umrah" kilicho tungwa na Umoja wa Wanachuoni, na kitabu "Al Tahqiiqu Wal i'dhwaah Likathiiri Min Masaailil Hajji Wal Umrah" kilicho tungwa na Shekh Abdul Aziz bin Baaz, Allah amrehem.

([231]) (Tazama kitabu "Miftaah Daaru Al Saadah" vol. 2, Uk. 384).

([232]) ا(Rejea Kitabu "Miftaahu Daaru Saadah" V.2, Uk.385, auKitabu "Diinul Haqq" Uk.67).

*        Kwa ufafanuzi zaidi rejea kitabu "Al Ubuudiyyah" kilicho tungwa na Sheykhul Islaam bin Taymiyah Allah amrehem.

([233]) (Ameipokea Imamu Muslim katika Kitabu "Al Zakaa" hadithi namba 1006).

(Imepokelewa na Imamu Bukhari katika kitabu "Al Zakaah" mlango wa 29. Na Imamu Muslim katika kitabu "Al Zakaah" hadithi No.1008), na lafdhi ni yake.

*        Kwa ufafanuzi zaidi rejea kitabu "Sharhu Uswuulul Imaani" kilichotungwa na Shekh Muhammad bin Utheymin, na kitabu "Al Imaan" kilichotungwa na Sheykhul Islaam bin Taymiyah, Allah awarehem.

([235]) (Mariyam: 65).

([236]) (Al An'am: 59)

([237]) (Rejea Kitabu "Aqiidatu Ahli Sunnatu Wal Jamaa" Uk.7-11).

([238]) (Rejea Kitabu "A'qiidatu Ahli Sunnah Wal Jamaa", Uk.44, na "Mabaadiul Islaami", Uk.80-84).

([239]) (Al Ambiyaa: 26-28).

([240]) (Al Ambiyaa: 19-20)..

([241]) (Qaaf: 17-18. Rejea Kitabu "A'qiidatu Ahli Sunnah Wal Jamaa", Uk.19).

([242]) (Al Hadiid: 25),

([243]) (Al An'am: 155).

([244]) (Al A'araaf: 158) Rejea Kitabu "Al Aqiidatu Al Swahiiha Wama Yudhwaaduha", Uk.17, na Kitabu "Aqiidatu Ahli Sunnati Wal Jamaa", Uk.22, na Kitabu "Mabaadiul Islaam", Uk.89.-

([245]) (Al Nahli:36).

([246]) (Al Nisaa:165)..

([247]) (Al Nisaa:164)..

([248]) (Huud: 31)..

([249]) (Al An'am:50)..

([250]) (Suratul Arafu: 188).

([251]) (Al Imran:19)..

([252]) (Maida:48)..

([253]) Rejea Kitabu "Al Aqiidatu Al Swahiiha Wama Yudhwaaduha", Uk.17, na Kitabu "Aqiidatu Ahli Sunnati Wal Jamaah", Uk.25.

([254]) (Al Baqara: 285)..

([255]) (Al Nisaa:150)..

([256]) Surat Qaf: 18

([257]) (Al Kahfi: 49).

([258]) (Fusswilat: 20-22),

([259]) (Fusswilat: 39),

([260]) (Ahqaaf: 33),.

([261]) (Al Muuminun:115).

([262]) (Swaad: 27).

([263]) (Zilzalah: 7-8. Rejea Kitabu "Diinul Haq", Uk.19)..

([264]) (Suratul Arafu: 187).

([265]) (Luqman: 34)..

([266]) (Al Ankabuut: 62).

([267]) (Al An'aam: 59.

Na lau katika Qur'an tukufu ingekuwa hakuna Aya yeyote isipokuwa Aya hii ingekuwa ni dalili ya wazi na hoja ya mkato ya kwamba maneno haya yanatoka kwa Allah, kwasababu viumbe katika zama zote zilizopita -mpaka katika zama hizi ambazo elimu imeenea na wanadamu kuwa na kiburi- hawaufikirii huu udhibiti ulio kienea kila kitu, mbali na kuwa na uwezo nalo, na kwa juhudi zake kubwa za kuweza kuchunguza mti au mdudu katika mazingira maalum ili kutugundulia kitu miongoni mwa siri zake, na yale yaliyo fichikana kwao kutokana na mti huo au mdudu ni makubwa zaidi. Ama kufikiria kuliko enea na kukizunguka pande zote jambo hili watu hawakulizoea na wala hawaliwezi.

([268]) (Yasin: 12).

([269]) (Al Haji: 70).

([270]) (Yasin: 82).

([271]) (Al Qamar: 49).

([272]) (Al Zumar:62).

([273]) (Al Hadid: 22-23. Rejea Kitabu "Al Aqiidatu Al Sswahiihah Wamaa Yudhwaadu", Uk.19, na Kitabu "Aqiidatu Ahli Sunnah Wal Jamaa", Uk.39, na Kitabu "Diinul Haqq", Uk.18).

([274]) (Ameipokea Imamu Ahmad katika Kitabu chake "Musnad" V.1, Uk.293, na Tirmidhi katika Sunani yake, V.4, Uk.76.)

([275]) (Rejea Kitabu "Jaamiul Uluumi Wal Hikami", Uk.128).

([276]) (Al Baqara: 83).

([277]) (Al Imran:134).

([278]) (Maida: 8).

*        Kwa maelezo zaidi kuhusu kipengere hiki rejea Kitabu "Al Duratu Al Muhtaswarah Fiy Mahaasini Al Diinil Islaamy" kimetungwa na Shekh Abdul Rahman Al Saady Allah amrehem, na Kitabu "Mahaasinul Islaami" kilichotungwa na Shekh Abdul Aziz Al Salmaan.

([279]) (Al Imra: 164).

([280]) (Al Maida: 3. Rejea Kitabu "Miftaahu Daaris Saadah", V.1, Uk.374-375).

([281])(Al An'am:38).

([282]) (Rejea Kitabu "Al I'laamu Bima Fiy Diini Al Naswaara Minal Fasaadi Wal Auhaam" kimetungwa na Imamu Qurtwuby, Uk.442-445).

([283]) (Al Haji: 78)..

([284]) (Al Nahli: 32).

([285]) (Al an'aam: 93

([286]) Al Anfaal: 50.

([287]) (Rejea Kitabu "Alfawaaidu" cha Ibnul Qayyim, Uk.116).

([288]) (Al Najmu: 39)..

([289]) ( Rejea Kitabu "Al Twariiqu Ilal Islaami", kilicho tungwa na Muhammad Asad, Uk.140), imebadilishwa kidogo.

([290]) (Al Najmu: 38)..

([291]) (Al Anfaal: 38)..

([292]) (Al Furqaan: 70).

([293]) (Tazama kitabu "Miftaah Daaru Al Saadah" vol. 1, Uk. 358،370).

([294]) (Ameipokea Abuu Yaalaa katika Musnadi wake, V.6, Uk.155, na Twabraany katika Muujamul Ausatwi, V.7, Uk.132).na kitabu "As swaghir" V.2 Uk 201, na Adhwiyau fil Mukhtarah V.5, Uk.151, 152, na amesema: upokezi wake ni sahihi, na amesema katika Mujmaa V.10, Uk.83: imepokewa na Abuu Ya'la na Alnbazar kwa upokezi mfano wake, na Twabarany katika kitabu As Swaghir na Al Awsat, na wapokei wake ni waaminifu.

([295]) (Ameipokea Ibni Abii A'swimu katika kitabu chake "Al A'haad Wal Mathaany" V.5, Uk.188, na Twabraany katika kitabu chake "Al Kabiir" V.7, Uk.314), na amesema Alhaythamy katika kitabu cha Majmai, V.1 Uk.32: Imepokelewa na Twabrani na Albazar, mfano wa hadithi hii, na wapokezi wa Albazar niwatu wazuri, ispokuwa Muhamad bin Harwun Abii nashiitwi yeye ni mwaminifu zaidi (Thika).

([296]) (Al An'am: 82).

([297]) (Twaha: 124).

([298]) (Al Ruum: 30).

([299]) (Fusswilat: 11).

([300]) (Mariyam: 88-93).

([301])Al Dukhaan: 29

([302]) (Luqman: 13).

([303]) (Al Nahli: 45-47),

([304]) (Raad:31)..

([305]((Al A'raaf: 98.

([306]) (Al Ankabuut: 40).

([307]) (Suratul A'raafu: 9).

([308]) (Al Zumar: 15.

([309])(Shuura: 45).

([310]) (Al Swaaffaat: 22-23).

([311]) (Al Nahli: 97).

([312]) (Al Swaff: 12).

([313]) (Suratul Arafu: 179).

([314]) (Al Furqaan: 44).

([315]) (Al Anfaal: 50).

([316]) (Ghaafir:46).

([317]) (Al Kahfi: 49).

([318]) (Al Nabaa: 40).

([319]) (Al Zumar:47)..

([320]) (Al Maarij: 11-14)

([321]) (Al Rahmaan: 43-44)

([322]) (Al Haji: 19-21)..

([323]) (Mariyam:67).

([324]) (Al Insan: 1-2).

([325]) (Al Ruum:54).

([326]) (Faatwir: 15).

([327]) (Al Haji: 73)..

([328]) (Rejea Kitabu "Alfawaaidu" cha Ibnul Qayyim, Uk.56).

([329]) (Al Nisaa: 28).

([330]) (Al Kahfi: 54).

([331]) (Yaasin: 77-79),.

([332]) (Al Infitwaar: 6-8).

([333]) (Tazama kitabu "Miftaah Daaru Al Saadah" vol. 1, Uk. 251).

([334]) (Al Nahli: 53-54)..

([335]) (Al Imran: 31).

([336]) (Al Nisaa: 69).

([337]) (Sabaa: 46).

([338]) (Al Nisaa: 39).

([339]) (Rejea Kitabu "Tafsiirul Qur'aaniAl Adhwiim" V.1, Uk.497).

([340]) (Rejea Taqdiim Takhriijih, Uk. 109).

([341]) (Al Nisaa: 170.

([342]) (Yunus: 108).

([343]) (Ameipokea Hadithi hii Imamu Muslim katika Kitabu "Al Birri Wa Swila" hadithi namba 2577).