Swaum ya Ashuraa

Maelezo

Mada hii inazungumzia umuhimu wa funga ya Ashuraa na fadhila zake.

Download
Tuma maoni kuhusu ukurasa huu kwa msimamizi

Maelezo ya Kina

  SWAUM YA ASHURAA.


  Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi waaalihi wasallam): ((Funga ya siku ya 'Aashuraa, nataraji kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia)) [Muslim].

  Sababu Ya Kufunga Siku Ya 'Aashuraa

  Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema: "Alielekea Mtume (Swalla Allahu 'alayhi waaalihi w sallam) Madiynah akawaona Mayahudi wanafunga siku ya 'Aashuraa, akasema: ((Nini hii?)) (yaani kwa nini mnafunga?) Wakasema hii ni siku njema, hii ni siku Allah Aliyowaokoa Wana wa Israili kutokana na adui wao, na Muusa alifunga siku hii. Akasema (Mtume (Swalla Allahu 'alayhi waaalihi wa allam):

  ((Mimi nina haki zaidi juu ya Mussa kuliko yinyi)). Akafunga siku hiyo na akaamrisha ifungwe" [Al-Bukhariy].

  Ni vizuri mtu kufunga siku ya kabla yake vilevile ambayo ni mwezi 9 Muharram na asipojaaliwa basi anaweza kufunga na siku ya baada yake ambayo ni mwezi 11 Muharram.
  Kwa nini muislamu afunge hivyo?

  ”Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allahu 'anhuma) kasema: "Alipofunga Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya 'Aashuraa na akaamrisha ifungwe wakasema: Ewe Mtume wa Allah, hii ni siku wanayoitukuza Mayahudi na Manaswara. Akasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi waaalihi wasallam): ((Ikifika mwakani In shaa Allaah tutafunga siku ya tisa pia)). Akasema (Ibn 'Abbaas) haukufika mwaka uliofuata ila alifariki Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Muslim]”.

  Hivyo ni vizuri muislamu afunge siku mbili ili kutofautiana na mayahudi ambao wanafunga siku moja tu.
  Allah atuwafikishe kuifunga funga hii na tusamehewe dhambi zetu. Allah ni mjuzi zaidi.

  Maoni yako muhimu kwetu