Nyumba Ya Peponi

Maelezo

Mada hii inazunguzia Sunna ambazo mtu akizifanya Allah anamjengea mtu huyo nyumba Peponi.

Download
Tuma maoni kuhusu ukurasa huu kwa msimamizi

Maelezo ya Kina

  بَيْتٌ فيِ الجَنَّةِ

  NYUMBA KATIKA PEPO

  تأليف: الشيخ ياسين طـه راجعها: الشيخ أبوبكر شعبان روكونكوا

  MTUNZI SHEKH: YASINI TWAHA

  KIMEREJEWA NA SHEKH: ABUBAKARI SHABANI RUKONKWA

  بسم الله الرحمن الرحيم

  Ndugu yangu Duniani kuna Nyumba nyingi za kila aina Lakini Nyumba zote hizo zimejengwa na Miti au Udongo au Tofari au Mawe au Mchanga au Simenti……Nk.

  Nyumba zote hizo zina Vyoo vya ndani na vya nje Wenye kuishi ndani ya Nyumba hizo hakupiti Siku wala Mwezi au Mwaka ila Utasikia Matatizo ndani ya Nyumbahizo, Utasikia Mtu Kaumwa, Mwengine Mnyonge, Mwengine Ana huzuni, au Nyumba ime Bomoka,Wengine Wana fukuzwa kwenye Nyumba za kupanga kwa Ajili ya kodi,Wengine Chakulatabu,Wengine Mpaka Waseme Uongo ndio wapate Kula! Yaani Matatizo Juu ya Matatizo, Hii ndio Hali ya Nyumba za Duniani na watu Wake.

  Lakini Ndugu Yangu Waweza kujenga Nyumba katika Pepo Ukiwa Hapa Hapa Duniani, Nyumba Ya ajabu kabisa, Nyumba Ambayo Tofari zake za Dhahabu na Fedha, Simenti ni Miski, ndani ya Nyumba hiyo kuna Wanawake wanaitwa Hurul-aini, Laiti Mwanamke wa Peponi Akichungulia kwenye Mbingu ya Dunia basi Dunia yote itajaa Nuuru na Harufu nzuri!!, Ndani ya Nyumba hiyo Pamejaa Neema zisizo katika, za kila Aina, Neema Ambazo Macho hayajawahi kuona, wala Masikio hayajawahi kusikia, sihivyo tu Hata Moyo kuwaza Namna ya Neema hizo zilivyo bado!, Watu Wanyumba hiyo Watakula na Kunywa Wataishi hawatokufa.

  Ndugu yangu Ukitaka Kuipata Nyumba hiyo Fanya Hili jambo:

  أَوْرَدَ اْلإِمَامُ مُسْلِمُ رَحِمَهُ اللهُ فِيْ صَحِيْحِهِ فِيْ:(بَابِ فَضْلِ السُّنَنِ الرَّاتِبَةِ قَبْلَ الفَرَائِضِ وَبَعْدَهَا):

  حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ نُمَيْرٍ حَدَّثَنَا أَبُو خَالِدٍ - يَعْنِى سُلَيْمَانَ بْنَ حَيَّانَ - عَنْ دَاوُدَ بْنِ أَبِى هِنْدٍ عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ سَالِمٍ عَنْ عَمْرِو بْنِ أَوْسٍ قَالَ حَدَّثَنِيْ عَنْبَسَةُ بْنُ أَبِى سُفْيَانَ فِيْ مَرَضِهِ الَّذِى مَاتَ فِيهِ بِحَدِيثٍ يُتَسَارُّ إِلَيْهِ قَالَ سَمِعْتُ أُمَّ حَبِيبَةَ تَقُولُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: « مَنْ صَلَّى اثْنَتَيْ عَشْرَةَ رَكْعَةً فِيْ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ بُنِيَ لَهُ بِهِنَّ بَيْتٌ فِي الْجَنَّةِ ». قَالَتْ أُمُّ حَبِيبَةَ فَمَا تَرَكْتُهُنَّ مُنْذُ سَمِعْتُهُنَّ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ. وَقَالَ عَنْبَسَةُ فَمَا تَرَكْتُهُنَّ مُنْذُ سَمِعْتُهُنَّ مِنْ أُمِّ حَبِيبَةَ.

  وَقَالَ عَمْرُو بْنُ أَوْسٍ مَا تَرَكْتُهُنَّ مُنْذُ سَمِعْتُهُنَّ مِنْ عَنْبَسَةَ. وَقَالَ النُّعْمَانُ بْنُ سَالِمٍ مَا تَرَكْتُهُنَّ مُنْذُ سَمِعْتُهُنَّ مِنْ عَمْرِو بْنِ أَوْسٍ.

  Kapokea Imam Muslim Mungu Amrehemu katika Swahihi yake: (Mlango unaoelezea Ubora wakuswali Sala za Sunna zilizo pangiliwa kabla ya Faradhi na baada yake).

  Kanihadithia Muhammad bin Abdullahi bin Numairi, Kanihadithia Baba yake na Khalid ambae ni Suleiman bin Hayyan' kutoka kwa Daaud bin Abiihindi, kutoka kwa Nuuman bin Saalim, kutoka kwa Amru bin Ausi, Amesema: Amenihadithia Ambasa bin Abii Sufyan katika Maradhi alioFishwa nayo, Mazungumzo Ambayo Ukiyasikia yanafurahisha, Amesema: Nilimsikia Mama Habiba Akisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) Akisema: {Yeyoto Atakae Swali Rakaa kumi na mbili kwa Usiku na Mchana Hujengewa Nyumba Katika Pepo kutokana na Rakaa hizo}.!!!

  Akasema Ummu Habiba: Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka nilipo Msikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake).

  Na Akasema Ambasa: Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka nilipo msikia Mama Habiba.

  Na Akasema Amru bin Ausi: Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka nilipo msikia Ambasa.

  Na Akasema Nuuman bin Saalim:Sikuacha kuswali Rakaa hizo toka nilipo msikia Amru bin Ausi.

  Ndugu zangu tukimbilieni kheri hizi na tujitahidini katika hali hii na tuwaamrishe tunaowamiliki akiwemo mke, motto, nawengineo.

  Ndugu yangu Jaribu kuiuliza Nafsi yako Maswali machache:

  1/ Miaka mingapi imepita katika Umri wangu Sijaswali Rakaa hizi?.

  2/ Thawabu ngapi zimenipita kwa sababu ya Mambo ya Kipuuzi?.

  3/ Mambo gani Mema Ambayo Nimekwisha yatanguliza mbele ya Mwenyezi Mungu?.

  4/ Lini nitaacha Kumuasi Mwenyezi Mungu?.

  5/ Nitaanza lini Kufanya Ibada?.

  6/ Kwa nini Nafsi yangu ni nzito Katika Mambo ya Kheri?.

  7/ Kwa nini Nafsi yangu ni nyepesi Katika Mambo ya Shari?.

  Mwisho kabisa:

  Ndugu yangu Muislam kuwa na pupa katika kutekeleza Sunna tulizo zitaja, Faida yake Utaikuta Mbele ya Allah pia Usisahau Kufanya Mambo ya Kheri kwa wingi kama vile: Kuswali Swala tano kwa Jamaa Muskitini, Funga za Sunna: J/tatu na Al-khamis na zile ayyaamulbiidh (Masiku meupe) Tarehe (13-14-15) Kila Mwezi ,na Funga ya Ashuraa, na Funga ya Arafaa, na Nyenginezo. Pia Katika Mambo ya Kheri kutoa Zaka na kutoa Sadaka kufanya Ibada ya Hija naUmra. Ndugu yangu Milango ya Kheri ni Mingi sanaTushindane Katika hilo, Mungu Atufanyie Wepesi.

  NAMNA YA KUTEKELEZA IBADA ZA SUNNA TULIZO ZITAJA:

  Al-fajri

  Adhuhuri

  Laasiri

  Maghreb

  Ishaa

  KABLIA

  BAADIA

  KABLIA

  BAADIA

  KABLIA

  BAADIA

  KABLIA

  BAADIA

  KABLIA

  BAADIA

  2

  4

  2

  2

  2

  Kuna Swala za Sunna Nyingine Tofauti na Tulizo zitaja:

  1/ Rakaa 2 Wakati Wa kuingia Mskitini.

  2/ Rakaa 4 Kabla ya Swala ya Laasiri 2unatoa Salam 2 unatoa Salam.

  3/ Rakaa 2 Kabla ya Maghreb kwa Mwenye Kutaka.

  4/ Rakaa 2 Baada ya Kumaliza Kutawadha. Nk….

  Tuna Muomba Mwenyezi Mungu Atupe Kila la Kheri, na Atuepushe na Kila la Shari, Atupe Mwisho Mwema Wakati Wa kufa kwetu, Atuepushe na Adhabu za Kaburini, Atufufue Siku ya MwishoTukiwa Nyuma ya Mtume wetu Muhammad (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) ,Atupe Kitabu chetu Kwa Mkono wa Kulia.

  Rehma na Amani za Allah zimuendee Nabii Muhammad Pamoja na Watu wa Nyumbani kwake na Maswahaba zake na Waislamu wote watakao Fuata Mwenendo wake Mpaka Siku ya Mwisho, Mwenyezi Mungu Atujaalie Tue Miongoni Mwa watu wema. Ameen!!

  AMIN.

  Maoni yako muhimu kwetu