KWANINI TUNAOGA JANABA?

Maelezo

Mada hii inazungumzia utofauti wa janaba na mkojo katika sheria ya kiislam

Download
Tuma maoni kuhusu ukurasa huu kwa msimamizi

Maelezo ya Kina

  بسم الله الرحمن الرحيم

  KWANINI TUNAOGA JANABA?

  لماذا نغتسل من الجنابة؟
  HALIYAKUWA SIO NAJISI
  NA WALA HATUOGI KUTOKANA NA MKOJO NA HALI YAKUWA MKOJO NI NAJISI?

  WAWEZA KUULIZA BAADHI YA WATU KWANINI UISLAM UMEAMRISHA KUOGA JOSHO LA JANABA HALI YA KUENEZA MAJI MWILI MZIMA HALI YAKUWA KIUNGO NI HICHO HICHO KIMOJA KINAHUSIKA KUTOA HAJA NDOGO NA MANII?

  HEKMA KUBWA AMBAYO MOLA AMEONDOA JOSHO KATIKA HALI BAADA YA KUKOJOA NI KUTAKA KUWAONDOLEA WAUMINI UZITO KATIKA DINI'

  HAKUNA ATAKAE BISHA KUWA KWA MWANADAMU MWENYE AFYA HAKOSI KWENDA HAJA NDOGO MARA ZISIZOPUNGUA KUMI KWA SIKU, TENA HII NI KWA MAKADIRIO YA CHINI BALI ANAWEZA KWENDA ZAIDI YA HAPO.

  LAITI SHERIA INGEWEKA JOSHO KWA HAJA NDOGO INGEKUWA NI UZITO KATIKA DINI KWANI INGEMLAZIMU KILA ANAEKOJOA HAJA NDOGO BASI AOGE JOSHO HALI AMBAYO HAJA NDOGO INAWEZA KUKUSHIKA MAHLA POPOTE WAKATI WOWOTE.

  LAKINI JANABA UKIMCHUKULIA MWANANDOA HATA AFANYE TENDO LA NDOA MARA ATAKAZO WEZA BASI LINAMTOSHA JOSHO MOJA TU KISHERIA KWANI HAIJAFUNGAMANISHWA KUWA KILA TENDO LIWE NA JOSHO LAKE.

  UKIMTAZAMA MTU ASIEKUWA KATIKA NDOA KWA YULE ALIYE BALEGHE JANABA LAKE ANAWEZA KULIPATA KWA NDOTO KISHERIA HALI AMBAYO SIO KILA SIKU ATAKUWA ANAOTA,
  HIVYO WAWILI HAWA WALIOLAZIMISHWA KUOGA JANABA UTAONA SIO MZIGO WALA UZITO KWAKUWA SIO KITU KINACHOJIRUDIA RUDIA MARA NYINGI KAMA MKOJO HIVYO NDIVYO SHERIA IKAWEKA KUOGA KWA MWENYE JANABA NA IKAWEKA KUTAWADHA KWA MWENYE KUKOJOA KWAKUWA KUOGA JANABA NI MWILI MZIMA HIVYO KUNAHITAJI TAKLIF KIDOGO HALI YA KUTAWADHA NI SEHEMU YA VIUONGO HIVYO KUTAWADHA NI WEPESI KULIKO KUOGA KWAKULE KUJIRUDIA RUDIA MARA NYINGI KULIKO YANAYOPELEKEA JANABA

  KAMA ALIVYOSEMA MOLA KATIKA QURANI:

  تشكرون وما يريد الله ليجعل عليكم من حرج ولكن يريد ليطهركم وليتم نعمته عليكم لعلكم

  MAANA YA AYA HII:NA HAJAWA MWENYEZI MUNGU NI MWENYE KUTIA UZITO KWENU NYINYI LAKINI ANATAKA AKUTWAHARISHENI NA ATIMIZE NEEMA YAKE KWENU ILI MPATE KUSHUKURU.

  ما قاله الإمام ابن القيم ردًا على من عجب من التفرقة بين المني والبول فأوجب الغسل من المني دون البول قال :

  NA YAMENIFURAHISHA SANA MAJIBU YA IBN AL KAYIM ALJAWZIY ALIPO MJIBU MWENYE KUSHANGAA TOFAUTI YA JOSHO LA MANII NA MKOJO IKAWA NI WAJIBU KUOGA JOSHO KUTOKANA NA MANII HALI YA KUTOKUOGA KUTOKANA NA MKOJO .

  AKASEMA:

  " هذا من أعظم محاسن الشريعة وما اشتملت عليه من الرحمة والحكمة والمصلحة، فإن المني يخرج من جميع البدن . ولهذا أسماه الله " سلالة " لأنه يسل من جميع البدن فتأثر البدن بخروجه أعظم من تأثره بخروج البول.

  NA HAYA NDIO YANAYOONYESHA UZURI WASHARIA YETU YA UISLAM NA YALIYOKUWEMO NDANI YAKE MIONGONI MWA HEKMA NA HURUMA PAMOJA NA MASLAHI,

  KWANI HAKIKA YA MANII YANATOKA MWILI MZIMA NA NDIO MAANA ALLAH AKAYAITA "SULAALA"
  KWAKUWA YANA CHOMOZA KATIKA MWILI MZIMA HALI AMBAYO YANAUWATHIRI MWILI ZAIDI PALE YANAPOTOKA KULIKO UNAVYO ATHIRI MKOJO
  WAKATI UKUTOKA .

  وأيضًا فإن الاغتسال من خروج المني من أنفع شيء للبدن والقلب والروح.

  NA VILE VILE JOSHO LA JANABA NI LENYE KUUNUFAISHA ZAIDI MWILI, MOYO NA ROHO KUTOKANA NA ATHARI YA KUTOKA MANII.

  فإنها تقوى بالاغتسال،
  والغسل يخلف على البدن ما تحلل منه بخروج المني وهذا أمر يعرف بالحس.

  KWA HAKIKA MWILI UNAPATA NGUVU KUTOKANA NA JOSHO

  NA JOSHO LINAFUATIA MWILI NA KURUDISHA YALE YALIO ONDOKA MIONGONI MWA NGUVU KWA KUTOKA KWA MANII.

  NA JAMBO HILI LINAJULIKANA KWA KUHISI TU BAADA YA KUOGA JANABA NA KABLA PUNDE TU BAADA YA KUTOKA KWAKUWA KUTOKA KWA MANII KUNAUTIA MWILI UCHOVU NA UVIVU AMBAPO KUOGA KUNATIA NISHATI NA UCHANGAMFU,

  HALI MKOJO UNAPOTOKA HAULETI UCHOVU WALA UVIVU HIVYO HAPAHITAJIKI JOSHO KAMA LA MWENYE JANABA.

  اللهم اجعلنا من التوابين ، واجعلنا من المتطهرين

  EWE MOLA TUJAALIE NI WENYE KUTUBIA NA UTUJAALIE KATIKA WATWAHARIFU (WASAFI) AMEEN!

  Imekusanywa na Abubakar shabani Imepitiwa na Yunus kanuni

  Utunzi wa kielimu: