(1) Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.
Ewe Muhammad! Hao wanao sema kwa kejeli, "Tusifie Mola wako Mlezi.": waambie: Yeye ni Mwenyezi Mungu wa pekee hapana mwenginewe, wala hana mshirika.
(2) Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.
Mwenyezi Mungu Mwenye kukusudiwa peke yake katika haja zote, na yote yanayo takikana.
(3) Hakuzaa wala hakuzaliwa.
Hana mtoto wala hakuzaliwa na baba wala mama,
(4) Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.
Wala hana yeyote aliye mshabihi, au mfano wake.