114 - Surat An-Nas ()

|

(1) Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu,
Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha mambo yao.

(2) Mfalme wa wanaadamu,
Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote wafalme wao na maraia.

(3) Mungu wa wanaadamu,
Mungu wa wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa ukamilifu atakavyo.

(4) Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas,
Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma ukiomba msaada kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake.

(5) Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,
Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.

(6) Kutokana na majini na wanaadamu.
Kutokana na majini na wanaadamu.