MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU UISLAMU

Download
Tuma maoni kuhusu ukurasa huu kwa msimamizi

Maelezo ya Kina

المملكة العربية السعودية

وزارة التعليم العالي

الجامعة الإسلامية بالمدينة المنورة

عمادة البحث العلمي

قسم الترجمة

تعريف موجز بالإسلام

(بللغة السواحلية)

بسم الله الرحمن الرحيم

MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU UISLAMU

Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, sala na amani ziwe juu ya Imamu wa Mitume, Nabii wetu Muhammad, na jamaa zake, na Masahaba wake wote.

 Ama baada:_

UISLAMU:_ ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja, na Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (kushuhudia) kwa moyo, na kwa ulimi, na kwa viungo.

Na (huo Uislamu) unajumuisha kuamini nguzo sita za Imani kwa kutekeleza nguzo tano za Uislamu, na nguzo mbili za Ihsani.

Na (huo Uislamu) ni risala ya mwisho miongoni mwa risala za Mwenyezi Mungu, ambayo ameiteremsha Mwenyewe Allah kwa mwisho wa manabii wake na mitume wake, Mtume Muhammad bin Abdillah (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

Na (huo Uislamu) ndiyo dini ya haki ambayo Mwenyezi Mungu hatakubali dini nyingine isiyokuwa uislamu, na hakika ameifanya Mwenyezi Mungu dini ya uislamu kuwa nyepesi na rahisi, hakuna ugumu au uzito ndani yake, wala tabu, hakuwalazimisha (Allah) wenye kuingia ndani ya dini hiyo mambo wasiyo yaweza, na wala hakuwakalifisha kwa yale wasiyoweza.

Na ni dini ambayo msingi wake ni TAUHID (kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada), na alama yake ni ukweli, na imezungukwa na uadilifu, na ndiyo usimamizi wa haki, na roho yake (dini hii) ni huruma, na ni dini tukufu ambayo huwaongoza waja (watu) kwenye kila jambo lenye manufaa katika dini yao na dunia yao, na huwatahadharisha kutokana na kila lenye madhara katika dini yao na maisha yao,

Na ni dini ambayo Mwenyezi Mungu amerekebisha kwayo itikadi na tabia, na akarekebisha kwayo maisha ya duniani na Akhera, na akaziunganisha kwayo nyoyo zilizo tafautiana, na matamanio mbali mbali, akazisafisha kutokana na sifa za upotofu, na akazielekeza kwenye haki, na akaziongoza kwenye njia iliyo nyooka.

Na ni dini iliyo sawa iliyo kamilika isiyokuwa na kasoro katika habari zake zote, na hukumu zake zote, haikuelezea ila ukweli na haki, na wala haikuhukumu ila kwa kheri na uadilifu, miongoni mwa itikadi sahihi, na vitendo vilivyo sawa, na tabia bora, na desturi za hali ya juu.

Na ujumbe wa Uislamu unalengo la kutimiza mambo yafuatayo:

~ Kuwajulisha watu mola wao na muumba wao kwa majina yake mazuri ambayo hakuna mwenye majina hayo isipokuwa yeye tu, na sifa zake za hali ya juu ambazo hakuna mwenye kufanana nae katika sifa hizo, na vitendo vyake vya hekima ambavyo hana mshirika kwenye vitendo hivyo, na kustahiki kwake (majina hayo, na sifa hzo, na vitendo hivyo) ambako hana mshirika ndani yake.

~ Kuwalingania waja (watu) ili wamuabudu Mwenyezi Mungu pekeyake hana mshirika, kwa kufuata mambo aliyo wawekea sheria katika kitabu chake (Qurani) na Sunna za mtume wake (Muhammad rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) miongoni mwa maamrisho, na makatazo ambayo ndani yake mna kutengenea kwao katika dini yao, na akhera yao.

~ Kuwakumbusha hali yao na marejeo yao baada ya kufa na mambo watakayo kutana nayo ndani ya makaburi yao, na wakati wa kufufuliwa kwao , na kuhesabiwa kwao, na mwisho wao ima peponi au motoni. Mwenyezi Mungu atawalipa kulingana na matendo yao, aliye tenda wema atalipwa wema, na aliye tenda uovu atalipwa uovu.

Na tunaweza kufupisha misingi muhimu ya Uislamu kwenye nukta zifuatazo:-

 NUKTA YA KWANZA: NGUZO ZA IMANI

 NGUZO YA KWANZA:- NI KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU MMOJA.

Nayo inajumuisha mambo yafuatayo:-

A-Kuamini kuumba kwake Mwenyezi Mungu mtukufu, yaani kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Muumba mwenye kumiliki kila kitu, mwenye kuendesha mambo yote ya viumbe vyake, mwenye uwezo wa utendaji kazi kwao.

B-Kuamini kuwa ibada ni kuabudiwa Mwenyezi Mungu mtukufu, yaani kuamini kuwa yeye Mwenyezi Mungu ndiye Muabudiwa wa haki, na kila kiabudiwacho asiyekua Mwenyezi Mungu ni batili.

C-Kuyaamini majina yake, na sifa zake Mwenyezi Mungu, yaani kuamini kuwa yeye Mwenyezi Mungu ana majina mazuri, na sifa zilizokamilika za hali ya juu, kwa namna yalivyokuja katika kitabu chake, na Sunna za Mtume wake (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)

 NGUZO YA PILI:- KUAMINI MALAIKA

MALAIKA: ni viumbe na waja walio tukuzwa, aliwaumba Mwenyezi Mungu mtukufu, wana muabudu, na wanamtii, na akawapa kazi tafauti tafauti.

Miongoni mwa hao ni: Jibril ambae alipewa kazi ya kuteremsha Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa amtakae katika manabii wake, na mitume wake. na miongoni mwa hao ni: Mikael aliyepewa kazi ya mvua, na mimea. na miongoni mwa hao ni: Israfil aliyepewa kazi ya kupuliza Baragumu wakati wa kutolewa viumbe vyote roho zao (mwisho wa dunia) na wakati wa kufufuliwa. na miongoni mwa hao Malaika ni Malaika wa mauti aliyepewa kazi ya kutowa roho wakati wa kufa.

 NGUZO YA TATU:-KUAMINI VITABU

Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na aliyetukuka aliteremsha vitabu kwa Mitume wake, ndani ya hivyo vitabu mna uongofu na kheri na utengenefu. Na tunavyovijuwa miongoni mwa vitabu hivyo ni:-

 A-TAURATI:

Aliiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume Musa (rehema na amani ziwe juu yake). Na ni kitabu kitukufu cha Wana wa Israili.

 B- INJILI:

Ambayo aliiteremsha Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) kwa Mtume Issa (sala na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

 C- ZABURI:

Ambayo Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) alimpa Mtume Daudi (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

 D- NYARAKA:

Alizopewa Nabii Ibrahimu, na Mtume Musa, (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao).

 E- QURANI TUKUFU:-

Ambayo Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) aliiteremsha kwa Nabii wake Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), mwisho wa Manabii wote, Mwenyezi Mungu akafuta kwayo (hiyo Qurani) Vitabu vyote vilivyo tangulia, na akachukuwa jukumu la kuihifadhi (hiyo Qurani) kwasabu itabaki kuwa hoja juu ya viumbe vyote hadi siku ya kiyama.

NGUZO YA NNE:-KUWAAMINI MITUME.

Mwenyezi Mungu aliyetukuka aliwatuma Mitume kwa viumbe vyake, na wa kwanza wao (hao mitume) ni Nuhu, na wa mwisho wao ni Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao. Na Mitume wote wakiwemo Issa mwana wa Mariyamu, na Uzeir (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao) na Salama, ni wanadamu walioumbwa, hawana sifa zozote za uungu. Wao ni waja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, aliwatukuza (mwenyewe) Mwenyezi Mungu aliyetukuka kwa (kuwapa) ujumbe (kwa viumbe wake) na amekamilisha Mwenyezi Mungu wajumbe wote kwa ujumbe aliokuja nao Mtume Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), na akamtuma kwa watu wote. Hakuna (Mtume wala) Nabii mwingine baada yake (Mtume Muhammad rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

 NGUZO YA TANO:KUAMINI SIKU YA MWISHO.

Nayo ni siku ya Qiyama, ambayo hakuna siku nyingine baada yake, wakati Mwenyezi Mungu atawafufuwa watu wawe hai ili wabaki ima katika nyumba ya neema (peponi), na ima katika nyumba ya adhabu iumizayo (motoni). Na kuiamini siku ya mwisho ni kuamini kila jambo litakalokuwa baada ya kufa.

Miongoni mwa mitihani ya kaburini na starehe zake na adhabu zake, na yatakayotokea baada ya hapo kama kufufuliwa, na kutawanyika, na hesabu, kisha iwe pepo au moto.

NGUZO YA SITA:KUAMINI KADARI

Kadari ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu alikadiria kila kitu, na akaumba viumbe kulingana na elimu yake iliyotangulia, na namna alivyotaka kuwa kutokana na hekima yake. Mambo yote Mwenyezi Mungu (Aliyetukuka) ayajuwa kwa elimu yake ya hapo awali, na yameandikwa kwenye Lauhil Mahfudh (Ubao ulio hifadhiwa), na Mwenyezi Mungu aliyataka na akayaumba yote, hakuna jambo lolote lenye kutokea ila kwa kutaka kwake, na kutengeneza kwake, na kuumba kwake.

 NUKTA YA PILI: NGUZO ZA UISLAMU

Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano. Na mtu hawi Muislamu wa sawa sawa mpaka aziamini, na azitekeleze, nazo ni:-

 NGUZO YA KWANZA: SHAHADA MBILI.

Ni kushuhudia kwamba hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu, na huku kushuhudia ndiwo Ufunguo wa Uislamu, na Msingi wake ambao hujengwa juu yake.

Na maana ya LA ILAHA ILLA LAHU yaani hakuna apasae kuabudiwa kwa haki isipokua Mwenyezi Mungu peke yake, yeye ndie Muabudiwa wa haki, na kila chenye kuabudiwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu ni batili. Na ILAHU maana yake ni:-mwenye kuabudiwa.

Na maana ya kushuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu:- Ni kukubali yale aliyoeleza, na kumtii katika yale aliyoamrisha, na kujiepusha na yale aliyoyakataza na akayakemea na asiabudiwe Mwenyezi Mungu ila kwa namna alivyo weka sheria.

 NGUZO YA PILI: SALA

Nazo ni Sala tano katika nyakati tano usiku na mchana, Aliziwekea sheria Mwenyezi Mungu ili ziwe ni utekelezaji wa haki yake Mwenyezi Mungu ambayo inawalazimu waja wake, na ziwe ni kushukuru neema zake Mwenyezi Mungu, na mfungamano baina ya Muislamu na Mola wake anamnong’oneza ndani yake na anamuomba, na ili ziwe ni zenye kumzuia Muislamu kutokana na mambo machafu na maovu, na akazifanya kuwa ni dini bora, na kutengenea kwa imani, na Thawabu za papo hapo na za baadae. Mja hupata kwa hizo Sala raha ya nafsi, na ya mwili, ambayo humfanya kufaulu duniani na akhera.

 NGUZO YA TATU: ZAKA

Nayo ni sadaka ambayo huitowa yule inaye mlazimu, kila mwaka kwa wanaostahiki kupewa, miongoni mwa Mafukara na wengineo miongoni mwa wale wanao faa kupewa Zaka, na hiyo Zaka si lazima kwa fukara ambae hana kiwango cha Zaka, lakini nilazima kwa matajiri, ili kutimiza dini yao, na Uislamu wao, na kuziendeleza hali zao, na tabia zao, na kuwaondoshea maafa wao na mali yao, na kuwatakaza kutokana na makosa, na kuwahurumia wenye kuhitaji, na mafukara, na kusimamia maslahi yao yote, na hiyo Zaka pamoja na hilo, ni fungu dogo sana ukilinganisha na kile alicho wapa Mwenyezi Mungu miongoni mwa mali na riziki.

 NGUZO YA NNE:SAUMU

Nayo ni kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa tisa miongoni mwa miezi inayokwenda kwa hesabu za kimwezi kwa kalenda ya kiislamu. Katika mwezi huo wa Ramadhani Waislamu huwacha kila kitu chenye kutamanisha, au kusababisha kufunguwa, kama vile kuwaingilia wake zao mchana wa ramadhani, kunywa, kula, na kadhalika, kutoka kuchomoza alfajiri mpaka kuzama kwa jua, na huwalipa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo miongoni mwa fadhila zake, na hisani yake, kukamilika dini yao, na imani yao, na kuwasamehe maovu yao, na kuwapandisha daraja zao, na mengineyo miongoni mwa yale aliyo yaweka kwenye Saumu miongoni mwa kheri kubwa katika dunia na akhera.

 NGUZO YA TANO:-HIJA

Nayo ni kuitembelea Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu (Al-Kaaba) kwa ajili ya kutekeleza ibada makhsusi katika wakati makhsusi kama inavyo eleweka katika sheria ya kiislamu, ameifanya Mwenyezi Mungu (Hija) kuwa lazima kwa anae weza, katika umri mara moja, na katika hiyo Hija hukusanyika Waisilamu katika eneo bora (Makka) kutoka kila sehemu, wanamuabudu Mola mmoja, wanavaa nguo aina moja, hakuna tofauti baina ya kiongozi na raiya, na tajiri na fukara, na mweupe na mweusi, wanatekeleza ibada maalum.

 Miongoni mwa hizo ibada tukufu ni:-

A-Kusimama kwenye uwanja wa Arafat.

B-Kuizunguka Al-Kaaba Tukufu (Kibla cha Waislamu).

C-Kutembea baina ya Safa na Marwa.

Na ndani ya hiyo Hija mna manufaa mengi ya kidini, na ya kidunia ambayo hayahesabiki.

 NUKTA YA TATU:IHSAN

Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu aliyetukuka kwa imani na kujisalimisha (kwake) kama kwamba unamuona na ukiwa haumuoni basi yeye anakuona, yaani uhisi hivyo, na uifanye kwa namna Sunna ya mtume wake Muhammad (rehema na amani za MwenyeziMungu ziwe juu yake) inavyoeleza na bila ya kuikhalifu.

Na yote yaliyotangulia yanakusanya maana ya Dini ya Kiislamu. Na ina eleweka ya kwamba Uislamu umekwisha panga maisha ya watu wake wakiwa mmoja mmoja, na wakiwa makundi makundi, kwa mambo ambayo yanawapa ufanisi katika dunia na akhera. Ukawahalalishia kuowa na ukawahimiza, na ukawaharamishia zinaa na liwati na mambo yote mabaya. Na ukawalazimisha kuunga jamaa na kuwasikitikia mafukara na maskini, na kuwatumikia, kama ulivyolazimisha na kuhimiza katika kila tabia iliyo njema, na ukaharamisha na kutahadharisha kutokana na kila tabia mbaya, na ukawahalalishia pato zuri (halali) kwa kupitia biashara na ukodishaji, na mfano wa hayo. Na ukaharamisha riba, na kila biashara iliyo haramishwa, na kila jambo lenye ulaghai na udanganyifu.

Kama ulivyotambuwa Uislamu tafauti ya watu kutengenea (kunyoka) katika njia yake, na kuchunga haki za wengine. Ukaweka sheria za adhabu zenye kukemea baadhi ya uvukaji mipaka inayofungamana na haki zake (Mwenyezi Mungu aliyetakasika), kama kutoka kwenye Uislamu na zinaa, na kunywa pombe, na makosa mengine kama hayo.

Kama ulivyoweka sheria za adhabu zenye kukemea uvamizi wa aina yoyote wa haki za watu katika nafsi zao na mali yao na heshima zao kama: kuuwa, au kuiba, au kumsingizia mtu (kuwa amezini bila ya kuwa na mashahidi) au uvamizi kwa kupiga na kuudhi na kuchukuwa mali za watu pasina haki. Na ni adhabu zenye kulingana na kosa bila ya kuongeza wala kupunguza,

Kama ulivyopanga na ukaweka mipaka na uhusiano baina ya raiya na viongzi. Na ukawalazimisha raiya kuwatii (viongozi), katika mambo yasiyopelekea kumuasi Mwenyezi Mungu. Na ukaharamisha kutoka katika amri zao hali itakayo pelekea ufisadi kwa watu wote kwa jumla na kwa watu binafsi.

Na mwisho tunaweza kusema kuwa Uislamu umefungamana na kujenga na kuweka uhusiano sahihi, na matendo sahihi baina ya mja na Mola wake, na baina ya mwanadamu na jamii yake katika mambo yake yote, hakuna kheri yoyote miongoni mwa tabia na utendajikazi isipokuwa Uislamu umekwisha uongoza Umma wake, na ukawahimiza kwayo, na hakuna shari yoyote katika tabia na utendaji kazi ila Uislamu umekwisha utahadharisha Umma wake, na ukawakataza, jambo ambalo lina bainisha ukamilifu wa dini hii, na uzuri wake katika pande zote.

 Na kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu

Mola wa viumbe vyote.

nnnnnnnnnnn

.