HUKUMU YA KUMTAKIYA MTU KRISMASI NJEMA

Maelezo

Mada hii inazunguzia madhambi ya kumtakia mtu krismasi njema

Download
Tuma maoni kuhusu ukurasa huu kwa msimamizi

Maelezo ya Kina

  بسم الله الرحمن الرحيم  HUKUMU YA KUMTAKIYA MTU KRISMASI NJEMA.

  Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin 'Uthaymiyn

  Imekusanywa na: Abubakari Shabani Rukonkwa.

  Imepitiwa na: Yunus Kanuni Ngenda.
  Chanzo: Fataawa al-'Aqiydah, uk. 246-248

  Swali

  Ipi hukumu ya kumpongeza mtu kwa krismasi? Vipi tuwajibie wakitupongeza? Je, inajuzu kushuhudia sikukuu zao? Je, ni dhambi kufanya jambo lolote katika haya tuliyoyataja bila ya nia? Tuchukulie ya kwamba mtu anafanya hivyo kwa kutaka kuwafurahisha, au kwa kuwa mtu anasikia haya na hataki kuwaumiza.

  JIBU.......
  Wanachuoni wote wamekubaliana ya kwamba ni haramu kuwapongeza makafiri kwa krismasi na sherehe zao zingine za kidini. Hili limesemwa na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake na akasema:


  “Hata hivyo, wamekubaliana wanachuoni ya kwamba ni haramu kuwapongeza makafiri kwa sikukuu zao kama sherehe na kufunga. Mfano wa hilo ni kusema:  "Uwe na sikukuu njema!.”

  Ikiwa kauli hii si Kufuru, basi angalau ni dhambi kubwa. Dhambi hii ni kubwa kama ambavyo mtu anavyowapongeza wanapoanguka (kufanya sujudu) kwa nyuso zao kwenye misalaba. Ukweli ni kwamba Allaah Anaona hili kuwa ni baya zaidi kuliko mtu kuwapongeza kwa kunywa pombe, na kuua mtu, zinaa na mfano wa hayo.  Watu wengi wasiojua thamani ya Dini wanaanguka katika kosa hili. Hawajui jinsi ya dhambi hii inavyotisha. Yule anayempongeza mtu kwa dhambi, Bid´ah au kufuru, amejisababishia mwenyewe hasira na ghadhabu za Allaah."

  Sababu ya kuwa ni haramu kuwapongeza kwa sherehe zao ni kwamba ina maana mtu anakubaliana na kuridhika kwa sherehe zao za kikafiri hata kama mtu mwenyewe haridhii kufuru hii. Ni haramu kwa Muislamu kuridhika kwa sherehe za kikafiri na kuwapongeza. Allaah (Ta´ala) Haridhii hilo. Allaah (Ta´ala) Anasema:

  إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ وَلَا يَرْضَى لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ وَإِن تَشْكُرُوا يَرْضَهُ لَكُمْ
  “Mkikufuru, basi (eleweni kuwa) hakika Allaah ni Ghaniyyun (Mkwasi, Hahitaji lolote) kwenu, na wala Haridhii kufuru kwa waja Wake. Na mkishukuru (Yeye) Huridhika nanyi.” (az-Zumar 39 : 07)  الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا
  “Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe (ndio) Dini yenu.” (al-Maaidah 05 : 03)  Kwa sababu hiyo ni haramu kuwapongeza kwa sherehe hizi sawa mtu ikiwa atazishiriki au hapana.


  Hata hivyo, ikiwa wao watatupongeza sisi na kututakia sikukuu njema, tusiwajibie. Kwa kuwa sikukuu hii si sikukuu yetu. Sikukuu hii Hairidhii Allaah (Ta´ala). Sherehe hizi aidha zimezushwa katika Dini yao au ipo [katika Dini yao lakini] ambayo Uislamu imeifuta wakati Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alipotumwa kwa viumbe vyote. Allaah (Ta´ala) Anasema:

  وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ
  “ Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (al-´Imraan 03 : 85)  Hali kadhalika, ni haramu kwa Waislamu kuitikia mialiko yao ya sikukuu. Kwa sababu hii ni aina kubwa ya kuwapongeza kwa kuwa mtu anashiriki huko.  Hali kadhalika, ni haramu kwa Waislamu kujifananisha na makafiri na hivyo ni kama kufanya sherehe kama hizi, kubadilishana zawadi, kugawa vitu tamutamu (pipi), kuweka meza ya chakula, kuacha kufanya kazi katika siku kadhaa na kadhalika. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

  “Yule mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.”

  Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kasema katika kitabu chake "Iqtidhwaa'-us-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalafah Aswhab-il-Jahiym":

  "Kuiga baadhi ya sikukuu zao, linapelekea katika mapenzi kwa uongo huu wanaofuata."  Yule ambaye anafanya matendo haya ni mwenye madhambi, sawa ikiwa atafanya kutaka kuwafurahisha, au anafanya hivyo kwa mapenzi, au anasikia aibu, au sababu nyingine yoyote. Hii ina maana ya kwamba mtu anafungua mafundo ya Dini ya Allaah. Hali kadhalika anawapa nguvu makafiri kwa hili na linawafanya kujifakhiri kwa dini yao.  Tunamuomba Allaah Awaimarishe Waislamu kwa Dini yao, Awape thabati na Awasaidie dhidi ya maadui wao – kwa hakika Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye uwezo. Ameen!!


  Utunzi wa kielimu: