Shekh anazungumzia: Uchafu wa wenye kupinga hadithi za mtume (s.a.w) kisha amenukuu maneno ya Imamu Suyutwiy ambayo yamebainisha hukumu ya mwenye kukanusha hadithi za Mtume (s.a.w) kuwa ni kafiri.
Shekh anazungumzia: njia za kuifanyia kazi Qur’an kupitia matendo ya Mtume (s.a.w) kisha amebainisha baadhi ya vitabu ambavyo vina warudi wenye kupinga hadithi za Mtume (s.a.w).
Shekh anazungumzia: Umuhimu wa elimu ya hadithi, kisha amebainisha kwamba asiye amini kuwa hadithi ni hoja basi atakuwa adui wa uislam, kisha amebainisha maana ya kumtii mtume (s.a.w)
Shekh anazungumzia: Wadhfa wa Hadithi za Mtume (s.a.w) na kwamba zinaweka wazi na kufafanua namna ya utekelezaji wa amri za Qur’an tukufu, pia amezungumza maneno ya Imamu Suyutwi kuhusu cheo cha hadithi za mtume(s.a.w).
Shekh anazungumzia: Utangulizi wa mtunzi pia amezungumzia Umuhimu wa elim ya hadithi, na maana ya hadithi, na cheo cha Quraan na Sunnah pia amewarudi wenye kuzipinga Hadithi.
Shekh anazungumzia: Historia fupi ya mwandishi wa kitabu hiki cha umdatul ahkami, Shekh Abdul Ghany Al Maqisy Allah amrehemu, na umuhim wa kuifanyia kazi elim.