معلومات المواد باللغة العربية

Abubakari Shabani Rukonkwa - Video

Idadi ya Vipengele: 1198

  • Kiswahili

    Madaa hii inazungumzia: Umuhimu wa kuzingatia katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na amebainisha neema ya viungo ikiwemo figo na alama za kuharibika kwake, na amebainisha kazi za figo mwilini, mwisho amezungumzia umuhimu wa kushukuru neema na kwamba mwanadamu ataulizwa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Maneno na wasia wa Mtume (s.a.w) kwa binti yake Fatwima na imeelezea heshima na adabu aliyokuwa nayo Fatwima (r.a), pia imezungumzia kwa ufupi historia ya Ummu Kuluthum mtoto wa Mtume (s.a.w).

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) bi Maimuna bint Harith na kwamba ni katika wakeze Mtume (s.a.w) waliosifika na ucha Mungu, pia imeelezea habari za bi Fatwima na Ally bin Abiy Twalib (r.a).

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Uzinduo kwa akina mama wa kiislamu na kuwausia kufuata mwenendo wa nyumba ya Mtume (s.a.w), pia imezungumzia idadi ya wakeze Mtume (s.a.w), na umuhimu wa kufanya uadilifu na sulhu katika ndoa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Nasaha kwa wanawake wote wa kiislamu kupitia mifano ya wanawake wa nyumba ya Mtume (s.a.w), pia imezungumzia umuhumu wa kushikamana na dini na kujiepusha na tabia mbaya za kimagharibi.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Sababu ya mama Aisha (r.a) kuachwa na msafara na hatimaye kusaidiwa na Swahaba Swaf’wan bin Muwatwal (r.a), pia imezungumzia hatari na maafa ya ulimi.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Maneno aliyosema mama Aisha (r.a) kabla ya kushuka Aya kwa Mtume (s.a.w) za kumtakasa kutokana na uchafu aliozushiwa, pia imezungumzia hatari ya kumzushia muislamu uchafu wa zinaa na kwamba ni katika madhambi makubwa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Mtume (s.a.w) kumruhusu bi Aisha (r.a) kwenda kwao wakati akisubiri suluhisho kutoka kwa Allah kutokana na uzushi aliozushiwa, pia imezungumzia kilio alicholia mama Aisha (r.a) mbele ya wazazi wake.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Kisa cha uzushi aliozushiwa mama Aisha (r.a) na kwamba madhara ya ulimi ni makubwa kulikoupanga, pia imezungumzia hatari na ubaya wa uzushi katika uislamu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kujifunza na kuiga namna Mtume (s.a.w) alivyoishi na wake zake ili kuzijenga familia katika uislamu wa kweli, pia imezungumzia hatari ya kuvuka mipaka na kuipotosha jamii.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) bi Aisha bint Abubakar (r.a) ambaye alisifika na sifa ya ujuzi (elimu), pia imezungumzia ubora na nafasi ya bi Aisha (r.a) katika uislamu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) bi Safia bint Huyay (r.a) ambaye ni mwanamke aliyesifika na sifa ya ukweli, pia imezungumzia mafundisho yanayopatika kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w).

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) Ummu Habiba Ramla bint Abi Sufiyan (r.a), na ukubwa wa imani na msimamo aliokuwa nao, pia imezungumzia sifa walizo kuwa nazo wake wa Mtume (s.a.w).

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) Zainab bint Jahshi (r.a), na sababu za kuolewa kwanza na Zaid bin Haritha (r.a), pia imezungumzia sababu ya Mtume (s.a.w) kumuoa Zainab bint Jahshi.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Nafasi ya bi Khadija (r.a) katika Uislamu na umuhimu kwa wanawake wa kiislamu kumuiga bi Khadija (r.a), pia imezungumzia ucha Mungu na uadilifu aliokuanao bi Khadija, na athari aliyoacha baada kufa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Wanawake katika nyumba ya Mtume (s.a.w) na imeanza na historia fupi ya bi Khadija (r.a), pia imezungumzia mwanzo wa wahyi (ufunuo) kumshukia Mtume (s.a.w).

  • Kiswahili

    Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya sita na yasaba, kuhusu na najsi ya mbwa, kisha amebainisha mbwa anaefaa kufugwa, kisha akabainisha namna ya kusafisha najsi ya mbwa, na akasema kuwa hadithi ya sita na ya saba zinabainisha kuwa mbwa ni najsi.

  • Kiswahili

    Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya sita, amebainisha kauli za wanachuoni kuhusu najsi ya mbwa, kisha akabainisha uwajibu wa kutumia mchanga katika kuosha najsi, kisha akabainisha faida katika hadithi hii: kwamba najsi ya mbwa na nguruwe ni najsi nzito, mbwa akilamba katia chombo kinakuwa najsi.

  • Kiswahili

    Shekh anazungumzia: Ufafanuzi wa hadithi ya tano ameleza faida za hadithi ikiwemo, kujuzu kujitwaharisha katika maji yanayo tembea na inajuzu kukidhi haja katika maji yanayo tembea kwa dharura. Kisha amebainisha hadithi ya sita inayo zungumzia namna ya kuosha chombo kilicho lambwa na mbwa na nguruwe kisha ametaja taratibu za kufuga mbwa.

  • Kiswahili

    Shekh anazungumzia: ufafanuzi wa hadithi ya tano na amebainisha upotovu wa rai ya dhwahiriya katika hadithi hii, kisha amebainisha faida za hadithi hii ikiwemo: makatazo ya kukojoa katika maji yalio tuwama, na kwamba Uislam unalinda mazingira, uislam unapiga vita uchafuzi wa mazingira, na usafi nikatika imani.