Shekh Jabir Yusuf Katura: Amemaliza masomo yake katika chuo kikuu cha kiislam Madina nchini Saudi Arabia. Kwa sasa ni mlinganiaji na khatwib katika Msikiti wa Ijumaa Mwanza, pia ni Mudir katika Markaz ya Thaqafah, Mwanza Tanzania.-
Jazzai Bin Flaih Alswuweylh: Amezaliwa mwaka 1969, ni mmoja kati ya wasomaji maarufu katika Nchi ya Kuwait, na alimaliza masomo yake ya sheria na Qur'an na tajweed katika chuo kikuu cha Kuwait.
Msomaji wa Misri mwenye sauti tamu, na mwenye kibali (ijaza) cha kumasomo visomo aina kumi, na ana nakala kadhaa za Qur'ani kwa riwaya mbalimbali.
Shekh Mahmoud Ahmad Abdulhakam: Amezaliwa siku ya jumatatu sawa na 1February 1915 katika kijiji cha Karnak, amehifadhi QUR'AN Misri katika Chuo cha Azhar, na alishiriki katika kuanzisha umoja wa wasomaji wa Qur'an, alifariki siku ya jumatatu sawa na 13September 1982, Mwenyezi Mungu amrehem.
Shekh Muhmmad Sharifu Famau: Alikua ni mlinganiaji maarufu nchini Kenya, pia alikua ni Mudir katika Madrast Tawhid mpaka alipofariki dunia katika mji wa Malindi nchini Kenya, Allah amsamehe na amrehem, Ameen!.-