NI YUPI RAFIKI MWEMA?

Maelezo

Mada hii inazungumzia umuhim wa kutafuta rafiki mwema

Download
Tuma maoni kuhusu ukurasa huu kwa msimamizi

Maelezo ya Kina

  بسم الله الرحمن الرحيم

  Utangulizi

  Ndugu zangu katika imani ni kawaida kwa binadam na ni muhim kuwa na rafiki, Lakini kwa Muislam kuchagua rafiki mzuri ni lazima kwa ajili ya kuhifadhi Dini yetu. Kufanya urafiki na watu wema wenye tabia nzuri, wenye dini na heshima ni moja ya mambo yanayotufanya sisi Waislam kuwa katika njia iliyonyooka, na kuwa mfano bora katika jamii.

  Mtume (Swalla Allahu Alaihi Wa Sallam) amesema:

  "Mtu yamkini (inawezekana) kufuata dini ya rafiki yake, kwa hivyo muangalie unayemfanya rafiki." {Abu Dawud na Tirmidhiy}

  Ukiona rafiki yako ana matendo maovu, jaribu kumkumbusha,kumpa nasaha na mawaidha, asipobadilika na akaendelea kufanya maovu, ni vema kumuepuka kwa sababu unaweza ukaiga tabia zake ambazo zinakwenda kinyume na Dini yako (ya kiislam). Lakini pamoja na kumuepuka inakupasa kumfanyia wema na kumuombea kwa Allah uongofu.

  Allah (Subhanahu Wa Ta'ala) amesema:

  "Na Siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: 'Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume (S.a.w) Ee Ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki! Amenipoteza nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, (kunijia) na kweli shetani ni khaini (mwenye khiyana) kwa mwanaadamu."
  {Surat Al-Furqaan 25:27-29}

  Allah (Subhanahu Wa Ta'ala) tena Anasema:

  "Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipokuwa wachaji Allah (wacha Mungu)" {Surat Az-Zukhruf 43:67}

  Muumini ni kioo cha ndugu yake muumini, akiona makosa ya mwenzake inampasa amueleze kwa uzuri na kumsaidia kurekebisha kosa hilo.

  Huo ndio urafiki unaotakiwa katika Uislam, na muumini wa kweli lazima ataangalia nani wa kumfanya rafiki.

  Lakini kwa masikitikiko makubwa vijana wa kiislam wa leo hawana habari na jambo kama hili, imefikia hatua marafiki wa zama hizi wanatumia muda mwingi kusaidiana katika mambo yasiyofaa, badala ya kusaidiana katika mambo ya dini na ya kheri.

  Tunamuomba Allah atuongoze pamoja na marafiki zetu. Ameen!!!

  Top of Form

  Bottom of Form

  Utunzi wa kielimu: