• Kiarabu

  PDF

  Kitabu Misingi ya Dini ya Uislamu cha Sheikh Muhammad bin Sulaiman Tamimy (r.h), kimepangiliwa kwa njia ya maswali na majibu na Sheikh Muhammad Twayib Answary Madany Allah amlipe, kimekusanya kitabu hiki mambo muhimu katika dini ya uislamu.

 • Kiarabu

  PDF

  Kitabu chaelezea visa mbali mbali kuhusu badhi ya watu wa falsafa na fani mbali mbali waliyo tangulia na wazama hizi sababu iliyo wapelekeya kuingia katika Uislamu.

 • Kiarabu

  PDF

  Muhadhara mzuri sana wa Sheikh Swaleh bin Abdul-aziz Ali-Sheikh (Allah amuhifadhi), mada yake ilikuwa ni (Huu ndio Uislamu), palikuwa na mambo mengi ndani yake: Huu ndio uislamu katika itikadi na ibada, katika sheria, hukumu za kidunia, tabia, uchumi, mambo ya kijamii, na udugu na kuto tengana, mahusiano nchi kwa nchi, nk...

 • Kiarabu

  PDF

  Kitabu cha sheikh Swaleh huswaini, akipinga vikali ripiti ya kimagharibi ikizungumzia utata kuhusu mada mbali mbali zinazo ambatana na uhuru katika dini ya kiislamu kwa ujumla na nchi ya saudia, akachambuwa na kuwafedhehesha.

 • Kiarabu

  PDF

  Kitabu asili yake ni muhadhara alio utoa sheikh Muhammad Amin bin Muhammad Almuhtar Ash-shanqitwi (r.h), katika muskiti wa Mtume (s.a.w), kaelezea mambo kumi yanayo zunguka dini: 1-Tauhidi. 2-Mawaidha. 3-Tofauti ya matendo mema na mengineyo. 4-Kuhukumu kinyume na sheria ya Mungu. 5-Hali ya kijamii. 6-Uchumi. 7-Siasa. 8-Gogoro la makafiri kuwatawala waislamu. 9-Tatizo la udhaifu wa waislamu na uchache wa maandalizi dhidi ya maaduwi wao. 10-Gogoro la kutofautiana nyoyo katika jamii.

 • Kiarabu

  PDF

  Akili zetu pindi hazipo huru kwa kufikiria mambo na kuhukumu kwa hakika hatuwezi kufahamu uzuri au uhakika au jambo lolote, lakini ukiwa na fikra tofauti kuhusu Uislamu, au umesoma au kusikia kutoka kwenye chimbuko lisilokua laasili utaona mambo yaajabu kuhusu Uislamu na Waislamu, twakutaka usome kitabu hiki kitakubainishia uhakika wa Uislamu na baadhi ya mazuri yake.

 • Kiarabu

  PDF

  Muheshimiwa Mwanadamu... nakwambia kwa sababu wewe ni Mwanadamu... haijalishi ukiwa mkristo au yahudi... au budhi au majusi... au mwenye kuabudia sanamu au ambae hana dini... au mwenye dini... mwanamume au mwanamke... nakwambia kwa sababu wewe ni binadamu... Jee kuna siku hata moja uliwahi kujiuliza swali kamahili: kwa nini wewe ni Muumini... na kipi unacho kiamini... kwa nini umechagua dini uliyokuwa nayo?.

 • Kiarabu

  PDF

  Njia ya kuokoka: Ni risala inayoelezea misingi ya Uislamu ambayo nilazima aijuwe kila mtu anaetaka kuingia katika Uislamu.

 • Kiarabu

  PDF

  Haki za muislamu: kasema mtunzi: fikra ya hii bahthi inakusanya hadithi zilizo tolewa na sunni na imamiyya zinazo ambatana na mada ya (haki za muislamu), malengo zifanyiwe kazi zote kwa njia ya kisheria....

 • Kiarabu

  PDF

  Siri za kuhujumu uislamu na mtume wa waislamu: katika ujumbe huu muhimu anabainisha mtunzi -Allah amuhifadhi- kuhusu vitendo vinavyo fanyika dhidi ya uislamu na nabii wa uislamu kwa upande wa makafiri, na alitaja mifano ya wagaidi dhidi ya uislamu na mtume (s.a.w), na daawa zao, na kubainisha makusudio yao miongoni mwa kazi zao hizi mbaya, na wajibu wa muislamu kuhusu kauli hizi na vitendo hivi vya chuki, mwisho kabisa kabainisha wenye vitendo hivyo ni mayahudi na washirika wao.

 • Kiarabu

  PDF

  Maana ya ujumla ya dini ya kiislamu: kitabu hiki kina milango (12), kinazungumzia kwa ufasaha njia za peponi na motoni na maana ya uislamu na kumuamini Allah na siku ya mwisho, na qadari, na ghaibu, na malaika, na majini, na mitume, na vitabu.

 • Kiarabu

  DOC

  Kuishi na wasiokuwa Waislamu katika jamii ya kiislamu: Risala hii yazungumzia namna za makafiri wanaoishi katika miji ya kiislamu, na hukumu zao, na haki zao na namna ya kutoa kodi na mengineyo.

 • Kiarabu

  PDF

  Kuujua uislamu: Kitabu hiki kinazungumzia namna ya kulingania kupitia Uislamu, na kufichua uhakika wa maneno yanayo semwa na baadhi ya watu kwa kuutuhumu Uislamu kama ni Ugaidi na kuuchukiya, na kwamba umemzulumu mwanamke haukumpa haki zake.

 • Kiarabu

  PDF

  Njia ya kuelekea katika uislamu: Kitabu hiki kinakuongoza katika uzima wa milele, kinakuongoza katika Imani ya kumjua Mola wako alie kuumba, na kinakuongoza katika itikadi sahihi inayo kubaliana na akili yako na maumbile yako,utajua kupitia kitabu hiki mwanzo wa kuumbwa binadamu na mwisho wake, na hikima ya kuwepo kwake, na mengineyo. kitabu hiki kimeandaliwa kwaajili ya wasiokuwa waislamu, kwa maana hiyo utaona kipo kwa ufupi.

 • Kiarabu

  PDF

  Amani ktk maisha ya watu: Mda hii inavipengele vitano na hitimisho. 1: Amani ktk Qur-an na sunna. 2: Maana ya Amani ktk jamii ya Kiislamu. 3: Sheria kufanya kazi na Amani kwa ujumla. 4: Kumpa Amani asie Muislamu ktk Nchi za Kiislamu. 5: Amani ktk Nchi ya Saudi arabia. Hitimisho: Mambo muhimu yanayo sababisha Amani ktk jamii ya Kiislamu.

 • Kiarabu

  PDF

  Haki za binadamu katika uislamu: Katika uchambuzi huu tutabainisha uhakika wa Haki za binadamu kama inavyo elezwa katika zama hizi, pamoja na kuelezea alama zake, na ufahamu wake, na matokeo yake, katika vipimo vya Uislamu.

 • Kiarabu

  PDF

  Kitabu hiki kimekusanya Yasiyo kuwa na budi kuyajuwa katika uislamu kwanjia nyepesi kutokana na itikadi na ibada na adabu na mengineyo, na msomaji atakuwa na fikra ilio wazi kuhusu dini ya kiislamu, na inawezekana akafahamu hukumu nyingi sana na amri nyingi na makatazo mengi.

 • Kiarabu

  PDF

  Niongoni mwa mazuri ya dini ya kiislamu: Kabainisha sheikh (r.h), badhi ya mazuri katika dini ya uislamu, na kitabu hiki nisehemu ya kitabu cha Mawaridi dwam-ani lidurusi ramadhani.

 • Kiarabu

  PDF

  Ubora wa Uislamu: kasema sheikh Swaleh bin Abdul-aziz Ali-sheikh Allah amuhifadhi: kitabu hiki ni katika vitabu muhimu sana alivyo andika sheikh Muhammad bin Abdul-wahab (r.h), akakipanga jina la ubora wa uislamu, kwa sababu kinazungumzia yanayo faa ndani ya uislamu na yasiyo faa na kubainisha namna wema walio tangulia namna walivyo kua, nakuelezea ubora wa uislamu na maana yake na mambo ya bida.

 • Kiarabu

  PDF

  Lulu kwa ufupi kuhusu Mazuri ya Dini ya Uislamu: Kubainisha baadhi ya mazuri ya dini ya uislamu, na umuhimu wa mada hii.

Ukurasa : 2 - Kutoka : 1
Maoni yako muhimu kwetu