• Maneno kuhusu haki za binadamu: katika makala hii anabainisha muandishi haki za binadamu katika miji ya kiislamu, na katika kivuli cha sheria ya kiislamu, sheria ambayo humpa kila mmoja haki yake, katika njia iliyo sahihi kwa misingi ya dini inayo ridhiwa na watu wote.

  • Mafhumu ya huria katika uislamu: Katoa khutba ya ijumaa sheikh Suudi shurem -Allah amuhifadhi- katika muskiti wa makkah tarehe 2-11-1432, kazungumzia Mafhumu ya huria katika uislamu, na kabainisha ufahamu ulio sahihi na kuwahadharisha na ufahamu wa kimakosa kutokana na neno hili, na kabainisha ya kwamba uislamu ndio ulio dhamini uhuru kwa kushikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na mtume wake (s.a.w).

  • Sherehe ya maana ya uislamu: katika makala haya tunaelezea maana ya uislamu na nguzo zake kwa ufupi, uislamu ni dini iliyo ridhiwa na Mwenyezi Mungu ili ifuatwe na nguzo zake ni tano: 1- kukubali kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu pekeyake, na Muhammad (s.a.w), ni mja wake na mtume wake. 2- kusimamisha swala. 3- kutoa zakka. 4- kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani. 5- kwenda hijjah kwa mwenye uwezo.

  • Uharamu wa kumwaga damu ya Muislamu: Katoa khutba ya ijumaa sheikh Swaleh bin Muhammad Ali-twalib Allah amuhifadhi katika muskiti wa makkah tarehe 17-02-1432, kazungumzia uharamu wa kumwaga damu ya Muislamu, akataja dalili katika Qurani na sunna, akaelezea kujiripua na adhabu zake siku ya qiyama, akawatahadharisha vijana wa kiislamu kumwaga damu za waislamu au wasio kuwa waislamu bila ya haki.

  • Mwandishi : Salah Mohammed Budair

    Uharamu wa kumwaga damu ilio hifadhiwa: Sheikh Swalah Budeir Allah amuhifadhi alitoa khutba katika msikiti wa madina tarehe 3-2-1432 kazungumzia uharamu wa kumwaga damu ikiwa ni muislamu au asie muislamu na akataja dalili zinazo kataza kufanya mambo hayo na akaashiria tukio lililo tokea misri iskandariyya kwa kubomoa kanisa.

  • Kukumbusha neema ya uislamu: katika khutba hii sheikh Allah amuhifadhi amekumbusha neema ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, na neema kubwa ni neema ya uislamu, niwajibu kumshukuru Allah na kushikamana nayo na kumuiga nabii Muhammad (s.a.w), hakika walio tangulia hawakukubali dini nyingine zaidi ya uislamu, kisha sheikh akataja mifano ya badhi ya maswahaba walio adhibiwa katika njia ya Allah ili warejee katika ukafiri lakini hawakukubali.

  • Huu ndio Uislamu kwa ufupi: Maneno mafupi na yenye kuenea kuhusu maana ya Dini ya Uislamu na misingi yake na nguzo zake, na mema yake na makusudio yake. kwa hakika ni funguo kwa mwenye kutaka kuufahamu Uislamu, au kuingia.

  • Njia ya Mtume (s.a.w), katika mambo yote kwa ujumla kwa kulinda heshima ya uislamu, na kuusafisha na kuutakasa kutokana na maneno yanayo weza kuuchafuwa na kuuweka dosari haliyakuwa uislamu upo mbali kabisa, na hii njia ya Mtume (s.a.w), ipo wazi kabisa kwa kila atakae zingatia historia yake nzuri, na katika makala hii yametajwa badhi ya maswali kuhusu mada hiyo. makala haya yamesambazwa katika gazeti la (sharqi ausatw) namba 10696 siku ya J/nne 3/3/1429هـ

Ukurasa : 1 - Kutoka : 1
Maoni yako muhimu kwetu