Shekh Ally Zuberi: Amemaliza masomo yake kitengo cha Hadith katika Chuo kikuu cha kiislamu Madina nchini Saudi Arabia. Kwa sasa ni mlinganiaji katika Mkoa wa Tanga na ni khatwib katika Msikiti wa Darul Uluum, pia ni Mudiri wa chuo cha Darul Uluum Tanga Tanzania.-
Shekh Al-Amin Ally Rajab amehitimu masomo katika chuo cha Maahad kisauni mombasa enya, na nimlinganiaji kenya na ni khatwibu katika msikiti wa Yusuf tudor Mombasa Kenya.
Arafat Magmoud amesoma katika chuo cha Kisauni College akapata Degree katika masomo ya kiislam, ni khatwibu katika kituo cha Ibn Taymiya na nimlinganiaji katika visiwa vya Zanziba.
Shekh Abuu Anasi Bwaluka ni katika walinganiaji wa Ahlusuna waljamaa katika nchi ya Tanzania na nikhatwibu katika msikiti wa Answari Kilimanjaro moshi Tanzania.
Shekh Abuu Hashim Abdulqaadir amesoma katika chuo kikuu cha kiislam Madina na nimwalimu katika markazi Tawhiid na Madrasatul Al-Munawara Mombasa Kenya na nikhateibu katika masjid mula Mombasa Kenya.
Shekh Abuu Musa Abubakari Musa Kiza amehitimu masomo katika chuo cha Maahad Kisauni Mombasa Kenya nanikatika walinganiaji katika mkoa wa Tabora na nirais katika kituo cha kislam Kaloleni Tabora.
Swaleh Al-Zahran amemaliza masomo katika chuo cha Imamu muhamad bi saud University na ana juhudi za Daawa africa mashariki.
سواحيلي
مؤلف,عدد العناصر : 2
Hasan Muhammad Swalih: Ni msomaji Mmisri amezaliwa sehem iitwayo Mahmudiyyah katika mji wa Buheyrah, amehitimu masomo katika Maahad, na akasoma elimu ya visomo kumi, na akajiunga na kitivo cha elimu ya Qur'an, nae ni Imamu katika Markaz ya kiislam katika mji wa New York
Shekh Salim Bafadhili: Ni naibu Mudiri katika taasisi ya Answar, na ni mwalimu katika chuo cha Maahad Imamu Shafii na Ummu Salama, pia ni mlinganiaji katika misikiti ya yote ya Answar Tanga Tanzania.
-Shekh Saidi Mtatuu Mango: Ni mwanafunzi katika Chuo kikuu cha kiislamu cha Imamu Muhammad Bin Soud Nchini Saudi Arabia. Pia ni mlinganiaji katika mji wa Singida.
Sheikh Hamza Rajabu Seyfu ni mmoja katika walinganiaji wa mji wa Mwanza nchini Tanzania kamaliza chuo kikuu nchini Saudi arabia kitengo cha Sheria (Usuluddin) ni Imamu na khatwibu katika masjid Taqwa jijini Mwanza yupo katika manhadi ya salafu sswaleh.