Msomaji Abdul Razak bin Abtan Dulaimi: msomaji wa asili ya Iraq, kajitahidi katika utekelezaji wa usomaji wa Quran tukufu, na amesajili nakala kadhaa za Qur'ani.
Abdurahmani bin Abdallah Al-Suhaym kazaliwa katika kijiji cha Basra katika mji wa Burayda Qswim, amehitimu katika Imamu muhamad bin saud islamic University, anafanya kazi ya Daawa chini ya wizara ya mambo ya kiislam na Daawa. (The Ministry of Islamic Affairs, Endowments, Call and Guidance).
Shekh Muhmmad Sharifu Famau: Alikua ni mlinganiaji maarufu nchini Kenya, pia alikua ni Mudir katika Madrast Tawhid mpaka alipofariki dunia katika mji wa Malindi nchini Kenya, Allah amsamehe na amrehem, Ameen!.-
Shekh Ahmad Al Zahran: Ni Muhadhir katika Chuo kikuu cha kiislamu cha Imamu Muhammad Bin Soud Nchini Saudi Arabia. Pia ni mkuu wa Da’awa katika taasisi ya World Assembly of Muslim Youth (WAMY) kwa nchi ya Tanzania, na anafanya kazi katika maktaba ya Jariyat Badia, Rayadh Saudi Arabia.
-Shekh Salim Qahtwani: Amemaliza masomo yake ya Dini nchini Sudan, kwa sasa ni mlinganiaji kupitia chanel ya Tv Afrika na ni khatwib ktika Misikiti ya Answar Tanga, pia ni mwalimu katika Maahad Imamu Shafii na Ummu Salama, Tanga Tanzania.
Shekh Muharam Idrisa Mwita: Amemaliza masomo yake katika kitengo cha sheria katika Chuo kikuu cha kiislamu cha Imamu Muhammad Bin Soud Nchini Saudi Arabia. Pia ni mlinganiaji kupitia chanel ya Tv Afrika na ni msimamizi wa lugha ya kiswahili katika Tv Afrika.-