Shekh Zuberi Athumani: Amemaliza masomo yake katika kitengo cha sheria katik Chuo kikuu cha kiislamu cha Imamu Muhammad Bin Soud Nchini Saudi Arabia. Na ni mlinganiaji maarufu nchini Burundi, pia ni khatwib katika Msikiti wa barabara ya saba Bujumbura Burundi.-
Sheikh: Zaidi Bashiri ni mmoja katika walinganiaji wa kisunna mwenyeji wa Mombasa Kenya pia ni mwanafunzi wa Sheikh: Abdallah Al-farisi Mfasiri wa Qur’ani tukufu kwa lugha ya kiswahili, nimtowaji wa mawaidha kwanjia ya Ahlu sunna wal-jamaa.
Shekh Nassor Abdallah Bachu: Alikua ni mlinganiaji maarufu nchini Tanzania, na alikua akitoa Darsa katika misikiti mbalimbali ndani na nje ya visiwa vya Zanzibar, pia alikua ni Imamu na Khatwib katika Msikiti wa Rahaleo Zanzibar mpaka anafariki dunia, Allah amsamehe na amrehem, Ameen!.-
-Shekh Salim Qahtwani: Amemaliza masomo yake ya Dini nchini Sudan, kwa sasa ni mlinganiaji kupitia chanel ya Tv Afrika na ni khatwib ktika Misikiti ya Answar Tanga, pia ni mwalimu katika Maahad Imamu Shafii na Ummu Salama, Tanga Tanzania.
Shekh Muharam Idrisa Mwita: Amemaliza masomo yake katika kitengo cha sheria katika Chuo kikuu cha kiislamu cha Imamu Muhammad Bin Soud Nchini Saudi Arabia. Pia ni mlinganiaji kupitia chanel ya Tv Afrika na ni msimamizi wa lugha ya kiswahili katika Tv Afrika.-
Shekh Ahmad Al Zahran: Ni Muhadhir katika Chuo kikuu cha kiislamu cha Imamu Muhammad Bin Soud Nchini Saudi Arabia. Pia ni mkuu wa Da’awa katika taasisi ya World Assembly of Muslim Youth (WAMY) kwa nchi ya Tanzania, na anafanya kazi katika maktaba ya Jariyat Badia, Rayadh Saudi Arabia.