معلومات المواد باللغة العربية

Abubakari Shabani Rukonkwa - Audios

Idadi ya Vipengele: 83

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia: Uzito wa dhambi ya uzinifu na kwamba ni katika madhambi makubwa yenye kuangamiza, pia imezungumzia makatazo ya Allah juu ya uchafu wa zinaa na kuto kuikaribia zinaa, pia amezungumzia nyumba za zinaa. 2- Mada hii inazungumzia: sifa za watu wema na adhabu za wazinifu, kisha amebainisha madhambi makubwa, kisha akataja kuwa kuikurubia zinaa niharamu na nitabia mbaya. 3- Mada hii inazungumzia: Sababu za uzinifu miongoni mwa sababu hizo nikuviachia viungo na kuto kuweka mipaka katika kuishi na wanawake, nakuto kuinamisha macho na ndimi, sababu ya pili nikuzurura na wanawake na kuongozana nao. 4- Mada hii inazungumzia: Dhambi za uzinifu na sababu zake sababu ya tatu nikupeyana mikono na kugusana, na amezungumza uzito wa dhambi ya kumshika mwanamke asie halali kwake, pia ametaja sababu zinazo pekelea kugusana, sababu ya nne nikuingia katika sehemu za wanawake. 5- Mada hii inazungumzia: Sababu za uzinifu miongoni mwa sababu hizo ya tano nikukaa faragha mwanamume na mke ila akiwa nimahrim, katika faragha nikurejea masomo wanawake na wanaume katika vyuo na mashule, na katika kuchumbiyana, kisha amezungumza uwezo wa mwanamke katika kumpa mtihani mwanamume.

  • Kiswahili

    • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu katika uislam amezungumzia maana ya haki na umuhimu wa kujuwa haki za binadamu na ulazima wa kuzilinda, pia ametaja haki tano katika Quraan kwa ujumla. • Mda hii inazungumzia: maana ya binadamu na maana ya uislam, na ametaja mafundisho ya uislam kuhusu haki za binadamu. • Amezungumza kuwa uislam ndio wakwanza kufundisha haki za binadam, Haki ya kwanza (Haki ya kuishi). • Mada hii inazungumzia: Uharam wa kujiua na niharam kutumia kitu ambacho kitamsababishia kifo, kama kuvuta sigara na pombe nk, pia amezungumzia haki ya pili (Kulinda mali za watu) na uharam wa kudhulumiana. • Mada hii inazungumzia: Uharam wa kudhulumiana na chanzo chake, pia amezungumzia uharam wa kula riba na njama za nchi zilizo endelea katika kula riba, pia kazungumzia uharam wa kula rushwa, na dhulma nimaradhi yanayo ambukiza. • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu ikiwemo mwanamke kuheshimiwa utu wake, amebainisha hali ya mwanamke kabla ya uislam, na jinsi uislam ulivyo linda heshima ya mwanamke, kabainisha jinsi mwanamke anavyo dhalilisha mwanamke katika karne ya 21. • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu ikiwemo haki ya kuabudu, na amebainisha kuwa hakuna kulazimishana, kasha akataja hali ya ulinganiaji wakati wa mtume na uongo wa wale wanao sema uislam ulienezwa kwa upanga, bali uislam uliingia kwa hoja zenye nguvu. • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu nayo nihaki ya mwanadamu kuwa huru, na msingi wa uhuru wa binadamu, ambayo inatolewa katika maneno ya Omar bin Khatwabi (r.a).

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia:Fadhila za kutawadha, ikiwemo kuwa na Nuru kwa mwenye kutawadha, pia miongoni mwa ubora wa Udhu nikufutiwa madhambi yake.na kwamba udhu ni silaha kwa Muumini.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kufanya bidii katika kutafuta elimu, na kuutumia wakati katika kujisomea fani tofauti, na kuto tosheka na masomo ya darasani.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Mambo mawili yanayomkinga mwanadam na adhabu za Allah, na imezungumzia pia masharti ya toba.

  • Kiswahili

    Anuwani ya mada hii ni Misingi ya da’awa ya kweli, pia inazungumzia: Umuhimu wa elimu na maoni ya watu katika kutengeneza umma wa kiislam.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Daraja za jihadi, ni wakati gani jihadi inakuwa ni lazima, vievile inazungumzia maneno ya wanachuoni kuhusu jihadi.

  • Kiswahili

    Anuwani ya mada hii ni: Hijabu ya kisheria na Nasaha kwa wanawake.shekh amezungumzia Sharti za Hijabu,na umuhimu wa kushikamana na dini kwa wakina mama.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia msimamo wa Uislam kuhusu kuhusu kupigana Jihadi katika njia ya Allah, na upambanuzi wake, na tatizo la waislam wengi kuto fatilia mambo kwa kina, na madhara ya Hamasa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia aina za jihadi,akasema shekh kuwa jihadi ina aina mbili :Jihadiya kujitetea, na Jihadi ya ilio tangazwa na Kiongozi.

  • Kiswahili

    Maana ya Aibu pila ameeleza kua Allah anazijua siri zetu, kisha ameeleza udhaifu wa mwanadamu na tabia za watu katika kusema aibu za wenzao, na tiba ya maradhi ya kutangaza aibu za watu.

  • Kiswahili

    Mada hii inaelezea nafasi ya nia katika ibada, ameeleza maana ya nia na mahala pake katika ibada na jinsi ya uweka nia katika ibada.

  • Kiswahili

    1. Mada hii inaelezea: Maana ya kusengenya (Umbeya) na kwamba ni katika madhambi makubwa, kisha amebainisha sifa za watu wenye umbeya, na kwamba nimtu washari, na ataadhibiwa katika kaburi lake. 2. Mada hii inaelezea hatuwa za kufanya katika kutibu maradhi ya Umbeya, na katika hatuwa hizo ni kuthibitisha habari unazo zipata, kisha akaeleza kuwa waganga wa kienyeji(Washirikina) na wachawi nikatika wanao ongoza kwa kusengenyaji(Umbeya).

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Maada ya pombe na hukumu ya kutumia na kuuza pombe, kisha amebainisha kuwa madawa ya kulevya ni katika yana hukumu ya pombe, na ameelezea madhara ya madawa ya kulevya kiafya kidini na kijamii na kwamba pombe ni mama wa Machafu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia sababu za kupata mali, miongoni mwa sababu hizo: Ni Uchamungu, na ukweli katika maneno na vitendo na katika niya yake, hiyo nisababu ya kutengamaa mambo yote.

  • Kiswahili

    1. Mada hii inazungumzia Umuhimu wa kuwa mchamungu na hasara za kukosa uchamungu kisha akaelezea kuwa Mwaka mpya nimwaka wa kuihesabu Nafsi. 2. Mada hii imezungumzia ufupi wa umri wa mwanadamu, nakwamba ameumbwa kutokana na masiku, kisha akabainisha kuwa katika kuihesabu nafsi nikujuwa mema aliyo yafanya, na kwamba kuikaguwa nafsi nikatika alama ya Uchamungu. 3. Mada hii inazungumzia miongoni mwa kuihesabu nafsi ni kuihesab nafsi na kujuwa chanzo cha uovu wake, na kwanini inapata uzito wa kuswali! Kisha amezungumzia umuhimu wa kujuwa uhalali na uharamu wa vyakula vyetu, na kwamba mtu asie swali nikafiri. 4. Mada inazungumzia Miongoni mwa kuihesabu nafsi nikutekeleza ibada ya swala, na familia yote, na kwamba swala ndio funguo za rizki, kisha ameeleza hali ya watu na swala zao pindi wanapo safiri zao, pia ameleza umuhimu wa kuhesabu mali ili kuzitolea zaka.

  • Kiswahili

    1. Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa Uchamungu, na maana ya khutbatu Alhaja, kisha akabainisha swala ya khusufu na Malengo ya khusufu. 2. Mada hii inazungumzia: Fursa ya kuyafikiwa na masiku bora duniani, kisha ametaja miezi mitukufu, na akaeleza ubora wa masiku hayo, na ubora wa siku ya Arafa. 3. Mada hii inazungumzia: umuhimu wa kufunga siku ya arafa, na mambo anayo takiwa afanye katika masiku kumi ya mfungo tatu. 4. Mada hii inazungumzia:miongoni mwa matendo mema katika masiku kumi ya mfungo tatu, na amebainisha ubora wa kutowa salam, Kuunga udugu na kuwafanyia wema wazazi, na kuchunga haki za mume na mke.

  • Kiswahili

    1. Mada hii inazungumzia khutba ya mkosi na sababu ya kuitwa hivyo pia amezungumzia vitisho vya siku ya Qiyama. 2. Mada hii inakamilisha mada iliyo pita imeelezea hali za watu wamotoni na vyakula vyao na nguo zao, pia mezungumzia maneno ya shetani atakayo zungumza motoni.

  • Kiswahili

    Silsila ya mada za sauti za Tarjama ya Quran tukufu kwa lugha ya kiswahili inayo itwa "Al Muntakhab Fi Tafsir Al Qur’an" iliyo fanywa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani tafsiri hii inasifika kwa ufasaha wa lugha, masahafu huu umekusanya sauti ya msomaji wa Quraan, na sauti ya anaesoma tarjama ya kiswahili.