معلومات المواد باللغة العربية

Abubakari Shabani Rukonkwa - Audios

Idadi ya Vipengele: 83

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia: Baadhi ya sababu za Muislam kuharakisha kuitekeleza ibada na nguzo ya Hajji, yakwanza nikuharakia kutumia nafasi ya kuwa na uwezo, sababu ya poli nikwamba hujuwi utakufa lini, pia amezungumzia sababu batili wanazo towa wasio taka kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni umuhimu na ubora wa ibada hiyo, pia imezungumzia umuhimu kwa muislam kukimbilia jambo la kheri 3- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba Hijja ni sababu ya kusamehewa madhambi yote, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga na kuhifadhi matendo ya Hijja 4- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba malipo ya Allah kwa mtu aliyefanya ibada ya Hijja ni Pepo, pia imezungumzia ubora wa neema ya Pepo ya Allah.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Ufalme wa Allah na kwamba anachukia pindi unapo acha kumuomba, na nahakika mwanadamu anapo ombwa anachukia, na anampa kila mwenye kumuomba na Allah ndio mmiliki wa mbingu na ardhi.

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia: makatazo ya kuudhiana waislam na kwamba wanao muudhi Allah na Mtume wake (s.a.w) wana laana kubwa, pia imezungumzia aina mbili za maudhi ambayo ni maudhi ya maneno na vitendo. 2- Mada hii inazungumzia: Hatari ya madhambi na maudhi ya kusengenya na kwamba hao ndio wanaokula nyama za watu, pia imezungumzia maudhi ya vitendo kama vile kumuudhi jirani kwa kutumia vyombo vya kileo na kutia uchafu katika katika njia.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia saa ya kujibiwa dua ambayo inapatikana siku ya ijumaa, amebainisha wakati huo, na pindi mtu anaposhtuka usingizini akiwa amelala na udhu, na baina ya Adhuhuri na Asri siku ya ijuma tano

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia umuhimu wa kuandaa darsa kwa wanawake, kwasababu ndio wengi motoni, na ametaja sababu za kuwa wengi motoni, kasha amehusiya watu wahifadhi ndimi zao. 2- Mada hii inazungumzia sababu ya wanawake kuingia motoni kama kulani sana na kukataa wema wa mume wake, ametaja jinsi mwaname anavyo shawishika katika zama hizi, kisha amezungumzia maana ya ugeni katika dini . 3- Mada hii inazungumzia baadhi ya mifano kwa wanawake walio pata mateso lakini wakathibiti katika dini, kama Mwanamke aliekuwa anafanya kazi ya kuwasuka mabinti wa Firauni, na mke wa Firauni amehimiza umuhimu wa kuithamini Dini. 4- Mada hii inazungumzi halia za wanawake wa kiislam na udhaifu wao katika ibada nakudai kwao haki sawa, na baadhi ya hoja dhaifu katika kuvaa hijabu, kisha akabainisha umuhimu wa mwanamke wa kiislam kushikamana na dini. 5- Mada hii inazungumzia tabia ya kusengenya wanawake, na uharamu wake, na uwajibu wa kuhifadhi ndimi, kisha akataja kuwa mwanamke atakaeshikamana na dini atakuwa peponi na familia yake.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, ubora wake, nakwamba Allah anashuka na kuwasogelea kwa waliosimama katika viwanja vya Arafa, na Allah anajifakhari kwa malaika, na yanayo takiwa kufanywa nawale ambao hawako katika viwanja vya Arafa.

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, maana yake na umuhimu wa kuomba dua katika siku hiyo, na amejibu kuhusu utata juu ya siku ya arafa na siku ya Iddi al Adhha nawale wasiofunga siku ya arafa bali wanafunga siku ya kuchinja. 2- Mada hii inazungumzia Majibu ya utata wa Arafa na hijja, amebainisha kuwa hija ilikuwepo tangu wakati wa nabii Ibrahim haikuwa faradhi, amefafanua mafungaamano ya Arafa na mwezi Dhulhijah, na Arafa ya mtu wa China na Est Africa, na mafungamano ya swala ya iddi na kupiga mawe na kuchinja kwa mahojaji . 3- Mada hii inazungumzia Majibu ya utata wa Arafa na hijja, amebainisha kuwa watu wanafuata mahujaji katika takbira, na kuchinja ili wafuate watu wa mina, na ametaja Qauli za wanachuoni kuhusu mafungamano ya hija na matendo ya wasiokuwa mahujaji.

  • Kiswahili

    1- Khutuba ya Iddi amezungumzia neema ya kuwa na uongofu nakufikishwa katika mwezi wa Ramadhan, na wepesi wa kumalizika umri, na kwamba Ramadhani nishule, na malengo ya swaumu niuchamungu, na kulifikia lengo hilo nikufanya mema baada ya Ramadhani. 2- Khutuba ya Iddi amezungumzia sababu za kufuata makundi yalio potea na fikra potovu nikuto kuisoma elimu ya dini, na kukosa malezi bora kwa mtoto, na wazazi kuwatupa watoto wao, Na kuinusuru dini nikuisoma dini, pia ametaja adabu za Iddi

  • Kiswahili

    1- Makala hii inazunguzia:Maana ya Iddi na neema ya Idd ya kiislam na historia yake, faida za Iddi na umuhimu wa kumfuata mtume katika katika kufunga na nakufungua na kusherehekea Iddi. 2- Makala hii inazunguzia:Chanzo cha siku za Iddi, nakwamba Iddi ilikuja kufuta siku kuu za kijinga, ameleza kuwa siku za Iddi zimewekwa kwalengo la kumtukuza Allah. 3- Makala hii inazunguzia:Adabu za kusherehekeya sikukuu za Iddi, ikiwemo kumtii Allah, na kusimamisha swala na kuwatembelea wagonjwa, nakuwafanyia wema majirani . 4- Makala hii inazunguzia: Mambo yanayo takiwa kuachwa katika siku za Iddi, ikiwemo kujiepusha na madhambi, na kujiepusha na miziki, na wanawake kutembea uchi nk.

  • Kiswahili

    Makala hii inazunguzia: Sababu za ugomvi katika ndoa amezungumzia sababu ya magomvi nikukosekana elimu ya ndoa kabla ya kuoa, pia amezungumzia haki za mke kwa mume wake.

  • Kiswahili

    Makala hii inazunguzia:Mambo manne mwenye kuyafanya yote kwa ujumla atapata pepo, miongoni mwa mambo hayo ni kufunga na kutoa sadaka na kumtembelea mgonjwa…

  • Kiswahili

    Makala hii inazungumzia:Ubora wa mwezi mtukufu wa ramadhani, pia amezungumzia Ubora wa laylatul Qadri na kuteremshwa Quraan. Pia kahusia umuhimu wa kufanya towba Makala hii inazungumzia: makatazo ya kuutangulia mwezi wa Ramadhan ila mwenye nadhiri, pia amezungumzia uwajibu wa kufunga pindi mwezi unapo onekana, na sharti za kukubaliwa mwezi wa shawali .

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swaumu ikiwemo kuzungumza katika swala, na kucheka, na kula katika swala, pia amezungumzia mambo ambayo yanaweza uharibu swala. Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swala, ikiwemo kunywa katika swala na kuonekana uchi katika swala, amezungumzia mambo yanayo pelekea kuonekana uchi kwa wanaume na wanawake katika swala.

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia zawadi ya kumi la mwisho katika mwezi wa Ramadhani, amebainisha maana ya Suratul Qadri, na amebainisha aina ya mipangilio ya Allah kwa mwaka mzima, pia amezungumzia zawadi za ramadhani ikiwemo usiku wa cheo na ziyara ya malaika Jibril . Mada hii inazunguzia zawadi ya kumi la mwisho katika mwezi wa Ramadhani, miongoni mwa zawadi za kumi la mwisho katika mwezi wa ramadhani ni kupewa umri mfupi na ibada chache zenye malipo makubwa, pia amebainisha kuwa miezi 1000 nisawa na kuishi miaka 81 ukiwa katika ibada.

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia Suna za swaumu ikiwemo ubora wa kufungua mapema, na kufturu kwa tende au maji, na kuchelewesha daku.

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia Nguzo za swaumu ikiwemo Nia ambayo mahala pake nimoyoni, pia kujuwa wakati wa kufunga tangu kutoka Alfajiri mpaka kuzama jua, na kujiziwiya na vitu vinavyo funguza .

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia Namna ya kuitafuta lailatul Qadri, amezungumzia umuhimu wa kuitafuta lailatul Qadri na ubora wake, na ubora wa Ummat Muhammad, na malipo ya atakae pata usiku huo, na malipo ya mwenye kuitafuta lailatul Qadri. Mada hii inazunguzia Namna ya kuitafuta lailatul Qadri, amezungumzia ibada ambazo anatakiwa kuzifanya muislam anaetafuta lailatul Qadri, na muda wa kuanza kuitafuta lailatul Qadri, miongoni mwa matendo hayo ni kusoma Quraan na kuhuyisha usiku.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Namna za kuhama katika uislam, kabainisha maana ya kuhama sifa za maswahaba wa Madina na wale walio hama kutoka Makkah kwenda madina,na sababu ya kuhama.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: mambo matatu yanayo mfuata maiti baada yakufa ikiwemo watu wake na mali yake na matendo yake, vyote vitarudi ila matendo yake, hakika matendo mazuri ndio rafiki yako kaburini.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Kufaulu kukubwa na maana yake, na aina za kufaulu, na kufaulu duniani na Akhera, na mambo yanayo ufanya uwe miongoni mwa walio faulu.