• Kiswahili

  Mhadhiri : Arafat Magmoud Kurejea : Yasini Twaha Hassani

  1- Mada hii inazungumzia: Neema za nyumba na faidazake, nakwamba nyumba niukamilifu wa neema za Allah kwa waja wake, pia imezungumzia baadhi ya faida za nyumba kama vile makazi, stara, kulala, ibada ya swala na ibada ya ndoa. 2- Mada hii inazungumzia: Nyumba ni sehem ya kumstiri mwanamke na kumlinda na swala iliyo bora kwa mwanamke ni nyumbani, na wanawake wema ni wale wenye kutulia majumbani mwao, pia imezungumzia umuhimu wa kuwafundisha dini na adabu wake na watoto katika majumba. 3- Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kuwafundisha wanawake na watoto mambo ya Sunna na mavazi ya stara ili kuepuka masuuliya siku ya Qiyama, pia imezungumzia ubora wa kulazimiana na nyumba na kutenga muda kwa ajili ya kumtaja Allah ili kuepukana na fitna. 4- Mada hii inazungumzia: Nyumba ni nyenzo kubwa ya kujenga jamii ya kiislam na kutoa wanachuoni pamoja na wanawake wema, pia imezungumzia umuhimu wa mzazi kuwaombea dua ya kheri wanae.

 • Kiswahili

  1- Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa Hija na kwamba (Alqaaba), na ameeleza kuhusu Maqamu Ibrahima, pia imezungumzia namna ilivyojengwa Alqaaba na chanzo cha kuswali rakaa mbili nyuma ya maqamu Ibrahima. 2- Mada hii inazungumzia: Ubora na umuhimu wa kuhiji katika nyumaba ya Allah Tukufu na kwamba ndiyo nyumba ya kwanza iliyo wekwa na Allah kwa ajili ya ibada, pia imebarikiwa na Allah na ni uongofu kwa waja. 3- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa alama zilizo wazi katika nyumba ya Allah Hajarul-as’wad na kwamba mwazo lilikua jeupe lakini limebadilika kuwa jeusi kutoka na madhambi ya watu kama alivyo lielezea Mtume (s.a.w).

 • Kiswahili

  1- Mada hii inazungumzia: Hijja ni wajibu kwa Muislam ambaye ni baleghe mwenye akili mwenye uwezo tena mukalafu aliye huru, pia imezungumzia hasara ya mtu mwenye uwezo kisha akafa bila ya kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Uzembe unaofanywa na baadhi ya waislam wenye uwezo katika kuitekeleza Hija na kwamba ni hasara kubwa kwa watu kama hao, pia imezungumzia kuwa hija ni mara moja tu katika umri

 • Kiswahili

  1- Mada hii inazunguzia: Umuhimu na nafasi ya Hijja katika Uislam na kwamba Hijja ni wajibu na inatekelezwa kwa ajili ya Allah peke yake, pia imezungumzia ruhusa aliyoitoa Mtume (s.a.w) ya kumfanyia Mzazi Hijja. 2- Mada hii inazunguzia: Umuhimu wa hija na umuhimu wa kuwafanyia hija wazazi walio fariki, na kuwafanyia wema wazazi kwa kuwawekea waqfu, na amezungumzia nyakati za hijja pia amebainisha ubora wa kuhiji ukiwa kijana.

 • Kiswahili

  Mada hii inazunguzia: Ubora wa kutia nia thabiti katika safari ili kupata malipo ya safari na malipo ya ibada ya Hijja, pia imezungumzia miongoni mwa sunna za safari kama vile kusoma dua mwanzo na mwisho wa safari kama alivyo fundisha Mtume (s.a.w)

 • Kiswahili

  Mada hii inazungumzia: Aina tatu za ibada ya Hijja ambazo ni Tamatu’u, Kiran na Ifrad, pia imefafanua namna ya kutekeleza ibada hizo.

 • Kiswahili

  Mada hii inazungumzia: Haifai kwa mwanamke kusafiri peke yake kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hajji mpaka awe na mahram nao ni Baba, babu, watoto, mume nk. pia imezungumzia hadhi na heshima ya mwanamke

 • Kiswahili

  Mada hii inazungumzia: Mipaka aina tano maalum ya Hijja na Umra, na yanayostahiki kufanywa sehem hizo, pia imezungumzia kafara ya mtu aliyepita Mi’qat bila ya kuhirimia au kuvaa ihram

 • Kiswahili

  Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kutekeleza ibada ya Hijja na kwamba ni miongoni mwa ibada bora na nguzo ya tano ya Uislam, pia imezungumzia yanayofanya Hijja iwe sahihi ikiwemo kujifunza utaratibu wa Hijja, ikhlasi na kufuata sunna za Mtume (s.a.w)

 • Kiswahili

  Mhadhiri : Swalehe Ibrahim Kurejea : Yasini Twaha Hassani

  1- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu zinazo pelekea nyoyo za watu kuwa ngumu, ni watu kuzama ktika maasi kama vile uzinifu, ulevi, kutembea uchi na kuchanganyika wanaume na wanawake, pia imezungumzia sababu za bani Israil kuwa na nyoyo ngumu na kulaaniwa. 2- Mada hii inazungumzia: Waumini wa kweli kwamba ni wale ambao wanaposikia Aya za Allah nyoyo na ngozi zao zina sisimka, pia imeelezea umuhimu wa kusikiliza maneno ya Allah na kuyazingatia

 • Kiswahili

  Mhadhiri : Swalehe Ibrahim Kurejea : Yasini Twaha Hassani

  1- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa alama za Qiyama ni pindi itakapo potea amana na atakapo pewa majukum mtu asiyefaa basi subirini Qiyama, pia imezungumzia umuhimu wa kuchagua viongozi wanao faa 2- Makala hii inazungumzia: Madhara ya kutegemeza majambo kwa wanawake na watu wajinga wasio na elimu basi umauti ni bora kuliko kuishi, pia imeelezea hatari za ubakhili.

 • Kiswahili

  1- Makala hii inazunguzia:Maana ya Iddi na neema ya Idd ya kiislam na historia yake, faida za Iddi na umuhimu wa kumfuata mtume katika katika kufunga na nakufungua na kusherehekea Iddi. 2- Makala hii inazunguzia:Chanzo cha siku za Iddi, nakwamba Iddi ilikuja kufuta siku kuu za kijinga, ameleza kuwa siku za Iddi zimewekwa kwalengo la kumtukuza Allah. 3- Makala hii inazunguzia:Adabu za kusherehekeya sikukuu za Iddi, ikiwemo kumtii Allah, na kusimamisha swala na kuwatembelea wagonjwa, nakuwafanyia wema majirani . 4- Makala hii inazunguzia: Mambo yanayo takiwa kuachwa katika siku za Iddi, ikiwemo kujiepusha na madhambi, na kujiepusha na miziki, na wanawake kutembea uchi nk.

 • Kiswahili

  Makala hii inazunguzia: Sababu za ugomvi katika ndoa amezungumzia sababu ya magomvi nikukosekana elimu ya ndoa kabla ya kuoa, pia amezungumzia haki za mke kwa mume wake.

 • Kiswahili

  Makala hii inazunguzia:Mambo manne mwenye kuyafanya yote kwa ujumla atapata pepo, miongoni mwa mambo hayo ni kufunga na kutoa sadaka na kumtembelea mgonjwa…

 • Kiswahili

  Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swaumu ikiwemo kuzungumza katika swala, na kucheka, na kula katika swala, pia amezungumzia mambo ambayo yanaweza uharibu swala. Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swala, ikiwemo kunywa katika swala na kuonekana uchi katika swala, amezungumzia mambo yanayo pelekea kuonekana uchi kwa wanaume na wanawake katika swala.

 • Kiswahili

  Mada hii inazunguzia Hukumu ya mtu asie swali kabainisha Qauli mbili za wanachuoni kuhusu mtu asie swali, na ametaja dalili nyingi za ukafiri wa asie swali, na amebainisha kuwa swala ninguzo ya dini, asie swali ameivunja dini. Mada hii inazunguzia Hukumu ya mtu asie swali, amebainisha hukumu ya mtu anae sahau swala zake, na mafikio yao siku ya Qiyama, na amebainisha umuhimu wa swala na swala ndio itakayo anza kuhesabika siku ya Qiyama.

 • Kiswahili

  Mada hii inazunguzia Suna za swaumu ikiwemo ubora wa kufungua mapema, na kufturu kwa tende au maji, na kuchelewesha daku.

 • Kiswahili

  Mada hii inazunguzia Nguzo za swaumu ikiwemo Nia ambayo mahala pake nimoyoni, pia kujuwa wakati wa kufunga tangu kutoka Alfajiri mpaka kuzama jua, na kujiziwiya na vitu vinavyo funguza .

 • Kiswahili

  Mada hii inazunguzia Namna ya kuitafuta lailatul Qadri, amezungumzia umuhimu wa kuitafuta lailatul Qadri na ubora wake, na ubora wa Ummat Muhammad, na malipo ya atakae pata usiku huo, na malipo ya mwenye kuitafuta lailatul Qadri. Mada hii inazunguzia Namna ya kuitafuta lailatul Qadri, amezungumzia ibada ambazo anatakiwa kuzifanya muislam anaetafuta lailatul Qadri, na muda wa kuanza kuitafuta lailatul Qadri, miongoni mwa matendo hayo ni kusoma Quraan na kuhuyisha usiku.

 • Kiswahili

  1- Mada hii inazungumzia jinsi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kusafisha moyo na machafu na kuwasamehe walio tukosea, pia miongoni mwa mapokezi ya Rmadhani ni kuisoma Fiqhi ya swaumu. 2- Mada hii inazungumzia jinsi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kujitwaharisha na shirki na kuwaidhika kutokana na maumbile ya mwanadamu, na maradhi yanayo wapata wanadamu, pia amezungumzia umuhimu wa kuhifadhi swala tano. 3- Mada hii inazungumzia jinsi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo uwajibu wa kujihifadhi na najsi katika nguo na mwili na sehemu ya kuswalia, na uhatari wa kuto kuhifadhi na haja ndogo na kuwachonganisha watu.

Ukurasa : 3 - Kutoka : 1
Maoni yako muhimu kwetu