معلومات المواد باللغة العربية

Yasini Twaha Hassani - Audios

Idadi ya Vipengele: 45

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Mipaka aina tano maalum ya Hijja na Umra, na yanayostahiki kufanywa sehem hizo, pia imezungumzia kafara ya mtu aliyepita Mi’qat bila ya kuhirimia au kuvaa ihram

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kutekeleza ibada ya Hijja na kwamba ni miongoni mwa ibada bora na nguzo ya tano ya Uislam, pia imezungumzia yanayofanya Hijja iwe sahihi ikiwemo kujifunza utaratibu wa Hijja, ikhlasi na kufuata sunna za Mtume (s.a.w)

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Swalehe Ibrahim Kurejea : Yasini Twaha Hassani

    1- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa alama za Qiyama ni pindi itakapo potea amana na atakapo pewa majukum mtu asiyefaa basi subirini Qiyama, pia imezungumzia umuhimu wa kuchagua viongozi wanao faa 2- Makala hii inazungumzia: Madhara ya kutegemeza majambo kwa wanawake na watu wajinga wasio na elimu basi umauti ni bora kuliko kuishi, pia imeelezea hatari za ubakhili.

  • Kiswahili

    1- Makala hii inazunguzia:Maana ya Iddi na neema ya Idd ya kiislam na historia yake, faida za Iddi na umuhimu wa kumfuata mtume katika katika kufunga na nakufungua na kusherehekea Iddi. 2- Makala hii inazunguzia:Chanzo cha siku za Iddi, nakwamba Iddi ilikuja kufuta siku kuu za kijinga, ameleza kuwa siku za Iddi zimewekwa kwalengo la kumtukuza Allah. 3- Makala hii inazunguzia:Adabu za kusherehekeya sikukuu za Iddi, ikiwemo kumtii Allah, na kusimamisha swala na kuwatembelea wagonjwa, nakuwafanyia wema majirani . 4- Makala hii inazunguzia: Mambo yanayo takiwa kuachwa katika siku za Iddi, ikiwemo kujiepusha na madhambi, na kujiepusha na miziki, na wanawake kutembea uchi nk.

  • Kiswahili

    Makala hii inazunguzia: Sababu za ugomvi katika ndoa amezungumzia sababu ya magomvi nikukosekana elimu ya ndoa kabla ya kuoa, pia amezungumzia haki za mke kwa mume wake.

  • Kiswahili

    Makala hii inazunguzia:Mambo manne mwenye kuyafanya yote kwa ujumla atapata pepo, miongoni mwa mambo hayo ni kufunga na kutoa sadaka na kumtembelea mgonjwa…

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swaumu ikiwemo kuzungumza katika swala, na kucheka, na kula katika swala, pia amezungumzia mambo ambayo yanaweza uharibu swala. Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swala, ikiwemo kunywa katika swala na kuonekana uchi katika swala, amezungumzia mambo yanayo pelekea kuonekana uchi kwa wanaume na wanawake katika swala.

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia Suna za swaumu ikiwemo ubora wa kufungua mapema, na kufturu kwa tende au maji, na kuchelewesha daku.

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia Nguzo za swaumu ikiwemo Nia ambayo mahala pake nimoyoni, pia kujuwa wakati wa kufunga tangu kutoka Alfajiri mpaka kuzama jua, na kujiziwiya na vitu vinavyo funguza .

  • Kiswahili

    Mada hii inazunguzia Namna ya kuitafuta lailatul Qadri, amezungumzia umuhimu wa kuitafuta lailatul Qadri na ubora wake, na ubora wa Ummat Muhammad, na malipo ya atakae pata usiku huo, na malipo ya mwenye kuitafuta lailatul Qadri. Mada hii inazunguzia Namna ya kuitafuta lailatul Qadri, amezungumzia ibada ambazo anatakiwa kuzifanya muislam anaetafuta lailatul Qadri, na muda wa kuanza kuitafuta lailatul Qadri, miongoni mwa matendo hayo ni kusoma Quraan na kuhuyisha usiku.

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia jinsi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kusafisha moyo na machafu na kuwasamehe walio tukosea, pia miongoni mwa mapokezi ya Rmadhani ni kuisoma Fiqhi ya swaumu. 2- Mada hii inazungumzia jinsi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kujitwaharisha na shirki na kuwaidhika kutokana na maumbile ya mwanadamu, na maradhi yanayo wapata wanadamu, pia amezungumzia umuhimu wa kuhifadhi swala tano. 3- Mada hii inazungumzia jinsi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo uwajibu wa kujihifadhi na najsi katika nguo na mwili na sehemu ya kuswalia, na uhatari wa kuto kuhifadhi na haja ndogo na kuwachonganisha watu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Jinsi ya kupata mapenzi ya Allah, shekh amezungumzia njia mbali mbali za kuyapata mapenzi ya Allah, ikiwemo kupewa hekima, na utulivu na amani na kukinai, pia amezungumzia mambo ukiyafanya utapendwa na Allah.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia:Hukumu ya kuutangulia mwezi mtukufu wa ramadhani, na maana ya shaka ilio katazwa kufunga ndani yake, pia kaeleza mwanzo wa kufunga na kufungua, pia kaelezea uwajibu wa kufunga kwa mwezi wa kutangaziwa na waislam.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia:Makosa makubwa wanayo fanya akina mama katika kupeyana mafunzo au misiba au sharia, pia ametaja sifa ya mwanamke ambae ni Dayuth, kisha amezungumzia Umuhimu wa kukumbushana katika Dini.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia:Kifo na mandalizi yake na mafanikio ya mwenye kufanya mema akiwa kaburini, pia kazungumzia maisha mapya kaburini, na uwajibu wa kufanya mema na kuacha maovu

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Baadhi ya makosa katika kuzika, na umuhimu wa kukumbushana na ubora wa kuijufunza ibada na kuisoma, na miongoni mwa makosa katika kuzika nikuweka mto wa maiti, na kufunguliwa sikio na kidole gumba, nakulifanya kaburi pembe nne.

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yasini Twaha Hassani

    Mada hii inazungumzia: Sheria ya kuoa wake zaidi ya mmoja na uadilifu katika kutekeleza haki za wake, na chanzo cha kukataa mke kuongezewa mke wa pili, na msimamo na subra kwa alie ongeza mke wa pili. 2- Mada hii inazungumzia:Utukufu wa ndoa na nasaha muhimu kwa mume katika kuoa, pia ndoa nisheria ya Allah, na pia inazungumzia malengo makuu ya sharia ya kiislam, ikiwemo kuhifadhi kizazi, na hukumu ya kuoa zaidi ya mke mmoja, na hukumu za kisheria katika kuoa wake zaidi ya mmoja.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Mbinu wanazozitumia maadui wa Uislamu lengo ni kuuchafua uislam, lazima watu waisafishe dini ya Allah (S.w), imezungumzia pia ubaya wa kundi la khawarij na uharamu wa kuua au kumwaga damu bila haki.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kuwafanyia wema wazazi wawili na hatari ya kuwaasi, pia ubora wa mke mwenye kuwapenda wazazi wa mumewe, na imezungumzia kisa cha mtu aliyemchinja mzazi wake baada ya muda na yeye akachinjwa na mwanae.

  • Kiswahili

    1-Mada hii inazungumzia:Faida ya malezi mema, na amezungumzia kuwa Allah ndio mwenye kutowa watoto, na amezungumzia misingi ya kupata mototo mwema ikiwemo kuchaguwa mke mwema,na Haki za mtoto baada ya kuzaliwa. 2-Mada hii inazungumzia: Ubora wa kuwasomesha Quraan, na Uhatari wa kutowasomesha watoto dini matokeo yake watoto wanakua hali ya kuwa hawajui yaliyo ya halali wala ya haram mpaka katika ndoa zao. 3-Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa elimu ya dini na Makosa ya wanawake wakati wa nifasi, na mtume kumtuma Muadhi kwenda Yemen ni mfano mwema wa malezi bora. 4-Mada hii inazungumzia: Kuenea kwa dhulma sababu kubwa ni kukosekana malezi mema, pia imezungumzia hatari ya kuvuta sigara na ulevi wa pombe. 5-Mada hii inazungumzia: Njia nne za kumfanya mtoto kuwa mwema, pia imezungumzia maadili na faida alizotufundisha Mtume (S.a.w)