Yunus Kanuni Ngenda - Audios
Idadi ya Vipengele: 62
- Kiswahili
- Kiswahili Mhadhiri : Shamsi Ilmi Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazunguzia namna dunia ilivyo uchanganya umma wa kiislam.
- Kiswahili Mhadhiri : Husseni Saidi Sembe Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii nazungumzia ubora wa elim ya sheria ya Dini ya kiislam, na umuhim kusoma elim nyingine.
- Kiswahili Mhadhiri : Abuu Musa Abubakari Musa Kiza Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
1- Mada hii inazungumzia: Sifa za Ghurabaa waliotajwa na Mtume (s.a.w), kwamba ni wale wanaotengeneza pindi watu wanapo haribu, pia imezunguzia Ghurabaa ni wale wanao shikamana na Manhaji ya Mtume (s.a.w). 2- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sifa za Ghurabaa ni kushikamana na Sunna na kuthibiti katika haki na kujiepusha na mambo ya batili, bid’a na uzushi, pia imezungumzia umuhimu wa kusoma na kuujua uislam.
- Kiswahili Mhadhiri : Abuu Hashim Abdulqaadir Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kuitekeleza nguzo ya Hajj, wanaopaswa kuitekeleza na namna ya kuitekeleza, pia imezungumzia miezi maalum ya Hajj kama ilivyotajwa katika Qur’an tukufu ambayo ni Shawwal, Dhul-Qaada na Dhul-Hijja
- Kiswahili Mhadhiri : Abuu Anasi Bwaluka Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
1- Mada hii inazungumzia: Nafasi ya vijana katika uislam, na neema ya ujana, na kila kijana ataulizwa siku ya qiyama, pia amezungumzia uwajibu wa vijana kuutumia ujana wao katika kufanya ibada, kama kusimamisha Swala, Funga na Hijja, ili kupata radhi za Allah. 2- Mada hii inazungumzia: Vijana ni hazina kubwa katika uislam tangu zamani, nakwamba vijana ndio wenye uwezo wa kuvumilia mashaka na misukosuko, pia imezungumzia umuhimu wa vijana kujipamba na tabia njema.
- Kiswahili Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
1- Mada hii inazungumzia: Maana ya Hijja kilugha na kisheria, na ni nguzo katika nguzo tano za uislam, pia imebainisha kwamba Hijja ni fardhi inatekelezwa mara moja katika umri. 2- Mada hii inazungumzia: Umuhimu kwa mwenye kuhiji kuwa na nia thabiti pamoja na kujikurubisha kwa Allah, pia imezungumzia mambo ya kujifunza katika ibada ya Hijja na tahadhari ya kuiga uzushi. 3- Mada hii inazungumzia: Hijja na Umra na fadhila zake pamoja na alama za mwenye kufanya Hijja ya kweli, pia imezungumzia kwamba Hijja ni fardhi kwa waislam wote wanaume na wanawake. 4- Mada hii inazungumzia: Aina za maandalizi ya Hijja na imefafanua kuhusu Hijja ya mtoto mdogo, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga utaratibu na makatazo baada ya Ihram. 5- Mada hii inazungumzia: Namna Mtume (s.a.w) alivyoruhusu kumuhijia mzazi asiyejiweza kutokana na uzee au ugonjwa, na kwamba inafaa mwanaume kumuhijia mwanamke na mwanamke kumuhijia mwanaume, pia mada hii ina maswali na majibu.
- Kiswahili Mhadhiri : Yasini Twaha Hassani Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
1- Mada hii inazungumzia: Hijja ni wajibu kwa Muislam ambaye ni baleghe mwenye akili mwenye uwezo tena mukalafu aliye huru, pia imezungumzia hasara ya mtu mwenye uwezo kisha akafa bila ya kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Uzembe unaofanywa na baadhi ya waislam wenye uwezo katika kuitekeleza Hija na kwamba ni hasara kubwa kwa watu kama hao, pia imezungumzia kuwa hija ni mara moja tu katika umri
- Kiswahili Mhadhiri : Yasini Twaha Hassani Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
1- Mada hii inazunguzia: Umuhimu na nafasi ya Hijja katika Uislam na kwamba Hijja ni wajibu na inatekelezwa kwa ajili ya Allah peke yake, pia imezungumzia ruhusa aliyoitoa Mtume (s.a.w) ya kumfanyia Mzazi Hijja. 2- Mada hii inazunguzia: Umuhimu wa hija na umuhimu wa kuwafanyia hija wazazi walio fariki, na kuwafanyia wema wazazi kwa kuwawekea waqfu, na amezungumzia nyakati za hijja pia amebainisha ubora wa kuhiji ukiwa kijana.
- Kiswahili Mhadhiri : Yunus Kanuni Ngenda Kurejea : Abubakari Shabani Rukonkwa
1- Mada hii inazungumzia: Baadhi ya sababu za Muislam kuharakisha kuitekeleza ibada na nguzo ya Hajji, yakwanza nikuharakia kutumia nafasi ya kuwa na uwezo, sababu ya poli nikwamba hujuwi utakufa lini, pia amezungumzia sababu batili wanazo towa wasio taka kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni umuhimu na ubora wa ibada hiyo, pia imezungumzia umuhimu kwa muislam kukimbilia jambo la kheri 3- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba Hijja ni sababu ya kusamehewa madhambi yote, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga na kuhifadhi matendo ya Hijja 4- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba malipo ya Allah kwa mtu aliyefanya ibada ya Hijja ni Pepo, pia imezungumzia ubora wa neema ya Pepo ya Allah.
- Kiswahili Mhadhiri : Yasini Twaha Hassani Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazunguzia: Ubora wa kutia nia thabiti katika safari ili kupata malipo ya safari na malipo ya ibada ya Hijja, pia imezungumzia miongoni mwa sunna za safari kama vile kusoma dua mwanzo na mwisho wa safari kama alivyo fundisha Mtume (s.a.w)
- Kiswahili Mhadhiri : Yasini Twaha Hassani Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazungumzia: Aina tatu za ibada ya Hijja ambazo ni Tamatu’u, Kiran na Ifrad, pia imefafanua namna ya kutekeleza ibada hizo.
- Kiswahili Mhadhiri : Yasini Twaha Hassani Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazungumzia: Haifai kwa mwanamke kusafiri peke yake kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hajji mpaka awe na mahram nao ni Baba, babu, watoto, mume nk. pia imezungumzia hadhi na heshima ya mwanamke
- Kiswahili Mhadhiri : Yasini Twaha Hassani Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazungumzia: Mipaka aina tano maalum ya Hijja na Umra, na yanayostahiki kufanywa sehem hizo, pia imezungumzia kafara ya mtu aliyepita Mi’qat bila ya kuhirimia au kuvaa ihram
- Kiswahili Mhadhiri : Yasini Twaha Hassani Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kutekeleza ibada ya Hijja na kwamba ni miongoni mwa ibada bora na nguzo ya tano ya Uislam, pia imezungumzia yanayofanya Hijja iwe sahihi ikiwemo kujifunza utaratibu wa Hijja, ikhlasi na kufuata sunna za Mtume (s.a.w)
- Kiswahili Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
1- Mada hii inazungumzia: Ubora wa mtu kuwa mkeli, na kwamba ukweli ni katika sharti za laa Ilaha ila Lllah, na ukweli ni utulivu wa nafsi bali uongo ni mashaka, pia imezungumzia umuhimu wa kufanya mambo kwa ajili ya Allah. 2- Mada hii inazungumzia: Alama za watu wakweli, kama vile utulivu wa moyo, na kuipa nyongo dunia na kujiepusha na riyaa, na anaeshikamana na Sunna wakati wa fitna, pia amezungumzia maana ya zuhdi. 3- Mada hii inazungumzia: Alama za ukweli nikuficha matendo mema, na kuhisi upungufu katika matendo yake, nakuyafanyia umuhimu na dini yake, na anathibiti kwenye dini wakati wa fitna, na kuikubali haki na kujisalimisha kwenye haki
- Kiswahili Mhadhiri : Swalehe Ibrahim Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
1- Mada hii inazungumzia: Hatari ya kukufuru neema na namna Mwnyezi Mungu alivyo angamiza baadhi ya watu baada ya kukufuru neema za Allah, pia imezungumzia jinsi Mwenyezi Mungu alivyotimiza neema zake juu ya waja wake, neema zilizo wazi na neema zilizo fichika 2- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa neema kubwa ni neema ya Uislam na neema ya kuletwa Mtume Muhammad s.a.w, pia imezungumzia, hatari ya kumuasi Allah ni sababu ya kukosekana kwa Amani, na rizki na kuanguka Uchumi
- Kiswahili Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazungumzia: Mambo yanayoifanya swaumu iwe sahihi na yanayoifanya swaumu kuwa si sahihi, pia imezungumzia umuhimu wa kujiepusha na uongo, kusengenya, na dhulma na vikao vya kipuuzi ndani ya mwezi wa Ramadhani.
- Kiswahili Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazunguzia: Neema ya kufikishwa katika mwezi mtukufu wa ramadhani pia amezungumzia jinsi unavyo ingia mwezi wa ramadhani na kutoka kwake na hali zawatu katika swala la mwandamo wa mwezi na njia sahihi ktika kuthibitisha mwezi. Mada hii inazunguzia: Kuingia kwa Mwezi wa Ramadhan na kutoka kuna njia mbili, njia ya kwanza ni kuonekana kwa mwandamo, na njia ya ya pili ni kutimiza siku thalathini, pia imezungumzia ubora wa kufunga na kufungua siku moja waislamu wote duniani.
- Kiswahili Mhadhiri : Abubakari Shabani Rukonkwa Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda
Mada hii inazunguzia zawadi ya kumi la mwisho katika mwezi wa Ramadhani, amebainisha maana ya Suratul Qadri, na amebainisha aina ya mipangilio ya Allah kwa mwaka mzima, pia amezungumzia zawadi za ramadhani ikiwemo usiku wa cheo na ziyara ya malaika Jibril . Mada hii inazunguzia zawadi ya kumi la mwisho katika mwezi wa Ramadhani, miongoni mwa zawadi za kumi la mwisho katika mwezi wa ramadhani ni kupewa umri mfupi na ibada chache zenye malipo makubwa, pia amebainisha kuwa miezi 1000 nisawa na kuishi miaka 81 ukiwa katika ibada.