101 - Surat Al-Qari'ah ()

|

(1) Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vituko vyake.

(2) Ni kitu gani hiko chenye kugonga?

(3) Na ni lipi lililokujulisha ni kipi hiko chenye kugonga?

(4) Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama pandzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni.

(5) Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika.

(6) Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito,

(7) atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi.

(8) Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito,

(9) makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu.

(10) Ni lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah»?

(11) Ni Moto unaowaka sana kwa kuni ziliomo ndani yake.