103 - Surat Al-Asr ()

|

(1) Mwenyezi Mungu Anaapa kwa zama

(2) kwamba wanadamu wako kwenye maangamivu na upungufu. Haifai kwa mja kuapa isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, kwani kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina.

(3) Isipokuwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakafanya amali njema, wakausiana wao kwa wao kushikamana na haki, kufanya matendo ya kumtii Mwenyezi Mungu na kusubiri juu yake.