114 - Surat An-Nas ()

|

(1) Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu, Mwenye uweza, Peke Yake, wa kulirudisha shari lao.

(2) «Mfalme wa watu, Mwenye kupeleka mambo yao yote Anavyotaka, Aliye Mkwasi kutowahitajia.

(3) «Mola wa watu, Ambaye hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye.

(4) «Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu.

(5) «Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu.

(6) «Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.»