109 - Surat Al-Kafirun ()

|

(1) Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu!

(2) «Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo.

(3) «Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwa.

(4) «Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo.

(5) «Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Mwenyezi Mungu Alijua kuwa hawataamini kabisa.

(6) «Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.»