113 - Surat Al-Falaq ()

|

(1) Sema, ewe Mtume, «Najilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa asubuhi.

(2) «Kutokana na shari la viumbe na udhia wao

(3) «Na shari la usiku wenye giza lingi ungiapo na ujikitapo na mashari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake.

(4) «Na shari la wchawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga.

(5) «Na shari la hasidi mwenye kutukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Aliyewaneemesha ziwaondokee.»