94 - Surat Ash-Sharh ()

|

(1) Kwani Hatukukunjulia, ewe Mtume, kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa tabia nzuri,

(2) Tukakuondolea mazito yako yaliyoemea mgongo wako

(3) na Tukakuweka, kwa matukufu Tuliyokuneemesha,

(4) kwenye cheo cha juu?

(5) Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa makero ya maadui zako. Kwani kwenye dhiki kuna faraji.

(6) Hakika kwenye dhiki kuna faraji.

(7) Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada.

(8) Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako.