80 - Surat Abasa ()

|

(1) Yalidhihiri mabadiliko na mkunjiko katika uso wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,

(2) na akapa nyongo kwa sababu ya kwamba Abdallah bin Ummi Maktum alimjilia akitaka aelekezwe. Na alikuwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ameshughulika kuwalingania miamba wa Kikureshi katika Uislamu.

(3) Ni kitu gani kinakufanya wewe ujue uhakika wa jambo lake? Kwani huenda ikawa, kwa kuuliza kwake, nafsi yake itatakasika na kusafika.

(4) Au pengine apate mazingatio zaidi na kutishika.

(5) Basi yule alijyejitosheleza na kutouhitajia uongozi wako,

(6) wewe ndiye unayemjali na wapulikiza maneno yake.

(7) Na ni kitu gani kinachokupa jukumu kwako iwapo hakusafika na ukafiri wake?

(8) Ama yule ambaye amekuwa na pupa la kukutana na wewe,

(9) na huku anamuogopa Mwenyezi Mungu asiwe na kasoro katika kupata uongofu,

(10) wewe unampuuza. Ilivyotakikana ufanye si kama ulivyofanya, ewe Mtume.

(11) Hakika Sura hii ni mawaidha kwako na kwa kila anayetaka kuwaidhika.

(12) Basi atakaye atamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja na atafuata Wahyi Wake.

(13) Wahyi huu, nao ni Qur’ani, uko katika kurasa zilizotukuzwa,

(14) zenye kuheshimiwa, zenye cheo cha juu,

(15) zilizosafishwa na uchafu, uongezaji na upunguzaji.

(16) Zilizoko mikononi mwa Malaika waandishi, mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, wenye maumbile mema, tabia zao ni nzuri na njema na pia matendo yao.

(17) Amelaaniwa mtu kafiri na ataadhibiwa. Ni uovu ulioje wa ukafiri wake kwa Mola wake!

(18) Kwani hajui ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Alimuumba kwacho mwanzo wake?

(19) Mwenyezi Mungu Alimuumba kwa maji machache, nayo ni manii. Akayakadiria miongo yake.

(20) Kisha Akambainishia njia ya kheri na ya shari.

(21) Kisha humkosesha uhai, na Amemuekea mahali pa kuzikiwa.

(22) Kisha Akitaka Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa mbaya, Atamhuisha na kumfufua baada ya kifo chake, kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa.

(23) Mambo siyo kama yale anayoyasema kafiri na anayoyafanya. Bado hajatakeleza Aliyomuamrisha kwayo Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda wema kwa kumtii.

(24) Na azingatie binadamu, vipi Mwenyezi Mungu Amekiumba chakula chake ambacho ndicho kinachoendeleza maisha yake?

(25) Aone kwamba Sisi Tumeyamimina maji ya mvua juu ya ardhi kwa wingi.

(26) Kisha Tumeipasua ardhi kwa Tulivyo vitoa kutoka humo miongoni mwa mimea tofauti.

(27) Tukaotesha humo nafaka

(28) na zabibu, na nyasi za wanyama.Na mizaituni na mitende.

(29) Na mabustani yenye miti mikubwa.

(30) Na matunda

(31) na ndisha.

(32) Mnajistareheshea kwazo, nyinyi na wanyama wenu.

(33) Utakapokuja Ukelele wa Siku ya Kiyama, ambao utayatia uziwi, kwa kitisho chake, masikizi.

(34) Siku mtu atakapomkimbia, kwa kitisho cha Siku Hiyo, nduguye

(35) na babake na mamake na

(36) mkewe na wanawe.

(37) Kila mmoja Siku Hiyo, atakuwa na jambo litakalomzuia asishughulike na mwingine.

(38) Nyuso za wenye neema, Siku Hiyo, zitakuwa ni zenye kung’ara,

(39) zenye furaha na nderemo.

(40) Na nyuso za watu wa Motoni zitakuwa na giza,

(41) nyeusi, zafinikwa na unyonge.

(42) Hao wenye kusifika na sifa hiyo ndiwo wale waliozikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wakazikanusha aya zake na wakayakeuka Aliyoyaharamisha kwa kutenda maovu na kukiuka mipaka.