75 - Surat Al-Qiyamah ()

|

(1) Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Hesabu na Malipo,

(2) na Anaapa kwa nafsi yenye kuamini na kuchamungu, inayomlaumu mwenyewe kwa kuacha matendo ya utiifu na kufanya matendo yenye kuangamiza, kwamba watu watafufuliwa.

(3) Je anadhanihuyu binadamu kafiri kuwa sisi hatutaweza kuikusanya mifupa yake baada ya kuwa mbalimbali.?

(4) Ndio! Tutaikusanya na tunaweza kufanya vidole vyake au ncha za vidole vyake- baada ya kuvikusanya na kuzioanisha- viwe kwenye umbo la sawasawa, kama vilivyokuwa kabla ya kufa.

(5) Bali binadamu anakanusha kufufuliwa, anataka asalie kwenye kufanya ubaya kwa siku za mbeleni za maisha yake.

(6) Kafiri huyu huwa akiuliza, akiliona jambo la kusimama Kiyama kuwa liko mbali, «Ni lini Siku ya Kiyama?’

(7) Basi macho yatakapoduwaa na yakashituka kwa kutishika na kile yalichokiona cha vituko vya Siku ya Kiyama,

(8) na ukafutika mwangaza wa mwezi,

(9) na vikakusanywa jua na mwezi katika kukosa mwangaza, kikawa kila mojawapo ya hivyo viwili hakina mwangaza,

(10) wakati huo binadamu atasema, «Pa kukimbilia ni wapi kuiepuka adhabu?»

(11) Mambo sivyo kama unavyotamani yawe, ewe binadamu, ya kutaka kukimbia. Huna mahali pa kukimbilia wala pa kupata uokozinfsi yake.

(12) Kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake ndio mwisho wa viumbe Siku ya Kiyama na ndipo mahali pao pa kutulia, na hapo Amlipe kila mtu kwa kile alichostahiki.

(13) Atapashwa habari binadamu Siku hiyo kwa matendo yake yote, mema na mabaya, aliyoyatanguliza miongoni mwa hayo katika maisha yake na aliyoyachelewesha.

(14) Bali binadamu ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake, yenye kumfuata kwa alichokitenda na alichokiacha,

(15) hata kama atakuja na kila udhuru wa kuelezea sababu ya uhalifu wake, hilo halitamfaa.

(16) Usitikise, ewe Nabii, ulimi wako kwa Qur’ani wakati wahyi unapoteremka ili ufanye haraka kuihifadhi kwa kuogopa isikuponyoke.

(17) Kwani ni juu yetu sisi kuikusanya kwenye kifua chako kisha uisome kwa ulimi wako wakati utakapo. Mjumbe wetu Jibrili akikusomea,

(18) basi kisikilize kisomo chake na umpulikize. Kisha isome kama alivyokusomea,

(19) kisha ni juu yetu kukuelezea kilichokutatiza kukifahamu katika maana yake na hukumu zake.

(20) Mambo sivyo kama mlivyodai, enyi mkusanyiko wa washirikina, kuwa hakuna kufufuliwa wala kulipwa.

(21) Bali nyinyi ni watu mnaopenda dunia na pambo lake na mnaacha Akhera na starehe zake.

(22) Nyuso za watu wema Siku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kung’ara, nzuri na zenye furaha,

(23) zitamuona Mola Aliyeziumba na Anayezimiliki, na zitastarehe kwa hilo.

(24) Nyuso za watu wabaya Silku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kukunjana na kusinyaa,

(25) zinatazamia kushukiwa na msiba mkubwa wenye kuvunja.

(26) Ni kweli! Pindi roho itakapofika sehemu za juu za kifua,

(27) na wakasema baadhi ya waliohudhuria kuwaambia wengine, «Je kuna mtu wa kumzungua na kumpoza kutokana na hali hii aliyonayo?»

(28) Na yule ambaye yuko katika hali ya kufa akajua kwamba lile lililomshukia ni kuaga dunia, kwa kuwa anawaona Malaika wa mauti.

(29) Na ikashikana shida ya mwisho wa duniani na shida ya mwanzo wa Akhera. Kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka.

(30) Watu watapelekwa Siku ya Kiyama: ima Peponi au Motoni.

(31) Hakuwa kafiri ni mwenye kumuamini Mtume na Qur’ani, wala hakuwa ni mwenye kumtekelezea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Swala za faradhi.

(32) Lakini aliikanusha Qur’ani na akaipa mgongo Imani,

(33) kisha akaenda kwa watu wake akijiona hali ya kujigamba katika kutembea kwake. Basi maangamivu

(34) ni yako baada ya maangamivu!

(35) Kisha maangamivu ni yako baada ya maangamivu!

(36) Je anadhani huyu binadamu anayekanusha kufufuliwa kuwa ataachwa bure: haamrishwi wala hakatazwi, hahesabiwi wala hateswi?

(37) Kwani hakuwa binadamu huyu ni tone la manii dhaifu linalotokana na maji matwevu yanayomwagwa na kumiminwa kwenye kizazi,

(38) kisha yakawa ni kipande cha damu iliyo kavu. Mwenyezi Mungu Akaliumba kwa uweza Wake na Akazilinganisha sura zake katika umbo la mwili lililo zuri kabisa?

(39) Akafanya kutokana na binadamu huyu jinsi mbili: ya kiume na ya kike. Je kwani hakuwa Mola huyo Muumba wa vitu hivyo ni Muweza wa kuwarudisha viumbe wakiwa hai baada ya kutoweka kwao.

(40) Ndio! Anaweza. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hakika ni Muweza wa hilo.