99 - Surat Az-Zalzalah ()

|

(1) Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.

(2) Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandi.

(3) Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?»

(4) Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya.

(5) kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa.

(6) Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo.

(7) Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera.

(8) Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera.