112 - Surat Al-Ikhlas ()

|

(1) Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo.

(2) «Mwenyezi Mungu Ambaye Peke Yake Ndiye Mwenye kukusudiwa kwa kukidhi haja na matakwa.

(3) «Hana mwana wala mzazi wala mke.

(4) «Wala hakuna yoyote katika viumbe Vyake mwenye kufanana wala kushabihiyana na Yeye katika Majina Yake, Sifa Zake wala vitendo Vyake.»