102 - Surat At-Takathur ()

|

(1) Kumewashughulisha kujifahiri kwa mali na watoto mkawacha kumtii Mwenyezi Mungu

(2) Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo.

(3) Siyo namna hii inatakiwa iwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu.

(4) Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera.

(5) Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali.Lau mnajua kikweli, mngalirudi nyuma na mngaliangusiliza kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu.

(6) Mtauona Moto!

(7) Kisha mtauona bila shaka!

(8) Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo.