97 - Surat Al-Qadr ()

|

(1) Sisi Tumeiteremsha Qur’ani katika usiku wa cheo na utukufu , nao ni moja wa masiku ya mwezi wa Ramdhani.

(2) Na nilipi liliokujulisha, ewe Mtume, ni upi usiku wa cheo na utukufu?

(3) Usiku wa cheo na utukufu ni bora fadhila zake kuliko fadhila za miezi elfu moja isiyokuwa usiku huo.

(4) Usiku huo hushuka Malaika na Jibrili, amani iwashukie, kwa ruhusa ya Mola wao kwa kila jambo Alilolikadiria liwe mwaka huo.

(5) Usiku huo wote ni amani, hakuna shari, mpaka kutokea alfajiri.