105 - Surat Al-Fil ()

|

(1) Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu?

(2) Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?

(3) Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana,

(4) ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu.

(5) Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa.