Utunzi wa kielimu

معلومات المواد باللغة العربية

How to Perform Pilgrimage

Idadi ya Vipengele: 5

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    1- Mada hii inazungumzia: Maana ya Hijja kilugha na kisheria, na ni nguzo katika nguzo tano za uislam, pia imebainisha kwamba Hijja ni fardhi inatekelezwa mara moja katika umri. 2- Mada hii inazungumzia: Umuhimu kwa mwenye kuhiji kuwa na nia thabiti pamoja na kujikurubisha kwa Allah, pia imezungumzia mambo ya kujifunza katika ibada ya Hijja na tahadhari ya kuiga uzushi. 3- Mada hii inazungumzia: Hijja na Umra na fadhila zake pamoja na alama za mwenye kufanya Hijja ya kweli, pia imezungumzia kwamba Hijja ni fardhi kwa waislam wote wanaume na wanawake. 4- Mada hii inazungumzia: Aina za maandalizi ya Hijja na imefafanua kuhusu Hijja ya mtoto mdogo, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga utaratibu na makatazo baada ya Ihram. 5- Mada hii inazungumzia: Namna Mtume (s.a.w) alivyoruhusu kumuhijia mzazi asiyejiweza kutokana na uzee au ugonjwa, na kwamba inafaa mwanaume kumuhijia mwanamke na mwanamke kumuhijia mwanaume, pia mada hii ina maswali na majibu.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kutekeleza ibada ya Hijja na kwamba ni miongoni mwa ibada bora na nguzo ya tano ya Uislam, pia imezungumzia yanayofanya Hijja iwe sahihi ikiwemo kujifunza utaratibu wa Hijja, ikhlasi na kufuata sunna za Mtume (s.a.w)

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, ubora wake, nakwamba Allah anashuka na kuwasogelea kwa waliosimama katika viwanja vya Arafa, na Allah anajifakhari kwa malaika, na yanayo takiwa kufanywa nawale ambao hawako katika viwanja vya Arafa.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, maana yake na umuhimu wa kuomba dua katika siku hiyo, na amejibu kuhusu utata juu ya siku ya arafa na siku ya Iddi al Adhha nawale wasiofunga siku ya arafa bali wanafunga siku ya kuchinja. 2- Mada hii inazungumzia Majibu ya utata wa Arafa na hijja, amebainisha kuwa hija ilikuwepo tangu wakati wa nabii Ibrahim haikuwa faradhi, amefafanua mafungaamano ya Arafa na mwezi Dhulhijah, na Arafa ya mtu wa China na Est Africa, na mafungamano ya swala ya iddi na kupiga mawe na kuchinja kwa mahojaji . 3- Mada hii inazungumzia Majibu ya utata wa Arafa na hijja, amebainisha kuwa watu wanafuata mahujaji katika takbira, na kuchinja ili wafuate watu wa mina, na ametaja Qauli za wanachuoni kuhusu mafungamano ya hija na matendo ya wasiokuwa mahujaji.

  • Kiswahili

    MP3

    The Manner Of Hajj And Umra

Ukurasa : 1 - Kutoka : 1