Utunzi wa kielimu

معلومات المواد باللغة العربية

Introducing Islam to Muslims

Idadi ya Vipengele: 217

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    1- Mada hii inazungumzia: Maana ya Hijja kilugha na kisheria, na ni nguzo katika nguzo tano za uislam, pia imebainisha kwamba Hijja ni fardhi inatekelezwa mara moja katika umri. 2- Mada hii inazungumzia: Umuhimu kwa mwenye kuhiji kuwa na nia thabiti pamoja na kujikurubisha kwa Allah, pia imezungumzia mambo ya kujifunza katika ibada ya Hijja na tahadhari ya kuiga uzushi. 3- Mada hii inazungumzia: Hijja na Umra na fadhila zake pamoja na alama za mwenye kufanya Hijja ya kweli, pia imezungumzia kwamba Hijja ni fardhi kwa waislam wote wanaume na wanawake. 4- Mada hii inazungumzia: Aina za maandalizi ya Hijja na imefafanua kuhusu Hijja ya mtoto mdogo, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga utaratibu na makatazo baada ya Ihram. 5- Mada hii inazungumzia: Namna Mtume (s.a.w) alivyoruhusu kumuhijia mzazi asiyejiweza kutokana na uzee au ugonjwa, na kwamba inafaa mwanaume kumuhijia mwanamke na mwanamke kumuhijia mwanaume, pia mada hii ina maswali na majibu.

  • Kiswahili

    MP4

    Mhadhiri : Yusufu Abdi Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Fadhila za Hijja na mapenzi ya Allah kwa waja wake na kwamba mwenye kufanya Hijja ya kweli malipo yake ni pepo, pia imezungumzia Hijja ni mazingatio kwa waja ili watu wasibaguane na wala wasidharauliane.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Hijja ni wajibu kwa Muislam ambaye ni baleghe mwenye akili mwenye uwezo tena mukalafu aliye huru, pia imezungumzia hasara ya mtu mwenye uwezo kisha akafa bila ya kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Uzembe unaofanywa na baadhi ya waislam wenye uwezo katika kuitekeleza Hija na kwamba ni hasara kubwa kwa watu kama hao, pia imezungumzia kuwa hija ni mara moja tu katika umri

  • Kiswahili

    MP4

    Mada hii inazungumzia: Hijja ni wito na kwamba ni muhimu kujitahidi kufanya ibada katika masiku ya Hijja nakumuomba Allah sana ili kupata radhi za Allah katika masiku yahija matukufu.

  • Kiswahili

    MP4

    Mada hii inazungumzia: Siku ya Arafa na fadhila zake na kwamba Hijja haikamiliki bila ya kusimama Arafa na ni siku ambayo dua zinajibiwa, pia imezungumzia umuhimu wa kushukuru neema za Allah.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa mambo yanayofanywa katika siku za Minah nayo: kurusha mawe na kunyoa nywele nakuchinja, kisha amebainisha wakati anaotakiwa alhaji kuvuwa ihram, na inatakiwa kwa alhaji kukithirisha kumtaja Allah.

  • Kiswahili

    MP4

    Mada hii inazungumzia: Matendo yanayofanywa katika siku za Minah (ayyamu Tashriq) na namna ya kurusha mawe (Jamarat) pia imezungumzia umuhimu wa kulala mina kama alivyofanya Mtume (s.a.w) na ubora wa kujiepusha na uzushi.

  • Kiswahili

    DOCX

    Kitabu hiki kinazungumzia masiku kumi bora ya Dhul-Hijja, na matendo yanayo pasa kufanya katika masiku hayo, kisha ameelezea swaumu, na ubora wa takbira, na kujikaribisha kwa Allah, kisha kimezungumzia siku ya Arafa, na namna ya kuhiji na kufanya Umra.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazunguzia: Umuhimu na nafasi ya Hijja katika Uislam na kwamba Hijja ni wajibu na inatekelezwa kwa ajili ya Allah peke yake, pia imezungumzia ruhusa aliyoitoa Mtume (s.a.w) ya kumfanyia Mzazi Hijja. 2- Mada hii inazunguzia: Umuhimu wa hija na umuhimu wa kuwafanyia hija wazazi walio fariki, na kuwafanyia wema wazazi kwa kuwawekea waqfu, na amezungumzia nyakati za hijja pia amebainisha ubora wa kuhiji ukiwa kijana.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Baadhi ya sababu za Muislam kuharakisha kuitekeleza ibada na nguzo ya Hajji, yakwanza nikuharakia kutumia nafasi ya kuwa na uwezo, sababu ya poli nikwamba hujuwi utakufa lini, pia amezungumzia sababu batili wanazo towa wasio taka kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni umuhimu na ubora wa ibada hiyo, pia imezungumzia umuhimu kwa muislam kukimbilia jambo la kheri 3- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba Hijja ni sababu ya kusamehewa madhambi yote, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga na kuhifadhi matendo ya Hijja 4- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba malipo ya Allah kwa mtu aliyefanya ibada ya Hijja ni Pepo, pia imezungumzia ubora wa neema ya Pepo ya Allah.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazunguzia: Ubora wa kutia nia thabiti katika safari ili kupata malipo ya safari na malipo ya ibada ya Hijja, pia imezungumzia miongoni mwa sunna za safari kama vile kusoma dua mwanzo na mwisho wa safari kama alivyo fundisha Mtume (s.a.w)

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Aina tatu za ibada ya Hijja ambazo ni Tamatu’u, Kiran na Ifrad, pia imefafanua namna ya kutekeleza ibada hizo.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Haifai kwa mwanamke kusafiri peke yake kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hajji mpaka awe na mahram nao ni Baba, babu, watoto, mume nk. pia imezungumzia hadhi na heshima ya mwanamke

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Mipaka aina tano maalum ya Hijja na Umra, na yanayostahiki kufanywa sehem hizo, pia imezungumzia kafara ya mtu aliyepita Mi’qat bila ya kuhirimia au kuvaa ihram

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kutekeleza ibada ya Hijja na kwamba ni miongoni mwa ibada bora na nguzo ya tano ya Uislam, pia imezungumzia yanayofanya Hijja iwe sahihi ikiwemo kujifunza utaratibu wa Hijja, ikhlasi na kufuata sunna za Mtume (s.a.w)

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, ubora wake, nakwamba Allah anashuka na kuwasogelea kwa waliosimama katika viwanja vya Arafa, na Allah anajifakhari kwa malaika, na yanayo takiwa kufanywa nawale ambao hawako katika viwanja vya Arafa.

  • Kiswahili

    PDF

    Makala hii inazungumzia: Usiku wa cheo (Laylatul qadr) usiku huo ni bora kuliko miezi elfu moja, pia imezungumzia namna Mtume s.a.w alivyokua akijitahidi kufanya ibada katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhan.

  • Kiswahili

    PDF

    Kitabu hiki kinazungumzia: Umuhimu na ubora na uzito wa funga ya mwezi wa Ramadhan kwa mujibu wa Aya na Hadithi za Mtume wetu Muhammad (s.a.w) pia kimezungumzia juu ya mambo yanayo tengua swaumu.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swaumu ikiwemo kuzungumza katika swala, na kucheka, na kula katika swala, pia amezungumzia mambo ambayo yanaweza uharibu swala. Mada hii inazunguzia mambo yanayo batilisha swala, ikiwemo kunywa katika swala na kuonekana uchi katika swala, amezungumzia mambo yanayo pelekea kuonekana uchi kwa wanaume na wanawake katika swala.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazunguzia Suna za swaumu ikiwemo ubora wa kufungua mapema, na kufturu kwa tende au maji, na kuchelewesha daku.