Utunzi wa kielimu

معلومات المواد باللغة العربية

Idadi ya Vipengele: 77

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Namna uislamu ulivyo na hali mbaya kwa sasa kutokana na watu kuacha Sunna za Mtume (s.a.w), pia imefafanua maana ya kushahidilia ya kwamba Muhammad ni mjumbe wa Allah. Mada hii inazungumzia: Nini maana ya Utume, na kwamba Mitume wote (s.a.w) ni chaguo la Mwenyezi Mungu, pia imezungumzia historia fupi ya Mtume Muhammad (s.a.w). Mada hii inazungumzia: Misingi ya kushahidilia ya kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allah, na tofauti kati ya Mitume waliopita na Mtume Muhammad (s.a.w), pia imezungumzia itikadi mbovu waliyonayo Mashi’a. Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa mambo yanayovunja (shahada) kushahidilia ya kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allah, pia imezungumzia kwamba asiyemuamini Mtume Muhammad (s.a.w) ni kafiri na mafikio yake ni motoni. Mada hii inazungumzia: Wajibu wetu ni kumtii Mtume (s.a.w) na kumfuata, na imefafanua juu ya umuhimu wa kumtii Mtume (s.a.w) pia imezungumzia uzito wa Sunna za Mtume (s.a.w) na hasara za kwenda kinyume na Sunna zake. Mada hii inazungumzia: Kumfuata Mtume (s.a.w) ndio kuongoka, na kwamba kumpenda Allah kunafungamana na kumfuata Mtume (s.a.w), pia imezungumzia umuhimu wa kushikamana na Qur’an na Sunna, na hatari ya kufuata mazoea.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Sheria aliyokuja nayo Mtume (s.a.w) na kwamba ndiyo iliyokuja kufuta sheria za nyuma, na kwamba nisheria inayo simamia haki zote, pia inazungumzia umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza mabaya. 2- Mada hii inazungumzia: Faida na muhimu wa mahakama ya Qadhi na kwamba sheria ya kiislam inajulikana duniani, pia imezungumzia waislam kuwa na tahadhari kutokana na maadui wa uislam. 3- Mada hii inazungumzia: Uislam siyo dini ya daraja la pili na kwamba imefika wakati waislam tubadilike na tuishike dini yetu, pia tuhamasishane katika dini na ucha Mungu tuache hamasa zisizo na faida katika dini yetu.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Makala hii inazunguzia: Umoja wa kweli amezungumzia kuhusu umuhimu wa kujifunza dini na na faida za mshikamano pia amebainisha matunda ya umoja, na umoja ni suna ya mtume (s.a.w). 2- Makala hii inazunguzia: Umoja wa kweli amezungumzia maana ya umoja na umoja wakweli katika Quraan na suna, pia amezungumzia mishikamano ilio haramishwa na Allah, pia amebainisha maana ya kamba ya Allah. 3- Mada hii imebainisha misingi ya Ahlu sunna waljamaa (Suni waljamaa), na umuhimu wa kuijuwa, miongoni hiyo, msingi wakwanza ni kuamini nguzo zote za imani, msingi wapili nikwamba: imani nikusema na vitendo inazidi kwa kufanya ibada na kupunguwa kwa kufanya maasi. 4- Mada hii imebainisha misingi ya Ahlu suna waljamaa, ikiwemo: uharam wa kumkufurushi muislam, na niwajibu kumtii kiongoza wa waislam, na niharam kuwasema vizuri maswahaba na kuto kuwatukama maswahaba wamtume (s.a.w), amezungumzia itikadi za mashie katika maswahaba.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazunguzia Hukumu ya mtu asie swali kabainisha Qauli mbili za wanachuoni kuhusu mtu asie swali, na ametaja dalili nyingi za ukafiri wa asie swali, na amebainisha kuwa swala ninguzo ya dini, asie swali ameivunja dini. Mada hii inazunguzia Hukumu ya mtu asie swali, amebainisha hukumu ya mtu anae sahau swala zake, na mafikio yao siku ya Qiyama, na amebainisha umuhimu wa swala na swala ndio itakayo anza kuhesabika siku ya Qiyama.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia:kuwa na adabu na Allah kazungumzia maana ya adabu na cheo cha Adabu, pia kazungumzia hatuwa za kuwa na adabu na Allah, na sifa za mwenye adabu, na jinsi ya kuwa na adabu na Allah.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia:Utukufu wa muislam kuwa na lailaha Illa Allah katika maisha yake, na mambo mengi alio yafanya Allah kwasababu ya neon hilo, na kuna habari njema kuwa mwenye kufa bila kufanya ushirikina ataingia peponi.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inafafanua: Uhalisia wa namna Mtume (S.a.w) alivyozikwa, inafafanua pia namna alivyozikwa Fatwima Binti Rasuli LLah (R.a), kinyume na wanavyopotosha Mashia.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Makundi ya Kishia na chimbuko la kila kundi,na namna walivyo tofautiana na viongozi wao.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Uzushi na propaganda za Mashia kwa Maswahaba (R.a) hasa kwa Abubakar na Omar (R.a) katika kutowa mkono wa utii kwa Abubakari.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Watu waliomfuata Abdillahi Bin Sabaa, pia Shekh anajibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu Mashia.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Madai ya Mashia kuhusu Qur’an tukufu yakwamba Maswahaba walipunguza baadhi ya Aya na Surah katika Qur’an wakati wa kuikusanya.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Madai ya Mashia kwamba wana Msahafu wenye ziada ya sura na ayah kuliko Msahafu huu tulionao, akinukuu shekh kutowa katika vitabu vya mashie, na nikatika maswali yasiyo jibika.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya Yushaa Bin Nuni, na asili ya Abdillah Bin Sabaa, inazungumzia pia namna Mashia walivyo mfanya Ally Bin Abi Twalib kuwa ni Mungu.

  • Kiswahili

    MP3

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Uadui wa Mashia dhidi ya Uisilam na Waislam, na kwamba Mashia wanafanya sana taqiyya, pia imezungumzia Ahlul bayti ni akina nani

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Uhatari na potofu la kishia, imezungumzia historia fupi ya Mtume (S.a.w) na Maswahaba wake (R.a) 2- Mada hii inazungumzia: Namna mayahudi wa Madina walivyoungana katika vita ya Ahzab, na makabila yaliyoritadi, inazungumzia pia historia ya Makhalifa waongofu kwa ufupi, na huo ndio mwanzo wa kupatatikana Mshia. 3- Mada hii inazungumzia: Chanzo cha fitina za myahudi Abdillahi Bin Sabaa, inazungumzia pia itikadi potofu za Mashia kwamba Qur’an ilibadilishwa. 4- Mada hii inazungumzia: Udanganyifu wa Mashia wa kutumia "taqiyya" inazungumzia pia uhalisia wa namna Qur’an ilivyo kusanywa na Othman Bin Afaan (R.a). 5- Mada hii inazungumzia: Namna Mashia wanavyojiweka karibu na waislamu ili waonekane ni waislam na hali siyo waislam, Mashia na Mayahudi ni sawa na wote ni maadui wa uislam. 6- Mada hii inazungumzia: Maswali na majibu ya darsa zima la uhatari na upotofu wa Mashia, ambapo swali la kwanza: ni vipi Abdillahi Bin Sabaa alishindwa kueneza fitina katika mji wa Madina?.

  • Kiswahili

    MP3

    1- Mada hii inazungumzia: Maana ya neno "Shia" kilugha na kisheria, na namna lilivyotajwa katika Qur’an Tukufu. 2- Mada hii inazungumzia: Ni nani Shia kwa mujibu wa wanachuoni wao, na kwamba ili uwe Shia lazima ukatae Uimamu wa Abubakar, Omar na Othmani (R.a). 3- Mada hii inazungumzia: Kujitokeza kwa Abdillahi Bin Sabaa mwishoni mwa utawala wa Othman Bin Affan (R.a), akaanzisha fitina kubwa ya kudai Utume na kudai kwamba Khalifa Ally Bin Abi Twalib ni Mungu 4- Mada hii inazungumzia: Kujitokeza kwa Abdillahi Bin Sabaa mwishoni mwa utawala wa Othman Bin Affan (R.a), akaanzisha fitina kubwa ya kudai Utume na kudai kwamba Khalifa Ally Bin Abi Twalib ni Mungu 5- Mada hii inazungumzia: Mashia wanadai kua Ukhalifa ni cheo kama Utume, pia inazungumzia kuwa vipi Mashia wanawakufurisha Abubakar na Omar (R.s) wakati Ally Bin Abi Twalib (R.a) kamuozesha Omar (R.a) binti yake Ummu Kuluthum?.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia:Umuhimu wa ikhlasi katika ibada na sababu ya kukubaliwa ibada na umuhimu wa kumfuata mtume katika kila jambo, na majuto kwa mwenye kuacha Sunnah.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Namna ya kutawadha, na umuhim wa kudum na udhu kwani hakika udhu ni silaha kwa Muumini.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia: Namna Mwenyezi Mungu alivyo amrisha binadam wamuombe yeye, na umuhim wa dua, na subra katika mitihani ya Da’wa.

  • Kiswahili

    MP3

    Mada hii inazungumzia mambo yafuatayo: umuhimu wa kuwatii viongozi, fitina za zama za mwisho na maana halisi ya jamaa.

Ukurasa : 4 - Kutoka : 1